SIMULIZI: Asali haitiwi kidole

SIMULIZI: Asali haitiwi kidole

Nimesoma tu aya moja ya kwanza nikaona nikushauri kwanza.....

Kama wewe ni mwandishi jitahidi kutumia lugha kwa ufasaha una makosa sana kwenye uandishi.

"Kubadiri" ni kubadili
"Shamla shamla" ni shamra shamra
"Harisi" ni halisi
"Hasilimia" ni asilimia
Nk nk nk

Bila shaka utaupokea ushauri kwa moyo mweupe.
 
Umeeleweka kiongozi litafanyiwa kazi na wahariri wangu
Nimesoma tu aya moja ya kwanza nikaona nikushauri kwanza.....

Kama wewe ni mwandishi jitahidi kutumia lugha kwa ufasaha una makosa sana kwenye uandishi.

"Kubadiri" ni kubadili
"Shamla shamla" ni shamra shamra
"Harisi" ni halisi
"Hasilimia" ni asilimia
Nk nk nk

Bila shaka utaupokea ushauri kwa moyo mweupe.
 
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA SABA
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITA: “yah!, ilikuwa lazima nije, nazani kuna jambo la kumsaidia Mukhsin akimaliza shule, japo ni mapema sana kuliongelea hilo” aliongea Edgar ambae utulivu ni jadi yake, “wakati huo alikuwa yeye, lakini sasa ndugu tumesha ongezeka, unaweza kuja kutusalimia siku moja moja” anasema Radhia ambae kila muda ulivyoenda alianza kumzowea kijana huyu, “alafu dada nimekumbuka kitu” alisema Zahara, nawote wawili wakamtazama. ENDELEA….

Bila kumwuliza amekumbuka nini, wakamwona anamtazama Edgar, “kaka namimi naomba ni nunulie vi….” alisema Zahara, kabla ajamaliza Radhia akadaka na kumziba mdomo, “we Zahara upitiwi” alisema Radhia, kwa sauti ya chini, “mwache seme bwana, siumesema sisi nindugu” alisema Edgar kwa sauti tulivu yenye uzito wake wakumsisimua Radhia, ambae alikuwa anatamani aendleea kukaa karibu na kijana Edgar.

Wakati huo huo, tayari Mukhsin alikuwa anarudi na begi lake mkononi, “sasa kaka Edgar wacha sie twende maana tulipitia tu kumwona huyu bwana anavyo cheza mpira” alisema Radhia, huku anataka kuondoka, “samahani dada Radhia, nivyema kama tutakaa sehemu, ilitupate juice au ice creem kidogo” alisema Edgar, na wakwanza kujibu alikuwa Zahara.

“ndiyoooo!, nahamu na ice creem” alisema Zahara, na kumfanya Radhia cheke kidogo, “mwone kwanza, uroho tu, basi twendeni, lakini atutakiwi kukaa sana, mama asije kugomba” alisema Radhia, huku wakianza kutembea, yeye mdogo wake Zahara wakitangulia mbele, na kupatia nafasi Edgar, ya kuusanifu mwili mzuri wa mwanadada Radhia.

Walienda na kukaa kwenye kijihotel kidogo cha pale Gymkana, pembeni ya barabara inayo pakana na viwanja vya maisala, wakaagiza kila mmoja anacho hitaji,. Ikiwa ni juice na vitafunwa vyake, kama vile chips mishikaki, nyama choma, na vinginevyo.

Wakaendelea kula huku wanaongea ili na lile walicheka kwa furaha, na kuzidi kuzoweana, hata saa tano na nusu za asubuhi, ikwiwa ni masaa matatu, toka wakutane, wakati wakuondoka Edgar akatoa fedha kiasi cha elfu 30, kwaajili ya kiatu cha shule cha Zahara.

Edgar alitaka kuwachukulia taxi, lakini Radhia akakataa, “tunakaa hapo nyuma tu” alisema Radhia, ambae ingekuchukuwa muda kidogo kubaini kuwa anatamani kuendelea kuwa karibu na kijana huyu, ambae kiukweli alionyesha kumheshimu na kumchukulia kama mwanamke wakawaida, tofauti na kule mtaani kwao.

“sawa basi, wacha niwasindikize mpaka hapo mbele, maana sijawai kutembelea mitaa ya huku mbele” anasema Edgar, huku wanaanza kutembea taratibu kuelekea upande wajang’ombe, kimya kilitawara kwa muda mfupi, Edgar ndie alie vunja ukimya, , “dada Radhia, nivyema ukichukuwa namba yangu ya simu, kama kuna lolote mna weza kunipigia” alisema Edgar.

Na hapo Radhia akatoa simu yake haraka, na kumpatia Edgar, ambae aliandika namba yake na kumrudishia, nae akasave kwa jina la Edgar, na kisha akamtumia sms kijana huyu, akiandika jina lake, “Radhia” Edgar nae akaisave, kwa jina ilo ilo la Radhia.

Walitembea taratibu huku wakiongea ili na lile, njiani watu walionekana kumshangaa sana kijana Edgar, asa wanawake, kitu ambacho Radhia akukipenda, aliona ni kama wanamshawishi Edgar awatazame pia.

Edgar akufika mbali sana, akawaaga na kuondoka zake, akionyeshwa njia ya mkato ya kutokea barabara kuu.********

Huo ndio ulikuwa mwanzo wa Radhia kufahamiana na jina huyu ambae ni rafiki wa mdogo wake, kijana ambae kila mwanamke angependa kuwa nae, japo kijana huyu akuwai kupiga simu wala kuwatuma ujumbe, toka alipochukuwa namba ya simu kwa Radhia.

