amoc thedon
JF-Expert Member
- Jul 19, 2016
- 345
- 531
Narudi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimesoma tu aya moja ya kwanza nikaona nikushauri kwanza.....
Kama wewe ni mwandishi jitahidi kutumia lugha kwa ufasaha una makosa sana kwenye uandishi.
"Kubadiri" ni kubadili
"Shamla shamla" ni shamra shamra
"Harisi" ni halisi
"Hasilimia" ni asilimia
Nk nk nk
Bila shaka utaupokea ushauri kwa moyo mweupe.
Naleta sehemu inayofuataTuendelee sasa,Edgar atabadili dini au ??
endelea bans wataikutaTuendelee au mpaka baadae watu watakapo kuwa free?
Edgar staili yake hio hajawahi badilika , ila ana idea nzuri sana , Somulizi zake zina addiction mbayaNimesoma tu aya moja ya kwanza nikaona nikushauri kwanza.....
Kama wewe ni mwandishi jitahidi kutumia lugha kwa ufasaha una makosa sana kwenye uandishi.
"Kubadiri" ni kubadili
"Shamla shamla" ni shamra shamra
"Harisi" ni halisi
"Hasilimia" ni asilimia
Nk nk nk
Bila shaka utaupokea ushauri kwa moyo mweupe.
Mi nikisoma hivyo nakatika stimuEdgar staili yake hio hajawahi badilika , ila ana idea nzuri sana , Somulizi zake zina addiction mbaya
ASALI HAITIWI KIDOLETuendelee
🤝🤝🤝ASALI HAITIWI KIDOLE
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA KUMI
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA TISA: Radhia na wadogo zake wanasimama pembeni ya barabara, wanatazama kushoto na kulia, kuona kama wangemwona Edgar, lakini awamwoni, Radhia kijasho kinamtoka, anaingiwa na wasi wasi, hofu inamtanda, anawatazama wadogo zake, anajiuliza watakuwa na hali gani pale watakapo ona wameachwa kwenye mataa. ENDELEA….
Kwanza kabisa ni ili eneo la mtaa ambalo waliambiwa waje kukutana na Edgar, ni mtaa ambao ukiachilia hotel ndogo, bar na nyumba ya wageni, pia na dispensal binafsi, kulikuwa na mitaa miwili iliyotenganishwa na barabara kuu ya lami, ya upande wapili iendayo uwanja ndege.
Upande wakulia wa barabara, ukiachana na nyumba ya kwanza kabisa ya rais wa zamani wa Zanzibar, kulikuwa na ikulu ya rais wa Zanzibar, pamoja na jengo mbali mbali ya ofisi za balozi za nchi mbali mbali, pia zaidi ya hapo kulikuwa na eneo la ngazi mia, hizo zote zikipakana na bahari ya hind, kwa upande wa magharibi mwa kisiwa hiki.
Upande wakushoto wa barabara hii, kulikuwa na majengo makubwa, ya watu mbali mbali, yaliyokuwa yanakaliwa na viongozi mbali mbali wa ngazi za juu wa serikali, na baadhi ya balozi toka nchi mbali mbali.
Radhia akiwa mwenye hofu na mashaka makubwa, anabofya simu yake, ili kupiga namba ya Edgar, ili hali anajuwa fika simu yake aikuwa na salio, tegemeo lake ni ule ujumbe ambao utaingia kwa Edgar, lakini kabla aja piga simu, mala anaiona simu yake inaanza kuita, na mpigaji akiwa ni Edgar.
Radhia anaachia tabasamu la matumaini, anaipokea haraka ile simu, “hallow, uko wapi weye, sie tupo hapa kilimani?” aliuliza Radhia, mala tu baada ya kupokea simu, huku anatazama kulia kwake, hakuna mtu yoyote, anatazama kushoto kwake, kama angeweza kumwona Edgar.
Radhia anawaona mtu wawili walio valia suit nyeusi miwani nyeusi na viatu vyeusi, ndani ya koti jeusi vifuani mwao likionekana shati jeupe, wakiwa nyuma ya mtu mmoja alie valia tishert jeusi, la mikono mifupi, kaputura ya kaki yenye mifuko chini yani usawa wa mapajani, kama nguo za jeshi, chini alivalia raba nyeupe zenye fito nyeusi, ambae pia alikuwa anaongea na simu, walikuwa wanatoka nje ya geti moja, la nyumba moja kati ya zile zilizopo upande wa kushoto, mita kama sitini toka walipo.
Radhia anawaona wale jamaa walio valia suit nyeusi, na yule mwenzao alie valia kaptula, wanatazama kushoto na kulia, “mme simama wapi mbona siliona Taxi” Radhia anamsikia Edgar anauliza toka upande wapili wa simu.
