DYLAN
Story by Elton Tonny
Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa
(R-rated 18+)
Enjoy!
★★★★★★★★★★★★
SEHEMU YA ISHIRINI
★★★★★★★★★★★★
Dylan alifumbua macho, akitambua Leila alichofanya, lakini akatulia asikilizie jambo hilo lingeelekea wapi. Leila alishindwa kuendelea kuzuia hisia zake, naye akaibusu kwa mara ya pili shingo ya Dylan. Dylan akalegeza mikono yake kutoka kiunoni kwa binti, naye Leila akawa kama amerudiwa na fahamu na kutambua alichofanya.
Wakaachiana taratibu na kuangaliana usoni. Leila alionyesha dhahiri kwamba alikuwa anamhitaji Dylan, na hapa ndipo Dylan alipoweza kuzielewa hisia za mwanamke huyu bila kuelezewa chochote. Leila alikuwa akisogeza uso wake kuelekea wa Dylan, kama anasita-sita, kila mara akiiangalia midomo ya jamaa na macho yake haraka-haraka. Ijapokuwa hii ilikuws ni mara ya kwanza kwa Dylan aliyepoteza kumbukumbu kuwa karibu namna hii na mwanamke aliyemwonyesha hulka ya kimahaba, hakuwa na wasiwasi hata kidogo. Kwa mpigo mmoja wa mapigo ya moyo, Dylan akaifata midomo ya Leila na kuibusu kwa wororo sana.
Misisimko mingi iliivaa miili ya wawili hawa, na sasa Leila akawa amepata kibali cha kuonyesha upendo wake kwa Dylan. Busu zao laini ziligeuka na kuwa denda zilizojaa huba nzito sana, nao wakashikana miili na kuendelea kudodosana kiaina.
Lakini Dylan akaivunja denda hiyo taratibu, huku Leila akipumua kwa hamu kubwa baada ya kupatiwa penzi kwenye midomo yake. Dylan akamtazama machoni, na ikawa wazi kwake kuwa binti alitaka mambo mengi zaidi, ila sehemu na wakati havikufaa.
"Leila..."
"Bee..."
"Baba na mama watapatwa na wasiwasi tukichelewa sana...nafikiri itakuwa vyema tukiwahi," Dylan akamkumbusha.
Leila akaibana midomo yake na kutikisa kichwa chake kukubali, huku anamwangalia jamaa kwa hamu nyingi sana. Dylan akatabasamu na kujitoa karibu yake, kisha akaanza kumwongoza waelekee nyumbani. Walitembea miili yao ikiwa karibu, na mara kwa mara wangeangaliana na kutabasamu. Dylan akakishika kiganja cha Leila na kuingiza vidole vyake kwenye vidole vya binti, naye Leila akavibana vyema, wakiendelea kutembea wameshikana mkono namna hiyo.
Hawakusemeshana kitu chochote tena mpaka wanaikaribia nyumba. Walipofika usawa wa mti fulani, Dylan akamvuta Leila na kumsimamisha hapo, akiwa ameuweka mgongo wake kwenye mti. Mapigo ya moyo wa Leila yalikimbia sana, huku akiwa anamwangalia Dylan kwa hamu kubwa, akisubiria afanye alichotaka kufanya. Dylan alimwangalia machoni kwa hisia nyingi za uvutio, naye akatabasamu kwa furaha kutokana na hisia hizi mpya zilizomsisimua sana.
Dylan akaisogelea midomo ya Leila taratibu, naye Leila akaifungua yake na kuipokea ya jamaa. Walianza kudendeshana kimahaba sana, huku Leila akivuta-vuta nywele za Dylan. Ijapokuwa kumbukumbu za Dylan zilikuwa mbali, hakuweza kusahau jinsi ya kupinga denda mwanamke hata kidogo! Aliinyonya midomo ya Leila kwa hamu kubwa, kisha akaiachia na kuweka paji lake la uso kwenye paji la binti. Wote wakawa wameyaelekeza macho yao chini, kisha Dylan akasogeza uso wake nyuma kidogo.
"Kwenye upande wako sing'oki."
