Simulizi - change (badiliko)

Simulizi - change (badiliko)

Yaani hicho kipande kifuatacho sio kwa hamu ninayoisubiria....
 
CHANGE

Story by Elton Tonny

Urafiki, Familia, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Ukatili, Mauaji, Mambo yasiyotazamiwa, Mambo yenye kuhofisha

R-rated 18+

Enjoy!

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…


Namouih akavitoa viganja vyake usoni kwa Draxton na kuendelea kumwangalia kwa ujasiri, naye Draxton, akiwa katikati ya badiliko lake sasa, akatoa sauti ya kuunguruma kwa mkwaruzo kama paka ili kumtisha Namouih, lakini mwanamke huyu akamwasha kofi! Ilikuwa ni kama kitendo hiki kilimkasirisha Draxton, kwa sababu akaishika shingo ya Namouih na kuanza kumsukuma kuelekea nje, lakini mwanamke huyu akatumia nguvu kiasi kuupiga ubavu wa Draxton na sehemu yake ya siri, naye Draxton akamsukuma mpaka alipodondoka chini. Namouih akawa anamwangalia huku akijivuta chini hapo taratibu, na sasa Draxton alikuwa anamfata kwa njia fulani ya kikatili kabisa, lakini mwanamke akarudisha mikono yake nyuma ya gauni alilovaa na kuishusha zipu ya nguo yake, halafu akalishusha sehemu za mabega yake na kufanya kifua chake cheupe kilichositiriwa na sidiria ya pink kiwe wazi.

Draxton mweupe, mwenye macho ya mnyama, na nywele nyeupe kichwani akabaki kumtazama huku akipumua kwa nguvu, na tayari vidole vyake vilikuwa vimetoa makucha marefu na makali sana.

Namouih akajinyanyua taratibu na kusimama, kisha akaanza kulishusha gauni lake lote huku akimwambia, "I know you love me. But you need to prove that you do. Not to me... but to yourself."

Alikuwa akimwambia kwamba anajua Draxton anampenda, yaani anajua upande huo wa kinyama unampenda yeye, lakini yeye mwenyewe Draxton angetakiwa kujithibitishia hilo. Draxton akatoa kama muungurumo kwa sauti ya chini, naye Namouih akawa amejitoa ndani ya nguo yake yote sasa. Alikuwa amebaki na sidiria yake na chupi laini ya pink pia, mwili wake maridadi ukiwa wazi mbele ya kiumbe huyo aliyekuwa nusu-mtu, nusu-mnyama, naye Namouih akapiga hatua chache na kusimama mbele yake.

"Slap me..." Namouih akasema hivyo.

Draxton akatoa muungurumo mdogo huku akimwangalia kwa hasira fulani hivi.

"Do it!" Namouih akamwamuru.

Draxton akamtandika kofi usoni lililofanya Namouih aanguke tena chini! Lilikuwa limeendana na sauti kali ya radi iliyosikika kwa nguvu sana huko nje. Mwanamke huyo akasikika akitoa mguno wa maumivu, kisha akamgeukia Draxton tena na kumtazama kwa hisia. Ni baada ya Draxton kuona kwamba alikuwa amemkwarua Namouih usoni kwa makucha yake ndiyo akaacha kumwangalia kwa njia ya kinyama na kumtazama kwa njia fulani ya kujali. Namouih alipotambua hilo, akatabasamu kwa mbali ingawa alikuwa anahisi maumivu makali kwenye shavu lake lililokwanguliwa na makucha matatu yaliyofanya damu itiririke kutoka hapo.

Alichokuwa anajaribu kufanya mwanamke huyu ilikuwa ni kuuchanganya upande wa Draxton wenye kujali zaidi ndani ya badiliko hilo la kati, ili akili ya Draxton PEKEE ndiyo iweze kuuendesha. Sijui kama inaeleweka? Kwa kumfanya Draxton aone kwamba alikuwa anamuumiza, Namouih angeunasa utu wake mzuri wa kujali ndani ya unyama huo ili uchukue "control" zaidi hata kama bado angekuwa katikati ya badiliko lake. Draxton alikuwa amemwambia kwamba akiwa namna hiyo angeona mambo kama mwanadamu lakini matendo yake yangekuwa kama mnyama, kwa hiyo Namouih alikuwa anataka amsaidie kuanza KUTENDA kama mwanadamu akiwa katikati ya badiliko hilo.

Draxton akawa anamwangalia kwa njia iliyoonyesha hisia zilizovurugika, naye Namouih akajitahidi kusimama tena na kumkaribia zaidi. Cha kushangaza kiasi ni kwamba mwanaume huyo akapiga hatua mbili kurudi nyuma, kama vile anataka kumwepuka Namouih, na mwanamke huyu akampa tabasamu hafifu.

"Max..." Namouih akaita.

Draxton akafumba macho yake kwa nguvu kama anaumia vile.

"Come to me..."

Namouih akamwambia hivyo huku amenyoosha kiganja chake mbele, naye Draxton akabaki kumwangalia kwa umakini sana.

"Come. Trust me."

Namouih akamwambia hivyo kwa uhakika kabisa, naye Draxton akaanza kumfata taratibu mpaka alipofikia usoni mwake. Namouih akamshika shingoni na kuupitisha mkono wake mpaka nyuma ya kichwa cha mwana-mnyama huyo, na Draxton alikuwa anamwangalia kwa umakini machoni huku pumzi zake nzito zikipuliza uso wa bibie. Kisha Draxton akapitisha mkono wake mmoja mpaka mgongoni kwa Namouih, na mwanamke huyu akasisimka sana. Draxton akainamisha uso wake kuielekea shingo ya Namouih na kuachama mdomo wake, uliokuwa umeshaanza kutokeza urefu kwenye meno yake makali, kisha akaing'ata shingo ya Namouih kwa ulaini, yaani akitaka kuinyonya. Namouih akafumba macho yake na kuachama mdomo kwa sababu alihisi namna ambavyo meno ya Draxton yalimchoma, na pia, makucha yaliyokuwa mgongoni kwake yalimuumiza kwa sababu yalimkandamiza sana, lakini akajikaza tu. Draxton akaacha kuinyonya shingo na kurudi kumwangalia Namouih usoni, naye Namouih akawa anamtazama kwa hisia za kimahaba na maumivu kwa wakati mmoja.

Badiliko hili la kati la Draxton lilitambua kwamba mwanamke huyu alionyesha ujasiri na uhakika wa kuwa pamoja naye, kwa hivyo hiyo ikafanya akili ya Draxton itulie sana kuruhusu upande wake wa mnyama utende kwa njia isiyo ya kikatili zaidi. Hiki ndiyo kitu ambacho Namouih alikuwa anamaanisha, na sasa kikawa kimeanza kufanikiwa. Hakumwonyesha Draxton woga, bali upendo hata kama alikuwa anaumia, na hiyo ikamfanya Draxton ajiamini zaidi. Mwanaume huyu akamnyanyua Namouih na kumpakata mikononi mwake, huku wakiendelea kuangaliana machoni, kisha akatembea pamoja naye mpaka ukutani na kumbamiza kwa nguvu hapo!

Namouih aliumia kwa kadiri fulani lakini akaweza kucheka kidogo kwa sababu hali hii ilimfurahisha kiasi, naye akamshika Draxton shingoni huku akimtazama kwa upendo. Draxton akaonekana kutabasamu kwa mbali, kisha akaanza kumlamba Namouih shingoni na kifuani, na kiukweli ulimi wake ulikuwa umeongezeka urefu na hivyo kumtekenya vizuri sana mwanamke huyo. Kisha akaing'ata sidiria ya Namouih na kuivuta kwa nguvu sana, halafu akatulia kidogo kutazama kifua cheupe cha mwanamke huyu kilichomtia hamu ya kinyama. (........).

Draxton akamwangalia Namouih machoni kama kuomba ruhusa hivi, na Namouih akatabasamu kilegevu na kutikisa kichwa kukubali. Mwanaume akaanza mashambulizi. (.........).

(.........)

(.........)

(.........)

Akamwangalia Draxton kutokea chini hapo na kuona namna alivyomwangalia kwa subira, na kiukweli mapigo ya moyo ya Namouih yalidunda kwa kasi sana kwa sababu jambo hili lote lilikuwa la marufuku kubwa sana ambayo hakuwahi kufikiri angekuja kushiriki. Huyo aliyesimama hapo alitakiwa kuwa mume wake, lakini haikuwa hivyo. Mbaya zaidi alikuwa ni mpenzi wa rafiki yake wa karibu sana, hivyo alikuwa anafanya usaliti wa hali ya juu. Lakini moyo wake ulikuwa umesharidhia kwa asilimia zote kabisa kuwa na Draxton haijalishi vikwazo, kwa hiyo akaishusha bukta ya mwanaume (........). Namouih alisisimka sana. Alikuwa na rundo kubwa sana la hisia za kimahaba alizohitaji zipozwe kwa muda mrefu mno, na sasa kitu ambacho kingemsaidia kilikuwa mbele yake.

(........).

(........).

Kisha Draxton akamvuta Namouih kwa nguvu sana na kumsimamisha, na akiwa bado ameshangaa kiasi, Namouih akabebwa tena na kupelekwa ndani ya chumba kile kidogo na kurushwa kitandani kama mfuko wa mzigo mzito.

"Max jamani...."

Namouih akasema hivyo huku anamwangalia usoni, lakini Draxton akaishika chupi laini ya bibie pande za mapaja yake na kuivuta kwa papara sana, kisha akaitupa pembeni utadhani ana hasira. Namouih akacheka kidogo, naye Draxton (........).

(........).

(........).

(........).

(........).

(........).

(........).

(........)

Mnyama-Draxton akawa amemaliza kumwaga raha zake, lakini alikuwa amevikandamiza vidole vyake kitandani na hivyo kufanya makucha yake yatoboe mpaka ndani ya godoro, naye akajilaza pembeni yake Namouih huku akipumua kwa uchovu. Namouih akageuza mwili wake na kulalia ubavu wake, akiwa anahisi maumivu mgongoni na usoni kiasi, lakini pia raha nyingi na amani ndani ya moyo wake, naye akamshika Draxton kifuani kwa wororo. Draxton akamtazama machoni pia, bado akiwa katikati ya badiliko lake, naye akafumba macho yake na kuyafumbua tena, kitu kilichomfanya Namouih atambue kwamba alikuwa anamshukuru. Mwanamke huyu akaachia tabasamu na kufanya hivyo hivyo kama Draxton alivyokuwa amefanya, kisha mwana-mnyama wake huyo akaelekeza uso juu na kuonekana akifumba macho kama kuvuta usingizi.

Namouih alihisi kufarijika sana moyoni. Ni ile hisia nzuri ya 'tumetoka mbali' ingawa kwenye safari yao hii jambo hili walilotoka kufanya lilikuwa jipya, na la marufuku. Akawa anatembeza vidole vyake taratibu kwenye ngozi imara ya Draxton, mara kwa mara akikumbukia namna alivyokuwa ametoka kupewa penzi la mnyama huyo mwenye mvuto sana, naye akafumba macho yake na taratibu usingizi ukampitia kwa mara nyingine tena.

β˜…β˜…

Namouih alikuja kuamka muda mfupi baadaye, na sasa alitambua kwamba mvua ilikuwa imeshakata kwa kutosikia sauti ya maji kumwagika. Alikuwa amelalia tumbo lake na kuitanua miguu kitandani kwa kujiachia sana, naye akahisi jambo fulani lilomshangaza kiasi. Maumivu yake usoni na mgongoni hayakuwepo tena, na alipojishika shavuni hakuhisi mikwaruzo ile iliyokuwepo baada ya Draxton kumkwarua muda fulani nyuma. Akanyanyua shingo yake na kuangalia vizuri kitandani, na hapo Draxton hakuwepo. Mwili wake usiokuwa na nguo hata moja ulikuwa umefunikwa kwa shuka safi jeupe, naye akajigeuza ili kutazama upande wa pili.

Mapigo yake ya moyo yakadunda kwa nguvu kutokana na msisimko uliomwingia baada ya kumwona Draxton akiwa ameketi kwenye kiti kimoja huku anamwangalia kwa utulivu. Wakati huu mwanaume huyo alikuwa amerejea hali yake ya kawaida kabisa, isipokuwa nywele zake kuwa nyingi na nyeupe bado. Namouih akaanza kumwangalia kwa uvutio mwingi sana, yale macho ya upendo yaani, naye Draxton akaangalia chini tu akionekana kutafakari mambo fulani. Namouih akajivuta na kuketi, na hiyo ikafanya sehemu ya kifua chake cheupe iwe wazi baada ya shuka kutelezea chini zaidi, na Draxton akakitazama kwa umakini. Kukiona tu ikawa ni kama kimemwamshia hamu kubwa, naye akameza mate na kumtazama Namouih machoni, jambo lililofanya mwanamke huyo atabasmu huku ameibana midomo yake.

Draxton akanyanyuka kutoka alipoketi na kupiga magoti karibu na kitanda, akiiegamiza mikono yake hapo huku uso wake ukiwa karibu na uso wa mwanamke huyo mrembo, kisha kwa sauti yenye kujali sana akauliza, "Are you okay?"

Namouih akafumba na kufumbua macho taratibu, kisha akasema, "Am okay."

"Am sorry..." Draxton akamwambia.

"Sorry for what?" Namouih akauliza kwa sauti ya chini.

"Nime.... nimekuumiza Namouih..."

"Haujaniumiza Draxton. Niko sawa."

Draxton akafumba macho na kuinamisha uso.

"Usiwe hivyo. Umejitahidi sana leo Draxton. Ume... umefanikiwa," Namouih akasema kwa furaha.

Draxton akawa anatikisa kichwa kukubali akionekana kufurahi pia, kisha akamwangalia Namouih na kuuliza, "Uliwezaje... yaani... siamini Namouih kama...."

"Ahah... uliniamini tu Draxton. Hilo lilitosha," Namouih akasema.

"Sijui tu nilikosea wapi kwa Ramona, Namouih...."

"Hayakuwa makosa yako... ilitokea tu. Nimekuelewa vizuri sana... na ninafurahi kuona sasa kwamba unaweza kuji-control ukiongoza hisia zako vizuri kwa unayempenda...." Namouih akaishia hapo na kuangalia chini.

Draxton akavishika viganja vyake na kumwambia, "Najua jambo hili ni zito sana, na sina maneno yoyote yale yatakayoweza kuonyesha shukrani yangu ya dhati kwa ulichofanya kunisaidia. Tumevuka mipaka Namouih, najua hatujawatendea haki wale wanaotupenda, lakini nahitaji ujue kwamba.... sijutii kufanya jambo hili pamoja nawe."

Namouih akaendelea kumwangalia kwa hisia.

"Ni ubinafsi I know, na sijui ni kwa nini lakini... lakini ndiyo ukweli... ndiyo ninavyohisi... na sitaficha hilo. Sijui... itakuwa vipi tukitoka hapa... ila nataka ujue kwamba nathamini sana ulichonipa leo Namouih... sana," Draxton akasema kwa hisia.

Namouih akatabasamu kwa mbali na kutikisa kichwa kuikubali shukrani hiyo. "Umenipaka damu yako, siyo?" akauliza.

"Ndiyo. Nilikukwangua vibaya sana... nimejihisi...."

"Usijihisi vibaya Draxton, angalau umeniponya. Ijapokuwa... hii ni... ahah... ajabu kidogo ila... nataka nikwambie ukweli pia. Nimefurahia kuwa pamoja nawe," Namouih akaongea kwa hisia.

Draxton akatabasamu kwa hisia pia, kisha akamwangalia Namouih kifuani. Alikuwa akimtazama kwa njia iliyotuma ujumbe wenye hisia nzuri kwa mwanamke huyo, naye Namouih akajiangalia kifuani pia na kumtazama Draxton kwa macho yaliyojaa huba nzito. Draxton akamtazama machoni tena na kuona kwamba hata Namouih pia alikuwa anasubiri hisia hii itendewe kazi kwa njia fulani, hivyo taratibu akapitisha kiganja chake usoni kwa bibie na kuanza kuuelekea mdomo wake. Namouih akafungua midomo yake kwa utayari, naye akapokea kinywa cha Draxton kwa raha zote na kuanza kupeana ndimi pamoja naye.

Busu hii ilikuwa ya mahaba ya hali ya juu, yaani, walidendeshana kwa upendo mwingi sana uliofanya wasahau muda, chakula, na hali zao kimahusiano kabisa. Walikuwa wanafanya usaliti, lakini kwao ilikuwa ni usaliti kwa mapenzi halali. Draxton akaiachia midomo ya Namouih na kuanza kumlamba kuelekea shingoni kwake, akifanya kama kuinyonya taratibu, na Namouih akawa anazungusha mikono yake mgongoni kwa mwanaume huyo. Taratibu Draxton akashusha mdomo wake mpaka kifuani kwa mrembo na kukipa upendo kwa hamu. Namouih alipatwa na msisimko mzuri sana, kwa kuwa alifurahia mno jambo hili lililokuwa linampata kwa wakati huu; sababu ikiwa kwamba alikuwa amepitisha muda mrefu bila kukutana na mwanaume yeyote, na hivyo Draxton kumwonyesha ana njaa ya kutaka kumla yeye kila mara kulimpa furaha sana.

Lakini Draxton akakatisha jambo hilo na kubaki ameinamisha uso, huku akipumua kwa nguvu kiasi. Namouih akawa ameelewa kwamba mzuka wa upande wa pili wa mwanaume huyu ulikuwa unamvizia, kwa hiyo alikuwa anatafuta utulivu. Akaushika uso wake, na ni kweli ulikuwa umeanza kuwa wa moto sana, naye Draxton akamwangalia.

"Labda itakuwa vizuri tuki... tukipata chai," Draxton akasema.

Namouih akatabasamu kilegevu kiasi na kuuliza, "Halafu?"

"Halafu ninyoe hizi nywele..."

"Ahah... halafu?"

Draxton akaangalia chini na kusema, "Halafu turudi jijini. Blandina atakuwa ameshanitafuta sana."

Namouih akavitoa viganja vyake usoni kwa Draxton taratibu na kuangalia pembeni.

Draxton akamtazama kwa hisia usoni kwa kuhisi labda maneno yake yalimkwaza.

"Naelewa Draxton. Sote tutapaswa tu kurudia maisha yetu ya kawaida. So it's okay," Namouih akasema bila kumwangalia.

Draxton akapitisha kiganja chake mgongoni kwa Namouih na kukishika kiuno chake kwa wepesi.

Namouih akamwangalia na kuuliza, "Kwa hiyo sasa hivi angalau utaweza kumpa Blandina...."

"La, Namouih... bado," Draxton akamkatisha.

Namouih akaendelea kumwangalia.

"Bado sijawa na uwezo wa kutosha kumpa jambo hilo nikiwa kama mimi. Umenisaidia kuweza kuji-control nikiwa katikati ya badiliko langu, ila mimi nitatakiwa kujizoeza zaidi... nione kama nitaweza kufanya hivyo bila kulifikia..."

"Bila kulifikia badiliko lako? Ni nani atakusaidia kufanya hivyo ikiwa huwezi kushiriki na Blandina, Draxton?" Namouih akauliza.

Draxton akamshika mkononi huku akimtazama kwa hisia.

"Hata mimi sijui nini kitatakiwa kufata... lakini unatakiwa ujue pia kwamba sitoacha kuwa hapa kwa ajili yako," Namouih akamwambia.

Wawili hawa walikuwa wakipita kwenye wimbi kubwa la kihisia kwa kujaribu kuondoa mawazo ya kujiona kuwa wabaya kwa sababu ya kuwasaliti wenzi wao, na kiukweli wimbi hilo ndani ya mioyo yao lilikuwa kubwa sana kuelekeana. Hii haikuwa kwa sababu tu walitaka kusaidiana, bali kwa sababu walikuwa na hisia za wazi kabisa za kimapenzi kuelekeana, na jambo walilokuwa wakifanya lilizikoleza hata zaidi. Ingekuwa ni kitu walichotakiwa kukomesha haraka mno lakini tayari walikuwa wamefika mbali sana kurudi nyuma; kwa kuwa walihitajiana sana.

Baada ya maongezi hayo mafupi, Draxton akanyanyuka na kufata gauni lile la Namouih pamoja na chupi yake, ambazo alikuwa ameshaziweka katika hali nzuri muda ambao Namouih alilala tena. Sidiria ile ilikuwa imechanika, hivyo mwanamke asingeweza kuivaa tena. Draxton akapanda kitandani na kuanza kumvalisha chupi mwanamke huyo taratibu, kitu kilichofanya Namouih atabasamu kwa haya kiasi baada ya kusisimka. Draxton akatabasamu pia na kuanza kumsaidia kuvaa gauni lake. Akawa anamwambia kwamba kwa nyumba hiyo hakukuwa na bafu, na mara nyingi alipokuja kukaa huku kwa muda mrefu angeogea nje kwa maji aliyoleta hapo, kwa hiyo kuoga kwa Namouih ingepaswa kuwa akirejea nyumbani kwake.

Alipomaliza kuivaa nguo yake, Namouih akaketi kitandani huku miguu yake ikikanyaga chini, na Draxton alikuwa amekaa nyuma yake kitandani. Mwanaume akawa anaipandisha zipu juu taratibu mpaka mwisho, kisha akaanza kuzilaza nywele za Namouih za kusukwa kwa nyuma kwa njia fulani ya kuzichezea. Namouih alipenda sana miguso ya Draxton, na ilikuwa kama hamu ambayo mwanaume huyo alikuwa amemwamshia dakika chache nyuma kabla ya kukatisha penzi lao iliendelea kuzunguka ndani yake, hivyo akayashika mapaja ya Draxton kwa kuirudisha mikono yake nyuma na kumgeuzia shingo yake ili amtazame machoni. Draxton akawa ameelewa kile ambacho mwanamke huyu mrembo alikuwa anaomba kutokana na namna ambavyo Namouih alimwangalia, hivyo akakishika kidevu chake na kuanza kuinyonya midomo yake taratibu kwa upendo mwingi.


β˜…β˜…β˜…


Muda mfupi baadaye, Namouih akawa barabarani kuelekea nyumbani baada ya kutoka msituni kule kwa Draxton. Ilikuwa imemchukua muda mrefu kiasi kuweza kutoka huko kwa kuwa njia ilitawaliwa na matope na utelezi shauri ya mvua kubwa kunyesha, lakini alijitahidi sana mpaka akawa amefanikiwa kuingia lami. Akiwa amemwacha Draxton kule, Namouih alikuwa anatafakari mambo mengi sana kuhusiana na jambo lililopelekea mpaka akajikuta ndani ya penzi la mwanaume yule.

Hangejizuia kutabasamu kwa hisia kila mara alipokumbuka namna ambavyo Draxton alimtendea, kuanzia kumpa penzi matata sana mpaka kumwambia kwamba hakujutia kushiriki naye jambo hilo. Ilikuwa ni hali yenye uajabu kwa kiasi kikubwa kwamba walikuwa wamefikisha mambo mbali namna hiyo, lakini moyo wake ulimfurahia sana mwanaume yule kwa asilimia zote. Ilikuwa imeshafika saa tisa alasiri Namouih alipowasili nyumbani kwake. Hakuwa akihisi njaa kwa sababu alipata chai na biskuti nzito kule kule kwa Draxton muda fulani nyuma baada ya wawili hao kupeana mapenzi. Alifunguliwa geti la hapo na kuliingiza gari ndani, liliokuwa limejaa matope mengi sehemu za matairi na hivyo kuchafua sehemu ya nje ndani ya uzio la nyumba kwa sababu ya ardhi kuwa imelowana kiasi.

Alipoliegesha gari lake, simu yake ikaita, ikiwa ni mama yake mzazi, naye akapokea ili kumsikiliza. Zakia alikuwa anamwambia kwamba ana shida na kiasi fulani cha pesa kutokana na uhitaji wa dharura uliompata, naye Namouih akamwambia asiwe na shaka kwa sababu angemtumia. Mama yake alikuwa anasema alijaribu kumtafuta kwa muda mrefu bila kumpata, na aharakishe kumtumia kwa sababu simu yake ilikuwa imepatwa na shida fulani hivi, na Namouih akamwambia tu kwamba simu yake ilikuwa imezima kwa wakati ule aliomtafuta kwa hiyo asihofu; atulie tu, na hiyo hela angemtumia.