Mama Radhia alishangaa na kushtuka kidogo, alipo ona Zuhura nae amemumuliwa kiatu na kijana huyo huyo, alie munulia viatu Mukhsin, “Radhia kuna usalama kweli?” aliuliza mama Radhia, “nikijana mstaarabu wala siyo mtu wa hovyo” alijibu Radhia, na mama yake akamwamini, maana anaifahamu tabia nje ya binti yake.

Zilipita week mbili na nusu, toka RAadhia akutane na Edgar, pale uwanjani, Radhia alitamani kumwona tena kijana huyu, lakini hakuwa na sababu, maana tayari mashindano yalikuwa yameisha, lakini zikiwa zimebakia siku tatu, kabla ya siku kuu ya Eid kubwa, maandalizi ya yalikuwa yamepamba moto, wakina Mariam walikuwa wanazungumzia mtoko wao na wapenzi wao utavyo kuwa, huku wakionyeshana nguo watakzo vaa siku ya mtoko huo, ambao walipanga kutoka na wadogo watoto wa kaka yao nayule mdogo wa dada yao.

Kwa upande wa Radhia yeye akuwa na lolote la kupanga, zaidi aliwafillia wadogo zake, japo huyu mkubwa alikuwa anauwezo wa kwenda kuzurula peke yake, lakini asingeweza kumwacha Zahara, ambae akipenda anyongee, pale atakapo waona wenzake wanaenda kutembea huku yeye akibakia nyumbani.

Uzalendo unamshinda Radhia, ambae anaamua kumchokoza Edgar, ambae hakuwai kuwasiliana nae toka alipo mpatia namba ya simu, hivyo aliitafuta namba ya kijana huyu, na kuipiga, “hauna salio la kutosha, kupiga namba hii, ongeza salio kisha jaribu tena” ndivyo ilivyosikika kwenye simu yake, siyo kwamba akujuwa kuwa hakuwa na salio, ila alifanya makusudi kwamaana kuna ujumbe ungeuingia kwenye simu ya mtu alie mtafuta.

Hii ilikuwa ni mida ya saa nne za asubuhi, lakini yalikatika masaa matatu, pasipo kupigiwa simu, nae akajikatia tamaa, lakini saa nane mchana, ndipo aliposikia simu yake inaanza kuita, simu ambayo toka aachike, nikama alikuwa anaitumia kuangalia muda tu, maana hapakuwa na mtu wa kumpigia mala ka mala.

Radhia anaikimbilia simu yake chumbani, na kuitazama mpigaji, anajikuta anatabasamu, “usingepiga ningekuchukia weye” anajisemea Radhia, huku anapokea simu, “hallow asalam aleykum” alisalimia Radhia kwa sauti tulivu nzuri yenye nidhamu ya hali ya juu, huku tabasamu likiwa limetanda usoni mwake, utasema amepokea simu ya mpenzi wake.

“aleykum salaam dada Radhia, habari za siku nyingi” ilisikika sauti nzito ya kiume toka upande wapili wa simu, na kumfanya Radhia azidi kuachia tabasamu, kwa kujiona afadhari kama ametuliwa mzigo mzito sana kichwani mwake, “salama tu, nimepia kukueleza kuwa, mama anasema asante sana kwa viatu vya Zuhura” alisema Radhia kwa sauti tulivu, yenye hali flani ya kijiaibu cha kike, “hoooo!, mwambie asante sana” ilisikika sauti ya Edgar, japo safari hii, ilikuwa imechangamka, lakini bado ilikuwa nzito.

Radhia anawaza namna ya kuwaombea offer ya mtoko wa siku kuu wadogo zake, lakini Edgar anamuwai, “vipi dada Radhia, unampango wa kunialika siku ya eid?” aliuliza Edgar huku anacheka kidogo, kicheko kiambukizwa kwa Radhia pia, “mh!, jamani sina uwezo huo, labda uje nyumbani, ule pilau kwa mzee Abeid” alisema Radhia, huku anacheka cheka. ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPAHAPA

Saa 2 tunashusha sehem inayofuata
 
Nimesoma tu aya moja ya kwanza nikaona nikushauri kwanza.....

Kama wewe ni mwandishi jitahidi kutumia lugha kwa ufasaha una makosa sana kwenye uandishi.

"Kubadiri" ni kubadili
"Shamla shamla" ni shamra shamra
"Harisi" ni halisi
"Hasilimia" ni asilimia
Nk nk nk

Bila shaka utaupokea ushauri kwa moyo mweupe.
Edgar staili yake hio hajawahi badilika , ila ana idea nzuri sana , Somulizi zake zina addiction mbaya
 
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA NANE
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA SABA: Radhia anawaza namna ya kuwaombea offer ya mtoko wa siku kuu wadogo zake, lakini Edgar anamuwai, “vipi dada Radhia, unampango wa kunialika siku ya eid?” aliuliza Edgar huku anacheka kidogo, kicheko kiambukizwa kwa Radhia pia, “mh!, jamani sina uwezo huo, labda uje nyumbani, ule pilau kwa mzee Abeid” alisema Radhia, huku anacheka cheka. ENDELEA….

Edgar nae akacheka kidogo, “ni mapema sana kuja nyumbani” alisema Edgar, huku anacheka kidogo, “rafiki zako wanashangaa tu, awajuwi wataingilia wapi siku ya Eid” alisema Radhia, kwa sauti ya kulalamika, ikiwa ni namna ya kuomba offer kwa wadogo zake, ili waweze kupata wasaa wamatembezi, “he!, kwahiyo mpaka leo hawajuwi watatokaje siku ya Eid?” anauliza Edgar kwa sauti yenye mshangao.

