Simu milioni 30 hatarini kuzimwa kwa kukosa usajili wa alama za vidole

Simu milioni 30 hatarini kuzimwa kwa kukosa usajili wa alama za vidole

Makanyaga

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2007
Posts
11,129
Reaction score
7,321
Takriban nusu ya laini milioni 44 za simu zinaweza kufungwa iwapo kasi ya utoaji vitambulisho vya Taifa haitaongezeka katika siku 49 kuanzia leo.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema itazizima laini hizo ifikapo Desemba 31 iwapo wamiliki watakuwa hawajajisajili kieletroniki kwa kutumia kitambulisho cha Taifa.

Hadi sasa zaidi ya laini milioni 30 hazijasajiliwa na mkurugenzi mkuu wa TCRA, James Kilaba alisema zilizosajiliwa ni takriban milioni 13 kati ya takriban milioni 44 zinazotambuliwa na mamlaka hiyo.

Kutokana na kutokuwapo uwezekano wa kuongeza hata dakika moja, Kilaba alisema hamasa inapaswa kuwa kubwa ili wananchi wasishindwe kutekeleza majukumu yao.

“Tumetoa matangazo matatu kuwaelimisha wananchi zikiwa zimebaki siku chache kabla utekelezaji wa sheria haujafika,” alisema Kilaba.
“Tunafahamu changamoto ya vitambulisho vya Taifa iliyopo lakini kila mmoja anapaswa kuharakisha kupata namba (ya kitambulisho cha Taifa).”

Endapo Nida watatoa vitambulisho walau milioni 10, alisema huenda vikatosha kusajili idadi kubwa kwani wapo wengi wanaomiliki zaidi ya laini moja.

Changamoto zilizopo alisema si za watoa huduma, bali upatikanaji wa vitambulisho hivyo kwani kuna vifaa vya kutosha kusajili wateja wote wa simu za mkononi endapo watakuwa na kitambulisho.

Ili kuhakikisha hakuna anayeachwa kwenye mchakato huo, alisema huwa wanaenda hata minadani vijijini ili kusajili wananchi lakini wanakuta wengi hawana vitambulisho.

Hata hivyo, alisema katika laini zilizopo, inawezekana zipo baadhi ambazo zinatambulika kwa watoa huduma ila wahusika wakawa hawazitumii kabisa.

“Kitakachofanyika ni kuzima laini hizo Desemba 31 ili wachache watakaobaki waende kutafuta kitambulisho na kusajili laini walizonazo. Hiyo itatusaidia kujua laini hai na ambazo zinatumika ni ngapi nchini,” alisema.

Simu za mkononi ndizo zinazoibeba sekta ya fedha kwani kati ya asilimia 65 ya Watanzania wanaozitumia, asilimia 48 wanafanya hivyo kupitia simu za mkononi.

Taarifa ya TCRA kwa miezi sita iliyopita inaonyesha miamala ya zaidi ya Sh16 trilioni ilifanyika mpaka Juni. Mamlaka hiyo inasema kwa robo ya kwanza iliyoishia Machi 30, miamala milioni 243.52 iliyofanyika ilikuwa na thamani ya Sh7.82 trilioni huku miamala milioni 260.43 iliyofanyika kati ya Aprili na Juni ilikuwa ya Sh8.31 trilioni.

Akiwasilisha taarifa za fedha za nusu mwaka ulioishia Septemba, mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Vodacom, Hisham Hendi alisema M-pesa ni miongoni mwa huduma muhimu inayoiingizia mapato kampuni hiyo, lakini kuna changamoto.

“Tunaendelea kuwasajili wateja wetu kwa alama za vidole ili kutii sheria, lakini changamoto iliyopo ni gharama za kufanya hivyo pamoja na upatikanaji hafifu wa vitambulisho vya Taifa,” alisema Hendi mwishoni mwa wiki iliyopita.

Huduma za M-pesa zilifanikisha miamala ya Sh29.1 trilioni ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 21.4 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana. Miamala hiyo iliingizia kampuni hiyo Sh182.02 bilioni.

