SIMULIZI: Asali haitiwi kidole

SIMULIZI: Asali haitiwi kidole

ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA TISINI
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA TISA: Ndani kuna watu kadhaa, ukiachilia wafanya kazi wawili, ambao walikuwa wanahudumia, huku chai na vitafunwa mbali mbali vikiwa mezani, pia kulikuwa na mheshimiwa rais mwenyewe, pamoja na waziri wa elimu, wote walikuwa wanamtazama kwa tabasamu, kama vile wanamfahamu, nyuma yao wakiwepo walinzi na wanahabari wawili wa ikuru, mmoja wao akiwa ameshika camera. ......... ENDELEA….


“Karibu bwana mwalimu Makame, umefanya chai ipoe kwa kukusubiri” alisema mheshimiwa rais kwa utani huku wanasimama toka kwenye makochi yao, na wote wakacheka kidogo, wote wanacheka, “hakika siku na habari ya wito huu” anasema mzee Makame kabla awajasalimiana huku wanshikana mikono, “Radhia akuweza kukudokeza atakidogo, maana tuliongea ili mbele yake” alisema mheshimiwa rais, kabla ajamluhusu mzee Makame wakae na kuanza kupata chai, huku maongezi yakiendelea


Waliongea mawili matatu, mpaka mheshimiwa rais alivyo anza kueleza nia na zumuni la wito wa mzee Makame, “mwalimu Makame, tumepitia wasifu wako, na tume ona kuwa una nafasi yako, katika kuisaidia serikali kuinua uchumi kupitia sekta ya kilimo” alieleza rais, akiendelea kueleza kuwa, “kwamaana hii utanapata uamisho toka wizara ya elimu, sasa utafanyakazi chini ya ofisi ya rais, kwasababu hatuna wizara ya kilimo” alisema mhesimiwa rais.


Hakika taarifa ile ilikuwa nzuri, na yakufurahisha moyoni kwa mzee Makame, “utaonyeshwa ofisi yako, utapewa wasaidizi na wafanyakazi wa idara yako, bajeti za kuanzia zimesha pangwa, utapewa form yakujaza, ambayo itakuonyesha staiki zako zote” aliambiwa mwalimu Makame, ambae pia alielezwa kuwa kuanzia siku hiyo ange pewa gari la serikali, na dereva atakae mwendesha, huku akijiandaa kuamia kwenye makazi mapya, yenye hadhi ya cheo chake, ambacho kina uenda sawa na waziri.


“mzee Makame, ukitoka hapa utapitia kwenye ofisi ya mhasibu, akupatie fedha zako za mavazi na huduma ndogo ndogo, nazani unafahamu unatakiwa kuwaje” alisema rais akimweleza mwalimu Makame, amae mpaka sasa akujuwa anaanzia wapi kuendesha sekta hii ya kilimo kwenye kisiwa hiki ambacho kiukweli kinamaeneo machache yenye kuweza kufanya kilimo na mifugo.


Lakini wakati anawaza hayo rais akaendelea kuongea, “pia dereva wako atakupitisha kwa barozi Edgar, maana aliomba kuonana na wewe, nazani kuna jambo la kifamilia mnatakiwa kujadiri” alisema mheshimiwa rais, huku akimaliza kwa kicheko kilicho ungwa mkono wote watatu, yani mwalimu Makame, na waziri wa elimu,


Kwataarifa hii ya mwisho ya kwenda kuonana na Edgar, hakika ilimfanya mzee Makame, ajihisi uafadhari, maana licha ya kutokujuwa anaitiwa nini, lakini pia alipanga kwenda kuongea mambo flani ambayo yangemsaidia katika kusimaia hii sekta ambayo ni mpya hapa kisiwani, na kwamba yeye ndie mwanzilishi.********


Sasa twende mitaa ya darajani, ambako tunamkuta kijana Idd kiparago, akiwa ofisini kwake anasubiria wateja, huku anaumiza kichwa kuhusu Radhia, ni vipi atamtoa kwa Edgar, akukumbuka lolote kuhusu wake zake wote wawili, yani siyo Shani, wala Ashura, yeye kilichomuuma ni kuona Radhia amepata mwanaume mwingine, namba ya zaidi ni kwamba, Radhia licha yakuwa na uzuri wa hasiri, lakini sasa amezidi kuwa mzuri mala mbili.


Idd anawaza kwenda donge kwa mganga, ilimloge Radhia na kumfanya akimbiwe na Edgar, au kufa kabisa, ili wakose wote, “au nimlipe mtu amvizie njiani amgonge na gari, afilie mbali” anawaza Idd, ambae asira yake ni kubwa kuliko ile ya kumwona Ashura akiwa amebebwa na Shaban, kwenye vesper.


Wakati Idd anaendelea kuwa ili nalile, mala analiona gari aina ya BMW jeusi, linasimama mita kama hamsini toka lilipo duka lake, mapigo ya moyo wake yakaanza kwenda mbio, maana alilifananisha lile gari na lile ambalo aliliona siku ile jioni, likimchukuwa Radhia.


Idd analitazama gari lile, ambalo anaona mlango wa mbele upande wa abiria unafunguliwa, na anashuka mwanamke mmoja mrefu kwenye kimo cha Radhia, alie valia gauni refu na miwani meusi, hijabu na viatu vya kudumbukiza, ambae anaelekea kwenye mlango wa nyuma na kuufungua.


Akiwepo Idd mwenyewe, na watu wengine wana tazama kwa macho yenye hamu, ya kumwona anaeshuka toka kwenye gari, kwamaana waliamini ya kuwa ni mheshimiwa au mke wa mheshimiwa.


Wote kwa macho yao wanamwona Radhia, alie pendeza na kunga’aa kwa uso wake mzuri wenye tabasamu na furaha, wenye wakuvutia, akishuka toka kwenye gari taratibu, na kumtazama mwanamke aliemfungulia mlango, tabasamu likizidi kuchanua.