Baada ya simu kukatwa, mwanamke huyu mrembo akashuka kutoka ndani ya gari na kuanza kuuelekea mlango wa kuingilia ndani ya nyumba. Alikuwa anatembea taratibu sana, akikumbukia penzi murua alilokuwa ametoka kupewa siku hiyo kwa mtindo ambao hakuwahi kufikiri angekuja kupata kabisa. Alikuwa amevunja kiapo chake cha ndoa, lakini bado ni kama alipuuzia jambo hilo kwa kuwa furaha aliyohisi ilipita uzito wake. Kitu alichokuwa anakililia kwa mume wake sasa akawa amekipata kwingine, na huko kwingine kulikuwa kutamu haswa! Akajichekea tu kidogo kwa kuingiwa na haya yeye mwenyewe, lakini akarudisha kumbukumbu za kutakiwa kumtumia mama yake pesa haraka, hivyo akafika mlangoni na kuufungua ili aende ndani kukamilisha hilo. Ni baada ya kuufungua tu mlango ndipo akashtuka sana na kutoa macho kwa mshangao, kwa kuwa hapo mbele aliyesimama hakuwa mwingine ila Efraim Donald mwenyewe!




β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

ITAENDELEA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…


Usikose sehemu za mwendelezo wa hadithi hii kali ya CHANGE. Ni story nzuri na ndefu sana. Waweza ipata nakala yote kwa gharama nafuu sana. Karibu WhatsApp au kwa E-mail yangu.

WhatsApp no: +255 678 017 280
 
Iko poa sana hii Mkuu Elton Tonny . Drax na Namu ni perfect combo sasa sijui itakuwaje next episode maana Efraim Donald naye atakuwa ameshashitukia tendo alilofanya Mke wake πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
CHANGE

Story by Elton Tonny

Urafiki, Familia, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Ukatili, Mauaji, Mambo yasiyotazamiwa, Mambo yenye kuhofisha

R-rated 18+

Enjoy!

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…


Namouih hakuwa ametarajia kabisa kumwona mume wake hapo, na Efraim alikuwa amesimama tuli huku akimwangalia mke wake kwa utulivu sana, kisha akaachia tabasamu lililoonyesha furaha. Namouih akameza mate kwa hofu kiasi iliyomwingia, na mapigo yake ya moyo yakaanza kumwenda mbio sana kutokana na kujua kwamba alikuwa ametoka nje kufanya kitu kisichokuwa halali kwenye ndoa yao. Akamtazama mume wake machoni na kushindwa hata kutoa tabasamu la kinafiki, yaani alishindwa.

"Suprise!" Efraim Donald akamwambia mke wake kwa shauku.

Namouih akaanza kutafuta utulivu katika upumuaji wake kwa kuwa alikuwa ameanza kupumua kwa kasi kiasi, naye Efraim Donald akaanza kumsogelea na kumkumbatia huku akicheka kwa furaha.

"I missed you honey," Efraim akasema hivyo akiwa bado amemkumbatia.

Namouih akadondosha pochi yake alipokuwa anataka kurudisha kumbatio la mume wake, naye Efraim akamwachia na kumtazama usoni kwa hisia za upendo.

"Vipi?" Efraim akauliza.

Namouih akaachia tu tabasamu lililoonyesha wasiwasi.

"Mbona hivyo? Nimekushtua sana?"

"Efraim... n..ndiyo... ume... umenishtua... honey jamani, umerudi saa ngapi?" Namouih akauliza.

"Ahahahah... yaani ndiyo nimeingia ndani tu na wewe unafika. Eeh! Check ulivyopendeza! Mambo mengi yamekwenda vizuri huku wakati sipo eti?" Efraim Donald akauliza.

"Aam...."

"Twende ndani tukaongee mpenzi. Nimekumiss sana," Efraim akasema.

Wanandoa hawa wakaanza kuelekea ndani pamoja, lakini Namouih akarudi nyuma tena ili aiokote pochi yake. Efraim Donald alikuwa anamwangalia kwa matamanio sana pale Namouih alipoinama ili aiokote, lakini akajizuia kuendelea kumwangalia kwa njia hiyo na kuendelea kutabasamu mke wake aliponyanyuka. Bado Namouih alikuwa anahisi hofu moyoni kwa kadiri kubwa, lakini akajikaza na kumfata tena mume wake ili waelekee ndani zaidi. Efraim Donald akafika kwenye sofa na mke wake, kisha wakaketi pamoja kwa ukaribu. Namouih alikuwa anahofia kwamba huenda mume wake angehisi kuna jambo haliko sawa kwenye mwili wake; kwa kuwa hakuwa ameoga, hakuvaa sidiria ndani ya nguo yake, na akahofia hata labda harufu ya Draxton ingepenya puani kwa mume wake kwa sababu yeye mwenyewe aliihisi vyema mwilini.

"Honey... mikutano kule imekwenda superb, yaani vyema, nafikiri tutaendelea kupata mambo mengi mazuri sana," Efraim akasema.

Namouih akatoa tabasamu la kujilazimisha, kisha akamwambia, "Ni vizuri Efraim... hongera sana."

Efraim Donald akawa ameishika sehemu ya pembeni ya shingo ya Namouih na kufanya kama anaisugua taratibu, kisha akauliza, "Ulikuwa wapi?"

"Kulikuwa na sherehe ya sendoff jana. Burudani kali mpaka muda ukaenda kwa hiyo... ikabidi nilale kwa rafiki yangu tu," Namouih akajibu.

"Ahaaa... umependeza sana..."

"Wewe pia. Ungeniambia unakuja usingenikuta... shaghalabaagala hivi..."

Efraim Donald akacheka kidogo.

"Ngoja nikajimwagie. Esma yuko wapi?"

"Nimemwagiza dukani mara moja," Efraim Donald akasema.

"Okay sawa," Namouih akasema.

Akawa ameanza kunyanyuka na kugeuka ili aanze kuelekea upande wenye ngazi, lakini Efraim akamshika mkononi. Namouih hakugeuka haraka, kwa sababu mapigo ya moyo wake yalidunda kwa nguvu sana kutokana na msisimko wa hofu uliokuwa ndani yake, lakini akajikaza na kugeuka taratibu, kukuta Efraim akiwa ameshasimama tena na akimwangalia usoni kwa umakini.

"Namouih..." Efraim akaita kwa sauti ya chini.

"Bee..." Namouih akaitika kwa sauti tulivu pia.

"Najua bado kuna vitu vingi vya kuzungumzia mke wangu... lakini nakuomba tu, for the sake of your birthday... tuyaweke pembeni kwanza," Efraim akamwambia.

Namouih akatazama chini.

"Ona... naelewa, naelewa tunakotoka na tulipo, ila nakuahidi... birthday yako ikiisha nitaweka kila kitu wazi na... hautateseka tena... nakuahidi. Unaniamini, siyo mke wangu?" Efraim akaongea kwa kubembeleza.

Namouih akamwangalia usoni na kutikisa kichwa kukubali.

Efraim Donald akamshika shavu kwa kiganja chake, kisha akapeleka mdomo wake kwake ili ambusu.

Namouih, Namouih, Namouih, mwanamke huyu hakujihisi uhakika tena wa kutaka kufanya jambo hilo pamoja na mume wake, sababu ikiwa ni kwamba tayari moyo wake ulikuwa umeanza kupeperukia mbali kutoka kwa Efraim Donald. Mwanaume huyo akaanza kumbusu kimahaba mdomoni huku akiubana mwili wake kwake, lakini Namouih alikuwa akijibu busu hiyo bila kuhusisha hisia hata kidogo. Alikuwa amefumbua macho yake tu huku ametazama pembeni kutokana na kutohisi jambo lolote tena lenye kusisimua kutoka kwa mume wake. Kisha busu hiyo ikavunjwa taratibu, naye Efraim akampa mke wake tabasamu la upendo, huku Namouih akilitoa lake kwa kujilazimisha.

"Haya kajimwagie maji mama... mimi nimeshatoka huko."

Efraim Donald akawa amemwambia maneno hayo huku akimsugua-sugua begani, na Namouih akaanza kuondoka kuzielekea ngazi hatimaye. Alikuwa anatembea taratibu na kuanza kuzipanda ngazi bila haraka yoyote, na mara kwa mara angemwangalia Efraim pale chini na kuona jinsi alivyomtazama sana kwa tabasamu la upendo, na mwanamke huyu hakuweza kujizuia kuhisi hatia moyoni mwake kwa kiasi fulani kutokana na ukweli wa kwamba alikuwa amekwenda nje ya ndoa yake. Akafika juu na hatimaye kuingia chumbani kwake, akafumba macho kwa kitambo kifupi akitafakari mengi sana, kisha akaanza kuvua nguo ili aelekee kusafisha mwili wake.

Tabasamu lililokuwa usoni mwake Efraim Donald lilififia baada ya mke wake kuwa amekwenda chumbani. Akabaki akitazama huko juu kwa umakini wa hali ya juu, kwa sababu ujio wa mke wake wakati huu ulikuwa umemfanya ahisi na kutambua kwamba kuna kitu kipya kilikuwa kimebadilika kwa Namouih. Uhakika aliokuwa nao kumwelekea kwamba hakutoka na mwanaume mwingine sasa ukawa umetiliwa mashaka, kwa sababu hata roho yake ya ndani ilimwezesha kuhisi kwamba mke wake alikuwa amechafuka; yaani amechafuka ndani ya dhamiri yake. Ikiwa hii ilimaanisha kwamba huenda Namouih ameanza rasmi kwenda nje ya ndoa yao, au huyo mtu mwingine aliyempenda tayari amemfahamu, basi angetakiwa kuimaliza ishu hii upesi sana, kwa sababu ni muda kidogo tu ndiyo aliokuwa amebakiza kabla ya mipango yake kukamilika.

β˜…β˜…

Upande wa Blandina, siku hii ya Jumapili haikuwa imeanza vizuri sana kwake. Baada ya kuachwa na Draxton usiku uliotangulia bila kupewa sababu iliyoeleweka, mwanamke huyu alirudi nyumbani na kujaribu kumtafuta mpenzi wake bila mafanikio. Siku hii ilianza pia kwa yeye kujaribu kumtafuta kwa simu tena bila kumpata, hivyo aliamua kwenda kule ambako mpenzi wake alipanga ili aonane naye. Yaani Blandina alimpenda sana Draxton, na kuona ukimya namna hiyo ni kitu kilichomfanya akose amani sana. Ilikuwa ni kama vile hakuwa na mambo mengine ya kufanya kwa sababu akili yake yote ilikuwa kwa mwanaume huyo tu siku hii.

Hata alipofika pale Draxton alipopanga hakumkuta, hivyo alirudi tu nyumbani kwake na kuamua kukaa kwa kutulia. Maeneo ya huku ilinyesha mvua ya kadiri tu, haikuwa kubwa kama ilivyokuwa msituni kule alipokuwepo Draxton. Jumbe alizomtumia Draxton hazikujibiwa, na hata kuna wakati alikuwa akimtumia Namouih jumbe fupi pia lakini naye hakumjibu. Kwa hiyo akatulia tu nyumbani akiwa ameshahisi kuchoka kwa sababu ya kutangatanga sana kiakili. Imefika mida mida ya saa kumi hivi jioni ndiyo akasikia sauti ya honi ya gari nje ya geti la nyumba yake. Tayari alikuwa na matumaini kwamba bila shaka huyo angekuwa ni Draxton, na alikuwa sahihi.

Akatoka ndani na kwenda mpaka nje ya geti, naye akamkuta Draxton akiwa amesimama kando ya gari lake huku akimtazama. Wakati huu mvua ilikuwa imeshakata na kubakiza upepo mkali kiasi uliopuliza huku na huko, naye Blandina akamwonyesha kwa ishara ya kidole chake kwamba amfate, kisha mwanamke akaingia tena ndani na kuuacha mlango wa geti lake wazi. Draxton alikuwa amevalia T-shirt yake nyeusi yenye mikono mifupi na kaptura ya samawati pamoja na raba nyeupe chini, naye akainamisha uso wake kidogo kutokana na kuwa na mambo mengi ndani ya akili yake yaliyofanya akose amani kwa kadiri fulani. Lakini alielewa wazi kabisa kwamba hii ndiyo sehemu aliyotakiwa kuwa kwa sasa haijalishi nini kilikuwa kinaendelea, kwa hiyo akalifunga gari lake kwa funguo na kuelekea kule ndani.

Blandina alikuwa amefika sebuleni kwake na kukaa kwenye sofa moja ambalo kama mtu angeingia ndani hapo angekuwa anatazamana naye moja kwa moja, hivyo Draxton alipofika tu ndani akamkuta mpenzi wake akiwa amekaa huku amekunja nne. Blandina alivaa khanga moja tu kutokea kifuani iliyofikia sehemu ya magoti, hivyo kwa namna alivyokaa ilifanya sehemu za mapaja yake ziwe wazi sana, lakini kwa sasa hakuwa ameweka umakini wake kwenye kumtamanisha mwanaume huyo kwa umbo lake zuri, bali alikuwa anamwangalia kwa umakini kama anasubiri ajielezee.

Draxton akiwa bado amesimama tu, akashusha pumzi na kusema, "Nimekuja Blandina."

"Ndiyo... nakuona umekuja. Mambo vipi?" Blandina akamuuliza kwa njia ya kizembe kiasi.

Draxton akabaki kimya, kwa kuwa alitambua hilo lilikuwa itikio la Blandina la kukwazika.

"Karibu ukae. Utakuwa umechoka sana maana... sijui ulikuwa unafanya nini huko ulikokuwa," Blandina akasema.

"Nakosa hata cha kukwambia Blandina kwa sababu ya tabia yangu isiyofaa hata kidogo," Draxton akasema kwa upole.

"Kuna sababu yoyote ya kueleza chochote Drax? Siyo kwamba labda umenioa kwa hiyo... uko free kufanya chochote unachotaka.."

"Am sorry Blandina..."

"Aagh... sorry za nini? Kuwa mwanaume basi. Mwanaume anapaswa kusimama imara kwa chochote anachoamua kufanya, lakini wewe ni kama hujiamini. Unafika tu hapa na cha kwanza kusema ni samahani, samahani, samahani... ina maana hauna mambo mengine ya kuongelea? Samahani inanisaidia nini Draxton? Wewe... njoo ukae hapa... nikuwekee hata chai au... kitu chochote ili utulie, mengine yafate, hizo samahani mimi nimeshazi...."

Draxton akamsogelea karibu na kuchuchumaa usawa wa miguu yake, kwa ile njia ya kupiga goti moja chini.

"Nisamehe Blandina. Najua ulijihisi vibaya mimi kuondoka bila kusema sababu na... kunikosa mpaka sasa. Haustahili kutendewa namna navyokutendea," Draxton akasema kwa upole.

"Ni kwa nini sasa bado unanitendea hivyo?" Blandina akauliza kwa mkazo.

"Niseme tu... bado ndiyo niko kwenye... harakati za kujizoeza zaidi ku... kusafisha maisha yangu... kama nilivyokwambia," Draxton akasema.

"Kwa nini unababaika sana ukiwa unaongea kuhusiana na hilo jambo? Ufasaha wako wote huwa unapotelea wapi? Kweli Draxton... ina maana mimi mpenzi wako... unashindwa kuniambia kinachokusumbua? Tatizo ni nini? Eeh? Mbona nimekuwa na subira vya kutosha lakini unaniweka kando tu? Nataka tupige hatua za mbele zaidi kwenye mahusiano yetu Draxton lakini hauniruhusu kufanya hivyo. Kila mara jambo kama hili likitokea inakuwa ni kama sikujui kabisa... inanifanya nishindwe kujua kama natakiwa kuendelea kukuamini maana unajionyesha kuwa tofauti na ninavyokufikiria..." Blandina akaongea kwa hisia sana.

Draxton akainamisha uso wake kidogo.

"Hhh... uliniambia unataka kutulia nami pia... nionyeshe hilo. Una... unachodili nacho hata kama ni kizito... niambie, maana huwezi kujua... labda hata naweza kusaidia. Lakini hali ikiendelea kuwa hivi... siri, siri, siri, tutatulia vipi mpenzi wangu?" Blandina akasema kwa hisia sana.

Kwa kiasi kikubwa roho ilikuwa inamuuma sana Draxton. Kuanza kumwelezea Blandina kitu kilichokuwa kinamsumbua kulimaanisha angepaswa kutoa na ushahidi pia, maana kwa mtu kama Blandina, akiwa kama mwanasheria pia, isingekuwa rahisi kwake kuamini mpaka ajionee mwenyewe. Na hata kama angeamini, msaada ambao Draxton alihitaji sasa aliweza tu kuupata kutoka kwa mtu ambaye upande wake wa pili ulimpenda, na huyo hakuwa Blandina bali Namouih. Angeanza vipi kumwelezea kwamba huo msaada tayari alikuwa ameanza kuupata, tena kutoka kwa rafiki yake Blandina wa karibu kabisa?

Ingekuwa bora kama na upande wake wa pili ungempenda Blandina, labda ingekuwa rahisi kwake kumpa msaada kwa utambuzi kama tu Namouih alivyofanya mapema ya siku hiyo, kwa sababu endapo kama angejaribu kujionyesha mbele ya Blandina akiwa mnyama au nusu-mwanadamu, nusu-mnyama, huenda angemuumiza vibaya sana mwanamke huyu. Hakutaka kile kilichompata mpenzi wake wa Venezuela kijirudie kwa Blandina pia, kwa hiyo kama ni kuendelea kupambana na hali yake kwa msaada wa pembeni angeendelea kufanya hivyo ili ije kufika siku ambayo angeweza kujitoa kwake kikamili bila kuwa na hofu ya kumuumiza.

Draxton akawa bado ameinamisha uso wake kidogo, naye Blandina akashusha pumzi na kuliegamia sofa kabisa huku akiegamiza kiwiko chake kwenye mkono wa sofa, na kiganja chake akikiweka mdomoni huku ameangalia pembeni kwa njia iliyoonyesha mfadhaiko.

"Ninajitahidi Blandina. Naomba tu ujue kwamba ninajitahidi kuji... kujitengeneza ili... kama nilivyokwambia, nikupe kilicho bora. Naomba tu uamini hilo," Draxton akamwambia kwa kumsihi.

"Ahah... niamini nini Drax? Sioni chochote... sikipati, sielewi, si... ahh... na mimi ninajitahidi kuwa na subira Draxton lakini naomba tu ujue kwamba siyo rahisi... angalau kama ungenipa uhakikisho kwa matendo yako kwamba hayo unayosema ni kweli ningeelewa lakini every time tunarudi kule kule tu... kule kule... agh..." Blandina akaongea kwa hisia za kukwazika na kupiga ulimi wake ndani ya mdomo.

Draxton ni kweli alikuwa amekosa hata cha kumwambia, lakini hata yeye pia alikuwa anataka kumwonyesha kwa matendo kwamba ni kweli anafanya jitihada hizo, lakini alichohofia ilikuwa ni kupitiliza. Akamwangalia Blandina usoni na kuona namna ambavyo mwanamke wake alikuwa amekwazwa kweli, naye akamshika kwenye goti lake taratibu. Blandina hakutoa itikio lolote na kuendelea kuangalia pembeni tu, na ndipo Draxton akauachanisha mguu wa mwanamke huyu uliokuwa juu ya mwingine, na yote ikakanyaga chini sasa.

Blandina akamwangalia Draxton usoni, na mwanaume huyu akasogea karibu zaidi na kuwa kama ameuweka mwili wake katikati kwa kupiga magoti chini sasa na kuyaachanisha mapaja ya Blandina yaliyokuwa wazi mpaka kuionyesha chupi laini ya rangi nyekundu aliyovaa, na kwa sababu ya urefu wa Draxton alikuwa ameelekeza uso wake karibu zaidi kwenye uso wa mwanamke huyo, akitazamana naye machoni kwa hisia. Kwa hapa Blandina alikuwa ameanza kupandwa na hisia nzuri, lakini alitaka kuona ikiwa Draxton alimaanisha kile alichoonyesha kudhamiria kufanya, kwa hiyo akaendelea kutulia. Mwanaume akaishika shingo ya Blandina kama anataka kumkaba vile, kisha akausogelea mdomo wake na kuanza kumlamba denda taratibu.

(.......). Blandina alikuwa anasikilizia tu jambo hilo, kwa kuwa alielewa kwamba Draxton alikuwa ameanza kumwonyesha kwa matendo yake kweli kabisa kuwa anamaanisha kile alichokuwa ametoka kumwambia.

(........).

(........).

(........).

(........).

Draxton alikuwa akijitahidi sana kuhakikisha anamhudumia mpenzi wake kwa umakini bila kuruhusu hisia zake za upande wa pili kutoka, na kiukweli alikuwa amejitahidi sana mpaka kufikia hapa, ila zikawa zimenza kumzidia.

(.......).

Blandina akiwa anaendelea kuuhisi vyema utamu wa ulimi wa mwanaume wake, mkono uliokishika kichwa cha Draxton ukaanza kulihisi joto la mwanaume huyo lililoongezeka haswa, na ni hapo hapo tu ndiyo Draxton akakiacha kito cha Blandina na kujirudisha nyuma kwa kasi sana! Blandina alikuwa ameachwa kwenye mshtuko wa hisi ya kimahaba baada ya Draxton kuachia kito chake ghafla, naye akabaki kumtazama huku macho yake yakiwa na ulegevu. Draxton akawa amekaa chini huku akipumua kwa njia ya kupuliza, naye Blandina akawa ametambua kwamba bila shaka ni shida ile ile iliyokuwa ikimtatiza mpenzi wake ndiyo iliyokuwa inamsumbua hata sasa. Akanyanyuka taratibu ili amfate hapo chini, lakini Draxton akamnyooshea kiganja kumzuia asimfate.

"Subiri..." Draxton akasema.

Blandina akabaki kumtazama tu.

Draxton akajinyanyua na kupiga goti moja chini, huku bado akiendelea kuutafuta utulivu Kwa pumzi zake.

"Draxton hiki ni nini? Na wewe umekuwa kama Edward wa Twilight? Una shida kama za ma-vampire au?" Blandina akauliza.

Draxton akamtazama kwa macho yake makini.

"Drax...."

Blandina akamwita hivyo na kuanza kumsogelea, akiwa bila nguo hata moja mwilini mwake, lakini Draxton akarudi nyuma zaidi.

"Bado ninahitaji mazoezi zaidi Blandina... usijali... ninajua nitafanikiwa..." Draxton akasema.

"Mazoezi gani? Mbona sikuelewi?" Blandina akauliza kwa kutatizika.

"Hhh... am sorry. Ni ngumu kuelewa, lakini ipo siku nitakuelezea Blandina... trust me," Draxton akamwambia kwa hisia.

Blandina akawa anamwangalia juku akitikisa kichwa kwa njia ya kufadhaika, naye Draxton akasimama na kuanza kuondoka huku akiwa na huzuni usoni. Alipoufikia mlango akasema tu kwamba angemtafuta baadaye, kisha akaondoka hapo. Mwanamke akabaki tu ndani kwake akiwa kama alivyozaliwa, na akijihisi vibaya sana. Akakaa kwenye sofa lake tena na kuanza kukumbukia kilichokuwa kimetokea muda mfupi nyuma. Kiukweli hali hii iliteteresha sana, kwa sababu alishindwa kujua ikiwa huu ulikuwa mchezo wa kitoto au maigizo yasiyokuwa na faida yoyote.

Kwa vyovyote vile, Blandina alikuwa ameanza kuchoshwa mno na tabia hiyo, na sasa akawa ameamua kujua na kutafuta ukweli yeye mwenyewe kwa njia yoyote ile ili aweze kuelewa kilichomharibia raha ya pendo lake kilitokana na nini.

