Simon Msuva kubali ukweli, wewe soka la kimataifa basi!

Simon Msuva kubali ukweli, wewe soka la kimataifa basi!

Msuva anasema yeye ni wa 93? Yaani amepishana na Samata mwaka mmoja? Huu sasa ni mzaha.
Ndiyo kaka, msuva passport yake inaonyesha amezaliwa 2/10/1993 ilhali mwaka wake halisi wa kuzaliwa ni 1986,
 
Miaka 38 hapana labda 35
Mkuu bongo ndio nchi ambayo mtu akifikisha tu miaka 30, umri wake huanza kurudi nyuma, hususani katika soka, sababu mpira wa bongo hapo zamani mtu alikuwa anaanza kupata jina akiwa na miaka 27,sasa akisema atumiale umri halisi si mtamstaafisha mapema? na wakati hiyo Ndiyo ajira yake, na yote haya yamechangiwa na kuwa na sura zile zile lig kuu, mfano hawa wachezaji unaowaona sasa ligi kuu watu kama kina salum kibaya,erasto Nyoni, juma nyoso, John Bocco,Kevin yondani wengi wanazaidi ya misimu 15 wanacheza ligi, sasa sura mpya zitakuja lini? Na hata zikija zitakuwa na umri gani? Imagine mchezaji kama madaraka sulemani mzee wa kiminyio aliyekuwa akiichezea simba sc alistaafu akiwa na miaka 44,so huoni kama kuna tatizo hapo?
 
Kwanza niseme Ninamuheshimu sana Saimon Msuva kama mchezaji na pia kama binadamu, nidhamu yake ndani na nje ya uwanja ni ya kiwango cha juu sana.

Lakini pia ni mchezaji ambae kila anapovaa jezi ya timu yetu ya taifa hujituma kwa moyo wake wote na passion yake juu ya mchezo wa soka huwa anaionyesha hata katika soka lake ngazi ya vilabu, na niseme wazi kwangu binafsi msuva ätabaki kuwa mmoja wa wachezaji nyota wa muda wote wa taifa letu.

Lakini kwa bahati mbaya mchezo wa soka unaenda na nyakati na umri, soka sio kama kuendesha gari kitu unachoweza kukifanya mpaka uzeeni, soka ni mchezo wa muda mfupi na uwezo unapoanza kushuka huwezi kujificha sababu mpira unachezwa hadharani.

Kila nikimtazama sSaimon Msuva wa sasa simuoni Msuva wa miaka 10 nyuma achilia mbali kupotea kabisa kwa Msuva wa mwaka mmoja nyuma, jamaa ameshuka sana kiwango kitu pekee alichobaki nacho ni kasi isiyo na faida, yaani anapokuwa uwanjani ni sawa na mbwa koko anaezunguka zunguka asijue nini cha kufanya.

Nafikiri club ya Js kabyle ya Algeria walikuwa sahihi kumvunjia mkataba na kwauwezo wake wa sasa simuoni akicheza Ulaya au club kubwa za nje ya nchi kwa mafanikio tena kama ambavyo amekuwa akijinasibu kwamba yeye kucheza bongo bado sana.

Saimoni Msuva, umri haudanganyi kaka yangu, mimi nakufahamu nje ndani, umri wako halisi ni miaka 38, kinachokufanya uwe angalau na nguvu za kukimbia ni nidhamu yako juu ya mchezo wa soka na namna unvyoutunza mwili wako, lakini kiuchezaji kwa sasa sioni kama unaweza pata namba hata kikosi cha kwanza cha Singida fountain gate, achilia mbali Azam fc au kwa miamba ya soka toka kariakoo Simba sc na sisi Dsm Yanga africa.

Msuva naomba ukubali kuwa wakati ni ukuta na nachokushauri kwa sasa tafuta timu uarabuni ukapige pesa zako mwisho kisha utulie sababu kama Yanga sc au simba sc wakikusajili watakuwa wamejiingiza hasara, lakini nawewe utapata aibu ya mwaka, sababu yatakutokea kama yaliyomkuta Thomas ulimwengu pale singida fc, alinyanyua mabega juu lakini ameishia kuwekwa benchi na habib Kyombo.