“dada Jasmin usifanye hivyo, mwenzio naona aibu, kama najichoresha hivi” alisema Radhia, kwa sauti ya chini, na wote wakacheka kidogo, “sawa dada Radhia, lakini inabidi uzowee” alisema Jasmin, ambae alifunga milango ya gari na kuondoka zao kuelekea upande wa sokoni, huku wakiongea ili na lile, watu wanao mfahamu Radhia, walitazama kwamshangao, maana awakuelewa kwanini Radhia anafanyiwa yale yote, baadhi walimsalimia na wengine waliishia kumshangaa.


Haraka sana, Idd akainuka toka kwenye kiti, na kutaka kumkimbilia Radhia, ata yeye mwenyewe akujuwa anaenda kumweleza nini, lakini kabla ajapiga hata hatua moja, akashtuliwa “Idd, unaenda wapi, huu mguu ni wako” Idd anasimama na kutazama kule sauti inakotokea, anamwona mzee Haji.


Idd anashtuka kwekweli, maana akutarajia kumwona mzee huyu, akiamini kuwa kila kitu kitapita kimya kimya, “shibaba, kunanini mbona ghafla ata simu ujanipigia?” anauliza Idd kwa sauti ya mshangao na mshtuko, huku anaghairisha safari ya kumfwata Radhia.


“kwani ujuwi kinacho endelea, kwani mke wako mdogo kwa sasa yupo wapi?” anauliza mzee Haji ambae ni mshenga wa kijana Idd, kwa mke wake wapili, “tulikwaluzana kidogo akakimbilia kwao” alisema Idd kwa namna ya kudharau, huku kichwani mwake, anamwona mzee Haji kama kizingiti cha kumzuwia kukutana na Radhia.


“sasa aijawa kidogo mwanangu, nimepigiwa simu nikiwa hapo stendi, taraka inatakiwa haraka iwezekanavyo” alisema mzee Haji, kama vile alikuwa anaongea swala la utani, “kwani taratibu zipoje, anawezaje kudai taraka akiwa nyumbani kwao, arudi kwanza nyumbani ndio tuongelee kuhusu taraka, napo naweza kumpatia taraka moja au mbili akajifikilie” alisema Idd, akionyesha msimamo wake kamamume. ......... ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPA HAPA jamii forums
Aiseeeeee shushaaa vitu kaka sasa mambo yameanza kunoga
 
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA TISINI NA MOJA
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA TISINI: “kwani taratibu zipoje, anawezaje kudai taraka akiwa nyumbani kwao, arudi kwanza nyumbani ndio tuongelee kuhusu taraka, napo naweza kumpatia taraka moja au mbili akajifikilie” alisema Idd, akionyesha msimamo wake kamamume. ......... ENDELEA….


Mzee Haji anamtazama Idd kwamacho ya mashangao, “sawa, kama ilo ndilo wazo lako, basi andaa sehemu ya kufikia mzee kiparago, na baadhi ya ndugu zao wa donge, maana wanatakiwa kuja kusikiliza malala miko ya mkeo mbele ya baraza la wazee wamsikiti wa magomeni, kule ambako ulipeleka ombi la kumchumbia Shani” alisema mzee Haji, pasipo dalili ya utani.


“mh!, anamalalamiko gani zaidi ya ujinga tu?” anasema Idd, ambae kwa haraka haraka anahisi kuwa Shani asingeweza kulalamika wazi wazi, juu ya kuto kupea unyumba, “unasema ujinga, unalala na mkeo kwa miezi minne na unamwingilia mala tatu tu, inamaana kunamwezi umepita bule, sasa kwanini ulimchumbia binti wa watu, siungewaachia vijana wenzio wamchumbie” alisema mzee Haji, na hapo Idd akaona iliswala limesha kuwa nje ya utani, na anatakiwa kuikwepa aibu iliyopo mbele yake.


“tatizo yeye mwenyewe mchafu, yani mzee Haji uwezi amini, ukiingia mala mja tu uwezi tena kurudia, mbona mke wangu mkubwa nilikuwa nafanya nae mala kwa mala, nitampa taraka, utaona kama atapata mwanaume mwingine” alisema Idd, huku anachukuwa kalamu na karatasi, “sasa kwanini ukumweleza ukweli mkeo ili ajisafishe, na hizo taraka uziandike tatu kama walivyosema” alisema, nipe nauli ya taxi, na vitu vyake yote, nivipeleke kwao” alisisitiza mshenga.********


Mzee Makame mida hii alikuwa amesha toka ofisini kwa rais na kuonyeshwa ofisi yake, ambayo ilikuwa inaendelea kuandaliwa, nakuwekewa kila kitu ambacho kilistahili kuwepo kwenye ofisi yenye hadhi ya waziri.


Tayari alisha pewa fedha kwaajili ya mavazi yake na wake zake, maana tayari nao walisha ingia kwenye hadhi ya VIP, na sasa alikuwa anashuka toka kwenye gari lililosimama nje ya ofisi ya ubarozi wa #Mbogo_Land, msaidi wake anafungua mlango na yeye anashuka toka kwenye gari, na kuelekea mapokezi, akiongozana na msaidizi wake alie kuwa amebeba mkoba wake.


Mzee Makame anapokelewa na mwanadada Monica, ambae anamfahamu mzee huyu, kuwa ni baba wa wa Radhia, yani mchumba wa boss wake Edgar Frank Nyati, “karibu sana baba, hongera kwa majukumu mpaya uliyo kabidhiwa” alisema Edgar mala baada ya Monica kumpeleka mzee Makame ofisini kwake.


“hakika mpaka sasa najiona nipo kwenye usingizi wa likizo, ngoja pakuche nitaelewa” alisema mzee Makame, kwa haraka ungejuwa ni utani, lakini ukweli alikuwa anamaanisha.


Baada ya kusalimiana maongezi yakaanza, kwa mzee Abeid Makame, kumweleza barozi Edgar, kuhusu kile alichoitiwa na mheshimiwa rais, “sasa baba, nitaanzaje kuendesha hii sekta katika nchi kama hii, ambayo kilimo kinachofanywa ni nikile cha mashamba madogo madogo, ya watu binafsi na aina ebeo tengefu la kilimo wala lile ambalo linaweza kutumika kwa ufugaji” alijieleza mzee Makame.


