SIMULIZI: Asali haitiwi kidole

SIMULIZI: Asali haitiwi kidole

ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI: Radhia na wadogo zake wanatazamana, kwa sekunde kadhaa, kisha wanatabasamu kwa furaha, “kweli kaka Edgar” aliuliza Mukhsin, “sidhani kama kuna siku niliwai kukudanganya” anasema Edgar, na wakati huo walikuwa wanaingia kilimani hotel ambako walikodi taxi moja na kuelekea mjini, “nyie ndio mnajuwa sehemu za kwenda kutembea, mimi siijuwi ata moja” alitahadhalisha Edgar, wakiwa njiani. ENDELEA….

Ukweli Radhia aliipenda ile safari, lakini akuifurahia sana, maana uvaa ji wake alijishtukia sana, hivyo akuipenda kuonekana mbele za watu wengi, asa anao fahamiana nao, wakiwa wale wa mtaani kwao na wale alio kaa nao wakati ameolewa, “leo kutakuwa na fujo sana, mimi napenda sehemu tulivu” alisema Radhia, na yule dereva wa taxi akadakia, “kwa heshimiwa kama nyie, kuna sehemu ya kukaa, nitawalekeza” alisema dereva wa taxi, ambae kiukweli aliwashangaza kuanzia Radhia mwenyewe adi wakina Zahara, ambao walijiuliza wanauheshimiwa gani.*******

Twende nyuki bar, iliyomo mita chache toka kwenye jambi la jeshi, maarufu kama IDD BA VUAI, ni bar inayomilikiwa na jeshi la ulinzi, watu walikuwa wajaa kiasi cha kuweza kukosa ata sehemu ya kukaa.

Idadi kubwa ya watu waliokuwepo eneo lile, wakiwa ni vijana wakuanzia umri wa miaka 38 kushuka chini, wakike kwa wakiume, watu wazima walikuwepo lakini siyo wengi sana, ila watoto walikosekana kabisa.

Kati ya watu waliokuwepo eneo lile, wengi wao walikuwa ni watu wakutoka nje ya kisiwa hiki cha unguja, japo walikuwepo wenyeji wachache, akiwepo Siwema, yani dada mkubwa wa Mariam, mtoto wa pili wa mke mkubwa wa wabwana Abeid Ally Makame.

Alikuwa amekaa meza moja na watu wengine watatu, wawili wakiwa ni wanaume na mmoja ni mwanamke, ni kama waligawana, yani wawili kwa wawili, huku meza yao ikiwa imejaa vyupa vya bia, hapakuwa na ata mmoja aliekuwa anakunywa soda kati yao, “tungeenda kulala nyumbani kwangu, sema wambea wengi, siunajuwa huku kwetu uswahili mwingi” alisikika akisema Siwema, akimweleza mwanaume alie kuwa amekaa nae karibu.

Yule mwanaume anaachia tabasamu pana, “ata hivyo siwezi kulala nyumbani kwa mke wa mtu, linaweza kutokea jambo ukashindwa kutoka” anajibu yule mwanaume, ambae sauti yake inaachiria ni mwenye hasiri ya kutoka mkoa wa mbeya, wote wakacheka, “wasi wasi wako tu, mtu yupo Oman huko, kurudi kwake tunapata taarifa miezi mitatu kabla” alisema Siwema kwakujiamini.

Maongezi yanaendelea, huku wanacheka na kufanyiana baadhi ya michezo mepesi ya kimahaba, “hivi Siwema yule mdogo wako Radhia alishapata mume mwingine?” anauliza yule mwanamke mwigine, “ampate wapi, yupo tu nyumbani anashindwa ata kununua chupi yake mwenyewe” alisema Siwema, kwa sauti yenye uzani mkubwa wa zarau, “jamani dada wawatu mzuriiiii, lakinindiyo anabahati mbaya kama nini” alisema yule mwanamke mwingine, akionyesha masikitiko.

“na wewe Amina bwana, kwani kunamtu alimtuma avamia waume za watu, wanaume wote awa unaenda kuolewa mke wapili ili iweje, unazani mwenye mume anajiskiaje” anasema Radhia kwa namna ya kumlahumu Radhia, kwamba alivamia ndoa ya watu kwa kuolewa mke wapili.

Maongezi yale yanadumu kwa dakika kadhaa, kabla wanaume mwingine ajabadiri maongezi, “jamani kesho wapi?” anauliza yule mwanaume ambae ni mpenzi wa Siwema, “kuna sehemu nyingine zaidi ya hii?” anauliza Siwema, kwa maana ya kwamba waje tena hapa hapa, “nyie mtakuja, mie nitakuwa kazini” anasema Amina, kwa sauti iliyojaa manung’uniko, “kazini kivipi, wakati kazini mpaka kesho kutwa?” anauliza Siwema, kwa sauti yenye mashaka.

“kesho kuna afla imeandaliwa ikuru, mimi na wakina dada Sada tumechaguliwa kwenda kama wauguzi wa zarula, hivyo tutakuwepo pale na gari la wagonjwa, yani wameniweza kweli kweli, na afla inaisha saa mbili usiku” alisema Amina, na hapo nikama mwanaume wa Siwema anaingiwa na unyonge, “kumbe, mwenzio sikuwa ata najuwa” alisema Siwema, kwa sauti ya kukata tamaa, “kuna afla ikuru shemeji, rais amewaarika mabarozi na familia zao, pamoja na mawaziri wake, ilasema kesho kutwa kuna taarab bwawani hotel” alisema yule mwanaume wa Amina, ambae alioneakana kuwa na taarifa zote za Amina kuwepo kazini.