β˜…β˜…

Siku hii ya Jumapili iliendelea kusongesha muda mpaka ikafika usiku. Nyumbani kwa wanandoa Efraim Donald na Namouih, walikuwa wametulia ndani tu wakiongea kuhusiana na mambo ya hapa na pale, na Efraim alipenda sana kumwonyesha mke wake vituko vya mitandaoni kwa simu yake. Namouih alijitahidi sana, sana, sana kuonyesha kwamba yuko sawa kabisa, lakini dhamiri yake ilikuwa ikimsunta kila mara alipotendewa kwa njia nzuri na mume wake na kukumbukia kwamba siku hiyo alikuwa ametoka kufanya usaliti. Kwa upande wake Efraim, maigizo aliyokuwa akifanya kuonyesha ni kama haelewi somo yaliendelea kumweka mke wake gizani ili asijue aina ya mtu aliyekuwa, na kwa kadiri kubwa yaliendelea kufanikiwa.

Wakawa wameshamaliza kula chakula cha jioni ilipotimia mida ya saa tatu, na sasa wakawa pamoja sebuleni wakitazama tamthilia pamoja. Namouih alikuwa akisubiri ujumbe wowote ule kutoka kwa Draxton, lakini mpaka kufikia wakati huu hakuwa amepokea ujumbe wowote ule. Akaendelea kujitahidi kujipa utulivu, lakini bado kichwa chake kiliendelea kuwashwa tu na tukio lililowapata yeye na mwanaume huyo siku hii, na kiukweli ingeweza kusemwa kwamba ni utamu aliokuwa ameonjeshwa leo baada ya kipindi kirefu ndiyo uliokuwa ukimchanganya. Yaani alihisi ni kama asingeweza kuvumilia tena mpaka ajue nini kinaendelea upande wa Draxton, hivyo akachukua simu yake na kuelekea chumbani; akiwa amemwambia Efraim kwamba anatangulia kupumzika.

Mwanamke akaingia ndani ya chumba chake cha ndoa, akiwa amesindikizwa na paka wake wa kufugwa, yaani Angelo, naye akaketi kitandani na kufungua simu yake. Akaitafuta namba ya Draxton, kisha akataka kumpigia lakini akasita kwanza. Ni ule woga wenye kusisimua sana uliomwingia kwa kujiona kama mtu mbaya lakini bado sehemu fulani ndani ya moyo wake ikimsukuma kufurahia jambo hilo, na kwa sekunde chache akafumba macho tu akiwaza kwamba labda kumshtua Draxton haikuwa jambo sahihi. Hakuwa hata amemfikiria Blandina, rafiki yake kipenzi, na ndiye ambaye alikuwa amemtendea kwa usaliti pia kwa sababu ya alichokifanya pamoja na mpenzi wake. Alijaribu kuziepuka fikira za hatia na kujiachia afanye kile ambacho moyo wake ulikuwa unamsukuma kufanya, na kwa haraka akatuma ujumbe mfupi kwa Draxton.

'Hey'

Namouih akafunika mdomo wake kwa vidole vyake, akijihisi ni kama amegeuka kuwa msichana mdogo mwenye kufanya vituko tu ingawa anaelewa kuna madhara. Akaanza tu kupitia picha mbalimbali kwenye simu yake alizokuwa ametunza, huku kihalisi nia yake ikiwa ni kusubiria jibu kutoka kwa Draxton, na baada ya dakika chache akalipata.

'Hey'

Ulisomeka hivyo ujumbe kutoka Draxton, na Namouih akatabasamu kidogo na kuibana midomo yake akiwa ameingiwa na msisimko wa furaha.

Ujumbe wa pili ukaingia kutoka kwa Draxton uliosomeka, 'Uko poa?'

Namouih akawa anajiandaa kujibu pale simu yake ilipoanza kuita. Tabasamu lake lilififia ghafla baada ya kuona kwamba mpigaji alikuwa ni rafiki yake, Blandina, na kwa sekunde chache akabaki kuitazama tu mpaka ilipokata. Zile hisia za kujihisi vibaya zikaanza kumwingia tena, lakini baada ya sekunde chache kupita bila ya Blandina kupiga tena, Namouih akaamua kurudisha umakini wake kwa Draxton.

Namouih akamwandikia, 'Yeah,' akiwa anajibu ule ujumbe wa kama yuko poa.

'Nilikuwa nawaza juu yako' Draxton akatuma ujumbe huo.

'Kw nn?'

'Ikiwa tu ulifika salama'

'Mbon hukunitafut?'

'Sikujua kama ingekufaa'

'Kwnn isinifae?'

'Kwa sababu bado sina uhakika ni jinsi gani ungependa tuendelee na suala letu Namouih'

'Hofu yako iko wap Max?'

'Sihitaji kusema Namouih, najua unaelewa nachomaanisha'

Namouih akatulia kidogo, kisha akamwandikia, 'Ndiyo naelewa. Lakini huna haja ya kuhofia lolote.'

'Hofu yangu iko juu yako Namouih. Bado nahisi ni kama utaumia.'

'Unawaz san juu yangu et?'

'Kuliko unavyoweza kufikiri.'

Namouih akatabasamu kwa kupendezwa na kauli hiyo. 'Usijali nitakuw sawa,' akamwandikia.

'Sawa.'

'Ulirudi huku mapem?'

'Ndiyo, sikuchelewa kutoka kule.'

'Umeonana na Blandina?'

Baada ya Namouih kuandika na kumtumia ujumbe huo, akaanza tena kujilaumu kwa nini aliuliza jambo hilo.

'Ndiyo nimeonana naye,' Draxton akajibu.

'Okay,' Namouih akaona akatishe kumzungumzia rafiki yake.

'You okay?' Draxton akauliza.

'Ndiyo, am okay. Kesho kazin'

'Ndiyo, mapema. Baada ya kazi wafanya nini?'

'Sitakuw na mamb mengi sana.'

'Okay sawa.'

'Wewe je?'

'Sitakuwa na mambo mengi pia. Bado kuna sehemu kadhaa za ile nyumba nazohitaji kufix so nitakwenda huko mida fulani.'

Namouih akatabasamu kwa mbali na kuandika, 'Ungepend nije kukusaidia?'

'Itapendeza,' Draxton akajibu.

Namouih akaanza kuivuta-vuta midomo yake kwa njia ya madaha, akiwa ameingiwa na msisimko hata zaidi, naye akaandika, 'Hakikisha unaandaa msos wa nguvu.'

'Usijali, utaukuta,' Draxton akamwandikia.

'Kweli?'

'Ndiyo. Ni ahadi kutoka kwa mzee mwenye miaka 95. Haitavunjika'

Namouih akacheka kidogo, kisha akamwandikia, 'Sawa nitaona babu.'

Namouih alifurahia sana jumbe hizi fupi, kwa sababu ya kuelewa kwa upana kile ambacho kilimaanishwa na haya yote. Matarajio yake ya kile ambacho kingetokea akikutana na Draxton tena yalimfanya akumbuke namna walivyopeana mapenzi siku hiyo, na badala ya kuhisi hatia kwa wakati huu alikuwa ameridhia furaha aliyoihisi kutokana na jambo hilo. Ni wazi alianza kumwelewa sana mwanaume yule. Draxton akawa amemtumia ujumbe uliosomeka 'Unafikiri mida gani utakuwa umefika huko kesho?' na kabla Namouih hajajibu, mlango wa chumbani hapo ukafunguliwa na moja kwa moja Efraim Donald kuingia. Namouih akaendelea kuonyesha utulivu tu, huku akiitoa sehemu ya kutumiana ujumbe na kuibadili kwenda kwenye picha.

"Nilifikiri utakuwa umeshalala..." Efraim Donald akasema huku akilielekea kabati.

"Hapana, nilikuwa napitia memory lane kidogo hapa," Namouih akasema.

Efraim Donald akatoa pensi ya kijani kutoka kabatini.

"Mechi imeisha?" Namouih akauliza.

"Wako half time," Efraim akajibu.

Wakati mume wake alipokuwa anabadili vazi lake, Namouih akarejesha simu yake sehemu ya kutuma ujumbe ili amjibu Draxton upesi.

"Una-chat na nani?" Efraim Donald akauliza.

Namouih akamwangalia mume wake na kuona kwamba aliuliza hivyo bila hata ya kumwangalia kabisa, naye akasema, "Si-chat. Ninaangalia picha za kumbukumbu."

Efraim akawa amemaliza kuvaa na kumtazama mke wake usoni kwa ufupi, kisha akatabasamu kidogo na kusema, "Sawa."

Namouih akaendelea kumwangalia kwa umakini.

"Ninaenda kumalizia mechi, usinisubirie, we' usingizi ukikuita lala tu mama," Efraim akasema.

Namouih akaachia tabasamu na kuweka uso mzuri kama kukubali, naye Efraim akaangalia chini kidogo, kisha akaondoka ndani hapo. Tabasamu la Namouih likafifia upesi kutokana na hali hiyo iliyomtatiza kiasi, kwa sababu mume wake alionyesha udadisi fulani hivi usio wa moja kwa moja; jambo lililomwambia mwanamke huyu kwamba alihitaji kuwa mwangalifu zaidi. Akajibu ujumbe wa Draxton kwa kusema angekwenda kule msituni mida ya mchana sanasana, bila kugusia kwamba mume wake tayari alikuwa amerudi, kisha akamtakia Draxton usiku mwema na kuanza kuzifuta jumbe zote walizotumiana kwa usiku huo. Akaiweka simu pembeni na kuinamisha uso wake juu ya viganja vyake alivyokunja kwa kuegamiza mikono kwenye mapaja yake, akiwa anafikiria vitu vingi.

Kama ni raha aliyokuwa akitamani kuipata kutoka kwa mume wake sasa alikuwa akiipata kutoka kwa mwanaume mwingine, tena kwa njia ambayo aliipenda sana. Huo ulikuwa usaliti kwa ndoa yake lakini pia usaliti mkubwa kwa rafiki yake wa karibu kwa kuwa mwanaume huyo alikuwa mpenzi wake. Haingekuwa rahisi kupuuzia uzito wa jambo hilo, lakini bado moyo wake uliridhia kuliendeleza. Akayatikisa mawazo mabaya kutoka kichwani kwake na kuamua kwenda tu kujimwagia ili alale mapema kabla hata ya mume wake kurejea chumbani.


β˜…β˜…β˜…


Namouih alikuja kuamka na kujikuta yupo ndani ya chumba hicho, lakini akiwa amesimama pembezoni mwa kitanda chake cha ndoa. Chumba kilipendeza sana, kikiwa na mapambo mengi yenye rangi nyekundu kama maua, maputo, vitambaa, midoli, na taa zenye kutoa mwanga wa kumeremeta kwa kujirudia. Harufu nzuri ilitawala ndani hapo, naye akajiangalia mwilini na kuona akiwa amevaa nguo nyekundu pia iliyokuwa kama gauni fupi lililoacha mapaja na mgongo wake wazi. Haikuchukua muda mrefu kwa mwanamke huyu kutambua kwamba alikuwa anatoa, na hii ilionekana kuwa ndoto nzuri sana kwa sababu kuna hisia fulani nzuri iliyokuwa ndani ya moyo wake kutokana nayo.

Mlango wa chumba hicho ukafunguka, na kwa matarajio yake alidhani ni mume wake ndiye ambaye angeingia, lakini haikuwa hivyo. Aliyeingia ndani hapo hakuwa mwingine ila Draxton mwenyewe. Namouih alimtazama kwa macho yenye uvutio mwingi sana. Draxton alipendeza kwa kuvalia suti nyeupe, na alikuwa ameshikilia chupa nene ya wine mkononi huku akimwangalia Namouih kwa upendo. Namouih akatabasamu kwa furaha, kwa sababu alielewa kuwa ndoto hii ingempatia kitu kitamu sana alichokuwa na hamu nacho kwa hali ya juu. Mwanaume huyo akaanza kumwelekea taratibu huku akitabasamu mpaka alipofikia karibu yake, na Namouih akamsogelea zaidi.

"Happy anniversary."

Draxton ndiye aliyesema maneno hayo, lakini sauti ilikuwa ya Efraim Donald.

Namouih akakunja uso kimaswali na kusema, "Sikujua anniversary yetu imewadia."

"Haihitaji kuwadia mke wangu, maana kila siku kwangu inakuwa ni kama nimekuoa upya. Kwa hiyo kila siku ni anniversary yetu," Draxton akasema, ikiwa ni sauti yake sasa.

Namouih akatabasamu kidogo na kuuliza, "Tulifunga ndoa lini?"

"Siku niliyokuoa," akajibu Draxton, sauti ikiwa ya Efraim.

Namouih akaangalia chini akiwa kama anajaribu kutafakari vitu hivi, naye "Draxton" akakinyanyua kidevu cha mwanamke huyu kwa kidole kimoja ili amtazame, na Namouih akamwangalia machoni.

"Nakupenda Namouih," akasema Draxton.

"Nakupenda pia," Namouih akajibu.

"Nakupenda Namouih," Draxton akasema hivyo tena, lakini sauti ikiwa ya Efraim Donald.

Namouih akatulia kidogo, kisha akasema, "Nakupenda pia."

"Draxton" akatabasamu, kisha akauliza, "Unampenda nani, Namouih?"

"Wewe," Namouih akajibu bila kusita.

"Wewe ni wa nani, Namouih?" ikauliza sauti ya Efraim.

"Mimi ni wako," Namouih akajibu kilegevu.

"Kwa nini moyo wako umegawanyika?"

Swali hilo aliliuliza Draxton, lakini wakati huu sauti yake ilikuwa imechanganyikana na sauti ya Efraim Donald. Kidogo hii ilimtia hofu Namouih kwa sababu sauti hiyo ilitisha, na alipotaka kurudi nyuma, "Draxton" akaishika shingo yake kwa nguvu sana na kuanza kumkaba. Namouih akaushikilia mkono wa mwanaume huyo, akijaribu kuuvuta pia ili usiendelee kumkaba namna hiyo lakini ikashindikana. Alikabwa kwa nguvu sana mpaka akahisi namna ambavyo mishipa yake ya kooni ilivyopasukia ndani na kusababisha aanze kutoa damu ndani ya mdomo mpaka nje. Aliumia sana.

"Hauwezi kupenda wanaume wawili kwa wakati mmoja Namouih!"

Sauti ya Efraim Donald na ya Draxton zilichanganyikana na kumwambia hivyo mwanamke huyu, na Namouih alikuwa akipata taabu sana kupumua na kubaki amekazika kichwa kwa maumivu aliyohisi. "Draxton" akamgeuzia kitandani na kumtupa hapo bila kuiachia shingo yake, akiendelea kumkaba huku anamwangalia kikatili, na ile Namouih alipofumba macho yake kwa ufupi na kuyafumbua, akakuta sura ya anayemkaba ikiwa ya mume wake, na si Draxton, huku macho yake yakiwa ya blue kama macho ya badiliko la Draxton. Mume wake alikuwa anamkaba huku akimwangalia kwa ukatili mwingi, na Namouih aliendelea kuhangaika sana, akili yake ikitamani aamke haraka ili aepukane na ndoto hii iliyokuwa.....

Namouih akashtuka sana na kunyanyua uso wake kutoka kitandani, mapigo ya moyo yakikimbia kwa kasi, na pumzi zake zikiwa nzito. Hatimaye akawa ameamka, ikiwa ni asubuhi sasa. Hakuwa hata amepiga kelele kutokana na ndoto hiyo, kwa kuwa hofu aliyohisi ilikuwa ya ndani zaidi kwenye moyo wake, naye akafumba macho na kuulaza tena uso wake ili ajaribu kupata utulivu. Ingawa hiyo ilikuwa ni ndoto tu, alijua ilichochewa na mambo halisi yaliyokuwa yanaendelea katika maisha yake. Alihisi ilisababishwa na hofu yake kuelekea wazo la ni nini kingetokea endapo kama mume wake angejua kwamba amemsaliti na mwanaume mwingine, bila kutambua kihalisi kwamba kuna jambo fulani muhimu ambalo ndoto zake zilikuwa zinajaribu kumwonyesha.

Aliponyanyua uso wake tena kuangalia kitandani hapo, hakumwona mume wake. Akajiuliza ikiwa tayari Efraim Donald alikuwa amekwenda kazini, na ndipo akajigeuza na kushtuka kiasi moyoni. Hapo pembeni yake, aliketi mume wake, akiwa ameishikilia simu yake Namouih huku akitazama jambo fulani kwa umakini. Namouih aliingiwa na wasiwasi mwingi sana kwa kujiuliza ni jambo gani ambalo mume wake angekuwa anaangalia hapo, na ndipo Efraim Donald akamgeukia Namouih na kumtazama usoni kwa macho makini sana.



β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

ITAENDELEA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…


Usikose sehemu za mwendelezo wa hadithi hii kali ya CHANGE. Ni story nzuri na ndefu sana. Waweza ipata nakala yote kwa gharama nafuu sana. Karibu WhatsApp au kwa E-mail yangu.

WhatsApp no: +255 678 017 280
 
CHANGE

Story by Elton Tonny

Urafiki, Familia, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Ukatili, Mauaji, Mambo yasiyotazamiwa, Mambo yenye kuhofisha

R-rated 18+

Enjoy!

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…


Namouih akabaki kumtazama tu mume wake usoni, akiwa ameingiwa na wasiwasi mwingi sana kwa kujiuliza ni jambo gani ambalo angekuwa ameona humo. Wazo la kwamba labda Draxton alikuwa ametuma ujumbe asubuhi hiyo na yeye Efraim akauona halikuwa mbali na akili yake, lakini akajitahidi kujikaza ili asimwonyeshe mume wake itikio la mshtuko. Efraim Donald akanyanyuka na kuanza kusogea usawa wa kitanda upande aliolala mke wake, huku akimwangalia kwa njia ya kawaida wakati huu.

"Vipi? Umeamkaje?" Efraim akauliza.

"Safi tu," Namouih akasema huku akimwangalia machoni kwa makini.

"Hauendi kazini leo?" Efraim akauliza.

"Naenda, kwani sa'hivi saa ngapi?"

"Saa tatu. Umelala mapema jana, ila umeamka umechelewa... uko sawa?"

"Niko sawa ndiyo. Ninaenda kazini... labda ilikuwa tu uchovu... ndiyo maana."

"Mmm..."

Efraim Donald akatoa mguno huo, na Namouih akawa anamwangalia tu kwa umakini.

"Kuna kitu hakiko sawa Namouih," Efraim akamwambia kwa umakini.

"Unamaanisha nini?" Namouih akauliza.

Efraim akanyanyua simu ya mke wake na kumwonyesha jambo fulani.

Namouih alihisi moyo wake unataka kupasua kifua chake kwa sababu ya wasiwasi mwingi kuongezeka ndani yake, hata akashindwa kuitazama simu na kubaki amemwangalia tu mume wake.

"Ulisahau kufanya nini jana?" Efraim akauliza.

Namouih alipoitazama simu yake, akaona ikiwa imewekwa upande wa ujumbe, na namba ya mtumaji ikiwa ni ya Zakia, mama yake.

"Oh noo..."

Namouih akasema hivyo kwa kusikitika, naye akakaa vyema na kuichukua simu yake. Hapo kulikuwa na jumbe kumi kutoka kwa mama yake, akimwambia namna alivyovunjika sana moyo kwa kuwa hakumtumia pesa kama alivyoahidi jana. Ingawa Namouih aliweza kupata utulivu wa kihisia kwa sababu ya hali hii kuwa tofauti na alivyohofia, bado akaingiwa na hisia za hatia kwa kuwa ni kweli alimsahau mama yake ilhali alimwahidi kumtumia pesa hizo. Ni kwamba ujio wa ghafla sana wa Efraim jana ulifanya akapoteza kabisa wazo la kumtumia mama yake pesa.

"Namouih, Zakia analalamika sana. Jitahidi basi uwe mwangalifu maana kwa vitu kama hivi anaweza kuanza kufikiri kwamba labda hatumjali. Nisingependa ahisi namna hiyo hasa kwa sababu sherehe inakaribja, kwa hiyo liweke hilo sawa, eti?" Efraim Donald akasema.

Namouih hakumwangalia, bali akatikisa kichwa kukubali huku akiitazama simu yake.

"Okay, I'm off. Tutaonana baadaye," Efraim akasema.

"Sawa," Namouih akajibu.

Efraim akawa ameanza kuondoka, kisha akasimama na kusema, "Oh, gari limeletwa."

Namouih akamwangalia na kuuliza, "Gari?"

"Premo yako. Imeshamalizwa, imeletwa leo asubuhi. Ukitaka kuanza kuitumia tena...."

"Oh sawa, sawa, asante. Asante Efraim," Namouih akamkatisha.

Efraim Donald akatikisa kichwa na kuondoka hapo ili aelekee kazini.

Namouih alibaki akitafakari hali aliyoamkia asubuhi hiyo kwa kina. Alijiuliza sana ikiwa mume wake alikuwa anajaribu tu kucheza na akili yake au jumbe za Zakia ndiyo lililokuwa dhumunj kuu la kuishika simu yake. Hawakuwahi kunyimana simu hata kidogo, na tena kila mmoja alifahamu neno siri la kufunga na kufungua simu zao wote kwa sababu waliaminiana, lakini wakati huu Namouih alielewa kuwa mambo yalikuwa yameanza kubadilika kwa upande wake, hivyo ingekuwa muhimu kuhakikisha anaweka njia zote za kujihami kwa mtindo ambao usingemshtua mume wake. Hakukuwa na jumbe yoyote kutoka kwa Draxton, hivyo Namouih akapata ahueni na kuamua tu kumpigia mama yake ili aombe radhi kwa sababu ya jana.

Zakia alilalamika kwa njia ya kudeka akisema binti yake hakufanya vizuri kabisa, lakini Namouih akamtuliza kwa kumwambia alitingwa kutokana na kuwa na mambo mengi sana akilini. Akamuuliza mama yake kwa nini hakumtafuta baadaye tena hata kumkumbusha, naye Zakia akasema simu yake ilizima jana na kwa sababu hawakuwa na umeme alishindwa kumtafuta kwa kuwa ulirudi usiku sana. Hivyo, Namouih akamwambia angemtumia kiasi alichoomba jana lakini mara mbili, yaani kingine achukue kama pole, naye Zakia akafurahi sana. Wakaagana baada ya hapo, kisha Namouih akaelekea bafuni kujisafisha ili aanze maandalizi ya kuelekea kazini.

β˜…β˜…

Muda mfupi baadaye, Namouih akawa amefika kwenye kampuni yao na kukuta kazi zikiendelea kama kawaida. Alikuwa amependeza kwa kuvalia nguo fulani ya kijani yenye kitambaa kigumu chenye kung'aa (kama satini), iliyokuwa kama gauni pana lakini lililoishia magotini, nalo lilizungukwa na urembo mwingi wa rangi ya dhahabu kuzungukia mikono na shingoni, huku sehemu ya kifua likiacha uwazi kidogo kuonyesha utuni mzuri wa matiti yake. Nywele zake alikuwa amezitengeneza kwa mtindo mzuri; za kusukwa zikiwa upande mmoja wa kichwa na zake laini zikiufunika upande mwingine wa kichwa chake kutokea juu, akionekana kuwa bonge moja la sista duu la kishua! Usoni kama kawaida alijiremba kwa kadiri inayofaa, midomo yake akiipaka lipstick ya rangi ya zambarau iliyopauka na kung'aa. Alivaa mkufu mweupe shingoni, hereni ndefu pia na pete za dhahabu vidoleni, na miguuni alivaa viatu virefu vyeupe. Alipendeza sana.

