Simon Msuva apewa mkono wa kwaheri na JSK

Simon Msuva apewa mkono wa kwaheri na JSK

DullyJr

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
13,983
Reaction score
11,857
๐—ฅ๐—ฒฬ๐˜€๐—ถ๐—น๐—ถ๐—ฎ๐˜๐—ถ๐—ผ๐—ป
JSK inatangaza kusitisha mkataba wa wachezaji wake wa zamani Hichem Mokhtar na Saimon Msuva. Tunawatakia mafanikio mema katika maisha yao yote.
#๐—ฉ๐—ถ๐˜ƒ๐—ฒ๐—๐—ฆ๐—ž #๐—ฉ๐—ถ๐˜ƒ๐—ฒ๐—๐—ฆ๐—ž
#mobilis #jskdigitalcom
๐ŸŸก๐Ÿข…
Screenshot_2023-12-21-14-15-19-57.jpg
 
MAPITO NA ALIPO, SIMON MSUVA

Habari za klabu ya-,Jeunesse Sportive de Kabylie au JS Kabylie au JSK ya nchini Algeria

Winga wa timu ya Taifa ya Tanzania โ€˜Taifa Starsโ€™, Simon Msuva, kwasasa ni mchezaji huru baada ya kuachana na Klabu yake ya JS Kabylie inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Algeria.

Msuva alijiunga na timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu na amehudumu hapo kwa kipindi kisichozidi miezi sita.

Timu ya JS Kabylie inashika nafasi ya tisa kwenye Ligi ya Algeria baada ya kucheza michezo 10 na kukusanya alama 14.

Kabla ya kujiunga na timu hiyo, Msuva alikuwa akicheza timu ya Al Qadsiah FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Saudi Arabia.

Akiwa ndani ya timu hiyo, amefanikiwa kucheza mechi sita za ushindani na hajawahi kufunga bao lolote.

Msuva alijiunga na timu hiyo ikiwa ni pendekezo la Kocha, Youcef Bouzidi lakini kocha huyo hakudumu kikosini hapo baada ya kutimuliwa kazi mapema Oktoba na nafasi yake kuchukuliwa na Rui Almeida. Tangu alipoingia kocha huyo raia wa Ureno, nafasi ya Msuva kwenye kikosi cha kwanza ikawa ni ya kususua.

Taarifa ya klabu ambayo ilitolewa katika kurasa rasmi, ilieleza kufikia makubaliano ya pande mbili kuvunja mkataba wa Msuva na hivyo walimtakia kila la kheri kwenye maisha yake mengine ya soka.

"Tumekubaliana kuvunja mkataba wa Simon Msuva, tunamtakia kila la kheri huko aendapo," ilisomeka taarifa ya klabu hiyo.

Kuelekea dirisha la usajili la Januari nchini Tanzania, kuna uwezekano wa Msuva kuhusishwa na baadhi ya timu ambazo zitahitaji huduma yake.

Ikumbukwe kuwa kabla hajaanza maisha yake ya soka nje ya nchi, Msuva amewahi kutamba na timu za Moro United na Yanga SC.

Kabla ya kwenda Algeria, timu za Simba na Yanga, zilikuwa zikihitaji huduma yake ila walishindwana katika ada ya uhamisho.
 
Kuna wachezaji inatokea unawapenda sana lakini mwisho wao unakua sio mzuri.... Siombei kabisa Msuva aende huko....

Kwa Tanzania nilimpenda sana Thomas Ulimwengu lakini roho inaniuma kumwona soka limemkataa na kumgeuka kabisa.... Ulaya nilimpenda Eden Hazard but soka limemkataa mpaka akaamua kustaafu kabisa.. Hii dunia mara nyingine haina fair kabisa.
 
Jambo la uzee kwa wachezaji halikwepeki. Msuva kwa sasa umri umemtupa. Hivyo ikimpendeza arudi tu Bongo, aje amalizie soka lake kwenye timu yake ya Wananchi kama alivyofanya Jonas Mkude.
 
Kiwango cha msuva kimeshuka sana hastahili kuchezea timu yoyote kubwa Tanzania .
Angalia mechi za stars za karibuni alizocheza kiwango kidogo .
Baada ya kugombana na wydad ile ndiyo ilikuwa bye bye ya msuva kutoka Kwenye ubora wake .
 
Alidharau sana kurudi kucheza ligi ya Bongo hasa timu yake ya zamani alipohojiwa tena akaongea kwa kejeli, ..naona itakuwa ngumu kwake sasa timu za maana North Africa kumchukua maana kachuja, kwa alivyoongea nadhani ataona heri aende vitimu kama vipers

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiv sijui ni kitu gan kinawashinda watu kujizuia katika mazungumzo?
 
Back
Top Bottom