Msuva sisi kama Yanga kwa sasa haitufai na sidhani kama makolo nao wanaweza kukuhitaji, na soka la kimataifa hutoliweza tena lakini unaweza fanya JANJA kama ya sawadogo ukapata dili lako la Mwisho.
Kila lakheri msuva[emoji2772]
shit!
 
Msuva na Karim Benzema ni kama mtu na mkewe siku hizi ni wameisha hatari. Tena kheri hata ya msuva anajikakamua huyo benzema wa uarabuni ndo Uozo mtupu anakula hela za Dizeli(mafuta) bure kabsa.
😂😂😂😂😂😂🙌🙌
 
Jamaa amepungua sana uwezo,
Simba na Yanga wasiwaze kumsajili, watafute damu changa. It's almost over for him!
 
Alisema hatazamii kucheza Bongo japo ofa ikija timu ya kwanza kuipa kipaumbele itakuwa Yanga.

Sema miaka hii Club zetu kama zina malengo ya kufika mbali zijifunze kuacha kusajili rejected players.

Heijalishi katoka kwenye ligi yenye ushindani kiasi gani bado hiyo ni kamari yenye risk mno.
Leo umeongea kama mwanasoka halisi, ukiacha unazi unakuwa na point za maana.
 
Sio chai, mkuu mimi namfahamu kindaki ndaki passport yake ya sasa inasoma October 1993 but sio umri halisi na nimesukuma nae ndinga sana enzi hizo kimara, lakini nimepiga nao ndinga wote wawili mtu na mdogo wake (James msuva) mambo ya soka la vijana copa coca cola msuva na vijeba wengine walikuwa wanachip in kuja kuongeza nguvu, so najua nachokisema
Tuliokulia baruti ,,kona na kibo tunakuelewa
 
Alisema hatazamii kucheza Bongo japo ofa ikija timu ya kwanza kuipa kipaumbele itakuwa Yanga.

Sema miaka hii Club zetu kama zina malengo ya kufika mbali zijifunze kuacha kusajili rejected players.

Heijalishi katoka kwenye ligi yenye ushindani kiasi gani bado hiyo ni kamari yenye risk mno.
Siku utakapoacha kuvaa mitumba na kununua gari second hand nasi tutaacha kusajili rejected
 
Hapo kwenye miaka 38 ni chai hiyo
Siyo chai, Msuva kasajiliwa na Yanga mwaka 2011, miaka 13 iliyopita. Wakati huo keshachezea vilabu viwili vya ligi kuu kwa misimu kadhaa. Leo anasema ana miaka 30 kweli? Kwahiyo alisajiliwa Yanga akiwa na miaka 17? Hivyo vilabu vingine alivichezea akiwa under 13?
 
Mpira ndo kazi pekee dunia ambayo kijana wa miaka 38 anaitwa mzee [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hivi huu ujinga mnazaliwa nao au mnajifunza ukubwani?
Sasa hapo ujinga ni upi mkuu , kufahamu umri halisi wa mtu ni kosa?. Bila shaka wewe ni Saimon msuva, umeamua kuja front kuitetea brand!
 
Mpira ndo kazi pekee dunia ambayo kijana wa miaka 38 anaitwa mzee [emoji23][emoji23][emoji23]
Katika soka 38 ni mzee kaka, kutokana na mahitaji ya mchezo wenyewe, söka inahitaji kukimbia sana, nguvu nyingi, akili, stamina ya kutosha pamoja na afya njema, hivyo inahitaji umri kuanzia 17 - 35 atleast, ingawa wapo wachache wanaokipiga mpaka 40, wale walioamua kuachana na nyapu, bia na sigara. Ila in real life 38 bado umri wa kijana kabisa anaejitafuta
 
Back
Top Bottom