SIMULIZI: Asali haitiwi kidole

SIMULIZI: Asali haitiwi kidole

Waungwana Hebu Tushauriane Kidogo Kabla Ya Kuendelea,
Mkasa Unaofuta (Simulizi Ijayo)
Tuendelee Kubakia Zanzibar au Turudi Dar Es Salaam?

Maoni Yenu Yanatakiwa Maana Zote Ni Nondo Nashindwa Nianze Na Ipi ,Kwasababu Radhia Tuna Malizana Nae Leo Baada Ya Kwenda Mbogo Land Kuoga Dhahabu.
Mkuu tubaki hapa hapa zanzibar mimi nimepapenda sana nina mpango kumioa siwema Mungu akipenda
 
Abou Shaymaa
Weka vitu mkuu mimi nimeshachukua likizo yaani nasubiri mwendelezo tu labda kama upo kazini

Ila ukileta mpya leta Ya mizagamuano kama hii tu ngumi hapana kwa kweli
 
Waungwana Hebu Tushauriane Kidogo Kabla Ya Kuendelea,
Mkasa Unaofuta (Simulizi Ijayo)
Tuendelee Kubakia Zanzibar au Turudi Dar Es Salaam?

Maoni Yenu Yanatakiwa Maana Zote Ni Nondo Nashindwa Nianze Na Ipi ,Kwasababu Radhia Tuna Malizana Nae Leo Baada Ya Kwenda Mbogo Land Kuoga Dhahabu.
embu kwanza tujue majina ya hizo zinazofata maana kwa upande wangu kupitia jina la simulizi ndo nitaweza kuchagua
 
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA MIA MOJA KUMI NA SITA
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA TANO: “baba tutafanyaje ili arudi katika hali yake ya kawaida?” anauliza mama Radhia, “kwanza mna bahati mlimleta mapema, kabla ajagusa chakula cha jalalani, pia mnabahati mlimuwai kabla ajaingiliwa na mwanaume yoyote, katika hali hii ya wazimu, kuna vitu vinaitajika, ili akae sawa” alisema mzee Chongo. ........ ENDELEA….


Naaaaaam! maitajio ya mganga yalitajwa, kati ya maitajio ambayo yaliitajika, yalikuwa pamoja na kondoo, ambapo mgonjwa ilibidi anyweshwe damu yake, dawa za kiasiri zenye hasiri ya kiarabu, ambazo ilibidi zikanunuliwe kwenye maduka amayo yanauza dawa hizo.


Vitu hivyo ilibidi vipatikane mapema ili kukamilisha tiba ya Siwema, ambayo aikutakiwa ivuke siku ya leo, kwa kuwekea wepesi jambo ilo, walilazimika kutoa fedha ambazo zinge fanikisha kununua vitu hivyo, kiasi cha laki sita, nje ya million mmoja ambayo ilikuwa ya matibabu.


Kwamaana hiyo tsh million moja na laki sita, iliyo tolewa na Edgar, maana mzee Makame akutembea na fedha ya kutosha, zilikabidhiwa kwa mganga, ambae alimtuma msaidizi wake akanunue maitajio kwaajili ya kuanza matibabu makubwa ya kumtoa uchizi Siwema.********


Saa mbili usiku kwa saa za afrika mashariki, ndio mida ambayo Shaban na Ashura wakiwa na mtoto wao Ashraf, waliondoka magomen kwa Aziza, yani dada wa Ashura, wakitumia gari dogo la kukodi, yani taxi.


Wakielekea nyumbani kwa Shaban, huku njiani wakifurahia uwepo wao pamoja, na mtoto wao mdogo, “inabidi tuwachukuwe ndugu zake toka kwa bibi yao, maana baada ya taraka tutaenda kupumzika dar kidogo” alisema Shaban na kumfanya Ashura atabasamu kidogo, “hakika natamani iwe ata leo, maana nimetamani kukaa na wanangu wote” alisema Ashura, akionekana mwenye furaha kupita kiasi.


Kumbe basi, wakati gari linaondoka kwa azazi, ambae mume wake alikuwa ameenda kwenye shuguri za uvuvi, dakika tano baadae Idd nae anasimamisha baskeri mbele ya nyumba ya Aziza, huku amejijaza hasira, akipania kutandika Ashura, kama itawezekana, ni kwakujiweka karibu na Shaban.