“kwa ilo baba ondoa shaka, nazani kuna baadhi ya nchi kama #Mbogo_Land, ambayo inamaeneo madogo sana, yenye kufanana na kisiwa iki, lakini kilimo kinaendelea, hatua ya kwanza utaenda kuonana na waziri wa kilimo na mifugo wa nchi ya #Mbogo_Land, ata kupatia mwanga, kabla ya kutafuta wataalamu wa kwenda kujifunza kilimo cha aina hiyo huko nchini kwetu, nakuja kusimamia huku, nitakutafutia ufadhiri mimi mwenyewe” alisema Edgar.


Hapo ikawa afadhari kwa mzee Makame, ambae alipanga kesho kazi yake ya kwanza ofisini, ni kuandaa mpango huo, na kuupeleka kwa rais, ili utolewe maamuzi, na luksa.


Baada ya maongezi ya awamu ya kwanza, ikafwata maongezi ya hawamu ya pili, “nazani mimi nilifanya haraka kueleza matatizo yangu, ila wewe pia ulikuwa na jambo lako” alisema mzee Makame, huku anamtazama kijana Edgar.


Ni wazi ukimtazama Edgar, ungeona ni kama kunajambo muhumu alitaka kumweleza mzee Makame, lakini lilikuwa lina muwia vigumu, “sijuwi nianzaje, maana sijajuwa taratibu zenu” alisema Edgar, kwa sauti yenye utulivu na nidhamu, “bila shaka baba, unaweza kuongea tu, kama itakuwa tofauti nitakueleza” alisema mzee Makame, katika hali ya uchangamfu.


Edgar anatabasamu kidogo, “mzee ukweli nikwamba, mimi na Radhia, tupo kwenye urafiki, na nimesha wajulisha nyumbani, na pia tuna week ya tatu sasa tupo pamoja, na nitaitaji kwenda nae nyumbani, ili kufwata utaratibu wa kupata luksa ya wazazi, kama mila na desturi zilivyo, iliniweze kuja kuja kumchumbia lasmi nyumbani kwako” alisema Edgar kwa sauti yenye tahadhari.


Mzee Makame anaanatabasamu kidogo, “nikuulize Edgar, unafahamu kuwa binti yangu alisha wai kuolewa na akaachika?” analiuliza mzee Makame, “ndiyo nafhamu, na mume wake wa zamani nimesha wai kumwona” lilikuwa jibu jepesi lakini lilimshtua mzee Makame, ambae akujuwa Edgar na Idd wameonana vipi.


“kama ni ilo tu kijana wangu wala hakuna shida, labda nieleze ulikuwa unataka kusemaje baada ya hapo” aliongea mzee Makame, ambae pengine alihisi kuwa, Edgar anataka kuomba luksa ya kuishi na Radhia, “baba hii ni sababu za kiusalama, maana tayari watu wengi wanafahamu kuwa Radhia nipo nae, hivyo naitaji kumpatia Radhia usafiri dereva na mlinzi” alisema Edgar, huku anamtazama mzee Makame kwa macho ya tahadhari.


Hapo mzee Makame akaachia tabasamu laini, “kwanza kijana nashukuru sana kwa kuniheshimisha, maana ndoa ya pili kwa binti alie talikiwa, sisi kwetu kama bahati tu, zaidi ya hapo angeishiwa kaa nyumbani tu, cha msingi kijana wangu, kama manapendana mimi sina pingamizi, lakini itakuwa vyema kama mtafunga ndoa na kuishi kwa amani” alisema mzee Makame.


Hapo Edgar akasimama na kuweka mkono wake kifuani, mwingine akiweka mgongoni, na kuinamisha kichwa chini, “asante baba yangu, nitamlea na kumtunza Radhia, kama alivyokuwa kwako” alisema Edgar, akimfanya mzee Makame, ashindwe cha kufanya, zaidi kusimama na kumpatia mkono Edgar, ambae pia aliupokea, “panapo majaliwa” aliitikia mzee Makame.


Baada ya hapo waliongea mawili matatu, eagar alimweleza mzee Makame, jukumu ambalo amempatia Radhia kwa sasa, lakuisimamia ugeni toka #Mbogo_Land, pia akamsisitiza jambo mzee Makame, “baba inabidi uwe na maandalizi makubwa sana kuanzia sasa, iwe nyumbani au ofisini, maana baada ya leo kutangazwa katika nyadhfa yako mpya, lazima wageni watakuwa wengi sana ofisini na nyumbani” alisema Edgar, katika maongezi hayo ya baba na mkwe wake.


“ilo nalo neno, wacha nikaandae juice nyingi na vireja, kwaajili ya ugeni, pia nitakujulisha kwenye nyumba nitakayo amia” alisema mzee Makame, akionekana mwenye furaha kubwa, “pia Siwema amesha ongea na waziri wa afya, na sasa amepangiwa kituo kingine” alieleza Edgar, ikiwa nitaarfa mpya na nzuri kwa mzee Makame. ......... ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPA HAPA jamii forums
 
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA TISINI NA MBILI
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA TISINI NA MOJA: “ilo nalo neno, wacha nikaandae juice nyingi na vireja, kwaajili ya ugeni, pia nitakujulisha kwenye nyumba nitakayo amia” alisema mzee Makame, akionekana mwenye furaha kubwa, “pia Siwema amesha ongea na waziri wa afya, na sasa amepangiwa kituo kingine” alieleza Edgar, ikiwa nitaarfa mpya na nzuri kwa mzee Makame. ......... ENDELEA….


“huu ndio wakati wa kumrudisha Himid, aje apate kazi hapa nchini, na kuishi na familia yake” alisema mzee Makame japo kwa utani lakini aliongea ukweli mtupu, awakukaa sana wakaagana na mzee Makame akaondoka zake akimpiitia msaidizi wake aliekuwa nje ya ofisi.


