Simulizi: Akwelina

Simulizi: Akwelina

Abdallahking

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2018
Posts
3,985
Reaction score
10,840
RUVULY DE FINISHER = AKWELINA.jpg


Simulizi: AKWELINA
Mwandishi: RUVULY DE FINISHER

Imeletwa kwenu na: BURE SERIES

SEHEMU YA 1 YA 50


""" Mke wangu unajua hii inchi yetu ina mambo mengi mno ambayo tukiyaangalia kwa macho tunaona ya kawaida sana lakini kwa mwenye akili na mwenye mtazamo wa kufikiria mbali lazima atatambua kwamba maisha ya sisi tulio vijijini tena mpakani na nchi jirani tunaishi kama swala ndani ya msitu wenye simba wengi alafu wananjaa Kali mno unafikiri tutapona kweli , hivi mke wangu kwa elimu niliyonayo Mimi unafikiri mimi ni wa kuishi maisha kama haya kweli !! nina elimu kubwa sana mke wangu lakini leo hii tunaishi maisha ya kimaskini zaidi ya masikini wenyewe kula kwetu shida , tupo kwenye nyumba ya nyasi mvua ikinyesha tunalala tumesimama lakini yote kwa yote nakushukuru sana mke wangu kwa mapenzi ya dhati unayonipa pamoja na ugumu wa maisha haya lakini bado upo na Mimi, nakupenda mke wangu nakupenda mno haya mke wangu ingia ndani tukalala.



Yalikuwa ni maneno ya #KAKINGA akimueleza mke wake #MONNA kutokana na ugumu wa maisha waliokuwa nayo pamoja na elimu kubwa aliyojaliwa Kakinga lakini bado maisha kwake yalikuwa ni duni sana Kakinga alimchukua mke wake wakaingia ndani. Usiku ulizidi kusonga mbele masaa yalikatika, ilipofika saa saba usiku Monna alibanwa na haja ndogo ( mkojo ) akamuamsha mume wake ili ampeleke chooni kwakua ulikuwa ni usiku mnene, Monna alijaribu sana kumwamsha mume wake lakini kakinga huwa akilala kuamka ni ngum sana, Monna alizidiwa na mkojo ikabidi achukue taa akatoka nje .



Monna alikwenda hadi chooni akajisaidia , alipomaliza kujisaidia Monna akachukua taa lake akarudi alipokuwa anarudi ndani Monna kabla hajafika ndani alisikia mbwa wao anabweka kuashiria kuna kitu kibaya ambacho hakipo mbali na mazingira ya nyumba yao. Monna alichunguza sana wakati anachunguza ghafla alitokea mama mmoja akiwa ametapaa damu mwili mzima , yule mama alikuwa amebeba mtoto mdogo sana, Mama yule alipomuona Monna alimfuata akamuomba kwa kusema :-



""""" Binti yangu naomba saidia maisha ya mtoto wangu huyu Mimi sio wa kupona tena nakufa hali yangu sio nzuri mchukue Mtoto huyu alafu nenda nae mbali tafadhali nakuomba binti yangu nisaidie .



Monna alikuwa bado ameduwaa kwa mshangao, Yule mama akaondoka chini akapoteza maisha mtoto akaanza kulia baada ya kuondoka chini akiwa katika mikono ya mama yule , Monna alimchukua yule mtoto, Mtoto aliendelea kulia sauti ya mtoto yule ilisafiri kwa kiasi kikubwa ndani ya msitu ule, Monna akiwa anamtuliza mtoto alisikia watu wakisema :-



"" Jamani huyu huku namsikia mtoto analia upande huu """"



Monna alikimbia na mtoto kurudi nyumbani , wale watu walifuata sauti ile wakamkuta mama wa mtoto ameshakufa, wakasikia sauti ya mtoto ikiendelea kulia wakafuata sauti ile, Monna alikimbia hadi nyumbani kwake kwakua hakuwa mbali na nyumba yake aliingia ndani akamziba mtoto mdomo , Muda mchache wale watu wakafika eneo lile wakasema :-



""" Hajaenda mbali huyu na inataikiwa na yule Mtoto achinjwe hastahili kubaki hai tawanyikeni sehemu zote mtafuteni sawa """



Wale watu walikubaliana wakaondoka, Monna alimshukuru sana mungu, Monna akamfunua nguo yule mtoto akakuta kuna kitabu kidogo pamoja na kitambaa kilichofungwa, Monna alihisi damu katika mikono yake akaitazama ile damu ilipotokea akaona ile damu imetoka mgongoni mwa mtoto, Monna akamgeuza yule mtoto akaona mtoto ameandikwa neno #AKWELINA katika mgongo wake. Monna alishangaa sana kutokana na kuona mtoto alivyofanyiwa ukatili kama huo kwa sababu mtoto aliandikwa jina lile kwa kitu chenye ncha kali. Monna alimwamsha mume wake akamueleza yote yalimtokea mume wake akasema:-



KAKINGA ?? Mke wangu mbona unatafuta matatizo Wewe Mtoto huyu humfahamu alafu unaona kabisa jina hili lilivyo andikwa kwa kutumia kisu si kisu kabisa hiki sasa huyu mtoto akifa hapa au hao watu wakairudi tena utafanyaje ?



MONNA ?? Mume wangu eeee sasa Mimi ningefanyaje lakini mbona wanilaumu kiasia hicho wakati nimetoa msaada tu .



Kakinga aligombana sana na mke wake usiku kucha. Asubuhi na mapema palipokucha walitokea watu waliovaa nguo za kijeshi katika makazi yale wakawaita watu wote wanaoishi mazingira yale,

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 2 YA 50

Monna na Mume wake nao wakaenda katika mkutano huo , baada ya wanaichi kufika alisimama kiongozi wao akasema :-



"""" Wanaichi wa eneo hili mimi mkuu wa majeshi katika inchi hii tunashida kubwa sana na ndio maana tunapita kila sehemu tuawatangazia wanaichi wote kwamba kuna Mtoto amepotea , mtoto huyo nyuma ya mgongo wake ameandikwa jina linalosomeka AKWELINA kwa yeyote aliyemuona Mtoto huyo atapata pesa kiasi cha shilingi bilioni moja. Je kuna yeyote aliyemuona mtoto huyo ?



Kakinga aliposikia fedha nyingi kama zile aliingiwa na tamaa akajitokeza mbele ya kiongozi yule kisha akasema :-



KAKINGA ?? Kiongozi Mimi...........................







KAKINGA ?? Kiongozi Mimi nina swali naomba kuuliza tafadhali .



KIONGOZI ?? Uliza kijana .



KAKINGA ?? Tunaomba picha ya huyo mtoto ili siku tukimuona iwe rahisi kumtambua na kwanini mtoto huyo ameandikwa jina hilo la AKWELINA katika mgongo wake ?



KIONGOZI ?? Picha zipo tutawaonesha wananchi wote na kuhusu historia ya mtoto huyo sio rahisi kuifahamu wewe mwanaichi wa kawaida kutokana na sheria ya nchi inavyosema sawa kijana ?



KAKINGA ?? Sawa kiongozi .



KIONGOZI ?? Vizuri sana sasa tutawapatia mawasiliano ili siku yeyote au kwa yeyote ataemuona ajitahidi kuwasiliana na sisi tunaomba ushirikiano wenu na yeyote ataebainika kwamba kamficha Mtoto huyo adhabu yake itakuwa kali isiyo na msamaha .



Kakinga akafikiria sana suala hilo akatamani kusema ukweli lakini nafsi yake ikakataa wakati Kakinga yupo katika dimbwi zito la mawazo Wanajeshi waligawa vipeperushi kwa wingi kisha wakaondoka, Monna akamchukua mume wake wakarudi nyumbani, walipofika nyumbani walimkuta mtoto analia sana , Monna alimchukua mtoto yule akajaribu kumnyonyesha kitendo hicho kilimfurahisha sana kakinga akamwambia mke wake (Monna) :-



KAKINGA ?? Mke wangu huwezi kutoa maziwa kwa sababu maziwa huwa yanatengenezwa ukiwa na ujauzito sasa Wewe ujauzito unao ?



MONNA ?? Heeeeeh Mimi nilikuwa sifahamu mume wangu sasa nifanyaje huenda huyu mtoto ananjaa sana , inabidi nikanunue maziwa ya ng'ombe au unasemaje ?



KAKINGA ?? Nenda kanunue mke wangu hilo ni jambo la busara sana lakini kwanini mtoto huyu anatafutwa sana na wanajeshi si hatari hii au aliyekupa mtoto huyu alikuwa ni mtu mbaya ndani ya nchi yetu ? Ninahofu mke wangu kwa sababu wale ni walinzi wa nchi hii huyu mtoto asiwe mtoto wa Raisi ohoo itakuwa hatari .



MONNA ?? Sijui bana na kwanini yule mama aliniambia nimtunze mtoto wake hiyo ndio hofu yangu huenda ni kweli usemayo lakini sina imani na wale wanajeshi Mume wangu naomba tumlee huyu mtoto hayo mengine anajua mungu .



KAKINGA ?? Mmmh haya kamletee maziwa na ununue na dawa uje tumuekee alipoumia .



Monna alichukua pesa akaenda kununua vitu alivyo hitaji baada ya muda Monna alirudi akachemsha maziwa akampatia mtoto, katoto kalikuwa na njaa sana kalikunywa maziwa kwa kasi sana kaliposhiba , Monna akachemsha maji akamuogesha, baada ya kumuogesha Monna alimpatia kakinga yule mtoto ili ampake dawa Sehemu alizoumia, kakinga wakati anampaka dawa mtoto roho ilimuuma sana akasema :-



KAKINGA ?? Mke wangu wanadamu wanaroho mbaya sana yaani mtoto mdogo kama huyu wamempatia majeraha kama haya daah aliyefanya hili tukio mungu anamuona, alafu mke wangu kuanzia leo mtoto huyu ataitwa jina hili hili aliloandikwa mgongoni kwake kwa sababu huenda hili jina linamaana kubwa kwake au unasemaje mke ?



MONNA?? Upo sawa Mume wangu kipenzi nahisi jina hili litalinda kumbukumbu zake siku sijazo .



Baada ya Mwaka mmoja maisha yalikuwa yenye furaha na upendo zaidi kwa kakinga na Monna baada ya kumpata Akwelina katika maisha yao walimpatia malezi bora na upendo zaidi, Monna alimpenda sana Akwelina, Siku baada ya siku watu wa maeneo aliopo mtoto Akwelina walimpenda sana kwakua Akwelina alikuwa binti mzuri sana, Monna hakuwa na kipingamizi kwa yeyote aliyehitaji kuondoka na mtoto, Upendo wa Monna kwa majirani zake ulimfanya asahau kuwa mtoto yule anatafutwa sana na Serikali.
 
SEHEMU YA 3 YA 50



Monna na mume wake kakinga waliendelea kuishi maisha hayo bila wasiwasi wowote, Siku moja majira ya asubuhi Monna alitembelewa na rafiki yake kipenzi ZILPA , Zilpa alimkuta Monna anafua nguo akiwa na mtoto mgongoni kwake, Monna akamkaribisha rafiki yake kipenzi akampatia kiti rafiki yake, Monna akaendelea kufua nguo wakiwa wanazungumza na rafiki yake .



Maongezi yaliendelea kwa muda akwelina akaanza kulia Zilpa akamchukua Akwelina ili amsaidie rafiki yake aweze kufua nguo, Zilpa alipokuwa anamtuliza Akwelina nguo ya juu aliyovaa Akwelina ilipanda juu kidogo, Zilpa alistuka baada ya kuona maneno baadhi yameandikwa mgongoni kwake, Zilpa akatamani kuona maneno aliyoandikwa Akweli Zilpa akazidi kumfunua akakuta jina limeandikwa AKWELINA katika mgongo wa mtoto Zilpa akastuka mno , Monna alipomaliza kufua nguo aliingia ndani kuchukua maji aliporudi nje Monna hakumuona Zilpa pamoja na mtoto Monna alidondosha ndoo ya maji chini aka...







Monna alidondosha ndoo ya maji chini akatoka nje ya nyumba yao akatazama pande zote hakumuona Zilpa, Monna alianza kulia akiwa anakimbia hovyo Kilio cha Monna kiliwastua majirani walijitokeza kwa wingi wakashangaa sana kumuona Monna anakimbia ovyo akiwa anamwita Zilpa, Monna alizunguka kijiji kizima toka asubuhi hadi majira ya saa sita mchana bado Monna hakufanikiwa kumuona Zilpa, Monna alirudi nyumbani masikini akiwa amechoka sana Roho ilimuuma sana Monna nguvu zilimuisha kichwa kikamuuma sana, Monna akajivuta taratibu taratibu hadi nyumbani kwake , Monna alipofika nyumbani aliingia ndani akaanza kulia kwa uchungu, Kilio cha Monna kiliendelea hadi majira ya usiku bado Monna alikuwa analia .



Siku hiyo Kakinga alichelewa sana kurudi nyumbani kutokana na shughuli zake kakinga akiwa kazini alifuatwa na rafiki yake , Rafiki huyo alipofika kwa Kakinga akashanga kumuona Kakinga bado anafanya kazi Rafiki wa Kakinga akasema:



RAFIKI: Kakinga ndugu yangu yaani bado unafanya kazi hadi muda huu inamaana huoni giza hili ?