Akasema Dylan na kumfanya Leila acheke kidogo kwa hisia. Kisha wakaachiana na kuanza kuelekea kwenye nyumba. Walipofika, Leila aliongea na mama yake kuhusu mambo yaliyotokea kwa mama Theodota, naye Dylan akatumia muda wake pamoja na Baraka. Mara kwa mara, wawili hao wangetazamana kwa kuibia-ibia, na Leila angetabasamu kwa njia yenye haya na shauku kiasi. Dylan pia alifurahia alichokuwa ameanzisha na mtoto wa kike, naye alitazamia mambo mengi mazuri kwenye uhusiano wao huu mpya.
Asubuhi iliyofuata, wanafunzi waliwahi shuleni, na sasa wakawa wamebaki wazazi, Leila, na Dylan. Shani alikuwa anasaidizana na Leila kuandaa vitu, naye Baraka alikuwa anaoga. Dylan alipokuwa sebuleni akimsubiri Baraka, Leila aliketi kwenye kochi baada ya Shani kwenda chumbani. Wakawa wanaangaliana kwa njia ya kichokozi. Dylan akapandisha nyusi zake mara mbili kumwelekea Leila kwa utundu, naye Leila akamwonyesha ishara ya busu kwa mdomo wake. Dylan akachekea kwa chini, huku Leila akitabasamu kwa furaha.
"Ethan..."
Dylan akageuka baada ya Shani kumwita. Alikuwa ameshika nguo fulani kubwa mikononi.
"Naam..." Dylan akaitika.
"...nitolee hilo pazia dirishani halafu uniwekee hili hapa," Shani akamwambia.
"Aaa...sawa."
Dylan akaenda upande wa dirisha na kulitoa pazia kutokea juu, akiwa amesimama tu chini kutokana na kuwa mrefu. Kisha akampatia pazia hilo na kuchukua lile alilotakiwa kuweka, naye Shani akaelekea chumbani. Wakati ameanza kuliweka kule juu, alimtazama kidogo Leila, aliyekuwa ameketi kwenye kochi huku ameiinua miguu na kuikunjia juu alipokaa. Alikuwa amevaa dera kama kawaida yake, naye akampa Dylan tabasamu hafifu huku akimwangalia kwa macho fulani hivi...wanajua wanawake tu wanavyofanyaga!
Dylan akatabasamu pia, na hapo hapo Leila akafanya jambo fulani lililoukamata umakini wake. Alishika pindo ya dera lake iliyofunika miguu, kisha akaanza kuipandisha juu huku anamwangalia Dylan kilegevu. Tabasamu la Dylan likafifia na sura yake ikawa makini kuangalia binti alichoelekea kukifanya. Leila alipandisha nguo yake taratibu, mpaka ikafikia sehemu ya paja.
Dylan alizubaa! Ni hapa ndipo Leila akalifunika paja lake haraka ili kumshtua Dylan. Alimpatia kwa kuwa kweli macho ya Dylan yalishtuka na kumwangalia Leila usoni, aliyekuwa anamcheka kwa kuweza kucheza vizuri na akili yake.
"Ethan...mbona bado hujaliweka tu?"
Sauti ya Shani ikamshtua nyuma yake na kufanya mikono yake ikurupuke na kuanza kuliweka pazia hapo juu. Alipompiga Leila jicho la wizi, alimwona jinsi alivyomcheka kichini-chini, naye akatikisa kichwa chake kwa kutambua jinsi gani Leila alimfanya awe kituko.
Baraka aliingia ndani kutoka bafuni na kwenda chumbani, naye Dylan akawa amemaliza kuliweka pazia. Shani akamshukuru, kisha akaenda kubeba vitu vyake pamoja na Leila. Wakati Shani ametangulia kutoka nje, Dylan akamsogelea karibu Leila na kumwambia, "Subiri na wewe zamu yako..." na kumfanya Leila acheke kidogo. Kisha binti akatoka nje ili ajiunge na mama yake kuelekea kwenye kazi zao.
★★★
Ilifika mida ya saa 4 asubuhi Baraka na Dylan wakiwa kwenye ofisi yao, pale mvulana mdogo alipokuja anakimbia na kumwambia Baraka kwamba Leila anagombana na watu fulani kule mgahawani kwao. Alichosema ilikuwa ni kwamba kuna watu fulani walitaka kumpiga Leila, na ugomvi huo ukawa mkubwa kwa sababu watu wengi walikuja kuuangalia. Dylan na Baraka wakatoka hapo upesi na kwenda kule ili kujua ni nini hasa kilichotokea.
