Simpendi na sikumchagua Magufuli lakini naunga mkono 100% msimamo wake kuhusu Korona

Mkuu heshima yako. Pamoja na hili andiko lako naomba nikuambie tu kwamba , inchi za Asia zimefanikiwa kudhibiti corona kwa sababu ya nidhamu katika uvaaji wa barakoa. Hapa kwetu barakoa zilitupwa kule kisa mtu mmoja katangaza korona imemalizwa na maombi
 
Amewaondolea kwa kuwaambia nyoka katoka nje kupitia mlango wa nyuma.

Ndiyo maana JPM kakomaa kwa kusema korona haipo nchini ili kutuondolea hofu.

Lkn angekiri hadharani hapo angesabbisha hofu kubwa.
Hilo hakuna anaelipinga. Watu tunajiuliza unatujengeaje hofu wakati huo huo wewe umejawa na hofu iliyokupelekea kujitenga??
 
Asia zimefanikiwa kudhibiti corona kwa sababu ya nidhamu katika uvaaji wa barakoa
Watanzania hawana nidhamu. "Usipite hapa usiku" kuna mbwa wakali ndiyo wanapita.

"Usikojoe hapa" ndiyo panageuzwa choo
 
Umeandika Mheshimiwa Rais kwa kuanza moyoni na caps.. hata udonoe vipi.. ni Rais wako mpendwa.. umemfikiria hivyo na kumtaja hivyo hata unajisutaaaaaa eeeeeeeh... tano tena.. mtaelewa tu.. huku mkijuwaga yule alikuwa hawezi ya JPM..
 
Naunga mkono hii hoja,upo sawa mkuu 🇹🇿🇹🇿
 
Hilo hakuna anaelipinga. Watu tunajiuliza unatujengeaje hofu wakati huo huo wewe umejawa na hofu iliyokupelekea kujitenga??
Mkuu mbona alikuwa na ziara huko Kagera na juzi tu alikuwa na mgeni toka Ethiopia. Hizo si ndiyo kazi za rais?

Labda tu tatizo la huyu dikteta ni kugeuza Kijiji chake kuwa makao makuu ya nchi. Na nyumba ya bibi yake kuwa ikulu. Simpendi jiwe huyu
 
Wacha kurukia watu usiowajua humu! Nani alikudanganya mimi ni Askofu? 😳😳😳
Chukua tahadhari acha ubishi wa kipumbavu.
Askofu acha chuki zako binafsi
Tz hakuna korona
 
Umeandika Mheshimiwa Rais kwa kuanza moyoni na caps.. hata udonoe vipi.. ni Rais wako mpendwa.. umemfikiria hivyo na kumtaja hivyo hata unajisutaaaaaa eeeeeeeh... tano tena.. mtaelewa tu.. huku mkijuwaga yule alikuwa hawezi ya JPM..
Hata ungenipa hongo ya kurefusha maisha yangu jiwe simpendi. Dikteta mkubwa huyu.
 
Hapana mkuu. Wagonjwa watibiwe.

Lkn fungu la wazungu huwa linaambatana na masharti ya kufanya lockdown. Ndiyo maana Kenya wanalazimika kuifanya lockdown kisanii.

Si kweli, maana kama ni hela ilishakuja na hakukuwa na lockdown. Mimi sio muumini wa lockdown na wala siko hapa kutaka lockdown, lakini nilitarajia kuona serikali ikitenga ward maalum hospitali kwa ajili ya wagonjwa hao, mfano wakati wa kipindupindu.
 
Hata ungenipa hongo ya kurefusha maisha yangu jiwe simpendi. Dikteta mkubwa huyu.
Kivipi.. kudonoa visivyo vyako ndio unahangaika!!!.. wewe hukuwa hivi alipoanza.. lazima ulikumbwa na kitu.. ufisadi au? nini haswaaa!! maana mupo wengi sababu ni uvivu tu na kupenda vya shoti kati.. nimepatia?
 
wewe baba zima unasubiri barua ama matangazo kwenye viwanja vua mpira!!!!


Inahitaji uwe na akili kubwa ndipo ungeweza kuelewa msingi wa swali langu na siyo kudandia gari kwa mbele kama ulivyofanya,

Siku nyingine jifunze kuwa na utulivu katika kuelewa swali kabla ya kulijibu.

Kama ni kweli Kwanini taarifa isitolewe rasmi kutoka vyanzo rasmi?

Kwanini tubaki na kuzania zania?

Kwanini hao wengine wanaumauma maneno huku wakisema ugonjwa haupo lakini tuchukue tahadhari, tahadhari ya nini iwapo hakuna ugonjwa?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…