Baada ya kuikaribia ofisi yake, akakuta kukiwa na watu wengi kiasi wakiwa wameketi kwa kumsubiri, bila shaka wakiwa ni wahusika wa kesi fulani ambazo angetakiwa kushughulika nazo. Akawapita tu bila kuwasalimu na kuingia ofisini moja kwa moja, naye akaelekea mezani kwake na kuketi. Akachukua simu yake na kuangalia muda, ikiwa ni saa tano kasoro sasa, naye akawaza kumtumia Draxton ujumbe wa salamu. Lakini bado akili yake ilikuwa imetatizwa sana na kilichotokea leo asubuhi baada ya yeye kuamka na kukuta mume wake ameshika simu yake, na hivyo akawa anawaza labda hata amemwekea mtego wa kunasa jumbe anazotumiana na watu. Yote hayo yalikuwa ni mawazo tu ya kuhakikisha anakuwa mwangalifu, na kwa kuona hata Draxton hakuwa amemtafuta ikawa ni jambo zuri kwa sababu hata yeye alitaka wawe makini.

Kwa hiyo akaghairi kutuma ujumbe na kuamua kuanza kushughulika na kazi za hapo, na jambo la kwanza ingekuwa kujua watu hao hapo nje wanahitaji nini. Hakuwa hata na uhakika kama Blandina ameshafika kwa sababu akili yake haikutaka hata kumruhusu amwone, maana hakujua ni namna gani angemwangalia rafiki yake wakati huu aliokuwa ameanza kutoka kimapenzi na mpenzi wake. Ni wakati huo huo tu amemuwaza ndipo mlango wa ofisi yake ukafunguka na Blandina mwenyewe kupita ndani. Kwa mara ya kwanza kabisa Namouih alihisi msisimko wa woga kumwona rafiki yake badala ya furaha, naye akawa anamwangalia huku akijitahidi kuzituliza hisia zake. Ni wazi hakuwa mnafiki mzuri.

Blandina alikuwa amevalia suti ya kike yenye suruali pana iliyochoresha umbo lake vizuri, na nywele zake za mawimbi alizibana kwa nyuma. Koti lake alilifungia kifungo kimoja tu kuonyesha blauzi nyeupe kwa ndani iliyoachia sehemu ya juu ya matiti yake ionekane kwa mbali, na alivaa viatu virefu vyeusi. Alikuwa amebebq kablasha lenye makaratasi kadhaa, naye akasogea mpaka usawa wa meza yake Namouih huku akitabasamu.

"Vipi?" Blandina akauliza.

"Safi," Namouih akajibu huku akitoa tabasamu hafifu.

"Uliamkia wapi?"

"Ahah... nimechelewa tu kuamka. We' umefika zamani?"

"Sana. Unaonaje... nimefanana na nani leo?" Blandina akauliza, akimaanisha namna alivyovaa.

"Mmm... kama Kim Nana wa City Hunter," Namouih akajibu.

"Ahahahah... kenyewe kembamba mno..."

Namouih akatoa tabasamu la kujilazimisha.

"Umependeza hivyo ulivyoziweka nywele," Blandina akamwambia.

"Asante, na we' uko bomba pia," Namouih akasema.

Blandina akatabasamu.

"Vipi hao watu?" Namouih akauliza.

"Yeah, kuna kesi kama kumi na moja hapa. Ufisadi ufisadi, wanataka uwahudumie..."

"Wote hao? Ina maana wamekosa wanasheria wengine hapa?"

"Ndiyo wanakutaka wewe tu. Halafu wanazo. Kama huyo mwenye suti nyekundu ndiyo atatoa bonge la cash... Edward kawaelekeza wote kwako kwa hiyo inabidi kuanza kazi," Blandina akasema.

"Aisee!" Namouih akashangaa.

"Siyo zote zitatupeleka mahakamani, na zingine nitakusaidia kusuluhisha. Mafaili yao haya hapa, nimeyapitia na kupangilia kwa hiyo we' teleza tu... najua hii ni keki ndogo sana ila italipa mbaya," Blandina akasema.

Namouih akatabasamu na kupokea kablasha hilo kutoka kwa Blandina.

"Nimepata msichana mwingine wa kazi, anakuja leo," Blandina akasema.

"Ahaaa... sawa. Nani amekutafutia?"

"Mama."

"Una CV yake huyo msichana au... yasije yakatokea yale yale ya Hamida."

"Hamna, namjua. Ni mtoto wa jirani yetu pale tulipokuwa tunaishi zaman. Sa'hivi amekua, ila kazi ngumu kupata so ameona asogee huku ili atafute."

"Sawa."

"Umeshakunywa chai?" Blandina akauliza.

"Ndiyo, nimekunywa home."

"Me, ndiyo naenda kunywa. Donald anasemaje?"

"Yupo tu. Kazi juu ya kazi kama kawaida."

"Ahahah... sawa."

"Vipi wewe? Draxton na wewe... mko poa?" Namouih akauliza bila kumwangalia.

"Yeah tuko poa... ahahah... yaani mambo yetu bwana, we' acha tu..."

"Vipi kwani?" Namouih akauliza na kumtazama.

"Ah, sidhani kama hii itakuwa sehemu sahihi kuzungumzia..."

"We' niambie. Hakuzingui siku hizi?" Namouih akawa anachimba zaidi.

"Ahahahah... bado bado. Si unakumbuka ile shida yake anasema huwa inamzuia kuni...."

"Yeah, yeah, nakumbuka..."

"Well, jana Draxton amenipa oral," Blandina akasema hivyo kwa njia fulani ya maringo.

Namouih akamtazama usoni kwa ufupi, kisha akaanza kucheka kwa kujilazimisha.

"Ahahahah... nini sasa?" Blandina akauliza.

"Ahah... hamna... ni kwamba tu... yaani, umepewa oral kwa hiyo unaona kama ushindi wa hali ya juu?" Namouih akauliza kikejeli.

"Ndiyo Nam. Draxton alijitahidi sana jana. Sijajua anasumbuliwa na nini, lakini alifika kule ambako hakuwahi kufika kabla, na ananiahidi atafanikiwa tu ili aje kunipa kilicho bora. Kinachomsumbua kilimpata jana pia, ila kwa kidogo alichonipa nilifurahia sana... hakujua tu," Blandina akaongea kwa hisia.

Namouih akaangalia chini, akiwa ameingiwa na hali fulani ya wivu ndani ya moyo wake ingawa yeye ndiyo alikuwa anapata zaidi ya kile ambacho rafiki yake alikuwa amepewa.

"Ninataka nianze kumchunguza vizuri zaidi... labda kwa njia moja au nyingine ninaweza kumsaidia ingawa hataki kunishirikisha," Blandina akasema.

Namouih akamtazama na kusema, "Sawa. Hongera. Na vizuri pia uki... msaidia... ngoja nianze kuzichangamkia hizi."

"Oh, sawa ahah... badae'," Blandina akasema na kuanza kuondoka.

Namouih aliachwa akiwa na hali ya kukosa amani kwa kadiri kubwa. Hakuelewa kwa nini alihisi namna hiyo ilhali ni yeye ndiye aliyekuwa ameingilia kati kwenye mahusiano halali ya rafiki yake. Furaha ya Blandina kumwelekea mpenzi wake ilimfanya ahisi ni kama bado yeye hakuwa ametoshelezwa vyema kihisia, na uhitaji wake wa mapenzi kutoka kwa mwanaume yule ukaendelea kuongezeka tu katika njia yenye kumfanya ahisi ni kama yeye pekee ndiye aliyestahili penzi la Draxton. Akajitahidi kuyafutilia mbali mawazo yenye kupelekea wivu wa mapenzi ndani yake ili aendelee kufurahia kile ambacho angekipata kutoka kwa Draxton, na kwa kuwa wangekutana baadaye tena, akaanza kushughulika na kazi zake upesi ili awahi kwenda kulipata penzi motomoto la Mnyama-Draxton.

β˜…β˜…

Upande wake Efraim Donald. Mwanaume huyu alikuwa ofisini kwake wakati huu, akiwa ametulia tu na kushughulika na masuala ya kikazi kwa utulivu. Lakini bado akili yake ilikuwa ikitafakari mambo aliyohitaji kufanya mbeleni ili dili lake la mali lifanikiwe, na ili aweze kubaki na mke wake pekee. Ila kwa kujua kwamba sasa hivi Namouih alianza kuondolewa kimya kimya kutoka kwenye kifungo chao cha ndoa kulimtatiza sana na si kwa sababu tu ya mipango yake, bali kwa sababu alimpenda. Kuigiza kwake kwamba hajui lolote kulimpa faida ya kumfanya mke wake asihisi lolote lile, na hivyo angeweza kumkamata kwenye usaliti wake kwa njia fulani ya kificho ili aweze kummaliza aliyekuwa anatoka naye.

Sasa akawa amekaa tu kwa utulivu akisubiri jambo fulani, na kwa kuwa halikuwa limefika bado akaamua kujaribu kutuliza hisia zake kwa kadiri ambayo ingemfaa. Akampigia simu msaidizi wake wa kazi, naye akamwambia aingie ofisini ili ampatie kazi fulani ya kufanya. Msaidizi wake hakukawia, yule mwanadada aliyeitwa Lucy, naye akaingia ofisini humo na kudogea mpaka mbele ya meza yake Efraim na kusimama kwa njia ya heshima. Mwanamke huyu alikuwa mweupe, mwenye urefu wa wastani kwa mwanamke na sura nzuri pia. Alivaa kwa unadhifu sana wa kiofisi, na mara nyingi alipendelea kuvaa ushungi kichwani kama mwanamke wa kiislamu ingawa hakuwa mwislamu, hata sasa. Alikuwa na umri wa miaka 27, na alibeba umbo zuri sana kwa nyuma lililovutia macho ya wengi.

Efraim Donald akawa anamwangalia kwa njia ya kawaida, naye Lucy akasema, "Unahitaji nikusaidie na jambo fulani boss?"

Efraim akaangalia mezani kwake, kisha akanyoosha mkono wake mpaka kiganja chake kilipogusa kifaa fulani hivi cha kioo, kilichokuwa kama pambo, halafu akaanza kukisukuma taratibu kuelekea upande alioketi yeye. Lucy akawa anamwangalia tu mpaka Efraim alipokidondosha chini makusudi, nacho kikapasuka. Mwanaume huyu akamwangalia Lucy kwa yale macho ya 'njoo ufanye kazi yako,' naye Lucy akatoka hapo alipokuwa amesimama na kuanza kwenda upande alioketi Efraim ili apasafishe pale chini. Lakini alipofika usawa wake, akasimama kwanza na kumtazama kwa umakini. Efraim alikuwa amekaa kwa njia ya kujiachia kwenye kiti, huku sehemu ya zipu ya suruali yake ikiwa wazi, na hapo mashine yake iliyosimama vyema ikionekana wazi mbele ya macho ya mwanamke huyo. Lucy akamtazama Efraim Donald machoni, naye Efraim akamtazama pia, kisha mwanamke huyo akaachia tabasamu la haya kiasi.

Wawili hawa walijuana. Sana. Hii haikuwa mara ya kwanza Lucy kuiona mashine ya mwajiri wake, na tena alikuwa ameshaikalia na kusuguliwa nayo mara nyingi tu. Efraim alifanya mchezo huo na msaidizi wake kwa muda mrefu, akiwa kitulizo chake cha kihisia kwa hapo wakati wowote aliomhitaji, naye Lucy aliwajibika vizuri kwa 'boss' wake kwa kuwa kwenye suala la pesa Efraim hakuwa mchoyo kwake. Hivyo, mwanamke huyo akamfata taratibu na kusimama mbele yake, kisha akainama kumwelekea kwa madoido huku akiyashika mapaja ya jamaa. Nyuso zao zikiwa kwa ukaribu sana sasa, Efraim akatoa ulimi wake, naye Lucy akautoa wake na wote wakaanza kulambana kwa kucgezesha ndimi kama nyoka. Efraim akalipiga kwa nguvu sana kalio la Lucy, na mwanamke huyo akaguna kidogo na kisha kupiga magoti chini ya miguu ya 'boss' wake.

(.......).

Ni wakati huu ambao mwanamke huyo alikuwa akiendelea kumpa Efraim penzi hilo ndipo simu ya jamaa ikaanza kuita. Ilikuwa mezani, naye Efraim akaivuta na kuangalia mpigaji, kisha akapokea na kusema "njoo." Lucy alisikia, lakini akawa hajaelewa kikamili 'boss' wake alimaanisha nini. Ndipo mlango wa ofisini hapo ukafunguliwa na moja kwa moja akaingia Suleiman ndani hapo. Lucy akaitoa mashine ya Efraim mdomoni mwake kwa kuingiwa na wasiwasi kiasi, lakini Efraim Donald akaushika uso wake na kutazamana naye machoni.

"Usijali mpenzi, hana shida. Wewe endelea."

Efraim akiwa amemwambia maneno hayo ili kumtuliza, Lucy akarudia zoezi lake taratibu, huku sasa Suleiman akiwa amefika mbele ya meza na kusimama. Alikuwa amebeba kifaa kidogo mkononi kama tablet, naye akawa anajaribu kupuuzia kilichokuwa kinaendelea hapo na kutulia kama kikaragosi mtiifu. Lucy akaendelea tu, naye Efraim akawa anatoa sauti za raha bila hofu yoyote ile.

(........).

(........).

Efraim, akiwa ameridhika na huduma hii, akakinyanyua kidevu cha Lucy ili amtazame na kumwambia, "Kazi nzuri sana. Zawadi yako nitakupa baadaye. Nenda mama."

Lucy akanyanyuka na kuanza kuondoka bila kumwangalia Suleiman usoni, lakini alipotazama usawa wa suruali ya mwanaume huyo akaona kwamba alikuwa amevimbisha kwa ndani, naye akaondoka hapo huku akitabasamu.

Efraim akairudisha mashine yake ndani ya suruali na kumuuliza Suleiman, "Vipi? Imekwendaje?"

"Vyema. Nimeipachika kama ulivyoagiza," Suleiman akajibu.

Akampatia Efraim kifaa kile, naye akakipokea na kukiwasha. Kulikuwa na programu iliyoonyesha maeneo kwa njia ya ramani ya kijani, na kulikuwa na alama nyekundu iliyocheza-cheza ikiwa imetulia sehemu moja. Hiyo Ilikuwa inaonyesha mahali ambapo kifaa cha ufatiliaji kilikuwa, yaani tracking device. Efraim akaachia tabasamu hafifu na kumtazama Suleiman usoni.

"Nimekipachika sehemu ambayo hawezi kuona... kwa ndani sana," Suleiman akasema.

"Na kwenye lile lingine?" Efraim akauliza.

"Na lenyewe pia. Hata akiendesha Vanguard au Premo, yote nimeyawekea. Leo ameendesha Premo," Suleiman akajibu.

"Mmm... sawa."

"Hapo inaonyesha bado yuko kwenye kampuni yao, ila akiondoka tu lazima utamnasa," Suleiman akasema.

"Hakuna jambo la uhakika. Hawa viumbe wana akili sana siku hizi. Anaweza akaliacha gari hapo, akachukua uber, akaenda kwa hawala yake. Nahitaji uendelee kumwangalia. Na sasa hivi sitaki makosa ya kipuuzi, unanielewa?" Efraim Donald akasema.

"Ndiyo boss."

Efraim akatazama tena kifaa hicho kwa umakini. Hii ndiyo iliyokuwa hatua ya kwanza katika ufatiliaji wa nyendo za mke wake ili aweze kufichua siri yake kwa kumnasa mtu aliyekuwa anatoka naye kimapenzi nje ya ndoa yao. Alikuwa amemwagiza Suleiman apachike vifaa vya ufatiliaji kwenye magari ambayo Namouih alitumia ili kokote kule ambako angekwenda kisiri Basi waweze kumwona, na ndipo ajue namna ya kumkamata mbaya wake aliyetaka kuharibu ndoa na mipango yake ya nguvu za giza. Akampatia Suleiman pesa nyingi na kumwambia aondoke, lakini kwa leo atulie tu mpaka Efraim akimpa maagizo mengine, naye Suleiman akatii na kuondoka. Sasa mambo mengi yangepamba moto kwa sababu ni leo ndiyo Namouih angekwenda kukutana na mpenzi wake wa siri bila kujua kwamba alikuwa amewekewa kupe kwenye mkia, tena ndani ya mkia. Kile ambacho kingefuata baada ya hapo ndani ya akili yake Efraim kingeelezewa kwa njia moja tu; ukatili.

Je, atamgundua mpenzi wa siri wa mke wake? Na kama akigundua, ataweza kweli kumwondoa Draxton?



β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

ITAENDELEA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…


Usikose sehemu za mwendelezo wa hadithi hii kali ya CHANGE. Ni story nzuri na ndefu sana. Waweza ipata nakala yote kwa gharama nafuu sana. Karibu WhatsApp au kwa E-mail yangu.

WhatsApp no: +255 678 017 280
T
 
CHANGE

Story by Elton Tonny

Urafiki, Familia, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Ukatili, Mauaji, Mambo yasiyotazamiwa, Mambo yenye kuhofisha

R-rated 18+

Enjoy!

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

SEHEMU YA THELATHINI

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…


Tayari Namouih alikuwa amemaliza kushughulika na mambo mengi ya kikazi ilipofika mida ya saa nane mchana, na hakuwa amepumzika mpaka muda huo hata mara moja. Blandina alikuwa pamoja naye kumsaidia, na baadhi ya watu walihitaji huduma ya mwanasheria mkuu walipatiwa tarehe za kupewa suluhu zao walizohitaji na wengine kukabidhiwa kwa wanasheria wengine ndani ya kampuni hiyo kwa sababu hangeweza kushughulika nao wote kwa kipindi kifupi sana cha wakati. Ingawa Blandina alikuwa mkono muhimu sana wa Namouih katika kazi, zamu hii Namouih hakujihisi amani ya asilimia zote kuwa naye sambamba kutokana na kujua alimfanyia unafiki. Na tangu walipoagana jana na mpenzi wa rafiki yake, Namouih hakuwa amemtafuta Draxton wala Draxton kumtafuta yeye. Ilikuwa wazi kwamba wote walifanya mambo kwa umakini, ingawa Namouih hakudhani ikiwa mwanaume yule alijua kwamba mume wake amerudi.

Basi, imefika mida ya saa tisa, Namouih akamwambia Blandina kwamba sasa ndiyo anakwenda kule alikopanga kwenda leo, na bila shaka hangechelewa kurudi. Blandina alikuwa anataka watoke wote kama huko alikotaka kwenda ilikuwa ni kwenda kupata chakula lakini Namouih akasema haikuwa hivyo, bali alipanga kukutana na mtu fulani wa muhimu. Blandina akawa anataka kujua ni nani, ila Namouih akamjibu kwa njia ya kejeli kwamba ni siri na hangetakiwa kumwambia yeyote. Blandina mdada wa watu aliachwa gizani kabisa, naye akamwambia rafiki yake awe na safari njema na asichelewe kurudi ili wajumuike pamoja baadaye kule walikopenda kukaa kupata vinywaji kama kawaida yao, ingawa mara ya mwisho Blandina alipigwa kwa chupa huko.

Mwanasheria mrembo sana Namouih akaondoka kutoka kwenye kampuni hiyo, na sasa akawa mwendoni kuelekea kule msituni bila ya kuwasiliana na Draxton hata mara moja. Alijua tu kwamba ni lazima mwanaume huyo angekuwa huko, hivyo kufika kwake tu kulitosha maana alielewana naye kutokea usiku wa jana. Lakini pia akikumbukia kwamba asubuhi hii mume wake alikuwa ameishika simu yake, Namouih alihisi kwamba huenda Efraim alikuwa amefanya kitu fulani, labda kuweka mfumo wa ufatiliaji kwenye simu yake wa kukamata sms au vinginevyo, lakini hakudhani sana kwamba hiyo ilikuwa ndiyo ukweli wa mambo, na kuona kama ni yeye tu ndiyo alikuwa akepandwa na presha kutokana na aliyofanya. Hivyo akamtumia ujumbe mume wake akisema kwamba alikuwa amekwenda kuonana na yule rafiki yake daktari, yaani Salome, kama njia ya kujihami mapema. Hangetambua namna alivyokuwa anajipeleka katika hatari ya kuukamatisha mchezo wake na Draxton, kwa sababu gari lake lilikuwa limewekewa kifaa cha ufatiliaji, na mpaka sasa mume wake alikuwa akitazama kule ambako mke wake alikuwa akielekea akiwa kule kule kazini kwake!

Mwanamke huyu akafanikiwa kufika huko msituni kwa kuwa mwangalifu sana ili kuhakikisha hakuna yeyote aliyemfatilia, naye akalikuta gari la Draxton nje ya ile nyumba yake. Aliingiwa na msisimko mzuri sana kwa kutazamia mengi, naye akashuka na kuanza kuelekea upande wa mbele. Sehemu ya ardhi kuizunguka nyumba ilikuwa imesafishwa vizuri kutokana na uchafu mwingi uliosababishwa na mvua iliyoonyesha siku ya jana, na hata sasa wingu la mvua lilikuwa limeanza kutanda angani. Namouih akaenda moja kwa moja mpaka sehemu ya mlangoni na kuingia ndani, naye akatabasamu kwa furaha baada ya kukuta aina fulani ya mazingira ambayo hakuwa ametarajia.

Sehemu hiyo ya sebule ilikuwa imeachwa nafasi pana kwa masofa na meza kusogezwa pembeni zaidi kwenye usawa wa madirisha, na chini hapo katikati aliketi Draxton huku akimtazama mwanamke huyu kwa njia ya kawaida tu. Alikuwa amekaa kwenye kitu kama zulia (carpet) nene sana jekundu, lililokuwa na muundo kama godoro laini, na katikati kulikuwa na vyombo kadhaa vilivyofunikwa; bila shaka kukiwa na chakula kwa ndani. Namouih alipendezwa sana na jambo hilo, kwa sababu ilikuwa ni kama Draxton ameandaa mlo wa pekee kwa ajili yao, kwa njia fulani ya wapendanao. Mwanaume huyo akamwonyesha kwa ishara ya macho kuwa akaribie hapo, na Namouih akaanza kuelekea sehemu hiyo taratibu na kuchuchumaa, kisha akavua viatu vyake na kuketi huku anatabasamu kwa hisia.

"Hii yote ni nini?" Namouih akauliza kwa sauti ya chini bila kumwangalia usoni.

"Lunch," Draxton akajibu.

"Mmmm..."

"Yeah. Nimetimiza ahadi yangu," Draxton akasema.

"Ahahah... Ingekuwa vizuri kama ningekuona ulivyopika kabisa. Au hujapika?"

"Nimepika."

"Mmmm... kweli? Siyo kwamba umenunua halafu unazuga tu hapa?"

"Ni ngumu sana kukushawishi mpaka uuone ushahidi eti?"

"Ndiyo."

"Nimeungua hapa hivi wakati nakaanga nyanya," Draxton akasema hivyo huku akimwonyesha mkono wake usiokuwa na alama yoyote.

"Em' kwenda huko!" Namouih akasema hivyo, na wawili hawa wakacheka pamoja.

Ukafata utizami fulani mzuri sana baina yao, kisha Draxton akasema, "Karibu Namouih."

"Asante," Namouih akajibu kwa sauti nyororo.

Draxton akanyanyuka na kuvuta jagi lenye maji na kibeseni kidogo, naye akamsogelea ili aanze kumnawisha mwanamke huyu kiganja chake. "Samahani ila huwa situmii vijiko hapa," akamwambia.

Namouih akatabasamu na kusema, "Usijali. Napenda kula kwa mikono pia."

Wakaendelea kuangaliana kwa sekunde chache, kisha mwanaume akaanza kumnawisha mkono. Namouih akawa anayaangalia macho ya Draxton kwa upendezi mwingi mno, na baada ya kumaliza kumnawisha Namouih, mwanaume huyo akachukua taulo ndogo na safi iliyokuwa pembeni na kuanza kuufuta mkono wa Namouih taratibu. Wakati Draxton anafanya hivi, Namouih akawa ametambua kwamba mwanaume huyu alikuwa anafanya mambo taratibu akiwa karibu yake ili aivute vyema harufu yake ambayo alionyesha kuipenda mara nyingi sana, na jambo hilo likampa Namouih hisi ya kujidai. Draxton akamaliza kumfuta na kurudi upande wake ili aketi, kisha akamwambia Namouih ajisikie huru kufunua na kujichukulia chakula.