Hapo Radhia anajuwa tayari mtego wake umefanikiwa, “ndiyo ni wao tu ndio hawana wa kuwatembeza, wengine wote wamesha panga safari zao, ningekuwa na senti ningewapa wakatembee” anasema Radhia, safari hii kwa sauti ya kulalamika “kwa hiyo shemeji amekataa usiongozane na wakina Mukhsin?” anauliza Edgar kwa sauti yenye thadhari.

Radhia anatoa macho ya mshangao, “shemeji yupo na alisha nitariki zamani, sina hata utokaji, nitakuwepo tu hapa nyumbani, nawafikiria wao haswa” anasema Radhia bila wasi wasi, japo anapo maliza anakumbuka kuwa, kuachika kwake kumekuwa shida sana, kwa jamii inayo mzunguka, ambayo imepelekea kudharaulika na kusimangwa, na sasa amesha mwambia Edgar kuhusu kuachika kwake.

Radhia anasubiri kusikia Edgar ata sema nini, baada kusikia kuachika kwake, pengine alitegemea kuambiwa nitakupigia baadae, ikiwa ndio mwisho wa kuongea na kijana huyu, “hooo!, pole sana, sikuwai kufikiria kama mwanaume anaweza kumwacha mwanamke mzuri kama wewe” alisikika Edgar, kwa sauti nzito iliyojawa na mshangao, ni maneno ambayo Radhia ana yasikia kwa mala ya kwanza toka alipo achika.

Sijuwi kwanini, maneno ya Edgar, yalimpa Radhia raha moyoni mwake, na kumfanya ajihisi kama mtoto mchana mikononi mwa mama yake, akajikuta analengwa na machozi, huku anatabasamu, “mzuri niwe mie, wewe unakutana na wazuri wengi tu” alisema Radhia, huku anata basamu peke yake.

Edgar anacheka kidogo, “katika wazuri niliowahi kuwaona, wewe ni namba moja, tena mumeo ana bahati mbaya sana, naamini atajutia uamuzi wake” alisema Edgar, akionyesha akuwa anatania, “kwanini unasema hivyo kaka Edgar?” anauliza Radhia, kwa sauti ya tahadhari, “alikuacha mapema sana, hakufikilia mala mbili, yupo mwanaume atakufanya malikia katika nyumba yake” alisema Edgar, na hapo Radhia akajikuta anacheka kwa sauti ya chini, akitamani kudodosa zaidi, ilikujuwa Edgar anamaana gani.

Lakini kabla ajauliza, mlango wa chumbani ukafunguliwa, akaingia Zahara, “basi sawa mimi nilitaka kukujulisha ilo” anasema Radhia, kibadiri maongezi, ili mdogo wake wamiaka kumi, asije akasikia, “ok!, vipi kuhusu hiyo kesho kutwa, utajiandaa pamoja na watoto, ili tutoke wote” alisema Edgar, na kumfanya Radhia atabasamu, huku anamtazama Zahara.

Tabasamu la Radhia lina mshtua Zahara, ambae anahisi kuwa kunakitu kizuri kinacho muhusu, “dada kuna nini?” anauliza Zahara, lakini Radhia akumjibu, zaidi aliendelea kumtazama huku anatabasamu, “unaenda nao wao, mimi sidhani kama nitaweza maana nitakuaibisha sina nguo za kuvaa” anajibu Radhia, akimaanisha toka moyoni, kwamba lile gauni lake moja la kuvaa msikitini, na matembezi ya mjini, lisinge faa kuvaliwa kwenye mtoko huo wa pamoja.

Lakini akasikia kicheko toka upande wapili wa simu, “nani kasema utaniaibisha bwana, labda mimi ndio nita kuaibisha, tutakuwa pamoja kuwasindikiza watoto wakafurahi” alisema Edgar, kama vile anaongea kwa utani.

Tayari Zahara alisha juwa kinachoendelea, maana alishaanza kutabasamu, huku anafwatilia maongezi kwa karibu sana, “mh!, acha utani bwana, mi nitawaambia wajiandae, “sawa utanitajia muda wa kuja kuwachukuwa” alisema Edgar kabla hawaja agana na kukata simu.

Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwa Radhia Zahara na Mukhsin, pamoja na mama yao, japo Radhia mwenyewe, hakuwa anawaza kama atatoka na wadogo zake, kutokana na ukosefu wa vazi jipya la sikukuu, lakini hii haikuzuwia wanafamilia hao kufurahi pamoja, kwa kupata offer ya mtoko wa siku kuu, japo hawakujuwa itakuwa kwa kiwango gani, lakini haikuzidi hamu yao ya kutoka kwenda matembezi.

Lakini yote kwa yote, swala hili lilibakia kwa wanafamilia wanne tu, yani mama Radhia, Radhia mwenyewe, Mukhsin na Zahara, ambao awakuongea lolote kwa wenzao, ambao muda wote walionekana wakijinadi kuhusu mtoko wa eid wakiwatambia wenzao ambao walionekana kuwa hawakuwa na mpango wala uwezo wa kutoka matembezi.********

Lakini basi, siku ya leo mpaka mida hii ya saa nane kasoro za mchana, Edgar alikuwa ajapiga simu yoyote, wala ujumbe wakueleza kinachoendelea, licha ya wakina Zahara kujiandaa kwa mtoko na kusubiri sana, lakini bado akuwa ametokea kijana huyu.