KAKINGA: Naliona lakini siwezi kulaza kazi hii inabidi niimalize kabisa ili kesho nishike kazi nyingine si unajua pesa sina kaka , Nivumilie kidogo nimalize kazi hii alafu tunaondoka nyumbani sawa ?



RAFIKI: Sawa lakini muda umekwenda kaka kumbuka kijiji chetu kimechafuka siku hizi sasa wewe poteza muda hapa ukute mke wako amebakwa kama Maria mtoto wa mwenyekiti alivyobakwa .



KAKINGA: Aaah weee wambake nani mke wangu mimi ?? Haha sio rahisi mke wangu mwenyewe komando wewe unamuonaje ??????



RAFIKI: Haya wewe shauri yako .



KAKINGA: Kuwa na amani bwana mkubwa kazi imeisha hii sasa hivi tunarudi nyumbani ondoa hofu .



Baada ya dakika ishirini kakinga akafanikiwa kumaliza kazi yake akabadili nguo kisha wakarudi nyumbani, Safari haikuwa ndefu sana walipofika mtaa wa nyumbani Rafiki wa Kakinga akamuacha kakinga akaenda nyumbani kwake nae Kakinga akaenda nyumbani kwake. Kakinga alipokaribia eneo la nyumbani akasikia sauti ya Mke wake kipenzi toka ndani ikilalamika kwa kutoa kilio cha hudhuni mno kakinga akastuka mno akatupa vifaa vya kazi chini alikurupuka mbio hadi ndani akamkuta Monna amekaa chini akiwa hovyo hovyo kakinga alimuuliza mke wake akiwa na hofu :-



KAKINGA: Kuna nini mke wangu umegongwa na nyoka au umebakwa ?



Monna hakujibu chochote akazidisha kilio kwa hasira Kakinga akazidi kuchanganyikiwa akauliza tena: Si ninakuuliza wewe umepatwa na nini mbona hunijibu Umebakwa sio ?



MONNA: Hapana mume wangu sijabakwa mimi aaaah .



Kakinga akapua kwa nguvu kisha akaikaa chini akasema: Tatizo nini Mke wangu au unaumwa ?



MONNA: Akwelina wangu jamani kaibiwa Mume wangu ????



KAKINGA: Haaaaah !! ?? Unasemaje Akwelina wangu kaibiwa ? Unajua sijakuelewa na sitaki matani kabisa, Unajua kiasi gani ninavyompenda mtoto wangu hebu acha kuniambia hizo simulizi zako sipendi utani Mke wangu niambie ukweli ?



MONNA: Kweli mume wangu Akwelina kaibiwa na Zilpa asubuhi ya leo nilikuwa nafua wakati huo nilikuwa nimembeba Akwelina Mgongoni Zilpa akaja kunitembelea ndio akaniomba anisaidie kumtuliza Akwelina kwa sababu alikuwa analia sana nikampatia kwa sababu namuamini sikuwa na hofu juu yake nikaingia ndani kuchukua maji nilipotoka nje sikumkuta tena Zilpa

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 4 YA 50

pamoja na Akwelina wangu jamani mimi nahisi kufa Mume wangu ??



KAKINGA: Zilpa anatafuta Vita na mimi nisubiri hapa hapa naenda nyumbani kwao Zilpa nahisi hawanifahamu vizuri pumbafu .



Kakinga alichukua Panga akatoka nje akiwa na hasira sana, Monna alijaribu kumziwia kakinga lakini alishindwa, Kakinga alikimbia mno bila kuchoka kutokana na umbali ilimchukua muda mrefu kakinga kufika nyumbani kwao na Zilpa, Japo palikuwa na umbali mrefu kakinga alijitahidi kukimbia bila kuchoka , kakinga alipokaribia nyumba anayoishi Zilpa alishangaa kuona wanajeshi wamezunguka nyumba yote, Kakinga alisimama na kujificha nyuma ya Nyumba nyingine.



Kakinga alijiuliza maswali mengi sana baada ya kuona wanajeshi wametapakaa eneo analoishi Zilpa lakini akakosa majibu, Kakinga akanyemelea ( kutembea taratibu ) kuifuata nyumba anayoishi Zilpa, kakinga alipofika karibu alichungulia akamuona Zilpa anampatia Mtoto yule kiongozi aliyetoa tangazo yule kiongozi akamvua nguo zote Akwelina akamkagua mgongoni alipoona lile jina akachukua begi kubwa akampatia Zilpa, Wakati huo Akwelina alikuwa analia sana kilio cha Akwelina kilimpatia maumivu makali sana kakinga .



Baada ya muda kidogo Wanajeshi waliondoka na Akwelina , Kakinga alishindwa afanya nini, Zilpa alibaki pale nyumbani na begi lake, Baada ya wanajeshi kuondoka Kakinga akamfuata Zilpa akamkuta akiwa na familia yake , Kakinga alianzisha vurugu kali Kaka wa Zilpa wakamchangia Kakinga wakamshinda nguvu wakampiga sana alafu wakambeba wakamtupa mbali na Nyumba yao, Kakinga alirudi nyumbani akiwa amevimba sura na nguo zake zimechanwa chanwa , Kakinga alipofika nyumbani kwake alikaa nje akawa analia kwa hasira Monna akatoka nje haraka baada ya kumsikia mume wake analia, Monna alimkuta kakinga yupo hovyo hovyo Monna akauliza :



MONNA: Umepatwa na nini mume wangu mbona upo hivyo ?



KAKINGA: Zilpa mshenzi sana mke wangu kampeleka Akwelina kwa wale wanajeshi na wamemchukua mtoto wetu masikini ?? .



MONNA: Mungu wangu nakufa mimi masikini Akwelina wangu daaah najuta Mimi Zilpa mungu atakulipa nakuchukia sana mbwa wewe ??



KAKINGA: Sikubali mke wangu, Akwelina wangu hawezi kwenda mbali na Mimi kwa hali yeyote sikubali nakuapia mke wangu sikubali lazima nitamrudisha katika mikono yetu subiri uone Monna ??



Kakinga na monna walikaa nje ya nyumba yao hadi asubuhi. Siku iliyofuata asubuhi wale wanajeshi waliwaita wananchi wote wa eneo lile, kiongozi wao akasimama kisha akasema :



KIONGOZI: Tunashukuru sana kwa ushirikiano wenu nimewapenda sana watu wa eneo hili hususa binti mmoja anayeitwa ZILPA yeye katusaidia kumpata mtoto tuliyekuwa tunamtafuta kwa muda mrefu, leo tutalala katika eneo hili na tutaweka sherehe usiku wa leo ili tufurahi kwa pamoja kwa hiki mlichofanya kwetu nawapongeza sana wananchi wetu .



Baada ya kiongozi kumaliza mazungumzo na wananchi, kiongozi aliwapatia Wanajeshi kazi ya kutafuta sehemu itayofanyika sherehe hiyo majira ya usiku, Wanajeshi hawakupoteza muda wakashirikiana na Wananchi wakatengeneza eneo kubwa sana kwa ajili ya sherehe hiyo. Baada ya masaa kadhaa jua lilizama giza nene likatawala anga, Usiku huo ulikuwa usiku wa furaha kwa wananchi wengi lakini usiku huo ulikuwa mbaya sana kwa Monna na mume wake Kakinga, Kakinga akiwa na mke wake nyumbani kwao alifikiria sana kisha akamwambia Mke wake :



KAKINGA: Mke wangu andaa vitu vyako muhimu vyote usisahau na vile vitu ulivyomkuta navyo Akwelina, naondoka naenda huko kwenye sherehe yao narudi na Akwelina hapa kwa hali yeyote siwezi kukubali .



MONNA: Hapana mume wangu watakuua wale watu hawana huruma kabisa mume wangu tafadhali usiende ukifa mimi nitaishi vipi bila wewe jamani usiende Mume wangu .



KAKINGA: Mungu atanisaidia kwa hilo ninaamini kabisa wale sio watu wazuri kwenye maisha ya yule mtoto.



Kakinga alipata ujasili wa ajabu sana akaondoka moja kwa moja hadi katika sherehe, alipokaribia hema alipokuwepo kiongozi wao akajificha katika majani, kakinga akiwa amejificha alimuona mwanajeshi mmoja anakuja eneo alilokuwepo katika alitetemeka akatulia kimya, yule mwanajeshi alifika akakojoa , kakinga alimvamia yule mwanajeshi akampiga jiwe la kichwa yule mwanajeshi akapoteza fahamu kakinga akavaa mavazi ya yule mwanajeshi kisha akaingia hadi katika chumba cha kiongozi akamuona
 
SEHEMU YA 5 YA 50

Akwelina amelala karibu na kiongozi huyo, Kakinga akiwa ndani ghafla akaja mwanajeshi mmoja akamchua kiongozi akatoka nae nje Kakinga akatumia nafasi hiyo hiyo akamchukua Akwelina akachana lile hema kwa upande wa nyuma akatoka nje, Kakinga alipopiga hatua chache akakutana na wanajeshi mbele yake, Kakinga akawapa mgongo wale wanajeshi wakampita ghafla Akwelina akalia kwa sauti wale wanajeshi waka.........





Kakinga alipopiga hatua chache akakutana na wanajeshi wengine kakinga akawapa mgongo wale wanajeshi wakampita ghafla akwelina akalia kwa sauti wale wanajeshi walisimama Mwanajeshi mmoja akamuuliza kakinga :-



MWANAJESHI ?? Simama askari huyo mtoto uliyenae umemtoa wapi na muda kama huu unampeleka wapi ?



KAKINGA ?? Aaah mtoto huyu anaumwa sana ninaenda kumpatia tiba ili kukoa maisha yake hiyo ni amri toka kwa kiongozi.



MWANAJESHI ?? Sawa naomba kitambulisho chako kwa sababu unaomekana unawasiwasi sana.



Yule mwanajeshi akamsogelea kakinga, Kakinga alijiandaa akamshika vizuri akwelina, yule mwanajeshi alipotaka kumshika kakinga, kakinga alitumua mbio wale wanajeshi walipomuona kakinga anakimbia walimfukuza wakiwa wanapiga firimbi kuwajulisha wenzao , mlio wa firimbi ile ulisambaa eneo lote wanajeshi walijigawa taa kubwa liliwashwa lile taa lilimmoreka kakinga taa lile liliwasaidia wanajeshi kumuona kakinga vizuri, wakati kakinga anakimbia wanajeshi wengine walitokeza mbele yake kakinga akasimama wale wanajeshi walimzunguka kakinga, wakamnyoshea silaha wakamwambia apige magoti, kakinga alipiga magoti akiwa chini alimshika akwelina vizuri akatazama mbele yake akaona kuna msitu kakinga alisimama ghafla akamsukuma mwanaheshi mmoja akapata njia kakinga akakimbia tena.



Wale wanajeshi walipiga risasi hovyo kakinga akajificha katika mti mkubwa uliokuwepo ndani ya msitu huo, baada ya muda wale wanajeshi waliacha kupiga risasi wakaingia msituni kumtafuta kakinga, Kakinga alipoona wale wanajeshi wameacha kupiga risasi anaendelea kukimbia kakinga alipita njia ya karibu ili awahi kufika nyumbani kwake. Wale wanajeshi walimtafuta kakinga msitu mzima lakini hawakumpata wakarudi kwa kiongozi , kiongozi aliwauliza :-



KIONGOZI ?? Mtoto yupo wapi ?



??WANAJESHI:-

“”** Tunastahili adhabu ya kifo mkuu yule kijana hatujamuona **””



KIONGOZI ?? Pumbafu kabisa askari zaidi ya elfu moja mnashindwa kumkamata mtu mmoja tena mwananchi wa kawaida shenzi kabisa nifuateni .



Kiongozi wa wanajeshi alichukua bastola yake akatoka nje akawafukuza wananchi wote waliokuja katika sherehe, alafu akachukua usafiri wakaondoka moja kwa moja hadi kwa zilpa walimkuta zilpa ametoka kuoga kiongozi alikuwa na hasira sana akasema :-



KIONGOZI ?? Wewe binti umemtuma mtu aje kumchukua mtoto sio ?



ZILPA ?? Nimemtuma mtu aje kumchukua mtoto !! Mbona sielewi Mimi sijafanya hivyo kiongozi wangu na siwezi kufanya hivyo kwani kuna nini jamani ?



KIONGOZI ?? Kuna kijana wa kiume amekuja akamchukua Mtoto na akatoweka nae .



ZILPA ?? Nahisi atakuwa ni KAKINGA .



KIONGOZI ?? KAKINGA ndio nani ?



ZILPA ?? Yule ndio alikuwa amemficha huyo Mtoto muda mrefu .



KIONGOZI ?? Nipeleke anapoishi sasa hivi .



Kiongozi alimchukua zilpa wakaondoka kuelekea nyumbani kwa kakinga. Kakinga baada ya kukimbia sana alifika nyumbani akamwita mke wake Monna , Monna alipotoka nje hakuamini kumuona akwelina amerudi katika mikono yake, Monna alimkumbatia akwelina akambusu sana kwa furaha machozi yalimtoka monna , kakinga akasema :-



KAKINGA ?? Mke wangu hakuna muda wa kupoteza jiandae tuondoke utaendelea kumbusu huko mbele maisha yetu nimeyaharibu kwa kumuokoa akwelina tuondoke mke wangu haraka.