“kesho kutwa tutakwenda bwawani nasikia wanaimbaji wote watakuwepo, lakini ainamaana kuwa kesho sitokuwa na nyie, yeye atatukuta akitoka kazini” alieleza yule mwanume wa Amina, ambae siyo mpenzi wake, ila ni mume wake, waliowana miaka minne iliyopita, wakati kijana huyu, alipo amia Zanzibar kikazi, akitoka morogoro, alikokuwa anafanyia kazi.

Yani kwakifupi ni kwamba, awa wanaume wawili ni askari wa jeshi la polisi, wakati mwanaume wa Amina anamiaka zaidi ya minne kisiwani unguja, huyu mwanaume wa Siwema, yeye anamiezi mitano tu, toka aingie kisiwani hapa, ambako ameamishiwa kwa muda, ndio maana akuona sababu ya kuichukuwa familia yake, kuja nayo Zanzibar.

Sijuwi tuiteje hii, ni bahati au bahati mbaya, alikutana na Siwema, kwa msaada wa sehemeji yake Amina, na kujikuta wakiangukia mapenzini, Siwema akisahau kabisa kuwa alikuwa anaisaiti ndoa yake.

Basi aina shida atatukuta, maana mimi kuwa peke yangu bla Amina sehemu kama hii, najisikia hovyo sana” alisema Siwema, ambae mume wake wakati anaondoka nchini kwenda nje kutafuta ugari wakila siku, alimwacha atumii kilevi cha aina yoyote.********

Forodhani mambo yalizidi kuwa moto, watu walikuwa wanaendelea kujiachia kwa mikao na michezo mbali mbali, Mariam na Zuhura wakiwa na wapenzi wao, wakia Mahadhi, walikuwa wajichanganya kwenye makundi ya watu waliokuwa wamejikalia zao kwenye nyasi nzuri za kupandwa, huku wanawatazama watoto wa kaka na yule wa dada yao, waliokuwa wanaendelea kucheza maeneo ya karibu.

Ukweli kuwepo eneo ili kuna raha yake, ila pia kuwa nafedha ya kunua vitu mbali mbali, kulileta raha zaidi, ilo ungelitambua kwa wakina Mariam na mdogo wake Zuhura, ambao tayari walikuwa amesha maliza ice creem zao na juice ya muwa, na sasa walikuwa wanawatazama wenzao ambao walikuwa wanashambulia vitu kama awakuwai kula mwezi mzima.

Hili jambo lilisababisha wakaukiwe na makoo yao, kwaajili ya kumezea mate vitu vya wenzao, na mbaya zaidi pale walipokuwa amekaa walikuwa wamekaa kwenye mchanganyiko wawatu wengi sana.

Tofauti na kule ambako Radhia alikuwa amekaa na Edgar, kulikuwa na watu wachache sana, nao wakatulia kwenye banda moja la vinywaji baridi, na kuendelea kunywea juice na vitafunwa mbali mbali, huku wadogo zake Radhia wakijichanganya kwenye makundi ya watu, upande wawatu wengi, huku kila mmoja akiwa na elfu kumi mkononi mwake, endapo itatokea akaitaji kunua kitu chochote. ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPAHAPA JAMIIFORUMS
 
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA MOJA: Tofauti na kule ambako Radhia alikuwa amekaa na Edgar, kulikuwa na watu wachache sana, nao wakatulia kwenye banda moja la vinywaji baridi, na kuendelea kunywea juice na vitafunwa mbali mbali, huku wadogo zake Radhia wakijichanganya kwenye makundi ya watu, upande wawatu wengi, huku kila mmoja akiwa na elfu kumi mkononi mwake, endapo itatokea akaitaji kunua kitu chochote. ENDELEA….

Maongezi ya Radhia na Edgar yalikuwa mazuri sana, asa kwa upande wa Radhia mwenywe, ambae kwajinsi walivyo kuwa wamekaa na kuongea, japo maongezi yalikuwa ya kawaida lakini kwake, alijisikia vizuri sana, ilimfanya asahau kama ajavaa nguo mpya.

Wao waliongea na kucheka kwa furaha, huku wakiendelea kula na kunywa juice za mabungo, hakika kam ungewaona, usingeitaji ushaidi wa chumbani ili kujuwa ni wapenzi, japo aikuwa hivyo, “hivi Edgar mkeo akikukuta hapahupo na mimi, atakuelewa kweli” aliuliza Radhia, ambae kwa alie mwona masaa machache yaliyopita na siku za nyuma, angeona utofauti mkubwa sana, leo uso wake ulinawili na kuonekana angavu, na mwenye furaha, kitu kilichosababisha kuonekana mzuri na wakuvutia zaidi.

“awezi kutulia, lazima ashikwe na wivu sana, na hivyo ulivyo mzuri, ata mimi mwenyewe nisnge mlahumu” alisema Edgar, huku anacheka, na hapo nikama Radhia akanyongea kidogo, akijiona mwenye bahati mbaya, kuwa karibu na mume wamtu, “unaongea kama mazuri vile, kwani we uoni kuwa ni vibaya” alisema Radhia kwa sauti iliyopoa.

Aikuonyesha kumshangaza Edgar, “kwani kuongea ukweli ni vibaya, we unazani kama ningekuwa nimekuoa alafu nimeakuacha nyumbani, nimekuja huku na mwanamke mwingine ata kama siyo mwanamke wangu, alafu awe nzuri kama wewe, unazani utajisikiaje?” aliuliza Edgar, ambae akuonekana kujari hali ya Radhia katika mabadiliko ya ghafla.