Radhia anaingiwa na unyonge mkubwa sana, anawaza mambo mengi sana, “au amegairi kwa kuwa nilimwambia kuwa nimeachika” anawaza Radhia huku anatazama saa kwenye simu yake, anaona kuwa ni saa nane kasoro dakika kumi, “inamaana hata yale aliyo niambia ni uongo, au amepatwa na dharura, ameshindwa kuja kuwachukuw…” aliwaza Radhia, ambae alikatizwa na mtetemo wa simu yake.

Hakika moyo wake ulilipuka kwa mshtuko na hofu ambayo akujuwa ni kwanini imetokea, maana moja kwa moja alijuwa kuwa mpigaji ni Edgar, sababu simu yake aikuwa inapigiwa mala kwa mala, Radhia akaitazama simu yake na kuona kuwa ni kweli ilikuwa inapigwa, na mpigaji alikuwa ni Edgar, anaachia tabasamu pana la furaha. ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPAHAPA KWA
 
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA TISA
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA NANE: Hakika moyo wake ulilipuka kwa mshtuko na hofu ambayo akujuwa ni kwanini imetokea, maana moja kwa moja alijuwa kuwa mpigaji ni Edgar, sababu simu yake aikuwa inapigiwa mala kwa mala, Radhia akaitazama simu yake na kuona kuwa ni kweli ilikuwa inapigwa, na mpigaji alikuwa ni Edgar, anaachia tabasamu pana la furaha. ENDELEA….

Radhia anapokea simu, huku wadogo zake wote wawili wanamtazama, “hallow, asalam aleykum” anasalimia Radhia kwa sauti tulivu yenye tahadhari, maana hakujuwa ataambiwa nini, “aleykum salam Radhia, samahani nimechelewa kukupigia simu, nilikuwa na sehemu kwa mwaliko wa chakula cha mchana” alisikika Edgar, akiongea kwa sauti yenye kujilaumu kwa kukosea jambo, “bila samahani, sasa je unakuja ama?” anauliza Radhia, kwa sauti ya ukali kidogo, maana alisha ona dalili ya mambo kwenda vibaya.

“Radhia bwana siunafahamu kuwa nyumbani kwenu sipajuwi, chakufanya wachukue watoto, mpande taxi, mnipitie hapa maeneo ya kilimani” alisema Edgar, na hapo Radhia akatoa macho ya mshangao, “we Edgar unapenda utani haswa, hiyo hela ya dala dala sina, nitaipata wapi hela ya taxi?” anauliza Radhia na kumfanya Edgar acheke kidogo, “nyie pandeni, nitakuja kulipia hapa nilipo” alisema Edgar, huku anamalizia kucheka.

Unaweza kusema kuwa, Radhia alisha sahau ya kwamba, hakuwa na mpango wa kutoka siku ya leo, “nisubiri mala moja niwapeleke” alisema Radhia huku anainuka haraka na kuingia ndani, ambako alitumia dakika kumi na tano, mpaka anatoka, huku akiwa amesha oga na kuvalia lile gauni lake la mtoko, yani lile la kuendea mjini.

“haya twendeni sasa, atakuwa anatusubiri kilimani, kwanza hakuna hata aja ya kupanda taxi, tupite njia ya mkato” alisema Radhia, ambae alifunga mlango, na kuifadhi sehemu ambayo wanahifadhigi, wakati watu wote wakiwa wametoka.

Safari ikaanza huku kila mmoja akiwaza la kwake, wakati Zahara ana Mukhsin wakiwaza kuhusu namna watavyo furahia mtoko, Radhia aliwaza jinsi atakavyo washuhudia wadogo zake wakifurahi kuungana na yule kijana mrefu mstaarabu, yani Edgar, ambae mpaka awakujuwa habari zake zozote, kisha yeye kugeuka zake na kurudi nyumbani, kitu ambacho aliamini kuwa kingemfanya moyo wake ulidhike.

Ukweli ni kwamba, hii ilikuwa ni afadhari kubwa sana, kwa Radhia ambae alijiona kuwa, yeye ndie sababu ya wadogo zake kutengwa na kusimangwa, na wakina Mariam, yani wa toto wa mama yao mkubwa, ambae ni mke mkubwa wa baba yao.

Na kwamba ile kualikwa na Edgar, ilitosha kabisa kupunguza ukali na maumivu ya majisifu na masimango ya wakina Mariam na Zuhura.*******

Naaaaaam!, stendi ya darajani, palikuwa pamejaa watu wengi sana, wakiwa kati mavazi mazuri ya kupendeza, wengi ndio kwanza walikuwa wanashuka toka kwenye magari na kuelekea forodhani, ambako siku hii uwa inasherehekewa, sehemu ambayo siku kama hii ya leo, inakuwa inafulika watu, na kuwa na mshamla shamla za music na burudani mbali mbali.

Sambamba na mabanda ya kuuzia vitu mbali mbali, kama vile vya kula na vinywaji mbali mbali, michezo ya watoto na burudani nyingine kama hizo, na ndio sehemu nzuri pia, ya wapenzi wa siri kukutana.

Mariam na Zuhura wakiwa na watoto wa kaka yao na yule wa dada yao, pamoja na wakina Mahadhi mpenzi wa Zuhura na Mahamud, ambae ni mpenzi wa siri wa Mariam, wanaonekana washuka toka kwenye dala dala, yani chai maharage, linalofanya safari zake fuoni darajani.

