ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA SABINI
MTUNZI:
edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI TISA: “baba aliagiza huyo rafiki yake Mu, aje wamfahamu” anajibu Mariam, lakini bado bado Zuhura ahalizia na jibu lile, “sijuwi kwanini wanamng’ang’ania, kwani awajuwi kama anatembea na dada?” anauliza Zuhura, akionyesha kutokupendezwa na jambo flani, kama siyo ujio wa mgeni wakesho, basi ni urafiki wa Radhia na huyo rafiki yake Mu. ......... ENDELEA….
Naaaaam!, mabinti wawili wa mzee Makame, wakiwa wanakaribia stendi ya kwamchina mwanzo, mala wanam, mwona dada yao akiwa akiwa ameongozana na msukuma mkokoteni, uliobeba mizigo mbali mbali, vikiwepo masufuria na mabegi ya nguo, dada yuleee” anasema Mariam, huku wote wakimtazama Siwema ambae alikuwa mita chache mbele yao.
“asalam aleykum” wanasalimiana na dada yao ambae anaonekana kunyongea kwa kiasi kikubwa sana, tofauti na wanavyo mfahamu, “aleykum salaam” anaitikia Siwema, na wakina Mariam wanampokea mkoba wake, “vipi baba, mme mwacha nyumbani?” anauliza Siwema huku wanatembea kuelekea nyumbani, wakiwa nyuma ya msukuma mkokoteni, aliekuwa anaongoza safari.
“ndiyo amekaa na wakina mama kibarazani, wana malizia kucmbua mchele wa kesho” anajibu Mariam, inamshtua kidogo, Siwema, “kesho kunanini?” anauliza Siwema kwa mshangao na mshtuko, “anakuja yule rafiki yake Mu, kumsalimia baba” alijibu Mariam, “mh!, rafiki yake au hawara wa Radhia, siwaseme ukweli tu, wameamua kumwachia Radhia awe na wanaume” alisema Siwema akionekana kuchukizwa na jambo ilo.
Kinafwata kimya kifupi, huku wanaendelea kutembea, kila mmoja nawaza la kwake, Siwema anawaza kuhusu Radhia, nikama anaishi maisha ya furaha kuliko kipindi kingine chochote, na mbaya zaidi ni kwamba, Radhia anaishi kwa furaha kipindi ambacho yeye anaikosa amani moyoni mwake.
Pia Siwema anawaza namna atakavyo karibishwa na baba yake, ambae anamfahamu kuwa apendi ujinga mdogo mdogo, hivyo angepokelewa na maneno mazito ambayo yangemkosesha hamu ya kula kwa week nzima, japo yaliyo mkuta yanatosha kumnyima hamu ya kula, yani kuachika kwa taraka tatu na kufukuzwa kazi kwa wakati mmoja.*******
Naaaam!, Idd anamtazama Edgar ambae anakimbia taratibu kupandisha kilima kueleka maeneo ya ngazi mia, nae anamfwata nyuma akiwa na baskeri yake.
Ata wanapofika maeneo ya kimani anakuwa amesha mfikia, “samahani kaka mambo vipi” anasalimia Idd, ambae anaendesha baskeri pembeni ya Edgar aliekuwa anakimbia taratibu, “poa tu, niaje” anaitikia Edgar huku anaendelea kukimbia taratibu, “poa kama siyo poa, ninaomba tuongee kidogo” alisema Idd.
Na hapo Edgar akasimama kabisa, ikiwa ni mbali wa mita kama hamsini toka iliponyumba anayoishi, “yah!, niambie, kunaishu?” anauliza Edgar huku anamtazama Idd kwa macho ya tahadhari, “bro!, nimeona nikufwate moja kwa moja, sababu wewe ni mwanaume mwenzangu, sijaona kama itakuwa vyema, kama nikucha bila kukuambia” alisema Idd kwa sauti tulivu iliyo jaa busara na uhekima.
Ilimshtua kidogo Edgar ambae alimua kujukaza kidogo, “ok!, nakusikiliza bro” alisema Edgar, huku moyoni mwake akijuliza kitu gani huyu jamaa anataka kumweleza, “sikiliza kaka, nimekuona hupo karibu na mwanamke flani hivi, anaitwa Radhia, ukweli nakuwambia akufai ata kidogo, ni vyema ukaachana nae kwa kulinda heshima yako.
Alisema Idd, ambae alipania kuongea vitu ambavyo vitamfanya Edgar amwache Radhia mala moja, “kivipi yani, unaweza kunifafanulia?” aliuliza Edgar, huku anamtazama Idd usoni, Idd anatazama pembeni, akikwepa macho ya Edgar, “kwanza kabisa ameachwa na mume wake, sababu ya tabia mbovu, yani nimalaya wa kutupwa, pili anatabia zote za ajabu, asa upanda kutoa mimba” alieleza Idd.
Edgar anatabasamu kidogo, tabasamu ambalo Idd anaona kama linadalili ya kijana huyu, kuto kuamini alichoelezwa, “kuna tabia nyingine umeisahau?” anauliza Edgar, huku anamtazama Idd, “isitoshe yule ni mke wa mtu bado maana mume wake alimpatia taraka mbili, hivyo inaweza kukuletea kashfa ya kutembea na mke wa mtu” alieleza Idd.