Walipofika, walikuta watu wakiwa wamechanganyikana mbele ya mgahawa wa mama Conso, huku Leila akitukanana na mwanamke fulani mwenye umri mkubwa kidogo kumzidi. Waliposogea karibu zaidi, Baraka alimshika Leila na kumuuliza nini kinaendelea, na kwa hasira binti akajibu kwamba hao washenzi wanataka eti kumpiga kwa sababu alisababisha Fabian apigwe jana. Baraka akashangaa kwa sababu jambo hilo lilikuwa geni kwake, lakini Dylan alielewa vizuri jambo hilo.
Huyo mwanamke aliyekuwa akitukanana na Leila, alikuwa ni mama yake mdogo Fabian, naye alikuwa amekuja na kaka yake Fabian, ambaye alikuwa na umri wa miaka 35. Walikuwa wanataka kumpiga Leila kwa sababu hakuwaambia ni nani aliyempiga Fabian jana na kumuumza vibaya. Kwa kuwa kaka yake Fabian alikuwa mwenye mwili mkubwa, alitaka kulipiza kisasi kwa mtu aliyemuumiza mdogo wake.
"Lazaro...nisikilize. Kufanya hivi haifai..huyu ni mtoto. Kwa nini tusi..." Baraka akajaribu kumtuliza huyo kaka.
"Mtoto? Mtoto huyo? Umesikia kila kitu alichokuwa ananiambia?" mama mdogo akapayuka.
"Ndiyo mwanao mshenzi! Akitaka kunibaka, lazima akung'utwe!" Leila akasema kwa hasira.
"Halafu nitakuzibua wewe ******* zako wewe!" Lazaro akamwambia Leila huku amemsonta.
"Leila hebu tulia. Lazaro, kwani hatuwezi kukaa chini tukazungumza kistaarabu?" Baraka akamwomba.
"Kistaarabu? Mpaka aseme kwa nini wamemchangia na bwana wake mwingine kumpiga Fabian! Na atuambie ni nani huyo!" akasema mama mdogo.
"Yaani leo huondoki hapa mpaka useme...la sivyo nitakufumua kama mlivyomfanya mdogo wangu," Lazaro akatoa kitisho.
Watu wengi wa eneo hili walimhofu Lazaro kwa sababu walijua alikuwa mwenye fujo nyingi sana, na mara zote ambazo alizinguana na mtu ilikuwa lazima ampige. Hata mke wake alipewa sana upendo huo wa vipigo mara kwa mara, na ni kama sikuzote yeye na ndugu zake walitafuta sababu za kugombana na watu kwa kuwa walijua kaka mkubwa angewanyooshea mambo kwa mtindo huo.
"Huyu ndiyo Lazaro aliyemfanyia fujo Baraka kipindi kile?"
Dylan akamuuliza mama Conso hivyo kwa sauti ya chini, ambaye alikuwa amesimama pembeni yake huku akimtazama Lazaro kwa makini.
"Ndiyo huyo," akajibu mama Conso kwa uhakikisho.
"Wewe malaya wewe! Ninakupa dakika tano haki ya Mungu usiponiambia ni nani..."
"Ni mimi," Dylan akamkatisha.
Watu wote waliokuwa eneo hilo wakamtazama Dylan (Ethan) kwa makini baada ya yeye kujisema. Dylan, akiwa ameudhika, akasogea mbele kumwelekea Lazaro, huku Baraka na Leila wakihofia sana. Jamaa akasimama katikati akiwatazama mama mdogo na kaka mtu, huku wawili hao wakimwangalia kwa hasira.
"Mimi ndiyo nilimpiga," Dylan akasema kwa ujasiri.
"Kwa nini ulimpiga?" Lazaro akauliza kwa kupandisha besi.
"Alifanya kitu ambacho ikiwa dada yako angefanyiwa, basi usingemwacha salama huyo mpumbavu," Dylan akamibu kwa utulivu.