Sijuwi kwanini Radhia alijikuta akishikwa na wivu, wakati akuwa mpenzi wa Edgar, “siyo mbaya, lakini ukuniambia kama una mke, ili nikae nikijuwa nipo na mume wamtu” hapo Edgar akaangua kicheko kifupi cha chini, “kwahiyo upendi kuwa karibu na mume wamtu, nyie sin ma luhusiwa kuolewa wake wawili” alisema Edgar akimalizia kicheko kingine.

Kauri hii nikama ilizidi kuumiza moyo wa Radhia, ambae sasa alitazama pembeni, kuficha macho yake, yaliyoanza kutengeneza machozi, na kuziba mboni za macho yake, Edgar aligundua ilo, nakujihisi vibaya kidogo, kwa kuleta utani usio faa.

Hivyo akatabasamu kidogo, huku anapeleka mkono wake wakushoto, na kwenye bega la kulia la Radhia akilaza kiganja cha mkono wake kwenye bega ilo, ikiwa ni mala ya kwanza Radhia anaguswa na kijana huyu, akajihisi msisimko wa hali ya juu, “dada Radhia, ondoa wasi wasi, mimi bado sijaoa, hivyo kuwa na amani, hakuna wakuja kukufanyia fujo, maana hakuna mwanamke anae jiita mke wangu wala mpenzi wangu kwa sasa” alisema Edgar kwa sauti yake nzito na tulivu.

Radhia ambae anazaidi ya mwaka aja wai kupata dudu kwenye kitumbua chake au kubembelezwa na mwanaume kiasi hiki, alijikuta anageuza uso wake kwa Edgar, huku anaachia tabasamu, na edhar anaonekana kushtuka na kwakuona machozi kwenye macho ya Radhia, anashangaa kidogo, maana aelewi kwanini mwanamke huyu anakuwa hivyo, “kwanini sasa unaleta masihala ya namna hii?” anauliza Radhia kwa sauti ya kujidekeza.

Inamshangaza zaidi Edgar, ukweli siyo kwamba, akumpenda Radhia au udekaji wake, lakini ukweli kwamba, akutegemea kama Radhia angefikia hatua ile kwa utani alio ufanya, “kwanini umekuwa hivyo kwa utani mdogo kama huu” aliuliza Edgar kwa sauti tulivu ya mshangao.

Hapo ndipo Radhia nae alipozinduka na kukumbuka kuwa Edgar akuwa mpenzi wake na wala akumtongoza, ila ni rafiki wa mdogo wake Mukhsin, “ni hadithi ndefu, uwa najisikia vibaya kutokana nay ale yaliyo nikuta miaka ya nyuma” alisema Radhia, huku akilazimika kumsimulia Edgar kisa chake chote, kuanzia kuolewa kwake, mpaka kuachika kwake na manyanyaso anayo yapata, katika maisha yake magumu ya kutengwa anayo ishi sasa hivi.

Hakika ilikuwa ni hadithi ngumu kuisikiliza, kwa mtu mwenye kujuwa maana ya upendo, “pole sana Radhia, lakini bado mdogo sana, unanafasi ya kusoma zaidi na kupata nafasi nzuri katika maisha yako” alisema Edgar kwa sauti ya tulivu ya kuliwaza, “lakini elimu siyo familia” alisema Radhia, akionyesha anaumizwa na kitendo cha kukaa kwenye ndoa kwa miaka miwili, bila kushika ujauzito.

Hapo Edgar nikama anayahisi maumivu ya mwanamke huyu, anatabasamu kidogo, “Radhia unaamini mungu alikuumba mwanamke kwa makusudi, na kazi moja wapo ya mwanake ni kuzaa?” anauliza Edgar kwa sauti tulivu.

Radhia anamtazama Edgar, kabla ya kuitikia kwa kichwa, akikuariana nae kwamba aliumbwa mwanamke, nakazi yake mojawapo ni kuzaa, “basi hipo siku utanyonyesha mtoto wako kwa matiti yako” alisema Edgar kwa sauti tulivu, na kumfanya Radhia atabasamu, “naiwe kweli, maana siyo kwa kusemwa huku” alisema Radhia, na wakaendelea kuongea mengio huku hali ya uchangamfu ikirudi kwa wote wawili.

Wakati huo huo, upande wapili kwa kina Mariam na Zuhura wakiwa na wapenzi wao wanawatazama wenzao waliokuwa wanaendelea kujiachia, huku wanakipata juice na burudani mbali mbali, nikama walikuja kuangalia wenzao na siyo sherehekea, wakati huo watoto wao wakiwa katika michezo na watoto wenzao, mikononi mwao hawakuwa na kitu chochote, siyo wao wala wapenzi wao, wala watoto waliokuwa wanaendelea kucheza.

Kikubwa walicho fanya wakina Zuhura, ni kusindana kujipiga picha na kupakia mtandaoni, huku wakiweka vichwa vizuri vya habari na matabasamu ya bandia, maana awakuwa wanafurahia uwepo wao pale forodhani, sababu hawakuw ana ata shilingi moja.

Mala ghafla Zuhura anaona jambo, “dada Mariam unawaona wale nao wamefikaje huku?” anauliza Zuhura huku anamgusa gusa Mariam, nae anatazama kule ambako anaonyeshwa na mdogo wake, siyo yeye peke yake ata wakina Mahadhi pia, wanatazama upande ule.

Wote kwa pamoja wanawaona Zahara na Mukhsin wakiwa wamesimama kwenye kibaskeri cha juice za mabungo, pamoja na watoto wa dada yao na kaka yao, “jamani mbona maajabu haya” anasema Mariam huku anaangua kicheko cha kustaajabu.