Hapo Idd anamshuhudia Edgar anaachia kicheko kikubwa, “kuna kitu ujuwi, ni kwamba, Radhia ameachika na mume wake, kwa taraka tatu, na kosa siyo umalaya, ila ni kuto kushika mimba, kitu ambacho mume wake ajakifanyia uchunguzi, ilikujuwa mwenye tatizo ni nani, na mume wake aliacha kufanya hivyo sababu tayari anawatoto wawili, kwa mke wake mkubwa” aisema Edgar, kisha akaanza kukimbia kuelekea nyumbani kwake,
Ilimvuruga Idd, ambae alijikuta anajawa na hasira, alitamani kamamkimbilie Edgar na kumshushia kipigo, lakini miili yao nivitu viliwi tofauti, yani endapo angekutana na ngumi moja ya kijana huyu, hakika angeokotwa nawatu wanao jihimu asubuhi, “unazania utamchumbia Radhia kilahisi lahisi, kwa taarifa yako unaingia mkenge” alinongo’ona Idd, ambae anageuza na baiskeli yake, na kurudi michenzani, huku kichwani mwake akijaribu kutafakari baadhi ya maneno ya Edgar.
“kitu ambacho mume wake ajakifanyia uchunguzi, ilikujuwa mwenye tatizo ni nani, na mume wake aliacha kufanya hivyo, sababu tayari anawatoto wawili, kwa mke wake mkubwa” baadhi ya maneno ambayo, yalijirudia kichwani mwa Idd, “inamaana Radhia amekaa na kumsimulia kila kitu huyo mpuuzi wake” anajisemea Idd, ambae anaendesha baiskeli kwa peed akishuka mtelemko, kuitafuta Maisala.********
Japo awakuwa uhuru sana, kutokana na kumfikilia dereva na muda wake, lakini Radhia na wadogo zake wote, walionekana kuwa katika furaha kubwa, moda wote wakati njiani ata wakiwa wananunua chips na urojo mishikaki, na vitafunwa vingine, kisha wakarudi kwenye gari na safari ya nyumbani ikaanza.
Njiani Radhia alikuwa amekaa seat ya nyuma na watoto, huku mkukhsin akiwa amekaa seat ya mbele akiwa ameupakata mpira wake mpya, Radhia alikuwa anawaza na kuvuta picha, ya namna alivyokuwa anatazamana na Edgar, huku wakishindwa kuongea chochote, anajikuta anaishia kutabasamu.*********
Siwema na wadogo zake wanafika nyumbani, wanamkuta mzee Makame anaongea na wake zake huku wakicheka na kufurahi kwa pamoja, furaha ambayo Siwema anaitafsili kuwa ni furaha ya ugeni wakesho, ugeni ambao yeye Siwema anaufahamu kabisa kuwa, licha ya kuwa ni ugeni wa rafiki yake Mukhsin, lakini yeye anafahamu kuwa kijana huyo ni mpenzi wa Radhia, na amewaona kwa macho yake, wakitoka usiku, na Radhia akurudi nyumbani usiku ule.
Siwema anawaona mama zake wakiwa na baba yake wanatazama mkokoteni wenye masufuria na begi, nae anaenda kukaa kwenye mkeka karibu na mama yake, huku wakina Mariam wanasaidia kushusha vitu, na kuingiza ndani, “asalam aleykum” anasalimia Siwema, ambae awaona watoto, ata binti yake Khadija, ambae amemzaa na mume wake alie mtariki leo mapema.
“aleykum salama, karibu nyumbani” anasema mzee Makame, ambae aonekani kushangaa wala kukasirika, ata msukuma mkokoteni anapo maliza kushusha mizigo na kuondoka zake akiwa ameshalipwa, mzee Makame akamtazama tena binti yake, “pole kwa yote, karibu nyumbani” anasema tena mzee Makame.
Ukweli nikama ile pole ya baba yake ilianzisha machungu moyoni kwa Siwema, ambae sasa machozi yanaanza kudondoka taratibu machoni mwake, “aina aja ya kulia Siwema, kikubwa ni kumwomba mungu akujalie upate mwingine, na ishi nae kwa elimu uliyoipata kutokana na ili lililotokea” alisema mzee Makame.
Na wakati huo huo wakaona mwanga afifu wa gari, una wamulika toka upande wa barabarani, sambaba na ngurumo ya chini ya gari ilo, wote wanalitazama gari dogo jeusi, linalokuja na kusimama karibuna kibara chao, kisha milango inafunguliwa na wakina Radhia wanashuka, huku watoto wote wakiwa na vijifuko vyao mikononi, yani kuanzia Zahara adi Khadija.
Hii ilimfanya Siwema ashangae kimoyo moyo, akijaribu kujizuwia asionekana anavyo shangaa, maana akutarajia kuliona gari lile likimleta Radhia nyumbani, pili ni kumwona binti yake akitoka matembezi na Radhia, kitu ambacho Siwema akutaka kukiona kinafanyika kwa wadogo zake kwenda kutembea na wadogo zake Radhia. ......... ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPA HAPA
jamii forums