Wanaanza kutembea kuelekea upande wa forodhani, huku njiani wakitazama vitu mbali mbali ambavyo vilikuwa vinauzwa, maalumu kwaajili ya kunogesha siku kuu, lakini wao awakuonekana kuangaika navyo maana, uwezo wa mifuko yao, ulikuwa ni ule mtoko na manunuzi madogo madogo, tena walichelea kuanza mapema, pengine wangekosa fedha ya kurudia.

Njiani hadithi na maongezi ya Mariam na Zuhura yalikuwa ni vile ambavyo wataenda kusimulia nyumbani, wakapo rudi, maana walimini kuwa, ingemuumiza sana dada yao Radhia, na wadogo zake, ambao waliamini kuwa, wasingeweza kutoka jang’ombe kwa soud mpaka forodhani, kwaajili ya kusherehekea, maana ukiachilia kuto kuwa na fedha ya nauri, pia awakuwa na nguo mpya.

“Mariam kesho inakuwaje” anauliza Mahamud, ambae alikuwa anaitaji kitumbua kwa siku ya kesho, “wewe tu, niwekee hela ya urojo na mishakaki tu (urojo ni chakula mfano wa uji, kinachotengenezwa kwa ngano viazi mbatata na mchanganyiko wa bagia nyama na viungo mbali mbali)” alisema Mariam, pasipo kupepea kope ya macho, “wala usijari, nitakuwekea” alisema Mahamud, ambae ni mtoto wa mwalimu wa shule ya kiembe samaki, huku yeye mwenyewe akijiusisha na ufundi wa TV, na redio.

Na wakati huo Zuhura akadakia, “Mahadhi mbona wewe uniambii, au auna ela ya urojo?” anauliza Zuhura, Mahadhi anacheka kidogo, akionekana wazi kupendezwa na mpango ule, “najuwa nyie ni mapacha, mmoja akitoka mwingine hawezi kubakia” anasema Mahadhi ambae baba yake ni mvuvi mzuri wa samaki, huku yeye mwenyewe akijusisha na ufundi wa redio na TV.

Zuhura anaachia tabasamu pana la furaha, “lakini tusikae sana huko, mi nataka na kesho tuje tumalizie huku forodhani” anasema Zuhura, kwa sauti iliyoonyesha wazi kuwa yenye furaha, “yani mdogo wangu wala usijari, mi mwenyewe nataka kila siku iwe ni mitoko tu, mpaka mjane aombe msahama, na laana yake ya wizi wa waume za watu” alisema Mariam, na wote wakacheka kwa nguvu wakisaidiwa na wapenzi wao.

Dakika kumi na tano baadae wanaibukia kwenye eneo la bustani nzuri za serikali, lililopo pembezoni mwa bahari maarufu kama malindi, ya mjini mangaribi, eneo ambalo leo hii, lilikuwa limefurika watu kibao, waliokuwa wamekaa kwenyenyasi fupi, wakijilia vitafunwa mbali mbali, na juice za hasiri au soda za viwandani.

Nao wanajichanganya na kujumuika na wenzao, sambamba na wapenzi wao, bila kuwaacha watoto wa kaka yao na yule wadada yao.*******

Saa nane na nusu Radhia, Zahara na Mukhsin, walikuwa wamesha ibuka maeneo ya kilimani, mita chache toka ilipo hotel maarufu ya kilimani, eneo ambalo, walionekana watu wengi wakiwa wanapita barabarani, wapo walio tembea kwa miguu, wapo walio panda dala dala, maarufu kama chai maarage, wapo wachache walio panda kwenye magari binafsi, pia wapo walio panda vipando, yani Vesper, hao wengi wao walikuwa ni mtu na mke wake mpenzi au rafiki, na wakizidi sana wapo na mtoto mdogo.

Wote hao walikuwa wanaelekea upande wa mjini, yani darajani au maeneo ya forodhani, kusherehekea siku ya eid, huku wakiwa wamependeza kweli kweli, na nyuso zao zikiwa zimepambwa kwa matabasamu.

Radhia na wadogo zake wanasimama pembeni ya barabara, wanatazama kushoto na kulia, kuona kama wangemwona Edgar, lakini awamwoni, Radhia kijasho kinamtoka, anaingiwa na wasi wasi, hofu inamtanda, anawatazama wadogo zake, anajiuliza watakuwa na hali gani pale watakapo ona wameachwa kwenye mataa. ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPAHAPA
USIKU MWEMA TUKUTANE ASUBUHI
 
Uchovu wa majukumu waungwana tutaendelea asubuh
 
Tuendelee
ASALI HAITIWI KIDOLE

ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA KUMI
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA TISA: Radhia na wadogo zake wanasimama pembeni ya barabara, wanatazama kushoto na kulia, kuona kama wangemwona Edgar, lakini awamwoni, Radhia kijasho kinamtoka, anaingiwa na wasi wasi, hofu inamtanda, anawatazama wadogo zake, anajiuliza watakuwa na hali gani pale watakapo ona wameachwa kwenye mataa. ENDELEA….

Kwanza kabisa ni ili eneo la mtaa ambalo waliambiwa waje kukutana na Edgar, ni mtaa ambao ukiachilia hotel ndogo, bar na nyumba ya wageni, pia na dispensal binafsi, kulikuwa na mitaa miwili iliyotenganishwa na barabara kuu ya lami, ya upande wapili iendayo uwanja ndege.