Monna aliingia ndani akachukua kanga akamfunga akwelina mgongoni kwake akachukua vitu muhimu vyote akasahau vile vitu alivyomkuta navyo akwelina, Kakinga alimkumbusha monna , Monna akarudi ndani akachukua mfuko mweusi pamoja na kile kitabu kidogo walichomkuta nacho akwelina. Kakinga alimchukua mke wake wakaondoka walipofika mbali kiasi waliona mwanga wa mataa makali eneo la nyumba yao wakasimama kwakua walikuwa kwenye mlima mdogo walimuona zilpa akiwa na wanajeshi Wengi. Wale wanajeshi walifika wakavunja mlango ndani hawakumkuta mtu kiongozi akasema :-



KIONGOZI ?? Ndani hakuna mtu ee sawa na wamekimbia wameacha mifugo tu sasa choma moto nyumba yote hii, choma na mifugo yao .



Wale wanajeshi walimwaga mafuta eneo lote wakachoma moto,
 
SEHEMU YA 6 YA 50

Kakinga na mke wake Monna wakiwa mbali kidogo walistuka baada ya kuona nyumba yao inawaka moto , roho iliwauma sana lakini walikuwa hawana uwezo wa kufanya chochote, Monna alimtazama sana mume wake alimuona kakinga ana huzuni Monna akamwambia mume wake :-



MONNA ?? Usijali mume wangu haya ni mapito tu na mungu ndio anayepanga twende mjini, huko mjini anaishi mama yangu mdogo tutamuomba hifadhi mume wangu sawa .



KAKINGA ?? Sawa mke wangu lakini ipo siku haya manyanyaso yataisha.



Monna alimshika mkono mume wake wakaondoka kuelekea stendi ya mabasi, walifika stendi wakapata usafiri, Safari ilikuwa ndefu sana. Yalipofika majira ya asubuhi walifika mjini walimshukuru mungu kufika salama , Wakachukua mizigo yao safari ikaendelea kwenda kwa mama yake mdogo na monna. Hapakuwa mbali sana muda mfupi walifika Monna akapiga hodi mlinzi akaja akamfungulia mlango Monna na kakinga wakaingia ndani , Wakamuomba mlinzi akamwite mama yake mdogo , Kakinga na Monna walipokuwa wanamsubiri mlinzi aje na mama yao mdogo, Ghafla geti liligongwa kakinga akasogea ili amfungulie huyo mtu anayegonga mlango kwakua mlinzi hakuwepo kakinga alipofungua mlango alistuka sana kumuona mtu anaegonga mlango ni yule kiongozi wa wanajeshi kakinga ali……







Ghafla geti liligongwa kakinga akasogea ili amfungulie huyo mtu anayegonga mlango kwakua mlinzi hakuwepo kakinga alipofungua mlango alistuka sana kumuona mtu anaegonga mlango ni yule kiongozi wa wanajeshi kakinga aligeuka na kutazama pembeni akaacha mlango wazi yule kiongozi akapitiliza moja kwa moja hadi ndani, kakinga akamfuata Mke wake haraka haraka akiwa na wasiwasi akamwambia :



KAKINGA: Mke wangu hii sio sehemu salama kwetu tuondoke sasa hivi .



Monna akamshangaa sana Mume wake alafu akamjibu: Kwanini mume wangu mbona unanitisha ?



KAKINGA: Sikutishi mke wangu umemuona yule mwanaume aliyeingia ndani dakika chache zilizopita ?



MONNA: Hapana sijamuangalia usoni vizuri kwani ni nani ?



KAKINGA : Mke wangu mtu yule ni yule kiongozi wa wanajeshi wanaomtafuta sana Akwelina .



MONNA: Mungu wangu sasa tunafanyaje mume wangu jamani ?



KAKINGA: Hebu nifuafe huku .



Kakinga alimchukua Mke wake monna wakatoka nje ya geti wakasogea mbali na nyumba ile, Kakinga na monna walikaa nje pale kwa masaa matatu wakamuona yule kiongozi anatoka nje na mama mdogo walipofika nje kiongozi alimuaga mama mdogo alafu akaondoka, Kakinga na monna walipomuona yule kiongozi kaondoka walirudi getini wakagonga geti tena Mlinzi alipowaona kwa mara ya pili akawaambia:



MLINZI: Ninyi mbona siwaelewa au ninyi ni majini? si nimewaambia mnisubiri hapa nikamwite madame Mimi naingia ndani ninyi mkaondoka narudi nje sijawakuta nahofu sana na ujio wenu au mnataka kuiba niite askari ?



MONNA: Hapana kaka sisi hatupo hivyo unavyofikiria mtoto alikuwa anataka maji ndio tukaenda kununua dukani na huyo madam ni mama yangu mdogo tafadhali tunaomba kuonana nae .



Mlinzi aliguna kisha akawazunguka kwa muda mrefu kisha akasema:



MLINZI: Sasa siwaruhusu kuingia ndani subirini hapa hapa nje ya geti nikamwite Madame siwaamini tena.



Mlinzi alifunga mlango akaingia ndani akamwita madame, Madame alitoka nje akamwambia mlinzi afungue geti baada ya Mlinzi kufungua geti Madame hakuamini kumuona Monna mbele yake madame alifurahi sana Kumuona Monna akasema: Njoo mwanangu jamani miaka mingi imepita Monna umekuwa msichana mkubwa sasa ingia ndani Mama njooo ??



Monna kwa furaha aliingia ndani akamkumbatia Mama yake mdogo kwa shauku na bashasha madame akampokea Monna kwa furaha pia, Madame akamuona Kakinga akamuuliza Monna: Huyo kijana ni nani Msichana wangu ?



MONNA: Huyu ni Mume wangu Mama anaitwa Kakinga na huyu ni mtoto wetu wa kwanza .



MADAME: Anhaa karibu sana Mkwe wangu karibu nyumbani mimi ndio Mama yake mdogo na Monna kwahiyo ondoa wasiwasi jione upo kama nyumbani kwako Baba alafu usiniogope buana mimi ni mzungu wa roho kwahiyo kuwa huru.



KAKINGA: Ahsante sana Mama yangu nimefurahi sana kukufahamu.



Baada ya mazungumzo hayo Madame alimchukua Monna na Kakinga wakaingia ndani walipofika ndani Madame akawapatia chakula kizuri sana kisha
 
SEHEMU YA 7 YA 50

akawaonesha chumba chao cha kulala alafu akaingia chumbani kwake , Monna na Kakinga walipomaliza kula waliingia chumbani kwao wakalala .



Baada ya mwezi mmoja kupita maisha ya monna na kakinga ndani ya nyumba ya Madame yalikuwa maisha mazuri sana siku baada ya siku monna na kakinga walizidi kupendeza na kunawili. Siku moja majira ya mchana Kakinga alikuwa anazungumza na mke wake monna kakinga akamuuliza :



KAKINGA : Mke wangu hivi Mama yako mdogo anafanya kazi gani kwa sababu kila siku usiku anatoka alafu anarudi asubuhi sijawahi kumuona anaenda kazini hata Siku moja lakini anafedha nyingi mno sasa fedha hizi yeye anazitoa wapi ?



MONNA: Mmmmh mume wangu umeanza kupekuwa pekuwa vitu visivyokuhusu yanakuhusu hayo ni maisha yake tumeyakuta na tuyaache kama yalivyo sawa mume wangu ?



KAKINGA: Sawa lakini mmh ninawasiwasi sana na Mama yako mdogo sijui ni kwanini lakini acha nikae kimya kama utakavyo Monna.



MONNA: Ni bora tu ukae kimya Mume wangu asije akatusikia akatufukuza bure pia jiulize tukifukuzwa tutakwenda wapi ?



KAKINGA: Sawa Mke wangu .



Monna alikuwa hapendi Mume wake azungumze kitu kibaya chochote kuhusu mama yake mdogo kwa sababu Monna alikuwa anamuamini sana pia alikuwa anampenda mno mama yake mdogo, Wakati Kakinga akiwa anazungumza na Monna Madame alitoka nje akamwita Monna , Monna akamfuata Madame alipofika Madame akamwambia: Leo nahitaji kutoka kidogo na Mume wako kama inawezekana Mtoto wangu .



MONNA: Kwanini isiwezekane Mama yangu yule ni Mtoto wako pia na hukuhitajika kuniomba ungemchukua tu Mama yangu .



MADAME: Ahsante Mtoto wangu naomba mueleze Mume wako suala hili nahitaji tutoke sasa hivi sawa ?



MONNA: Sawa Mama yangu kipenzi.



Monna akamfuata Mume wake akamueleza ombi la Mama yake mdogo Kakinga hakupinga ombi la Mama ikabidi akubali , Kakinga akajiandaa kisha wakaondoka, Safari ilikuwa ndefu sana wakafanikiwa kufika eneo moja lililokuwa linatoa harufu mbaya sana Madame akamwambia Kakinga: Pole kwa harufu mbaya Mkwe vumilia kidogo wala hatukawii eneo hili .



KAKINGA: Aaah Usijali Mkwe tupo pamoja lakini tumefuata nini hapa ?



MADAME: Kuna picha nitaletewa hapa kwahiyo ilinilazimu niwe na kijana wa kiume kama walivyotaka wao hiyo ndiyo sababu ya kukuchukua wewe Mkwe .



KAKINGA: Watu gani hao Mkwe ?



Madame aligeuka akamtazama sana Kakinga alafu akasema: Mbona unaniuliza maswali mengi una hofu na Mimi Mkwe ?



KAKINGA: Hapana hapana Mama yangu nilikuwa nauliza tu .



Muda huo huo akatokeza Kijana mmoja akampatia Picha Madame kisha akaondoka , Madame akaitazama picha hiyo akastuka mno alafu akairudisha picha ndani ya Bahasha wakarudi Nyumbani, Walipofika Nyumbani Madame akambeba Akwelina akamtazama kwa muda mrefu kisha akamrudisha kwa Monna Madame akaingia ndani, Kitendo hicho kilimshangaza sana Kakinga akatamani kuzungumza na Monna lakini akasita akaacha .



Usiku ulipoingia majira ya saa saba Kakinga alibanwa na haja ndogo ( mkojo ) kakinga aliamka akaenda chooni wakati anakwenda chooni alimuona Mama mdogo sebuleni anatazama TV alafu ameshika picha mkononi kwake Kakinga aliendelea na safari yake baada ya hatua chache Kakinga alimsikia mama mdogo anapokea simu akasema :-



MADAM: Ndio mkuu yule kijana uliyenipatia picha yake yupo kwangu leo amefikisha mwezi na siku kadhaa akiwa katika nyumba yangu sasa muda huu atakuwa ameshalala chukua watu sita alafu njooni mimi nipo macho nawasubiri msikawie fanyeni haraka sawa .



Kakinga alistuka baada ya kusikia maneno hayo akarudi chumbani kwake taratibu alipofika alimuamsha Monna akamueleza yote aliyosikia toka kwa Mama mdogo ( madame ) Monna alitaka kupinga alichokisikia kakinga akamuomba Monna watoke nje ya nyumba hiyo , Monna alikubali kwa shingo upande kakinga alimshika mkono Monna akatoka nae kwa mwendo wa taratibu mno, kakinga na Monna walipokaribia mlango taa ziliwaka ghafla wakamuona Mama mdogo yupo mbele yao ameshika bastola Monna hak......................................................





Monna hakuamini macho yake monna alihitaji kumsogelea mama mdogo, mama mdogo akanyanyua bastola juu kisha akasema :-



MADAM ?? Usijaribu kunyanyua hatua nyingine najua utashangaa sana mtoto wangu lakini sihitaji kuiponza damu ya mtoto wa dada yangu
 
SEHEMU YA 8 YA 50

cha maana muda huu naomba nipatie huyo mtoto hilo tu linaweza kusaidia maisha yenu .



MONNA ?? Lakini mama mdogo mtoto wangu kakukosea nini na kwanini unamtaka ukiwa umeshika silaha huyu ni Mjukuu wako mama yangu muda wowote ukimtaka unampata lakini sio kwa shari kama hivyo ulivyo .



MADAM ?? Nisikilize Monna huyo mtoto sio wako na kwa kukuhakikishia hilo huyo mtoto ana jina katika mgongo wake ameandikwa AKWELINA kweli au siokweli ?



KAKINGA ?? Mama sio kweli hayo unayosema huyu mtoto ni wangu tangu nipo nae toka anazaliwa hadi leo lakini sijamuona ana jina hilo mgongoni ngoja nimlete kwako ili umchunguze Mjukuu wako kama hautuamini.



Kakinga alimchukua mtoto kutoka katika mikono ya Monna , Monna alikataa kakinga asimchukue mtoto, kakinga akambonyeza monna katika kidole cha mguu Monna akampatia kakinga mtoto, kakinga alimsogelea mama mdogo bila hofu yeyote, kitendo kile kilimjengea imani mama mdogo akashusha bastola chini akajiandaa kumpokea mtoto katika wakati anampatia mtoto mama mdogo mtoto alimkwapua ( kumnyanganya ) mama mdogo ile bastola alafu akamnyoshea mama mdogo Kakinga akamwambia Monna :-



KAKINGA ?? Mke wangu mchukue ingia ndani chukua mizigo yetu tu tuliyokuja nayo alafu mchukue na mtoto.



