Curtain_mastertz
Member
- Jun 16, 2013
- 25
- 19
Shusha mzigo kaka
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakika ilikuaaaa safari njemaaa na hadithi ilikuaaaa mzuri sanaaaa....tunasubiri kigongo kipyaaa usisahau kututag nasi hatutokuangushaaaaaaASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA MIA MOJA ISHIRINI NA SITA
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA ISHIRINI NA TANO: Mshenga akuishia hapo, “japo Radhia nae alimkosea Idd, lakini Idd ndie mkosefu zaidi, amewakosea wazazi wake, amemkosea wakwe zake, pia amemkosea mke wake, amenikosea na kama mshenga” kila mmoja alikuwa kimya anatafakari maneno ya mshenga. ........ ENDELEA….
“kama kunapingamizi juu ya ilo, naomba mstuite hapa, twendeni msikitini maana hapo ndio sehemu sahihi ya kuliweka sawa, chamsingi naomba busara zitumike binti wawatu asiendelee kuwa katika kifungo hiki cha ndoa, na kuendelea kuzini nje ya ndoa” alisema mshenga, akimaliza kuongea la kwake.
Ilimuuma sana Idd, ambae kiukweli ni kama alikuwa amezinduka toka usingizini, maana kila kilichoongelewa pale ni ukweli mtupu, japo mwanzo alijiona yupo sahihi, sababu akuwai kumsikia mke wake Ashura au Radhia, wakilalamika kuhusu tendo la ndoa, baada yake, alimwona Shani kuwa ni mwanamke asie na aibu, kwa kudai haki yake ya kitandani.
Idd sasa ndio aligundua kuwa hakumtendea haki Radhia, kwa kumfukuza nyumbani kwake akipatia taraka kwa masimango ya hali ya juu, na kwamba ilibidi ajuwe udhaifu wake mapema ili aweze kupata tiba, na pengine kupata watoto wake mwenyewe, maana ata Radhia tayari sasa alikuwa anaujauzito.
Idd ambae sasa alikuwa na kitu cha kumweleza Radhia, ilikumwomba msamaha, huku akijuwa fika isingine wezekana, kutokana na kile alicho kiona usiku huu waleo, ukiachilia kumwona Radhia akiwa amekasirika, ila pia ndie alie mbomoa teke la mdomo.
Idd akawa tazama watu waliopo mle ndani kwa hawamu, kabla ya kuanza kuongea, “kwanza niwaombe radhi wote mliopo hapa, pili naomba mfahamu kuwa, sikuwai kujuwa kama nina tatizo lolote kiafya, nilijiona nipo sawa, ata hali ya kuto kuweza kushiriki tendo, niliona ni kawaida tu” alisema Idd, kwa sauti ya upole yenye majuto ya wazi kabisa.
Watu wote walitega masikio yao wakimsikiliza kijana huyu, aliewai kuowa wanawake watatu, “hakika mke wangu angenieleza kama ninautofauti na wanaume wengine, nazani nisingefikia hapa, japo ingekuwa vigumu kuelewa” alieleza Idd, ambae alionekana tofauti kidogo.
“nakubari kumpa taraka mke wangu, na sito owa tena mpaka nipate tiba ya tatizo nililonalo” alisema Idd kabla ya kuanza kuandika taraka na kumpatia mke wake mbele ya mshenga na wazazi wao.*********
Miezi mitatu baadae, ikiwa tayari Radhia amesha rudi toka nchini #Mbogo_Land, ambako alitambulishwa kwa wazazi wa Edgar, pamoja na ndugu na jamaa na marafiki.
Radhia alikutana na wifi yake, yani Dorin, dada wa Edgar, pia alikutana na Deus, pamoja na mke wake Doctor Monica, wote walimpokea Radhia wakimkaribisha majumbani mwao, mialiko iliyo ambatana na afla kubwa zenye waalikwa wengi, wakiwepo viongozi na watu maarufu.
Katika matukio makubwa yaliyo mpendeza Radhia, nikupakwa unga wa dhahabu, wakati anaingia nyumbani kwa wakwe zake, hakika ni matukio mengi yaliyo chukuliwa na kutunzwa katika video na picha nyingi sana, zilizowekwa mtandaoni, na kutazama mwa na watu wengi sana.
Baada ya kurudi kisiwani unguja, akiwa mwenye furaha isiyo na kifani chake, barua ya posa ililetwa nyumbani kwa kina Radhia, na ndoa ya kwanza ikapita, ikifanyika kwenye viwanja vya ikulu kama ilivyo aidiwa, na kuuzuriwa na viongozi pamoja na watu maarufu sana.
Sasa ikiwa ni miezi mitatu mbele, palikuwa natukio kubwa la harusi iliyo sherehekewa baada ya ndoa ya kimila, iliyofungwa nchini Mbogo land, harusi ambayo baadhi ya matukio yake yalirushwa moja moja, katika vituo sabini na mbili, ndani ya nchi kumi za afrika.
Tanzania ni ni mmoja ya nchi ambazo tukio la sherehe za harusi ya kimila ya Edgar na Radhia, ilirushwa moja kwa moja na vituo viwili vya television, na kutazamwa na watu wengi sana.
Kisiwani unguja, watu walisimamisha shuguri zao, kama walivyo onekana majumbani, au madukani huko mitaani na katikati ya mji, wakishuhudia sherehe kubwa ya harusi, iliyokutanisha viongozi wengi sana.