Upande wakulia wa barabara, ukiachana na nyumba ya kwanza kabisa ya rais wa zamani wa Zanzibar, kulikuwa na ikulu ya rais wa Zanzibar, pamoja na jengo mbali mbali ya ofisi za balozi za nchi mbali mbali, pia zaidi ya hapo kulikuwa na eneo la ngazi mia, hizo zote zikipakana na bahari ya hind, kwa upande wa magharibi mwa kisiwa hiki.

Upande wakushoto wa barabara hii, kulikuwa na majengo makubwa, ya watu mbali mbali, yaliyokuwa yanakaliwa na viongozi mbali mbali wa ngazi za juu wa serikali, na baadhi ya balozi toka nchi mbali mbali.

Radhia akiwa mwenye hofu na mashaka makubwa, anabofya simu yake, ili kupiga namba ya Edgar, ili hali anajuwa fika simu yake aikuwa na salio, tegemeo lake ni ule ujumbe ambao utaingia kwa Edgar, lakini kabla aja piga simu, mala anaiona simu yake inaanza kuita, na mpigaji akiwa ni Edgar.

Radhia anaachia tabasamu la matumaini, anaipokea haraka ile simu, “hallow, uko wapi weye, sie tupo hapa kilimani?” aliuliza Radhia, mala tu baada ya kupokea simu, huku anatazama kulia kwake, hakuna mtu yoyote, anatazama kushoto kwake, kama angeweza kumwona Edgar.

Radhia anawaona mtu wawili walio valia suit nyeusi miwani nyeusi na viatu vyeusi, ndani ya koti jeusi vifuani mwao likionekana shati jeupe, wakiwa nyuma ya mtu mmoja alie valia tishert jeusi, la mikono mifupi, kaputura ya kaki yenye mifuko chini yani usawa wa mapajani, kama nguo za jeshi, chini alivalia raba nyeupe zenye fito nyeusi, ambae pia alikuwa anaongea na simu, walikuwa wanatoka nje ya geti moja, la nyumba moja kati ya zile zilizopo upande wa kushoto, mita kama sitini toka walipo.

Radhia anawaona wale jamaa walio valia suit nyeusi, na yule mwenzao alie valia kaptula, wanatazama kushoto na kulia, “mme simama wapi mbona siliona Taxi” Radhia anamsikia Edgar anauliza toka upande wapili wa simu.

Radhia anaingiwa na kigugumizi, anashindwa kujibu kwa haraka, “hooo!, nimewaona, mbona kama hamna taxi, inamaana ame waacha na kuondoka bila kumlipa?” anauliza Edgar upande wapili wa simu, huku Radhia anamwona, yule aliekuwa amesimama na wale watu walio valia suit anaanza kutembea kuwa fwata, huku ameshikilia simu usawa wa sikioni.

“da Radhia kaka Edgar yule paleeee” anasema Zuhura, huku anaonyesha upande ule walipo wale watu waliokuwa wamevalia suit nyeusi, ambao sasa walikuwa wanakuja upande wao wakiongozana na yule alievalia kaptula, ambae anamtambua moja kwa moja, kuwa ni Edgar rafiki yake Mukhsin, “hapana atukuchukuwa taxi, niliona tutakuongezea gharama” anasema Radhia, “hapana bwana, usiwaze kuhusu gharama, umewachosha hao madogo” anasema Edgar kabla ya kukata simu.

Radhia na wadogo zake wakiwa na matumaini ya kukutana na Edgar, wanamwona anasimama na kuwageukia wale watu wawili, anawaamiwa jambo, kisha nao wanageuka na kurudi walikotokea, yani kwenye lile jumba kubwa, lenye uzio mkubw waukuta, na geti kubwa sana la chuma, huku Edgar anaendelea kutembea kuwa fwata wao.

Wakina Radhia wanaendelea kumtazama, “kumbe anakaa pale?” aliuliza Zahara, kwa sauti yenye kujawa na furaha, huku anamtazama kaka yake Mukhsin, swali ambalo ata Radhia alitamani kuuliza, “ata mi mwenyewe sijuwi, mi uwa namwona kwenye mazoezi tu” ilo ndilo jibu toka kwa Mukhsin.

Edgar anawafikia, na kuungana nao, “asalm alykum” anasalimia Edgar, Zahara na Mukhsin wanaikia kwa pamoja, kasoro Radhia ambae anabakia ametabasamu, “asalam aleykum” anasalimia Radhia, huku uso wake ujawa na tabasamu na kijiaibu, sijuwi kwanini uwa anajikia aibu mbele ya Edgar, “alekum salaam” anajibu Edgar, kisha wanaanza kutembea taratibu, kufwata barabara.

“basi mie niwaache, narudi zangu nyumbani” anasema Radhia, huku anasimama na Edgar nae anasimama sambamba na wakina Zahara, “ni sawa kama kuna mtu anakusubiri au kuna jambo unaenda kufanya nyumbani, lakini ikikupendeza nivyema tukiwa pamoja kwaajili ya kumsimaia dada mdogo” alisema Edgar.

Radhia alishtuka kwa furaha moyoni mwake, maana alitamani sana hii safari iwe ya wote, lakini aliingiwa na wasi wasi jinsi alivyokuwa amevaa, na ukichukulia hakuwa na nanguo nyingine mpya, lakini kabla ajajibu lolote, Zahara akaaribu zaidi, “mie sina shaka lolote, naweza kujisimamia mwenyewe, labda ukaaongee na kaka Edgar, maana atakuwa peke yake wakati sisi tunacheza” anasema Zahara, na hapo Radhia anamtazama Edgar, ambae pia alikuwa anamtazama yeye.