Namouih akawa anatabasamu tu na kuanza kufunua vyakula, na kiukweli alivutiwa sana na mapishi ya Draxton kwa kuvuta harufu nzuri sana iliyotokana navyo. Kulikuwa na nyama za kukaangwa, kupikwa, chips kavu, wali kiasi, na dagaa fulani wa baharini waliokaangwa pia (dagaa mchele). Draxton alikuwa amenunua na mtindi mweupe pakti mbili pia, hivyo akampatia Namouih moja, nao wakaanza kula taratibu. Namouih alimtania sana Draxton kwa kusema hajui kupika, naye Draxton akawa anacheka tu kwa sababu jinsi Namouih alivyokichangamkia chakula ilipingana na kauli zake za kimasihara kukielekea. Kiukweli Namouih alikifurahia sana chakula cha Draxton, na wawili hawa wakaendelea kula taratibu huku wakiongelea masuala ya kazi. Ilikuwa ni kama hawakutaka kuzungumza kuhusu jambo lao lile, lakini akili zao kwa pamoja zililifikiria sana na kufanya iwe ni kama wanasubirishiana.

Namouih akawa ameshiba kwanza, na Draxton alipotaka kumnawisha mkono, akakataa, akimwambia amalize kula chake kwanza, na yeye angenawa mwenyewe. Akaanza kunawa huku anamwangalia kwa macho yenye upendezi sana, kisha akajifuta mikono na kukaa sawa tena. Draxton akamalizia kula na kutaka kuvuta jagi lenye maji ili anawe, lakini Namouih akajinyanyua na kulichukua jagi kisha kupiga magoti karibu yake, akionyesha kwamba anataka kumnawisha, lakini Draxton akawa anamwambia hiyo si sahihi kwa kuwa Namouih alikuwa mgeni hapo. Akawa anasisitiza kwamba angenawa yeye mwenyewe, lakini Namouih akaweka uso wa kununa huku akimwangalia kwa njia hiyo ya kudeka, naye Draxton akaweka mikono yake mbele ili anawishwe kwa kutotaka kumuudhi mtoto. Namouih akaanza kumnawisha huku akiangalia chini na kuibana midomo yake kwa njia ya shau, naye Draxton akawa anautathmini tu urembo wake.

Namouih alipomaliza kumnawisha, akatoa na kuweka vyombo vyote pembeni, kisha akaketi tena chini hapo; wakati huu akiwa karibu zaidi na Draxton. "Asante kwa chakula kizuri sana Max," akamwambia huku akimwangalia kwa hisia.

"Oooh sa'hivi ndiyo kimekuwa kizuri eh?" Draxton akauliza.

Namouih akacheka kidogo, kisha akasema, "Tokea mwanzo. Una style nzuri sana."

"Siyo kama wewe. Chako ni kitamu kupitiliza," Draxton akamwambia.

"Ulishawahi kula chakula changu?"

"Umeshahau mara ya kwanza nimekuja kwako?"

"Aaaa... kweli! Eh... ahahahah... ni muda. Angalau sa'hivi wote tumejua ladha ya vyakula vyetu. Hata we' chako ni kitamu mno yaani, siwezi kuacha kusifia," Namouih akasema.

"Ahah... asante. Natamani tu kama... all of this would've been on a different note."

"Unamaanisha kwamba...?"

"Kama tu ulivyoniambia siku ile. Huwa nawaza pia... ingekuwa vipi kama mimi na wewe tungekutana chini ya hali tofauti na tulizonazo sasa," Draxton akasema.

Namouih akaanza kutembeza kiganja chake mkononi kwa Draxton taratibu, naye akasema, "Unahisi kuwa na majuto kwa sababu ya hili jambo linaloendelea baina yetu."

"Siyo rahisi Namouih... unajua... kutoka hapa... kurudi kwa Blandina na kuigiza kana kwamba mambo yako shwari... ina...."

"Inakufanya ujione kama mtu anayetia kinyaa sana. Kutoka na rafiki ya mpenzi wako..."

"No, Namouih, sijamaanisha hivyo. Unaelewa tu kwamba... kwamba..."

"Ninaelewa Max, usijali. Lakini mimi.... sijui ni kwa nini ila ni kama hisia hizo naziweka tu pembeni kwanza na kuamua kufurahia wakati huu pamoja nawe... hivyo yaani," Namouih akamwambia hivyo na kukishika kifua cha Draxton.

"I don't know Namouih. Bado nahisi kama utaumia sana kwa sababu ya haya yote," Draxton akasema.

"Mhm... napenda sana unavyoonyesha kunijali. Unajua... Blandina ameniambia jinsi mlivyokuwa wote jana," Namouih akasema.

Draxton akamwangalia kwa njia ya kuelewa kile alichomaanisha.

"Ni jambo zuri kwamba angalau umemtuliza kidogo... ijapokuwa bado anakuhitaji. Usiwaze kuhusu mimi kuumia kwa sababu hata mimi pia nakuwa narudi kwa mume wangu... ni jambo zito... lakini Max... bado ninataka kuendelea kuwa nawe... haitajalisha kama ni kwa kipindi kifupi cha kukusaidia wala nini... I just wanna be here... with you," Namouih akasema kwa hisia.

"Kwa nini imegeuka kuwa namna hii Namouih? Kwa nini... kwa nini ilipaswa kuwa wewe?" Draxton akauliza.

Namouih akakipandisha kiganja chake mpaka shingoni kwa Draxton na kusema, "Kwa sababu umeshanipenda Max."

Draxton akaangalia chini kidogo.

"Unakumbuka ulichoniambia jana?" Namouih akauliza.

Draxton akamtazama.

"Ulinishika ghafla halafu... ukasema 'I love you.' Ahah... nataka kujua ikiwa ilikuwa ni akili yako au ya upande wa pili iliyosema hivyo Max..." Namouih akasema.

"Ni... haikuwa akili Namouih. Nafikiri kuna kitu tu kutoka hapa... kilichonisukuma kusema hayo maneno," Draxton akamwambia huku akijinyooshea kidole usawa wa moyo wake.

Namouih akatabasamu kwa hisia sana, naye akamwinamia karibu zaidi na uso wake kama anaelekea kumbusu.

Draxton akafumba macho na kuivuta harufu tamu ya bibie kwa hisia, kisha akasema, "Uhakika ulio nao... unanivutia. Ila tu wazo la mume wako likija akilini naona...."

"Efraim hajawahi kunipa kile nilichokipata kutoka kwako Max... hata mara moja," Namouih akasema.

"Nini?" Draxton akauliza kwa sauti ya chini.

"Toka amenioa... hatujawahi," Namouih akamwambia.

"Kwa nini?" Draxton akauliza.

"Sijui. Hanipi sababu kila mara nikijaribu kumwomba tushiriki... iko tu kama jinsi ilivyo kwako na Blandina, lakini si kama yeye ana tatizo kubwa namna ilivyo kwako... ni kama tu hataki," Namouih akasema.

Draxton akabaki kumtazama tu kwa hisia.

"Imepita miaka zaidi ya sita Max... miaka sita bila ya mimi kufanya tulichofanya jana... na ninaweza kusema ni moja ya penzi ambalo sijawahi kupewa na mwanaume yeyote... kwa sababu wewe siyo wa nchi hii," Namouih akasema.

Draxton akatabasamu, naye Namouih akacheka kidogo.

"Kwa hiyo... mume wako anakuacha tu... kama mimi navyofanya kwa Blandina?" Draxton akauliza.

"Angalau unaweza hata kumpa Blandina kidogo Max... Efraim hanigusi kabisa. Huwa inanivunja sana moyo kwa sababu sielewi ana maana gani... ndiyo maana ninathamini sana unachofanya kwa ajili yangu..."

"Hapana Namouih... wewe ndiyo unanisaidia mimi... na inaumiza tu fikira kwamba mambo mengi yako kwa mvurugo lakini ninathamini sana ulichofanya kwa ajili yangu. Natamani hali zingekuwa tofauti... ila kwa sababu unataka kuendelea kunisaidia ingawa kuna vizuizi, nitajitahidi pia kukupa unachohitaji. Ila unapaswa tu kukumbuka kwamba...."

Namouih akamkatisha Draxton kwa kukifata kinywa kumbusu moja kwa moja kwa hisia sana, kisha akauachia mdomo wake na kusema kwa sauti yenye deko, "Achana na mawazo hayo... ninahitaji tu penzi lako Max."

"Namouih..." Draxton akaita kwa sauti ya chini huku akikishika kiuno chake.

"Please.... nimeshalemewa mno... siwezi tena kusubiri..." Namouih akaongea kwa sauti yenye deko na hamu kubwa sana.

Wawili hawa walikuwa wamekaribiana sana, Draxton akiwa amekaa kwa kuitandaza miguu chini, na Namouih akiwa ameketi katikati yake huku akiishika shingo ya jamaa na nyuso zao zikiwa karibu mno. Ingawa bado Draxton hakujiamini vya kutosha, alikumbuka vizuri kuwa upande wake wa pili ulivutiwa na Namouih, na hivyo yeye alichotakiwa kufanya ilikuwa kumwamini mwanamke huyu ili asitawaliwe na fikira za kumuumiza na hivyo afanikiwe kumpatia penzi kwa kujiendesha vyema. Aliuhitaji sana msaada huu kutoka kwa Namouih, lakini haikuwa tu kwa sababu ya msaada, alikuwa anahitaji pia penzi la mwanamke huyu mrembo.

(........).

Namouih akauachia mdomo wa Draxton taratibu na kumwangalia, na sasa mwanaume huyu alikuwa ameinamisha uso wake kidogo huku amefumba macho yake. Namouih hangehitaji kumwambia la kufanya, kwa sababu aliona tayari Draxton alikuwa akilifanya, yaani, kuuacha upande wake wa pili utoke. Nywele za Draxton zikaanza kukua na kuwa nyeupe, hata ngozi yake pia, kisha akafumbua macho yake na kumtazama Namouih usoni. Yalikuwa yale macho ya blue, lakini wakati huu hakumtazama mwanamke huyo kwa njia ya kinyama, bali ilikuwa kwa njia yenye umakini wa kawaida. Kuanzia hapo, Namouih akawa ametambua kwamba mwanaume huyu alikuwa anajitahidi sana kujiendesha vyema, naye akaishika shingo yake tena na kutabasamu kidogo.

Sasa Draxton akawa katikati ya badiliko lake, na ilikuwa ni kama tayari upande huu ulikuwa umeshamzoea Namouih hasa baada ya kilichotokea siku ya jana baina yao, kwa hiyo akawa ametulia tu. Namouih akaanza kuifata tena midomo ya Draxton, lakini Mnyama-Draxton akamkwepa kiasi. Mwanamke akawa anamwangalia kwa kushangaa kidogo, naye Draxton akafungua kinywa chake kumwonyesha meno kwa njia iliyomwambia Namouih kwamba alikuwa anakwepa kumbusu kinywani kwa kuhofia kumuumiza kwa yale meno yake makali, kitu kilichomfanya Namouih atambue kwamba upande huu ulionyesha hisia ya kumjali kwa mara nyingine tena. Lakini kama jana waliweza kupeana mapenzi bila Namouih kuumia sana, mwanamke huyu alitaka kumhakikishia kwamba hakuhitaji kuhofia hilo, hivyo akamsogelea mdomoni zaidi na kusema kwa kunon'goneza, "Trust me."

Draxton akatulia, kisha Namouih akamfata mdomoni tena na kumbusu mara tatu. Mwanamke huyu alikuwa anajitahidi kupeleka mambo taratibu, lakini tayari Draxton alikuwa amezidiwa na hisia za kimahaba zenye nguvu zaidi akiwa namna hiyo, hivyo ghafla akakishika kiuno cha Namouih na kukiminya kwa nguvu, kitu kilichomuumiza sana Namouih kutokana na makucha marefu ya jamaa kumkandamiza. Akatoa sauti ya kuumia kidogo, kisha naye akamkandamiza Draxton kwa makucha yake marefu ya urembo shingoni kwake, lakini haikuonekana kama Draxton aliumia. Namouih akawa anamwangalia kwa uso ulioonyesha maumivu kiasi, na ndiyo Draxton akaacha kukikandamiza kiuno chake polepole.

Namouih akajirudisha nyuma taratibu na kugeuza mwili wake pembeni kujituliza kwa sababu hakuwa ametarajia jambo hilo tofauti na ilivyokuwa jana, na katikati ya sekunde chache alizogeuka ili kutuliza maumivu, akahisi pumzi za moto za Draxton nyuma ya shingo yake, na hapo hapo nguo yake ikachanwa kutokea mgongoni! Alishtuka, lakini hakuwa hata na muda wa kujisawazisha na tayari Draxton akawa ameushika mwili wake na kuuvuta karibu naye kwa nguvu; yaani Namouih akiwa amempa mgongo kwa ukaribu sana, kisha mwana-mnyama akaivuta nguo yake yote kwa fujo na kuirusha pembeni. Namouih alikuwa amesisimuliwa sana na jambo hilo, hata mawazo ya angevaa nini baada ya hapo hayakuingia akilini kabisa, na sasa akawa amebaki na sidiria nyeupe na chupi laini nyeupe pia.

Draxton akawa amekaa nyuma yake, akiwa ameishika shingo ya Namouih kama ameikaba kutokea nyuma na kumfanya mwanamke huyu aelekeze uso wake juu huku akipumua kimahaba, kisha mwanaume akaivuta sidiria hiyo na kuirusha pembeni pia. Namouih alikuwa amemwachia tu mwanaume huyo mwili wake autendee kwa njia aliyotaka, kwa sababu tayari moyo wake ulikuwa umeridhia aina ya penzi ambalo angelipata kutoka kwake. (........).

(........).

(........).

(........).

(........).

(........).

(........).

Namouih akacheka kidogo huku akipumua na kumwangalia kwa ulegevu, kisha akamwambia kwa kunong'oneza, "I want you inside of me Max."

Ilionekana kwamba Draxton akiwa katikati ya badiliko lake hakuweza kuzungumza kama mtu wa kawaida, lakini alichokisikia alikielewa. Baada tu ya Namouih kumwambia hivyo, mwanaume akararua T-shirt lake kwa mikono yake na kuivuta bukta yake yote mpaka ikachanika, na sasa yeye pia akawa mtupu mbele ya Namouih. (........). Ingawa hali hii ilikuwa mpya na tata, bado Namouih aliifurahia, na ndiyo maana alimwachia aendelee kumpa penzi kwa njia aliyoona kuwa sahihi. Kama ni kupewa mapenzi kwa njia ya mnyama, basi na yeye angetakiwa kujifunza kuyapokea kama mnyama tu.

(........).

(........).

Ilikuwa kama ndoto vile kwa Draxton. Ingawa alikuwa katikati ya badiliko lake, akili yake ilielewa vizuri kabisa kwamba jambo alilokuwa akilifanya ni jambo ambalo hakuwahi kufikiri angekuja kuweza kufanikiwa kufanya, na sasa alikuwa akilifanya kwa mara ya pili bila kupitiliza mpaka kuwa mnyama kabisa na hata kumuumiza mwanamke huyo sana. Yeye pia alifurahia mno joto la mwanamke huyu, na akili yake ilikubali kwamba alikuwa mtamu balaa!

(........).

(........).

Namouih akabaki kupumua kwa uchovu sana kama vile alikuwa ametoka kutua zigo zito mno, kisha Draxton akamvuta kidogo na kupiga magoti ili amwingie tena.

Namouih akanyanyua uso kilegevu na kusema, "Hapana... Max... that's enooough... hhh... you'll kill me!"

Draxton, akiwa mnyama pia, hakuelewa hii kauli, naye akaupiga mkono wa Namouih uliokuwa unataka kumzuia kuingia ndani tena na kisha akapenya ndani.

"Ahsss.... maamaahh...."

Namouih akalia kwa deko ya hali ya juu, kwa kuwa alielewa hapa habari yake ilikuwa imekwisha. Mwanaume hakutaka kumwacha hata kidogo, na kama wangeendelea hivyo kwa muda mrefu basi angechelewa sana kutoka hapo; tena akiwa hoi bin taaban.

(........).

(........). Hiyo ilikuwa ni ni safari ndefu, siyo mchezo!

Draxton akaiachia miguu ya Namouih na kujirudisha nyuma, akiwa ameitoa mashine yake ndani ya hekalu la mwanamke huyo na kubaki anapumua kwa nguvu. Namouih alikuwa ndiyo kama hajitambui vile. Mwili wake ulikuwa umeiva joto la ajabu kutokana na mahaba aliyopata hapo, naye akabaki akipumua kwa njia iliyoonyesha uchovu na mridhiko wa hali ya juu. Kuna sehemu za mwili wake alizohisi zikiuma sana, lakini bado moyo wake ulikuwa umeridhika sana na penzi alilolipata siku hii, naye akawa anatabasamu kilegevu katikati ya pumzi zake za uchovu. Draxton akawa anamwangalia sana, jinsi alivyolala hapo chini kwa kujiachia, naye akanyanyuka na kutambaa kumwelekea mpaka alipomfikia usawa wa uso wake.

Nywele za Namouih zilikuwa zimelowana kutokana na jasho tele lililomjaa, naye akamtazama Draxton machoni kwa hisia. Mnyama-Draxton akapitisha kiganja chake kifuani kwa Namouih mpaka usoni, na hisia ya kusisimua mwili wake ikampata mwanamke huyu. Yeye pia akanyanyua kiganja chake na kuushika uso wa Draxton, kisha akasema, "I love you Max."

Inaonekana maneno hayo yalimgusa sana mwana-mnyama Draxton, kwa sababu alifumba macho yake kidogo, kisha alipoyafumbua, yakawa yamerudi katika hali ya ukawaida bila kuwa na lenzi za blue. Namouih akatabasamu kidogo, akiwa amestaajabishwa na jambo hilo kwa kutambua kwamba Draxton aliweza kuji-control vizuri kurudia hali ya kawaida, na taratibu ngozi yake ikaanza kurudi kuwa ya kawaida na kuiacha ya uzungu.

Draxton sasa akawa anamwangalia Namouih kwa hisia sana, nywele zake zikiwa nyeupe bado, naye akasema, "I love you too, Namouih."

Hii ilishangaza kiasi, lakini Namouih akatabasamu kwa furaha sana baada ya kusikia hivyo, naye akakishika kichwa cha Draxton na kumvutia kwake ili wapeane busu. Wakalambana ndimi pamoja taratibu, nao wakaivunja taratibu na kutazamana machoni kwa ukaribu.

"Sijui ni kwa nini... lakini nimetokea kukupenda sana..." Namouih akasema.

"Umenipenda kama Draxton... au Max?" Draxton akauliza.

"Wewe ni yule yule kwangu..." Namouih akamwambia.

"Hhh... hii imefika mbali sana Namouih... sana," Draxton akasema.

"Najua. Lakini bado sitaki ifikie tamati," Namouih akasema kwa hisia.

Draxton akashusha pumzi, kisha akasema, "Ninaweza kuhisi jinsi ambavyo mwili wako umekuwa wa moto sana... ni kwa sababu nimekuumiza kwa kadiri kubwa. Wacha nikupake damu yangu."

Namouih akamwangalia tu machoni na kisha kutikisa kichwa kukubali.

Draxton akatoka usawa wa uso wa mwanamke huyo na kunyanyuka kabisa, naye akaenda pembeni kwanza. Ni kweli Namouih alikuwa ameumizwa sehemu za nyonga yake kwa makucha ya Draxton, pamoja na kifua na kalio lake kutokana na meno ya Draxton, na hata kuchubuka sehemu ya kitoweo chake, hivyo mwanaume huyo akaenda kuchukua kisu na kujikata kiganjani, halafu akarejea kwa mrembo na kuketi karibu na mwili wake uliolala bado. Akaanza kumpaka damu yake taratibu kwenye sehemu hizo, na Namouih akajinyanyua na kugeuka ili apakwe na nyuma pia. Walikuwa kimya kwa muda huu wote mpaka Draxton alipomaliza kumpa tiba hiyo isiyoeleweka vizuri, na ile tu Draxton alipotaka kunyanyuka tena, Namouih akakishika kichwa chake na kuanza kumpiga denda taratibu. Draxton akarudisha busu hiyo kwa upendo pia, halafu akamwacha chini hapo na kuelekea sehemu ya chumba.

Namouih akawa anajitazama mwilini mwake na kuona jinsi ngozi yake ilivyokuwa nyekundu kutokana na mchezo wenye rafu nyingi sana kutoka kwa mwanaume yule, naye akaichukua simu yake na kuangalia muda. Ilikuwa ni saa kumi na mbili jioni sasa, na kwa makadirio ya haraka angeweza kusema yeye na Draxton walipeana mapenzi kwa masaa mawili mfululizo kama siyo zaidi! Kuona namna ambavyo muda ulisonga kulimfanya atambue kwamba hangetakiwa kuendelea kukaa hapo kwa muda mrefu, lakini angevaa nini wakati Draxton alikuwa amezirarua nguo zake zote? Ni hapo ndipo akaanza kusikia mvua ikinyesha huko nje, naye akacheka kidogo kwa kutoamini hilo maana ilizidi kuongezeka tu.

Draxton akarejea kwa mrembo hatimaye, akiwa ameshika nguo fulani mikononi na yeye akivaa bukta nyingine tena. Namouih akawa anauangalia mwili wa mwanaume huyo, jinsi ulivyokuwa umejikata kiume haswa, naye akatabasamu na kuendelea kumtazama tu kwa uvutio. Mwanaume akaketi karibu yake na kumpatia T-shirt nyeupe yenye mikono mirefu, pamoja na bukta nyingine ngumu. Namouih akamwangalia na kuachia tabasamu, naye Draxton akatabasamu pia.

"Samahani kukuchania nguo... nitakununulia zingine," Draxton akasema.

"Asante. Kwa hiyo... natakiwa kurudi nyumbani nikiwa nimevaa hizi?" Namouih akauliza.

"La. Vipi ukipita kwa duka fulani kuchukua zingine zitakazokufaa?" Draxton akasema.

"Halafu hizi unazonipa?"

"Ukipenda zitupe tu."

"Kwa nini nizitupe?"

"Namouih..."

Namouih akatabasamu kidogo.

"Bila shaka Efraim amesharudi," Draxton akasema.

Namouih akatikisa kichwa kukubali.

"Itabidi uwahi... mvua inaweza kuendelea mpaka usiku," Draxton akamwambia.

Namouih akamsogelea mdomoni taratibu na kusema, "Hauoni kwamba hicho ndiyo kisingizio kizuri cha kunifanya nichelewe?"

"Lakini...."

"Efraim anajua niko na rafiki... usijali," Namouih akasema.

Draxton akatazama pembeni.

"Na wewe? Blandina hatakwazika tena maana uko mbali naye kwa mara nyingine?" Namouih akauliza.

"Nimemwambia nimeondoka kwenda nje ya jiji kwa muda mfupi..." Draxton akasema.

"Ahaaa... ndiyo maana hakuwa na mchecheto leo," Namouih akasema na kutabasamu.

Bado mwanamke huyu hakuwa amevaa chochote, hivyo ukaribu aliouweka kwa Draxton ukamsisimua sana mwanaume huyo.

"Unajua... unanifanya nitake kuku... kukushika tena..." Draxton akamwambia.

"Kuna kitu kinakuzuia kwani?" Namouih akaongea kwa njia ya madaha.

"Haitakuwa jambo zuri nikiwa nakupaka damu yangu kila mara Namouih... unaelewa nachomaanisha," Draxton akasema.

"Ndiyo naelewa."

"Yeah. Unanifanya nihisi kama... njaa... kila mara... ila ni muhimu sana nijizuie maana hata kama hautakubali, ninajua huwa unaumia. Sema tu una king'ang'anizi sana," Draxton akasema.

Namouih akatabasamu kwa hisia na kutazama chini.

