Kumbe kila kitu kina madhara yake , na zile zinazokaa kwenye moto masaa mawili na nusu inakuwaje swala la betri ?
Mkuu mimi ninatumia oppo a3s tangu mwaka 2018 mwezi wa 11 mpaka leo , kwa sasa betri ndo limeanza kupungua makali maana zamani hata nipigeke mziki ilikuwa haitoi bar moja , lakini kwa sasa inakula kula nikiitoa kwenye chaji asubuhi kufikia jioni nikiingia na mtandaoni moto unakata.
Ila tangu nimemiliki simu zote kwa mikono yangu hii ndiyo simu niliyoiona bora , haijawahi nisaliti kama ilivyonisaliti Samsung J5 Prime , maana baada ya mwaka ilianza marue rue mengi tu ila hii tangia nimeinunua tena used sijawahi kurestore.