Simu milioni 30 hatarini kuzimwa kwa kukosa usajili wa alama za vidole

Line yangu ya Simu niliisajili kwa kutumia kitambulisho cha kupigia kura

Kitambulisho cha kupigia kura huwezi kukipata mpaka uweke finger print!!

Maana yake ni kwamba hata zoezi la kusajili line kwa finger print halina maana yoyote ile!!

Kwanini nisajili line kwa fingerprint tena wakati iyo line nilishaisajili kwa kutumia kitambulisho nilichokipata kwa kutumia fingerprint??!!

Bogus Tz!!
 
Pulchra Animo,
Jina utabadili na sura pia utabadili?
Pathetic unafikiria kwa ubongo gani kaka?
Wewe badili jina lako ila jua wakitrace finger print tu na sura wanapata haijalishi jina unatumia Masakuu au Mwanjombe
 
Mimi ili zoezi ata sijui alietoa mawazo ni nani, mtaani tuna madogo wana miaka 17 mwezi wa kwanza au mwaka kesho wanatimiza miaka 18 vp wao hawatapata ruhusa ya kuwa na simu uko siku za mbeleni? Mimi nijuavyo ni kua wao watafanya ilo walioangalo ila ili zoezi la kuchukua namba za Nida na kusajili halitaisha leo ni endelevu
 
Ni Mateso Kwa Kweli!Juzi Nmeenda Ofisi Za NHIF mbeya,wamekataa kuchukua fomu ya mtegemezi eti kisa sijaambatanisha kitambulisho chake cha taifa!!!hivi nipo nahangaika,kwenda ofsi za NIDA MBEYA kuna umati wa watu hadi kero,kuna raia wanalala palepale!!
 
Takriban nusu ya laini milioni 44 za simu zinaweza kufungwa iwapo kasi ya utoaji vitambulisho vya Taifa haitaongezeka katika siku 49 kuanzia leo.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema itazizima laini hizo ifikapo Desemba 31 iwapo wamiliki watakuwa hawajajisajili kieletroniki kwa kutumia kitambulisho cha Taifa.

Hadi sasa zaidi ya laini milioni 30 hazijasajiliwa na mkurugenzi mkuu wa TCRA, James Kilaba alisema zilizosajiliwa ni takriban milioni 13 kati ya takriban milioni 44 zinazotambuliwa na mamlaka hiyo.

Kutokana na kutokuwapo uwezekano wa kuongeza hata dakika moja, Kilaba alisema hamasa inapaswa kuwa kubwa ili wananchi wasishindwe kutekeleza majukumu yao.

“Tumetoa matangazo matatu kuwaelimisha wananchi zikiwa zimebaki siku chache kabla utekelezaji wa sheria haujafika,” alisema Kilaba.
“Tunafahamu changamoto ya vitambulisho vya Taifa iliyopo lakini kila mmoja anapaswa kuharakisha kupata namba (ya kitambulisho cha Taifa).”

Endapo Nida watatoa vitambulisho walau milioni 10, alisema huenda vikatosha kusajili idadi kubwa kwani wapo wengi wanaomiliki zaidi ya laini moja.

Changamoto zilizopo alisema si za watoa huduma, bali upatikanaji wa vitambulisho hivyo kwani kuna vifaa vya kutosha kusajili wateja wote wa simu za mkononi endapo watakuwa na kitambulisho.

Ili kuhakikisha hakuna anayeachwa kwenye mchakato huo, alisema huwa wanaenda hata minadani vijijini ili kusajili wananchi lakini wanakuta wengi hawana vitambulisho.

Hata hivyo, alisema katika laini zilizopo, inawezekana zipo baadhi ambazo zinatambulika kwa watoa huduma ila wahusika wakawa hawazitumii kabisa.

“Kitakachofanyika ni kuzima laini hizo Desemba 31 ili wachache watakaobaki waende kutafuta kitambulisho na kusajili laini walizonazo. Hiyo itatusaidia kujua laini hai na ambazo zinatumika ni ngapi nchini,” alisema.

Simu za mkononi ndizo zinazoibeba sekta ya fedha kwani kati ya asilimia 65 ya Watanzania wanaozitumia, asilimia 48 wanafanya hivyo kupitia simu za mkononi.