Radhia anaingiwa na kigugumizi, anashindwa kujibu kwa haraka, “hooo!, nimewaona, mbona kama hamna taxi, inamaana ame waacha na kuondoka bila kumlipa?” anauliza Edgar upande wapili wa simu, huku Radhia anamwona, yule aliekuwa amesimama na wale watu walio valia suit anaanza kutembea kuwa fwata, huku ameshikilia simu usawa wa sikioni.
“da Radhia kaka Edgar yule paleeee” anasema Zuhura, huku anaonyesha upande ule walipo wale watu waliokuwa wamevalia suit nyeusi, ambao sasa walikuwa wanakuja upande wao wakiongozana na yule alievalia kaptula, ambae anamtambua moja kwa moja, kuwa ni Edgar rafiki yake Mukhsin, “hapana atukuchukuwa taxi, niliona tutakuongezea gharama” anasema Radhia, “hapana bwana, usiwaze kuhusu gharama, umewachosha hao madogo” anasema Edgar kabla ya kukata simu.
Radhia na wadogo zake wakiwa na matumaini ya kukutana na Edgar, wanamwona anasimama na kuwageukia wale watu wawili, anawaamiwa jambo, kisha nao wanageuka na kurudi walikotokea, yani kwenye lile jumba kubwa, lenye uzio mkubw waukuta, na geti kubwa sana la chuma, huku Edgar anaendelea kutembea kuwa fwata wao.
Wakina Radhia wanaendelea kumtazama, “kumbe anakaa pale?” aliuliza Zahara, kwa sauti yenye kujawa na furaha, huku anamtazama kaka yake Mukhsin, swali ambalo ata Radhia alitamani kuuliza, “ata mi mwenyewe sijuwi, mi uwa namwona kwenye mazoezi tu” ilo ndilo jibu toka kwa Mukhsin.
Edgar anawafikia, na kuungana nao, “asalm alykum” anasalimia Edgar, Zahara na Mukhsin wanaikia kwa pamoja, kasoro Radhia ambae anabakia ametabasamu, “asalam aleykum” anasalimia Radhia, huku uso wake ujawa na tabasamu na kijiaibu, sijuwi kwanini uwa anajikia aibu mbele ya Edgar, “alekum salaam” anajibu Edgar, kisha wanaanza kutembea taratibu, kufwata barabara.
“basi mie niwaache, narudi zangu nyumbani” anasema Radhia, huku anasimama na Edgar nae anasimama sambamba na wakina Zahara, “ni sawa kama kuna mtu anakusubiri au kuna jambo unaenda kufanya nyumbani, lakini ikikupendeza nivyema tukiwa pamoja kwaajili ya kumsimaia dada mdogo” alisema Edgar.
Radhia alishtuka kwa furaha moyoni mwake, maana alitamani sana hii safari iwe ya wote, lakini aliingiwa na wasi wasi jinsi alivyokuwa amevaa, na ukichukulia hakuwa na nanguo nyingine mpya, lakini kabla ajajibu lolote, Zahara akaaribu zaidi, “mie sina shaka lolote, naweza kujisimamia mwenyewe, labda ukaaongee na kaka Edgar, maana atakuwa peke yake wakati sisi tunacheza” anasema Zahara, na hapo Radhia anamtazama Edgar, ambae pia alikuwa anamtazama yeye.
Macho yao yanakutana, wote wanatabasamuliana huku Radhia anakwepesha macho yake, na kutazama chini, “jamani kaka Edgar, nitawatia aibu huko, ebu ona nilivyo” anasema Radhia, kwa sauti iliyo jaa aibu, huku anacheka cheka kikike, “kwanini Radhia, mbona hata mimi nipo kaiwada tu, twenzetu unielekeze mitaa” alisema Edgar kwa sauti yake nzito, kwa namna ya kushawishi.
“anaona aibu hajanunuliwa nguo mpya kama wakina dada Mariam” alisema Zahara, na hapo Radhia akamgeukia mdogo wake na kumkosa kibao, huku Zahara mwenyewe akimkimibilia Mukhsin, na kumfanya kinga yake, “mpuuzi wewe naniamekuambia unisemee” anasema Radhia, huku anamfwata tena Zahara, alie jibanza kwa Mukhsin, “we mwenyewe si umemchokoza, subiria saa akunyukue” alisema Mukhsin, huku anajitoa pembeni, kumwachia Radhia adabue Zahara.
Kuona hivyo Zahara anakimbilia kwa Edgar, ambae ndie msaada wake wamwisho, “Radhia bora unipige mimi baada yake, maana ndio niliuliza” anasema Edgar huku anamzuwia Radhia kwa kusimama mbele ya Zahara, bahati nzuri Radhia anaingiwa na aibu ya kumsogelea Edgar, anaacha kumfwata Zahara.
