Abou Shaymaa
JF-Expert Member
- Oct 19, 2022
- 1,479
- 3,229
- Thread starter
- #161
ASALI HAITIWI KIDOLEyani hichi kigongo kila siku kinazidi kuwa kitamu ninaposoma sitamani hata iishe
SEHEMU YA HAMSINI NA NANE
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA SABA: “unaona sasa, nilijuwa tu mama mdogo lazima amtetee mwanae, yeye aangalii heshima ya familia yetu inaaribiwa, anachojari yeye ni hivyo vinguo anavyo nunuliwa Radhia na wanaume zake” alisema Siwema, kwa sauti ya juu ya kupayuka yenye hasira, “unamkosea mwenzieo Siwema, kwani yeye kuwa na mwanaume ni vibaya, lakini pia wewe ulisema unaenda huko, kuna mtu amekusema vibaya?” aliuliza mama Radhia kwa sauti ya upole na tulivu. ......... ENDELEA….
Hapo ni kama mama Radhia alikuwa ameuwasha moto upya, “ya Siwema yanakuhusu nini, yeye si anandoa yake, pia anakazi yake, zungumzia kuhusu huyo mjane wako” huyo alikuwa ni mama Mariam, na Siwema nae akadakia, “nilijuwa tu anaunga mkono umalaya wa mwanae” alisema Siwema, na Mariam akadakia, “kila siku anatoka wala amwulizi anaenda wapi, na leo amemwacha alale huko huko, kama siyo umalaya nini” analisema Mariam.
Ilimuuma sana mama Radhia, “dada wote ni wanawake, na tuna watoto wakike, ni muhimu kutunza maneno, ni bora kujambia makalioni, kuliko kujambia mdomoni” alisema mama Radhia, ambae kiukweli sasa ata sauti yake ilionekana wazi kuudhunishwa na kile kilichokuwa kinaendelea.
Lakini aikusaidia kitu, “mama mdogo lazima ukubari, Radhia anatia aibu familia, yani na ujane wake awezi kutulia nyumbani, kazi kiguu na njia, kwanini asikubari kuwa muda wake umeisha, akae nyumbani na ujane wake, aache kututia aibu, ata mume wake wa zamani Idd anamwonea huruma, kwa jinsi anavyo jipeleka kwa wanaume ” alisema Siwema kwa sauti ya juu yenye hasira.
Hapo mama Radhia akaona awezi kuvumulia, ni bora aingie ndani, hivyo akainuka tayari kwa kuondoka, “dada Siwema umezidi sasa, hivi nimekukosea nini lakini, mbona nilikuiwa vizuri na watu wenye heshima zao” ilisikika sauti toka upande wa kulia wa nyumba yao, ambako ndiko ueleko wa barabara ya kiembe samaki.
Wote wanageuka na kumwona Radhia alie valia nguo mpya kabisa, tena nigauni zuri la kupendeza, lililo mkaa vyema, pamoja na hijab yake mpya na vibanio vyakupendeza, kichwani kwake, katika hijab ile, huku nguo zote mpaka viatu vikiwa ni vya gharama, huku uso wake angavu ulio pendeza na kuonyesha rangi yake ya uchotara, ukionekana kuwa katika uzuni, na unyonge, mkono mwake akiwa ameshika mkoba wake, na pochi yake ndogo.
Kuonekana kwake, ni kama alianzisha upya ule ugomvi, “nimekukosea nini kwani we unaona nini, kwani unayoyafanya ni mazuri, au unataka nifurahie unavyo zurula na wanaume usiku huko mitaani, uoni kama unaiaibisha familia, nimekutana na Idd alikuona unaingia kwenye nyumba ya mwanaume gani sijuwi kule migombani” alisema Siwema, kwa sauti ya juu.
Mama Radhia anaghairi kuingia ndani, anamtazama Radhia, ambae leo anaonekana wazi akutaka mambo yawe mengi, “dada Siwema, idhani kama kuna aja ya kunitukana na kunisema vibaya, mwaka sasa nipo peke yangu kwani ni vibaya kuwa na mwanaume, ata kama anamalengo mazuri na mimi, unazani Idd atanitakia mema licha ya yote aliyonifanyia” alisema Radhia kwa sauti ya chini kama ilivyokuwa kwa mama yake.