MADAM ?? Monna ukimchukua mtoto Mimi nitakuwa sio mama yako tena nitageuka na kuwa adui yako nitakutafuta dunia nzima na nikikupata kichwa chako halali yangu. alafu wewe kijana huwezi kutoka katika himaya yangu hii na kama ulikuwa hujui nyumba yangu yote imejaa walinzi utapita wapi hahaha rudisha bastola yangu haraka .



KAKINGA ?? Monna nimekwambia mchukue mtoto harakaaaaa .



Monna aliingia ndani akachukua mizigo yao muhimu akatoka nje akamchukua akwelina toka katika mikono ya mama mdogo , kakinga alimchukua mama mdogo akamtanguliza mbele wakatoka nje, walipofika nje waliwakuta wanajeshi wengi kakinga hakuogopa akamtumia mama mdogo kama ngao, Kakinga aliendelea kutoka nje zaidi akafanikiwa kutoka nje ya geti la mama mdogo. Kakinga alipotoka nje ya geti akafunga lile geti alafu akaitupa mbali ile bastola kakinga akamsukuma mama mdogo akashika mkono wa mke wake Monna wakakimbia, mama mdogo alifungua lile geti haraka wanajeshi wakatoka wakawaona kakinga na Monna wameshafika mbali, Mama mdogo na wale wanajeshi waliwafuata wakiwa wanapiga risasi hovyo. Milio ya risasi ilizidi kuwapatia wasiwasi kakinga na Monna walikimbia zaidi, Baada ya muda mrefu Monna alichoka sana akashindwa kuendelea kukimbia, kakinga akaona gari limebeba takataka dereva wa gari lile alikuwa pembeni anakojoa, Kakinga akatumia nafasi hiyo akapanda kwenye gari lile akampandisha na mke wake Monna, Monna wakati anapanda alidondosha mzigo mmoja ikabidi kakinga ashuke akaufuata ule mzigo, Mzigo ule ulikuwa mbali kidogo kakinga alifika akauchukua ule mzigo ghafla akasikia gari linaondoka, kakinga alistuka akaanza kulikimbiza lile gari, Kakinga alijitahidi kukimbia kadri ya uwezo wake, lakini akachoka gari likamuacha.



Monna alibaki analia baada ya kumuona mume wake kakinga gari limemuacha. Kakinga alijuta sana kwa kile alichofanya kakinga ikabidi atembee kwa mguu , lile gari lilitembea kwa muda mrefu sana likafika Sehemu ya kutupa uchafu likasimama Monna bila kuchelewa alishuka chini akasogea mbali na lile gari. Monna alitazama huku na kule akashindwa kutambua yupo sehemu gani, Yule dereva alimwaga taka alipomaliza akaondoka. Monna alitazama upande wa kulia aliona bonde dogo akaingia ndani ya bonde hilo akamfunika mtoto vizuri alafu akalala. Kakinga akiwa njiani aliona gari lingine limebeba uchafu kakinga aliomba msaada aliomba msaada akapanda ndani ya gari lile. Monna akiwa amepitiwa na usingizi walikuja wanaume wanne hadi katika lile bonde wakamkuta binti akiwa amebeba mtoto amelala mmoja akasema :-

“””” Nani huyu kalala katika chumba chetu alafu ni binti mzuri sasa huyu leo ni zawadi yetu, alafu amekuja muda mzuri kuna baridi kweli “”””



Monna akiwa amelala alistuka amekamatwa na watu asiowajua, Mmoja kati ya wale watu alimchukua mtoto akaenda kumuweka mbali akarudi wakamshika Monna wakamlaza chini wakamvua nguo, Kiongozi wao akasimama akafungua zipu ya suruali yake alafu aka……









Monna akiwa amelala alistuka amekamatwa na watu asiowajua,
 
SEHEMU YA 9 YA 50

Wanaume hao wakamnyanganya mtoto Monna alafu wakamuweka chini kisha wakamshika Monna wakamlaza chini wakamvua nguo, Kiongozi wao akasimama akafungua zipu ya suruali yake alafu akajiandaa kumuingilia Monna , Kiongozi wa vijana hao kabla hajamfikia Monna walisikia mngurumo wa gari, wakamziba mdomo Monna wakaingia nae ndani ya Pango wakamthibiti Monna vizuri, Gari lililofika eneo hilo lilikuwa limembeba Kakinga , Kakinga aliposhuka toka kwenye gari alianza kumwita Monna kwa sauti ya juu sana , Kakinga aliita kwa hisia na machungu makali lakini kimya kilizidi kutawala eneo hilo .



Kakinga alizidi kumwita Monna bila kuchoka kakinga alizunguka eneo kubwa katika eneo hilo la kutupia uchafu ( Jalalani ) bila mafanikio, wakati huo Monna alikuwa anamuona na anamsikia mume wake lakini hakuweza kumjibu kutokana na kuzibwa mdomo, Muda ulizidi kwenda Dereva aliyemsaidia kakinga alimfuata Kakinga akamwambia:



DEREVA: Tuondoke Kaka muda unazidi kwenda alafu hili gari sio langu kwahiyo nataka kurudisha gari ofisini vinginevyo nitapigwa faini .



KAKINGA: Kaka nivumilie kidogo nahisi mke wangu hayupo mbali na eneo hili naomba nivumilie kidogo??



DEREVA: Ndugu yangu kwa hali yeyote hakuna binadamu anaeweza akawa eneo hili labda mbwa na viumbe wengine wanaotembea usiku lakini si binadamu hebu angalia tumezunguka eneo kubwa tu lakini hakuna hata dalili ya kuwepo huyo Mke wako, Mimi naondoka Kaka niambie nikuache huku au tunarudi wote tulipotoka ?



Kakinga alifikiria sana kisha akamjibu Dereva: Wewe waweza kuondoka kaka lakini siwezi kuondoka eneo hili nahisi mke wangu yupo eneo hili, nashukuru kwa msaada wako kaka mungu akulipe.



Dereva alipanda kwenye Gari lake akawasha na kuondoka akamuacha Kakinga eneo hilo la kutupa takataka, baada ya Dereva kuondoka Kakinga nae akasogea upande wa pili wa eneo hilo, Vijana waliomkamata Monna walifurahi mno kiongozi wao akasema: Wajinga hawa badala ya kutupa takataka na kuondoka wanaanza kupotezeana muda tu pumbafu kabisa sasa vijana wangu Muda ndio huu kazi iendelee nitafaidi leo ????



Monna alipomuona Mume wake anaondoka aliishiwa nguvu Dereva aliyemsaidia akiwa anatoka eneo hilo alisikia sauti ya Mtoto akilia ikabidi asimame kisha akazima gari ili aisikie sauti hiyo ya Mtoto anaelia , Sauti ikasikika kwa mara ya pili Dereva akashuka chini akawasha taa na kuanza kuifuata sauti ya mtoto huyo. Baada ya kutafuta sana Dereva akafanikiwa kumuokota mtoto mdogo Dereva akarudi eneo alilomuacha Kakinga cha ajabu hakumuona Dereva akamwita Kakinga kwa bahati nzuri Kakinga hakuwa mbali na eneo hilo, Kakinga aliposikia anaitwa alimfuata Dereva alipofika Dereva akampatia Mtoto aliyemuokota alafu akasemwambia:



DEREVA: Huyo mtoto nimemuokota hapo nyuma sasa sijui kama unamfahamu ? Kwa maana uliniambia unamtafuta mke wako pamoja na mtoto mdogo .



Kakinga alimpokea mtoto haraka haraka akamtazama akamuona Akwelina, Kakinga hakuamini kama amempata mtoto Kakinga alimbusu akwelina na kumkumbatia alafu akasema : Ndio ndugu yangu mtoto huyu ni wangu na alikuwa na mama yake sasa sijui mke wangu ameuwawa masikini ??



Kakinga alishindwa kujiziwia baada ya kuhisi Monna huenda atakuwa ameshapoteza maisha , kakinga alipiga magoti akalia sana kwa uchungu, Monna alikuwa anamuona mume wake anavyoteseka kumtafuta roho ilimuuma sana Monna , Monna alipowaona vijana hao wameshangaa akatumia nafasi hiyo akarudisha kichwa chake nyuma ghafla kwakua vijana hao walikuwa wamezubaa Mkono wa aliyemziba mdomo Monna ukatoka Monna akaita kwa sauti ya juu mno :



" KAKINGAAAAAAAAAA "



Sauti ya Monna ilimstua Kakinga pamoja na Dereva wakaanza kumtafuta Monna huku na huko Dereva akawasha tochi lake wakati anamoreka tochi lilimdondoka yule dereva alipoinama ili achukue tochi alihisi kuna kitu kitu upande wake wa kushoto yule dereva alisogea taratibu akiwa makini sana akaona pango dogo akamoreka ndani ya lile pango akamuona msichana mmoja akiwa ameshikwa na wanaume zaidi wanne yule dereva alimuita Kakinga, kakinga alipofika alimuona mke wake ameshikwa na wanaume wengi. Kakinga alishikwa na hasira akaingia ndani ya pango hilo akawapiga sana wale wahuni kwa hasira alizokuwa nazo kakinga alifunja mikono ya vijana hao na kuhitaji kuwauwa kabisa , yule Dereva akamziwia Kakinga Vijana hao wakakimbia .
 
SEHEMU YA 10 YA 50



Kakinga akamtoa mke wake ndani ya pango , Monna hakuamini kama amepata msaada monna alimkumbatia mume wake yule dereva akawapatia msaada hadi nyumbani kwake, yule Dereva alikuwa amepanga chunga kimoja na sebure, kwakua yalikuwa ni majira ya usiku Kakinga na Monna walilala sebuleni. Asubuhi palipokucha yule Dereva aliamka mapema sana akawapa pesa ya chakula akaondoka kwenda katika shughuli zake, Monna alimshukuru mungu kwa kumpata kijana mwenye roho nzuri .



Baada ya wiki mbili kakinga aliiamka asubuhi sana akaingia mtaani kutafuta kazi siku hiyo kakinga alizunguka mji mzima lakini hakupata kazi, Kakinga hakukata tamaa aliendelea kupambana kutafuta kazi mungu akamjalia kakinga akapata kazi ya kubeba mizigo stenti ya magari , kakinga alifanya kazi bila kuchoka kuanzia asubuhi hadi majira ya saa mbili usiku akapata shilingi 10000 Kakinga akarudi nyumbani akiwa hoi Mwili wote unamuuma kama donda .



Wakati huo njaa ilikuwa inamuuma kwa sababu alikuwa hajala toka asubuhi Kakinga alitamani anunue chakula ale lakini alishindwa kwa sababu alitambua Monna atakuwa hajala kama yeye, Kakinga alitumia zile fedha akanunua vyakula vya kutosha akiwa njiani anarudi nyumbani alimuona mtoto mdogo anataka kuingia kwenye moto Kakinga akashangaa sana akatazama eneo lote akaona kimya ikabidi Kakinga akimbie haraka akamchukua yule mtoto kabla hajaufikia Moto , Kakinga akiwa amembeba mtoto alisikia mtu mmoja ikisema :



"" Jamani yule Mwizi wa mtoto huyu hapa njooni njooni ..



Watu wa mtaa ule walitoka nje na silaha mbalimbali wakamva.............





Watu wa mtaa ule walitoka nje na silaha mbalimbali wakamvamia kakinga wakamshambulia kakinga , kakinga alijaribu kuwaelezea ukweli kuhusu mtoto lakini wananchi hawakumuelewa kabisa, waliendelea kumpiga kwa bahati nzuri askari wa lindo la usiku walitokea eneo lile wakamchukua kakinga wakaenda nae kutuo cha police walipofika kituoni askari hawakutaka kumsikiliza kakinga wakamueka mahabusu. Siku hiyo monna alikuwa anawasiwasi mkubwa sana, muda ulizidi kwenda monna alitoka nje na mtoto akamtazama sana mtoto akasema kwa sauti ya chini sana :-



“”* Akwelina mtoto wangu najua unahisi njaa unahitaji kula masikini tangu asubuhi hadi muda huu hujala kitu chochote nitafanyaje mimi ndani hakuna kitu, pesa hakuna baba yako tangu aondoke hajarudi hadi muda sasa sijui kapatwa na tatizo gani daaah matiti ninayo lakini hayana maziwa ndani yake hayatoi kitu vumilia mtoto wangu *””””



Monna alipomaliza kuzungumza aliimba wimbo mzuri akiwa anambembeleza akwelina taratibu taratibu akwelina alilala, Monna akaingia ndani akamlaza mtoto alafu akatoka nje akakaa karibu na mlango monna alizungumza mouoni :-



“”** Upo wapi mume wangu , umepatwa na nini mbona wanifanya nikose amani rudi mume wangu *”””



Muda ulizidi kwenda hadi saa saba usiku monna alikuwa bado yupo nje anamsubiri mume wake, Yule dereva alikuja amelewa sana akamkuta monna yupo nje akasema :-



DEREVA ??Wewe mwanamke unawanga nini mbona upo nje hadi muda huu unafanya nini anhaaaa kumbe wewe ndio unakujaga usiku chumbani kwangu unanichapa bakora weeee nikiamka asubuhi nakuwa nimechoka sanaaa sasa nasema ondokeni wewe na mume wako siwezi kuwalea watu wazima kama ninyi nasema ondokeni pumbafu “”



MONNA ?? Shemeji mimi nitaenda wapi usiku huu jamani mume wangu hajarudi pia ninamtoto mdogo jamani najua umelewa nenda kalale shemeji tutazungumza kesho .