Baada ya kutoka ofisini kwa barozi wa #Mbogo_Land, mzee Makame akaelekea moja kwa moja shule ya sekondari ya mwanakwelekwe A, ambako alimkutana na mwalimu mkuu na kumweleza juu ya jukumu jipya alilopatiwa na mheshimiwa rais, mwalimu mkuu na walimu wengine walimpongeza na kumwomba asi waache katika mafanikio yake.


Pia mzee Makame aliwaaga wanafunzi wa baadhi ya badarasa ambayo alikuwa anafundisha, kabla ya kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwake akipanga kwenda kuwa chukuwa na mjini kufanya manunuzi ya nguo mpya na vifaa vya pale nyumbani, kwaa jili ya wageni wa muda wowote ambao wangeanza kuja pale nyumbani, ikiwa ni tahadhari, ya matarajio ya ugeni wa kila aina.*****


Wakati huo tayari Radhia na Jasmin walikuwa wamesha jichanganya sokoni wananunua vitu flani flani kwaajili ya kupika, sasa walikuwa wanaongea kama marafiki wakawaida, “kwahiyo Edgar aniamini mpaka ameniwekea mlinzi, au wivu unamsumbua?” aliuliza Radhia, akijaribu kupata ukweli juu ya ulinzi alio wekewa.


Jasmin anacheka kidogo, “hapana dada Radhia, sasa hivi wewe ni VIP, utakiwi kuonekana hovyo na wala kutembea mwenyewe, kwa salama wako” alisema Jasmin, sambamba na kicheko laini, huku akimwacha Radhia kwenye mshangao ilio ambatana na tabasamu la chini chini.


“kwanini sasa, itakuwaje nyumbani hawajuwi kama nina usiana na Edgar” alisema Radhia, huku hali flani ya mshangao na aibu kwambali ikimtawala usoni mwake, “nazani kuna utaratibu unafanyika, kila kitu kitakuwa sawa, isitoshe baba yako asubuhi hii, akitoka ikulu ataenda ofisini kwa mheshimiwa barozi” alisema Jasmin, huku wanamalizia kununua vitu na kuana safari ya kurudi kwenye gari.


Taarifa ya baba yake kuitwa ikulu ilikuwa ngeni kwa Radhia, japo alisha wasi kusikia akizungumziwa mala kwa mala, kwamba baba yake anaweza kupatiwa majukumu mapya, nje ya kazi yake ya ualimu.


Wakiwa wanatembea huku wanaongea na kucheka kwa pamoja, wakiwa wamesaidiana kubeba mizigo mbali mbali waliyo nunua sokoni, hawana ili na lile, wanakatiza usawa wa maduka, ya vifaa vya umeme vilivyo tumika.*******


Siwema ndie aliekuwa wakanza kufika nyumbani, ambako aliwakuta mama zake na wadogo zake wanakunywa chai, “aya tueleze habariza huko” alisema mama Mariam, kwa shahuku, maana licha ya yote yanayoendelea, alifuirahi kuona binti yake anarudishwa kazini, japo kukwepa aibu moja, kati ya mbili ambazo zilikuwa zina mkabili, yani kutarikiwa na kufukuzwa kazi.


“nimesha rudishwa kazini, lakini naamia hospital ya magomeni, ila Radhia sijuwi kamwambia nini yule waziri, eti anasema nisimtie tena aibu mdogo wangu, yani bora ata asingenisaidia, kama ndiyo kunisimanga kule” alilalamika Siwema, ambae alimshangaza ata mama yake mwenyewe.


“lakini alie ongea na waziri ni Edgar, na sidhani kama Edgar anaweza kumweleza hivyo waziri” alisema mama adhia, na wakati huo huo wakaliona gari jeusi aina ya Toyota V8, lenye namba za serikali, likija upande wa nyumbani kwao, kila mmoja akahisi kuwa ni Radhia alikuwa anarudi toka alikokuwepo, “ona sasa amesubiri baba ameenda kazini, ameamua kujionyesha wazi wazi, anarudishwa na mwaume kweupeeee” alisema Siwema, na mama yake akaunga mkono.


“ata kama ni mjane, lakini mama Radhia unapaswa kumweleza Radhia ajiheshimu kidogo, unazani majilani wanavyoona wanasema” alisema mama Mariam, kwa sauti ya kusisitiza na kusimanga, huku mama Radhia akiwa amekaa kimya, kwa kuona kinachosema kina ukweli ndani yake.


Gari lina simama, mbele ya kibaradha cha nyumba yao, linazidi kuwa tia hasira wakina mama Mariam na mabinti zake, “alafu toka alipo ondoka juzi, ajarudi mpaka leo, ata huyo mwanaume si ata mchoka” anasema Siwema kwa sauti ya chini huku wanaona mlango wa mbele wa gari, na ule wa nyuma inafunguliwa, ule wa nyuma anashika mwanaume mmoja kijana wa umri wa kati ya miaka 30, alie bena mkoba ambao wana ufahamu kuwa ni mkoba wa mama yao anao utumia kubebea vitabu vyake vya shuleni.


Wote wanatazama gari kwa tahadhari, wanamwona baba yao anashuka toka kwenye seat ya mbele, ambayo hipo upande wapili wa gari, yani upande wa kushoto, chuki zina watawala watoto wa mama Mariam na mama Mariam mwenyewe, ambao wanahisi kuwa, gari ili ni moja kati ya magari yaliyokuja ijuma mosi yakimleta Edgar.


Yule kijana anasogea mpaka kwenye ngazi akiwa na mkoba wa mzee Makame, “asante kijana, nisubirini dakika chache, tujiandae ili twende mjini” alisema mzee Makame, huku ananyoosha mkono kupokea mkoba wake, “sawa mheshimiwa” aliitikia yule kijana na kumpatia mzee Makame mkoba wake, kisha aka rudi kwenye gari.


