Simulizi : Facebook Imeharibu Maisha Yangu

Simulizi : Facebook Imeharibu Maisha Yangu

SEHEMU YA 41

Siku mbili alizokaa pale hospitali hakuja hata mwanafunzi mmoja kutoka pale chuoni kuja kutoa pole kwa Reshmail wote waliogopa wakiamini alikuwa mshirikina .

Eve hakukubaliana hata kwa mbali na shutuma hizo kwani alimwamini sana Reshmail hivyo aliendelea kuwa pale hospitalini pamoja na mchumba wake kumuuguza Reshmail ambaye alitoka siku tatu baadaye.

?baba mimi nitaenda na Eve kwake nitakaa siku tano ndio nitakuja huko? Reshmail alimpa taarifa hiyo baba yake naye hakupinga kwani amani aliyokuwa nayo Resh akiwa na Eve ilikuwa kubwa mno hali iliyowapa faraja hata wazazi wake hivyo walimruhusu bila kusita.

Siku hiyohiyo walipanda ndege kwa gharama za mchumba wa Eveline aitwaye Benjamin Simon,kuelekea Iringa ambapo Eve alikuwa amepata ajira katika benki ya N.B.C tawi la hapo.

Maisha yao yalikuwa mazuri sana kwani Benny alikuwa mwalimu wa shule ya sekondari hivyo katika majukumu waliweza kusaidiana na upendo wa dhati kati yao ulipendezesha zaidi nyumba yao.Reshmail alivutiwa sana na maisha hayo na kumkumbuka sana Adam wake ?laiti angekuwepo tungeishi hivi siku moja ? alijiwazia Reshmail wakati akiwaangalia Eve na Benny wakiwa kwenye kochi wamebebana kwa furaha huku wakitaniana

Ilikuwa jioni moja Reshmail na Eve wakiwa katika mizunguko ya hapa na pale mizunguko ambayo kwa namna moja au nyingine iliibua ghafla safari ya kuingia sokoni,waliingia hapo kununua matunda matunda,zilikuwa zimepita siku tano na tofauti na alivyowahaidi wazazi wake hata hakuwa amefikiria kurudi Dar maisha ya Iringa yalikuwa yamempendeza sana .

?Eveline ona eveline jamani angalia kale katoto!!!? Reshmail alimgusagusa begani Eveline huku akimwonyesha kikundi fulani cha watoto pale sokoni

?wewe achana hao machokoraa walionikwapua pochi langu sina hamu nao hata kidogo,kisimu changu cha mchina na shilingi elfu thelathini zikapotelea hewani looh!! Wabaya hao? aliongea kwa hasira Eve huku akisitisha zoezi la kula chungwa aliliokuwa anafanya kwa wakati ule.

?mh!! Eve jamani achaga uongo yaani katoto kama kale jamani hebu kaone kale kadogo ?Reshmail alizidi kusisitiza lakini Eve alionyesha bado ana uoga na uchungu moyoni wa kuibiwa vitu vyake na watoto aliowaita machokoraa
 
SEHEMU YA 42

?Reshmail shauri zako vitakuliza hivyo we endelea kusema ni vitoto???..mh!! Resh lakini kale kadogo kazuri kweli? aliongea Eve alipokaona kale katoto ambako Reshmail alisisitiza sana.

?toto zuri jamboo!!?

?sijambo shkamoo!!? kalijibu katoto kale kwa uchangamfu sana baada ya Reshmail na Eve kukasogelea na kukasalimia.

?marahaba mtoto mzuri mbona upo hapa! Mwenyewe au hawa ni kaka zako?? Resh alimuuliza

?a a sio kaka zangu mi namsubiri mama ameondoka na watu wameenda huko amesema anarudi nimsubiri? alijibu tena kwa sauti ya kitotototo

?umekula??? aliuliza Eve.

?looh!! Eve hujaacha tu maswali yako ya kichoyo ya uchagani kwenu mh! Unataka aseme amekula ili umnyime au ?? Reshmail alimshushua Eve kiutani

?mh! Limeniganda shoga,una mashushu wewe!!? alijibu Eve kiaibuaibu huku akimpa yule mtoto chungwa lililokwisha menywa tayari.

?mama anarudi saa ngapi??? Reshmail alimuuliza yule mtoto tena
?sijui nimemsubiri hata hajaja amenipa chai tu akaondoka na wale wanaume wawili? alijieleza vizuri motto yule

?mh!! Mjini mjini tu katoto kanajieleza utadhani mtu mzima dah!? Eve alimnon?goneza Reshmail
 
SEHEMU YA 43


?haya twende ukale eti motto mzuri!? Reshmail alimwambia yule motto naye akakubali kwa ishara ya kichwa,akiwa pekupeku akafuatana na Reshmail hadi kwenye mgahawa ulioandikwa ?MAMA FRED MGAHAWA? uliokuwa pembeni kidogo ya soko kuu la Iringa.