DEREVA ?? Mimi nimelewa ? Haaaah !! Mimi sijawahi kulewa toka nizaliwe nasema toka hunijui eeh subiri sasa nimewachoka nawalisha kila siku kama watoto ondokeni .



Yule dereva aliingia ndani akatoa nguo za monna akawa anazitupa nje monna alimuomba sana lakini yule dereva hakusikia kilio cha Monna, monna aliingia ndani akachukua mizigo yake akambeba akwelina mgongoni akatoka nje akaenda hadi stenti ya magari iliyokuwa karibu na nyumba waliyokuwa wanaishi, Monna alifika stenti akamtoa akwelina mgongoni akakaa kwenye kiti. Kakinga alikuwa na mawazo sana mahabusu , kakinga akiwa na mawazo alisema :-



“” Eee mungu kwanini kila siku napata matatizo mimi tu au kuna binadamu mwingine anapata matatizo kama mimi , hivi nimekosa nini mimi? Wema wangu wa kumsadia yule mtoto leo hii napata shida kiasi hiki nyumba yangu imechomwa kisa mtoto , nimenusurika kufa kisa mtoto leo nimekuja kuja humu mahabusu kwa ajili yake kwa sababu moyoni niliweka nia natafuta kazi ili nimnunulie maziwa au huyu mtoto sio binadamu ni jini, shetani au ni pepo, Nimechoka sasa nikifanikiwa kurudi nyumbani nitamchukua mtoto nitaenda kumtupa bila kujali kama mke wangu atapenda au hatopenda.
 
SEHEMU YA 11 YA 50

Hayo ni maneno aliyokuwa anazungumza kakinga baada ya kuona matatizo yanamuandana kila siku. Kakinga alikesha usiku kucha bila kulala yalipofika majira ya asubuhi wale askari waligundua kakinga hana makosa wakamtoa mahabusu kakinga alitoka mahabusu akiwa na hasira sana, kakinga alipofika nyumbani hakumkuta monna akawauliza majirani wakamwambia yote yaliyotokea Jana , kakinga alipata maumivu makali sana , wakati kakinga amesimama anahasira zilizopitiliza alisikia sauti ya monna ikimwita, kakinga alipogeuka alimuona mke wake akamfuata akamchukua akwelina akaondoka nae akiwa anakimbia , kitendo kile kilimshangaza sana monna , Kakinga alimbia hadi sokoni akasimama akapiga magoti akamtazama sana akwelina akasema :-



“”” Utanisamehe sana kwa unyama huu lakini nitafanyaje unanitesa sana akwelina nakuacha hapa atapita mtu mwema mwingine atakuchukua kwaheri sana akwelina nakupenda.



Kakinga alizungumza maneno hayo machozi yakimtoka , kakinga akamuweka chini akwelina akahitaji kuondoka kakinga alishangaa kuona akwelina amemshika kidole chake kwa nguvu kakinga aka……..





Kakinga akatoa mkono wa akwelina katika kidole chake akasimama akaondoka akwelina alianza kulia, kilio cha akwelina kilitesa nafsi ya kakinga, Kakinga alitamani kurudi lakini akajitahidi akaondoka, Akwelina aliendelea kulia masikini Kakinga hakujali aliendelea kuondoka kurudi kwa Monna, Kakinga alikutana na monna njiani, monna alimuona Kakinga hana mtoto monna alichanganyikiwa sana alimuuliza Kakinga :-



MONNA ?? Mume wangu akwelina yupo wapi ?



KAKINGA ?? aaaah achana na habari hizo nimempeleka kwa wengine watusaidie kumlea kama wema tumeufanya sana yule mtoto katuletea matatizo ya ajabu sana Wewe angalia tulipotoka na hapa tulipo yote ni mikosi kwahiyo ndio hivyo nimewapelekea wengine.



MONNA ?? Unasemaje wewe sikuelewi mume wangu namtaka akwelina wangu sikuelewi Mimi siwezi kuishi bila yeye tafadhali nenda kaniletee akwelina wangu .



KAKINGA ?? Nakwambia hivi sahau kuhusu akwelina turudi nyumbani .



MONNA ?? Nyumbani wapi mume wangu rafiki yako ametufukuza amesema ametuchoka siwezi kukuelewa bila kumuona akwelina niambie yupo wapi nimfuate Mimi jamani .



Monna alilia sana katika mikono ya mume. Kakinga aliishiwa nguvu baada ya kuambiwa rafiki yake aliyemsaidia amewafukuza katika nyumba yake kakinga alikaa chini akashika kichwa, monna alipomuona mume wake amechanganyikiwa ghafla monna alijaribu kumfariji japo walikuwa na ugomvi kuhusu mtoto , Monna alikuwa hapendi kumuona mume wake akose furaha hata siku moja mbele yake, Kakinga alisema kwa uchungu :-



KAKINGA ?? Umeona mke wangu sijui sisi tumemkosea nini mungu kila siku matatizo yapo kwetu tu daah na kwa hali hii tutaenda wapi ? Na akwelina tungemleaje kwa hali kama hii mke wangu ? Ni bora nimewapelekea wenye uwezo wamlee mke wangu ama kweli jasho lako ndio lako lakini jasho la mwingine mke wangu ni sumu liokope kabisa .



MONNA ?? Usijali mume wangu maisha ni kokote nipo tayari kulala nje ndani ya jiji hili kwa ajili yako nakupenda mume wangu sihitaji kingine katika maisha haya zaidi ya furaha yako.



Monna alimshika mkono mume wake wakasimama wakaondoka, Monna na mume wake walipita katika migahawa wakiomba kazi kwa bahati nzuri monna alipata kazi ya kuosha vyombo, Monna alipopata kazi alifurahi sana Kakinga akamwambia monna :-



“””””* Mke wangu kwakua Wewe umepata kazi endelea kufanya kazi Mimi naenda kutafuta kazi kwenye viwanda nitarudi jioni kama nikipata kazi na ukimaliza kazi nikukute stenti pale usitoke hadi nifike hapo pia usisahau kule chakula tangu jana hujala kitu mke wangu sawa *”””



Kakinga aliondoka akaenda kutafuta kazi. Muda ulizidi kwenda akwelina alizidi kulia katika eneo lile aliloachwa na Kakinga watu walimvuka na kumruka bila kumsaidia wala kumuokota, jua lilizidi kuwa kali likamchoma akwelina, akwelina alilia zaidi lakini hakupata msaada wowote. Baada ya muda mfupi kiongozi wa wanajeshi anayemtafuta sana mtoto akwelina alikuja na wanajeshi wake katika ofisi moja iliyokuwepo eneo hilo , Akwelina baada ya kulia sana akajitokeza msalia mwema mmoja bibi kizee akamuokota akwelina , yule bibi aliuliza kila mtu aliyekutana naye njiani lakini kila aliyemuuliza alimjibu hamtambui mtoto yule.
 
SEHEMU YA 12 YA 50

Bibi kizee alitembea sana bila mafanikio kwa bahati nzuri akamuona yule kiongozi amevaa nguo za kijeshi bibi alifurahi sana akasema :-



“”””* Ahsante mungu kwa maana hii ni kesi kubwa ngoja nimpelekee yule askari wa kijeshi ili mtoto awe kwenye mikono salama *””””



Bibi alimfuata yule kiongozi alipomkaribia bibi alim….





Bibi alimfuata yule kiongozi alipomkaribia bibi alimpatia mtoto yule kiongozi yule kiongozi alishangaa sana baada ya kumuona bibi kizee anamletea mtoto kiongozi alimuuliza bibi :-



KIONGOZI ?? Samahani bibi kwanini umenipatia huyu mtoto wewe wanitambua Mimi ?



BIBI ?? Hapana Mjukuu wangu sikufahamu na hata huyu mtoto simtambui pia, Mimi nimemuokota huyu mtoto na nimejaribu kuwauliza watu wengi katika eneo hili, wote wananijibu hawamtambui ndio nilipokuona wewe umevaa nguo za jeshi la nchi nimekuletea nahisi atakuwa Sehemu salama akiwa kwako Mjukuu wangu dunia imeisha



KIONGOZI ?? Sawa upo sahihi bibi lakini sheria ni ngumu sana nakushauri nenda kituo chochote cha police kilichopo karibu yako ukawakabidhi wao hiyo ndio njia salama bibi .



Wakati kiongozi anaendelea kuzungumza na bibi alikuja mwanajeshi mmoja akasema :-



“”* Mkuu tumepata taarifa kuhusu yule mtoto kuna sehemu yupo *”””



Kiongozi hakutaka kuzungumza na bibi tena akaondoka haraka haraka kuelekea sehemu hiyo, bibi alianza kujilaum kwa kitendo alichofanya cha kumuokota akwelina. Yule kiongozi na kundi lake walifika katika eneo lililosemekana akwelina alikuwepo hapo wale wanajeshi waliwauliza watu wa eneo lile



“** Kuna bibi mmoja ndio alikuwa na huyo mtoto mnamzungumzia nilimuona huyo mtoto hapa toka majira ya asubuhi *”””””



Ilikuwa ni sauti ya muuza matunda maarufu wa eneo hilo akiwapatia Maelezo wale wanajeshi kuhusu mtoto, Kiongozi alimuuliza yule muuza matunda kuhusu huyo bibi , muuza matunda alimueleza kiongozi yule bibi alivyokuwa , kiongozi akamkumba huyo bibi ndio yule aliyemletea mtoto , kiongozi akaingia kwenye gari akarudi maeneo yale aliyemuona bibi huyo. Bibi alizidi kutembea huku na huko akiwa na mtoto mkononi ndani ya mji huo baada ya kutembea sana bibi alikutana na Kakinga akamwambia :-



“””* Kijana wangu nisaidie kumshika huyu Mjukuu wangu nataka nifunge nguo vizuri nimechoka sana *”””



Kakinga alitua mfuko wa Cement chini akamshika mtoto, bibi akaondoka zake , Kakinga akiwa amemshika mtoto alimuona bibi anaondoka kakinga akamfuata yule bibi akamziwia :-



KAKINGA ?? Bibi unakwenda wapi unaniachia Mjukuu wako ?



BIBI ?? Wala sio Mjukuu wangu huyo nimemuokota tu na nimetembea nae sana lakini sijamuona mwenye mtoto huyo na unavyoniona umri wangu huu huyo mtoto nitampeleka wapi lakini wewe bado Kijana unaweza kufanya kitu ili umsaidie mtoto huyo .



Bibi aliondoka kakinga alizidi kumsumbua bibi ili amchukue mtoto , bibi hakujali hilo akazidi kuondoka kakinga alikuwa bado hajamtazama vizuri mtoto yule kakinga akasema :-



“””” Jamani sasa hili ni balaa akwelina nilimuacha kule ili wasalia Wema wanjsaidie kumlea yaani leo leo hii tena nimeletewa mtoto mwingine hivi hii ni mikosi gani jamani mungu nimekukosea nini Mimi daaaah sijui nijiue aaaaah ??



Kakinga alilalamika sana akamtazama vizuri mtoto aliyepewa Kakinga alistuka sana kumuona mtoto yule ni akwelina aliyemtupa mbali, Kakinga alishindwa kuamini macho yake , Kipindi kakinga akiwa bado yupo katika mshangao mkali alisikia magari yamesimama mbele yake, alipotazama alimuona yule bibi aliyempatia akwelina akiwa na kiongozi wa wanajeshi, Kiongozi wa wanajeshi alisema :-



“”** Kijana ulidhani unaweza kunikwepa kamwe hautaweza katika maisha yako na vita hii umeyoinunua itakuponza naomba kwa wema tu niapatie huyo mtoto kabla sijakupiga risasi na huwezi kunikimbia leo *”””



Yule kiongozi akachomoa bastola yake akaweka risasi akamwambia kakinga amlete mtoto, Kakinga alimsogelea yule kiongozi aliyekuwa ndani ya gari kakinga alikuwa makini sana kipindi anamsogelea yule kiongozi kakinga alipofika karibu ya gari aliona njia upande wa kushoto kakinga alitimua mbio akiwa na akwelina mikononi mwake, Yule kiongozi akampiga kakinga risasi ya mgongo , kakinga akadondoka chini kakinga alijitahidi akasimama tena japo alikuwa na maumivu makali sana akaendelea kukimbia kakinga alijikongoja hadi kwa mke wake monna , Monna alikuwa anaendelea na kazi katika mgahawa ule alimuona mume wake kakinga anakuja akiwa anachechemea damu nyingi zinamtoka monna alimkimbilia mume wake Kakinga akamuona akwelina , Kakinga alimpatia monna mtoto akasema :-
 
SEHEMU YA 13 YA 50



“””* Kimbia na akwelina mke wangu watu wabaya wanakuja kumchukua usipate tabu kuhusu Mimi okoa maisha ya akwelina kwanza haraka ondoka mke wangu *”””””



Monna hakukubali kumuacha mume wake akajaribu kumnyanyua ili waondoke pamoja baada ya hatua chache monna na Kakinga walizungukwa na wanajeshi , Yule kiongozi alishuka kwenye gari akachomoa kisu akamfuata kakinga akamch………





Yule kiongozi alishuka kwenye gari akachomoa kisu akamfuata kakinga akamchoma kisu cha tumbo, Monna alitetemeka sana baada ya kumuona mume wake kakinga amechomwa kisu na yule kiongozi. Yule kiongozi alimvuta kakinga akamsogelea katika sikio akamwambia :-



KIONGOZI ?? Nilikwambia kijana huwezi kunikimbia ulijifanya wewe mjanja sana sasa mwisho wako ndio huu kufa mjinga wewe .



