Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Baadhi ya Wananchi wengine pia walifunga Barabara ya Kuu ya Mwanza-Simiyu-Mara, baada ya tukio hilo inadaiwa Jeshi la Polisi limetumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya
Pia soma:
IGP Wambura: Polisi hatuhusiki na matukio ya utekaji watu
Hakuna haja ya kuongeza neno, Taarifa yake hii hapa. --- Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura amesema jeshi hilo halihusiki na matukio yanayodaiwa kuwa ni ya utekaji, kwani jukumu lake la msingi na la kikatiba ni kuhakikisha linalinda usalama wa raia na mali zao. IGP Wambura...
Taarifa zaidi zitafuata
MAANDAMANO SIMIYU, RPC ASEMA “HALI SIYO NZURI NITAWAPA TAARIFA BAADAYE
Chanzo cha Maandamano inadaiwa baadhi ya Wananchi wanashutumu Polisi kutowajibika wakidai kuna ongezeko la matukio ya Watoto kupotea
Kamanda wa Polisi Mkoa, Edith Swebe amesema “Nipo kwenye eneo la tukio 'situation' sio nzuri, naomba mnipe muda niwape taarifa baadaye.”
Inadaiwa kuna uharibifu wa mali, Watu kadhaa wamejeruhiwa na Waandamanaji wameweka Magogo Barabara ya Mwanza-Simiyu-Mara.
==============
Wananchi wa mji mdogo wa Lamadi Wilaya Busega Mkoani Simiyu, wamelazimika kuandamana na kufunga Barabara kuu ya Mwanza - Lamadi - Mara kwa magogo huku wakiyarushia mawe magari kuzuia yasipite, kwa kile wanachodai kuchoshwa na matukio ya watoto kupotea ambayo wamesema kwamba yamekuwa yanatokea katika Mji huo.
Sintofahamu hiyo imedumu kwa takribani Saa Tano kuanzia Saa Tatu Asubuhi hadi Saa Nane Mchana ambapo Jeshi la Polisi na Askari, wamefika katika eneo hilo na kuanza kuwatuliza kwa kupiga mabomu ya machozi, wakiwatawanya wananchi wanaoandamana, huku magari ya abiria yakilazimika kusindikizwa na Askari ili kusaidia yaweze kupita katika eneo hilo kwa usalama pasipokupigwa mawe.
Kwa sasa hali ya utulivu imerejea katika eneo hilo huku jeshi la polisi likisalia maeneo hayo kwa ajili ya kuendelea kuimarisha ulinzi.
=============