Mvua bado ilikuwa inanyesha, hata sauti za ngurumo za radi zilisikika. Draxton akachukua T-shirt lile na kuanza kumvalisha Namouih, kisha akafanya hivyo hivyo na ile bukta. Alikuwa anamvalisha huku akimwangalia usoni kwa umakini, na mwanamke huyo alikuwa anamwangalia tu kwa uvutio mwingi. Kisha mwanaume akanyanyuka na kwenda kufata chupa za maji ya kunywa zilizokuwa pembeni, na ni hapa ndiyo Namouih akaanza kujishika sehemu zile zilizokuwa na maumivu na kuhisi akiwa amepona kabisa. Ilikuwa ni kama hakuumia kabisa, naye akamtazama Draxton baada ya mwanaume huyo kufika hapo tena na kumpa maji anywe.

Namouih akayafungua maji huku akisema, "Kuna kitu fulani huwa nafikiria sijui kama kilishawahi hata kupita kwenye akili yako."

"Kitu gani?" Draxton akauliza.

"Hivi unavyonipaka damu halafu... napona tu... ngozi inajishikiza yenyewe tu yaani... ingekuwa kama msaada mkubwa kwa watu wanaojeruhiwa vibaya labda... kama kwenye ajali...."

"Ndiyo tunarudi kule kule kwenye mimi kutumiwa kama kifaa cha experiment endapo kama ingefahamika damu yangu inaweza kuponya. Baba alikuwa anajaribu kunitengeneza kwa njia ya pekee, kwa ajili yangu mwenyewe, niwe tofauti tu... lakini jinsi watu wanavyoona mambo kwa njia mbaya ndiyo sababu aliamua kunificha... maana aliona ningekuwa hatari kwa wengi katika njia ambazo hata yeye hakufikiria..." Draxton akasema.

"Napenda unavyoongea Max. Ila bado huwa ni ngumu kiasi kukuelewa..." Namouih akamwambia.

Draxton akatabasamu.

"Miaka 95 ni mingi sana. Halafu hivi ulisomea wapi sheria? Ulihitimu wapi?" Namouih akauliza.

"Nilisoma sheria nikiwa Venezuela. Nilichukua madarasa kwa miaka mingi... huku nikijitahidi kuendelea kuficha siri yangu. Nili-pass bar exam vizuri sana, tena level ya juu..." Draxton akajisifia.

"Wow!" Namouih akamwambia na kumpigia makofi laini.

"Ahahahah... yeah. Baada ya kilichompata Ramona... sikuhitaji... yaani, nilikuja tu Tanzania kuendelea, au niseme kutafuta maisha mapya. Nilijifunza lugha yenu kwa miaka miwili tu."

"Yote?"

"Yote."

"Una kichwa chepesi."

"Ahah... mwanzoni nilikaa mwenyewe sana... ila ilipita kipindi kirefu pia bila ya mimi kubadilika kwa hiyo niliweza tena kujiamini na hata kutafuta uraia wa huku huku... angalau nijipe utambulisho mpya... na... nikarudia miaka ya uanasheria kwa huku pia ili niwe na mambo ya kufanya na siyo kukaa tu."

"Kuhama sehemu tofauti na kuishi muda wote huo... ulikuwa unatoa wapi pesa ya...."

"Oh, baba alikuwa pesa. Aliniachia urithi mwingi chini ya mwongozo wa mama na hata mama pia alikuwa akifanya kazi za hapa na pale kunipa support. Over the years... ziliendelea kuongezeka... na siyo kwamba me nilikuwa mtu wa kukaa tu... nilifanya kazi pia nilipokuwa Venezuela... na angalau huku thamani ya pesa ilikuwa ndogo kwa hiyo nilizokuwa nazo zilinisukuma kwa kipindi kirefu sana."

"Okay. It's touching. Halafu... hiyo tattoo... uliyonayo mgongoni... alikuchora nani?" Namouih akauliza.

"Ramona," Draxton.

"Oh kumbe! Alikuwa artist eeh?"

"Yeah."

"Hayo maneno huwa yanamaanisha nini? Kwa nini ulimwambia aandike... living in my heart you are, so you aren't dead? Au ilikuwa idea yake?" Namouih akauliza.

"Kuna siku nitakuelezea," Draxton akasema.

Namouih akatulia kidogo, kisha akasema, "Sawa. Uliniambia umekuja huku 90' eeh?"

"Yeah... we' ndiyo unazaliwa."

"Ahahah... ni miaka yangu ya kuishi we' ndiyo umekaa Tanzania. That's so cool. Umejitahidi sana kukaa muda wote huo bila kuumiza mtu yeyote Max... miaka 32! Umejitahidi sana," Namouih akamwambia kwa shauku.

Draxton akaangalia chini kwa njia iliyoonyesha huzuni.

Namouih alipogundua hilo, akamuuliza, "Max, uko sawa?"

Draxton akatikisa kichwa kukubali na kusema, "Yeah, niko sawa."

"Mbona hivyo?"

"Nilijitahidi ndiyo... kutoumiza watu... lakini kuna kipindi nilishindwa Namouih..." Draxton akasema na kumwangalia.

"Unamaanisha umeshaumiza mtu fulani ukiwa huku Tanzania?"

Draxton akatikisa kichwa kukubali na kusema, "Yeah. Ni... ni jambo lililoniumiza sana yaani... nilijichukia mno."

Namouih akakishika kiganja chake na kumwambia, "Pole Max. Unajua siyo jambo zuri lakini naweza kusema ulijitahidi sana... miaka mingi kupita ukiwa umeshaweza kuji...."

"Hakuna kitu kizuri Namouih. Yaani mimi ndiyo definition sahihi ya neno ubaya!" Draxton akamkatisha.

"Max...."

"Alikuwa mtoto, Namouih," Draxton akasema.

Namouih akatulia.

"Sikumbuki mambo vizuri lakini najua niliua mtoto. Ni kitu kilichoitesa conscious yangu sana... mpaka leo," Draxton akasema na kuinamisha uso wake.

Namouih akamwangalia kwa huruma, kisha akauliza, "Mtoto... alikuwa mtoto wa miaka mingapi?"

"Sikujua. Ila najua alikuwa mdogo sana... ninakumbuka walikuwa wawili na mwenzake mdogo pia ila yeye alikimbia... bila shaka wazazi wake walikuwa wanamtafuta alipoingia msituni na ndugu yake... na mimi nikapitiliza, nika... hhh... iliniuma sana..."

Namouih akaweka umakini wake zaidi, kisha akaushika uso wa Draxton na kumtazamisha usoni kwake. "Huyo mtoto... alikuwa wa kiume?" akamuuliza.

Draxton akatulia kidogo, kisha akatikisa kichwa kukubali.

"Alikuwa... mweupe... mdogo kama miaka 6 hivi... alikuwa na ndugu yake mwingine wa kike mdogo mdogo, si ndiyo?" Namouih akauliza huku pumzi zake zikianza kutetemeka.

Draxton akavishika viganja vya Namouih huku akimwangalia kwa umakini, kisha akamuuliza, "Kwa nini unauliza hivyo?"

"Nijibu kwanza Max. Hilo tukio... ulipomuua huyo mvulana... ilikuwa 2013?" Namouih akauliza tena.

Draxton hakuelewa ni jinsi gani Namouih aliweza kujua hilo, lakini akatikisa kichwa chake kukubali.

Namouih akauachia uso wa Draxton na kuweka kiganja chake mdomoni, naye akaanza kulengwa na machozi kwa sababu alikuwa ameshaelewa hilo lilimaanisha nini.

Draxton akamshika mabegani na kuuliza, "Vipi Namouih? Kuna tatizo gani?"

Namouih akainamisha uso wake na kuanza kulia bila kutoa sauti, na ni kitu kilichomfanya Draxton akose amani.

"Namouih..."

Draxton akamwita hivyo, lakini Namouih akajitoa mikononi mwake na kwenda pembeni kwanza. Draxton akanyanyuka pia akiwa haelewi mwanamke huyo alikuwa amepatwa na nini, na hivyo akamsogelea karibu na kuugeuzia mwili wake kwake. Namouih alikuwa anadondosha tu machozi huku ameangalia chini, naye Draxton akaanza kumfuta huku akijihisi vibaya sana moyoni kumwona analia.

"Namouih what's wrong?" Draxton akamuuliza huku akiwa ameshika uso wa mwanamke huyo kwa wororo.

Namouih akamwangalia machoni kwa huzuni, kisha akasema, "Huyo... mvulana... alikuwa mdogo wangu Max."

Uso wa Draxton ukatoa umakini wake wenye kujali na kubaki akimwangalia Namouih kwa njia ya kawaida, lakini akiwa ameshangazwa sana na kauli hiyo.

"Itakuwa upande wako wa pili ulimuua Nasri.... alikuwa mdogo wangu... hhh... Max...." Namouih akaanza tena kulia.

Draxton alikosa hata cha kusema. Macho yake yakaanza kutangatanga tu, kwa sababu zile hisia za kujiona kuwa mbaya kutokana na kuua mtoto mdogo zilikuwa zimeongezwa maradufu baada ya kujua aliua mdogo wa mtu muhimu sana kwake kwa wakati huu. Akautoa mkono wake usoni kwa Namouih na kurudi nyuma, akiwa ameshindwa afanye nini sasa.

Namouih akashusha pumzi na kujifuta machozi upesi, kisha akasema, "I need to go."

"Namouih..." Draxton akaita kwa huzuni.

"Nina... nahitaji... nahitaji kwenda Max... nahitaji kutuliza akili."

"Samahani... Namouih...."

Draxton akiwa anataka kuongea maneno kidogo, Namouih akampita na kuifata simu yake, kisha akavichukua viatu vyake na kuvishikilia tu mkononi. naye akaanza kuondoka kuelekea nje.

Draxton akaanza kumfata huku akisema, "Namouih... tafadhali just...."

Namouih akasimama na kumgeukia huku amenyanyua kiganja chake kumzuia asimfate, naye Draxton akasimama. "Please... nina... ninahitaji muda wa kuwa mwenyewe hiki ni... kitu kizito sana kwangu..."

Draxton hakuwa na namna ila kumwelewa tu, kwa sababu hata yeye alikuwa ameshtushwa sana na utambuzi wa jambo hilo ambalo hakuwahi kufikiri lingekuja kuleta mvurugiko mkubwa zaidi ya ilivyokuwa kwake mwanzoni. Namouih akatoka ndani hapo na kuelekea nje, mvua bado ikiwa inanyesha na giza likiwa limeanza kuingia, naye akaenda mpaka kwenye gari lake na kuingia. Akatulia kwa muda mfupi ndani hapo, akiwa anamwona Draxton sehemu ya mlangoni kwenye ile nyumba, naye akaligeuza gari upesi na kuondoka msituni huko.



β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

ITAENDELEA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…


Usikose sehemu za mwendelezo wa hadithi hii kali ya CHANGE. Ni story nzuri na ndefu sana. Waweza ipata nakala yote kwa gharama nafuu sana. Karibu WhatsApp au kwa E-mail yangu.

WhatsApp no: +255 678 017 280
 
CHANGE

Story by Elton Tonny

Urafiki, Familia, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Ukatili, Mauaji, Mambo yasiyotazamiwa, Mambo yenye kuhofisha

R-rated 18+

Enjoy!

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…


Efraim Donald alikuwa amesharudi nyumbani mapema tu, naye alifika na kujisafisha, kisha akakaa zake kuangalia mpira. Lakini tayari hali yake ya kihisia ilikuwa imevurugwa sana kutokana na mambo aliyopata kujua leo. Namouih alikuwa amebadilika. Hakuwa tena na upekee ule aliokuwa nao mwanzoni; mwanamke msafi kidhamiri, kiutu, na aliyekuwa hadanganyi kabisa. Lakini alielewa kwamba kubadilika kwa mke wake kulisababishwa na yeye mwenyewe Efraim, kwa sababu ya Namouih kuchoka kumvumilia kwa muda mrefu sana, na sasa alichokuwa anakitaka akawa ameanza kukipata nje ya ndoa yao.

Jambo hili lilikuwa limekuja kwenye utambuzi wake mapema ya leo baada ya kuangalia kifaa chake kilichoonyesha ramani ya eneo ambako gari la mke wake lingekuwa, na kutambua Namouih alikuwa ameanza kupatiwa mapenzi na mtu mwingine; tena mbali sana. Yaani, alikaa kuangalia jinsi gari la mke wake lilivyotoka ndani ya jiji na kwenda eneo lisilokuwa na makazi ya watu, huku Namouih akiwa amemtumia ujumbe kwamba ameenda kukutana na Salome, naye akamjibu tu kuwa ilikuwa sawa huku akielewa kwamba alidanganywa. Alikuwa amekasirika sana. Alijiuliza ni nani angethubutu kumshika mke wake na kumvua nguo, kufanya naye jambo ambalo ni yeye tu ndiyo alitakiwa kufanya naye, tena hadi kumrubuni vya kutosha mpaka yeye Namouih aende mbali namna hiyo ili tu afanye usaliti?

Haingepatana na akili kudhani labda mke wake alikwenda huko kwa masuala mengine tu, kwa sababu Efraim Donald alimtafuta Salome kwa kigezo cha kumsalimia, na mwanamke huyo akasema yeye pia aliwakumbuka sana wanandoa hawa na kugusia suala la kuja hapo nyumbani kuwatembelea. Kwa hiyo sasa mwanaume huyu alikuwa ameshajihakikishia kwamba Namouih kapotea, na kilichobaki ilikuwa kutambua ni nani kampoteza ili amuue, la sivyo huenda mke wake angekuja kuota ndoto ambayo ingemfunulia vitu vingi sana kuhusu uhalisia wa maisha ya mume wake. Maisha ya masharti ni mabaya sana!

Efraim Donald alikuwa ameamua kumwacha tu Namouih kwa leo, ili akirudi, yeye aanze harakati za kuifata sehemu ambayo mke wake alikwenda ili aukomeshe mchezo wake, na njia ya kwanza ingekuwa kumtumia Suleiman. Alikuwa amepanga kumwagiza Suleiman akaiangalie hiyo sehemu ambayo gari la Namouih liliweka kituo cha mwisho huko nje ya jiji, kisha angepanga namna ya kummaliza mbaya wake bila Namouih kuhisi lolote. Ilikuwa imeshafika mida ya saa mbili na nusu hivi pale gari la Namouih lilipoingia ndani ya nyumba yao. Efraim akaendelea kukaa kwa kutulia tu ili aje amsikie mke wake, namna ambavyo angemdanganya kuhusu mahali alipokwenda.

Baada ya kuegesha gari, Namouih akashuka na kuanza kuuelekea mlango wa kuingilia ndani ya nyumba taratibu. Hivi sasa alikuwa amebadilisha mavazi yake baada ya kupita kwenye duka fulani kubwa la nguo na kununua zingine; akiwa amevalia gauni la kijani lililoendana kwa kadiri kubwa na nguo aliyokuwa amevaa leo alipokwenda kazini. Hata mwili wake alikuwa ameuweka katika hali ya usawa kabisa. Bado suala lile la Draxton kuhusika na kifo cha mdogo wake liliendelea kuzunguka akilini mwake kiasi kwamba hata raha ya mahaba aliyokuwa ametoka kupata muda mfupi nyuma ilisahaulika, naye akaingia ndani huku akionekana kutokuwa na raha yoyote usoni mwake.

Esma ndiyo alikuwa ameingia sebuleni baada ya kumaliza sehemu ya kazi zake jikoni, naye akamfata Namouih na kumsalimu kwa heshima. Namouih alikuwa na mwonekano wa mtu aliyechoka usoni, naye akamuuliza tu mambo yamekwendaje hapo na kujibiwa kila kitu kilikuwa safi, na kama anahitaji msosi tayari ulikuwepo hivyo Esma angewapakulia. Akakubali na kumshukuru binti huyo, kisha akaanza kuelekea pale alipoketi mume wake. Alipofikia karibu na usawa wa Efraim, Angelo akamfata miguuni na kuanza kukisugua taratibu, na Namouih akatabasamu na kuchuchumaa chini kabisa ili amlaki. Efraim Donald akamtazama sana Namouih, kwa umakini wa hali ya juu, naye Namouih akawa anamtazama kwa njia iliyoonyesha kutojiamini. Esma akawa ameelekea jikoni tena ili aweze kuandaa mambo ya misosi mezani pa chakula.

"Za hapa?" Namouih akamuuliza Efraim kwa sauti ya chini.

"Safi. Mbona simu yako haipatikani?" Efraim Donald akauliza.

"Aa... ni... nafikiri ni kwa sababu ya mvua labda hali ya hewa ndiyo maana. Umenitafuta sana?"

"Yeah, kiasi. Nilitaka tu angalau tutoke labda mapema tukajifurahishe. Ungeniambia kama hivyo kwamba utachelewa kutoka kwa rafiki yako."

Namouih akamwachia Angelo na kunyanyuka huku akisema, "Niliondoka ofisini saa tisa Efraim. Nisingewahi kihivyo."

Efraim Donald akatazama upande wa runinga.

Namouih akamfata mpaka kwenye sofa na kuketi karibu naye. "Am sorry. Nitajitahidi kuwa nakwambia mapema."

"Haina shida sana Namouih. Nilikuwa tu nataka angalau tuwe wote kwa muda fulani maana sijawa huku wiki nzima," Efraim akasema.

"I know. Tutaangalia nafasi nyingine, sawa?"

"Sawa. Mshauri na saha anasemaje?"

"Aam... yupo tu. Angalau kuongea naye kuna-refresh," Namouih akadanganya.

"Mlikuwa mnaniongelea mimi?"

"Ahah.... hapana. Kuna kumbukumbu ambazo zimenirudia... zenye kuhuzunisha tu..."

"Kama?"

"Mdogo wangu."

"Nasma? Au Sasha?"

"Nasri."

"Ahaaa... kwa hiyo... angalau Salome amekufariji eh?"

Namouih akatulia kidogo, kisha akasema, "Ndiyo."

Hiki ni kitu ambacho kilimchoma sana Efraim Donald, kujua kwamba Namouih alikuwa anamdanganya, lakini akaendelea kumwangalia kwa utulivu zaidi na kuweka mkono wake begani kwake ili ambembeleze. Namouih pia akakilaza kichwa chake kifuani kwa mume wake, akiwa anahisi vibaya sana moyoni.

Wanandoa hawa walikuwa wakifichiana siri nzito sana, ijapokuwa kwa upande wake Efraim tayari alielewa kwamba mke wake alimdanganya kwa kwenda nje ya ndoa yao makusudi. Hakuyaona hayo kuwa makosa ya Namouih, kwa kuwa alielewa kwamba sababu ya jambo hilo ilikuwa ni yeye mwenyewe, na ni yeye mwenyewe ndiye angetakiwa kuliondoa tatizo hilo upesi ili malengo yake yafanikiwe, na Namouih abaki kuwa wake peke yake. Kwa upande wake Namouih, roho bado ilikuwa inamuuma sana baada ya kugundua leo kwamba muuaji wa mdogo wake hakuwa mnyama wa ovyo tu, bali mnyama aliyejikuta anampenda sana. Alihitaji utulivu mkuu wa kihisia na kiakili ili aweze kuja kushughulika na jambo hilo kwa njia nzuri kwa wakati ambao angekutana tena na Draxton, kwa sababu hakutaka kabisa hisia zake zilizovurugwa zimwongoze kuongea au kutenda kwa njia ambayo angekuja kujutia baadaye kumwelekea mwanaume yule.

Baada ya sekunde chache za kumbembelezwa, Namouih akatoka hapo na kuelekea chumbani kujimwagia maji ili aweze kurudi kula, naye akaenda bafuni na kutumia zaidi ya robo saa akitiririkiwa na maji. Sababu ilikuwa kwamba mawazo yake yote yalikuwa kwa Draxton; jinsi alivyompa mahaba mazito siku hiyo mpaka kuja kumwambia mambo mengine mazito yaliyomchanganya sana. Akamaliza kuoga na kuvaa, naye akarudi kwa mume wake tena kuendelea kuigiza kwamba alikuwa sawa kihisia.


β˜…β˜…β˜…


Asubuhi ya siku ya Jumanne ikafika. Namouih aliamshwa na mume wake taratibu, na bado alikuwa na wenge zito la usingizi kutokana na uchovu wa mwili kwa sababu ya mechi kali ya masaa mawili aliyocheza na Mnyama-Draxton jana. Ilikuwa mapema sana, naye Efraim alikuwa anamwambia kwamba anapaswa kupokea simu yake maana Edward Thomas anamtafuta. Namouih akajinyanyua na kuketi kitandani hapo, naye akamuuliza mume wake shida ilikuwa ni nini mpaka 'boss' wa kampuni yao amtafute mapema namna hiyo, naye Efraim akamwambia kwamba alipompigia kwenye simu ya Namouih na kukosa kujibiwa, Edward akampigia yeye Efraim na kumwambia kwamba anahitaji sana kwa hali na mali azungumze na mke wake maana kuna jambo fulani muhimu sana kikazi lililokuwa limezuka.

Namouih akaichukua simu yake na kukuta ni saa kumi na mbili kasoro dakika kumi, naye akajiweka katika hali nzuri ya usikivu na kumpigia Edward mwenyewe. Baada ya Edward kupokea, akaanza kumwambia sasa kwamba kulikuwa na kesi ya dharura aliyohitaji ishughulikiwe upesi sana; ya mtu fulani wa muhimu mno. Alitaka Namouih ndiyo aisimamie na kufanya yote awezayo ili ushindi upatikane, kwa kuwa mbali na mtu huyo kuwa wa hali ya juu na kutoa faida kubwa sana endapo kama angeshinda, alikuwa ni rafiki yake wa karibu pia. Namouih akamuuliza Edward ni kwa nini alimpigia simu mapema namna hiyo ili kumwambia jambo ambalo angeweza kuambiwa akishafika ofisini, na ndipo Edward akasema kuwa ishu hiyo haikuwa ndani ya mkoa huu, bali mkoa wa mbali, tena mkoa ambao familia ya Namouih iliishi. Akamwambia kwamba tayari mipango ya makazi ya muda kwa ajili yake na mwanasheria wake msaidizi ilikuwa ishafanywa, hivyo yeye alitakiwa kuondoka tu pamoja na Blandina haraka sana ili kwenda kushughulika na jambo hilo upesi.

Namouih alikuwa ameshangazwa na uharaka wa mambo hayo yote, akiwa hajajua ni kesi ya nini, ashughulike nayo vipi, na kwa nini ndiyo alikuwa anapewa taarifa hizo wakati huu. Edward Thomas akamweka wazi kwamba huyo "rafiki" yake alikuwa akiandamwa sana na kesi hiyo kwenye masuala ya benki, kwamba alikuwa ameiba pesa nyingi sana, na alihitaji kushinda kwa sababu hakuwa na hatia. Aliahidi kutoa pesa nyingi mno kwa mwanasheria ambaye angemsaidia, na baada ya kuwa amemtafuta Edward ndiyo 'boss' huyu wa Namouih akaona amwambie haraka ili akamsaidie. Kulikuwa na mambo mengi yaliyohusika, ndiyo sababu Edward akawa amemwambia na Blandina amsindikize mwanasheria wake mkuu kwenda kumpa msaada na mambo yoyote yaliyomhitaji, kwa hiyo tayari Blandina alikuwa ameanza kujiandaa ili aelekee huko pia.

Ingawa jambo hilo lilikuja ghafla sana, Namouih akamkubalia mkuu wake wa kikazi, akisema yeye pia angeondoka huku haraka ili kwenda kukamilisha mambo yaliyohitajika huko. Baada ya kuagana na Edward Thomas, Namouih akaanza kumwelezea mume wake kila jambo alilokuwa amekabidhiwa kufanya, akisema kwamba angetakiwa kuwahi ili kumalizana na hayo yote mapema. Efraim Donald akawa anamwangalia kwa umakini tu, kama vile anatathmini mambo aliyoambiwa.

"Efraim... umenielewa?" Namouih akauliza baada ya kuona mume wake yupo kimya tu.

"Ndiyo, nimeelewa," Efraim akajibu.

Namouih akabaki kumtazama kwa njia ya kawaida, lakini kama anasubiri mumewe aseme jambo lingine.

"Kwa hiyo unarudi lini?" Efraim Donald akauliza.