Mmoja kati ya watu walio ishuhudia sherehe hiyo ni kijana Idd, ambae kiukweli alikuwa amekaa kiunyonge sana sebuleni kwake, anatazama TV, huku macho yake yanalengwa na machozi, anapo mtazama Radhia ambae sasa usingezania kuwa ndie yule aliekuwa anatembea kwa mguu toka jang’ombe mpaka forodhani, maana alikuwa mwarabu kabisaaaa.************
Kwa upande wa Ashura na Shaban, hapakuwa na kusubiri, siku moja tu baada ya Ashura kupewa taraka, wazazi wake walipokea barua ya uchumba toka kwa Shaban, siku chache baadae ndoa ikafungwa, nao wakaishi pamoja na watoto wao watatu, safari hii waliamua kwenda kuishi kigamboni dar es salaam.
Walisha sahau kuhusu fitina na ujuma walizofanyiwa na Idd, sasa walishi kama wanafamilia, huku wakipanga kuficha kwa watoto wao kile kilicho tokea, walifurahia maisha yao kwa pamoja.*********
Kijana Idd kwa sasa anaudhuria tiba, kwa Doctor mmoja wa dawa za hasiri, ambae anapambana, uona Idd anarudisha uwanaume wake, Idd anajilahumu kwa kuto kukubari mapema kuwa yeye ndie mwenye shida na siyo wake zake.
Idd ambae sasa anagundua kitu ambacho alikuwa anakikosa, kitu ambacho kilimkimbiza Ashura na Shani, kitu ambacho Radhia alienda kukipata kwa mwanaume mwingine, sasa Idd alipanga kuwa, akipona aowe tena wake watatu, ili aweze kufaidi kitumbua.***********
Miezi mitatu baada ya harusi ya Edgar na Radhia, ilimkuta Siwema akiwa anachumbiwa na mwanaume mwingine, baada ya kuachana na Said, ikiwa ni maamuzi mapya ya Siwema, aliemua kubadirika na kuishi kwa kufwata maadili.
Sasa Siwema alikuwa ameacha chuki zidi ya mdogo wake yani Radhia, na kuishi nae vizuri, akizingatia kuwa, Radhia akuwa na ubaya wowote zidi yake, maana ata mtoto wake Khadija alikuwa anaishi na nyumbani kwa Radhia, ni kutkana na Khadija kuwa analilia kuondoka na Edgar mala kwa mala anapokuja kuwatembelea.
Mume wa zamani wa Siwema, bado yupo nje ya nchi, lakini kaka yake Siwema amesha rudi, na anasimamia miladi ya familia, akisaidiana na wakina Mariam, iliyoanzishwa na baba yao, yani mzee Makame.
Wakati huo tayari Mariam na Zuhura walikuwa wamesha pata wachumba, ambao ni walinzi wa Edgar, na tayari walikuwa katika mipango ya ndoa, nao pia hawakuwa na kinyogo wala chuki zidi ya Radhia.
Edgar na Radhia ambao wanatarajia kupata mtoto hivi karibu, bado wapo zanzibar, ambako Edgar anawakilisha nchi yake kama barozi, wanaishi kwa furaha, huku anashubiri mke wake aende akajifungue #Mbogo_Land, kisha aende akasomee usimamizi na uongozi wa kampuni, kwaajili ya kujiandaa kuwa msimamizi wa miladi yao.
Wakati huo pia alikuwa anakaa nyumba moja na Zahara, huku Mukhusin akiwa anaishi kwa Dorin nchini #Mbogo_Land, alikuwa ametafutiwa shule, lengo lilikiwa ni kusoma, huku anaendelea kujifunza mpira wakikapu.
Kwakifupi wanaishi maisha mazuri yenye furaha, katika vitu ambavyo Radhia anapenda kulambwa asali, na ukizingatia alisha ambiwa kuwa #ASALI_AITIWI_KIDOLE.
MPAKA HAPO TUNAFIKIA MWISHO WA HADITHI HII, AMBAYO IMECHUKUWA MUDA KIDOGO KUMALIZIKA, ASANTE KWA KUWA PAMOJA NA MWANZO MPAKA MWISHO WA HADITHI, TUONANE KWENYE HADITHI NYINGINE, ZITAKAZO KUJIA HAPA HAPA KWA Mbogo Edgar, KWA MAONI NA USHAURI WASILIANA NA MIMI.
HAYA SASA MKASA UNAOFUATA UNA MUHUSU DOKTA MONICA NA DEUS KAKA YAKE EDGAR HUU MOTO SIO WA KUKOSA
NAANZA KUUPANDISHA HEWANI KUANZIA KESHO PANAPO MAJAALIWA NA UHAI.
Musijali ndugu zangu tutakuwa pamojaHakika ilikuaaaa safari njemaaa na hadithi ilikuaaaa mzuri sanaaaa....tunasubiri kigongo kipyaaa usisahau kututag nasi hatutokuangushaaaaaa
Ahsant KiongoziNitakuwa Sina Fadhila pasipo kushukuru kwa kutupa burudani hii.Shukran sana kaka endelea kutupa burudani sisi wasomaji wako
Hadithi mpya iweke hapa hapa wala usianzishe uzi mpyaAhsant Kiongozi
Na mimi Nawaza kama weweTuendelee sasa,Edgar atabadili dini au ??