Ilikuwa ni tukio flani la kuwachangamsha, “usijari Zahara kesho tuta toka tena pamoja, kuna sehemu nimealikwa, nita nunua nguo nzuri kwaajili ya wote” anasema Edgar, huku wanaanza kutembea kuelekea kilimani hotel, ambapo palikuwa na magari ya kukodi yani taxi.
Radhia na wadogo zake wanatazamana, kwa sekunde kadhaa, kisha wanatabasamu kwa furaha, “kweli kaka Edgar” aliuliza Mukhsin, “sidhani kama kuna siku niliwai kukudanganya” anasema Edgar, na wakati huo walikuwa wanaingia kilimani hotel ambako walikodi taxi moja na kuelekea mjini, “nyie ndio mnajuwa sehemu za kwenda kutembea, mimi siijuwi ata moja” alitahadhalisha Edgar, wakiwa njiani. ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPAHAPA JAMII FORUMS
OkASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA KWANZA
MTUNZI: EDGAR MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
TAHADHARI: Hadithi hii ya #ASALI_HAITIWI_KIDOLE inayo somwa na mtu mwenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea, ni hadithi yenye kisa chenye ubunifu kwa hasilimia mia moja, sehemu, mitaa na majina yaliyo tumika, siyo harisi, ni ya kufikilika, na ayausiani na kisa hiki.
Kama kuna tukio au kitu chochote kitafanana katika hadithi hii, na tukio la kweli, basi aikuwa dhamira ya mwandishi, kama utakuwa na maoni ushauri au lolote wasiliana na mwandishi wa hadithi hii, si luksa kunakiri au kubadiri hadithi hii kwa lolote, katika matumizi yoyote, pasipo kibari cha mwandishi kupitia whatsapp namba 0717924403 au 0743632247.
Naaaaaaam!, hadithi yetu inaanzia kisiwani Zanzibar, ilikuwa ni jumanne yenye shamla shamla za sikuu za eid ya mfungo mosi, hii ni eid Ahl hadji, moja kati ya kuku kubwa sana kisiwani hapa.
Kama ilivyo kawaida, kwa wakazi wa kisiwa hiki, siku ya leo ilikuwa na pilika nyingi sana, toka asubuhi walionekana wake kwa waume wakitoka msikitini, huku wamependeza kwa mavazi mazuri mpya yenye kuvutia, huku wanawake wakiongoza kwa kupendeza, wakifwatiwa na watoto.
Hakika leo ni siku ambayo, hasilimia kubwa ya watu, walionekana wakiwa wenye nyuso za furaha, arufu nzuri ya vyakula ilizagaa mitaani, na kushibisha pua za kila wapita njia na wakazi, sambamba na sauti za music wa kasiwida, zilizokuwa zinasikika toka kwenye nyumba za watu, kila kona ya mitaa, na sehemu mbali mbali za biashara, zikizidi kuing’alisha siku kuu hii, ambayo kwa huku kisiwani uwa inasherehekewa kwa muda wa siku mbili, mpaka nne.
Mida ya saa saba za mchana, tupo mtaa wa jang’ombe kwa Soudi, ni mtaa wapili, toka kituo cha Mchina mwanzo, barabara kuu ya kiembe samaki, kupitia uwanja wa Amani.
Mtaa umechangamka sana kama mitaa mingine ya kiswahili, wanaonekana watu wengi wa lika mbali mbali, yani watoto vijana na wazee, wakike kwa wakiume, waliokuwa wamevalia nguo nzuri na mpya za kupendeza, huku wanawake wakiwa wamejipamba zaidi kwa kuchora mikono yao mauwa mazuri kwa kutumia wino wa ina.
Pia wanawake wananukia vyema utuli wa udi, wameficha miili yao kwenye magauni mazuri aina ya baibuhi na habaya, huku vichwani mwao wakificha nywele zao kwa hijab, za rangi mbali mbali, zilizoendana na nguo walizovaa.
Lakini tofauti ilikuwa nyumbani kwa mzee Abeid Ally Makame, ambapo kwanza kabisa, tuna mwona mzee Abeid mwenyewe anatoka nyumbani, akiwa ameongozana na wake zake wawili, yani mke mkubwa, akiwa mwenye hasiri ya Africa bila chembe chembe yoyote ya uchotara, huku bi mdogo akionekana kwenye dalili ya mbali ya uchotara.
Wake wote wawili wa Abeid Makame, wakiwa wamevalia vizuri, magauni yao mapya na hijab zao, zilizo zidi kuwapendezesha, pamoja na viatu vyao vizuri vya mikanda, kama ilivyokuwa kwa mume wao, ambae ni mwalimu wa shule ya sekondari ya mwanakwelekwe A, alie valia kanzu yake nyeupe mpya, na baraghashia nzuri yenye rangi ya kanzu yake.