Mama Radhia anainuka na kumpkea mume wake mkoba, kisha mzee Makame akiwa mwenye furaha akawatazama wanafamilia wote, “njooni ndani kuna jambo niwaambie” alisema mzee Makame kisha akaingia ndani, ambako tayari alikuta mke mdogo, anatoka chumbani akiwa ameacha mkoba.


Naaaaaam!, sasa watu watano wapo sebuleni, pamoja na mzee Makame, “jamani kama nilivyo dokezwa, siku zilizo pita na wakina Mukhsin, leo nimeitwa ikulu, na nimepatiwa wadhfa mkubwa sana, ni sawa na kuwa waziri, chini ya rais mwenyewe, kesho naweza kuapishwa” alisema mzee Makame, pia akawaeleza kuhusu maandalizi ya pale nyumbani, kunauwezekano wa watu kuja kumpongeza, pia aliwaeleza swala la kupatiwa nyumba nyingine, huku akiwahaidi kuilekebisha nyumba ile wanayoishi.


“nazani Siwema umesha rudishwa kazini, hivyo unaitaji kujitunza na kujiheshimu, maana sasa tunaenda kuwa familia ya VIP, kamaana chochote atakachokifanya mwanafamilia kitafwatiliwa kwa karibu sana” alisema mzee Makame, ambae pia aliwaeleza juu ya swala la Radhia.


Zilikuwa taharifa nzuri kwa wanafamilia, kila mmoja alionekana kufurahia taarifa ile, na kupanga kichwani mwake, jinsi atakavyo utumia wadhfa wa baba yao, navile watakavyo ishi kama wanafamilia toka familia ya VIP, “lakini aya yote ni sababu ya urafiki wa Radhia na huyu barozi, ulio wakutanisha na rais na kuulizia kuhusu mimi” alifafanua mzee Makame, lakini aikuonyesha kuwachukiza wala kuwafikilisha wakina mama riam na mabinti zake, japo mama Radhia alijionea fahari kwa binti yake.


Mzee Makame akuwa ameishia hapo, “nazani mnafahamu kuwa Radhia aliachika kwa mume wake, na sasa amepata rafiki mwingine, niyule kijana barozi wa #Mbogo_Land” hapo kila mmoja akarudisha akili yake maali pale, akitokra kwenye furaha ya kuwa mtoto mkulugenzi wa idara ya kilimo.


“yule kijana ameamua kufwata taratibu kwa kumchumbia Radhia, kwa taratibu za nchi yao, nazani hii ni makubariano yao na Radhia, kikubwa ni kwamba, amemweka katika orodha ya wanafamilia yake, hivyo basi, kuanzia sasa atapata stahiki zake kama mke” ilo liliwashtua wakina Mariam Siwema na mama mama yao, ambao walitamani kuongea kitu, lakini mzee Makame akawai.


“kwamaana hiyo msishangae kuona anatembelea gari kama wake wa viongozi wengine, na pia msishangae kuona anasimamiwa na mlinzi kama wake wa viongozi wengine, hii ni kwasababu ya usalama wake kutokana na hadhi aliyonayo, maana anaweza kupangiwa kusimamia miradi yoyote ya serikali ya nchi ya #Mbogo_Land” alisema mzee Makame, na kuzidi kuwa weka taharuki vichwani mwa watoto wake na mke wake mkubwa. . ......... ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPA HAPA jamii forums
 
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA TISINI NA TATU
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA TISINI NA MBILI: “kwamaana hiyo msishangae kuona anatembelea gari kama wake wa viongozi wengine, na pia msishangae kuona anasimamiwa na mlinzi kama wake wa viongozi wengine, hii ni kwasababu ya usalama wake kutokana na hadhi aliyonayo, maana anaweza kupangiwa kusimamia miradi yoyote ya serikali ya nchi ya #Mbogo_Land” alisema mzee Makame, na kuzidi kuwa weka taharuki vichwani mwa watoto wake na mke wake mkubwa. . ......... ENDELEA….


Ilikuwa tofauti kwa mke mdogo, ambae alijawa na furaha isyo kifani, japo aliificha asionyeshe wazi wazi, “hivyo basi, kuanzia leo msishangae wala kusema vibaya, anapoenda kumtembelea mwenzie, na akija Edgar au popote mtakapo mwona mchukulieni kama mwanafamilia, na ukichukulia kijana wawatu ni mtu mstaarabu na mwenye moyo mzuri” alimaliza mzee Makame, kisha akawaeleza wake zake wakajiande wanatakiwa kwenda manunuzi.********


Akiwa amekaa dukani kwake, anawaza jinsi mke wake mdogo yani Shani alivyo enda kueleza nyumbani kwao, hakika roho ilimuuma sana Idd, ambae sasa anaanza kukumbuka kuhusu maneno ya Shani juzi usiku, na chanzo cha ugomvi wao, “sasa kama sijisikii ningefanyaje, ni umalaya tu mbona mwenzie anakaa ata miezi miwili bila kumtombw….., na asemi chochote, au anajini mahaba yule” anajisemea Idd kwa sauti yenye hasira.


“mwache aende tu, atanikumbuka mwenyewe, na kuwa ni hasira zake tu, sababu nilimtandika” anawaza Idd, huku macho yake yakiwa kwenye kijinia cha mtaa ule, na wakati huo huo anamwona Radhia kwambali, akiwa na yule mwanamke mwingine, wanaelekea walipoliacha gari, ambalo sasa alilikuwa limegeukia lilikotoka.


Idd anainyka haraka na kutoka dukani, anaanza kukimbilia aliko Radhia, ambae anamwona anaingia kwenye gari, na gari linaondoka, Idd anasimama huku akishindwa kupiga kelele, roho inamuuma anageuka alikotoka, na kurudi dukani, anaumiza kichwa afanyaje, ili amtoe Radhia kwa mpemzi wake mpya, moyo unamuuma kweli kweli, kuona Radhia anafuraha na anaishi vizuri zaidi ya zamani.