Idd anabisha hodi, na bahatii ilivyo nzuri kwake, hodi yake ilisikika kwa watu walipo ndani, “karibu” alijibu Aziza toka ndani, kwa sauti iliyo changamka kwa furaha, huku vishindo vyepesi vikisikika vikifwata mlango, na sekunde chache mlango ukafunguliwa, na Aziza akaibuka akiwa ajawa na tabasamu, ambalo liliyeyuka sekunde chache baadae, baada ya kuonana uso kwa uso na kugundua kuwa, mgeni mwenyewe ni Idd, ambae alikuwa amekunja uso kwa hasira.


“asalam aleykum” anasalimia Aziza, kwa sauti iliyopoa, “aleykum salam” aliitikia Idd, ambae alikuwa anamtazama Aziza aliekuwa amesimama katikati ya mlango, alio ufungua nusu, “naaaam!, nakusikiliza” alisema Aziza, kama vile anaongea na mtu ambae licha ya kumfahamu, lakini hakuwa na umuhimu kwake, wala kwa familia yake.


“inamaana utanisikilizia hapa mlangoni?” aliuliza Idd kwa mshangao, huku sura yake ikibadirika toka kwenye hasira kuanza kuja kwenye mshangao wawazi kabisa, “shemeji hii mida siyo ya kuja kutembelea watu, si unajuwa nililala hospital kwa siku tatu, leo nataka kulala mapema” anasema Aziza, kwa sauti yenye msisitizo, isiyo na chembe ata moja ya utani.


Idd anaachia kicheko kifupi cha uchungu, “shemeji bwana, aya basi kama umeshindwa kunikaribisha basi niitie Ashura na maongezi nae” alisema Idd, akionekana wazi kuzuwia hasira.


Sasa ilifwata zamu ya Aziza kuachia kicheko cha uzuni, “nani kakuambia mkeo yupo hapa?” aliuliza Aziza kwa sauti kavu, isiyo na utani ata kidogo, Idd anahisi kuwa ni utani, au Aziza amejibu uongo sababu ya hasira, “shemeji bwana, sasa kama hayupo hapa atakuwa wapi?” aliuliza Idd huku anajilazimisha kucheka.


“kama wewe ujuwi alipo mkeo mimi nitajuwaje, yani mkeo toka juzi ajifungue umeenda hospital mala moja, leo unakuja kuniuliza alipo mkeo” alisema Aziza kwa sauti ya kusimanga.


Idd anajichekesha kidogo, “shemeji bwana, siunajuwa tunaangaika kutafuta fedha ili wale” alijibu Idd, huku anaendelea kujichekesha, “eti kutafuta fedha, unazani tujuwi jinsi ulivyochanganyikiwa baada ya kusikia Radhia amempata mwanaume barozi?” anauliza Aziza kwa sauti ya kusuta, huku anamtazama Idd, ambae alitoa macho kwa mshangao, akikosa jibu la swali lile la Aziza.


“najuwa uwezi kunijibu, nenda kwako, mimi naitaji kupumzika sasa” alisema Aziza ambae anafahamu hadithi nzima ya Idd kufanya fitina ya kumchukuwa Ashura toka kwa Idd, “shemejinaomba uniambie mke wangu yupo wapi….” alisema Idd, ambae akupewa nafasi ya kumaliza kauri yake.


“eti mkeo, wakati ujuwi sasa hivi yupo wapi na anakula nini” alisema Aziza, kabla ajaingia ndani na kufunga mlango, akimwacha Idd amesimama mlangoni anashangaa, pasipo kuamini anacho kiona au kusikia.


Idd anasimama pale mlangoni kwa sekunde kadhaa, huku anawaza la kufanya, hasira imeshika, anatamani kama Ashura angekuwepo mbele yake amzabe makofi kadhaa, maana anawaza kuwa pengine Ashura yupo kwa Shaban, “au yupo mle ndani ameagiza nisikaribishwe” anawaza Idd, huku anachukuwa baskeri yake na kuanza kuondoka zake taratibu.


“atapoa tu, nikimpgia baadae nitamtuliza” anajismea Idd, ambae anajipa moyo kuwa Ashura atakuwa ndani ya nyumbani ile ya Aziza, ila tu amechukia sababu akuwenda kumwona hospital toka juzi.


