Ndugu zangu watu wa Wilaya ya Songwe msipokuwa makini mtaonekana ni watu wa ajabu kwa kila mteule wa Rais atakaeletwa kuja kuwatumikia kwasababu ya watu wawili Mbunge Philipo Mulugo na Mwenyekiti wake wa Halmashauri ya Wilaya Mzee Abraham Sambila.
Hivi wazaliwa wa Songwe
Naona tumeanza upya na mteule huyu wa Rais. Tulianza na Elias Nawera akiwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe tukamchafua akaondolewa, tukaja kwa Fauzia yeye bahati nzuri ameteuliwa kuwa DC, tuhamia kwa aliekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Samuel Jeremia Upulukwa tulimfanyia kila aina visa, majungu, umbeya na kila aina ya fitina nae akaondolewa.
Sasa naona tumehamia kwa kijana watu asiekuwa hata na chembe ya hatia Simon Simalenga.
Kinara wa haya yote ni Mbunge wa jimbo la Songwe Philipo Mulugo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya yetu Abraham Sambila wakiwatumia vijana wao Shaibath Kapingu na wengine.
Hivi sisi watu wa Songwe tuna laana gani? Ni kwanini kila anaeteuliwa na Rais kwenda Songwe ni lazima tumuundie zengwe?
Hivi huyu Mulugo na Sambila ni akina nani ndani ya Wilaya hii?
Nimesoma uzi huu mwanzo mwisho hatimae nikasema hebu niwasiliane na wenzangu kule Songwe nijue haya yaliyoandikwa kama yana ukweli.
Ndugu zangu tuache majungu na ifike mahali hebu Mulugo tumpuuze. Taarifa zinaonesha kuwa siku ulipoletwa uzi huu Mkuu wa Wilaya hiyo Simon Simalenga alifanya ziara kwenye Kata ya Mbangala na kuzungumza na wananchi wa Kata hiyo ambayo ndipo anapotoka Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo na ambae hakuwepo siku hiyo kwa kumkimbia Mkuu wa Wilaya.
Nimeambiwa moja ya mambo yaliyojitokeza ni pqmoja na kero ya milipuko mikubwa inayotoka kwenye Mgodi wa Mbunge Mulugo kiasi cha kupasua nyumba za wananchi wa kijiji cha Mbangalq, katika mqjibu yake Mkuu wa Wilaya kumbe alielekeza Afisa Mkazi wa Madini wa Wilaya hiyo kuchukua hatua za haraka kushughulikia kero hiyo.
Ndipo Mulugo alipopata taarifa hiyo na kuwatuma vijana wake akiwemo Diwani wa Kata ya Mkwajuni Shaibath Kapingu kumshughulikia Mkuu wa Wilaya kwa kuleta tuhuma hizi.
Taarifa zilizopo Wilaya ya Songwe inasemekana kuwa Simalenga anapendwa na wananchi wa Songwe kuliko Mkuu wa Wilaya yoyote aliewahi kwenda Songwe tena makundi yote kuanzia Wafugaji, Wachimbaji wadogo, wakulima mpakq wananchi wa kawaida.
Tusipokuwa makini Songwe itaendelea kudidimia kwasababu ya ukilaza wa Mulugo na genge lake ili aendelee kuwa Mbunge mpaka mwaka 2040 kama anavyotamba