Simu ya mwenza wako ya nini? Unajipa presha bure

Mimi siafiki kushika simu na kuanza kuichunguza na kuiwekea routine kwamba lazima uichunguze.

Bali ni kuishika unajiachia nayo kama ya mwandani na wa mwili wako. Yangu inaweza kuwa imeisha salio naweza kutumia ya mama. Kuangalia picha,n.k. mwisho wa siku utaogopa kutembea naye ukiogopa msikutane na michepuko yake
 
Daah. Sitaki kukumbuka huo ugonjwa wangu wa zamani sababu nilitaka kubaki mifupa mana nilikuwa na mawazo hasi kila kukicha kumbe nilikuwa najimaliza mwenyewe.
Duh!!...... Siamini kama mapenzi yaliwahi kukutafuna mkuu! Mimi sifa kuu ya mwanamke nitakaeoa lazima awe mwanamke ambae simpendi kwa sababu sipo tayari kufa magonjwa ya pressure, kisukari na kiharusi kisa wivu wa mapenzi!!
 
Inategemea kama mmewekeana utaratibu huo fine, na kama mna utaratibu huo unafikiri simu za mazabe zitaingia, thubutu, kutakuwa na line nyingine anayoijua yeye na Mola wake.
 
But deep down you know he's not loyal, sio?
No If he is noto loyal there some other ways to find out not on his phone, mind you if he has never invited me to use his phone how can I invite myself?
 
Exactly uncle. Huichunguzi ila unakuwa huru nayo
 
Hahaa me hiyo siku ntakayokufa kwa presha kisa kushika simu ndo utakuwa mwisho wa kushika simu. Me simu ntaishika tu anytime nikijisikia. Privacy ndo mdudu gani?
Umeona tatizo watu tunajiendekeza.Kuishika au kutoishika hakutabadilisha kitu.Kama nikuchepuka atachepuka tu manake hiyo ni tabia simu ishikwe au isishikwe.Tuendelee zetu kuzishika mwaya.
 
Umeona tatizo watu tunajiendekeza.Kuishika au kutoishika hakutabadilisha kitu.Kama nikuchepuka atachepuka tu manake hiyo ni tabia simu ishikwe au isishikwe.Tuendelee zetu kuzishika mwaya.
Teh tuzishike tu mwenzangu. Sio guarantee ya kuwa hachepuki ila sina sababu ya kutoishika pia
 
Exactly uncle. Huichunguzi ila unakuwa huru nayo
Ndiyo maana matatizo ya ndoa yamezidi. Sasa kama mnawekeana password za simu wanandoa je za bank.

Ukiachana na yangu, mzee na mama ndiyo ndoa ya demo kwangu. Wanaishi kwa raha hadi unapenda. Mama ali(kitaka) simu ya mzee anachukua bila wasiwasi mzee vivyo hivyo pia. Password za bank hadi leo zao wote nazijua na wote kila mmoja anaijua ya mwenzake.

Ndoa yenye siri siri za kishamba huwa ndiyo hizi zinazopumulia mipira tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…