Abdallahking
JF-Expert Member
- Mar 19, 2018
- 3,985
- 10,840
Simulizi: AKWELINA
Mwandishi: RUVULY DE FINISHER
Imeletwa kwenu na: BURE SERIES
SEHEMU YA 1 YA 50
""" Mke wangu unajua hii inchi yetu ina mambo mengi mno ambayo tukiyaangalia kwa macho tunaona ya kawaida sana lakini kwa mwenye akili na mwenye mtazamo wa kufikiria mbali lazima atatambua kwamba maisha ya sisi tulio vijijini tena mpakani na nchi jirani tunaishi kama swala ndani ya msitu wenye simba wengi alafu wananjaa Kali mno unafikiri tutapona kweli , hivi mke wangu kwa elimu niliyonayo Mimi unafikiri mimi ni wa kuishi maisha kama haya kweli !! nina elimu kubwa sana mke wangu lakini leo hii tunaishi maisha ya kimaskini zaidi ya masikini wenyewe kula kwetu shida , tupo kwenye nyumba ya nyasi mvua ikinyesha tunalala tumesimama lakini yote kwa yote nakushukuru sana mke wangu kwa mapenzi ya dhati unayonipa pamoja na ugumu wa maisha haya lakini bado upo na Mimi, nakupenda mke wangu nakupenda mno haya mke wangu ingia ndani tukalala.
Yalikuwa ni maneno ya #KAKINGA akimueleza mke wake #MONNA kutokana na ugumu wa maisha waliokuwa nayo pamoja na elimu kubwa aliyojaliwa Kakinga lakini bado maisha kwake yalikuwa ni duni sana Kakinga alimchukua mke wake wakaingia ndani. Usiku ulizidi kusonga mbele masaa yalikatika, ilipofika saa saba usiku Monna alibanwa na haja ndogo ( mkojo ) akamuamsha mume wake ili ampeleke chooni kwakua ulikuwa ni usiku mnene, Monna alijaribu sana kumwamsha mume wake lakini kakinga huwa akilala kuamka ni ngum sana, Monna alizidiwa na mkojo ikabidi achukue taa akatoka nje .
Monna alikwenda hadi chooni akajisaidia , alipomaliza kujisaidia Monna akachukua taa lake akarudi alipokuwa anarudi ndani Monna kabla hajafika ndani alisikia mbwa wao anabweka kuashiria kuna kitu kibaya ambacho hakipo mbali na mazingira ya nyumba yao. Monna alichunguza sana wakati anachunguza ghafla alitokea mama mmoja akiwa ametapaa damu mwili mzima , yule mama alikuwa amebeba mtoto mdogo sana, Mama yule alipomuona Monna alimfuata akamuomba kwa kusema :-
""""" Binti yangu naomba saidia maisha ya mtoto wangu huyu Mimi sio wa kupona tena nakufa hali yangu sio nzuri mchukue Mtoto huyu alafu nenda nae mbali tafadhali nakuomba binti yangu nisaidie .
Monna alikuwa bado ameduwaa kwa mshangao, Yule mama akaondoka chini akapoteza maisha mtoto akaanza kulia baada ya kuondoka chini akiwa katika mikono ya mama yule , Monna alimchukua yule mtoto, Mtoto aliendelea kulia sauti ya mtoto yule ilisafiri kwa kiasi kikubwa ndani ya msitu ule, Monna akiwa anamtuliza mtoto alisikia watu wakisema :-
"" Jamani huyu huku namsikia mtoto analia upande huu """"
Monna alikimbia na mtoto kurudi nyumbani , wale watu walifuata sauti ile wakamkuta mama wa mtoto ameshakufa, wakasikia sauti ya mtoto ikiendelea kulia wakafuata sauti ile, Monna alikimbia hadi nyumbani kwake kwakua hakuwa mbali na nyumba yake aliingia ndani akamziba mtoto mdomo , Muda mchache wale watu wakafika eneo lile wakasema :-
""" Hajaenda mbali huyu na inataikiwa na yule Mtoto achinjwe hastahili kubaki hai tawanyikeni sehemu zote mtafuteni sawa """
Wale watu walikubaliana wakaondoka, Monna alimshukuru sana mungu, Monna akamfunua nguo yule mtoto akakuta kuna kitabu kidogo pamoja na kitambaa kilichofungwa, Monna alihisi damu katika mikono yake akaitazama ile damu ilipotokea akaona ile damu imetoka mgongoni mwa mtoto, Monna akamgeuza yule mtoto akaona mtoto ameandikwa neno #AKWELINA katika mgongo wake. Monna alishangaa sana kutokana na kuona mtoto alivyofanyiwa ukatili kama huo kwa sababu mtoto aliandikwa jina lile kwa kitu chenye ncha kali. Monna alimwamsha mume wake akamueleza yote yalimtokea mume wake akasema:-
KAKINGA ?? Mke wangu mbona unatafuta matatizo Wewe Mtoto huyu humfahamu alafu unaona kabisa jina hili lilivyo andikwa kwa kutumia kisu si kisu kabisa hiki sasa huyu mtoto akifa hapa au hao watu wakairudi tena utafanyaje ?
MONNA ?? Mume wangu eeee sasa Mimi ningefanyaje lakini mbona wanilaumu kiasia hicho wakati nimetoa msaada tu .
Kakinga aligombana sana na mke wake usiku kucha. Asubuhi na mapema palipokucha walitokea watu waliovaa nguo za kijeshi katika makazi yale wakawaita watu wote wanaoishi mazingira yale,
ITAENDELEA