“nikifika nyumbani nita mpigia simu, na tutaongea vizuri tu” anajisemea Idd, ambae pia anakumbuka jambo jingine, “hivi huyu mshenzi amejuwaje kama mfukuzia Radhia” anawaza Idd, ambae sasa amesha panda baskeri ananyonga penda kwa miguu kuelekea michenzani.


“kwahiyo Aziza anazani nita mwacha Radhia, kwani yeye ajuwi Radhia ni mali yangu, kwanza ni mzuri kuliko huyo Ashura wake” anajisemea Idd, ambae anazidi kutokomea upande wa mjini.********


Naaaaaam!, saa tatu na nusu za usiku, nyumbani kwa mzee Makame, ambae sasa naitwa mheshimiwa, wanaonekana wanafamilia wote wakiwa sebuleni, kuanzia wakina mzee Makame mwenyewe, wake zake, Edgar na Radhia na Edgar, mpaka wakina Mariam, Zuhura na Mukhsin, bila kuwasahau wakina Zahara na watoto wa kaka yao pamoja na Khadija mtoto wa Siwema alie pakatwa na Edgar, alie mzowea kupita kiasi, kutokana na kumletea zawadi kila mala anapofika.


Hao wote walikuwa wanamtazama Siwema, aliekuwa amekaa kwenye kochi la peke yake, muda wote amejiinamia chini analia kilio cha chini chini, akisaidiwa na mama yake mzazi, ambae hapo mwanzo aliwashutumu wakina Radhia na mama yake, kuwa wamemfanya ulozi, binti yake.


“Siwema, unaweza kutueleza mbele ya wadogo zako, shemeji yako, na mama zako, kikubwa alicho kukosea Radhia, mpaka ukaamua kujibebea jukumu la kwenda kumfanyia ushirikina mwenzio?” aliuliza mzee Makame, ambae kiukweli, alikuwa katika hali ambayo, mala ya mwisho ni miaka mingi sana kuwa hivi.


Ukumbi ulikuwa kimya, kila mmoja akisubiri maelezo ya Siwema, ambayo pengine yange shusha hasira ya mzee Makame, ambae alikuwa amejawa na hasira kali, zilizoonekana wazi wazi.


Siwema ajibu kitu, anaendelea kulia, huku kichwa amekiinamisha chini, “Siwema naongea na wewe, ni kosa gani amekufanyia Siwema, kiasi cha kushindwa kumsamehe na kuamua kwenda kwa mganga kuloga ili awe kichaa, na kuachana na mume wake?” anauliza mzee Makame, ambae licha ya kuwa na hasira kiasi alichokuwa nacho, lakini ni wazi asingeweza kummwadhibu kwa kumchapa binti yake huyu mkubwa.


“baba Siwema, uwezi kuona mtoto bado ajakaa sawa, ungemwacha kwanza uongee nae kesho…..” alisema Siwema, ambae pia alikuwa anatokwa na machozi muda wote, lakini akufanikiwa kumalizia kuongea, maana mzee Makame, alimdaka juu juu, “na wewe usiongee kitu, zaidi kuniambia ninani anastahili kupewa taraka, kati yako wewe na mama Radhia” alisema mzee Makame, kwa sauti kali yenye hasira, huku anamtazama mke wake mkubwa kwa macho makali. ........ ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPA HAPA jamii forums
 
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA MIA MOJA KUMI NA SABA
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA KUMI NA SITA: “baba Siwema, uwezi kuona mtoto bado ajakaa sawa, ungemwacha kwanza uongee nae kesho…..” alisema Siwema, ambae pia alikuwa anatokwa na machozi muda wote, lakini akufanikiwa kumalizia kuongea, maana mzee Makame, alimdaka juu juu, “na wewe usiongee kitu, zaidi kuniambia ninani anastahili kupewa taraka, kati yako wewe na mama Radhia” alisema mzee Makame, kwa sauti kali yenye hasira, huku anamtazama mke wake mkubwa kwa macho makali. ........ ENDELEA….


Kila mmoja anashtuka mle ndani, siyo watoto wakina Mariam au wajukuu, ambao awakujuwa ata maana ya taraka, Siwema pia alishtuka vibaya sana, kwakuona wivu wake wakijinga, siyo tu umemletea aibu kubwa, ila pia umemwingiza mama yake kwenye mtego wa kuachika.


