ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA ALOBAINI NA NANE
MTUNZI:
edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA ALOBAINI NA SABA: “ok!, kwa hiyo umesha tosheka na music?” anauliza Edgar, huku anainuka toka kwenye kiti, akiwa ameshika simu na ile pochi ya Radhia, “nimesha tosheka, na nimefurahi aswaaaa” anasema Radhia, kwa sauti ya kitoto, sambamba na kakicheko flani katamu. ......... ENDELEA….
Edgar anampatia Radhia vitu vyake, kisha wanaanza kutembea kuelekea nje, wakiwa wameshikana mikono, kitu ambacho sasa Radhia alikuwa ameshaanza kukizowea, maana akuona aibu wala kushtuka, ijapokuwa alijihisi msisimko mtamu sana, msisimko ambao ulimfanya atamani Edgar atamke neno, ama hakika leo hii hii angekuwa tayari kumpatia shamba la bibi akaanze kulichimbua.
Edgar na Radhia wanaibukia nje, wakiwa wameshikana mikono, kama ilivyo kuwa kwa wenzao wengi waliokuwa VIP, yani baadhi ya viongozi na wafanya biashara wengine, ambao baadhi yao walikuwa na wake zaidi ya mmoja.
“Radhia ebu tazama kule, si yule dada yako?” anauliza Edgar, huku anatazama kwenye kundi dogo la watu, waliokuwa wanamtazama mwanamke mmoja aliekuwa amelewa sana, anabwabwaja maneno, ya kumwita mpenzi wake asimwache pale nje peke yake.
Radhia anatazama upande ule na kumwona dada yake Siwema, akiwa katika mwonekano usio pendeza kabisa, Radhia anajikuta anaingiwa na simanzi moyoni mwake, “ndio yeye masikini, sijuwi kwanini anakuwa vile, alafu mume wake yupo safarini” anasema Radhia kwa sauti ya kinyonge.
Hapo Edgar anawaza kwa sekunde kadhaa, “sikia Radhia ngoja tumsaidie aende nyumbani, itaaribu sifa ya mzee Makame, ambae sasa anakaribia kupata mafanikio” alisema Edgar bila kufafanua, huku anabofya remote ya gari aliyoishika mkononi mwake, na kumfungulia Radhia mlango, upande wa abiria wambele.
Radhia asemi kitu, sababu ajuwi Edgar anataka kufanya nini, japo akili yake ilimtuma kuwa, Edgar anataka akamchukuwe Siwema, aje apande kwenye lile gari, lakini aikuwa hivyo, maana alimwona Edgar anaelekea kwenye magari ya kukodi, na kuongea kitu na dereva wa taxi, kisha akampatia kiasi flani cha fedha, alafu yeye akarudi kwenye gari, wakati lile taxi, linasogea pale alipokuwepo Siwema.
Edgar anaingia kwenye gari, na kuiliwasha, kisha anatulia wakilitazama lile gari la kukodi, ambalo lilisimama karibu na pale alipo kuwepo Siwema, kisha wanamwona dereva wa taxi anamwita Siwema, ambae analifwata gari kwa haraka, kisha anaonekana akiongea na dereva wa Taxi, Siwema anaingia kwenye gari, na gari linaondoka.
Hapo Radhia anamtazama Edgar kwa macho ya kumtafakari, ni kama ajui amwambie nini, Edgar anagundua ilo, nae asemi kitu, zaidi ya kutabasamu, na Radhia nae anatabasamu, Edgar anaondoa gari taratibu, kimya kinatawara, Radhia anamwona Ashura akiwa na Shaban, wanatoka ukumbini, na kuifwata vesper yao.
Wao wanaendelea na safari yao, kimya kimya, kila mmoja anatafakari jambo, wakati Radhia ambae alikuwa anawaza juu ya upende na moyo wa kujari alionao kijana Edgar, akujuwa anacho waza Edgar, ambae alikuwa anawaza namna atakavyo vumilia pasipo kumgusa mwanamke huyu, ambae kiukweli amesha mvumilia sana, na uikichukulia leo alipomkumbatia kule vyooni, alikuwa na joto moja tamu sana.
Ukimya unaendelea, sasa Radhia anangoja kuona kama ni kweli wanaelekea nyumbani kwa Edgar, au alikuwa anamtania, Edgar nae anawaza kama ni kweli huyu mwanamke anaenda kwake, au alikuwa anatania.
Wanaendelea kuwaza kimya kimya, mpaka wanapo ikamata barabara ya kuelekea darajani, wanaivuka darajani, wanaikamata ile barabara ya kuelekea maisala, wakiacha mchepuko wa michenzani.