?utamsalimia mama eeh!!? baada ya kumnunulia chakula walilipa na kumuaga

?haya mamdogo!? alijibu yule mtoto

?unaitwa nani vile?Eve akamuuliza

?naitwa Christian motto wa mama Bite? alijibu na wote kwenye mgahawa wakacheka


Kuifananisha na picha ya Adam, dimplez za yule mtoto zilimfananisha kabisa na Adam, achilia mbali rangi yake ya maji ya kunde na ucheshi wake.

"Eve hapana,mbona kesho naenda kumtafuta Christian ili nimjue baba yake anavyofanana,haiwezekani kufanana kwa kiasi hchi hapana "Aliongea Resh huku akiifunika album ile .

Eve alikubaliana naye na siku iliyofuata majira ya saa nne,walikuwa katika hoteli ya yule mama ambapo walimwacha Christian.

"Nyie watoto ni kesi gani hyo mmetaka kuniachia jana" mama mnene kiasi mmiliki wa mgahawa wa Mama Fred aliwapokea kwa maneno hayo makali huku akifunga kanga yake vizuri kiunoni.

Resh na Eve hawakuwa na jibu la kutoa walidhani amewafananisha labda

"Mama ni nini tena,mbona sisi...." alijaribu kujieleza Eve huku akiishiwa maneno ya kujieleza.

"Mmenitekelezea mtoto hapa anaanza kunililia hapa usiku he! jamani mnataka mniuwe kwa presha mkurya wa watu mie" aliongea kwa ghadhabu na mshangao mkubwa sana yule mama.
 
SEHEMU YA 44

"Mama sisi tumempata hapo sokoni,ndio kumleta hapa kwako kwa ajili ya kupata chakula tu mama yangu" Reshmail alinyanyua mdomo wake na kuzungumza kwa sauti iliyojaa mshangao pia.

"He! mauzauza gani haya jamani,mi nimempeleka pale kituo cha polisi usiku uleule ndugu


Baridi kali ya Mbeya ilikuwa imemkataa motto wa Bite (Christian) kwa hali hiyo alipotimiza miaka miwili waliondoka na kurudi tena Iringa ambapo Bite alitaka kukaa kidogo halafu aende Mwanza kuweka makazi mapya huko.

Jambo la kushangaza licha ya baridi ya Iringa hali ya Christian ilianza kuwa njema kama awali jambo lililosababisha Bite aendelee kukaa katika mkoa huo.

Hadi anatimiza miaka mine hali yake kiafya ilikuwa njema sana na tayari Bite alikuwa amesahau suala la kwenda Mwanza. Akaanzisha genge la kuuza uji na karanga mida ya jioni na mihogo ya kukaanga majira ya asubuhi.

Ilikuwa biashara ndogo lakini iliyomuingizia kipato kizuri tofauti na matarajio yake.aliweza kupanga nyumba ya chumba kimoja na sebule aliyoishi na mwanae kwa furaha sana tu bila masumbufu yoyote hadi siku hiyo asubuhi alipokuwa anauza mihogo yake ambapo wanaume wawili ambao sura zao hazikuwa ngeni machoni pake walipofika eneo la biashara yake.Aliwapokea kwa furaha sana na bashasha kama wateja wengine aliozoeana nao.

?Bite tukuone pembeni kidogo samahani lakini? wawili wale walimvuta pembeni Bite

?mh! Mikopo asubuhi asubuhi hamna kwakweli mtadhalilisha hizo suti zenu? aliongea Bite kwa utani huku akiwafata walipo wawili hao

?funga biashara tunaondoka na ukithubutu kupiga kelele au kukimbia nasambaratisha ubongo wako nadhani hujawahi kufikiria kifo cha namna hiyo,hivyo basi fanya kama unavyoagizwa? aliambiwa Bite na wale wanaume huku mmoja akifunua koti lake jeusi la suti na kumwonyesha Bite kitu ambacho hakujiuliza mara mbili mbili kuwa ile ilikuwa ni Bunduki,
 
SEHEMU YA 45

Kwa kuutambua uoga alioupata Bite,yule mwenye bunduki alimbandika kitu mfano wa kishikizo cha nguo na kumwambia ?hiyo ni sound recorder nenda ukawaambie wateja wako sisi ni ndugu zako tumekuletea taarifa za msiba nitakuwa nakusikiliza hapa, ole wako nasema ole wako usifuate maelekezo? alipewa masharti hayo ya uongo Bite ambaye laiti isingekuwa pensi yake ya jinsi ambayo huwa anavaa kwa ndani ili kuhifadhia pesa zake za mauzo basi mkojo uliopenya bila yeye kujua ungemwagika palepale hadharani na wala asingepatwa ma aibu yoyote ile.

