ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA MIA MOJA KUMI NA SITA
MTUNZI:
edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA TANO: “baba tutafanyaje ili arudi katika hali yake ya kawaida?” anauliza mama Radhia, “kwanza mna bahati mlimleta mapema, kabla ajagusa chakula cha jalalani, pia mnabahati mlimuwai kabla ajaingiliwa na mwanaume yoyote, katika hali hii ya wazimu, kuna vitu vinaitajika, ili akae sawa” alisema mzee Chongo. ........ ENDELEA….
Naaaaaam! maitajio ya mganga yalitajwa, kati ya maitajio ambayo yaliitajika, yalikuwa pamoja na kondoo, ambapo mgonjwa ilibidi anyweshwe damu yake, dawa za kiasiri zenye hasiri ya kiarabu, ambazo ilibidi zikanunuliwe kwenye maduka amayo yanauza dawa hizo.
Vitu hivyo ilibidi vipatikane mapema ili kukamilisha tiba ya Siwema, ambayo aikutakiwa ivuke siku ya leo, kwa kuwekea wepesi jambo ilo, walilazimika kutoa fedha ambazo zinge fanikisha kununua vitu hivyo, kiasi cha laki sita, nje ya million mmoja ambayo ilikuwa ya matibabu.
Kwamaana hiyo tsh million moja na laki sita, iliyo tolewa na Edgar, maana mzee Makame akutembea na fedha ya kutosha, zilikabidhiwa kwa mganga, ambae alimtuma msaidizi wake akanunue maitajio kwaajili ya kuanza matibabu makubwa ya kumtoa uchizi Siwema.********
Saa mbili usiku kwa saa za afrika mashariki, ndio mida ambayo Shaban na Ashura wakiwa na mtoto wao Ashraf, waliondoka magomen kwa Aziza, yani dada wa Ashura, wakitumia gari dogo la kukodi, yani taxi.
Wakielekea nyumbani kwa Shaban, huku njiani wakifurahia uwepo wao pamoja, na mtoto wao mdogo, “inabidi tuwachukuwe ndugu zake toka kwa bibi yao, maana baada ya taraka tutaenda kupumzika dar kidogo” alisema Shaban na kumfanya Ashura atabasamu kidogo, “hakika natamani iwe ata leo, maana nimetamani kukaa na wanangu wote” alisema Ashura, akionekana mwenye furaha kupita kiasi.
Kumbe basi, wakati gari linaondoka kwa azazi, ambae mume wake alikuwa ameenda kwenye shuguri za uvuvi, dakika tano baadae Idd nae anasimamisha baskeri mbele ya nyumba ya Aziza, huku amejijaza hasira, akipania kutandika Ashura, kama itawezekana, ni kwakujiweka karibu na Shaban.
Idd anabisha hodi, na bahatii ilivyo nzuri kwake, hodi yake ilisikika kwa watu walipo ndani, “karibu” alijibu Aziza toka ndani, kwa sauti iliyo changamka kwa furaha, huku vishindo vyepesi vikisikika vikifwata mlango, na sekunde chache mlango ukafunguliwa, na Aziza akaibuka akiwa ajawa na tabasamu, ambalo liliyeyuka sekunde chache baadae, baada ya kuonana uso kwa uso na kugundua kuwa, mgeni mwenyewe ni Idd, ambae alikuwa amekunja uso kwa hasira.
“asalam aleykum” anasalimia Aziza, kwa sauti iliyopoa, “aleykum salam” aliitikia Idd, ambae alikuwa anamtazama Aziza aliekuwa amesimama katikati ya mlango, alio ufungua nusu, “naaaam!, nakusikiliza” alisema Aziza, kama vile anaongea na mtu ambae licha ya kumfahamu, lakini hakuwa na umuhimu kwake, wala kwa familia yake.
“inamaana utanisikilizia hapa mlangoni?” aliuliza Idd kwa mshangao, huku sura yake ikibadirika toka kwenye hasira kuanza kuja kwenye mshangao wawazi kabisa, “shemeji hii mida siyo ya kuja kutembelea watu, si unajuwa nililala hospital kwa siku tatu, leo nataka kulala mapema” anasema Aziza, kwa sauti yenye msisitizo, isiyo na chembe ata moja ya utani.
Idd anaachia kicheko kifupi cha uchungu, “shemeji bwana, aya basi kama umeshindwa kunikaribisha basi niitie Ashura na maongezi nae” alisema Idd, akionekana wazi kuzuwia hasira.
Sasa ilifwata zamu ya Aziza kuachia kicheko cha uzuni, “nani kakuambia mkeo yupo hapa?” aliuliza Aziza kwa sauti kavu, isiyo na utani ata kidogo, Idd anahisi kuwa ni utani, au Aziza amejibu uongo sababu ya hasira, “shemeji bwana, sasa kama hayupo hapa atakuwa wapi?” aliuliza Idd huku anajilazimisha kucheka.
“kama wewe ujuwi alipo mkeo mimi nitajuwaje, yani mkeo toka juzi ajifungue umeenda hospital mala moja, leo unakuja kuniuliza alipo mkeo” alisema Aziza kwa sauti ya kusimanga.
