Simon Simalenga, hujifunzi kwa Sabaya? Kila lenye mwanzo lina mwisho

Simon Simalenga, hujifunzi kwa Sabaya? Kila lenye mwanzo lina mwisho

captain dunga

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2014
Posts
282
Reaction score
634
Habari zenu ndugu zangu.

Kuna huyu mkuu wa wilaya ya Songwe ambaye aliwahi kuwa mwanamuziki anaitwa Simon SIMALENGA.

Alifika hapa Songwe kwa mbwembwe na utoto mwingi tukadhani hajazoea cheo akizoea atajifunza lakini wapi.

Alifika hapa akaifungia bar Moja pale mkwajuni bila sababu kisa tu anamchukia mmiliki.

Anatembea na wake za watu na anawatishia wahusika kuwa hawana Cha kumfanya.

Sasa ameingia kwenye kiini Cha wilaya ya Songwe yaani madini, anawatesa wachimbaji wadogo huku akiwatisha wakisema chochote "ATAWAPOTEZA".

Tunajua wakuu wa wilaya wanaoletwaga sehemu za madini wanaletwaga strategically ili watimize matakwa ya watu Fulani.

Lakini nawashauri Hawa watu (sisi wananchi tunawajua) ambao wanaubia na huu mgodi wa Shanta gold mine, Kama wamemleta huyu mtu asimamie maslahi Yao wajue wamemleta kichaa wataharibu.

Jifunze kwa SABAYA.
 
Ndio yule aliyewahi kuchana jukwaani wakati wa tamasha la FIESTA
 
Unataka kusema alimteka au??

Na mnaposema anatembea na wake za Watu ni anawateka na kuwabaka au hao wake zenu wanaenda wenyewe??
Nimekuelewa sana. Watu wanakurupuka na chuki zao wanataka wote tukubaliane nae.
 
Back
Top Bottom