Kama alivyoagizwa aliwaeleza wateja wake wawili waliokuwa wanamalizia kuitafuna mihogo waliyokuwa wameinunua,wakampa pole za dhati .

jasho lilikuwa linamtoka alitamani kutumia ishara kuwaambia kwamba yupo katika hatari lakini alipowazia mdomo wa bunduki alikaa kimya kabisa,bila kificho Bite aliiogopa sana bunduki na hakupenda kumwacha Christian katika umri ule.

Tayari akili ilisharudi nyuma akatambua hasa,hao watu alikutana nao wapi,walikuwa ni baadhi ya wafanyakazi katika ile ngome aliyekaa miaka miwili na ni hao waliomleta Adam pale ngomeni

?nimekwisha mimi Beatrice? alijiwazia Bite huku akitetemeka.

Baada ya kuifunga biashara yake aliwafuata akiwa na mwanae amemshikilia mkono.

?nadhani unajua hatuhitaji mtoto!!! Tunakuhitaji wewe tena sasa hivi? aligombezwa Bite na bila kujijua akajikuta akimwacha mwanae pale

?Christian narudi sawa nisubirie pale sokoni sawa mwanangu!

?haya mama alijibu Christian kwa furaha kwani alijua amepata fursa kubwa na ya kipekee kwenda kucheza na watoto wenzake pale mtaani

?ulidhani unaweza kutuzidi ujanja sisi,umepotea sisi hatupimiki hata kidogo umeumia tena umeumia sana aliambiwa Bite na wale wanaume wakiwa kwenye gari kuelekea kwenye gari kuelekea kule katika ngome jambo hilo Bite hakulitamani hata kidogo,japo alimpata Christian kwa bahati mbaya lakini alikuwa akimpenda sana kutoka moyoni na hakuwa tayari kutenganishwa naye kwa namna yoyote ile.

Alijiuliza maswali mengi sana ni nani atakayempa chakula mwanaye siku hiyo na nyingine zitakazoendelea wakati yeye hayupo,michezo ya kukimbizana aliyoipenda Chriss pia ilimtia hofu Bite na kuhisi huenda mwanae anaweza kupoteza uhai wake kwa kugongwa na gari.

Funda la hasira lilimkaba kooni alitamani kufanya lolote lile wakati huo lile jambo liwe ndoto kwake, machozi yaliyotoka ndio yaliyeyusha lile fundo japo kidogo,hasira kali ilikuwa imemkaba Bite aliyekuwa amekaa siti ya nyuma na jamaa mwenye Bunduki katika koti lake lakini maskini hakuwa na la kufanya hadi gari lilipoingia ndani ya ngome ile


* * * * *
 
SEHEMU YA 46


Macho ya Reshmail yalitawaliwa na taswira ya yule mtoto Christian, zilikuwa ni siku nyingi zimepita tangu afungue album yake kumwangalia mpenzi wake (Adam) aliyeaminika kuwa tayari ni marehemu.Ni katika usiku huu alipokuwa akipitia album ya Eveline ndipo tena anakutana na picha ya Adam ambayo yeye (Adam) alimpa Eveline walipoenda Mwanza.

?Eveline,Eveline,Eve???.huyu hapa ni nani????

?we umechanganyikiwa tena eti hebu acha mambo yake ya ajabu huyu Adam? Alijibu Eve kwa uoga.

? na tuliyemwona leo kule sokoni ni nani??? aliuliza Reshmail

?we Reshmail jamani wanafanana Mungu wangu mbona wamefana hivyo lakini eeh!! Eve alijikuta picha ya mtoto Christian ikiumbika kichwani mwake na Zangu kwa sababu nimekaa naye hadi saa nne tumemsubiri huyo mama yake aje wapi!! Nikaona isiwe shari ngoja nimpeleke polisi penye usalama kuepuka balaa kumbe na nyie hamjui ni wa nani he!!? alitoa maelezo hayo yule mama na kueleweka vyema kwa Reshmail na Eveline.