"Nimekuuliza swali...jibu swali!" Lazaro akasema huku amemnyooshea kidole.
"Kwani nimejibu tako lako au?" Dylan akauliza kwa kejeli.
"Nini? Unasemaje (...)nge wewe?!" Lazaro akauliza huku amekunja sura.
Kufikia hapa, watu wote waliokuwa eneo hilo wamewazunguka, walitulia kimya wakiangalia tukio hili. Wote wenye biashara zao waliziacha ili kushuhudia mambo ambayo yangetokea hapo, huku wengi wakihofia usalama wa Ethan (Dylan) kwa kuwa walifikiri hakumjua Lazaro.
"Umetoa miguu yako kutoka kote huko ili kuja kupiga mwanamke...unajitambua?" Dylan akamuuliza kwa hisia kali.
"(....)mae zako wewe!"
Lazaro akamtukana na kuanza kupiga hatua kumwelekea.
"Subiri..."
Dylan akanyoosha kiganja chake juu ili kumsimamisha. Lazaro akatulia kidogo huku anamwangalia kikatili. Dylan akawageukia watu wote huku amenyoosha kidole chake cha shahada juu.
"...ninaomba mtu YEYOTE yule asije kuingia hapa katikati! Baraka msogeze Leila nyuma..." Dylan akasema kwa sauti ya juu.
"Ethan..." Baraka akaita.
"Ethan!" Leila akaita kwa sauti ya kutaadharisha.
Wakati huu Dylan alikuwa anawaangalia Baraka na Leila, hivyo Lazaro alikuwa anamfata Dylan kwa kasi ili aanze kumshambulia kabla hajageuka. Lakini Dylan alikuwa anatambua jambo hilo vizuri sana, naye alipohisi Lazaro amemkaribia zaidi, aligeuka upesi na kuuwahi mkono wake aliokuwa anauleta moja kwa moja ili ampige Dylan ngumi ya shingo. Aliukwepa na kuushika kwa kasi, kisha kuigeuza nguvu ya Lazaro ilipoelekea kwa kuutega mguu wake mmoja. Hii ilifanya upande mmoja wa Lazaro uangukie mgongoni kwake, kwa hiyo akatumia bega kumnyanyua na kumtupia kwa mbele kama anashusha gunia kubwa la mchele kutokea begani.
Watu walianza kusikika wakiongea ovyo ovyo, naye Lazaro akanyanyuka kwa hasira akiwa anahisi maumivu mgongoni. Akamfata Dylan kwa kasi, lakini Dylan akamkwepa kwa ufundi sana na kuzungukia nyuma yake, kisha akampiga kwa kalio nyuma yake na kumfanya Lazaro aangukie mbele kwa kukosa muhimili (balance). Watu wengi walicheka baada ya Dylan kumfanya Lazaro aonekane kama mtu duni sana.
Faida kubwa aliyokuwa nayo Dylan ni kwamba, alijua mwanaume huyo alitegemea sifa zake za kuogopwa na baadhi ya watu kwa sababu alijiona kuwa hashikiki, na ni kujiamini huko kupita kiasi ndiyo kungekuwa jambo la kumwangusha kwa sababu alitegemea zaidi nguvu badala ya kutumia akili. Dylan hakujua ni kwa nini, lakini kuna kitu moyoni mwake kilimwambia angeweza kumdhibiti huyo mpuuzi.
Baada ya kusikia watu wamemcheka, Lazaro alinyanyuka kwa mara nyingine tena akiwa na hasira kali sana, naye alikuwa amechukua jiwe kubwa na kulirusha kwa nguvu kumwelekea Dylan. Kwa kasi, Dylan aliweza kukwepa, lakini kwa tukio baya jiwe hilo likampiga kifuani msichana mdogo aliyekuwa amesimama hapo karibu. Watu walihuzunika sana kwa kuwa msichana huyo alianguka na kuzimia, na baadhi wakaanza kumhudumia haraka.
Dylan alikasirika sana! Alimgeukia Lazaro akimtazama kwa hasira sana, ambaye hakuonyesha kujali kilichompata msichana yule. Watu wengi walipiga kelele kuwaambia waache ugomvi huo, lakini Lazaro akamfata Dylan tena akijaribu kumpiga. Dylan alikuwa ametulia akimwangalia kwa hasira, na Lazaro alipomfikia akarusha ngumi ambayo Dylan aliizuia kwa kuupiga mkono wake kwa kiwiko.