Maneno yale yalipokelewa kwa mshtuko mkubwa sana, na kuibua hasira za wanandugu awa wa mama mmoja na mama yao, “nani awe na malengo na wewe mjane usie zaa” alisema Siwema, na hapo kikafwatia kicheko cha kebei toka kwa mama Mariam na mabinti zake.
Hapo nikama Siwema aliona amepatia, na kuamua kuongezea maneno, “kwa taarifa yako basi, watu wote wanajuwa kuwa wewe ni mjane, tena uliachika kwa ugumba, nani sasa akuchukue ukajeze choo chake, kama ulikuwa ujuwi mwenzio anakuchezea kisha anakuacha” ukweli imwingia vyema Radhia, akiamini kuwa pengine maneno ya dada yake licha ya kusabishwa na wivu, lakini niwazi yalikuwa na dalili ya ukweli.
Maana kwajinsi anavyo mfahamu Edgar, licha ya kufahamu mambo mengi juu ya familia yao, kama alivyo ongea sikuile akitaja mpaka umri wa baba yao elimu na idadi ya familia ya wazazi wa baba yake, pia kuhusu wao na wadogo zake, pamoja na ndugu zake wengine, lazima atakuwa anafahamu vyema tatizo lake la kutokushika mimba, na isitoshe ata yeye, alisha msimulia Edgar kuhusu tatizo lililo sababisha apewe taraka.
Kilicho muumiza Radhia siyo kwamba Edgar anaweza kuwa, hakuwa na mpango wa kuowana nae, ukweli ata yeye akutegemea hivyo, akutegemea kuolewa na mwaume mwenye uwezo mkubwa kama yule tena anaependwa na wanawake wengi, tena wenye hadhi ya juu.
Atayeye Radhia alipokuwa anakutana na Edgar alikuwa tayari kwalolote, ikiwa nakuburudika bila ndoa, maana kama engezamilia ndoa, basi asinge kubari jana kwenda kulala kwa kijana huyu, na kumpatia kitumbua chake.
Kilicho muuma ni kuanza kuhisi kuwa, Edgar ameamua kumchezea akiwa anajuwa yeye afai kuolewa, na kwamba anamchezea kama vitu vingine vinavyo chezewa na kuachwa, Radhia anaona macho yake yanajaa machozi, anafuta kwa mkono wake “unajifanya kulia nini, kwani ujuwi kuwa wewe ni mgumba, jana nakuambia ukajifanya kunishambulia, alafu unamwacha yule mwanamke awaambie wale mgambo wanitoe ukumbini, bila rafiki zangu ningeondokaje pale ukumbini” alisema Siwema.
Na hapo nikama wakina Mariam wakaikumbuka ile video, “lakini kama ujuwi hao rafiki zako walikuukimbia, Edgar ndie aliekukodia taxi” alisema Radhia, kwa sauti ya chini, yenye kupoa kwa uzuni na unyonge wa masimango.
Hapo Siwema anatulia kidogo kama vile anavuta kumbu kumbu, lakini akaishia kuangua kicheko cha dharau, nani alikuambia naitaji msaada wako, wakati ulinisababishia we mwenyewe” alisema Siwema kwa hasira, huku anamsogelea Radhia pale alipokuwa, kwa lengo la kumshambulia.
Lakini kabla ajamfikia, akasikia sauti toka kwenye malango wa kuingilia ndani, “Siwema, ni nani anae itia aibu familia yetu?” ilikuwa ni sauti yenye utulivu bandia ya mzee Makame, aliekuwa anatoka nje, akiwa ameongozana na Mukhsin, wote wanatazama mlangoni, wanamwona mzee Abeid Makame, ambae sasa alisimama mita chache toka mlangoni, usowake ukiwa umejawa na hali ya fadhaha, na unyonge wa hali ya juu.
Radhia anatamani kukimbia arudi alikotoka, maana sasa alijuwa kila kitu kinawekwa hadharani, na yanafwata masimango, na ikiwezekana kipigo, toka kwa baba yake, ambae mala zote uwa ataki ujinga, “ni huyu hapa Radhia, watu wanamwona anazurula na wanaume huko mtaani, na jana alikuwa kwenye taharab na mwanaume mmoja hivi, na mwanaume mwenyewe anamchezea tu, namjuwa vizuri awezi kumuowa” alisema Siwema, kwa kujinasib. ......... ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPA HAPA@Jamii forums