Idd amesahau kuhusu mke mdogo, ambae amesha mpatia taraka, wala akumbuki kuhusu mke mkubwa mjamzito, ambae ajamjulia hali toka alipo ondoka nyumbani kwake, usiku wa juzi kuamkia jana, na wenda kwa dada yake, na wala hakuwa na mpango wa kumtembelea, licha ya kujuwa kuwa, Ashura anaweza kujifungua wakati wowote, kuanzia week tatu zijazo.*******


Dakika kumi na tano baadae, jang’ombe kwa soud, gari jeusi aina ya Toyota V8, linaonekana limesimama mbele ya kibaradha cha mbele cha nyumba kongwe, ya mzee Abeid Ally Makame, Radhia Zuhura na dada yao Siwema wapo kibaradhani, wamekaa kwenye mkeka wanaongea kwa mbwe mbwe, na kujichekesha chekesha kimitego, huku mala kwa mala macho yao yakielekea upende lilipo gari, ambalo ndani yake kulikuwa na wanaume wawili.


Dakika tano mbele mzee Abeid anatoka ndani na wake zake, wakiwa wamevalia vizuri na kinadhifu, mzee Makame akiwa amebeba mkoba wake wa kazini, ambao sasa ulikuwa na fedha za kufanyia manunuzi, “tutawakuta jamani make vizuri hapa nyumbani” anasema mama Mariam, ambae uso wake unaonyesha kuwa na furaha isiyo kifani, kama ilivyokuwa kwa mke mdogo, yani mama Radhia, na mume wao mzee Makame.


Kijana mmoja anashuka toka kwenye gari, na kupokea mkoba kwa mzee Makame, safari hii mzee Makame anakaa seat ya mbele kama kawaida, wake zake wanakaa seat ya katikati, wakati yule mlinzi akikaa nyuma kabisa, na safari ya kuelekea mjini inaanza, wakina Siwema wanalisindikiza kwa macho.


Lakini kabla gari walilopanda wazazi wao alija toweka, wanaliona linapishana na gari dogo aina ya BMW, lililokuwa linakuja upande wao, gari ambalo, siku moja walisha liona likija pale nyumbani kwao, likiwaleta wakina Radhia.


“kisilani hicho kinaingia, akichoki kutombw…, yani siku ya tatu ameilaza huko huko” anasema Siwema kwa hasira na chuki, huku wote wanalitazama lile gari lililosimama kidogo, nakusimama kwa sekunde kadhaa, bila mtu yoyote kushuka, ni wazi waliokuwa wanaongea walishusha vioo, na kuongea wakiwa ndani ya gari, kisha kila gari likaendelea na safari.


“anavyo jifanya sasa, mi mwenzenu ananiuzi” alisema Zuhura, akionyesha wazi kuwa na chuki kubwa zidi ya dada yake huyo, ambae kwa sababu yake maisha yao yanaenda kubadirika, “unishindi mimi, yani namchukia, anajiona amepaaaata” anasema Mariam, huku wanazidi kulitazama gari ambalo lilikuwa linazidi kusogea nyumbani kwao.


“mtu mwenyewe ataachika siku siyo nyingi, kwani kuna wanaume anapenda kuishi na mwanamke asie zaa, huyo kaka anajiburudisha tu, kisha anamwacha” alisema Siwema kwa sauti ya chini, huku wanalitazama gari ambalo sasa lilikuwa linasimama.


Kitu ambacho awakukijuwa ni kwamba, sura zao zilionyesha chuki za wazi kabisa, kiasi kwamba ata wakina Radhia Jasmin na Nadia, waliokuwepo ndani ya gari waliliona jambo ilo, lakini wakina Nadia walishindwa kuhoji, sababu walichukulia kuwa ni jambo ambalo lilikuwa hali wahusu.


Gari linasimama wakina Mariam waliotegemea kumwona Radhia anashuka peke yake, au pamoja na Edgar, wanashangaa kuona Radhia anashuka na mwanamke mwingine, alie kuwa anamsaidia kushusha mizigo toka kwenye gari.


Wakina Siwema wamekaa pale pale kibaradhani, wakimtazama Radhia akisaidiana na yule mwanamke, kuingiza mizigo ndani, awakusaidia wala kupokea mfuko wowote, na ata walipo maliza na kusalimia, waliitikia kama wagonjwa, ni wazi awakupendezwa na jambo flani, toka kwa Radhia au yule mwanamke.


“dada Jasmin awa ni dada zangu, kuna dada Siwema, Mariam na Zuhura, popote utapo waona ujuwe ni ndugu zangu” alisema Radhia, akiwatambulisha wakina Mariam, ambao kiukweli walikuwa wamekunja sura zao kwa chuki, kiasi cha kumshangaza Jasmin, “nimfurahi kuwafahamu dada” alisema Jasmin ambae alikuwa amesimama pembeni kidogo ya mkeka.


Kwakuona mazingira jinsi yalivyo, na mwonekano wa ndugu zake, Radhia ambae alikuwa na kazi flani flani za kufanya, akaamua tumia busara na akili zake za kuzaliwa, ilikuepusha migogoro na aibu, “dada Jasmin mnaweza kwenda, nitawapigia simu baadae mje kunichukuwa, sasa hivi nitakuwa na panga mambo yangu, juu ya ugeni unaotoka #Mbogo_Land”, alisema Radhia, huku muda wote tabasamu limemtawara usoni.


Bila ubishi Jasmin akakubariana nae na kuondoka zake, kuelekea kwenye gari, ambako awakutumia ata sekunde kumi, tayari gari lilishaanza kuondoka, likishika uelekeo wa barabara kuu.


Baada ya gari kuondoka, Radhia anamtazama Mariam na kisha Zuhura, “Mariamna Zuhura, kuna vitu vya kupika nimekuja navyo, vipo kwenye jiko la ndani, mimi kunakitu naenda kufanya, nikimaliza nitakuja kuwasaidia” alisema Radhia, kwa sauti yenye uchangamfu, akijaribu kuwa leta ndugu zake kwenye furaha toka kwenye hali waliyokuwa nayo.