Papo hapo Dylan alitumia mkono mwingine kumpiga tumbo, kisha mguu mmoja kuupiga uso wake alipoinama, na alipounyanyua akaushika mkono wake na kuuvuta kwa nguvu huku akiugeuzia mgongo wake kwake, na hapo akauvunja kwa kuukunjia kwa nguvu kwenye bega lake kwa kasi ya ajabu!
"Aaaagh!"
Yowe hilo la maumivu lilitoka kinywani mwa Lazaro, aliyehisi maumivu makali sana. Lakini Dylan wa wakati huu hakuwa na huruma hata kidogo baada ya kuona msichana yule ameumia. Hapo hapo alimgeukia Lazaro kwa kumpiga kiwiko shingoni, kisha teke la usoni lenye nguvu sana lililofanya Lazaro aangukie chini huku akisikilizia maumivu ya mkono.
Wahuni walishangilia sana. Sauti nyingi zilisikika zikisema 'mpige huyoo' ili kumhamasisha Dylan aendelee kumshushia mpuuzi huyo kichapo. Akamfata hapo chini na kuanza kumpiga ngumi za usoni, huku watu wakisogea karibu zaidi na kuendelea kushangilia. Ijapokuwa Lazaro alijitahidi kufurukuta, Dylan alimdhibiti kisawasawa, na sasa akawa amelegea zaidi.
Baraka alimfata Dylan na kumwambia aache, na kijana huyu akatulia huku anapumua kwa hasira. Hapo hapo wakaja askari watatu, ambao walikuwa wa kituo kidogo cha eneo hilo, na kufanya watu wasambae kwa kuhofia. Kihalisi, walikuwa wamefika tokea Dylan alipoanza kumsumbua Lazaro, lakini wakabaki kutazama tu kwa umbali fulani. Sasa wakamnyanyua Lazaro, ambaye alikuwa amedebweda haswa, nao wakasema yeye pamoja na Dylan waende kituoni.
Ijapokuwa baadhi ya watu walijaribu kutetea upande wa Dylan, kijana huyo akatii tu na kuongozana nao mpaka kituoni kwenye ofisi ya kituo chao. Mmoja wao alikuwa ameshika bunduki kubwa, hivyo kwa kiasi fulani watu waliogopa. Baraka, mama Conso, na Leila walikuwa wameambatana nao, huku askari wawili wakiwa wamemshikilia Lazaro kwa kuwa aliyumba-yumba sana huku damu zikivujia usoni. Mama mdogo wa Lazaro alikuwepo pia, akilalamika njia nzima, na watu wengi njiani waliwaangalia sana mpaka wanafika kwenye kituo kile.
"Hakuna! Hawa ndiyo wametuanza sisi! Wamempiga mwanangu mpaka wamemvunja kidole...na sasa hivi wamemvunja mkono kaka yake...afungwe tu huyu mbwa!" mama mdogo akaendelea kulalamika.
"Punguza jazba Sofia. Wewe kijana...ni kwa nini unachukua sheria mikononi na kuvunja mtu mkono?" akauliza askari mkuu wa kituo hicho.
"Masoud...kama mama Conso alivyokuelezea, hawa ndiyo walioanzisha fujo. Walitaka kumpiga Leila ndiyo Ethan akaingilia kati..." Baraka akasema kwa ustaarabu.
"Alikuwa hakuulizi wewe, alikuwa anamuuliza huyu..." mama mdogo akadakia.
"We naye vipi? Linakuuma tu kwamba mdebwedo wako amegalagazwa...funga tako lako!" Leila akamwambia.
Lazaro alikuwa pembeni akiendelea kusikilizia maumivu tu, naye Dylan alikuwa ameketi kimya kwenye benchi.
"Nyie hebu tulieni," akasema afande mmoja.
"Tako lako mwenyewe mshenzi wewe! Umekalia kuuza k*** tu malaya uliyekubuhu mpaka majalalani wewe!" mama mdogo akamtukana Leila.