Chini alivalia makubanzi, (sendo) za kisasa, ya rangi nyeusi, huku hasiri ya mzee huyu akiwa ni mwafrika hasiria bila chembe chembe yoyote ya mshanganyiko wa hasiri ya taifa au kabila jingine toka nje ya bara la africa.
Lakini ukiwatazama vyema watu awa watatu, utagundua utofauti kati yao, asa katika mwonekano wa hali ya nyuso zao, maana wakati mzee Abeid akiwa katika hali ya kawaida, mke mdogo alionekana kuwa katika hali ya kukosa furaha, kwa kiasi flani, huku mke mkubwa akiwa mwingi wa tabasamu.
Wakati huo huo, kwenye kibaraza cha nyumba ya mwalimu Abeid Makame, wanaonekana watu watatu, wote wakiwa na hasiri ya uchotara japo ulikuwa umefifia, lakini uliwapendezesha, kati yao alikuwepo binti mdogo wakike mwenye umri wa kati ya miaka kumi adi kumi na moja, pia wakiume mwenye umri wa miaka kati ya kumi sita adi kumi na saba.
Walikuwa na dada yao, ambae umri wake, ni mkadilio wa miaka kati ya ishilini sita au ishilini na tano, aliekuwa anawasindikiza kwa macho baba na mama zake, huku uso wake ukiwa umenyongea kwa mawazo, nae pia kama wale watoto, alikuwa na hasiri ya uchotara, ambao licha ya kuwa ulio fifia, lakini uzuri wake ulionekana wazi wazi, kuanzia sura adi mwili wake, ata uzuni aliyonayo usoni mwake ilishindwa kuondoa uzuri wake wa hasiri.
Tofauti na wadogo zake ni kwamba, yeye alikuwa amevalia mavazi ya kawaida, ambayo japo yalikuwa ni masafi, na unaweza kuvalia popote katika siku za kawaida, pengine ata leo ndiyo aliyovaa msikitini, lakini ni wazi yalikuwa ya zamani, tunaweza kusema yalisha maliza eid moja au mbili kabla ya leo.
Ila pia licha mwonekano wa uzuri wake huo, akuwa amejipamba kwa chochote, kama wanawake wengine wahuko mtaani, ni kama wale watoto wawili, ambao mavazi yao licha ya kuwa masafi, ila pia yalionekana ayakuwa mapya, huku wote wakiwa wamekaa kibarazani, nyuso zao zimekata tamaa, macho yao yakitazama kushoto na kulia, yani kwenye barabara ya mtaa, ni wazi walitarajia kumwona mtu flani.
“kaka Mu, mbona rafiki yako mwenyewe aji sasa?” aliuliza yule mschana mdogo, wa miaka kumi na moja, huku anamtazama yule kijana wamiaka kumi na saba, ambae akujibu kitu zaidi ya kutazama kushoto na kulia, huku uso wake ukionyesha wasi wasi na kukata tamaa.
Dada mkubwa anawatazama wadogo zake, huku anawaona jinsi walivyo sawajika nyuso zao, “dada Radhia, mpigie kwanza umuulize mbona aji” anasema yule mschana mdogo, ambae ni kama alisha kata tamaa, au aliona anacheleweshwa jambo flani.
“Jamani Zahara, uwe mvumilivu kidogo, kwani na yeye binadamu eti, lazima ale akoge ndio aje” anasema yule mwanamke mkubwa, kwa sauti tulivu iliyolemewa na uchungu flani, ambae kwa matazamo wa kawaida, ni mzuri wa sura umbo na rangi ya ngozi yake, “alisema anakuja mchana, lakini mpaka sasa ajaja” alilalamika Zahara.
Zilisha pita dakika kumi, toka mzee Abeid na mke wake waondoke, sasa mlango mkubwa wa mbele unafunguliwa, wanatokea watu watano, yani wanawake wawili wakubwa, mmoja akiwa na umri wa miaka 24 na mwenzie akiwa na umri wa miaka 21, wakiwa na watoto watatu, wakike wawili na wakiume mmoja, ambao umri wao aukuzidi miaka sita, mdogo kabisa akiwa na mkadilio wa miaka mitatu.
Wote walikuwa wenye hasiri ya weusi, lakini awa dada wawili walikuwa wamejipamba wakapambika, na kufanya ule msemo wa usichague mke ngomani utimie, maana licha ya kuwa walikuwa ni wazuri kiasiri, na wenye kuvutia lakini siyo kama Radhia, huyu alie kaa hapa kibarazani, ila walizidi kupendeza kwa mapambo walivyo jiweka. ITAENDELEA…….