?hicho kituo cha polisi umesema kipo wapi?? aliuliza Eve

?kile pale kinaonekana hata kwa hapa,lile jingo la bluu nyuma yake? alielekeza yule mama
Ndani ya dakika tano tayari Reshmail na shoga yake walikuwa mbele ya mapokezi ya kituo cha polisi Iringa mjini, na walikuwa kwenye foleni wakisubiri zamu yao ya kuhudumiwa ifike.

?nyie ni ndugu zake? Au mmoja wenu ndio mama yake??

?hapana sisi si ndugu zake ila???aliishia njiani katika maongezi yake Resh baada ya kukatishwa na yule askari ?ila nini? Yaani nyie wanawake wa siku hizi suala la kujali watoto wenu hamtaki kabisa kulisikia mnachojali ni urembo tu wa sura zenu?

?jamani sio kwamba kuna ndugu yake hapa kati yetu ila sisi tumemkuta jana kule sokoni ndio tumemnunulia chakula halafu tukajiondokea zetu,leo hii ndio tunapita pale kwa mama Fred yule mwenye mgahawa yeye ndiye ametupatia taarifa hiyo tukaona sio vibaya nasi tukifika kumwona huyo motto? aliongea Eve aliyeonekana kutokuwa na hofu na kituo cha polisi lakini Reshmail alikuwa ana uoga kwa mbali kama vile anatuhumiwa kwa lolote lile.
 
SEHEMU YA 47

?haya yupo tumemuhifadhi na tumepeleka taarifa kwenye vyommbo vya habari wataanza kutangaza kama mama yake bahati mbaya haya atakuja kumchukua na kama amemtelekeza akajiandae kwenda kuishi kwa watoto yatima sisi hatuna uwezo wa kuhifadhi watu hapa zaidi ya mahabusu? alijieleza askari yule huku akijipepea joto kwa kutumia kofia yake iliyochakaa


Majuma mawili yalipita bila mama wala ndugu wa motto kupatikana licha ya kituo cha redio maarufu mjini iringa cha Ebon fm kutangaza kila siku bila kukoma

?Eve naenda kumchukua yule motto nafsi yangu inanishauri hivyo na ni lazima nifate ambacho nafsi yangu inaniamuru? Reshmail alimwambia Eve siku moja wakiwa wamekaa sebuleni wakiangalia habari katika luninga.Eve alikuwa amejenga tabia ya kutobishana na rafki yake huyo kwani furaha yake ilikuwa ni kumwona Reshmail akiwa na furaha tele

?lakini Resh,mama yake si atamtafuta ssana???

?Eve yaani imetangazwa hivyo redioni na hajajitokeza leo hii mie tu kumchukua ndipo ajitokeze? Looh! Acha nae ahangaike kidogo? alijibu Reshmail kwa jeuri

?mh! Haya sikuwezi mwanasheria wangu?

Polisi hapakuwa na usumbufu ni wazi kwamba walikuwa wamechoshwa na matukio ya watoto kutelekezwa na wazazi wao pasipo sababu zilizo wazi,hivyo kitendo cha Resmail kuamua kumchukua Christian ilikuwa ahueni kwao.aliandiokishwa maelezo mafupi tu kabla ya kuruhusiwa kondoka na mtoto ambaye alikuwa dhaifu tayari kutokana na lishe duni na upweke wa kutomuona mama yake kwa siku hizo zote.

Reshmail alikuwa ameyafurahia sana maisha ya Iringa,kampani kubwa kutoka Eveline na mchumba wake ilibeba nusu ya furaha yake huku nusu nyingine ikikamilishwa na uwepo wa Christian mikononi mwake,mara kwa mara alipenda kuwa naye karibu huku akimwita mume wako jambo lililompa faraja kubwa moyoni
 
SEHEMU YA 48


?Eve jamani nitakumiss kipenzi changu lakini nitarudi tena asanteni sana kwa ukarimu wenu mlionionyesha tangu mwanzo nimeishi kwa furaha kubwa sana hapa? Reshmail aliyazungumza hayo alipokuwa anawaaga Eve na Benny usiku ambapo kesho yake alitegemea kurejea Dar-es-salaam akiwa ameandamana na Christian mtoto aliyempata katika mazingira ya kutatanisha
Kwa Christian safari ya kutoka Iringa kwenda Dar ilikuwa safari yake ya kwanza ndefu zaidi kuwahi kusafiri

Siku iloyofuata wawili hawa walikuwa ndani ya basi la ?budget? litokalo Mbeya kwenda Dar likipitia Iringa.