Leila akasimama kwa shari na kumtemea mate usoni. Mama mdogo aliponyanyuka ili agombane naye, askari wawili pamoja na Baraka wakawatenganisha huku wakiwaambia watulie, na wanawake hawa wakaendelea kusimama huku wanaangaliana kwa hasira.
"Masoud...huyu bwege afungwe miaka 30 kwa hiki alichokifanya..." mama mdogo akamwambia mkuu wa askari.
"Nyoo! Miaka 30 ya maisha yako uliyotumia kutafuta wa kukubebesha mimba ila ukashindwa au?" Leila akamwambia kwa dharau.
"Binti nimesema kaa chini!" askari mmoja akamwambia Leila, huku amemnyooshea kirungu.
"Chonde! Usininyooshee jiti lako hilo..." Leila akamwambia kwa ujasiri.
"Leila!" Baraka akamzuia binti yake.
"Unasemaje wewe?" askari akamuuliza kwa ukali.
"Nyie hamna lolote. We na wenzako mlikuwepo muda wote hadi mtoto wa watu anapigwa jiwe lakini mkakaa tu. Mlivyoona Ethan amemkalisha huyu fala ndiyo mkajifanya mnajua kuamua sana ugomvi..." Leila akawaambia ukweli.
"Shenzi wewe ngoja nikuonyeshe!"
Askari huyo akasema hivyo kwa kuudhika na kuanza kumfata Leila. Dylan alinyanyuka na kusimama mbele ya Leila, akimzibia njia askari huyo ili asimfikie Leila. Askari alisimama na kumtazama Dylan usoni akiwa amekunja sura.
"Ah-aaah jamani mambo haya yasiende hivi! Eeh...Masoud..." Baraka akajaribu kutuliza hali.
"Nipishe..." askari akamwamrisha Dylan.
Dylan akasimama hapo hapo huku anamwangalia tu.
"Nimesema toka! Nitakuumiza!" akamfokea.
"Kama vipi twende hapo nje, lakini siwezi kukuacha upige mwanamke," Dylan akamwambia kwa sauti thabiti.
"Ethan...Masoud mbona husemi kitu jamani?" mama Conso akamwambia askari mkuu.
"Ethan...kaa chini," Masoud akamwambia Dylan kwa ustaarabu.
Maaskari hawa walifahamiana vizuri sana na familia ya Baraka na Dylan mwenyewe (waliyemjua kama Ethan), hivyo Masoud alijua Ethan huyu ndiye yule kijana anayejulikana kuwasaidia watu wengi wa hapo kutengeneza upya daraja lao. Alijua pia kuhusu tabia za Lazaro, lakini kuna sababu iliyomfanya yeye pamoja na askari wengine wawe kama...wanamhofu. Kwa hiyo kuona kwamba Dylan aliweza kumnyamazisha jamaa kiaina, kuliwafanya askari hawa waone aibu, na hasa kwa sababu Masoud alikuwa anamheshimu kijana huyu.
Baada ya askari Masoud kumwambia Dylan akae, kijana huyu aliendelea tu kusimama huku anamwangalia afande aliyetaka kumpiga Leila. Masoud akamwambia afande wake awaache, naye akarudi nyuma kidogo na kumsonta Dylan kwa kirungu chake, akijifanya mbabe. Angetoka naye nje kweli ndiyo angeona!
"Masoud, Lazaro anahitaji matibabu, hapaswi kuendelea kukaa hapa. Tuachie tuondoke," mama mdogo akasema.
"Kwa nini awaachie wakati shida mmeanzisha nyie wenyewe?" Leila akasema.
"Aah yaani we msichana wewe! Hivi unashindwa kufunga mdomo wako?" yule afande akamwambia Leila.
"Mbona huyu akiongea humwambii? Tena hadi amenitukana lakini unaniona mimi tu!" Leila akasema kwa ukali.
"Leila...nyamaza!," Baraka akamfokea binti yake.
"Ni kweli. Lazaro atapaswa kwenda hospitali, lakini bado siwezi kuwaacha hawa bila kuwaadhibu," Masoud akasema kwa uthabiti.
"Kwa nini umwadhibu Ethan wakati hana kosa?" Leila akauliza.