Macho yao yanakutana, wote wanatabasamuliana huku Radhia anakwepesha macho yake, na kutazama chini, “jamani kaka Edgar, nitawatia aibu huko, ebu ona nilivyo” anasema Radhia, kwa sauti iliyo jaa aibu, huku anacheka cheka kikike, “kwanini Radhia, mbona hata mimi nipo kaiwada tu, twenzetu unielekeze mitaa” alisema Edgar kwa sauti yake nzito, kwa namna ya kushawishi.

“anaona aibu hajanunuliwa nguo mpya kama wakina dada Mariam” alisema Zahara, na hapo Radhia akamgeukia mdogo wake na kumkosa kibao, huku Zahara mwenyewe akimkimibilia Mukhsin, na kumfanya kinga yake, “mpuuzi wewe naniamekuambia unisemee” anasema Radhia, huku anamfwata tena Zahara, alie jibanza kwa Mukhsin, “we mwenyewe si umemchokoza, subiria saa akunyukue” alisema Mukhsin, huku anajitoa pembeni, kumwachia Radhia adabue Zahara.

Kuona hivyo Zahara anakimbilia kwa Edgar, ambae ndie msaada wake wamwisho, “Radhia bora unipige mimi baada yake, maana ndio niliuliza” anasema Edgar huku anamzuwia Radhia kwa kusimama mbele ya Zahara, bahati nzuri Radhia anaingiwa na aibu ya kumsogelea Edgar, anaacha kumfwata Zahara.

Ilikuwa ni tukio flani la kuwachangamsha, “usijari Zahara kesho tuta toka tena pamoja, kuna sehemu nimealikwa, nita nunua nguo nzuri kwaajili ya wote” anasema Edgar, huku wanaanza kutembea kuelekea kilimani hotel, ambapo palikuwa na magari ya kukodi yani taxi.

Radhia na wadogo zake wanatazamana, kwa sekunde kadhaa, kisha wanatabasamu kwa furaha, “kweli kaka Edgar” aliuliza Mukhsin, “sidhani kama kuna siku niliwai kukudanganya” anasema Edgar, na wakati huo walikuwa wanaingia kilimani hotel ambako walikodi taxi moja na kuelekea mjini, “nyie ndio mnajuwa sehemu za kwenda kutembea, mimi siijuwi ata moja” alitahadhalisha Edgar, wakiwa njiani. ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPAHAPA JAMII FORUMS
 
Hivi hili jukwaa halina kigezo cha umri wa member kujoin, au wafanye namna wadogo wasiaccess hizi nyuzi negative kwa watoto ambao wakikua nao watakuwa followers
 
🤝🤝🤝
 
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA KWANZA
MTUNZI: EDGAR MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.

TAHADHARI: Hadithi hii ya #ASALI_HAITIWI_KIDOLE inayo somwa na mtu mwenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea, ni hadithi yenye kisa chenye ubunifu kwa hasilimia mia moja, sehemu, mitaa na majina yaliyo tumika, siyo harisi, ni ya kufikilika, na ayausiani na kisa hiki.

Kama kuna tukio au kitu chochote kitafanana katika hadithi hii, na tukio la kweli, basi aikuwa dhamira ya mwandishi, kama utakuwa na maoni ushauri au lolote wasiliana na mwandishi wa hadithi hii, si luksa kunakiri au kubadiri hadithi hii kwa lolote, katika matumizi yoyote, pasipo kibari cha mwandishi kupitia whatsapp namba 0717924403 au 0743632247.

Naaaaaaam!, hadithi yetu inaanzia kisiwani Zanzibar, ilikuwa ni jumanne yenye shamla shamla za sikuu za eid ya mfungo mosi, hii ni eid Ahl hadji, moja kati ya kuku kubwa sana kisiwani hapa.

Kama ilivyo kawaida, kwa wakazi wa kisiwa hiki, siku ya leo ilikuwa na pilika nyingi sana, toka asubuhi walionekana wake kwa waume wakitoka msikitini, huku wamependeza kwa mavazi mazuri mpya yenye kuvutia, huku wanawake wakiongoza kwa kupendeza, wakifwatiwa na watoto.

Hakika leo ni siku ambayo, hasilimia kubwa ya watu, walionekana wakiwa wenye nyuso za furaha, arufu nzuri ya vyakula ilizagaa mitaani, na kushibisha pua za kila wapita njia na wakazi, sambamba na sauti za music wa kasiwida, zilizokuwa zinasikika toka kwenye nyumba za watu, kila kona ya mitaa, na sehemu mbali mbali za biashara, zikizidi kuing’alisha siku kuu hii, ambayo kwa huku kisiwani uwa inasherehekewa kwa muda wa siku mbili, mpaka nne.

Mida ya saa saba za mchana, tupo mtaa wa jang’ombe kwa Soudi, ni mtaa wapili, toka kituo cha Mchina mwanzo, barabara kuu ya kiembe samaki, kupitia uwanja wa Amani.

Mtaa umechangamka sana kama mitaa mingine ya kiswahili, wanaonekana watu wengi wa lika mbali mbali, yani watoto vijana na wazee, wakike kwa wakiume, waliokuwa wamevalia nguo nzuri na mpya za kupendeza, huku wanawake wakiwa wamejipamba zaidi kwa kuchora mikono yao mauwa mazuri kwa kutumia wino wa ina.

Pia wanawake wananukia vyema utuli wa udi, wameficha miili yao kwenye magauni mazuri aina ya baibuhi na habaya, huku vichwani mwao wakificha nywele zao kwa hijab, za rangi mbali mbali, zilizoendana na nguo walizovaa.