Kakinga akiwa amechomwa kisu tumboni aliona bastola katika mkanda wa yule kiongozi kakinga akachomoa ile bastola akamteka yule kiongozi wa wanajeshi, Wanajeshi walipoona kiongozi wao ametekwa waliweka silaha zao chini wakapiga magoti, kakinga japo alikuwa na maumivu makali sana alimshikilia vizuri yule kiongozi akaondoka nae, Kakinga akiwa na mke wake monna pamoja na yule kiongozi wa wanajeshi walizidi kuondoka walipofika mbali kakinga alimwambia yule kiongozi alale chini , yule kiongozi alilala chini kakinga akaweka ile bastola chini taratibu , Monna akamshika vizuri mume wake wakaondoka. Baada ya masaa matatu kupita wale wanajeshi walifuata njia ile aliyopita Kakinga wakamkuta kiongozi wao bado amelala chini wakamwita, kiongozi wao akasimama wanarudi kwenye magari yao wakapanda wakaondoka.



Kakinga na monna walienda mbali sana wakatokezea ufukweni mwa bahari , kakinga alishindwa kuendelea na safari kutokana na kutokwa na damu nyingi sana, kakinga alindoka chini akapoteza fahamu, Monna alilia sana baada ya kumuona mume wake amepoteza fahamu , Monna alimshusha akwelina akamuweka chini akaondoka kwenda kutafuta msaada, Monna alizunguka sehemu kubwa lakini hakupata msaada monna hakukata tamaa aliendelea kutafuta msaada kwa bahati nzuri akakutana na babu mmoja aliyekuwa anaishi hapo ufukweni mwa bahari monna alimuomba msaada yule babu , Yule babu alikubali kumsaidia monna akachukua baadhi ya dawa kutokana na Maelezo ya monna akaondoka nae walipofika yule babu alikuwa mtaalamu alimtoa risasi kakinga akamchoma kile kisu alafu akamshona sehemu zote alizopata majeraha baada ya tiba yule babu pamoja na monna walimnyanyua kakinga wakaondoka kuelekea katika nyumba ya huyo babu, kipindi wanaondoka babu alisema :-



BABU ?? Mbona mtoto umemuacha ? hujui sehemu hii sio nzuri kuna baridi Kali .



MONNA ?? Tuondoke tu babu huyo mtoto sio wangu nilimuokota tu na huyo mtoto katuletea matatizo makubwa sana Mimi na mume wangu huyu bila wewe mume wangu angepoteza maisha kwa sababu ya huyu mtoto nimegundua kile alichonieleza mume wangu ni sahihi.



Monna akaenda bila kujali kile babu alichomwambia kuhusu mtoto ( akwelina ) Nyumba ya babu haikuwa mbali na bahari, walipofika walimlaza kakinga nje ili apate hewa safi. Kakinga alilala nje hapo hadi majira ya usiku akarudisha fahamu , Monna alifurahi sana kumuona mume wake alirudisha fahamu monna alimkumbatia mume wake kwa furaha, babu akatoka nje kakinga akamsalimia babu alafu akamuuliza monna :-



KAKINGA ?? Mke wangu tupo wapi hapa na huyu babu ni nani ?



MONNA ?? Huyu babu ndiye aliyesaidia maisha yako na hapa ni nyumbani kwake mume wangu .



KAKINGA ?? Ahsante sana babu kwa msaada wako mungu atakulipa kwa Wema uliyonifanyia alafu Akwelina yupo wapi au amelala ?



MONNA ?? Aaaaah sahau kuhusu akwelina nilishindwa kukusikia mwanzo leo hii kidogo nikupoteze mume wangu kwa ajili ya mtoto yule nimemtupa mbali sana huko .



KAKINGA ?? Weeee Unasemaje siwezi kukuelewa nasema hivi ili tuelewane nenda sehemu uliyomtupa akwelina uniletee hapa sasa hivi.



Kakinga na monna waligombana kwa muda mrefu mwisho monna akakubali akamfuata akwelina akamkuta amefunikwa na uchafu wa bahari nguo alizokuwa amevaa akwelina zote zilikuwa zimerowa na maji, Monna japo alikuwa ameanza kumchukia akwelina lakini alimuonea huruma sana kwa sababu akwelina alikuwa anatetemeka sana, Monna alimtoa akwelina zile nguo mbichi akamfunika kanga aliyokuwa nayo.
 
SEHEMU YA 14 YA 50

Monna akarudi nyumbani akiwa na akwelina , Alipofika nyumbani kakinga alifurahi sana kakinga akambusu akwelina kwa furaha. Baada ya wiki moja kupita majira ya usiku kakinga alimwita mke wake akamwambia :-



“”* Mke wangu hebu niletee vile vitu tulivyomkuta navyo akwelina *”””



Monna alimletea Kakinga vitu alivyohitaji alafu akaenda jikoni kupika , Kakinga aliona kitabu kidogo akakiweka pembeni , akaona mfuko mweusi umefungwa vizuri Kakinga alihitaji kuufungua ule mfuko lakini akasita akauweka pembeni mwisho akaona bahasha juu ya bahasha ile kulikuwa na michirizi ya damu, kakinga akaifungua ile bahasha akaona picha nyingi zipo ndani ya ile bahasha kakinga alipoziangalia zile picha aliona sura mbalimbali ikiwepo na sura ya yule kiongozi, Kakinga alizidi kuzitazama zile picha, picha ya mwisho kakinga alimuona Madam ( mama yake mdomo monna ) kakinga alistuka sana akajiuliza Kwanini zile picha awekewe akwelina , Kakinga alishindwa kuelewa kabisa akazirudisha zile picha ndani ya bahasha akashika uke mfuko mdogo mweusi akaufungua ndani ya mfuko aliona vitu kama mawe mdogo madogo yanang’aa sana Kakinga alipotazama vizuri akagundua yale sio mawe ya kawaida ni …..





Kakinga alipotazama vizuri akagundua yale sio mawe ya kawaida ni mawe yenye madini ndani yake , kakinga alizidi kuyashangaa yale mawe yale mawe yalikuwa mengi sana kakinga aliyageuza geuza akagundua mawe yale yalikuwa ni almasi Kakinga japo aligundua kuwa zile ni almasi lakini hakuwa na uhakika wa kutosha kakinga alichukua jiwe moja akamfuata yule babu , Babu alikuwa kandokando ya bahari anavua samaki babu alikuwa anapenda kufanya hivyo kila siku majira ya usiku Kakinga alipofika kwa babu alikaa karibu yake kakinga akamuuliza babu :-



KAKINGA ?? Hivi babu kwanini unaishi huku ufukweni peke yako wewe hauna familia ?



BABU ?? ???? Unanifanya nifurahi sana kijana wangu , Unazungumzia familia Mimi nilikuwa na familia yangu na nilikuwa na pesa za kutosha nakumbuka mwaka 1943 Nilipokuwa kijana mwenye umri kama wako Maisha yangu yalikuwa magumu sana kwa sababu nilikuwa sina baba wala mama Mimi nimelelewa katika vituo vya watoto yatima tu, Nilipokuwa kijana ninayejitambua niliwafuata wale walezi wa kituo cha watoto yatima nikawauliza historia ya maisha yangu daaah walinijibu kwamba hawajui Mimi nilitoka wapi kwa sababu walinikuta nje ya kituo chao nikiwa mtoto mdogo sana. Ukweli sikuridhika na majibu ya wale walezi wetu ikanibidi nimfuate mkuu wa kituo kile nilipofika kwa mkuu wa kituo alinikaribisha vizuri nikamuomba historia ya maisha yangu nilipewa majibu yale yale kama niliyopewa mwanzo lakini akaenda chumba cha kuhifadhi kumbukumbu za watoto wote wanaoishi pale akarudi na mfuko akanipatia akaniambia waliniokota na mfuko ule labda nikague naweza kugundua kitu niliuchukua ule mfuko nikarudi chumbani kwangu, Nilipoufungua ule mfuko nilikuta kuna picha mbili ya mwanamke na mwanaume nyuma ya zile picha zilikuwa zimeandikwa MAMA na BABA , Kwa haraka haraka niligundua wale watakuwa ni wazazi wangu nilitokwa na machozi mengi sana kwa kuwaona wazazi wangu kwa kupitia picha , niliendelea kukagua vitu ndani ya mfuko ule nikaona mfuko mweusi umefungwa vizuri nilipoufungua ule mfuko mweusi nikakuta kuna almasi nyingi sana nilitetemeka sana nikaficha ule mfuko japo nilikuwa nipo peke yangu chumbani, nikaurudisha ule mfuko kwa hofu kipindi naurudisha niliona kitabu kidogo nilichukua kile kitabu nilipokifungua nilikutana na historia nzima ya maisha yangu , kitabu kile alikiandika baba kabla hajapoteza maisha nililia sana daaah unanikumbusha machungu niliyoyapata kijana wangu ??????.



KAKINGA ?? Pole sana babu Nisamehe kwa kukumbusha mambo yaliyopita .



BABU ?? Usijali kijana wangu nili…niliii… Daah niligundua wazazi wangu waliuwawa kutokana na Mali walizokuwa nazo kuna kundi limejitengeneza na lina nguvu sana hadi ndani ya serikali yetu wapo watu hao kila sehemu wapo watu hao kazi yao ni kuwanyanganya watu Mali zao ardhi na kuwapoteza duniani, Niliumia sana nilitamani kulipa kisasi kwa watu hao lakini nilishindwa niliamua kuuza zile almasi nikafunga ndoa na nikajaliwa watoto watatu. Siku moja nikiwa na familia yangu nilivamiwa na watu nisiowajua wakambaka mke wangu alafu wakamchinja mke wangu pamoja na watoto wangu mbele ya macho yangu niliumia wakaninyanga Mali zangu zote.
 
SEHEMU YA 15 YA 50

Wakanipiga risasi wakajua nimekufa wakanitupa baharini nilisaidiwa na mtu nisiyemjua maisha yangu yakaishia hivyo hadi leo na walikuwa wananitafuta kwa kutumia alama hii.



Yule babu alivua shati lake akamuonesha Kakinga alama ile kakinga alistuka kumuona babu ameandikwa neno AKWELINA katika mgongo wake kama alivyo andikwa mtoto waliyenaye hadi leo. Kakinga akiwa na hofu kubwa alimuuliza babu :-



KAKINGA ?? Hiyo alama inamaana gani babu ?



BABU ?? Hii sio alama ni jina la huyo mshenzi anayeendesha kundi la hao watu na niliandikwa na wazazi wangu walitambua siku moja nitaweza kulipa kisasi lakini siwezi kutokana umri wangu huu lakini ninaamini ipo siku mungu ataleta mtu wa kuja kuwatoa hao mashetani kwa sababu kila siku wanazidi kuwatesa watu wasio na hatia na niligundua waliniwekea kifaa maalumu kilichokuwa kinawapatia taarifa sehemu yeyote nilipokuwepo walikiweka hapa katika mkono wa kulia kwamba huwezi kuwakimbia .



Kakinga aliposikia maneno yale toka kwa babu alikimbia haraka kumfuata akwelina ndani akamkuta amelala kakinga akamfunua nguo akwelina akamkagua katika mikono yote miwili akaona kovu katika mkono wa kushoto kakinga alipotazama vizuri akaona kuna kitu kinatoa mwanga mwekundu ndani ya kovu lile. Kipindi kakinga anashangaa kile kitu alisikia mlio wa risasi nje kakinga akatoka nje akamuona babu amedondoka ndani ya maji kwa mbali akaona meli ndogo inakuja ikiwa na wanajeshi kakinga ali………





Kakinga alirudi ndani haraka haraka akambeba akwelina akamweleza mke wake wapo katika hatari kubwa sana, Monna alianza kutetemeka , mapigo ya moyo walimwenda mbio Monna , Kakinga alitoka nje tena baada ya kukumbuka vitu walivyomkuta navyo Monna alivisahau nje. Wale wanajeshi walizidi kusogea sehemu alipokuwa kakinga na mke wake Monna , Kakinga alikaza moyo akamshika mkono mke wake.



“”” Kuwa jasiri mke wangu tupo sehemu hatari maisha yetu yapo hatarini lazima uwe na nguvu ili tumsaidie akwelina “””



Yamekuwa maneno ya kakinga akimwambia mke wake Monna ili kumpatia nguvu na faraja kwa sababu kakinga aligundua mke wake anatetemeka sana baada ya kumshika mkono, Maneno ya kakinga yaliupatia nguvu ya kutosha moyo wa Monna, Kakinga hakuhitaji kupoteza muda akatoka nje akiwa amemshika mkono Monna mke wake walitoka taratibu kakinga akachukua vile vitu walivyomkuta navyo akwelina kwakua kakinga alikuwa na wasiwasi sana alidondosha mfuko uliokuwa na almasi ndani yake, Walifanikiwa kutoka sehemu hiyo hatari kakinga na monna walipofika mbali wakajificha wakawaona wale wanajeshi wanauchukua mwili wa babu wakauchoma moto pamoja na nyumba yake masikini kitendo kile kilimuuma sana kakinga, Kakinga na monna wakiwa wamejificha eneo hilo walisikia sauti kali ikilia karibu yao kakinga alijaribu kuitafuta sauti ile ilipokuwa inatoka akagundua ilikuwa inatoka katika mkono wa akwelina.



