Abou Shaymaa
JF-Expert Member
- Oct 19, 2022
- 1,479
- 3,229
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA KWANZA
MTUNZI: EDGAR MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
TAHADHARI: Hadithi hii ya #ASALI_HAITIWI_KIDOLE inayo somwa na mtu mwenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea, ni hadithi yenye kisa chenye ubunifu kwa hasilimia mia moja, sehemu, mitaa na majina yaliyo tumika, siyo harisi, ni ya kufikilika, na ayausiani na kisa hiki.
Kama kuna tukio au kitu chochote kitafanana katika hadithi hii, na tukio la kweli, basi aikuwa dhamira ya mwandishi, kama utakuwa na maoni ushauri au lolote wasiliana na mwandishi wa hadithi hii, si luksa kunakiri au kubadiri hadithi hii kwa lolote, katika matumizi yoyote, pasipo kibari cha mwandishi kupitia whatsapp namba 0717924403 au 0743632247.
Naaaaaaam!, hadithi yetu inaanzia kisiwani Zanzibar, ilikuwa ni jumanne yenye shamla shamla za sikuu za eid ya mfungo mosi, hii ni eid Ahl hadji, moja kati ya kuku kubwa sana kisiwani hapa.
Kama ilivyo kawaida, kwa wakazi wa kisiwa hiki, siku ya leo ilikuwa na pilika nyingi sana, toka asubuhi walionekana wake kwa waume wakitoka msikitini, huku wamependeza kwa mavazi mazuri mpya yenye kuvutia, huku wanawake wakiongoza kwa kupendeza, wakifwatiwa na watoto.
Hakika leo ni siku ambayo, hasilimia kubwa ya watu, walionekana wakiwa wenye nyuso za furaha, arufu nzuri ya vyakula ilizagaa mitaani, na kushibisha pua za kila wapita njia na wakazi, sambamba na sauti za music wa kasiwida, zilizokuwa zinasikika toka kwenye nyumba za watu, kila kona ya mitaa, na sehemu mbali mbali za biashara, zikizidi kuing’alisha siku kuu hii, ambayo kwa huku kisiwani uwa inasherehekewa kwa muda wa siku mbili, mpaka nne.
Mida ya saa saba za mchana, tupo mtaa wa jang’ombe kwa Soudi, ni mtaa wapili, toka kituo cha Mchina mwanzo, barabara kuu ya kiembe samaki, kupitia uwanja wa Amani.
Mtaa umechangamka sana kama mitaa mingine ya kiswahili, wanaonekana watu wengi wa lika mbali mbali, yani watoto vijana na wazee, wakike kwa wakiume, waliokuwa wamevalia nguo nzuri na mpya za kupendeza, huku wanawake wakiwa wamejipamba zaidi kwa kuchora mikono yao mauwa mazuri kwa kutumia wino wa ina.
Pia wanawake wananukia vyema utuli wa udi, wameficha miili yao kwenye magauni mazuri aina ya baibuhi na habaya, huku vichwani mwao wakificha nywele zao kwa hijab, za rangi mbali mbali, zilizoendana na nguo walizovaa.
Lakini tofauti ilikuwa nyumbani kwa mzee Abeid Ally Makame, ambapo kwanza kabisa, tuna mwona mzee Abeid mwenyewe anatoka nyumbani, akiwa ameongozana na wake zake wawili, yani mke mkubwa, akiwa mwenye hasiri ya Africa bila chembe chembe yoyote ya uchotara, huku bi mdogo akionekana kwenye dalili ya mbali ya uchotara.
Wake wote wawili wa Abeid Makame, wakiwa wamevalia vizuri, magauni yao mapya na hijab zao, zilizo zidi kuwapendezesha, pamoja na viatu vyao vizuri vya mikanda, kama ilivyokuwa kwa mume wao, ambae ni mwalimu wa shule ya sekondari ya mwanakwelekwe A, alie valia kanzu yake nyeupe mpya, na baraghashia nzuri yenye rangi ya kanzu yake.
Chini alivalia makubanzi, (sendo) za kisasa, ya rangi nyeusi, huku hasiri ya mzee huyu akiwa ni mwafrika hasiria bila chembe chembe yoyote ya mshanganyiko wa hasiri ya taifa au kabila jingine toka nje ya bara la africa.