Meneja uhusiano wa kampuni ya Airtel, Jackson Mmbando alisema kampuni zote za mawasiliano zinashirikiana na mamlaka husika kuhakikisha wateja wote wenye sifa wanasajiliwa kwa alama za vidole.

Kwa sasa, karibu ofisi zote za Nida hujaa wananchi wanaosaka vitambulisho hivyo ambavyo vimegeuka kuwa nyaraka muhimu inayotakiwa sehemu kadhaa kama utambulisho rasmi.

Kampuni za simu zimegawa ving’amuzi maalumu vya alama za vidole kwa mawakala wake ili kurahisiha usajili, lakini changamoto ni vitambulisho.

Chanzo: Mwananchi


Namna ya kuomba namba ya utambulisho wa Taifa kwa kutumia simu ya mkononi

Piga *152*00# halafu chagua AJIRA NA UTAMBUZI halafu tena chagua NIDA

Source: Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
 
Siwezi poteza muda wangu kuhusu hili zoezi najua kabisa haliwezi fanikiwa kwanza kuna kundi kubwa la vijana hawafikia miaka 18 wanamiliki simu lakini hawana vitambulisho je nao watazimiwa simu
Sheria hairuhusu wenye chini ya miaka 18 kumiliki simu, so watakuwa wametumbuliwa automatically
 
Taratibu inayolazimisha kwamba ili usajiliwe uwe na NIDA haina maana, fingerprint ilikuwa usajili tosha kwa mmlik wa siku kwani duniani Kuna zaidi ya watu billion Saba, lakini kila mmoja ana utambulisho wake wa alama ya dole gumba 'fingerprint'. Suala mtanzania kuwa na ID ya NIDA lingejitegemea na si kuhusishwa na usajili
 
Ni hapo ndiyo napoona waafrika tunastahili kutawaliwa tena kwa kucharazwa bakora za migongoni. Mtu wamsajili kwa alama za vidole bado uhusishe na ID ya taifa.
Ni nchi pekee za kishenzi za Afrika mambo mepesi hufanywa magumu na magumu kufanywa kiwepesi.
Waafrika tuna matatizo. Inapaswa kuwa wabunifu zaidi, haiwezekani line milioni 30 zipoteze mapato serikalini na kampuni za simu. Hata wenye dhamana na sekta hii wangekaa na wadau wa mawasiliano na kuhusishwa serikali za mtaa je tutumie mbinu ipi tusajili line bila usumbufu. Wenzetu nchi zilizoendelea uongozi maana yake unoe bongo ili kurahisisha maisha, Sasa NIDA imefanya maisha ya wengi kuwa magumu , process ndeefu , Mimi nilishudia mtu akiambiwa shortcut ili apate ID ya NIDA atoe 15,000 Sasa kwa asiekuwa nayo si Haki hata kidogo
 
TCRA na NIDA zote ni taasisi za serikali kwanini wasikae watafute suluhisho la pamoja. Badala yake wanataka watuzimie simu zetu sisi wananchi wanyonge wa awamu ya 5.
Yani mkuu ulikuwa kichwani mwangu, nachelea kusema kwamba si wabunifu, wathubutu, Sasa mnyonge afanyaje Kama wahusika wanalalamika hawatafuti suluhisho
 
Siwezi poteza muda wangu kuhusu hili zoezi najua kabisa haliwezi fanikiwa kwanza kuna kundi kubwa la vijana hawafikia miaka 18 wanamiliki simu lakini hawana vitambulisho je nao watazimiwa simu
Hivi ukiwa under 18 huwezi pata kitambulisho cha NIDA?
 
Yani mkuu ulikuwa kichwani mwangu, nachelea kusema kwamba si wabunifu, wathubutu, Sasa mnyonge afanyaje Kama wahusika wanalalamika hawatafuti suluhisho

me mwenyewe nashangaa si kuna uzi humu mleta mada alisema kwa nini nida na tcra wasibadilishane nyaraka juu kwa juu
 
Back
Top Bottom