Simu milioni 30 hatarini kuzimwa kwa kukosa usajili wa alama za vidole

Yaani utaratibu wa Nida ni usaha kabisaaa alafu wanatishia kuzima ? Wazime tu
Ndio wanaona suluhisho. Wangefanya hivi vigezo usajili, kila mtanzania alieyefikisha 18yrs, aende na cheti Cha kuzaliwa, barua ya mtendaji, ikiwezekana vyeti vya shule, kwa ambao hawana vyeti vya kuzaliwa walazimike kubeba vyeti vya wazazi wao kuthibitisha ni watz, hii ni kwa sababu watz waliowengi wanavyeti vya kuzaliwa tungeanzia hapo, ili ambao hawana vyeti vya kuzaliwa warudi RITA kuvipata coz ni rahisi. Kuliko hii ya NIDA Mara tuambiwe malighafi hakuna, ndio mana wanaishia kutupa namba huku tukisubiria ganda la kadi OG. Simple tu usajili kigezo cheti Cha kuzaliwa..ushaur tu
 
Wanaongea tu wana jeuri hiyo? mwaka mpya fufua huu uzi!
 

Hivi kuwa na fingerprints za mtu bila kuwa na uhakika wa jina lake kutasaidia nini? Kwa mfano, mimi nikijisajili kwa kutumia fingerprints zangu, lakini kwa jina lisilokuwa la kwangu (jina bandia) na baadaye nikaitumia hiyo simu kufanya uhalifu, fingerprints zangu walizonazo zitawasaidiaje kunipata mimi kwa haraka?
 
Soma comment yangu #24 , mkuu.
Vyeti vya kuzaliwa navyo ni feki?
 
Hapana, huu usajili wewe nadhani haujaelewa vizuri. Unapojisajili kwa kutumia fingerprints, huhitaji kuwatajia majina yako. Wanazo details zako zote kwenye system yao, hadi line ya simu unayokwenda kusajili. Unachohitaji kuwa nacho ni line yako ya simu, namba yako ya kitambulisho cha taifa, pamoja na vidole vyako tu basi. Jina lako watalipata kwenye system zao, wanalo tayari. Zoezi la kusajili kwa mtindo huu halichukui hata dakika 5 linakuwa limemalizika
 
Kama wangekuwa na akili.
Ilitakiwa kila penye ofisi ya nida KUWE NA WASAJILI LAINI WA MAKAMPUNI YOTE.
pale pale unapewa namba unakwenda kwa wakala unasajili unasepa zako.
Lakini BURE KABISA
TCRA na NIDA zote ni taasisi za serikali kwanini wasikae watafute suluhisho la pamoja. Badala yake wanataka watuzimie simu zetu sisi wananchi wanyonge wa awamu ya 5.
 

leseni za udereva, vitambulisho vya kupigia kura , vitambulisho vya kazini , vyeti vya shule, vyeti vya kuzaliwa vyote hivyo vina jina halisi la mhusika..

why wasiruhusu vitambulisho vingine vitumike pia pamoja na hizo alama za vidole
 
Wazo lako linakwamisha kuongeza idadi ya viwanda kwny awamu hii.
leseni za udereva, vitambulisho vya kupigia kura , vitambulisho vya kazini , vyeti vya shule, vyeti vya kuzaliwa vyote hivyo vina jina halisi la mhusika..

why wasiruhusu vitambulisho vingine vitumike pia pamoja na hizo alama za vidole
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…