“kwahiyo wewe ndiyo mama mwenye nyumba, unatupangia kazi sisi vijakazi wako?” alieuliza alikuwa ni Siwema, tena kwa sauti yenye chuki na hasira, huku wakina Zuhura wakichekea pembeni, “siyo hivyo dada, nimesema kuna kazi naenda kuifanya, nikimaliza nita……” alifafanua Radhia, kwa sauti ye upole, lakini kabla ajamaliza Siwema akadakia.


“unakazi gani bwana, kunyoa vuz.., yani umekaa huko siku tatu unatombw…, leo una rudi ujifanye unakazi, waache wenzako nao wapumzike” alisema Siwema, kwa sauti ya juu ya kali na chuki, na kufanya wakina Mariam wacheke kile kicheko cha kuzomea.


Hakika ilimwacha Radhia mdomo wazi, “dada hivi kuna kitu ambacho nimekukosea na mimi sikijuwi, mbona kama sikuhizi umezidisha chuki kupita kiasi?” anauliza Radhia kwa sauti ya upole, lakini yenye machungu.


“nani anachuki na wewe, utaki kuambiwa ukweli, kwani ulikuwa wapi siku mbili zote hizi, au ulikuwa umeenda kwa mama mdogo, mtu mwenyewe unajijuwa tasa, alafu unaangaikia wanaume, kama siyo kujizalilisha tu, maana watakuchezea na kukuacha” alisema Siwema, kwa sauti ya kusimanga. . ......... ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPA HAPA jamii forums
 
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA TISINI NA NNE
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA TISINI NA TATU: “nani anachuki na wewe, utaki kuambiwa ukweli, kwani ulikuwa wapi siku mbili zote hizi, au ulikuwa umeenda kwa mama mdogo, mtu mwenyewe unajijuwa tasa, alafu unaangaikia wanaume, kama siyo kujizalilisha tu, maana watakuchezea na kukuacha” alisema Siwema, kwa sauti ya kusimanga. . ......... ENDELEA….


Hapo Radhia aliwaza mambo mawili kwa haraka sana, moja ni chanzo cha chuki aliyonayo Siwema, maana licha ya kusaidiwa kurudi kazini na mchumba wake, yani Edgar, lakini bado anaonyesha chuki za hali ya juu zidi yake.


Pili kwa ni sababu ya chuki zidi yake kuzidi mala mala dufu, maana yeye akuona sababu wala kisa cha dada yake kuwa na chuki zidi yake, “dada Siwema, kama kunakitu nimewakosea mimi au mama yangu au wadogo zangu, naomba mnieleze ili tumalize, hakika hii siyo sawa, wala aipendezi, kwa wanafamilia kuwa hivi” alisema Radhia kwa sauti yenye machungu.


Hapo kinasikika kicheko toka kwa Siwema, kicheko ambacho kina wanashangaza ata wakina Mariam, ambao kiukweli ata wao waliingiwa na maneno ya Radhia, nakujiona ni wakosefu, “nani anakuchukia Radhia, unanini cha kuchukiwa mgumba kama wewe, au utaki tukuambie ukweli unavyo tutia aibu, kuwa kwa mwanaume, auna ata muda wakukaa nyumbani kupika” alisema Siwema, kwa sauti ile ile ya ukali yenye kusimanga.


Radhia akainuka na kuelekea ndani, ambako alikaa kwa dakika kumi na tano, akiwaacha Siwema na wadogo zake wakipongezana kwa kile alichokifanya Siwema, na baadae Radhia akatoka na vitu vya kupika, na kuanza mapishi, ambayo aliyaendesha kimya kimya, huku Siwema na wadogo zake wakiongea maneno ya mafumbo, yaliyo mlenga Radhia, ambae akujibu chochote, zaidi ya kuendelea kupika.


Mapishi yaliendelea kimya kimya kwa upande wa Radhia, vijembe vikiendelea kumiminika, toka kwa Siwema na wadogo zake, ambao walitegemea kumwona Radhia anakosa amani, lakini baada yake wakaanza kumwona anapika huku mala kwa mala akipokea na kutuma ujumbe kwenye simu, yake, wakati mwingine alionekana aitabasamu kwa sfuraha, pale alipokuwa anausoma ujumbe.


Zilikuwa ni jumbe tamu, toka kwa Edgar, ambao walikuwa wanakumbushana kuhusu matukio waliyokuwa wanayafanya nyakati tofauti tofauti, asa wakiwa chumbani kule nyumbani kwa Edgar.


Hali ya furaha, aliyokuwa nayo Radhia, kwa wakati huu ilianza kuwa chukiza wakina Siwema, ambao mala nyingi uwa awawezi kuficha chuki zao, “mambo ya watoto anafanya mtu mzima, mjane ni mjane, waachie ambao awajawai kuachwa” alisema Siwema, kwa sauti ya chuki, na kusimanga, huku akisaidiwa na vicheko toka kwa wakina Mariam.


Safari hii Radhia nae akajikuta anacheka kwa sauti, ni wazi alicheka kile alichoongea Siwema, na kuwafanya wakina Mariam na Zuhura, watazamane kwamasho ya kujisuta, lakini ilikuwa tofauti kwa siwea ambae alimtazama Radhia kwa macho ya ukali, “unacheka nini?” aliuliza Siwema kwa ukali, ni wazi alijuwa kwanini Radhia alicheka.


“jamani dada sasa unataka nichukie au ninune, wakati unachoongea kinachekesha, mimi nicheka hivyo ulivyosema niwaachie ambao awajawai kuachwa, kwani kuachwa ni ugonjwa, na kama ugonjwa mimi nimesha pona” alisema Radhia, kwa sauti ya uchangamfu.


Hakika ilimuuma Siwema, ambae aliongea pasipo kukumbuka kuwa na yeye ni mjane, “jamani siwezi kuvumilia dharau kama hii…” alisema Siwema kwa sauti ya juu yenye hasira, na wakati huo huo wote wakashtuliwa na ngurumo ya gari alililokuwa linakaribia nyumbani kwao.