Lakini tofauti ilikuwa nyumbani kwa mzee Abeid Ally Makame, ambapo kwanza kabisa, tuna mwona mzee Abeid mwenyewe anatoka nyumbani, akiwa ameongozana na wake zake wawili, yani mke mkubwa, akiwa mwenye hasiri ya Africa bila chembe chembe yoyote ya uchotara, huku bi mdogo akionekana kwenye dalili ya mbali ya uchotara.

Wake wote wawili wa Abeid Makame, wakiwa wamevalia vizuri, magauni yao mapya na hijab zao, zilizo zidi kuwapendezesha, pamoja na viatu vyao vizuri vya mikanda, kama ilivyokuwa kwa mume wao, ambae ni mwalimu wa shule ya sekondari ya mwanakwelekwe A, alie valia kanzu yake nyeupe mpya, na baraghashia nzuri yenye rangi ya kanzu yake.

Chini alivalia makubanzi, (sendo) za kisasa, ya rangi nyeusi, huku hasiri ya mzee huyu akiwa ni mwafrika hasiria bila chembe chembe yoyote ya mshanganyiko wa hasiri ya taifa au kabila jingine toka nje ya bara la africa.

Lakini ukiwatazama vyema watu awa watatu, utagundua utofauti kati yao, asa katika mwonekano wa hali ya nyuso zao, maana wakati mzee Abeid akiwa katika hali ya kawaida, mke mdogo alionekana kuwa katika hali ya kukosa furaha, kwa kiasi flani, huku mke mkubwa akiwa mwingi wa tabasamu.

Wakati huo huo, kwenye kibaraza cha nyumba ya mwalimu Abeid Makame, wanaonekana watu watatu, wote wakiwa na hasiri ya uchotara japo ulikuwa umefifia, lakini uliwapendezesha, kati yao alikuwepo binti mdogo wakike mwenye umri wa kati ya miaka kumi adi kumi na moja, pia wakiume mwenye umri wa miaka kati ya kumi sita adi kumi na saba.

Walikuwa na dada yao, ambae umri wake, ni mkadilio wa miaka kati ya ishilini sita au ishilini na tano, aliekuwa anawasindikiza kwa macho baba na mama zake, huku uso wake ukiwa umenyongea kwa mawazo, nae pia kama wale watoto, alikuwa na hasiri ya uchotara, ambao licha ya kuwa ulio fifia, lakini uzuri wake ulionekana wazi wazi, kuanzia sura adi mwili wake, ata uzuni aliyonayo usoni mwake ilishindwa kuondoa uzuri wake wa hasiri.

Tofauti na wadogo zake ni kwamba, yeye alikuwa amevalia mavazi ya kawaida, ambayo japo yalikuwa ni masafi, na unaweza kuvalia popote katika siku za kawaida, pengine ata leo ndiyo aliyovaa msikitini, lakini ni wazi yalikuwa ya zamani, tunaweza kusema yalisha maliza eid moja au mbili kabla ya leo.

Ila pia licha mwonekano wa uzuri wake huo, akuwa amejipamba kwa chochote, kama wanawake wengine wahuko mtaani, ni kama wale watoto wawili, ambao mavazi yao licha ya kuwa masafi, ila pia yalionekana ayakuwa mapya, huku wote wakiwa wamekaa kibarazani, nyuso zao zimekata tamaa, macho yao yakitazama kushoto na kulia, yani kwenye barabara ya mtaa, ni wazi walitarajia kumwona mtu flani.

“kaka Mu, mbona rafiki yako mwenyewe aji sasa?” aliuliza yule mschana mdogo, wa miaka kumi na moja, huku anamtazama yule kijana wamiaka kumi na saba, ambae akujibu kitu zaidi ya kutazama kushoto na kulia, huku uso wake ukionyesha wasi wasi na kukata tamaa.

Dada mkubwa anawatazama wadogo zake, huku anawaona jinsi walivyo sawajika nyuso zao, “dada Radhia, mpigie kwanza umuulize mbona aji” anasema yule mschana mdogo, ambae ni kama alisha kata tamaa, au aliona anacheleweshwa jambo flani.

“Jamani Zahara, uwe mvumilivu kidogo, kwani na yeye binadamu eti, lazima ale akoge ndio aje” anasema yule mwanamke mkubwa, kwa sauti tulivu iliyolemewa na uchungu flani, ambae kwa matazamo wa kawaida, ni mzuri wa sura umbo na rangi ya ngozi yake, “alisema anakuja mchana, lakini mpaka sasa ajaja” alilalamika Zahara.

Zilisha pita dakika kumi, toka mzee Abeid na mke wake waondoke, sasa mlango mkubwa wa mbele unafunguliwa, wanatokea watu watano, yani wanawake wawili wakubwa, mmoja akiwa na umri wa miaka 24 na mwenzie akiwa na umri wa miaka 21, wakiwa na watoto watatu, wakike wawili na wakiume mmoja, ambao umri wao aukuzidi miaka sita, mdogo kabisa akiwa na mkadilio wa miaka mitatu.

Wote walikuwa wenye hasiri ya weusi, lakini awa dada wawili walikuwa wamejipamba wakapambika, na kufanya ule msemo wa usichague mke ngomani utimie, maana licha ya kuwa walikuwa ni wazuri kiasiri, na wenye kuvutia lakini siyo kama Radhia, huyu alie kaa hapa kibarazani, ila walizidi kupendeza kwa mapambo walivyo jiweka. ITAENDELEA…….
Ok
 
Back
Top Bottom