Simu za mkopo pasua Kichwa

Simu za mkopo pasua Kichwa

Mikopo inafilisi,anayefaidika na mikopo ni mkopeshaji na siyo mkopaji,ukiona mkopaji amefaidika na mkopo ujue kuwa alikuwa na mtaji wake kabla ya kukopa,ndio maana hata wakopeshaji hawatowi mali zao kama mtaji,wanatoa kwa mtu mwenye mtaji wake kwanza.
 
Sasa mkuu hiyo sio kidogo ni pasuu kwa pasuu
Kuna kitu kinaitwa vigezo na masharti kuzingatiwa. Yaani unaambiwa bei ya simu kwa Cash,then unaambiwa bei ya simu kwa mkopo then unapima ukiona kubwa unaenda kwenye maduka yanayobandika ikiwa huna uwezo wa cash.
 
Mikopo inafilisi,anayefaidika na mikopo ni mkopeshaji na siyo mkopaji,ukiona mkopaji amefaidika na mkopo ujue kuwa alikuwa na mtaji wake kabla ya kukopa,ndio maana hata wakopeshaji hawatowi mali zao kama mtaji,wanatoa kwa mtu mwenye mtaji wake kwanza.
Kivipi? Una biashara mtaji ni 50M ukaamua upanue biashara ili uweze kuagiza mizigo China, unaenda bank kukopa 50M shida iko wapi hapo?
 
Kivipi? Una biashara mtaji ni 50M ukaamua upanue biashara ili uweze kuagiza mizigo China, unaenda bank kukopa 50M shida iko wapi hapo?
Ndio maana nikasema kuwa wanaofanikiwa ni wale ambao wanakopa kwa ajili ya kuongezea kwenye mitaji yao lakini wanaokopa kama mtaji wao wakuanzia huwa wanaishia kufilisika,kwanza hata wakopeshaji hawakubali kukukopesha ni mpaka uwe na kitu chako kwanza.
 
Nunua ila huyo mdada muuza simu atakukata jicho hilo mwanaukomeeee
 
Ukikopa kutoka Samsung wenyewe haina bei ila wabongo ndio tatizo ni kama hawaelewi wanacho kifanya ila njia ya kuuza kwa kukopesha inalipa zaidi ya cash
 
Juzi tu nimemaliza mkopo wa simu, sio mchezo, nimekauka kisawasawa. Nipo kwenye mlo wa matembele angalau damu iongezeke. Wamenikaribisha kwenye mkopo wa bodaboda, nimewaambia hawataniona tena.
 
Haki ya nani, Leo nimeingia duka la simu za mikopo, nimekuta simu ya 280k kesh. kwa miez 12 ni 420k yani nusu kwa nusu duh. Aisee.
Si huwa mbakimbia na hela za mikopo ya MGODI,NIVUSHE etc. Hizi simu hakuna uwezekano wa kukimbia mkaacha deni?
 
Back
Top Bottom