Walipotazama mbele yao waliwaona wale wanajeshi wanakuja eneo walilokuwepo wakiwa na kitu chenye mfano wa simu katika mikono yao kakinga akamshika mkono mke wake wakakimbia. Safari yao ilikuwa ndefu sana Kwa bahati nzuri walifanikiwa kuwakimbia wale wanajeshi na ule mlio ulikuwa unatoka katika mkono wa akwelina uliacha kulia. Walimshukuru mungu kisha wakaendelea na safari japo walikuwa hawajui wapi wanapoelekea walitembea Kwa muda mrefu monna alikuwa amechoka sana akamuomba mume wake watafute sehemu wapumzike , kakinga alimsikiliza mke wake wakapumzika , Walipokuwa wamepumzika kakinga alimsimulia mke wake yote aliyozungumza na babu kule ufukweni, Monna alishangaa sana akamwangalia akwelina katika mkono wake akagundua ni kweli alichoambiwa na mume wake.



Monna alimuomba mume wake kakinga wampeleke akwelina hospital wakamtoe hicho kitu katika mkono, Kwakua walikuwa hawana pesa Monna alichukua cheni aliyopewa na marehemu mama yake akauza pesa walizopata wakaenda hospital walipofika daktari alimfanyia vipimo akwelina alafu akawaambia :



DAKTARI?? Ni kweli mtoto wenu anakifaa mkononi na hiyo ni GBS kifaa maalumu kinachotoa taarifa popote mtoto huyu atapokuwepo hiyo ni Moja , Mbili kifaa hicho kimewekwa kitaalamu sana kimeungwa kupitia mifipa ya fahamu sasa katika upasuaji wa mtoto huyu kuna matukio mawili KUFA au KUPONA kama mpo tayari niwaletee mkataba tunahitaji sahihi ( sign ) zenu .



Kakinga na monna walitazamana sana kakinga akasema …..
 
SEHEMU YA 16 YA 50





Kakinga na monna walitazamana sana kakinga akasema :-



KAKINGA ?? Fanya upasuaji dakatari naomba huo mkataba niweke sahihi .



MONNA?? ?? Hapana mume wangu hapana mtoto akifa ?



KAKINGA ?? Huwezi kuiziwia roho ya mtu kama muda wake umefika mke wangu tumuachie mungu kwa hili. Daktari Fanya kazi yako .



DAKTARI ?? Sawa nisubirini .



Daktari alitoka nje dakika kadhaa alafu akarudi ndani ya chumba chake akiwa na karatasi mkononi alipofika akampatia karatasi ile kakinga , Kakinga bila hofu alichukua kalamu alipotaka kuweka sahihi Monna alishika mkono wa mume wangu, kakinga alipomtazama mke wake alimuona amejawa na wasiwasi mkubwa, Kijasho chembamba kilikuwa kinamteremka Monna. Kakinga aliweka chini ile kalamu akamtazama Monna kwa muda mrefu sana alafu akamwambia :-



“””* Mke wangu wewe ndio mama wa mtoto huyu na siku zote mama huwa hakubali kumpoteza mtoto wake, Mama yupo tayari kuyapoteza maisha yake kwa ajili ya kupambania maisha ya mtoto wake na siku zote tiba ya kweli ya mtoto ni nafsi ya mama kama mama hujaridhia kwa mtoto kamwe kitu hicho hakiwezi kufanikiwa , samahani daktari kwakua mama amepinga jambo hili basi naomba tuondoke .



Kakinga alisimama akampatia Monna mkono ili waondoke Monna alifikiria sana akachukua ile kalamu akampatia kakinga, kitendo hicho kilimpatia faraja kakinga akaweka sahihi katika karatasi zile. Daktari alichukua zile karatasi akaziweka pembeni , akamchukua akwelina akaenda nae maabara. Daktari alichukua muda mwingi sana katika upasuaji huo , hali hiyo ilimpatia wasiwasi mkubwa Monna , Monna alikuwa anazunguka huku na huko ndani ya chumba cha daktari. Baada ya masaa sita kupita daktari alirudi :-



“””* Ndugu zangu tumshukuru mungu nimefanikiwa kufanya upasuaji salama wa mtoto wenu kwahiyo kuna dawa mnazotakiwa kununua.



Kakinga alimshukuru sana dakatri yule. Akwelina alitumia muda mrefu sana kupona hali iliyowatesa sana kakinga na mke wake Monna kutokana na kipato chao. Baada ya miezi mitatu akwelina alipona daktari aliwaruhusu warudi nyumbani lakini daktari alikuwa anamtazama sana Monna walipokuwa wanataka kuondoka daktari alimuuliza Monna :



DAKTARI ?? Samahani mnaishi sehemu gani ?



MONNA ?? Ni historia ndefu sana kifupi Mimi na mume wangu hatuna sehemu ya kuishi maisha yetu ni magumu sana .



DAKTARI ?? Ooh poleni sana na kwa hali ya mtoto anatakiwa apate chakula kizuri na sehemu safi kwakua umesema hamna sehemu ya kwenda basi Mimi nitawasaidia tutaenda sote kwangu mtaishi kwangu hadi mtapopata makazi yenu jina langu naitwa PATRICK .



Hakika ilikuwa ni furaha kwa kakinga na mke wake monna, waliendelea kumsubiri Dr Patrick katika chumba chake hadi alipomaliza kazi zake, Patrick alipomaliza kazi aliwachukua wakaenda hadi nyumbani kwake, Maisha yalianza kuwa matam na mazuri kwa kakinga na monna. Wanasema mapenzi ni kitu cha ajabu sana hiyo ilimkuta Patrick baada ya kuishi na familia ya kakinga taratibu taratibu Patrick alianza kuvutiwa na monna kutokana na uzuri aliokuwa nao , Monna alikuwa Mrembo sana baada ya kupata matunzo hali iliyosababisha Patrick kushindwa kuziwia hisia zake. Kwakua Patrick alishindwa kumwambia ukweli monna , Patrick alikuwa anamletea zawadi mbalimbali zenye thamani mno, kakinga alianza kuwa na mashaka kwa mke wake. Siku moja Patrick hakwenda kazini siku hiyo ilikuwa ni siku ya mapumziko. Monna alimka mapema sana siku hiyo kwakua alitambua Patrick yupo nyumbani , monna akiwa jikoni akiandaa chai Patrick alimfuata monna jikoni wakati huo monna alikuwa hajatambua kama Patrick yupo nyuma yake , Patrick alimshika kiuno monna , Monna alisisimka sana akageuka kumwangalia aliyemshika kiuno ni nani akashangaa kumuona ni Patrick monna ali……….





Monna alishikwa na aibu ya ajabu sana monna akabaki kutazama chini muda wote, Patrick alijisogeza karibu zaidi kwa monna akamshika mkono , Mapigo ya moyo ndani ya mwili wa monna yalikuwa yanakwenda mbio zaidi ya siku zote, Patrick alipogundua monna anatetemeka alitumia nafasi hiyo hiyo akamsogeza mdomo wake karibu ya sikio la monna akasema :-



?? Monna unajua wewe ni mrembo sana na hakika nimeshindwa kuziwia hisia zangu juu yako, kweli natambua umeolewa na pengine mume wako unampenda sana lakini nami ni binadamu pia naomba usinifikirie vibaya hizi ni hisia zangu kwako nipo tayari kufanya chochote utachohitaji katika dunia hii nakupenda monna naomba nipe nafasi japo theluthi nikuoneshe jinsi gani ninavyokupenda nakutakia asubuhi njema andaa chai vizuri nakupenda monna ??



Patrick baada ya kumwambia maneno hayo monna alimsogelea zaidi monna , monna hakuwa jasili akafumba macho , P
 
SEHEMU YA 17 YA 50

Patrick alitumia nafasi hiyo akahitaji kumpiga busu monna lakini kabla hajaufikia mdomo wa monna walisikia sauti ya kakinga akimwita mke wake , Patrick akaondoka jikoni haraka alitumia mlango wa nyuma kwa sababu jiko hilo lilikuwa na milango miwili tofauti , Kakinga alipoingia jikoni alimuona mke wake monna ana wasiwasi uliopitiliza kakinga alijaribu kjmuuliza monna lakini monna hakuzungumza kitu.



Siku zilizidi kwenda tabia ya Patrick kumletea zawadi monna haikuisha kila kukicha Patrick alizidi kumjali monna Kwa kumpatia fedha na vitu vikubwa zaidi. Siku iliyofuata kakinga alikuwa na monna sebuleni wanacheza na akwelina Patrick aliingia akiwa na boksi mbali za simu mkononi mwake kakinga aliwapatia simu wote, Daah kakinga alifurahi mno Kwa sababu katika maisha yake yote hakuwahi kumiliki simu. Yalipofika majira ya usiku simu ya monna iliita monna alipoitazama aliona namba mpya , Monna akapokea simu



?? Monna ni mimi Patrick kuna zawadi nimekununulia ipo nyuma yako ichukue hiyo kesho naomba kutoka na wewe peke yake kuna sehemu nahitaji twende kama hautojali *””



Monna aligeuka akaona mfuko alipofungua alikuta nguo nzuri sana , Monna alifurahi sana akamkubalia Patrick ombi lake . Siku iliyofuata asubuhi na mapema kakinga alimuaga mke wake kuna sehemu alituma maombi ya kazi, Monna kwakua hakuhitaji mume wake ajue safari yake na Patrick alifurahi. Muda ulizidi kwenda yalipofika majira ya mchana Patrick alichukua gari lake akamchukua monna , wakamuacha akwelina ndani peke yake akiwa amelala , Safari yao ilichukua muda kiasi hatimae wakafika sehemu husika hakika eneo lile lilikuwa linavutia sana , wakati monna anashangaa eneo lile Patrick alimkumbatia monna akamwambia :-

“”” NAKUPENDA MONNA nipe nafasi tafadhali “”



Monna alimgeukia Patrick Kwa macho ya kimahaba aka….





Monna alimgeukia Patrick Kwa macho ya kimahaba akajaribu kuzungumza maneno ambayo Patrick hakuyaelewa kabisa :



~~ Patrick mmmh unajua mimi daah sijui nifanyaje mimi Patrick unanipatia wakati mgumu daah .



Yalikuwa ni maneno ya monna akijing’atang’ata mbele ya Patrick, wakati wote huo Patrick alikuwa anamsoma monna aligundua monna hawezi kumkubalia kile alichohitaji kwa sababu monna alikuwa hajiamini pia monna alikuwa na wasiwasi uliotawala mwili na akili yake , Patrick hakuchoka akamvuta monna , monna alikuwa laini zaidi ya bamia monna alijikuta yupo katika kifua cha Patrick , Monna akiwa kifuani kwa Patrick, Patrick alisema :-



“”* Mungu kweli fundi muda aliopoteza wakati anakuumba wewe ninaamini hakujutia, Monna moyo wangu unaomba kuzungumza na wewe tafadhali zungumza na moyo wangu “”



Patrick alishika kichwa cha monna akamgeuza sikio la monna lilituwa upande wa kushoto mwa kifua cha Patrick monna aliyasikia mapigo ya moyo wa Patrick yanapiga kwa kasi sana Patrick alishika kichwa cha monna kwa Mara ya pili alafu akayatazama macho ya monna kwa muda mrefu sana, monna alishindwa kumtazama Patrick , Patrick akatumia nafasi hiyo akasogelea midomo ya monna alipoigusa tu monna akamsukuma Patrick , Patrick alidondoka chini monna aliogopa sana akamfuata Patrick akamuomba msamaha, Patrick alimwambia monna asijali lakini bado Patrick alikuwa analilia penzi kwa monna. Monna alisema :-



MONNA ?? Nisamehe Patrick kwa kukusukuma nimesikia ombi lako na usijali nipatie muda nitakujibu tafadhali vuta subira .



Patrick alifurahi sana kusikia maneno yale kutoka kwa monna, Patrick akamchukua monna wakapanda kwenye gari wakaenda sehemu nyingine. Kakinga alitoka katika ile kampuni aliyoomba kazi alitamani sana kumnunulia mke wake zawadi lakini kakinga hakuwa na pesa yeyote , kakinga alifikiria njia rahisi inayoweza kumpatia pesa kwa muda ule kwa ajili ya kumnunulia zawadi mke wake kipenzi, kakinga akaona bora aigize kama mlemavu ili apate pesa za kumnunulia zawadi mke wake baada ya kupata wazo hilo kakinga alifanikiwa kupata pesa kwa muda mfupi akachukua zile fedha akaenda kununua viatu kwa ajili ya mke wake, Kakinga aliporudi nyumbani alikuta nyumba imefungwa cha ajabu alisikia sauti ya mtoto ndani analia kakinga alichungulia dirishani akamuona akwelina analia akiwa chini , Kakinga alichanganyikiwa sana kakinga alitafuta njia ya kuingia ndani akaikosa ikabidi avunje dirisha akaingia ndani akamkuta akwelina amedondoka chini damu zinamtoka puani.