?Mama alisema baba yupo pale kwenye ile nyumba, tushuke nikamsalimie!? Chriss aliongea hayo huku akielekezea kidole chake kwenye jingo lililoonekana kwa mbali mno kutokea pale barabarani na hapakuwa na dalili ya kuishi mtu pale hivyo Reshmail akachukulia kuwa ni akili ya utoto imemtuma Chriss kuzungumza akaamua kupuuzia

?chriss alikwambia nani we muongo!!?

?alinambia mama siku moja hivi tulipita hapa ,halafu mama alinikataza kusema uongo ni dhambi? alijieleza Christian haraka haraka

?mh! Haya tutakiuja siku nyingine sawa mfalme wangu? Reshmail alimjibu Chriss ili kumlidhisha kwa aliyokuwa anasema


** ** ** **

Nyumba tulivu kabisa ya mh.Manyama ililipuka kwa furaha kwa kurejea kwa Reshmail akiwa mwenye furaha tele ?umetuletea na mjukuu!!? alitania mama Resh.

?mtoto wa Eve huyu anamwita mama mdogo? Resh naye akadanganya

?kazuri kweli kama??????? alisita kumalizia baba yake
 
SEHEMU YA 49

?ni kama Adam baba usiogope kufananisha wamefanana kweli? alimtoa baba yake wasiwasi huku akimkumbatia baba yake kasha mama yake.

?mh!! Tulikuwa wapweke kweli jamani dada? msaidizi wa kazi za ndani aliyeitwa Fatuma alimwambia Reshmail huku akimkumbatia na kumbusu shavuni

?na huyo mtoto kama mwanao vile hebu kaone? aliendelea Fatuma

?sio kama wa kwangu ila ni wa kwangu humwoni alivyonifanana?? alijibu kimzaha na wote wakacheka kwa pamoja

** ***** *****

Hali ya sintofahamu iliwakumba wale wafanyakazi wa lile jumba (ngomeni) alipokuwa anatunzwa Adam. Mkuu wa ngome hiyo bwana Lwebe alikuwa na ghadhabu kubwa sana,kila mbua alikuwa na ghadhabu kubwa sana,kila kitu kilikuwa shaghala baghala kila mara aliongea kwenye simu hukuakitoa vitisho vikali sana na hata kutishia kuua.

Wafanyakazi hawakumwelewa lolote walizitambua hasira za bosi wao huyo ambaye mara chache anazokuwa katika hali kama hiyo humalizia hasira zake kwa kutoa roho ya mtu

?mlete Adam hapa mara moja !!? aliamrisha huku akijikuna ndevu zake kwa kutumia mdomo wa bunduki aliyokuwa nayo

?maskini Adam sijui amekosa nini? alijiuliza aliyekuwa anaenda kumwita. Bila wasiwasi wowote Adam akamfikia Lwebe D kwa ishara ya mkono akamwamrisha kumfuata,pamoja na mabaunsa wawili waliotinga suti nyeusi .

lwebe hakuongea neno lolote hadi walipofika kwa nje,tayari kigiza cha saa mbili kilikuwa kimetawala
?mlete na yule mwingine wa nyumba ya chini? alitoa amri nyingine tena baada ya tano walioagizwa wakarejea na mtu mwingine

?we kinyamkera una bahati sana aliyekuleta hapa amesema haujasambaza taarifa zozote mbaya laiti kama ungethubutu ningeiondoa shingo yako sasa hivi.
 
SEHEMU YA 50


Nakuacha uende tena lakini tambua mtandao wangu upo popote katika nchi hii sasa ole wako uthubutu kunyanyua mdomo wako kutangaza ujinga? aliambiwa yule binti aliyeletwa pale huku akionyeshwa njia ya kutokea

?we kidume kwa jeuri ya bosi wako kujaribu kunidhurumu pesa yangu wakati wewe unakula na kulala bure hapa;lazima nimwonyeshe mimi ni nani na ni wewe utakayeumia? aliongea Lwebe huku akipuliza moshi wa sigara hewani.

**********

Ilikuwa ni mwezi mmoja tangu Bite arejeshwe kwenye ile ngome lakini katika chumba kingine,hakuwa msaidizi wa kazi tena bali mtuhumiwa na hakupata fursa ya kuonana na Adam hata siku moja .

siku alipotolewa nje usiku na kwa mahesabu ya miaka mitano ambayo Adam angekaa pale machale yalimcheza,alivyopewa uhuru wa kuondoka hakwenda mbali sana alifika eneo moja kwenye mtaro na kuanza kusubiria ni nini kitatokea japo hakusikia vizuri maneno lakini alisubiri hata vitendo


**********


Mkataba wa miaka mitano alioandikishana Bi.gaudensia na Lwebe wa Adam kuhifadhiwa pale ulikuwa umeisha tayari na miezi mitatu zaidi ilikuwa imepita,suala hilo la kuchelewesha pesa lilimkera sana Lwebe na pia ahadi za uongo kutoka kwa Gaudencia zilichochea sana hasira za Lwebe kufikia hatua ya kuamua kuzipooza kwa huyo Adam aliyehifadhiwa hapo.

