Siyo kila anayepiga kelele ni mpinzani mkuu. Maaskofu umewasikia, na Kuna watu chungu nzima. Lkn wote hawana hoja zenye mashiko.
Binafsi naona jiwe ana misimamo yake fulani tu. Lkn siyo kwamba anawaogopa wapinzani eti watamzodoa.
Mkuu amini ninacho kuambia hawa wanao lilia Sana kuwa Rais atamke hadharani kuwa Kuna Corona ujue kabisa kuna kitu ama nguvu kubwa nyuma yao, hawa maaskofu na wengineo si mara yao ya kwanza kutamka maneno Kama hayo.
Labda nikuulize, wakati Corona ilipo anza na watu wakawa na hofu kubwa hadi baadhi ya makanisa kufunga makanisa yao mfano Yule Askofu wa Karagwe, kelele nchi nzima kuwa Rais afunge baadhi ya miji mfano dar es salaam je ni nani aliyekuja kuwapa uhakika kuwa Corona hakuna hadi wakarudia maisha ya kawaida hadi hivi leo?? Kuna dawa ililetwa kuizuia hiyo Corona??
Aliye wapa amri ya kufungua yale makanisa wakati waliyafunga kwa amri yao wenyewe ni nani?
Kwanini walifungua? Je Corona iliisha na Kama iliisha iliishaje ishaje?
Kwanini leo kina Askofu Bongaza na wenzake walio amua kufunga makanisa yao kipindi kile wasifunge tena Kama kweli wameona wimbi kubwa la vifo vya Corona Kama walivyo fanya mwanzo, kwanini wasubiri amri ya Rais?
Tuje kwa hawa wana siasa, wakati wanaondoka bungeni kwenda kujiweka karanitini ilikuwa ni amri ya nani??
Na walirudi kwa amri ya nani?? Na waliporudi ugonjwa ulikuwa umeisha na Kama uliisha uliishaje?
Kwenye kampeni walizungumza nini kuhusu Corona na walikuwa wanatumia mbinu zipi kuwalinda watu (wote tuliona jinsi kampeni zilivyo endeshwa)
Sasa leo kwanini watumie nguvu kubwa namna hii kushinikiza Rais atangaze Corona kurudi tena ( kwani ilikwenda wapi ikiwa walipinga kila kitu kilichosemwa na kufanywa na serikali?)
HAPO KUNA KITU KINATAFUTWA KWA MGONGO WA CORONA.
Watu wanaugua, wapi wanako ugua je unaona jinsi wanafunzi wanavyo jazana vyuoni kwenye ma hostel ilipuke Corona kikweli kweli utaweza kuificha mule??
Watu wawe wanapukutika pale k/koo unaweza kuficha pale tusijue hadi tusubiri waraka wa maaskofu ndio tujue Kuna Corona.?
Narudia tena tahadhari haihitaji kauli ya Rais na Corona si mtaji wa kisiasa hauta wasaidia na wala si mbinu nzuri ya kupenyeza propaganda zisizo na mashiko.