Lakini pia wote mle ndani, akiwepo edgara na Radhia, mshtuko wao hauku mzidi mama Siwema, ambae anashtuka kwa nguvu, kwa kujuwa kuwa anaenda kuachika kutokana na maneno yake mabaya, na shutuma mbaya alizo zitoa kwa mke mwenzie na binti yake, mama Radhia anaongeza kilio, na kuanza kulia wazi wazi, huku anapaga magoti mbele ya mume wake,


“mume wangu naomba unisamehe, zile zilikuwa ni hasira tu, wala sikudhamilia kuwa naitaji taraka, usifanye hivyo mume wangu, tumetoka mbali na sasa tuna wajukuu” alipiga kelele mama Siwema, huku anaendelea kuangua kilio, watu wote waliganda kama masanamu, kwa kuona sasa mzee Makame anamwacha mke wake, maana akuonyesha dalili ya utani.


Lakini mama Radhia alikuwa tofauti kidogo, “baba Radhia, taraka aitajwi wakati wa hasira, ni vyema tuka likaweka sawa jambo ili, na turejeshe amani yetu” alisema mama Radhia, yani mke mdogo wa mzee Makame, huku anamtazama mume wake, na mkono wa kushoto ameulaza kwenye bega la kulia la mume wake.


“ni upuuzi, kila siku tuna fumbia macho kwa kujuwa ni mambo ya watoto tu, sasa mtu amekuwa mama, bado anaendeleza chuki kwa mwenzie, amemsaidia kurudi kazini, malipo yake anaenda kuloga kwa washirikina, alafu unaniambia tumwache mtoto akae mpaka kesho, ili iweje sasa, nilitegemea ungeomba radhi kwa maneno yako pale tu tuliposhuka kwenye gari, lakini umekaa kimya unajiliza kinafiki” alisema mzee Makame, kwa sauti ambayo sasa ilianza kupoa.


“nisamehe mume wangu, sirudii tena makumba baba” aliendelea kuombeleza mama Siwema, huku Siwema nae akizidisha kilio kwa kuona yale aliyo msababishia mama yake, kutokana na wivu usio na kichwa wala miguu, mama Siwema alitia huruma kwa jinsi alivyokuwa anaonekana wakati ule.


Mama Radhia ainuka toka kwenye kochi alilokaa na mume wake, “dada hauto ondoka, siwezi kukuacha uondoke, tutakuwa kuwa pamoja, na kama akikuacha ata tuacha wote wawili” alisema mama Radhia, huku anamshika mkono mama Siwema yani mke mwenzie na kumwinua toka pale chini.


Mzee Makame anashindwa kuongea lolote kwa mama Radhia, ambae sasa anaenda kukaa pembeni ya mama Radhia upande wakushoto, huku upande wakulia akiwepo mzee Makame.


Mzee Makame anamtazama Siwema aliekuwa bado analia, “aya tuleze nini alichokufanyia mwenzio kiasi cha kutaka kumfanyia hayo yote” alisema mzee Makame, huku anamtazama Siwema, ambae bado alikuwa amejiinamia analia kwa uchungu.


Ukweli Siwema akiwa anajihisi aibu na maumivu moyoni mwake, anainua macho yake na kumtazama Radhia, alie kaa karibu na Edgar, alie mshika binti yake khadija, ambae alionekana kuwa na amani mikononi mwa baba yake mdogo huyu.


Maumivu yanazidi, Siwema anajiona wazi jinsi alivyo mkosefu, “Radhia naomba unisamehe, lilikuwa ni wazo la Idd” alisema Siwema, kwa sauti iliyoambatana na kilio.


Ukiachilia watoto watatu wadogo kabisa, hakuna mwingine ambae akushangaa maneno ya Siwema, asa alipo mtaja Idd, “Idd huyu huyu wa kiparago?” anauliza Radhia kwa mshangao, huku anamtazama dada yake Siwema, ambae anaaanza kwa kuitikiwa kwa kichwa.


“alisema ataki kukuona unaolewa na mwanaume mwingine, pia alisema ulifanya makusudi usishike ujauzito wake, lakini mganga amesema kuwa Idd bado ajabahatika kupata mtoto, kwa wake zake wote alio wai kuishi nao” alisema Siwema, ambae kila sekunde alikuwa anapunguza kilio, na sasa alikuwa analia kilio cha kwikwi.


Wenye umri mkubwa, na wanao tambua mambo wanatazamana kwa mshangao, kama wanaulizana inawezekana vipi, “kivpi wakati Ashura amezaa nae watoto wawili?” anauliza Radhia, kwa sauti ya mshangao, “ata mimi sijuwi, lakini mganga alimwambia hivyo” alijibu Siwema, ambae muda wote alikuwa ameinamisha kichwa chini.