Ni usiku huo alipoamua kwa mkono wake mwenyewe Adam duniani kama kisasi kwa Bi.Gaudensia

?paa!! Paa!!? mlio mkali wa risasi ulisikika na kumzindua Bite ambaye alikuwa amepitiwa na usingizi pale kwenye mtalo, kidogo apige kelele lakini viganja vya mkono wake vikawahi kuuziba haraka sana. Hakusikia hata chembe ya kilio na baada ya dakika kama saba akasikia milango imefungwa
 
SEHEMU YA 51



Kwa ujasiri na tahadhari kubwa Bite akajisogeza hadi karibu kabisa na eneo ambalo aliamini hakika ndipo mlio wa risasi umetokea huku kichwani kwake akiwa ana jibu la ?nimesahau saa yangu? iwapo atakutana au kushtukiwa na mlinzi, kwa hofu alizurura katika lile eneo dakika tatu bila kuona chochoten?au wameingia nae ndani??? alijiuliza bila kupata jibu

?koh!! Koh!! Alishtuliwa na sauti ya kikohozi nyuma yake, mawazo yake alidhania ni mlinzi eneo lile lakini alipogeukz hakuwa mlinzi tena ni mwili wa binadamu ukiwa chini,hakutambua mara moja yule ni nani hadi macho yake yalipolizoea giza la pale ?Adam!!!!!?

?we ni nani??? alijibiwa kwa sauti ya chini sana iliyokuwa inaunguruma kama mnyama anayechinjwa

?Bite mimi jamani Adam?

?ondoka watakuua hao Bite ondoka niache mi nife hapa? alijibu Adam

?hapana Adam usife,usife Adam twende tukamtafute mwanetu Chrstian anatamani sana kukuona,usife Adam tafadhali? Bite alibembeleza



**********

Risasi mbili zilizopenya katika paja lake la kulia zilikuwa zimemsababishia Adam kuvuja sana damu na mbele yake alichokitarajia ni kifo hakuna kingine lakini maneno ya Bite.

Nguvu zilirejea upya kabisa tena kwa kasi?Bite ulijifungua, mtoto wangu yuko wapi? Ni wa kiume au wa kike?? alihoji maswali mfululizo Adam huku akijitutumua kusimama kwa nguvu alizokuwa amezipata


?ni stori ndefu na hapa sio mahali pake tuondoke tafadhali jitahidi kuna hatari kubwa kama unampenda mwanao jitahidi tuondoke? aliongea Bite huku akiuweka mkono wa Adam katika bega lake na kuanza kumkongoja kutoka eneo lile huku (Adam) akitumia mguu mmoja na ule uliojeruhiwa ukiwa juu juu.

Kutoka pale walipokuwa hadi barabarani haukuwa umbali mrefu sana na walifanikiwa kufika,kwa giza nene lililokuwepo hawakuweza kuonekana na mtu yeyote,nguvu zilikuwa zinamwishia Adam kutokana na kuvuja damu lakini alijikaza kijasiri sana na kuendelea mbele
 
SEHEMU YA 52

********* ******* *******


Lwebe na kundi lake baada ya kumpiga risasi mbili Adam waliamini katu asingeweza kunyanyuka kutoka katika eneo lile,na hata angeweza kuinuka hakuwa na pa kwenda hakuujua mkoa huo hata kidogo. Waliingia ndani na kupiga simu kwa Bi.Gaudensia kwamba mtu wake tayari ana risasi mbili mwilini

?msimuue jamani,tafadhali sana kesho naileta pesa yenu mapema kabisa?

?nimechoshwa na ahadi zako mheshimiwa jiandae kuchukua maiti yako siku yoyote utakayotaka utaikuta nimeihifadhi na kama na kuizika nitakusaidia? alijibu kwa ghadhabu kasha akakata simu
Bi Gaudencia akapiga tena

?nakusikiliza?

