Wanafunzi wa sekondari ni wengi mno kwenye haya usemayo...Siwezi poteza muda wangu kuhusu hili zoezi najua kabisa haliwezi fanikiwa kwanza kuna kundi kubwa la vijana hawafikia miaka 18 wanamiliki simu lakini hawana vitambulisho je nao watazimiwa simu
Tatizo Kuna Jitu fulani ivi ndio limewaweka Wenye Sekta husika mtu kati kwa manufaa binafsi najua wenye sekta husika inawauma sana na ni kitu kigumu ila hawana namnaWaafrika tuna matatizo. Inapaswa kuwa wabunifu zaidi, haiwezekani line milioni 30 zipoteze mapato serikalini na kampuni za simu. Hata wenye dhamana na sekta hii wangekaa na wadau wa mawasiliano na kuhusishwa serikali za mtaa je tutumie mbinu ipi tusajili line bila usumbufu. Wenzetu nchi zilizoendelea uongozi maana yake unoe bongo ili kurahisisha maisha, Sasa NIDA imefanya maisha ya wengi kuwa magumu , process ndeefu , Mimi nilishudia mtu akiambiwa shortcut ili apate ID ya NIDA atoe 15,000 Sasa kwa asiekuwa nayo si Haki hata kidogo
Basi hapo kampuni za simu lzima ziingie hasara
Jina utabadili na sura pia utabadili?
Pathetic unafikiria kwa ubongo gani kaka?
Wewe badili jina lako ila jua wakitrace finger print tu na sura wanapata haijalishi jina unatumia Masakuu au Mwanjombe
Iko hivi, ili uweze kusajili laini ya simu kwa kutumia alama za vidole, inabidi kwanza uwe umeshajiandikisha kitambulisho cha Taifa, kwa sababu ili uweze kufanya zoezi hilo, lazima aidha uwe na namba ya kitambulisho cha Taifa au kitambulisho chenyewe. Kwa hiyo ukishajiandikisha, Database ya watu wa NIDA ndiyo itawapa details zako watu wa makampuni ya simu unapokwenda kusajili line. Na kama utafanya hivyo, maana yake utakuwa tayari una simu yako na line yako. Otherwise kama huna simu, huhitaji usajili wa alama za vidole, unachohitaji ni kitambulisho cha Taifa tu pekee. UbarikiweHii ni perfect-world assumption, mkuu wangu! Hii dunia haijawahi na haitawahi kuwa perfect.
Kuna watu hawakuwahi kumiliki simu huko nyuma, hawajawahi kuwa na kichinjio cha mpigakura wala hawana vyeti vya kuzaliwa. Hawa details zao sahihi na za kuaminika watazipata wapi?