Kakinga alishikwa na hasira sana akampatia huduma ya kwanza akwelina alafu akatoka nje ya nyumbani ile akakaa chini . Muda ulikwenda sana hatimae usiku ukaingia kakinga akiwa ndani ya giza nene kwa sababu hakuwasha taa lolote katika nyumba ile alimuona Patrick anafungua geti akiwa na monna, Patrick akiwa amemshika kiuno monna waliingia ndani monna akiwa na furaha sana , walipoona giza monna akasema :



MONNA ?? Mbona giza hivi au mume wangu hajarudi ?
 
SEHEMU YA 18 YA 50



PATRICK ?? Aaah yule ni mwanaume buana atarudi tu kwani mimi sio mume wako ?



MONNA ?? Usijali nawe siku moja utakuwa mume wangu hata sio mbali washa taa ya simu tuingie ndani basi .



PATRICK ?? Subiri kidogo monna kwani unawahi nini huko ndani sasa siingii ndani hadi unipige busu la nguvu kama sivyo nalala nje hapahapa .



MONNA ?? Jamani Patrick sawa sogea nahofu mume wangu asije nikuta lakini si nilikuambia nipe muda ila usijali busu tu sawa.



Patrick alifurahi akamvuta karibu monna akamshika kiuno kimahaba alafu akambusu kwenye shavu , baada ya hapo wakasogea karibu ya nyumba Patrick akawasha taa ya simu yake ule mwanga wa taa ulipowaka walimuona kakinga amekaa karibu na mlango monna ali……..





Ule mwanga wa taa ulipowaka walimuona kakinga amekaa karibu na mlango, monna alistuka sana:



“”* Mume wangu kumbe upo jamani nisamehe mume wangu tulikuwa mbali kwenye vikao , Patrick aliniomba nikamsaidie kazi Kwa sababu wewe uliondoka mapema sana .



Yalikuwa ni maneno ya monna akijaribu kumuelezea mume wake kakinga, Kakinga alimtazama sana monna hali iliyomfanya monna atetemeke kakinga akasema :



KAKINGA ??Na huko kushikana viuno na kupigana mabusu ni moja ya kazi za ofisini huko mlipokuwa ?



MONNA ?? Jamani mbona wanifikiria vibaya lakini nakuomba mume wangu tuliza hasira nisamehe kwa nilichofanya mbele yako najua umenitafsiri vibaya lakini sio kweli hicho unachofikiria kwa sasa.



KAKINGA ?? Sawa na vipi kuhusu mtoto kwanini usiondoke nae je kama ungemkuta kapoteza maisha unamuona alivyopata majeraha yote kwa ujinga wako.



PATRICK ?? Nisamehe mimi kaka kwa sababu mimi ndio nilimuomba niondoke nae na nilifahamu tutawahi kurudi lakini kwa bahati mbaya tumechelewa nisamehe mimi.



Siku zote kakinga huwa ni mwelewa sana japo alihisi kuna kitu kinaendelea baina ya Patrick na mke wake monna, kakinga alicheka sana akasema :-



KAKINGA ?? Hahaha ?? acha uoga mke wangu mimi nakuamini siwezi kuweka hofu kwako japo umeniudhi kwa kumuacha mtoto ndani si unajua nampenda sana mtoto wangu .



Monna na Patrick walishusha pumzi nzito baada ya kusikia maneno hayo toka kwa kakinga, Kakinga akamshika mkono mke wake wakaingia ndani walipofika ndani walisha taa Patrick aliona dirisha limevunja kakinga akamueleza hali iliyokuwepo. Siku baada ya siku ukarimu wa monna na Patrick ulizidi kuwa karibu zaidi, Kakinga alikuwa anaona yote hayo lakini alikuwa mkimya sana, Patrick hakuchoka kumletea monna zawadi mbalimbali kama kawaida yake kutokana na ukaribu huo, Monna alianza kumpenda Patrick. Siku baada ya siku monna alijikuta yupo busy sana na Patrick kuliko mume wake .



Kakinga hakuchoka kumchunguza mke wake, Baada ya siku mbili kupita monna alijikuwa nyumbani anafanya usafi siku hiyo Patrick alirudi nyumbani mapema akamkuta monna anafanya usafi monna alipomuona Patrick aliacha kufanya usafi akamkumbatia Patrick cha ajabu monna akambusu Patrick alafu akaondoka, Patrick alifurahi sana akasema :-



“”* Kazi imekwisha kilichobaki ni kufanya kitu ambacho nakihitaji toka kwake wooooooooh hahaha.



Patrick akaingia ndani kwake yote yalikuwa yanatendeka kakinga alikuwa anayaona akiwa nyuma ya ukuta, Roho ilitaka kupasuka kwa maumivu aliyokuwa nayo kakinga kwa sababu kakinga alikuwa anampenda sana mke wake. Usiku ulipofika wakawi katika meza ya chakula monna macho yake yote yalikuwa kwa Patrick bila kujali kakinga yupo nae eneo hili kitendo hicho kilimfnya kakinga aache chakula akaondoka , Monna alipoona kakinga kaondoka alifurahi sana akamsogelea Patrick akawa anamtania kwa kumtekenya tekenya yote hayo kakinga alikuwa anayashuhudia, Kiukweli kakinga alishindwa kuvumilia maumivu hayo.



Yalipofika majira ya asubuhi kakinga aliamka mapema sana akakusanya nguo zote akazifunga vizuri kakinga akamuamsha monna , monna alipoamka alimshangaa mume wake kakinga akamshika mkono monna wakatoka nje japo monna alikuwa hataki walipofika sebuleni wakammuta Patrick monna akamshika mkono Patrick kakinga akasimama akamuuliza monna :-



KAKINGA ?? Chagua Mona monna kuondoka na mimi au kubaki na Patrick ?



Cha ajabu monna ali…



Cha ajabu monna alitoa mkono kwa kakinga alafu akasogea kwa Patrick, Kakinga aliishiwa nguvu akadondosha begi la nguo alilokuwa ameshika , Ilikuwa ni ngumu sana kuamini kile anachoona mbele yake !



“”””””” Nisamehe sana kakinga “”””



Moyo wa kakinga ulizidi kwenda mbio kwa kusikia leo Monna kwa Mara ya kwanza anataja jina hilo , kakinga alizoea kuitwa mume , mpenzi na baba watoto hasira alizokuwa nazo kakinga zilimfanya ashikwe na kizunguzungu , kakinga alishika kichwa chake kwa muda mrefu kiasi Monna hakumuonea huruma kakinga akaendelea kusema:



MONNA???? Naomba msamaha tena mbele yako kwa kufanya hiki ninachofanya katika maisha yako , Najua nimetoka mbali na wewe na umenivumilia kwa mambo mengi sana, Kakinga hadi sasa nimeishi na wewe kwa miaka mingi zaidi ya sita bado hali yako sio nzuri kimaisha nimekuvumilia sana kakinga lakini
 
SEHEMU YA 19 YA 50

bado unahali mbaya ya kimaisha , kula kwetu tabu , kuvaa tabu hatuna sehemu ya kuishi daah nimechoka kakinga naomba taraka yangu leo hii hii na nitakurudishia pesa yako ya mahari. Mimi nahitaji mwanaume mwenye pesa miaka zaidi ya sita hata mtoto sina na sijapata hata kichefuchefu sasa hebu niambie napata faida gani kwako ?



PATRICK ?? Heeeeh !!?? yule mtoto sio wako ?



MONNA ?? Nizae wapi huyo mtoto nimemuokota tu hata sio wangu pia huyu mwanaume nikiwa nae ndani anakuwa mvi…



KAKINGA ?? Basiiiiiiiiii monna ?? unapokwenda sipo ni kweli upo sahihi Mimi sio mzima siwezi kuzalisha si ndiyo ? Na pia Mimi masikini sana lakini tatizo kwanini haukuniambia mapema laiti ungeniambia mapema nisingeruhusu moyo wangu ukupende kiasi hiki , Monna nakupenda mke wangu mtoe shetani kichwani naomba shika mkono wangu huu twende tukatafute maisha nakupenda monna siwezi kupinga hili kweli nakupenda.



Pamoja na kakinga kutetea penzi lake haikusaidia kitu monna aliingia ndani baada ya muda alitoka nje akiwa ameshika karatasi pamoja na kalamu akampatia kakinga, Monna akaomba taraka . Kakinga alifikiria sana mwisho akaamua kuchukua maamuzi magumu akaandika taraka wakati anampatia taraka kakinga alimwangalia sana monna machozi yakiwa yanamteremka alisema :-



“” Monna kwa sasa upo huru nimefanya hivi kwa sababu wewe umetaka hivyo nilikuahidi kwamba nitafanya chochote ili uwe na furaha hata kama kitaniumiza Mimi lakini wewe uwe na furaha milele chukua taraka yako monna lakini kumbuka “” Kimvuli chako ndio rafiki yako kipenzi popote utapokuwepo hakiwezi kukuacha lakini ukiwa gizani kamwe hautakiona , Patrick ndugu yangu nakukabidhi binti huyu naomba mpende kweli usimdanganye kwa sababu maumivu ya mapenzi leo nimeyafahamu hakika mapenzi yanauma sana kwaheri monna.



Kakinga alirudi ndani akatoka na akwelina akiwa amelala akamtazama tena monna masikini kisha akaondoka. Maneno aliyosema kakinga yalimpatia mawazo sana monna lakini, Patrick akamshika mkono monna wakarudi ndani. Kakinga akiwa na akwelina mgongoni hakutambua aende wapi masikini , Kakinga alitembea huku na huko akiwa na mawazo yaliyotawala fikra zake, Kakinga alijikuta yupo barabarani hadi majira ya usiku kutokana na kutembea sana akwelina alikuwa amechoka sana akaanza kulia hali iliyomfanya kakinga atambue akwelina atakuwa anataka kula kakinga alienda kuuza simu aliyonunuliwa na Patrick akapata pesa akamnunulia chakula akwelina.



Majira hayo hayo monna akiwa ndani pamoja Patrick, Patrick alikuwa huru katika mwili wa monna usiku huo Patrick aliutawala mwili wa monna atakavyo , Monna nae hakuwa mchoyo alimpatia chochote alichohitaji Patrick wakiwa katika mambo hayo maneno ya kakinga yalijirudia katika masikio ya monna , monna akabadirika ghafla hali iliyomfanya Patrick alazimishe kufanya mapenzi na monna , Monna hakukubali kufanya mapenzi kwa nguvu Patrick akachukia akatoka kitandani akafungua kabati akachukua bastola akamnyoshea monna kisha ……..



Monna kisha akamfuata akasema :-



“” Sikia wewe mwanamke Mimi katika maisha yangu sipendi kukataliwa kile Mimi ninachohitaji na siwezi kufanya kile ambacho wewe unataka hapa upo kwangu sasa sikia unafanya ninachotaka au hutaki ?



Monna alikuwa anatetemeka sana , pamoja na jeuri aliyokuwa nayo lakini alianza kulia , Patrick alipomuona monna bado anasita kufanya kile anachohitaji akaiweka sawa bastola ile ( Kuikoki ) ;-



“”” Basi basi Patrick mpenzi wangu nimekubali usiniue nipo tayari kufanya mapenzi na wewe tafadhali usiniue njoo mume wangu Mimi ni wako kwanini nisikupatie kile unachohitaji nakupenda sana Patrick wangu .



Yalikuwa maneno ya monna akimwambia Patrick akiwa na hofu kubwa moyoni, Patrick alicheka sana kwa , Patrick alicheka zaidi akasema:



“” Oooh kumbe unaweza kukubali kufanya mapenzi baada ya kulazimishwa na kwanini iwe hivyo wakati nakupenda , sikia monna nilikuwa nakupima imani tu hii sio bastola hili ni toy nilikuwa nimenunua kwa ajili ya mtoto wako kabla yule mjinga kakinga hajaondoka nae hahaha siku nyingine jitahidi kutokubali kufanya kitu amacho hukipendi bora ufe sawa inatakiwa uwe na msimamo mke wangu sawa acha kuogopa hovyo leo hatutafanya kwakua hautaki usijali siku ukiwa tayari utaniambia sawa mke wangu .



Patrick akaweka ile bastola pembeni akarudi juu ya kitanda akamkumbatia monna wakalala , Patrick alizima taa akasema moyoni.



“” Unabahati mjinga wewe leo umepona lakini nitakupata ngoja nikujengee uaminifu kwanza .



Hali ya hewa ilianza kubadirika baada ya masaa kadhaa mvua ilinyesha , mvua ilikuwa kubwa yenye upepo na baridi ndani yake , Mvua hiyo ilimkuta kakinga bado yupo ndani ya mgahawa akimpatia chakula akwelina, Baada ya muda mchache kupita muuza mgahawa alifunga mgahawa wake akamwambia kakinga aondoke , kakinga alimuelezea muuza mgahawa yote yaliyomkuta lakini haikusaidia kitu muuza mgahawa alimfukuza kakinga akiwa na akwelina mkononi kakinga alipofika nje alivua shati akamfunika akwelina ili asinyeshewe na mvua hiyo kakinga akaanza kutembea ovyo huku na huko kutafuta sehemu ya kujikinga na mvua baada ya kutembea sana kakinga ilimbidi akae kwenye kituo cha daladala japo kilikuwa wazi , kakinga akamfunika vizuri akwelina.
 
Back
Top Bottom