?basi nielewe kwa leo na hili ni ombi la mwisho tafadhali usimuue kesho asubuhi sana nakuja huko,ninaondoka huku saa nane usiku tafadhali? alibembeleza

?na iwe hivyo atalala nje leo na hata kula hadi utakapokuja

?sawa mkurugenzi? alijibu kwa unyenyekevu Gaudensia

Akini ya Bi.Gaudensia ilifanya kazi haraka haraka akapekua kila kona katika chumba anacholala na mumewe na kwa bahati nzuri kwa akakutana na kadi ya benki ya mume wake ambayo alikuwa akifahamu vizuri kabisa namba zake za siri.

Bila kupoteza muda akampigia dereva wake wa siri ambaye huwa anampeleka Iringa naye haraka haraka bila kuhoji akatii amri aliyopewa.bila Reshmail kujua Bi.Gaudensia akaondoka majira saa saba usiku,nafsi ilikuwa ikimuhukumu juu ya baya lolote litakalomkuta Adam

?damu ya Adam ipo juu yangu?
 
SEHEMU YA 53

?naenda kwa rafiki yangu ameugua ghafla ? mama Reshmail alimuaga mlinzi wa getini

?sawa bosi? alijibu mzee yule wa makamo huku akifunga geti baada ya mama kuwa ametoka nje
Kwa kasi ya ajabu gari iliondoka jijini Dar-es-salaam kwa kuwa ilikuwa usiku sana vizingiti vya watu wa usalama pamoja na foleni havikuwepo sana hivyo dereva alikimbiza gari kwa kadri ya uwezo wake.

Breki ya kwanza ilikuwa ni katika benki ya C.R.D.B maeneo ya Ubungo ambapo mama Reshmail alishuka na kuvuta pesa kutoka katika akaunti ya akiba ya mzee Manyama
Badala ya masaa matano kwa gari binafsi kufika Iringa walitumia masaa matatu pekee

?mh!! Huku napo kijijini kweli huyo nae sijui ni mgonjwa sasa usiku huu atapata wapi lifti ya gari?

Mama Reshmail alimwambia dereva wake alipoona watu wawili wakisimamisha gari

?ah!! Ndo maisha ya Tanzania yalivyo? alijibu dereva huku akiongeza zaidi mwendo wa gari hadi wakaifikia ngome ya vigogo waliyokuwa wakiifuata

**** **** *****

Magari makubwa ya mizigo yatokayo Morogoro kwenda Zambia na Malawi ndiyo yaliyotoa msaada kwa Bite na Adam ambapo Bite alijitambulisha kama mke wa Adam na kwamba wamevamiwa na majambazi na mumewe (Adam) amepigwa risasi.

Laiti kama madereva wangekuwa watanzania kwa jinsi walivyo waoga katu wasingewapandisha wawili hawa lakini wakongomani wale ambao vita kwao ni jambo la kawaida waliwachukua Adam na Bite hadi Iringa mjini walipowaacha jirani kabisa na hospitali ya rufaa.

?bila RB hatupokei mgonjwa wa aina hii? alisema muuguzi wa kike wa hospitali ile wakati Bite anajieleza.

Ni kweli yule muuguzi(nesi) alikuwa na haki zote za kupingana na ujio ule kwani hali aliyokuwa nayo Adam ilihitaji taarifa za polisi kwanza

?haa!!! Mama Christian, ni wewe hata siamini au nakufananisha??
 
SEHEMU YA 54

wakati Bite akijiegemeza kwenye ukuta huku akiwa amekata tama alishangaa kutambulika kwake na nesi yule

?Mungu wangu mama wawili jamani!!!?

Baada ya kumkazia macho naye Bite akamtambua yule nesi kuwa waliwahi kufanya nae biashara katika soko la Uyole Mbeya na pia alikuwa jirani yake pale alipokuwa anaishi,ulikuwa mshangao mkubwa sana

?ehe!! Kulikoni tena ndugu yangu yamekukuta yapi tena mwenzangu?? alihoji nesi huku akiwa amechangamka sana safari hii

?ni makubwa sana,lakini ningeupata msaada wako kwanza kwa mume wangu ndio tungeongea vizuri shoga? alijibu Bite akiwa na matumaini tele

?ondoa shaka shoga huduma mnaipata sasa hivi tena huduma bora,daktari tunaheshimiana naye sana na pia ni shemeji yangu? nesi aliongea hayo huku wakisaidiana kumwingiza Adam ndani ya chumba cha wagonjwa,hapakuwa na maswali mengi,undugu ulitawala pale.