Wote wakalitazama gari lile, ambalo nilile walilo ondoka nalo wakina mzee Makame, lililokuja na kusimama mbele ya kibaradha, kisha wakina mzee Makame wakashuka, na bindi zake wakawapokea na kuingiza mizigo ndani, dereva akiondoka zake, kwamaangizo ya kwamba kesho mapema aje amchukue kwaajili ya kuelekea kazini.


Radhia akamwomba mama yake amsaidie kupika, na yeye akafanye kazi ambayo ilikuwa inamkabiri, “kwanini usinge waachia wadogo zako, siungekuwa umesha maliza kazi zako” alisema mama Mariam, ambae alisisitiza Radhia akaendelee na kazi zake, kwamba yeye na mama Radhia wangeendelea kupika.


Radhia kueleza kilichotokea kwa mama zake, zaidi aliingia ndani na kuanza kazi zake, akifwata maelekezo ya Edgar, ambapo alitumia masaa mawili kuikamilisha, na kubakia utekelezaji, kuna wakati mama yake aliingia chumbani na kuungana na Radhia wakiongea ili nalile.


Mama Radhia alimweleza Radhia jinsi mzee Makame alivyo eleza kuhusu yeye, kwamba kwa sasa niluksa kukutana na Edgar, pia atozuiliwa kwenda kumtembelea Edgar nyumbani kwake, kwatafsiri ya kwamba, kwenda kulala siku na wakati wowote.


Radhia alimweleza mama yake, juu ya chuki za wazi za wakina Siwema, hakika ilimshangaza sana mama Radhia, ambae alishindwa kuelewa ni roho au moyo wa ainagani aliokuwa nao Siwema, “achana nae Radhia, kikubwa angalia mambo yako yaenda sawa, ila kuwa nae makini, maana sijawai kuona moyo wa aina hii” alisema mama Radhia.********


Naaaaaam!, usiku wa saa mbili, watu wapo majumbani mwao, wanapata chakula cha jioni, huku macho yakiwa kwenye television wanaangalia taaria ya habari ambayo ilikuwa inaanza.


Mida hii ilimkuta Radhia akiwa nyumbani kwa Edgar, wametulia chumbani mezani zinaongekana grass mbili za juice ya matunda harisi, wao wame po juu ya kochi moja kubwa, Radhia akiwa amevalia gauni jepesi la kulalia, Edgar amevalia bukta nyepesi ambayo utumia kulalia, Radhia amejilaza juu ya kufua cha Edgar, amelegea kiasi, kutokana na jambo walilolo lifanya nusu saa iliyopita.


Maana aikuwa kazi ndogo, mala tu baada ya Radhia kukutana na Edgar mazoezini, alikopelekwa na dereva, ambapoko alimkuta Edgar anacheza mpira wakikapu na wakina Mukhsin.


Radhia alitulia akifwatilia mazoezi, mpaka muda ulipotamatika, na wakina Mukshin kushika uelekeo wa nyumbani kwao, huku Radhia na Edgar wakielekea nyumbani kwa Edgar, ambako awakupeana nafasi ya kuuliza habari za mchana.


Maana ile kuingia tu chumbani, wakavua nguo na kuingia bafuni, kuoga ambako walianza kuoga huku wanapeana dudu kisawa sawa, na kila mmoja akionekana kufurahia anachokifanya au kufanyiwa na mwenzie, Radhia nae alionekana kumzowea Edgar na kuwa huru kwa kile wanachofanya, ilifikia wakati yeye akawa anabadiri mkao bila ata kuambiwa.


Kitu ambacho uwezi kuamini ni kwamba, walitumia lisaa lizima wakiwa bafuni, ikiwa ni kuoga na kunyanduana, “ulifanikiwa kupangilia mapokezi ya wageni wetu?” aliuliza Edgar huku anachezea nywele za Radhia aliekuwa amelala kifuani kwake, “ndiyo nimefanikiwa, bado kwenda kwenye hotel watakayofikia, na kujuwa gharama kwa ujumla, nimeilenga Zanzibar beach resort” alisema Radhia, ambae kimoyo moyo anashukuru serikali ya #Mbogo_Land kumleta Edgar Unguja, na kukutana na yeye.


Wakati huo huo nyumbani kwa mzee Abeid, familia nzima ilikuwa sebuleni, inasubiri taarifa ya habari, huku kijana Idd akiwa mwenyewe sebuleni, anakula urojo huku anatazama taarifa ya habari, japo mawazo yake yalikuwa ni juu ya kumvuruga Radhia na kumtoa kwa mpenzi wake mpya.


Idd ambae akukumbuka lolote kuhusu mke wake mkubwa, ya bi Ashura, akiwa anaendelea kuwaza ili na lile, namna ya kumvurugia Radhia, mala masikio yake yakanasa kitu toka kwenye TV, “nahuu ni muktasali wake, rais wa serikali ya mapinduzi aanzisha sekta mpya na kufanya uteuzi wa mkurugenzi mpya wa sekta hiyo ya kilimo na mifugo” ilikuwa ni sauti ya mtangazaji maarufu wa taarifa za habari wa television hiyo.


Kwamala ya kwanza aikumwingia hakilini, lakini pale ilipoanza habari kamili, ndipo Idd alipo shtuka na kuona kutega vyema masikio yake, “mheshimiwa rais amefanya uteuzi huo, leo mapema katika ikulu, na kumteuwa mwalimu Abeid Ally Makame, kuwa mkurugenzi wa idara hiyo mpya” hakika taarifa hii, ilimshtua kidogo Idd, “au Makame mwingine?” alijiuliza Idd, huku akikosa jibu, maana ata taarifa yenyewe aikuonyesha video wala picha ya mwalimu Makame.


Lakini pia taarifa ilieleza kuwa, mwalimu Makame ata apishwa kesho, kwenye ukumbi wa ikulu, “naomba isiwe hivyo, mbona Radhia atazidi kulinga” alijisemea Idd, ambae licha ya tamaa aliyonayo juu ya Radhia, lakini ameshindwa kumiliki mke mwingine, ambae leo amempatia taraka. ......... ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPA HAPA jamii forums
 
Back
Top Bottom