Lakini kabla ajamaliza kucheka, anaona kitu kingne, ni kwamba, wakina Zahara wanawanunulia wakina Khadija, juice na visheti, “he!, wamokota wapi ela awa?” anauliza Zuhura, kwa sauti yenye mshangao kiasi cha watu wapembeni kumsikia. ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPAHAPA KWA JAMIIFORUMS
 
Haya sasa tunaendelea naona inaanza kukolea mdogo mdogo
 
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA KUMI NA TATU
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA MBILI: Lakini kabla ajamaliza kucheka, anaona kitu kingne, ni kwamba, wakina Zahara wanawanunulia wakina Khadija, juice na visheti, “he!, wamokota wapi ela awa?” anauliza Zuhura, kwa sauti yenye mshangao kiasi cha watu wapembeni kumsikia. ENDELEA….

Lakini kwa upande wa Mariam anabakia ametoa macho ya mshangao, anawatazama wakina Mukhsin, ambao walirudishwa chenj zao na kuendelea kucheza kidogo na wakina Khadija, kabla ya kutoweka wakiamia upande mwingine.

Wakina Mukhsin wanajichanganya sehemu nyingine, pasipo kusogea kule walikokuwepo Edgar na dada yao Radhia, labda kama umejisahaulisha, kuwa, Mukhsin ana miaka kumi na saba, hivyo alikuwa amesha juwa na kuelewa hali ya dada yake, pale anapokuwa karibu na Edgar, ambae yeye ni rafiki yake, japo hakuwa anafahamu mambo mengi kuhusu yeye.

Huku nyuma waliwaacha wakina Mariam na Zuhura, wakiwa wameshangaa shangaa pasipo kuamini walicho kiona, “inamaana walijifanya hawana kitu, kumbe baba amewapa ela, na kuwaambia waiondoke kwanza mpaka sisi tuondoke” alilalama Zuhura, akiona kama ameonewa sana, “baba awezi kufanya hivyo, huyo atakuwa ni mama mdogo tu, ndiyo ameficha ela na kuwapa kwa siri, ilisisi tukosea kabisa” alilalamika Mariam.*******

Saa kumi nambili kamili, ndio mwisho wa kuwepo viwanja vya forodhani, mida mbayo eneo ili linakuwa na usumbufu mkubwa wa usafiri, kama ukiitaji usafiri wa haraka basi tumia taxi, kama walivyo fanya wakina Edgar ambao, kabla ya kuchukuwa taxi, walitafuta sehemu nzuri ya kupata chakula cha jioni.

Walikula taratibu, kila mmoja chakula alicho kipenda, kwa kiasi alichoona kinamtosha, huku Zahara akiomba kununuliwa chips za kubeba nyumbani akale na wadogo zake, yani wa wakina Khadija, kitu ambacho unatikiwa msomaji ukijuwe ni kwamba, familia ya mama Radhia, aikuwa na tabia za utenganifu, sema ni vile tu, awakuwa na uwezo wa kifedha.

Muda wote wa chakula waliongea kwa furaha na kucheka kwa pamoja, “kesho naimani itakuwa nzuri zaidi, japo hii yaleo nimeipenda sana, sijai kushiriki sherehe katika mazingira kama aya changamfu namna hii” alisema Edgar, ambae alimaanisha akuwa kujuika kwenye maeneo ya wazi yenye mchanganyiko wawa tu kama aya ya forodhani.

“hivi hiyo kesho unatupeka wapi, mi mwenzio nguo zenyewe ndio hizi hizi, na nikizifua zitakauka saa ngapi?” aliuliza Radhia, “wala usijari kesho tutavaa tofauti kidogo, cha msingi umweleze mama kuwa tutatoka kidogo” alisema Edgar, kwa sauti yake nzito lakini ikiwa na uchangamfu kiasi, “tutavaa tofauti kivipi na mimi hapa ndio nimevunja kabati?” anauliza Radhia, na Zahara akadakia, “mwenzio nzuri anayo hii tu…” akuweza kumaliza akakumbuka kosa alilolifanya mchana.

Edgar akacheka kidogo, “ilo niachieni mimi, kila mmoja watu atapata nguo yake, kisha tunaenda kuburudika pamoja, cha msingi kunamtu ata kupigia simu wakati analeta nguo” alisema Edgar kama vile anatania.

Saa mbili na rodo ndio mida ambayo waliingia kwenye taxi, na kuondoka zao wakielekea upande wa kilimani, ata walipofika gymkana, waliwacha Edgar nae akaanza kutembea taratibu kuelekea upande wa kilimani, huku wao wakiingia upande wa jang’ombe, wakipanga kesho kwenda mwenye mwaliko wakiwa pamoja, japo wakina Radhia walichukulia kaida, tena akupanga ata kumweleza mama yake.*******

Upande wa Mariam na mdogo wake na watoto wao, ilisha pita nusu saa tangu wafike nyumbani, huku Mariam ameshika viatu mkononi, akiona vina mnyima mwendo, nae alitaka kuwai nyumbani, akaulie wakina Mukhsin walipata wapi fedha za kununulia vitu kule forodhani.

Mariam na Zuhura wanafika nyumbani, anawakuta mama wote wawili wakiwa pale kibarazani, pamoja na baba yao, “mama, da Radhia yupo wapi?” anauliza Mariam, huku uso wake umejaa kwa hasira, “sie wenyewe atuja mkuta yeye na wakina Mukhsin, tukajuwa mme toka wote, anajibu mama Mariam, huku wote wanamtazama Mariam kwa macho ya tahadhari.

Hapo Mariam anahisi kuwa pengine Radhia alikuwa pamoja na wakina Zahara, “kwahiyo mliwapa ela mkasubiri sisi tumeondoka ndio na wao wakaondoka” anausema Mariam kwa sauti ya kulalamika, hapo wote wakatazama kwa mshangao, kasoro mzee Abeid, mzee mwenye busara zake, ambae anaelimu ya juu ya ualimu wa saikorojia na sayansi ya viumbe hai.