"Sijajua. Hajasema mambo mengi sana, nadhani nitajua kila kitu nikielekea huko. Ila kuona jinsi anavyoniharakisha inamaanisha kwamba usikilizwaji wa hiyo kesi hauchukui siku nyingi... labda hata leo au kesho," Namouih akasema.

"Mmm... so you gotta get to work."

"Yeah."

"Okay."

Namouih alipokuwa anataka kutoka kitandani, Efraim Donald akaushika mkono wake, naye Namouih akamwangalia.

"Hauja... haujasumbuliwa na ndoto mbaya leo?" Efraim akauliza kwa njia ya kujali.

Namouih akatikisa kichwa kukanusha. "Leo hapana. Ila najua sooner or later zitakuja tena... na imekuwa ni kama napuuzia kutafuta suluhisho la hizi ndoto mbaya."

Efraim Donald akatulia kidogo, kisha akasema, "Usijali. Kila kitu kitakuwa sawa. Nenda tu kajiandae... nimetoka safari, na we' unaingia safari."

Namouih akatabasamu kwa mbali, kisha akatoka kitandani na kuelekea bafuni.

Efraim Donald alibaki kitandani akitafakari vitu vingi. Alitarajia kwamba kwa kuwa Namouih alianza rasmi kwenda nje ya ndoa yao basi angepatwa na ndoto mbaya ambayo bila shaka ingemwonyesha mambo fulani, na kujua ni mambo gani hayo ndiyo lililokuwa lengo lake la kumuuliza kama aliota. Namouih kumwambia kwa uhakika kabisa kwamba hajaota ndoto mbaya leo kulimshangaza, kwa kuwa kama alitoka nje na mtu mwingine basi lazima tu kuna mambo yangevurugika, ila haikuwa hivyo. Akashindwa kuelewa kabisa ni nini kilikuwa kinaendelea. Lakini pia, hii safari ya ghafla haikuonekana kuwa kitu kizuri, kwa sababu alihisi uwezekano wa Namouih kwenda huko mkoani kwao ili akutane na mpenzi wake kisiri ulikuwepo, kwa hiyo angehakikisha haondoi jicho lake kwa mke wake ili amwelewe vyema hata zaidi kabla ya kuifanikisha mipango yake.

Mwanaume huyu alikuwa na mambo mengi ya kushughulika nayo, lakini kwa kuwa leo Namouih angeondoka huku basi ilikuwa nafasi nzuri sana ya yeye kumtuma Suleiman aende kule msituni kugundua sehemu ile ambayo mke wake alikwenda ilihusiana na nini, na nani.

β˜…β˜…

Muda mfupi baadaye, Namouih akawa ameondoka jijini kwao kwa ajili ya safari yake ya dharura kikazi. Efraim Donald akawa amempatia Suleiman maagizo ya kwenda kule ambako Namouih alikuwa amekwenda jana, tena aende kwa tahadhari kabisa, kumaanisha abebe silaha endapo kama angekutana na nuksi iliyohitaji kudhibitiwa upesi. Lengo lake lilikuwa kujua huko palikuwa na nini, maana mke wake asingeenda sehemu isiyo na makazi na kukaa kwa muda mrefu bila ya kuwa na kitu chochote cha kutuliza, katika maana ya nyumba iliyojificha. Kama sehemu hiyo isingekuwa na nyumba yoyote basi aliwaza labda mke wake alikuwa anakwenda huko na kufanya mapenzi na hawala yake ndani ya gari, ingawa hiyo haikuonekana kuwa kitu ya Namouih kabisa.

Suleiman alikwenda huko kama maagizo ya Efraim, akifuatilia ramani ya jana, na kiukweli alikuwa anashangazwa na ugumu wa kukariri eneo hilo mpaka kufika huko na kujiuliza Namouih aliwezaje kuingia eneo hilo lililokuwa na mwonekano wa pori kubwa sana. Ni lazima kilichomleta mwanamke huyo huku kilikuwa kitu cha kipekee, na hatimaye akawa amekifikia. Alifika kwenye ile nyumba ya Draxton, naye akatambua kwamba hapo ndiyo ilikuwa sehemu ya kichali cha mapenzi cha mke wa 'boss' wake nje ya ndoa yao. Suleiman akajaribu kumpigia Efraim Donald ili amweleze alichokipata, lakini mtandao ukakataa. Hivyo, akaamua kushuka kutoka ndani ya gari na kwenda kuichunguza nyumba hiyo.

Ile hali yenye kutisha kutokana na eneo hilo la msitu kufunikwa vyema na matawi ya miti pamoja na ukimya wa hali ya juu ni vitu anbavyo Suleiman alihisi vyema, lakini alikuwa na moyo mgumu sana kuogopa chochote. Akaikaribia nyumba hiyo na kuanza kuikagua kwa kuizunguka. Aliona jinsi iliyokuwa imeundwa kwa ubunifu wa hali ya juu, na angeweza kusema kwamba ilikuwa ni ya muda mrefu. Haikuonekana kuwa nyumba iliyojengwa na watu wa msituni hata kama wangekuwepo, maana kuna vitu vilipangiliwa kwa njia ya kisasa zaidi.

Mlango wa kuingilia hapo ulikuwa umefungwa kwa kufuri zito, naye akachungulia ndani kupitia vioo vya madirisha yale na kuona kwamba kulikuwa na vitu vizuri vya kisasa hata ndani pia. Hakuwa na shaka yoyote kwamba hii ndiyo iliyokuwa sehemu ambayo mke wa Efraim alikuja kufanyia usaliti na mpenzi wake mwingine, na kwa sababu ya kukosa mtandao huku, akaamua kuchukua picha za nyumba hiyo kwa kutumia simu yake ili aweze kwenda kumwonyesha 'boss' wake, halafu amsikilize kuhusu ni nini ambacho angetaka wafanye kuhusiana na jambo hilo. Akapiga picha mbili tatu, kisha akarudi kwenye gari lake na kuondoka msituni hapo.

Alipofika jijini zaidi, akamwambia Efraim kwa njia ya simu kwamba alipata jambo jipya kutokana na uchunguzi wake kule alikoenda, na ndiyo alikuwa anampelekea Efraim Donald ofisini. Efraim akamwambia awahishe ili aone mwenyewe, na baada ya dakika kadhaa Suleiman akafika ofisini kwa mkubwa wake na kumfikishia ushahidi sasa. Efraim alizitazama picha zile kwa umakini sana, naye akatabasamu na kutikisa kichwa kwa kusikitika sana. Suleiman akamwambia kwamba ikiwa angetaka, basi amwagize arudi kule ili aichome ile nyumba moto, lakini Efraim akasema hiyo ingekuwa ni kazi bure.

Kama alitaka kumkamata mtu aliyemtoa mke wake ndani ya ndoa yao basi alichotakiwa kufanya ilikuwa kumshika akiwa huko huko ili ammalizie huko huko bila Namouih kujua, na kwa sababu sasa hivi mke wake alikuwa ameondoka, akamwambia Suleiman arudi kule baadaye ili aweke kifaa fulani kidogo sana cha camera kama mtego ili mtu yule akifika kule tu endapo Namouih hatakuwa amerudi jijini bado, basi amfate na kummaliza. Ingawa alielewa kwamba huenda aliyemrubuni mke wake mpaka akaanza kwenda nje ya ndoa yao hangekuwa huku hasa baada ya Namouih kuondoka, bado njia hiyo ingemnasa tu akirudi. Hata huko Namouih alikoenda kuna macho yangekuwa yanamtazama, kwa hiyo njia zake zote Efraim zingekuwa na matokeo chanya kama tu ndege mwarabu wa mke wake angeingia mtegoni.

Akamwamuru Suleiman aondoke kwenda tena kule kufanya hayo, naye akampatia pesa nyingi sana, kisha jamaa akaondoka. Efraim alikuwa amejawa na hasira sana, akimwaza mke wake na mtu aliyetoka naye nje ya ndoa yao tu, naye akawa amekunja ngumi kwa nguvu sana akiitafakari adhabu kali aliyokuwa amepanga kumpa mtu aliyekuwa anaiba mali yake pekee!


β˜…β˜…β˜…


Safari ya Namouih kuelekea mkoa ilipoishi familia yake ilimchukua mwanamke huyu masaa kadhaa kwa gari lake mwenyewe, naye alifika huko kwenye mida ya saa kumi na mbili jioni. Ilikuwa mbali na angefika usiku sana kama angekuwa amechukua usafiri wa basi, naye akaelekea moja kwa moja kwenye hoteli aliyokuwa amepangiwa kuchukua chumba cha muda katika makao yake huku. Tayari alikuwa amewasiliana na Blandina, rafiki yake huyo akisema yeye tayari alikuwa ameshafika hapo dakika chache nyuma na ndiyo alikuwa ameingia ndani ya chumba walichopewa.

Ilikuwa hoteli ya kifahari kwa kadiri kubwa, hivyo Namouih alielewa kwamba hata chumba walichopewa kingewatoshea wote kwa pamoja. Kutokana na kutofahamu wangekuwa huku kwa muda mrefu kadiri gani, wote walikuwa wamebeba nguo kadhaa za ziada kwa ajili ya kazi na za kuvaa kawaida. Kulikuwa na mtu aliyewekwa tayari kwa ajili ya mapokezi ya wanawake hawa kwenye hoteli hiyo, hivyo Namouih akaongozwa kuelekea chumba chao na Blandina, kilichokuwa ghorofa ya nne kwenye jengo hilo, naye akaingia na kumkuta Blandina akiwa ndani amekaa kwenye kitanda huku anatazama tamthilia kwenye TV ya flat screen ukutani.

"Wooow!" Blandina akasema kwa shauku na kuanza kumfata Namouih huku anatabasamu.

Namouih akaachia tabasamu hafifu pia, naye Blandina akamfikia karibu na kumkumbatia.

"Karibu Nam. Za safari?" Blandina akauliza huku akivunja kumbatio lake na Namouih.

"Nzuri tu. Vipi wewe?"

"Safi. Nimewahi kufika utafikiri nimekuja kwa ndege..."

"Ahahah... umejitahidi."

"Mwenzangu, ndiyo ilikuwa kukurupushwa asubuhi asubuhi..."

"Yaani!"

"Mhm... njoo upumzike, nimeambiwa chakula kinakuja," Blandina akasema hivyo na kuelekea kitandani tena.

Namouih hakuwa amesahau kuhusu siri nzito aliyoficha dhidi ya rafiki yake kipenzi, siri ya usaliti mkubwa kumwelekea. Hapa kuigiza kwamba kila jambo lilikuwa sawa ilikuwa lazima, kwa hiyo akajitahidi kuiondolea akili yake mawazo ya hatia na kuvua nguo ili aingie bafuni kujimwagia, kisha akarejea kwa rafiki yake na kuketi naye kitandani kwa njia ya kupumzika. Blandina alikuwa amevalia T-shirt nyeupe nyepesi na kikaptura kifupi sana cha rangi ya pink, naye Namouih alivaa gauni fulani nyepesi sana kama dera lakini iliyoonyesha viungo vyake, na wote walizibana nywele zao za kusukwa.

Namouih akawa amefungua laptop yake huku Blandina akiendelea kutazama runinga na ku-chat kwenye simu yake. Kitu kilichovuta uangalifu wa Namouih kutoka kwenye laptop yake kumwelekea rafiki yake ni namna ambavyo Blandina alikuwa anatabasamu sana alipokuwa akijibu jumbe za kwenye simu, na Namouih akawaza kwamba bila shaka alikuwa ana-chat na Draxton. Hakuwa amemtafuta wala kutafutwa na mwanaume yule tokea walipoachana jana, na kiukweli tayari akili yake ilikuwa inamtafakari sana mwanaume huyo baada ya kufika hapo hotelini.

"Uko kwenye love zone, I presume?" Namouih akauliza huku akiendelea kubofya kwenye laptop.

"Mm?" Blandina akaguna kwa kuuliza kwa kuwa hakumsikia.

"Una-chat na Draxton?" Namouih akauliza.

"Yeah. Baby Drax amenimiss sana it seems," Blandina akamwambia.

"Mmm... ulimwambia unakuja huku?"

Blandina hakujibu swali hilo la Namouih kwa kuwa aliendelea kuweka umakini wake kwenye simu, na hilo likamfanya Namouih audhike kiasi.

"Blandina... umeshafatilia chochote kuhusu hiyo kesi?" Namouih akauliza.

"Yeah," Blandina akasema kwa ufupi.

Namouih akamwangalia na kusema, "Unaweza kuelezea au?"

Blandina akamwangalia na kuona yuko makini sana, kisha akasema, "Sorry Nam... wacha nikuelezee."

Namouih akawa anaonekana kuudhika sana, na Blandina aliona hilo ila akawa hajaelewa sababu.

"Tunayemtetea anaitwa Douglas Temba, ana historia ya accountancy kwenye benki kubwa kubwa kwa miaka zaidi ya 10, na kufikia wakati huu alikuwa ametumikia kama mkurugenzi mtendaji ndani ya benki ya kibinafsi kwa miaka mingine 10... benki yetu ya kijani..." Blandina akaongea kwa mbwembwe.

"Mm-hmm..."

"So... now kulikuwa na hizi process za kumpandisha cheo, kumfanya awe vice president kabisa, ila amekamatwa kuwa subject wa wizi wa shilingi milioni 140 za benki," Blandina akaeleza.

"140? Ni nini kilimzuia kuiba zaidi?"

"Sijajua. Zilikutwa kwenye akaunti yake, ila anasema hajajua zimeingiaje, kwamba anasingiziwa..."

"Well, ndivyo ninavyoona pia. Ametumikia kazi yake kwa zaidi ya miaka 20 bila kuwa na case za namna hiyo, halafu sasa hivi anaenda kupandishwa cheo mara ghafla kageuka mwizi, really?"

"Tutapaswa kupiga kazi vyema. Tunakutana naye kesho. Utaona jinsi mambo yalivyo, na Edward yuko hell bent kuhakikisha Douglas hagusi jela maana ni rafiki yake sana. We'll need to get him out of this at all costs," Blandina akasema.

"Na si ndiyo katuahidi pesa nyingi?"

"Yeah. Lakini pia nikafikiria... vipi kama ni kweli... je kama kaziiba hizo pesa?"

"Tumeshabebeshwa mzigo wa kesi yake Blandina, hakuna namna. Tufanye tu kazi yetu, end of story," Namouih akaongea kwa njia iliyoonyesha hakujali.

Akaendelea kubofya kwenye laptop yake, naye Blandina akawa anamwangalia kwa umakini.

"Kama... kama ndiyo hivyo... endelea ku-chat... mengine zaidi nitajua kesho," Namouih akasema.

"Uko... sawa, Namouih?" Blandina akauliza.

Namouih akamwangalia.

"Unajua... hizi siku chache zilizopita mimi na wewe hatujazungumza sana. Sikuwa nime...tilia maanani jambo hili ila ni kama... umekuwa distant nami yaani... kuna kitu kinakusumbua?"

Namouih akaendelea kumwangalia tu usoni, akiwa ameshindwa kujua cha kusema.

Blandina akamshika begani na kusema, "Ni Efraim eeh? Bado anasumbua kichwa?"

Namouih akatikisa kichwa kukubali, naye akasema, "Mambo ni mengi. Lakini angalau hajapoteza ule mguso wake aliokuwa nao mara ya kwanza tumekutana... kwa hiyo naendelea kuvumilia maana naweza kusema na yetu bado changa."

"Pole. Sijui sana kwa level yako ila naweza kusema naelewa. Unampenda sana mtu, ila anakuvunja moyo, lakini huachi kumpenda. Mhm... imekuwa kama shida, au laana kwetu sisi ma-best... ila ina raha yake ndani ya hiyo hiyo shida," Blandina akasema.

Namouih akatabasamu kwa mbali.

"Usijali. Nina imani kila jambo litakuwa sawa. Tuendelee tu kuvumilia Nam-Nam," Blandina akamwambia kwa kujali.

Namouih aliendelea kumtazama rafiki yake, naye Blandina akairudia simu yake na kuendelea kuwasiliana na Draxton. Hisia za hatia ziliendelea kumsumbua Namouih kila mara alipokumbuka penzi lake la siri na mpenzi wa Blandina, na hii hasa ilikita mizizi kwa huku kwa sababu alikuwa pembeni ya rafiki yake, hivyo akaamua tu kufunga laptop yake na kuanza kuelekea nje. Blandina akawa anamkumbusha kwamba chakula kwa ajili yao kinaletwa hivyo asiende mbali, naye Namouih akakubali na kwenda kusimama nje ya chumba chao.

Ilikuwa ishafika saa mbili, na Namouih akasimama pembezoni mwa mlango wa chumba chao akihisi kuchoka kihisia. Lakini pia, alikuwa anamuwaza Draxton. Ingawa alitaka wasiongee kutokea jana, baada ya kuona namna ambavyo Blandina alikuwa amezama kwenye furaha yake pamoja na mwanaume yule kulimfanya aikumbuke sehemu aliyonayo mwanaume huyo ndani ya maisha yake pia, na hilo likamfanya amkose sana. Lakini bado hakuwa na jinsi ya kuanza kumtafuta kwa wakati huu hata kama alijiona mpweke kwa kadiri fulani, na hivyo akajihakikishia moyoni mwake kuwa angeendelea kuvuta subira kwanza. Akiwa anawaza mambo hayo, akageuza mwili wake na kuangalia upande mwingine wa korido pana na refu la ghorofa aliyokuwepo, na kufikia mwishoni kabisa, akaona jambo fulani lililovuta umakini wake.

Huko palikuwa na kuta ya mwisho iliyotenganisha korido hili na korido la upande wa vyumba vingine, ambapo kulikuwa pia na milango ya lifti ya hoteli, na sehemu hiyo alikuwa amesimama mtu ambaye hakuonekana uso vizuri. Alivaa nguo za kawaida tu, lakini kofia aliyovaa kichwani ilipitilizishwa mpaka mbele zaidi ya uso wake na hivyo haungeweza kuonekana vyema. Namouih alibaki kumtazama tu kwa umakini, na mtu huyo, aliyeonekana kumtazama mwanamke huyu, akaanza kuondoka taratibu, kana kwamba alikuwa amesimama hapo kwa makusudi ya kumwangalia au kumchunga Namouih.

Namouih aliingiwa na wasiwasi kwa kweli. Hakupenda jambo hilo hata kidogo. Ilimfanya akumbuke kuhusu kipindi kile baba yake anaumwa sana, namna ambavyo kuna mtu aliyekuwa anamfatilia na kumtokea mara kwa mara nyakati za usiku. Akawaza labda sijui mambo yale ya ndoto na maono yenye kutisha yalikuwa yameanza kumwandama tena, lakini hangeweza kujua kwa uhakika, kwa sababu mtu huyo alikuwa ni mmoja wa watu wa Efraim Donald walioagizwa kuchunga nyendo za mke wake ili kuona kama angekutana na mwanaume mwingine, kisha wamtumie taarifa.

Ni wakati huu ndiyo Namouih akaanza kumwona mhudumu maalumu wa hoteli hiyo upande huo huo ambao alikuwa ametoka kumwona mnyatiaji yule, akiwa anasukuma kama meza fupi yenye magurudumu madogo iliyobeba vyombo kadhaa vyenye chakula ndani. Akaendelea kumtazama mpaka alipofika usawa wake, naye akamwambia kwamba ameleta chakula kwenye chumba chenye namba 507. Hicho ndiyo chumba walichopewa warembo wetu, hivyo Namouih akamwambia akiingize ndani hapo kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa mmiliki wa muda pamoja na rafiki yake. Mambo haya yote alikuwa anagharamia Edward Thomas, kwa hiyo vyakula na mambo mengi tayari vilikuwa vimelipiwa. Mhudumu akapeleka vyakula hivyo ndani na kumwacha Namouih akitazama tena upande ule kwa umakini, kisha akarudi ndani ya chumba chao na kupotezea suala lile.



β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

ITAENDELEA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…


Usikose sehemu za mwendelezo wa hadithi hii kali ya CHANGE. Ni story nzuri na ndefu sana. Waweza ipata nakala yote kwa gharama nafuu sana. Karibu WhatsApp au kwa inbox ya hapa hapa JF.

WhatsApp no: +255 678 017 280
 
CHANGE

Story by Elton Tonny

Urafiki, Familia, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Ukatili, Mauaji, Mambo yasiyotazamiwa, Mambo yenye kuhofisha

R-rated 18+

Enjoy!

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…


Siku iliyofuata, mapema kabisa wanawake hawa marafiki wakajipa maandalizi mazuri sana kwa ajili ya kwenda kukutana na Douglas Temba ili waanze kushughulika na kisa chote kilichozunguka kesi aliyokuwa nayo. Walikwenda kumwona kule alikokuwa akishikiliwa na maafisa wa ulinzi, ambako palikuwa kwenye jengo maalumu la kuwahifadhi watuhumiwa wa mashtaka, na yeye alikuwa ndani ya chumba cha peke yake tu chenye mwonekano salama sana tofauti na vyumba vya rumande za kienyeji! Alikuwa mtu mwenye pesa, na alionekana kuwa mstaarabu, ila alikuwa amekasirishwa sana na tuhuma zilizowekwa juu yake, na hivyo akawa na uhitaji mkuu wa kushinda kesi hiyo ili awe huru.

Baada ya Namouih na Blandina kuongea naye, walipata kujua mambo mengi ambayo wangeyatumia kwa ajili ya kumtetea. Alitaja watu hususa ambao alifikiri walihusika na mchezo uliofanyika wa kumshikisha na pesa zile zilizodaiwa kuibwa naye, na hivyo hiyo ingewapa Namouih na Blandina kazi ya kuchimba zaidi kuhusu mambo yote hayo ili wapate ushindi kwa njia nzuri, na kuwafichua wafitini waliotaka kumharibia sifa mzee wa watu. Angeweza hata kusema atoe pesa yake mwenyewe kwa ajili ya faini waliyotaka kumtoza lakini hangeruhusu jambo hilo kwa sababu alikuwa ameonewa, na alielewa waliomfanyia hayo walitaka tu kumkomoa maana mambo yake mengi yalikuwa yananyooka. Alikuwa mwanaume mtu mzima vya kutosha kabisa kumzaa Namouih, naye akasema angempa mwanamke huyu zawadi nzuri sana kama angemsaidia; siyo kwa sababu tu alikuwa na pesa kwa kadiri fulani, bali kwa kuwa kazi ambayo wanawake hawa wangefanya ingestahili pongezi endapo kama wangefanikiwa kupata ushindi.

Basi, kwa kuwa sasa waliweza kuonana na kuzungumza na mwanaume huyo, Namouih na Blandina wakaelekea kwenye ofisi ya hakimu ili kuweka mambo mengi rasmi zaidi juu ya usimamizi wa kesi ya Douglas Temba. Walielekezwa taratibu zilipofikia, taarifa za mwanasheria wa upande wa mashtaka, na tarehe ya usikilizwaji mkuu wa kesi (trial). Ingechukua siku tano tu, kwa hiyo labda marafiki hawa wangekaa kwenye mkoa huu kwa zaidi ya wiki moja. Namouih alikuwa ameshafikiria njia nyingi za kufanikisha ushindi wa kesi hii, na kiukweli wakati huu alikuwa makini sana. Alitafuta, kwa msaada wa Blandina, mambo yote yaliyotumiwa kama vigezo vya ushahidi dhidi ya Douglas Temba ili ausome mchezo wa watu waliotaka kumwangusha mwanaume yule, naye akawa amejihakikishia njia nzuri za kuwafichua na kumsaidia Douglas apate ushindi.

Imefika mida ya saa nane mchana, wawili hao wakarejea hotelini na kupata chakula pamoja, kisha wakakaa na kutulia kwa ufupi. Namouih alikuwa ametafutwa na mume wake mara kwa mara ili kujuliwa hali, naye akawa anamwambia yuko poa kabisa huku aliko, na kwamba kazi iliyowaleta huku ingechukua siku kadhaa kabla ya yeye kurudi jijini kwao. Blandina akawa anamwambia Namouih kwamba kwa leo alikuwa amemtafuta Draxton asubuhi na kumpata vizuri tu, ila kwa sasa kila alipomtumia ujumbe au kumpigia simu, hakumpata. Namouih yeye tayari alikuwa amekisia kwamba huenda Draxton angekuwa kule msituni bila shaka, hivyo akamwambia Blandina labda mtandao kule ulisumbua au simu ya jamaa ilizima. Sasa Blandina akawa anahisi ni kama vile hana cha kufanya, kwa hiyo akamwambia Namouih walale ili usiku watoke kwenda kujifurahisha mjini kama alivyopenda.

