Baadhi ya Wananchi wameandamana na kuvamia Kituo cha Polisi cha Lamadi wakidai askari Polisi wa eneo hilo wameshindwa kuwajibika wakidai kuna muendelezo wa matukio ya Watoto kupotea Mkoani hapo.
Baadhi ya Wananchi wengine pia walifunga Barabara ya Kuu ya Mwanza-Simiyu-Mara, baada ya tukio hilo inadaiwa Jeshi la Polisi limetumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya
Taarifa zaidi zitafuata
MAANDAMANO SIMIYU, RPC ASEMA “HALI SIYO NZURI NITAWAPA TAARIFA BAADAYE
Chanzo cha Maandamano inadaiwa baadhi ya Wananchi wanashutumu Polisi kutowajibika wakidai kuna ongezeko la matukio ya Watoto kupotea
Kamanda wa Polisi Mkoa, Edith Swebe amesema “Nipo kwenye eneo la tukio 'situation' sio nzuri, naomba mnipe muda niwape taarifa baadaye.”
Inadaiwa kuna uharibifu wa mali, Watu kadhaa wamejeruhiwa na Waandamanaji wameweka Magogo Barabara ya Mwanza-Simiyu-Mara.
==============
Wananchi wa mji mdogo wa Lamadi Wilaya Busega Mkoani Simiyu, wamelazimika kuandamana na kufunga Barabara kuu ya Mwanza - Lamadi - Mara kwa magogo huku wakiyarushia mawe magari kuzuia yasipite, kwa kile wanachodai kuchoshwa na matukio ya watoto kupotea ambayo wamesema kwamba yamekuwa yanatokea katika Mji huo.
Sintofahamu hiyo imedumu kwa takribani Saa Tano kuanzia Saa Tatu Asubuhi hadi Saa Nane Mchana ambapo Jeshi la Polisi na Askari, wamefika katika eneo hilo na kuanza kuwatuliza kwa kupiga mabomu ya machozi, wakiwatawanya wananchi wanaoandamana, huku magari ya abiria yakilazimika kusindikizwa na Askari ili kusaidia yaweze kupita katika eneo hilo kwa usalama pasipokupigwa mawe.
Kwa sasa hali ya utulivu imerejea katika eneo hilo huku jeshi la polisi likisalia maeneo hayo kwa ajili ya kuendelea kuimarisha ulinzi.