Lakini ukiwatazama vyema watu awa watatu, utagundua utofauti kati yao, asa katika mwonekano wa hali ya nyuso zao, maana wakati mzee Abeid akiwa katika hali ya kawaida, mke mdogo alionekana kuwa katika hali ya kukosa furaha, kwa kiasi flani, huku mke mkubwa akiwa mwingi wa tabasamu.
Wakati huo huo, kwenye kibaraza cha nyumba ya mwalimu Abeid Makame, wanaonekana watu watatu, wote wakiwa na hasiri ya uchotara japo ulikuwa umefifia, lakini uliwapendezesha, kati yao alikuwepo binti mdogo wakike mwenye umri wa kati ya miaka kumi adi kumi na moja, pia wakiume mwenye umri wa miaka kati ya kumi sita adi kumi na saba.
Walikuwa na dada yao, ambae umri wake, ni mkadilio wa miaka kati ya ishilini sita au ishilini na tano, aliekuwa anawasindikiza kwa macho baba na mama zake, huku uso wake ukiwa umenyongea kwa mawazo, nae pia kama wale watoto, alikuwa na hasiri ya uchotara, ambao licha ya kuwa ulio fifia, lakini uzuri wake ulionekana wazi wazi, kuanzia sura adi mwili wake, ata uzuni aliyonayo usoni mwake ilishindwa kuondoa uzuri wake wa hasiri.
Tofauti na wadogo zake ni kwamba, yeye alikuwa amevalia mavazi ya kawaida, ambayo japo yalikuwa ni masafi, na unaweza kuvalia popote katika siku za kawaida, pengine ata leo ndiyo aliyovaa msikitini, lakini ni wazi yalikuwa ya zamani, tunaweza kusema yalisha maliza eid moja au mbili kabla ya leo.
Ila pia licha mwonekano wa uzuri wake huo, akuwa amejipamba kwa chochote, kama wanawake wengine wahuko mtaani, ni kama wale watoto wawili, ambao mavazi yao licha ya kuwa masafi, ila pia yalionekana ayakuwa mapya, huku wote wakiwa wamekaa kibarazani, nyuso zao zimekata tamaa, macho yao yakitazama kushoto na kulia, yani kwenye barabara ya mtaa, ni wazi walitarajia kumwona mtu flani.
“kaka Mu, mbona rafiki yako mwenyewe aji sasa?” aliuliza yule mschana mdogo, wa miaka kumi na moja, huku anamtazama yule kijana wamiaka kumi na saba, ambae akujibu kitu zaidi ya kutazama kushoto na kulia, huku uso wake ukionyesha wasi wasi na kukata tamaa.
Dada mkubwa anawatazama wadogo zake, huku anawaona jinsi walivyo sawajika nyuso zao, “dada Radhia, mpigie kwanza umuulize mbona aji” anasema yule mschana mdogo, ambae ni kama alisha kata tamaa, au aliona anacheleweshwa jambo flani.
“Jamani Zahara, uwe mvumilivu kidogo, kwani na yeye binadamu eti, lazima ale akoge ndio aje” anasema yule mwanamke mkubwa, kwa sauti tulivu iliyolemewa na uchungu flani, ambae kwa matazamo wa kawaida, ni mzuri wa sura umbo na rangi ya ngozi yake, “alisema anakuja mchana, lakini mpaka sasa ajaja” alilalamika Zahara.
Zilisha pita dakika kumi, toka mzee Abeid na mke wake waondoke, sasa mlango mkubwa wa mbele unafunguliwa, wanatokea watu watano, yani wanawake wawili wakubwa, mmoja akiwa na umri wa miaka 24 na mwenzie akiwa na umri wa miaka 21, wakiwa na watoto watatu, wakike wawili na wakiume mmoja, ambao umri wao aukuzidi miaka sita, mdogo kabisa akiwa na mkadilio wa miaka mitatu.
Wote walikuwa wenye hasiri ya weusi, lakini awa dada wawili walikuwa wamejipamba wakapambika, na kufanya ule msemo wa usichague mke ngomani utimie, maana licha ya kuwa walikuwa ni wazuri kiasiri, na wenye kuvutia lakini siyo kama Radhia, huyu alie kaa hapa kibarazani, ila walizidi kupendeza kwa mapambo walivyo jiweka. ITAENDELEA…….
Sehemu Ya Pili
SIMULIZI: Asali haitiwi kidole
Sehemu Ya Tatu
SIMULIZI: Asali haitiwi kidole
Sehemu Ya Nne
SIMULIZI: Asali haitiwi kidole
Sehemu Ya Tano