“nani kasema tumewapatia fedha wakia Radhia?” anauliza mama Mariam, ka sauti yenye mshangao huku anamtazama Mariam mwenyewe, ambae pia anamtazama mama Radhia kama vile anasema mwulize huyo.

Niaka mama Radhia anafahamu kuwa lile swali inabidi yeye ndiyo alijibu, “ata mimi nashangaa wamewezaje kutoka wote wakati ata fedha wakuwa nayo” anasema mama Radhia ambae ndie mama wa Mukhsin na Zahara, “uongo, tumewaona wana nunua vitu forodhani, tena wakarudishiwa chenji” alisema kwa kulalamika Mariam, na wakati huo huo wakasikia ngurumo nyepesi ya gari, ikija upande wa nyumba yao sambambana mwanga wataa afifu uliokuwa unamulika kwenyekuta za kibaradha cha nyumba yao.

Wote wanageuka kulitazama gari ilo, ambalo lilikuwa ni gari dogo lenye kibandiko cha taxi, lililokuja na kusimama usawa wanyumba yao, nao wakaendelea kulitazama wakiwa na hamu ya kumwona anae shuka.

Kama ambavyo awakutegemea, wakaona milango mitatu ya gari ikifunguliwa na wakashuka Radhia na wadogo zake, huku wakionekana wenye furaha kupita kiasi, na kufunga milango ya gari kisha gari likaondoka.

Wote wanawatazama watatu hawa, ambao walishuka na kusogelea kibaradha, huku Zahara akiwa ameshika kifuko chake chenye kunukia chipis, “asalam aleykum” anasalimia Radhia, ambae siyo tu kuchangamka kwa uso wake tofauti na siku nyingine, ila pia ata ungavu wa sura yake ulionekana tofauti na siku nyingine, au masaa machache yaliyopita.

“aleykum salaam” anaitikia baba na mama Radhia pekee, wengine wanamtazama Radhia kama vile amemwaga mboga ya mwisho, “mie nilizania utoki, ilikuwaje ukatoka ghafla namna hii?” anauliza mama Radhia kwa sauti yenye mashaka, huku anamtazama mwanae toka chini mpaka juu, kwa ukaguzi wa nguo alizo vaa, Radhia aliligundua ilo, lakini akuitaji kuliwaza sana, maadamu Edgar akuona kasoro yoyote, yeye hakuwa na shaka lolote.

“sikuwa na mpango wakutoka, ila niliwapeleka wakina Mukhsin kwa rafiki yao aliwaita” alisema Radhia, na hapo nikama mzee Abeid alihisi kitu, maana aliinuka toka kwenye kiti na kuingia ndani, akipisha maongezi ya wakina mama, “yeye ndie alie wapa hiyo ela ya kununulia vitu?” anauliza mama Radhia, na kumfanya Radhia ashangae kidogo, wakati huo Mukhsin akaingia ndani, ni wazi aliona maongezi yanayofwata aya kumhusu.

Ilimshangaza sana Radhia, ambae akujuwa habari zile zimefikaje nyumbani, lakini akuwa na muda wakuuliza, zaidi ya kujibu swali alilo uliza, jibu ambalo akuitaji kulificha wala kuongopa, “ndiyo walipewa elfu kumi kumi na rafiki yao” alijibu Radhia, akimweleza mama yake ambae alikuwa anafahamu kuhusu rafiki huyo wa Mukhsin.

Mpaka hapo hapa kuwa na maswali zaidi, ata Mariam na Zuhura walipoa kidogo, japo iliwauma sana kitendo cha Radhia kwenda forodhani wakizania kuwa ata bakia nyumbani kwa kukosa fedha wala uwezo wa kwenda kutembea, “sasa ndio uende hivyo na miguo ya zamani?” alisema Zuhura kwa namana ya kusimanga, wote wakashangaa.

Ni wazi mama Radhia aimpendezi kauri ya Zuhura, “ebu mheshimuni dada yenu, kwani lazima kuvaa nguo mpya” alisema mama Radhia, kwa sauti ye kuchukia, “mwache seme bwana, ata kama ni dada yao, lakini anatia aibu, ya nini kulazimisha kutembea na miguo ya zamani” anasema mama Mariam, na Mariam anadakia, “mtu mwenyewe mjane lakini bado anazurula kutafuita nini” anasema Mariam huku anaingia ndani, akifwatiwa na Zuhura. ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPAHAPA JAMIIFORUMS
 
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA KUMI NA NNE
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA TATU: Ni wazi mama Radhia aimpendezi kauri ya Zuhura, “ebu mheshimuni dada yenu, kwani lazima kuvaa nguo mpya” alisema mama Radhia, kwa sauti ye kuchukia, “mwache seme bwana, ata kama ni dada yao, lakini anatia aibu, ya nini kulazimisha kutembea na miguo ya zamani” anasema mama Mariam, na Mariam anadakia, “mtu mwenyewe mjane lakini bado anazurula kutafuita nini” anasema Mariam huku anaingia ndani, akifwatiwa na Zuhura. ENDELEA….

Radhia anaingiwa na unyonge, anajiinamia chini, anakosa la kusema, lakini anakumbuka kuwa kuna mwanaume anamchukulia kawaida licha ya kuwa ameachika na sababu ni kukosa kushika ujauzito, “mwanangu wala usijari, kuachika siyo kilema, ata mimi nilichelewa kupata mtoto wa kwanza” anasema mama Radhia, na Radhia anajifuta machozi, huku anashindwa kutoa taarifa ya mwaliko wakesho, maana atasimangwa kwa kukosa nguo mpya.