Taarifa ya TCRA kwa miezi sita iliyopita inaonyesha miamala ya zaidi ya Sh16 trilioni ilifanyika mpaka Juni. Mamlaka hiyo inasema kwa robo ya kwanza iliyoishia Machi 30, miamala milioni 243.52 iliyofanyika ilikuwa na thamani ya Sh7.82 trilioni huku miamala milioni 260.43 iliyofanyika kati ya Aprili na Juni ilikuwa ya Sh8.31 trilioni.

Akiwasilisha taarifa za fedha za nusu mwaka ulioishia Septemba, mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Vodacom, Hisham Hendi alisema M-pesa ni miongoni mwa huduma muhimu inayoiingizia mapato kampuni hiyo, lakini kuna changamoto.

“Tunaendelea kuwasajili wateja wetu kwa alama za vidole ili kutii sheria, lakini changamoto iliyopo ni gharama za kufanya hivyo pamoja na upatikanaji hafifu wa vitambulisho vya Taifa,” alisema Hendi mwishoni mwa wiki iliyopita.

Huduma za M-pesa zilifanikisha miamala ya Sh29.1 trilioni ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 21.4 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana. Miamala hiyo iliingizia kampuni hiyo Sh182.02 bilioni.

Meneja uhusiano wa kampuni ya Airtel, Jackson Mmbando alisema kampuni zote za mawasiliano zinashirikiana na mamlaka husika kuhakikisha wateja wote wenye sifa wanasajiliwa kwa alama za vidole.

Kwa sasa, karibu ofisi zote za Nida hujaa wananchi wanaosaka vitambulisho hivyo ambavyo vimegeuka kuwa nyaraka muhimu inayotakiwa sehemu kadhaa kama utambulisho rasmi.

Kampuni za simu zimegawa ving’amuzi maalumu vya alama za vidole kwa mawakala wake ili kurahisiha usajili, lakini changamoto ni vitambulisho.

Chanzo: Mwananchi

Namna ya kuomba namba ya utambulisho wa Taifa kwa kutumia simu ya mkononi

Piga *152*00# halafu chagua AJIRA NA UTAMBUZI halafu tena chagua NIDA

Source: Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
Halafu kodi zitapatikana wapi? Nida ni issue tusidanganyene
 
Hapana, huu usajili wewe nadhani haujaelewa vizuri. Unapojisajili kwa kutumia fingerprints, huhitaji kuwatajia majina yako. Wanazo details zako zote kwenye system yao, hadi line ya simu unayokwenda kusajili. Unachohitaji kuwa nacho ni line yako ya simu, namba yako ya kitambulisho cha taifa, pamoja na vidole vyako tu basi. Jina lako watalipata kwenye system zao, wanalo tayari. Zoezi la kusajili kwa mtindo huu halichukui hata dakika 5 linakuwa limemalizika

Kwa mtu anayesajili simu kwa mara ya kwanza, details zake wanakuwa nazo kwenye system yao kutoka wapi?
 
wazime tu..mimi ntatumia whatsapp niliyosajili kwa line yangu nilokua natumia Dermark....nikihitaji data kununua natumia app ya Dent kununua internet budles, kwani shi ngapi bana.wanataka alama zangu za vidole ili wazicheshe!?
 
Takriban nusu ya laini milioni 44 za simu zinaweza kufungwa iwapo kasi ya utoaji vitambulisho vya Taifa haitaongezeka katika siku 49 kuanzia leo.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema itazizima laini hizo ifikapo Desemba 31 iwapo wamiliki watakuwa hawajajisajili kieletroniki kwa kutumia kitambulisho cha Taifa.

Hadi sasa zaidi ya laini milioni 30 hazijasajiliwa na mkurugenzi mkuu wa TCRA, James Kilaba alisema zilizosajiliwa ni takriban milioni 13 kati ya takriban milioni 44 zinazotambuliwa na mamlaka hiyo.

Kutokana na kutokuwapo uwezekano wa kuongeza hata dakika moja, Kilaba alisema hamasa inapaswa kuwa kubwa ili wananchi wasishindwe kutekeleza majukumu yao.

“Tumetoa matangazo matatu kuwaelimisha wananchi zikiwa zimebaki siku chache kabla utekelezaji wa sheria haujafika,” alisema Kilaba.
“Tunafahamu changamoto ya vitambulisho vya Taifa iliyopo lakini kila mmoja anapaswa kuharakisha kupata namba (ya kitambulisho cha Taifa).”

Endapo Nida watatoa vitambulisho walau milioni 10, alisema huenda vikatosha kusajili idadi kubwa kwani wapo wengi wanaomiliki zaidi ya laini moja.

