Simon Msuva kubali ukweli, wewe soka la kimataifa basi!

Msuva anasema yeye ni wa 93? Yaani amepishana na Samata mwaka mmoja? Huu sasa ni mzaha.
Ndiyo kaka, msuva passport yake inaonyesha amezaliwa 2/10/1993 ilhali mwaka wake halisi wa kuzaliwa ni 1986,
 
Miaka 38 hapana labda 35
Mkuu bongo ndio nchi ambayo mtu akifikisha tu miaka 30, umri wake huanza kurudi nyuma, hususani katika soka, sababu mpira wa bongo hapo zamani mtu alikuwa anaanza kupata jina akiwa na miaka 27,sasa akisema atumiale umri halisi si mtamstaafisha mapema? na wakati hiyo Ndiyo ajira yake, na yote haya yamechangiwa na kuwa na sura zile zile lig kuu, mfano hawa wachezaji unaowaona sasa ligi kuu watu kama kina salum kibaya,erasto Nyoni, juma nyoso, John Bocco,Kevin yondani wengi wanazaidi ya misimu 15 wanacheza ligi, sasa sura mpya zitakuja lini? Na hata zikija zitakuwa na umri gani? Imagine mchezaji kama madaraka sulemani mzee wa kiminyio aliyekuwa akiichezea simba sc alistaafu akiwa na miaka 44,so huoni kama kuna tatizo hapo?
 
shit!
 
Msuva na Karim Benzema ni kama mtu na mkewe siku hizi ni wameisha hatari. Tena kheri hata ya msuva anajikakamua huyo benzema wa uarabuni ndo Uozo mtupu anakula hela za Dizeli(mafuta) bure kabsa.
😂😂😂😂😂😂🙌🙌
 
Jamaa amepungua sana uwezo,
Simba na Yanga wasiwaze kumsajili, watafute damu changa. It's almost over for him!
 
Sahihi kabisa, na huyu jamaa amedanganya umri kwamba ana miaka 29 sasa, na wakati kiuhalisia ana miaka 38, umri haujifichi katika soka
Hivi huu ujinga mnazaliwa nao au mnajifunza ukubwani?
 
Leo umeongea kama mwanasoka halisi, ukiacha unazi unakuwa na point za maana.
 
Tuliokulia baruti ,,kona na kibo tunakuelewa
 
Siku utakapoacha kuvaa mitumba na kununua gari second hand nasi tutaacha kusajili rejected
 
Hapo kwenye miaka 38 ni chai hiyo
Siyo chai, Msuva kasajiliwa na Yanga mwaka 2011, miaka 13 iliyopita. Wakati huo keshachezea vilabu viwili vya ligi kuu kwa misimu kadhaa. Leo anasema ana miaka 30 kweli? Kwahiyo alisajiliwa Yanga akiwa na miaka 17? Hivyo vilabu vingine alivichezea akiwa under 13?
 
Mpira ndo kazi pekee dunia ambayo kijana wa miaka 38 anaitwa mzee [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hivi huu ujinga mnazaliwa nao au mnajifunza ukubwani?
Sasa hapo ujinga ni upi mkuu , kufahamu umri halisi wa mtu ni kosa?. Bila shaka wewe ni Saimon msuva, umeamua kuja front kuitetea brand!
 
Mpira ndo kazi pekee dunia ambayo kijana wa miaka 38 anaitwa mzee [emoji23][emoji23][emoji23]
Katika soka 38 ni mzee kaka, kutokana na mahitaji ya mchezo wenyewe, söka inahitaji kukimbia sana, nguvu nyingi, akili, stamina ya kutosha pamoja na afya njema, hivyo inahitaji umri kuanzia 17 - 35 atleast, ingawa wapo wachache wanaokipiga mpaka 40, wale walioamua kuachana na nyapu, bia na sigara. Ila in real life 38 bado umri wa kijana kabisa anaejitafuta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…