View attachment 3221663Kuanzia Jana simu yangu kupitia mtandao wa Yas imekuwa ikituma hii sms Kwa namba nyingi nisizozifahamu. Kila baada ya dakika kadhaa nakuta imetuma tu Kwa namba nisioifahamu.
Hii itakuwa nini?
View attachment 3221662
Pole mkuu,
Tuelewe kwanza hicho ni kitu gani then tuangalie tatizo alafu tulitatue
imsi = International Mobile Subscriber Indentification.
uid = unique identification number.
Hizi ni nini?
imsi - Hii ni nambari ya kipekee ya kitambulisho inayotolewa kwa kila mtumiaji wa simu ya mkononi(rununu). Huhifadhiwa kwenye SIM kadi na kutumiwa na waendeshaji simu(kama Yas,Voda etc) kutambua na kuthibitisha waliojisajili. Nambari ya IMSI inaruhusu watumiaji kupiga simu na kuhakikisha ulinzi wa utambulisho wa simu ya mkononi. Inajumuisha Msimbo wa Nchi ya Simu (MCC), Msimbo wa Mtandao wa Simu (MNC), na Nambari ya Utambulisho ya Msajili wa Simu (MSIN),
Kila SIM kadi hubeba IMSI ya kipekee inayofafanua wasifu wa mteja ndani ya mtandao
uid - Nambari ya kipekee iliyopewa kila programu ili kuhakikisha kuwa inaendesha mchakato wake yenyewe na ina rasilimali zake kivyake vyake
Kwanini unaona sms za namna hii?
Vitambulishi hivi hutumiwa ndani na mitandao ya simu na vifaa kwa madhumuni ya uthibitishaji na utambulisho.
Au
Inaweza kuwa kutokana na hitilafu ya simu au SIM, programu hasidi(malicious), au suala la usanidi(configuration). Unapaswa kuangalia mipangilio ya simu yako na programu zilizosakinishwa(installed) hivi karibuni ili kuhakikisha kuwa hakuna shughuli isiyoidhinishwa inayofanyika.
Nini kifanyike?
1.Soft reset - zima cm chomoa betri dk 30 rudishia washa
2.Safe mode - weka simu yako katika safe mode uone itajirudia?
3.Kama simu yako ni clone,badili simu
4.Test line ya mtandao mwingine ikiwa okey,bus SIM card yako ina mushkeli kidogo
NB.Wanao ongelea HACKING wapuuze
Kuna kitu cha kitaalamu sana wanaita
IMSI Catchers - Hivi ni vifaa vinavyotumika kukatiza mawasiliano ya simu ya rununu(mkononi). Inaweza kukusanya nambari za IMSI, ambazo hutambulisha kifaa cha rununu kwa njia ya kipekee kwa opereta wa mtandao wako. Ingawa hazitumiwi kutuma jumbe za SMS moja kwa moja, zinaweza kutumika kufuatilia na kunasa ujumbe wa SMS unaotumwa na kifaa chako(TCRA)
Hii ni very very unlikely,as it needs special devices na close proximity(few hundred meters)
Hope mmejifunza kitu hapa
Thanks