Radhia anakumbuka tukio la kumwona Ashura akiwa na mwanaume mwingine nyakati za usiku, tena akiwa mjamzito, kitendo ambacho kwa maume anachepuka na mume mke wamtu, ni mala chache sana kuchepuka na mwenye ujauzito mkubwa kama ule.


“kwahiyo Ashura amezaa na mwanaume wake wa zamani” Radhia alijikuta anasema hivyo, bila ata kutarajia, na kuzidi kuwashangaza watu wote walio kuwepo pale sebuleni, “kwanini unasema hivyo Siwema?” aliuliza mama Radhia kwa sauti ya kuto kuamini.


“mdiyo mama, nilimwona siku ile usiku kwenye taharab, alikuwa na Shaban, tena alikuwa na ujauzito mkubwa” alisema Radhia, akionyesha kuwa na uhakika wa hali ya juu.


Hapo moja kwa moja, kwa wale watu wazima, wakapeleka mawazo yao kuwa, Idd alikuwa na tatizo la uzazi, na pengine ndio sababu ya kushindwa kumpatia Radhia ujauzito, nakukimbilia kumwacha, pasipo kujitazama yeye mwenyewe kwanza.


“hayo mengine hayatuhusu, ebu tuachane nayo” alisema mzee Makame na kumtazama Siwema, “kwahiyo uliamua kushirikiana na huyo mpuuzi kumzuru mdogo wako?” aliuliza mzee Makame, huku anamtazama Siwema, aliekuwa amejiinamia kichwa chini, “baba naomba unisamehe, ni ibirisi alinipitia, na apa sito rudia tena” alisema Siwema huku akianza kulia tena, kilio cha kwikwi.


“hii tabia imeanza zamani sana, na nilisha mwambia mama yenu awakataze, lakini ndio kwanza akawachochea” alisema mzee Makame kwa sauti yenye hasira, huku anamtazama mama Siwema, “hapana mume wangu, niliwaambia waache, siunawaona wakina Mariam wameacha” alisema mama Siwema, kwa sauti yenye kumbeleza.


Hapo kikapita kimya kifupi, kabla mzee Makame ajavunja ukimya, “Radhia, unasemaje kuhusu ili?” aliuliza mzee Makame, huku anamtazama Radhia aliekaa na mume wake, alie mshika mtoto Khadija.


Kwanza Radhia anamtazama Edgar, Edgar anampa ishala ya kukubari kwa kichwa, kisha Radhia anamtazama mama yake, ambae anafanya hivyo hivyo, mwisho Radhia anamtazama Siwema, ambae alikuwa ameinamisha kichwa chini, “yeye ni dada yangu, siwezi kuvunja undugu sababu tumeunganishwa na damu moja” alisema Radhia, ambae nikama alikuwa analengwa na machozi.


Radhia anaweka kituo kidogo cha kufuta machozi kabla ya kuendelea, “siwezi kuacha kumsemehe dada yangu, na wala sijawai kufikilia kumfanyia ubaya, kama kuna kitu nimemkosea naomba anisamehe, na kama nikimkosea naomba aniambie ili nijirekebishe, ila naomba ahache kuni chukia” alisema Radhia, ambae sasa alikuwa anakaribia kulia kwa kwikwi.


Radhia alishindwa kuendelea kuongea, kutokana na kilio cha kwikwi, Edgar anatoa kitambaa chake mfukoni, na kumpatia mke wake, ambae anakitumia kujifutia machozi, “baba nazani na wewe umeona kilicho tokea, sijuwi unasemaje juu ya ili” alisema mzee Makame akimtazama Edgar, ambae muda wote alikuwa anasikiliza. ........ ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPA HAPA jamii forums
 
Wekaaaaaaa maandishi kaka tuenjoy Pancho keshanunuaaaa suti ya kwenda nayo mbogo land kuhudhuliaaaa harusi ya barozi Edgar na bibl radhiaaaaaa
Mkuu hapa nanyoosha suti yangu tayari kwenda kushuhudia
Tangu juzi sili ili nikienda huko kazi yangu kula tu kitimoto na bia za kutosha .

Ila ningependa kwenda na siwema nikamgegede huko huko
 
Back
Top Bottom