Simu za Huawei zinauzika balaa ulaya Samsung akina Samsung hoi


Soma hiyo link hapo,Trump mwaka jana alisign sheria ya kuzuia matumizi ya bidhaa za Huawei na ZTE nchini USA.
 
Huo ni uongo mweupee hata dogo wa nasary atakupinga

Hivi ushawahi shika hiyo simu ya 6GB achilia mbali kutumia??
Mkuu mimi simu ya ram gb 6 nimetumia.... Pia na iphone ya ram gb 3 nimetumia na ndo naitumia... Ufanisi wake wa kazi ni tofauti sana ram 6 ya android ishawai niletea (unfortunately application stopped) ila hio taabu kwenye iphone ya gb 3 cjawai iona... Pia kwenye masasisho ya version za os zao unaona kabisa tofauti ya version mpya na ya zamanii... Android phones ni nzuri sababu unakua na uhuru wa mambo yako lakini iphones ni simu nzuri ever....
 
Mbona ndiyo maelezo yale yale niliyoyatoa, kwamba Trump alikuwa anazuia bidhaa za Huawei kutumika serikalini marekani na kwenye taasisi za serikali lakini siyo kwa mtu mmoja mmoja labda nifafanue hivi.
Unajua unaweza soma kiingereza na usielewe chote ukawa unadaka neno moja moja .hapo utapata tafsiri tofauti na mwandishi.

Kwanza nikwambie yote hayo ni kwa sababu ya ushindani wa kibiashara kwa Huawei wako juu kuzidi makampuni ya hapo, mfano iPhone nk.
Wamarekani wananunua Huawei kwa wingi sana, na kabla ya hapo Huawei ilikuwa inakubalika mpaka serikali ya marekani na taasisi zake za kiusalama kwa kiwango kikubwa sana.
 
Hakuna kampuni la simu marekani linalouza simu za Huawei punguza ubishi man,waliingia mkataba na ATNT, Verizon pamoja na best buy Ila pressure ya serikali ikasababisha hayo makampuni yajitoe. Wewe nitajie kampuni gani ya simu inayouza simu za Huawei.
 
Hakuna cha matumizi mkuu toka ni nunue Huawei Sijawahi kupata tatizo hilo na matumizi yake naona nimezidisha zaidi
Toka nitumie samsung mwaka wa 5 huu na sijawahi ona virus kwenye simu yangu.
 
Embu acha ku post pumba,hivi unajua kuna simu za HUAWEI zina bei sawa au zaidi ya Samsung ambazo hapa bongo watu wengi hawawezi ku afford?HUAWEI ni brand kubwa,brand ambayo haiuzi Europe ni TECNO
Aiseee chalii yangu jitahidi kuwa mpole. Kwanza hupo state gani? Ebu agizia chochote hapo ntalipia. Najua trump kawaminya sana kwenye food stumps na government handouts

Fanya kazi
 
Huawezi zinazouzwa ulaya ni tofauti zinazouzwa africa... in terms of quality.... sisi tunanunua simu zimeandikwa for East africa only....
Hawawezi kukuelewa wabongo huwawei anauza sana simu kuanzia canada,England na sasa USA kishaanza kushika soko why anauza sana kuna kitu ambacho wengi hawajakijua kuhusu huawei hawa ni wataalam katika sekta ya internet simu zao zina speed sana ya internet,Zaidi ya yote taarifa za kiinterejensia ni kwamba huawei kishagundua 5G technology ambayo ina speed pengine kushinda akili za binadamu hii imeleta shida kwa Marekani maana hayuko tayari technolojia hii itoke kwa sasa.Sisi tunaletewa cheap phone tofauti kabisa na zunazoenda ulaya.
 
Marekani alikuwa anategemea kutoa matumizi ya 5G 2021 Ndyo matumizi yake yawe moja kwa moja kwa wananchi ila Huawei yeye kashaanza kuweka minara Canada na nchi nyingine za ulaya ndyo maana Marekani akaona aweke burn bidhaa zake na kumkamata mtoto wa mmiliki wa kampuni kwa kisingizio cha kuiuzia Irani vifaa vya teknolojia toka marekani lakini hii yote ni figisu za kibiashara. Waafrika wengi wanaichukulia poa Huawei ila ni kampuni kubwa sana duniani na ukaribu na serikali ya China ndyo unasababisha viongozi wengi wa ulaya na Marekani kutoamini bidhaa zake ila ni kampuni kubwa sana duniani kuliko ata Samsung ambayo wengi wanaisemea
 
Sijafahamu kitu japo sina wazimu wa kukurupukia simu na declare ni muumini wa sammy owning a s8+na sijawahi nuna kwa hii simu.
Back to topic nimefanya compariso ya galaxy s 10 na huawei p30 ukiondoa mp kwenye camera naona specs za sammy zinatisha sasa sijui mleta hoja katumia ufananishi upi kuja na hitimisho kuwa huawei ni nyoko?
Nilitembelea gsm arena
 

Galaxy S10 ina tatizo la battery yake kuisha mapema.

Pia hii simu imeingizwa katikati ya Samsung S10e na S10Plus ili kukidhi soko la vijana khasa wale wapendao kuangalia video za Netflix na YouTube.

Hiyo ni kutokana na upana wa kioo chake wa 6.1 inch.


Samsung galaxy S10

Ni simu ya bei nafuu sana.

Nafahamu utakuwa umeipenda Samsung S10 kwa sababu ina radio ya FM frequency wakati Huawei haina radio na pia unaweza kuweka SIM cards mbili yaani Dual SIM wakati Huwawei huwezi kufanya hivyo.

Pia Card slot ya Huawei inatumika moja kwa memory card na Sim Card.

Huawei ina RAM 6 GB hivyo kuwa na kasi ya uchambuzi wa kazi mbalimbali unapotumia na pia inakuwezesha kufanya editing ya picha zako za kawaida na zile za video.

Halafu uki-charge simu ya Huawei inachukua saa 1 tu na usei kuwa na bttery fully charged.


Huawei P30


Ila kwenye general performance Samsung S10 na Huawei P30 zinalingana pamoja na bei zake madukani.
 
Unfortunately action huletwa na android version sio ram
 
Iphone ipo on a league of its own. Kwanza materials zinazotumika kutengeneza Iphone ni top-notch. Huwezi kulinganisha na simu za kichina hata Huawei. Pili IOS ni unique siyo kama Android. Binafsi natumia Iphone XR baada ya kuwa mteja wa simu za Samsung za bei mbaya kama Samsung Note8 ambayo ilkuwa simu yangu ya mwisho ya android iliyoibiwa na wakaiflash na kuendelea kuitumia bila mimi kuweza kui lock na kui trace pamoja na kuwa na google account inayo onyesha simu ilipo at all times. Iphone ikiibiwa unai block hakuna mtu ataweza kui flash.
 
Nina Huawei p9 ila sijajua namna ya ku switch users. Mwenye uelewa tafadhar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…