Hapo nikama Radhia anapata uhakika wa kuwa, anaenda kulala kwa Edgar, na Edgar nae anapata uhakika wa kuwa, Radhia anaenda kulala nyumbani kwake, “ilikuwa nzuri sana, siku nyingine nitaomba kwa baba yako unipeleke dar es salaam, kule naona matamasha yapo kila wakati” Edgar ndie alie vunja ukimya.
Radhia anatabasamu kidogo, “kule nasikia taharab aina matamasha makubwa, ila kuna wanamusic wa kawaida tu” alisema Radhia, kwa sauti yenye furaha ya wazi kabisa, ni wazi alipenda wazo ilo, maana alijuwa kwa umbali huo, lazima Edgar angeshawishika.
“kwani upendi aina anyingine ya music, mbona mimi leo nimefurahi sana” anasema Edgar, huku anakanyaga mafuta kuitafuta maisala, “napenda” alijibu Radhia huku anacheka cheka, kwa kile kicheko chake kitamu cha kitoto, sambamba na kijiaibu kwambali.*******
Naaaaam!, taxi linasimama nje ya nyumba moja mtaa wa Mombasa, nyumbani anayoishi Siwema, “dada tumesha fika” anasema dereva wa taxi, huku anamtazama Siwema, alie anza kusinzia.
Siwema anashtuka na kufungua mlango wa gari, kisha anashuka, “mimi sina ela, siulisema wamesha lipia?” anauliza Siwema, huku anatembea kwa yumba yumba akifwata mlango wa nyumba, lakini akuna anae jibu, zaidi anasikia ngurumo ya gari likiondoka.
Seiwema anaingia ndani ya nyumba ya chumba chake, ambacho ni chumba na sebule, anaweka vitu vyake mezani, “mjinga sana Radhia, amesababisha nimegombana na said” anasema Siwema, huku anajilaza kwenye kochi, ikiwa ni mala ya kwanza tunasikia jina la mpenzi wake.
“yani simwachi, kesho namfwata huko huko nyumbani, akanieleze kwanini aliwaacha wakina Mariam, au anaogopa yule mwanaume atawapenda sana wadogo zangu, na kumwacha yeye, mbona yeye mwenyewe aliolewa na mume wamtu, tena ana bahati ningemnyonyoa zile nywele zake anazo jivunia” anasema Siwema, huku anamaliza kwa msonyo mrefu.
Siwema anaanza kusinzia, lakini bado anamuwaza Radhia, “anajiona amepaaaaata, mwanaume mwenyewe siyo lolote, siyo chochote, kwanza mweusi” alijisemea Siwema, akisahau kuwa wanaume wake wote wawili, yani mume wake na huyu mchepuko wake wote ni weusi, tena huyu mchepuko ni mweusi kuliko ata Edgar.
Ukimya mfupi unafwatia, dakika mbili baadae simu yake inaanza kuita, lakini aonekani kuangaika nayo, jina kwenye kioo cha simu linaonyesha mpigaji ni Amina, Siwema apokei simu mpaka inaacha kuita, sasa kwambali tunaanza kusikia mkoromo, unao ashilia kuwa Siwema tayari alisha pitiwa na usingizi.*******
Naaaaaaaam! Saa tatu asubuhi, siku ya ijumaa, Radhia anafumbua macho yake taratibu, na kujikuta akiwa amelala kwa kuegemea kifua kipana cha kijana Edgar, huku licha ya kuwa walikuwa wamejifunika mashuka, lakini walikuwa uchi wa nyama, yani watupu kama wametoka kuzaliwa, huku nusu ya mwili wake ukiwa juu ya kijana huyu.
Radhia anainua uso wake kumtazama Edgar usoni, anamwona akiwa amelala fofo, anataka kujitoa pale kifuani kwa Edgar kwa kumpunguzia uzito kijana wa watu, lakini anaghairi, na kurudisha kichwa chake kifuani kwa Edgar, maana anahisi raha isyo kifani, sababu akuwai kulala hivi ata na mume wake wazamani.
Radhia akiwa kifuani kwa Edgar anatazama vizuri mle ndani ambako jana usiku akuweza kumtazama vizuri, anajiona yupo ndani ya chumba kimoja kipana sana, chenye vitu vichache muhimu, pasipo na makolo kolo yoyote.
Yani upande wa kulia kwake kulikuwa na TV kubwa, ya nchi alobaini na mbili, ambayo ilikuwa aijawashwa, meza mfano wa kabati, lenye kubeba seti ya music, ambayo sasa ilikuwa cheza muwimbo mzuri sana wa taratibu toka mwanamusic nguri wa music wa taratibu, wa nchini marekani, I will always love you, japo yeye akuwa mpenzi wa music huo, lakini alijikuta anaupenda ubembelezaji wa music ule. ......... ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPAHAPA Jamii Furoms