Namouih akamwambia ni wazo zuri, ila yeye alikuwa amewaza kitu kingine. Akamwambia kwamba alipanga kwenda nyumbani kwao, aifanyie familia yake kama "surprise" ndogo ya ujio wake wa bila kutarajiwa, kwa sababu alikuwa amewakumbuka sana. Blandina akamwambia hilo ni wazo zuri sana ila akahofia kwamba familia yake ingemng'ang'ania kwa muda mrefu, naye Namouih akasema angekaa nao kwa muda fulani kisha ndiyo yeye na rafiki yake wangekuja kujifurahisha. Kwa hiyo Blandina yeye angebaki hapo hotelini kulala, halafu Namouih angekwenda nyumbani kumwona Zakia na Nasma; alikuwa na hamu kubwa sana ya kuwaona wapendwa wake tena, na ni jambo ambalo angalau kwa huku lingempa ahueni kiasi kutokana na mikazo mingi ya kihisia aliyokuwa anapitia. Kwa hiyo Blandina akajitupa kitandani ili aupige usingizi wake, naye Namouih akaanza kujiandaa ili aelekee nyumbani.

β˜…β˜…

Mwanasheria mrembo Namouih aliondoka hotelini na kwenda moja kwa moja mpaka nyumbani, walipoishi watu wa familia yake. Ingawa alikuwa na hamu kubwa sana ya kuona itikio lao pale atakapokutana nao, Namouih hakuwa kama binti mwenye mchecheto, yaani aanze kuchekelea sana kana kwamba ameenda sehemu iliyopita upekee wa kawaida, bali alikuwa ameweka sura tulivu tu na kutarajia kupokelewa vyema nyumbani hapo. Kwa sehemu kubwa ya ujirani, mambo mengi yalikuwa yamebadilika, lakini mpangilio wa mtaa na nyumba nyingi zilikuwa kama vile alivyozikumbuka tu.

Alikuwa amefika hapo nyumbani kwao kwenye mida ya saa kumi jioni na kuliegesha gari lake upande wa nyuma wa nyumba, naye angeweza kuona baadhi ya watu na watoto wakisimama kuangalia gari lake lililofikia hapo; bila shaka wakitaka kujua nani amekwenda kwa Zakia. Akashuka taratibu, akiwa amependeza sana kama kawaida yake, na wale wote waliomwona wakaendelea kumtazama tu kana kwamba wameona kitu kigeni sana. Kulikuwa na watoto waliopenda kucheza kwenye uwanja wa sehemu hiyo ya nyumba yao, hivyo wakawa wanamwamkia naye kuwaitikia vizuri. Ni hapa ndipo binti fulani mwenye rika kama la Sasha akawa amekuja upande wake na kusimama; akimtazama usoni huku anatabasamu.

Namouih hakumtambua haraka, lakini tabasamu hilo lilimaanisha anafahamika kwake. Alikuwa mweusi kiasi, mwenye umbo zuri kama tu Blandina alivyokuwa ameumbika, naye alikuwa amevaa blauzi laini na khanga iliyomsitiri vizuri kwa chini. Namouih akawa amemfikia karibu zaidi, na mwanadada huyo akamwamkia na kusubiri Namouih aitikie. Namouih akaitikia salamu yake vizuri sana, kisha akamuuliza ikiwa walifahamiana. Binti huyo akamwambia anaitwa Manka, kitu kilichomfanya Namouih atambue kwamba ni mtoto wa ndugu yao ambaye ndiyo aliishi pamoja na Zakia kwa sababu alihudhuria masomo huku, naye akamsifia kwa kusema amekua sana. Aliwahi kumwona wakati yuko mdogo zaidi, ila sasa kweli alikuwa amekua na kuwa mwanadada mzuri sana.

Manka akamkaribisha Namouih vizuri sana, naye Namouih akaanza kumfata taratibu. Aliweza kutambua kwamba kuna majirani fulani kwenye nyumba ya pembezoni waliokuwa wanamchungulia dirishani, naye akachekea kwa chini tu kwa sababu vitu kama hivyo alivizoea sana huku mitaani kwao, na ilikuwa ni kitambo kirefu toka alipofika hapo. Manka akamkaribisha ndani, mpaka sebuleni, naye Namouih akaenda na kuketi sofani. Mpangilio wa ndani hapo ulikuwa mzuri sana, na palikuwa safi. Kulikuwa na marafiki zake Manka watatu waliokuwa pamoja naye hapo, nao pia walimfahamu Namouih na kumsalimu kwa heshima, kisha wakatoka sehemu ya sebuleni na kuelekea upande wa jikoni. Manka akawa amemfatia Namouih juice baridi kutoka kwenye jokofu, huku marafiki zake wakiongelea kuhusu namna mwanamke huyo alivyokuwa mzuri sana mpaka kukera.

Baada ya Manka kumletea Namouih juice, akaiweka mbele yake kwa heshima sana, na Namouih akashukuru. Akamuuliza binti huyo ni wapi ambako mama yake alikuwa, naye Manka akamwambia kwamba Zakia alikuwa ameenda kwenye mikutano ya vikundi na wanawake wenzake, na Nasma pia hakuwa ametoka shule ila ndiyo muda huu angekuwa anarudi. Namouih akasema haina shida, naye akaanza kumuuliza Manka kuhusu familia yake na maendeleo yake shuleni. Manka alikuwa msichana aliyejua kujieleza vizuri, na Namouih akatambua pia kwamba binti huyo alikuwa mpole lakini mchangamfu. Alimwona kama Sasha tu, naye akapendezwa naye upesi sana.

Hazikupita dakika nyingi na Nasma akawa amerejea kutoka shuleni. Namouih alifurahi sana kumwona, naye akamwita aje kumsalimu. Lakini, Nasma alionekana kuchoka sana, kama vile alikuwa ametembea mwendo mrefu mno kutoka shuleni ingawa shule yao haikuwa mbali kihivyo, na waliletwa kwa basi la shule. Alikuwa amefurahi sana kumwona dada yake, lakini uso wake ulikuwa na uchovu sana kiasi kwamba hakuweza hata kuonyesha furaha hiyo kwa kutabasamu. Akawa anatembea polepole sana kumwelekea dada yake, na jambo hilo likamshangaza Namouih kwa kiasi kikubwa.

Nasma alipomfikia Namouih karibu zaidi, akamkumbatia kivivu kwa kulalia bega lake.

Namouih akapokea kumbatio lake na kusema, "Nasma... vipi... unaumwa?"

Nasma akatoa mguno kukanusha.

Namouih akamwangalia na kumtoa mwilini mwake, kisha akasema, "Mbona hivyo? Hujala?"

"Nimekula. Nimechoka tu dada. Nataka kulala," Nasma akasema kwa sauti ya deko huku akiangalia chini.

Namouih akamwangalia Manka, ambaye alikuwa anawatazama pia, kisha akasema, "Nenda kaoge kwanza, sawa? Ulikula saa ngapi?"

"Mchana," Nasma akajibu.

"Kaoge... Manka atakuwekea chakula kidogo ili ule tena, sawa? Maji umekunywa?" Namouih akaongea kwa kujali.

Nasma akatikisa kichwa mara moja lakini taratibu sana kukubali, na Namouih akamwambia aende chumbani sasa.

Binti akaondoka hapo polepole, akijivuta sana yaani mpaka Namouih akahisi labda anaumwa.

"Leo asubuhi ameondoka namna hiyo?" Namouih akamuuliza Manka.

"Ndiyo yaani... anakuwa anaenda shule kawaida... anarudi kwa mtindo huo, nikimuuliza kama anaumwa anasema tu amechoka. Yaani dada siku hizi Nasma siyo mchangamfu kihivyo... nilidhani labda kuna mtoto huko shuleni huwa anamsumbua sijui ila hakuna taarifa yoyote ya namna hiyo," Manka akaeleza.

"Na mama? Ameshaongea naye labda?" Namouih akauliza.

Manka akatazama chini kwa ufupi na kumwangalia tena Namouih usoni.

Namouih akamtazama kwa umakini.

"Sijajua kama shangazi ameongea naye au nini ila... anachukulia kila kitu kiko sawa," Manka akasema.

"Anachukulia? Kumaanisha haongei na mtoto, si ndiyo?" Namouih akauliza kwa uthabiti.

Manka akabaki tu kimya na kuangalia pembeni, na Namouih akatazama chini kwa umakini.

"Ngoja... nikampakulie Nasma..."

Manka akasema hivyo, kisha akaelekea sehemu ya jikoni. Marafiki zake walitoka nje kwa sababu walikuwa wanasukana, kwa hiyo Manka alipomaliza kuandaa chakula akakiweka kwenye chombo kilichofunikwa na kukiweka mezani, halafu akasema anakwenda nje kwa rafiki zake mara moja kisha anarudi kumwangalia Nasma. Lakini Namouih akakanusha, akimwambia aende tu kwa rafiki zake hapo nje ili yeye akamwangalie mdogo wake, lengo lake likiwa kuona kama angejua ni nini kilichokuwa kinamsumbua.

Hivyo Manka akaelekea nje, na Namouih akanyanyuka na kuanza kuelekea chumbani. Kulikuwa na bafu la ndani na la nje pia, na alikuwa anategemea labda Nasma angekuwa amemaliza kuvua nguo ili aende kuoga, lakini alipoingia chumbani akamkuta mtoto amelala tu kwenye kitanda. Akasimama kwa ufupi na kumwangalia kwanza. Nasma hakuwa hata amebadili nguo za shule, na jinsi alivyojilaza kitandani ilikuwa kwa ule mtindo wa mtu aliyechoka kupitiliza, na Namouih akaanza kumfata taratibu mpaka alipofika usawa wake. Akakishika kichwa na shingo yake, nazo zilikuwa zimechemka sana kama kuonyesha ana homa kali. Hisia ya kujali zaidi kuhusu hali ya mdogo wake ikaongezeka, naye akaanza kumwamsha huku akimvuta.

"Nasma... Nasma..."

"Mmm..."

"Amka... amka mdogo wangu..."

Namouih akamnyanyua, Nasma akiketi kivivu sana, naye ikabidi akae kitandani hapo karibu yake, miguu yao wote ikikanyaga chini. Akawa anamwangalia kwa umakini sana, huku Nasma akionekana kuwa kama mtu mwenye usingizi mzito.

"Nasma, nini shida?" Namouih akamuuliza kwa kujali.

Nasma akatikisa kichwa kuonyesha hakukuwa na shida. Tena, na hapa alionekana kama mtu mwenye usingizi sana, alikuwa amechoka, na hali hii ikamtatiza mno dada yake. Akamshika kichwani kuhisi joto kwa mara nyingine, na kiukweli alikuwa amechemka.

"Unaumwa? Mbona umechemka hivi? Kwa nini unaumwa halafu bado unaenda shule? Umemwambia mama kwamba unaumwa?"

Kimya.

"Nasma... naomba unijibu nikikuuliza swali. Umeanza lini kuumwa na mbona husemi ukapewa dawa au kwenda hospitali?" Namouih akauliza kwa kujali lakini kwa ukali kiasi.

Nasma akamtazama kivivu, macho yake yakionyesha machozi yaliyokaribia kumwagika.

"Niambie mdogo wangu... tatizo ni nini? Kuna kitu mama amekufanya? Niambie. Niambie ili nimfundishe adabu," Namouih akambembeleza kwa njia hiyo, akisubiri jibu kutoka kwa mdogo wake.

"Nimechoka..."

Hayo ndiyo maneno yaliyofanikiwa kutoka kinywani mwa binti huyo. Namouih akashindwa kuelewa alimaanisha nini.

"Wewe... unamaanisha nini? Ume..ume..umechoka kwenda shule au?" Namouih akauliza huku presha ikianza kupanda.

"Nikimwambia mama hanisikilizi..." Nasma akaongea taratibu sana.

Machozi yakaanza kumtoka Namouih, bila hata ya yeye kuwa amejua sababu. "Nasma niambie unamaanisha nini. Mama amekufanyaje? Umemwambia nini hajakusikiliza? Ulimwambia akupeleke hospitali akakataa? Nini kinakusumbua? Sema..."

Alikuwa anamwomba aongee namna hiyo huku amemshikilia mabegani, na mwili wa binti huyu mdogo ulikuwa legevu sana.

"Mwa... mwalimu... mwalimu Joseph...."

Namouih akaacha kukaza macho yake na kubaki amemwangalia kwa njia iliyoonyesha mshtuko kabla hata mtoto hajamalizia maneno hayo. Ni kama tayari angeweza kukisia alikokuwa anaelekea, lakini bado akawa hataki aelekee huko.

"Mwalimu Joseph... mwalimu Joseph amefanyaje? Huwa anakupiga? Huwa anakupiga sana?" Namouih akauliza.

Nasma akawa anageuza shingo yake huku na huko, akionekana kupata shida fulani hivi, na Namouih aliposhika tena kichwa chake, kilikuwa cha moto sana.

"Twende Naa... twende hospitali now..."

Namouih akasema huku akinyanyuka, na alikuwa ameanza kumvuta mdogo wake pia ili watoke pamoja, lakini Nasma akaachia kilio kidogo kilichoonyesha aliumia kiasi. Namouih alipomwangalia usoni, alikuwa amekunja sura kama anataka kulia, naye akamwambia ajikaze ili waende kwenye gari upesi. Lakini Nasma alikuwa anagoma kwenda kabisa, kama vile hataki kutoka sehemu hiyo aliyosimama, na baada ya Namouih kumwangalia kwa chini, macho yake yakatanuka baada ya kuona michirizi ya damu ikishuka kutoka kwenye mguu wake wa kushoto! Akamwangalia Nasma usoni na kuona jinsi neno "naumia" lilivyoitawala sura yake.

"Naa!"

Namouih akaita hivyo akiwa ameshangaa sana. Nasma akalegea zaidi na papo hapo kudondoka chini!

Namouih akaanza kumwita, kwa wasiwasi mwingi sana, akijaribu kumwamsha kwa kuwa fahamu zilikuwa zimemtoka. Manka alikuwa nje na rafiki zake wale aliposikia Namouih akisema kwa sauti ya juu sana, naye akaenda ndani upesi kujua tatizo lilikuwa nini. Namouih akawa anajitahidi kumnyanyua mdogo wake kwa uangalifu sana, na ni hapo ndiyo Manka akawa amefika nje ya mlango wa chumba hicho na kumwita ili ajue kama alihitajika. Namouih akamwambia aingie ndani ili amsaidie, naye Manka akaenda na kuanza kusaidizana na Namouih kumtoa Nasma nje.

Wakatoka na kuelekea mpaka ndani ya gari lake Namouih, huku marafiki zake Manka wakisindikiza jambo hilo kwa ukaribu mpaka walipofanikiwa kumwingiza mtoto kwenye gari. Manka akamwambia Namouih anarudi kule ndani kuifunga nyumba kisha anakuja, naye akatoka upesi akimwacha Namouih ameanza kuwasha gari. Baada ya Manka kuifunga nyumba haraka akarejea kwa Namouih na kukuta ndiyo analigeuza gari, kisha likatulia kidogo kumruhusu aingie, naye akaliondoa hapo upesi sana kuelekea hospitalini.

β˜…β˜…

Nasma alifikishwa kwenye hospitali ya serikali na kupelekwa moja kwa moja kwenye chumba cha wagonjwa mahututi. Namouih alikuwa akitokwa na machozi kwa sababu ya hofu kubwa sana, naye Manka akawa pembeni yake tu akisubiri. Namouih akatoa simu yake na kuanza kumtafuta Zakia, mama yake, lakini akawa hampati. Akamuuliza tena Manka kwa mara nyingine ni wapi ambapo mama yake angekuwa, naye Manka akajibu vile vile, kwamba atakuwa kwenye vikundi vyao vya wanawake bila shaka.

Namouih aliweza kuona aina fulani ya udanganyifu kwenye maneno ya binti huyo, naye akambana zaidi kwa kumwambia aseme ni wapi mama yao alikuwa. Ndipo Manka akafunguka. Akamweleza Namouih kwamba mama yake hupenda kwenda nje na kijana fulani, mwenye umri mdogo kwake, akiwa kama mpenzi wake. Hata leo, kijana huyo alikwenda pale nyumbani, kisha baada ya muda ndiyo wakaondoka pamoja bila yeye kujua walikoenda. Namouih hangeshangazwa na tabia hiyo ya mama yake ya kupenda vijana wadogo, kwa sababu tokea baba yake amekufa, Zakia alikuwa anatoka kimapenzi na wanaume wa namna hiyo, ila Namouih akawa anataka kujua ni namna gani Nasma amekuwa akiishi kwa muda mrefu sasa.

Manka akamwelezea mengi. Akasema mtoto amekuwa akijitenga sana, jinsi alivyokuwa mchangamfu mwanzoni siyo ambavyo alivyo sasa. Mara nyingine angerudi kutoka shule akiwa amenyong'onyea sana, na hata kama yeye Manka angejaribu kuongea naye, Nasma asingesema lolote lile zaidi tu ya kusema kwamba alikuwa amechoka. Akasema mtoto alilala sana pia. Yaani angetoka shuleni na kufikia kulala kwa masaa hata zaidi ya manne kabisa, na Zakia hakuwa hata na muda wa kufuatilia maendeleo yake ya shule labda mpaka imlazimu, kwa sababu alifurahia zaidi matembezi na kijana wake. Namouih alikuwa ameshapatwa na hofu nyingi sana hasa baada ya kile ambacho Nasma alitoka kusema muda mfupi nyuma. Hakutaka kile ambacho alidhani ndiyo shida yenyewe kiwe kweli, lakini angetakiwa kusubiri kusikiliza ni nini ambacho daktari angesema.

Baada ya dakika nyingi kupita, daktari aliyekuwa amekwenda kushughulika na Nasma akatoka nje, huku wauguzi kadhaa wakitoka na kuingia humo pia. Alikuwa mwanaume mwenye umri mkubwa kama tu baba yake Namouih, na mwanamke huyu akamfata ili ajue hali ya mdogo wake.

"Wewe ni..." Daktari akawa anauliza, kwa upole.

"Dada yake. Anaendeleaje? Nini tatizo?" Namouih akaongea kwa hisia.

"Unamaanisha haujui alikuwa akisumbuliwa na nini?" Daktari akauliza tena.

"Ahh... yaani ndiyo nimefika leo nyumbani nikamkuta na hiyo hali... sijui tatizo ni nini, amedondoka tu ndiyo tukamwahisha huku...."

"Kwa hiyo wewe hauishi huku... anakaa na nani?"

"Mama yetu... ila ametoka."

"Okay. Nahitaji kuzungumza nawe. Nifate," Daktari akamwambia.

Kisha akaanza kuelekea upande mwingine wa hospitali hiyo huku Namouih na Manka wakifuata. Mapigo ya moyo wa Namouih yalifanya riadha ya kasi sana kwa sababu ya wasiwasi mwingi aliokuwa nao kuhusu kile ambacho daktari alitaka kumwambia. Wakafika mpaka kwenye ofisi ya kibinafsi ya daktari huyo, nao wakaingia kwa pamoja ndani.

"Huyu ni?" Daktari akauliza.

"Ni Manka, ni mdogo wangu pia," akasema Namouih.

"Na huyu mdogo wako mwingine? Ana miaka mingapi?"

"Ana miaka 11 doctor."

"Okay. Unafanya kazi gani?"

"Ni mwanasheria."

"Sawa. Dada kiukweli, ninachotaka kusema siyo kitu kizuri. Hali ya huyo msichana imenihuzunisha sana," Daktari akasema.

Namouih akajawa na machozi, naye akasema, "Nielezee tafadhali."

"Mdogo wako amekuwa akitendewa vibaya... oh my God... yaani nashindwa hata ku...."

"Doctor ninakuomba useme kila kitu. Niambie, usifinye chochote kile," Namouih akasema kwa uimara.

"Baada ya kumfanyia vipimo tumekuta akiwa na homa kali sana iliyokuwa inasababishwa na yeye kutendewa vibaya kimwili. Sehemu yake ya siri ina michubuko mikubwa na imetanuka sana, kuonyesha kwamba amekuwa akiingiliwa kimwili na mtu mzima kabisa..."

Namouih akawa amefunika mdomo wake kwa kiganja huku akidondosha machozi kwa huzuni.

Manka alishtushwa sana na maneno hayo kiasi kwamba akabaki kumtazama daktari kwa njia ya butwaa.

Daktari akaendelea kusema, "Yaani kwa umri wake hicho ni kitu kibaya sana dada, na inaonekana lilikuwa ni zoea kwa sababu michubuko ile ni ya muda mrefu. Ambaye amemfanyia hivyo siyo mtu yeyote tu, ni mtu anayemjua vizuri na ametumia njia fulani ya kumdanganya au kumtisha mtoto ili asiseme lolote lile. Amemharibu sana mtoto. Yaani sijui nitumie neno gani ili..."

"Amefanya imeoza... amefanya imeoza..." Namouih akasema huku akilia.

Manka akaanza kulia pia.

"Mnafahamu yeyote ambaye anaweza kuwa amefanya haya?" Daktari akauliza kwa upole.

Manka akatikisa kichwa kukanusha. "Hizi wiki chache Nasma hajaongea lolote yaani yeye amekuwa mtu wa kunyong'onyea tu," akasema.

"Oh Allah... Doc... niambie ni nini kinahitajika. Chochote kinachohitajika kwa ajili ya matibabu niambie tutafanya," Namouih akasema huku akijifuta machozi.

Daktari akabaki kumtazama tu kwa njia ya huruma.

"Nini kinahitajika? Hata kama ni nje ya nchi tutampeleka akatibiwe upesi sana. Na ninajua aliyekuwa anamfanyia hayo, nitahakikisha anafikishwa mikononi mwa sheria... ila kwa sasa nahitaji mdogo wangu afanyiwe kila kitu mpaka apone. Niambie tafadhali..." Namouih akaongea kwa uimara.

Daktari akatazama meza yake kwa njia ya huzuni, akiwa kama anatafakari kitu fulani.

Manka akanyanyuka taratibu kutoka alipokuwa amekaa huku akimtazama daktari kwa uelewa wa kile alichokuwa anawaza.

"Doctor... Doctor nini... nini tufanye?" Namouih akauliza kwa sauti ya chini.

Daktari akamwangalia na kusema, "Samahani sana dada. Mdogo wako hatuko naye tena."

Manka akaziba mdomo wake huku akidondosha machozi mengi.

Namouih aliendelea kumwangalia daktari kana kwamba hakusikia wala kuelewa alichokisema. "Mmempeleka wapi?" akauliza kwa sauti ya chini.

Daktari akaangalia tu chini.

Namouih akaendelea kububujikwa na machozi bila kutoa sauti, huku Manka akilia kwa kwikwi akiwa amejifunika mdomo wake.

"Haikuwa rahisi kwake kuendelea kupambana, na alijitahidi sana, lakini alikuwa amechoka mno. Roho imeniuma sana dada, natamani tungeweza kumwokoa au kumpa msaada mapema lakini...."

Daktari akaishia hapo baada ya Namouih kuinamisha kichwa chake mpaka mezani, akiulaza uso wake kwenye mkono wake alioweka hapo, naye akawa analia sana. Hakutoa sauti kubwa, lakini alilia sana.



β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

ITAENDELEA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…


Usikose sehemu za mwendelezo wa hadithi hii kali ya CHANGE. Ni story nzuri na ndefu sana. Waweza ipata nakala yote kwa gharama nafuu sana. Karibu WhatsApp au kwa inbox ya hapa hapa JF.

WhatsApp no: +255 678 017 280
 
Back
Top Bottom