Changamoto zilizopo alisema si za watoa huduma, bali upatikanaji wa vitambulisho hivyo kwani kuna vifaa vya kutosha kusajili wateja wote wa simu za mkononi endapo watakuwa na kitambulisho.

Ili kuhakikisha hakuna anayeachwa kwenye mchakato huo, alisema huwa wanaenda hata minadani vijijini ili kusajili wananchi lakini wanakuta wengi hawana vitambulisho.

Hata hivyo, alisema katika laini zilizopo, inawezekana zipo baadhi ambazo zinatambulika kwa watoa huduma ila wahusika wakawa hawazitumii kabisa.

“Kitakachofanyika ni kuzima laini hizo Desemba 31 ili wachache watakaobaki waende kutafuta kitambulisho na kusajili laini walizonazo. Hiyo itatusaidia kujua laini hai na ambazo zinatumika ni ngapi nchini,” alisema.

Simu za mkononi ndizo zinazoibeba sekta ya fedha kwani kati ya asilimia 65 ya Watanzania wanaozitumia, asilimia 48 wanafanya hivyo kupitia simu za mkononi.

Taarifa ya TCRA kwa miezi sita iliyopita inaonyesha miamala ya zaidi ya Sh16 trilioni ilifanyika mpaka Juni. Mamlaka hiyo inasema kwa robo ya kwanza iliyoishia Machi 30, miamala milioni 243.52 iliyofanyika ilikuwa na thamani ya Sh7.82 trilioni huku miamala milioni 260.43 iliyofanyika kati ya Aprili na Juni ilikuwa ya Sh8.31 trilioni.

Akiwasilisha taarifa za fedha za nusu mwaka ulioishia Septemba, mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Vodacom, Hisham Hendi alisema M-pesa ni miongoni mwa huduma muhimu inayoiingizia mapato kampuni hiyo, lakini kuna changamoto.

“Tunaendelea kuwasajili wateja wetu kwa alama za vidole ili kutii sheria, lakini changamoto iliyopo ni gharama za kufanya hivyo pamoja na upatikanaji hafifu wa vitambulisho vya Taifa,” alisema Hendi mwishoni mwa wiki iliyopita.

Huduma za M-pesa zilifanikisha miamala ya Sh29.1 trilioni ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 21.4 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana. Miamala hiyo iliingizia kampuni hiyo Sh182.02 bilioni.

Meneja uhusiano wa kampuni ya Airtel, Jackson Mmbando alisema kampuni zote za mawasiliano zinashirikiana na mamlaka husika kuhakikisha wateja wote wenye sifa wanasajiliwa kwa alama za vidole.

Kwa sasa, karibu ofisi zote za Nida hujaa wananchi wanaosaka vitambulisho hivyo ambavyo vimegeuka kuwa nyaraka muhimu inayotakiwa sehemu kadhaa kama utambulisho rasmi.

Kampuni za simu zimegawa ving’amuzi maalumu vya alama za vidole kwa mawakala wake ili kurahisiha usajili, lakini changamoto ni vitambulisho.

Chanzo: Mwananchi

Namna ya kuomba namba ya utambulisho wa Taifa kwa kutumia simu ya mkononi

Piga *152*00# halafu chagua AJIRA NA UTAMBUZI halafu tena chagua NIDA

Source: Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
Wote wanaoratibu hili zoezi ni wapumbavu.
Regardless umri wao elimu zao au vyeo vyao
 
Soma comment yangu #24 , mkuu.
Vyeti vya kuzaliwa navyo ni feki?

Watu wakiweza kufanya kwa usahihi hayo uliyopendekeza (at #23) kama mbadala, nadhani hawatakuwa na sababu ya kushindwa kupata kitambulisho cha NIDA. Haichukui zaidi ya wiki mbili kupata hiyo number, kama taarifa ulizowasilisha hazina tatizo. Hili zoezi nimelifanya!
 
wazime tu..mimi ntatumia whatsapp niliyosajili kwa line yangu nilokua natumia Dermark....nikihitaji data kununua natumia app ya Dent kununua internet budles, kwani shi ngapi bana.wanataka alama zangu za vidole ili wazicheshe!?
Hahaaa
 
leseni za udereva, vitambulisho vya kupigia kura , vitambulisho vya kazini , vyeti vya shule, vyeti vya kuzaliwa vyote hivyo vina jina halisi la mhusika..

why wasiruhusu vitambulisho vingine vitumike pia pamoja na hizo alama za vidole
Hati ya kusafiria
 
Kuzima simu hilo jambo halitekelezeki,Siku wakizima Magu kesho yake ataziwasha.......kuelekea 2020 unazimaje simu za wapiga kura?
 