Radhia akiwa katika hali ya unyonge, akaingia ndani, na kwenda kuoga, kisha akajilaza kitandani, akaanza kuwa za mambo mengi sana, aliwaza juu ya maisha yake ya zamani akiwa kwenye ndoa, maisha ambayo mwanzo yalikuwa mazuri, akiongea na kucheka na mume wake, pamoja na mke mwenzie, aliweza kuwa hudumia wadogo zake, kwa vitu vidogo vidogo.

Pia alikumbuka mambo waliyokuwa wanafanya na mume wake chumbani, japo katika kumbu kumu zake, akumbuki siku ambayo aliwai kumaliza kiu yake ya dudu, kwenye kitumbua chake, maana mala zote, pale alipokuwa anaanza kunogewa na mchezo, na kuanza kuipata raha ya dudu, ndipo mume wake alipo maliza mchezo.

Na mbaya zaidi, mume wake wazamani, alipokuwa anamaliza mchezo, akuwa na uwezo wa kurudia tena, na hapo ingepita ata week moja na zaidi, pengine ni kutokana na uchovu wa kazi za mchana kutwa.

Radhia aliendelea kuwaza na kuvuta kumbu kumbu ya matukio ya toka siku ya kwanza alipo kutana na Edgar, ambae ni rafiki wa mdogo wake Mukhsin, kimtazamo umri wa kijana huyo, uliendana na umri wake yeye Radhia.

Radhia alivuta picha ya kijana huyu, ambae licha ya kuwa mkarim, na mjuzi wa kutoa maneno ya kuliwaza, lakini kijana huyu akuonyesha dalili ya kumwitaji kipenzi, “anaumbo zuri” anawaza Radhia, ikiwa ni kwa mala ya kwanza akijihisi kutamani mwanaume kutokana na umbo lake, ambae anafurahi kwa ujio wa kijana huyu katika maisha yao.

Maana ukichilia kuwasadia wadogo zake kwasasa, lakini pia, amemsikia kijana huyu akimweleza Mukhsin kuwa, akijitaidi katika masomo na mchezo wa mpira wakikapu, atampelaka nchini #Mbogo_Land, nchi maalufu kwa mpira huo wa kikapu, ambao wachezaji wake wamenufaika kwa kiasi kikubwa sana katika maisha yao.

Naaaaam! kwakati Radhia anaendelea kuwaza ili na lile, mala akasikia simu yake inaanza kuita, akaichukuwa haraka na kuitazama, akaona mpigaji ni Edgar, hapo Radhia akajikuta anatabasamu kwa raha aliyo isikia moyoni mwake.

Nikukumbushe kitu, toka Radhia ameachika kwa mume wake Idd, hapakuwa na mtu wakumpigia simu mala kwamala, labda mama yake ambae ni mala chache sana kuwa nae mbali.

Radhia anaiachia simu, nakuitazama ikiendelea kuita kwa sekunde kadhaa, usoni amejawa na tabasamu pana, lenye uangavui wa furaha, kisha akaipokea, “hallow!, asalam aleykum” alisalimia Radhia kwa sauti nyororo na tulivu, “aleykum salaam dada Radhia, vipi mlifika salama?” inasikika sauti nzito na tulivu toka upande wapili wa simu, Radhia anahisi msisimko wa mwili, unao anzia kwenye sehemu nyingine za mwili.

“ndiyo tumefika salama, nilishindwa kukujulisha sina salio” alisema Radhia kwa sauti tulivu, kama ile ya mwanzo, “ok!, nimefurahi kusikia mme fika salama, pia asante sana kwa matembezi ya mchana, nimefurahi sana, siku yangu ilikuwa nzuri sana” alisema Edgar.

Hapo Radhia akajikuta anaachia tabsamu lenye mchanganyiko wa furaha na mshangao, “mie ndio napaswa kusema asante, yani umenitendea jambo zuri sana, maana wadogo zangu wamefurahi sana” alisema Radhia, akiongea ksauti yenye hisia toka moyoni.

Wawili awa waliongea mawili matatu, huku wakicheka kwa furaha, awakutumia muda mrefu sana, wakaagana huku Edgar akisisitiza kuwa, kesho wataenda kwenye mwaliko.

Hakika Radhia alijihisi furaha kubwa sana, ata wadogo zake walipoingia kulala, walimkuta akiwa mwenye furaha kubwa sana, na dakika kumi baadae, uliingia ujumbe kwenye simu yake, ukimweleza kuwa ametumiwa salio la vocha ya elfu tano, ikiwa ni muda wamaongezi, alishangaa sana, maana simu yake toka anunue ata wakati akiwa kwa mume wake, akuwai kuweka vocha nyingi kiasi hicho.

Haraka sana akajiunga kifurushi, na kutuma ujumbe kwa Edgar, “asante sana nipata vocha” hapo zikapita dakika tatu, ujumbe ukaingia kwenye simu yake, “ok! karibu” ndivyo ujumbe ulivyosema.

Hapo Radhia akatoa macho kwa mshangao, “mh!, karibu ya nini tena” anajiuliza Radhia kwa sauti ya chini, ajuwi kama wadogo zake wanamsikia, nae akiwa amekosa jibu, anaamua kujibu, “nimekaribia” kisha anaituma kwenda kwa Edgar, kisha anasubiri ujumbe mwingine, lakini mpaka anaanza kusinzia akuona ujumbe wowote, mpaka alipochukuliwa na usingizi.*******

Upande wapili chumbani kwa kina Mariam na Zuhura, wao bado walikuwa macho, tayari wamesha kula na sasa wamejilaza kitandani, wanapekuwa simu zao na kusoma maoni ya watu, waliyo yatoa kwenye picha zao walizo post kule forodhani, “hivi huyo rafiki yake Mu, unamfahamu?” anauliza Zuhura, huku anaacha kupekuwa simu na kumtazama dada yake.