"Hana kosa?" mama mdogo akadakia.
"Kosa gani? Ni nini kilichomtoa huyo mtu wako kule kwenu kote mpaka kwenye mgahawa wetu? Si ili ampige Leila? Halafu alipopigwa yeye ndiyo amegeuka malaika," mama Conso akamwambia mama mdogo.
"Kwenda huko na wewe hayakuhusu!" mama mdogo akamwambia mama Conso.
"Wewe ndiyo hayakuhusu. Kiherehere tu kunusanusa boxer za haya majitu unayoyaita matoto. Unaniambia mimi nauza k(...), ulishaniona? Wakati we unaiuza ya kwako hadi kwa afande mtu hapa, unafikiri hatujui?" Leila akamwambia mama mdogo.
"Wewe binti wewe! Unamaanisha nini?" yule afande akadakia.
"Hee..baba tulia...sijakutaja. Mbona unajishtukia?" Leila akamwambia kwa kejeli.
"Lakini Leila mbona husikii?" Baraka akamnyamazisha binti yake.
Afande huyo akaanza tena kumfata Leila, lakini Dylan akamzibia njia kwa mara nyingine. Akalishika shati lake kwenye kola na kufanya kama anamvuta, naye Dylan akaitoa mikono yake kwa nguvu sana. Jambo hilo lilifanya askari wengine waingilie kati na kuwaachanisha.
"...mjinga huyu, niacheni nimwonyeshe!" afande akasema kwa kujitutumua.
"Beba rungu lako, twende hapo nje!" Dylan akamwambia kwa hisia kali pia.
Jambo hilo lilikuwa limegeuka kuwa la kibinafsi baina ya askari huyo Na Dylan. Damu ya Dylan ilikuwa ya moto sana, naye alikuwa tayari kupambania kile alichoona ni sawa, haijalishi aliyembana naye alikuwa "askari."
"Inatosha jamani. Haina haja ya kugombana."
Wote waligeukia upande wa mlangoni baada kusikia sauti hiyo. Walikutana uso kwa uso na mwanamke fulani aliyekuwa mgeni kabisa kwenye macho yao. Alianza kutembea kuelekea sehemu hiyo waliyokuwepo, kisha akasimama usawa wa Dylan na kumwangalia machoni. Walitazamana kwa sekunde kadhaa, kisha mwanamke huyo akampita na kusogea mpaka kwenye meza ya Masoud.
"Habari, naitwa Grace. Nimekuja kumtolea dhamana kijana huyu."
Akamwambia maneno hayo Masoud kwa ufupi sana huku akimwelekezea Dylan mkono. Kwanza kabisa, wote walikuwa wakiangalia mwonekano wake. Alivalia gauni fupi iliyoishia magotini yenye rangi ya maroon, nayo ililichora umbo lake vizuri sana. Alikuwa na kalio kubwa kwa nyuma, na alikuwa mrefu kumfikia Dylan. Macho yake yalikuwa makubwa kiasi, na nywele zake zilikuwa zimechanwa juu na kunyolewa pembeni kidogo kwa mtindo wa kiduku. Alinukia vizuri mno, na kuingia kwake kwenye kituo hicho kuliisambaza harufu ya marashi ya mwili wake.
Baraka, mama Conso, Leila, wote waliangaliana wakiwa hawajui mtu huyu ni nani, naye Dylan alikuwa anamtazama kwa makini pia. Kabla Masoud hajamjibu lolote, mwanamke huyo, Grace, akafungua mkoba wake mdogo aliobeba na kutoa pesa nyingi zilizofungwa kwenye 'rubber band.' Wote walimshangaa, naye akamnyooshea Masoud mkono uliozishika huku anatabasamu.
"Umesema huwezi kumwacha bila adhabu. Chukua...milioni moja hiyo, nafikiri ni adhabu tosha," Grace akasema.
Wote walibaki wakiwa wamepigwa na butwaa. Mwanamke huyo alikuwa nani? Na ni nini kilichopelekea mpaka atoe kiasi kikubwa hivyo cha pesa kwa ajili ya mtu ambaye hakumfahamu?
★★★★★★★★★
ITAENDELEA
★★★★★★★★★
WhatsApp +255 787 604 893