Mikwara tu hakuna ata laini moja itazimwa, hao wametumia hiyo njia ya kusajili laini mpaka uwe na kitambulisho cha taifa ili watanzania tuwe na vitambulisho hivyo. Maana kama wangetoa tamko tu la kwenda kuchukua kitambulisho bila ya matumizi ya kusajili laini basi ni idadi ndogo sana ambayo ingefuatilia kitambulisho hicho. Kwanza Lugola kasema hakuna laini itakayo zimwa, jamaa wana mikwara unaweza shangaa siku hiyo ikazimwa baada ya siku moja wakaziachia.
 
Kwa mtu anayesajili simu kwa mara ya kwanza, details zake wanakuwa nazo kwenye system yao kutoka wapi?
Wana Database ambayo wanaitumia ku-share information, Serikali pamoja na wenye makampuni ya simu. Line uliyonayo ulishawahi kuisajili ila si kwa vidolle. Kitambulisho cha Taifa ulishawahi kujiandikisha nacho pia wana details zake. Hizi zote zinawekwa pamoja kwenye Database na wenye makampuni ya simu wanakuwa na uwezo wa kuzi-access, na ndiyo maana huhitaji kuwatajia majina yako. Unachohitaji ni kuwatajia namba yako ya simu na ya kitambulisho cha taifa tu basi, haya mengine wataya-confirm wao kwenye sytem yao. Cha msingi tu siku ukienda usisahau kuchukua vidole vyako vyote vya mikono yote miwili!
 
Zoezi lilipoanza la usajili NIDA walikuja kama siku 3 kazini kwetu ili tujisajili unfortunately nilikuwa safarini. Tuliokosa tukaambiwa tuende kujisajili ofisi za mkoa za NIDa, sikwenda.

kuna kipindi nilikuwa Dar nikaenda ofisi za kawe ili nijisajili, watu hawakuwa wengi sana tulikuwa kama 60 hivi, ila kadri muda unavyoenda watu wakazidi kuongezeka, hili zoezi zima ni lakidhalilishaji, mara mpange foleni mara askari wale wa Suma wawafokee, mara afisa uhamiaji ajifokeshe, sikujua mtu akiuliza maswali kwa utaratibu kitu gani kitatokea, unakaguliwa form zako kule chini unaelekezwa sehemu ya kwenda kule juu kwa ajili ya kupiga picha na kuchukuliwa fingerprints watu wazima wanakimbizana kuwahi kupanga foleni, wakichoka kusimama wanakaa chini sakafuni. Mtu ametoka ofisini kwake aje akae chini sakafuni NIDA akitoka hapo arudi ofisini kwake! Mara network hakuna mnasubiri hata masaa mawili network irudi, wahudumu mara wanakunywa chai mara ujinga gani sijui!

Nilijiuliza maswali mengi sana, hivi kwanini hii serikali haijali kabisa utu wa mtu, haijali kabisa kutopoteza muda wa mtu, zoezi zima limejaa udhalilishaji, mambo ya hovyo, process za hovyo. Nchi hii inahitaji uvumilivu sana na kuipenda sio rahisi.
 
Wana Database ambayo wanaitumia ku-share information, Serikali pamoja na wenye makampuni ya simu. Line uliyonayo ulishawahi kuisajili ila si kwa vidolle. Kitambulisho cha Taifa ulishawahi kujiandikisha nacho pia wana details zake. Hizi zote zinawekwa pamoja kwenye Database na wenye makampuni ya simu wanakuwa na uwezo wa kuzi-access, na ndiyo maana huhitaji kuwatajia majina yako. Unachohitaji ni kuwatajia namba yako ya simu na ya kitambulisho cha taifa tu basi, haya mengine wataya-confirm wao kwenye sytem yao. Cha msingi tu siku ukienda usisahau kuchukua vidole vyako vyote vya mikono yote miwili!

Hii ni perfect-world assumption, mkuu wangu! Hii dunia haijawahi na haitawahi kuwa perfect.

Kuna watu hawakuwahi kumiliki simu huko nyuma, hawajawahi kuwa na kichinjio cha mpigakura wala hawana vyeti vya kuzaliwa. Hawa details zao sahihi na za kuaminika watazipata wapi?
 
Back
Top Bottom