Hapo nikama Mariam, anakumbuka kitu flani, “nimjulie wapi, usikute ni hawara yake, anasingizia rafiki yake Mu” anasema Mariam, na hapo Zuhura anacheka kwa dharau, “hawara ampate yeye mjane, mtu mwenyewe mlinda kuku” alisema sema Zuhura akimaanisha dada yao Radhia ni mtu wa kukaa nyumbani, hapo Mariam nae akacheka.

“lakini tutajuwa tu ujanja wa mama yao, yani amewapa ela, alafu wanasingizia wamepewa na rafiki yao, rafiki gani huyo mwenye ela yote hiyo” alisema Mariam, huku wote wakionekana kuumia sana, kwa kitendo cha kuwaona wakina Zahara na Mukhsin, wakiwa forodhani na fedha nyingi, huku wao wanakosa ata ela ya maji.

“tuone na kesho kama watatoka tena, kama sisi” alisema Zuhura, na Mariam akadakia, “alafu kesho watoto tunawaacha, siunajuwa tuna jambo letu” alisema Mariam, “ila da Mamu tusiende kuchelewa sana, ili tuwai forodhani tukale urojo” alisema Zuhura, “atuwezi kuchelewa, mwenzio Mahamud yeye akiweka tu, wala achelewi” alisema Marim, na Zuhura akasema yak wake, “ata Mahadhi, tena anapenda ya kuinama, anamwaga haraka” alisema Zuhura.********

Lakini wakati huo huo, huko sebuleni kulikuwa na kikao cha dharula, kikao ambacho mwenyekiti alikuwa ni mzee Abeid Makame, “kwakweli lazima mtambue Radhia ni binti kubwa sana, na kilicho mkuta lazima kimuumize kama ambavyo mwanamke yoyote anavyo weza kuumizwa” alisema mzee Abeid kwa sauti tulivu yenye umakini mkubwa. ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPAHAPA JamiiForums
 
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA KUMI NA TANO
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA NNE: Lakini wakati huo huo, huko sebuleni kulikuwa na kikao cha dharula, kikao ambacho mwenyekiti alikuwa ni mzee Abeid Makame, “kwakweli lazima mtambue Radhia ni binti kubwa sana, na kilicho mkuta lazima kimuumize kama ambavyo mwanamke yoyote anavyo weza kuumizwa” alisema mzee Abeid kwa sauti tulivu yenye umakini mkubwa. ENDELEA….

Mama Radhia na mama Mariam wanamsikiliza kwa umakini mume wao, “amuwezi kumsimanga kwa kukuachika, tena mwaka sasa umepita, na bola angeachika kwa uzembe wake au uzinzi, lakini ameachwa kwa tatizo la kuto kushika ujauzito” anasema mzee Abeid Ally Makame, kwa sauti yenye machungu makubwa.

Wake zake wote wawawili wanamsikiliza, huku wameinamisha vichwa chini, “mama Mariam, ongea na wakina Mariam, waache kumsimanga Radhia, kwa nza yule ni dada yao, pili yeye ndie mwenye haki ya kwenda matembezi muda wote kuliko wao, maana tayari alisha wai kuingia kwenye maisha ya ndoa, na kwa namna nyingine, inabidi asaidiwe ili aweze kujitegemea, na kupata maitajio yake mwenyewe” alisema mzee Abeid huku anamtazama mama Mariam, ambae aliitikia kwa kichwa, kukubariana na mume wake.

Mzee Abeid anamgeukia mke mdogo, ambae ni mama Radhia, “na wewe jitaidi kuwa karibu na Radhia, uwe unampa moyo na kumjenga kitabia, ili asiendelee kunyongea, pia msisitize awe anatembelea marafiki, pengine inaweza kumsaidia kuondoa mawazo” alisema mzee Abeid, na mke wake akaitikia kwa kichwa kukubariana nae.

Hii ilimfanya mama Radhia ajawe na furaha moyoni mwake, akiwa anaamini kuwa, alicho kisema mume wake kinaweza kusaidia kupunguza masimango na dharau kwa Radhia, nae ataishi kwa amani na kulejewa na furaha, na kama ujuwavyo, amani ya binti yake ni amani yake pia, na mni amani ya watoto wake wadogo pia.*******

Siku ya pili ilianza vizuri kwa wanafamilia wote, kasoro Radhia na mama yake mkubwa, yani mke wa mkubwa wa mzee Abeid, ndio ambao waliamka wakiwa wamenyongea.

Ni kwamba, wakati mama Radhia anafurahi na kuliwazika kwa maagizo aliyo yatoa mume wake, juu ya Radhia, huku mama Mariam anawaza jinsi watoto wake watakapo ambiwa, kuacha kumsimanga na kumdharau Radhia, kwa vyovyote wataona kuwa Radhia anapendelewa, hii tabia waliijenga toka zamani, kipindi ambacho Radhia anasifiwa kwa tabia njema, uzuri wa sura na umbo, japo bado sifa hizo alikuwa nazo, lakini alialibiwa na tarataka tatu ambazo alipewa na mume wake.

Wakati Zahara na Mukhsin wakifurahia mtoko wa siku hii yaleo, pamoja na ahadi ya nguo mpya waliyo aidiwa na Edgar, ambae akuwai kuacha ktimiza ahadi zake kwao, Mariam na Zuhura nao walikuwa wanafurahia mtoko wao wa mchana waleo, siyo kwamba walifurahia dudu au kile ambacho wataenda kufanyiwa na wapenzi wao.