Idd anajichekesha kidogo, “shemeji bwana, siunajuwa tunaangaika kutafuta fedha ili wale” alijibu Idd, huku anaendelea kujichekesha, “eti kutafuta fedha, unazani tujuwi jinsi ulivyochanganyikiwa baada ya kusikia Radhia amempata mwanaume barozi?” anauliza Aziza kwa sauti ya kusuta, huku anamtazama Idd, ambae alitoa macho kwa mshangao, akikosa jibu la swali lile la Aziza.
“najuwa uwezi kunijibu, nenda kwako, mimi naitaji kupumzika sasa” alisema Aziza ambae anafahamu hadithi nzima ya Idd kufanya fitina ya kumchukuwa Ashura toka kwa Idd, “shemejinaomba uniambie mke wangu yupo wapi….” alisema Idd, ambae akupewa nafasi ya kumaliza kauri yake.
“eti mkeo, wakati ujuwi sasa hivi yupo wapi na anakula nini” alisema Aziza, kabla ajaingia ndani na kufunga mlango, akimwacha Idd amesimama mlangoni anashangaa, pasipo kuamini anacho kiona au kusikia.
Idd anasimama pale mlangoni kwa sekunde kadhaa, huku anawaza la kufanya, hasira imeshika, anatamani kama Ashura angekuwepo mbele yake amzabe makofi kadhaa, maana anawaza kuwa pengine Ashura yupo kwa Shaban, “au yupo mle ndani ameagiza nisikaribishwe” anawaza Idd, huku anachukuwa baskeri yake na kuanza kuondoka zake taratibu.
“atapoa tu, nikimpgia baadae nitamtuliza” anajismea Idd, ambae anajipa moyo kuwa Ashura atakuwa ndani ya nyumbani ile ya Aziza, ila tu amechukia sababu akuwenda kumwona hospital toka juzi.
“nikifika nyumbani nita mpigia simu, na tutaongea vizuri tu” anajisemea Idd, ambae pia anakumbuka jambo jingine, “hivi huyu mshenzi amejuwaje kama mfukuzia Radhia” anawaza Idd, ambae sasa amesha panda baskeri ananyonga penda kwa miguu kuelekea michenzani.
“kwahiyo Aziza anazani nita mwacha Radhia, kwani yeye ajuwi Radhia ni mali yangu, kwanza ni mzuri kuliko huyo Ashura wake” anajisemea Idd, ambae anazidi kutokomea upande wa mjini.********
Naaaaaam!, saa tatu na nusu za usiku, nyumbani kwa mzee Makame, ambae sasa naitwa mheshimiwa, wanaonekana wanafamilia wote wakiwa sebuleni, kuanzia wakina mzee Makame mwenyewe, wake zake, Edgar na Radhia na Edgar, mpaka wakina Mariam, Zuhura na Mukhsin, bila kuwasahau wakina Zahara na watoto wa kaka yao pamoja na Khadija mtoto wa Siwema alie pakatwa na Edgar, alie mzowea kupita kiasi, kutokana na kumletea zawadi kila mala anapofika.
Hao wote walikuwa wanamtazama Siwema, aliekuwa amekaa kwenye kochi la peke yake, muda wote amejiinamia chini analia kilio cha chini chini, akisaidiwa na mama yake mzazi, ambae hapo mwanzo aliwashutumu wakina Radhia na mama yake, kuwa wamemfanya ulozi, binti yake.
“Siwema, unaweza kutueleza mbele ya wadogo zako, shemeji yako, na mama zako, kikubwa alicho kukosea Radhia, mpaka ukaamua kujibebea jukumu la kwenda kumfanyia ushirikina mwenzio?” aliuliza mzee Makame, ambae kiukweli, alikuwa katika hali ambayo, mala ya mwisho ni miaka mingi sana kuwa hivi.
Ukumbi ulikuwa kimya, kila mmoja akisubiri maelezo ya Siwema, ambayo pengine yange shusha hasira ya mzee Makame, ambae alikuwa amejawa na hasira kali, zilizoonekana wazi wazi.
Siwema ajibu kitu, anaendelea kulia, huku kichwa amekiinamisha chini, “Siwema naongea na wewe, ni kosa gani amekufanyia Siwema, kiasi cha kushindwa kumsamehe na kuamua kwenda kwa mganga kuloga ili awe kichaa, na kuachana na mume wake?” anauliza mzee Makame, ambae licha ya kuwa na hasira kiasi alichokuwa nacho, lakini ni wazi asingeweza kummwadhibu kwa kumchapa binti yake huyu mkubwa.
“baba Siwema, uwezi kuona mtoto bado ajakaa sawa, ungemwacha kwanza uongee nae kesho…..” alisema Siwema, ambae pia alikuwa anatokwa na machozi muda wote, lakini akufanikiwa kumalizia kuongea, maana mzee Makame, alimdaka juu juu, “na wewe usiongee kitu, zaidi kuniambia ninani anastahili kupewa taraka, kati yako wewe na mama Radhia” alisema mzee Makame, kwa sauti kali yenye hasira, huku anamtazama mke wake mkubwa kwa macho makali. ........ ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPA HAPA
jamii forums