Hapana, wao kunyanduana, awakukupa sana kipa umbele, ukichukulia ni kwamba, wakina mahadhi siyo wapenzi wao wakwanza, hii nikama hawamu ya tatu ya ya nne ya wanaume walio wai kutembea nao, na awakuwai kunufaika kwa lolote, zaidi ya kusikia au kusoma kwenye mitandao ya kijamii, kwamba kuna wakati mwanamke anafikishwa kileleni na kumaliza kiu ya dudu.

Yani kitu ambacho wao binafsi uwa wanakipata kwa kujihudumia wao wenywe, wakisaidiwa na video za ngono, walicho furahi kwenye mtoko wa leo ni ile kwenda matembezi fordhani kula urojo, na kibwa zaidi waonekane wanauwezo wa kutoka kwa siku zote nne za eid.

Radhia yeye alinyongea kwa kuona kuwa, anashindwa kutoka matembezi, kwasababu ya kwamba akuwa na nguo mpya, ya kuvaa, lakini ata hivyo akupanga kuacha kutoka, tena alipnga asiage kwa mtu ata mmoja, zaidi angetoka na wadogo zake kimya kimya, kama ilivyokuwa jana.

Furaha ya Mariam na Zuhura inageuka kelo kwa Radhia, maana kila walipokuwa karibu na Radhia, wangejiongelesha makusudi, “da, mamu leo tunatoka saa ngapi?” Zuhura angemwuliza Mariam huku anamkata Radhia jicho la pembeni, “tukisha kula mchana tu, tuonaondoka zetu” anasema Mariam kwa sauti yenye manjonjo ya ujivuni.

Hapo ni kama aitoshi, wangeanza kuongelea mambo ya jana, “hivi uliona jinsi watu walivyokuwa wanatushangaa tulivyo pendeza” yani waliongea kila walichoona kinafaa kumwumiza Radhia, “weeee!, nilimwona mwanaume mmoja amemsahau adi mke wake anatushangaa sisi” anajibu Mariam, kwa mbwembwe, huku wanamtazama dada yao mwa macho ya wizi, kuona kama anaumia kiasi gani.

Lakini wakashangaa kumwona yupo kawaida kabisa, tena wakati wanendelea kujiongelesha, wakasikia ujumbe unaingia kwenye simu yake, nae akausoma ujumbe “mwambie Mukhsin asogee barabarani, ninamzigowenu” ulikuwa ni ujumbe toka kwa Edgar.

Hapo Radhia akajikuta akitabasamu mwenyewe, “Mukhsin, we Mukhsin” aliita Radhia, huku atatazama mlango wa nyumba kubwa, “naaaaam” aliitika Mukhsin ambae alikuwa ndani, “kuna messeji ya rafiki yako hapa, njoo usome” alisema Radhia, ambae uso wake ulikuwa umetakata kwa tabasamu la furaha.

Mwonekano wa Radhia unaonekana kuwashangaza Mariam na Zuhura, ambao wanaachana na maongezi yao wanamtazama Radhia, ambae ameshika simu anapapatia Mukhsin, aliekuja nje mbio mbio, anausoma ujumbe, kimya kimya, kisha anamgeukia dada yake, huku usowake umechanua kwa tabasamu, “kwahiyo niende stendi nikapokee” aliuliza Mukhsin kwa sauti iliyo changamka.

“ndiyo, chukuwa hiyo simu uende nae huku unampigia” alisema Radhia, ikiwa ni habari mpya kwa kina Mariam, maana siku zote wamezowea kuona au kusikia Radhia akisema kuwa hakuwa na salio kwenye simu.

Mukhsin anavaa sendo haraka, kisha anaanza kutembea kuelekea upande wa barabarani, huku anabofya simu ya dada yake, na kuiweka sikioni, ikionyesha kuna mtu anampigia, na mtu mwenyewe siyo mwingine, ila ni rafiki yake Edgar, wakati huo huo wakina Mariam na Zuhura, walikuwa wanamsindikiza kwamacho, huku mioyoni mwao, wakijaza chuki na hasira, japo awakujuwa huyo rafiki yake Mukhsin, ameleta kitu gani.

Ata Mukhsin alipotokweka usawa wamacho yao, wote wawili wakamtazama Radhia, ambae akuwa na habari nao, zaidi alionekana akiwa amezama kwenye mawazo.

Nikweli Radhia alikuwa anawaza, alikuwa anawaza kuhusu vitu ambavyo wameletewa wadogo zake, kama wameletewa nguo walizo aidiwa, au kuna vitu vingine wameletewa wadogo zake, lakini yote kwa yote, furaha yake ikuwa pale pale, na furaha yake kubwa, nikuona Edgar anawajari wadogo zake.

Wakati wakina Mariam wanaendelea kumtazama Radhia kwa macho makali ya mshangao, mala wakasikia mama yao anawaita kutokea ndani, “Mariam njoo na Zuhura” alisema mama yao, nawao wakaingia ndani, wakipishana na mama Radhia aliekuwa anatoka nje, akiwa ameongozana na Zahara.

Tuanze na huko ndani, ambako mama Zuhura aliwaita wakina Mariam, ambao aliingia nao chumbani kwake, “nimewaita wote wawili, kuna kitu nataka tuongee” alisema mama Mariam kwa sauti ya chini, kiasi kwamba, ata kama kunamtu alikuwa amekaa nje ya chumba iki yani mlangoni asinge sikia. ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPAHAPA JamiiForums
 
Ni ipi hatima ya radhiya na edgar? ni nini mama yao akina mariam anataka kuwaambia wanae? haya tuendelee sasa
 
Back
Top Bottom