Adam akafanyiwa upasuaji mdogo wa kuondoa risasi katika ambao haukuchukua hata hata nusu saa damu na maji pia vikaongezwa katika mwili wake uliokuwa dhaifu sana.kufikia majira ya saa kumi na moja alfajiri Adam alikuwa amepata nafuu kubwa na aliweza kutembea japo kwa kuchechemea

?shoga nikueleze wazi tu kwamba sisi pa kufikia hapa Iringa mimi na mume wangu hatuna! Tangu niondoke ghafla niliacha sijalipa kodi nina uhakika chumba sio changu tena kwa hiyo pa kwenda hatujui? Bite alimweleza hayo mama wawili baada ya kuwa amemsogeza pembeni ili mtu mwingine asiweze kusikia

?Ondoa shaka Bite mimi kwangu pana nyumba kubwa tu!! Nimejengewa na mnyakyusa mmoja,nimemweka kwenye kiganja kwangu mimi hasikii,haoni wala hasemi,ni kaka yake na huyu daktari we mwenyewe si umeona alivyowashughulikia haraka? kwa sauti ya chini kabisa nesi alijibu

Wote watatu katika teksi wakaongozana hadi nyumbani kwa nesi ni kweli nesi hakuwa na chembe ya utani hata kidogo nyumba ile ilikuwa kubwa sana na haikuwa haki kukaliwa na watu wawili pekee vilikuwa ni vyumba sita pamoja na sebule
 
SEHEMU YA 55

?karibuni! Karibuni sana! Nesi aliwakaribisha walipofika nyumbani kwake.

?asante sana ndugu yangu ama kweli ishi na watu uvae viatu? alisema Bite kwa upole sana

?usijali Bite tumeishi vizuri,hatukuwahi kugombana hata siku moja,tumetwishana matenga ya nyanya kwa nini sasa nishindwe kukutendea wema!!!? nesi alimtoa hofu Bite

Chumba walichopewa kilikuwa kikubwa cha kuwatosha kabisa,kitanda cha tano kwa sita kilikuwa saizi yao kabisa.

Adam alishangazwa sana na wema huo wa nesi lakini mshango wake uliongezeka maradufu baada ya kukutana na mume wa nesi siku ambayo walikuwa wakitambulishwa kwake kama shemeji zake yaani ndugu zake Bite.mzee huyu wa kinyakyusa aliyeitwa Gwakisa ni kama heshima ilipitiliza na kuwa kama anawanyenyekea wawili hawa.

Adam alihudumiwa na yule daktari kana kwamba alikuwa ni mgonjwa wa kisukari au alikuwa ni mtoto wa mfalme,Adam alipata farijiko kubwa sana kuishi pale

Bite kama kawaida alikuwa mwanamke wa kujituma sana,ndani ya wiki moja tayari alikuwa amepata kazi ya ndani katika nyumba nzuri waliyoishi wanafamilia watatu, mwanaume na mke pamoja na mtoto wa kama miaka mitatu wa kike aliyekuwa anasoma shule ya awali


***** ****** ****** ******

?bite mama!!?

?bee mama?

?mpeleke mtoto shule halafu baadaye mpeleke pale zahanati akapimwe jana usiku amekohoa sana?

ilikuwa sauti ya Eveline akimpa maelekezo Bite ambaye alikuwa mfanyakazi wake mpya na wa kwanza wa ndani ya nyumba yake na mchumba wake.
 
SEHEMU YA 56

Ratiba ya Bite ilikuwa ni kazi kuanzia asubuhi ya saa mbili ambapo alikuwa akimpeleka Loyce {mtoto wa kaka yake Benny} shuleni na kisha akirejea anaandaa chakula cha mchana kwa siku ambayo Benny hurudi nyumbani mchana na baada ya hapo humfuata Loyce shuleni,kisha maandalizi ya chakula cha jioni na majira ya saa kumi na mbili huaga na kuondoka,ilikuwa kazi ambayo haikumtoa jasho Bite na malipo ya shilingi laki moja kila mwezi yalimtosheleza kabisa kupanga chumba kidogo walicholipia shilingi 15000 kwa mwezi

?tunashukuru sana kwa ukarimu wenu bwana na bibi Gwakisa Mungu awazidishie baraka katika kazi zenu? alitoa shukrani za dhati Adam kwa niaba ya mke wake wa bandia (Bite).

uchangamfu wake na wingi wa vituko ulifanya nyumba ya Gwakisa iwe iwe yenye shangwe na tabasamu kila siku,kitendo chake cha kuaga pale kilimsononesha Gwakisa na mkewe lakini hawakuwa na jinsi, kutoka mfukoni mwake aliwakabidhi shilingi laki mbili za kuanzia maisha yao huko waendako
Tayari Adam alianza kumpenda kwa dhati Bite uchapakazi wake na jinsi alivyomwokoa kutoka katika kifo ulichangia sana lakini kiunganishi cha mtoto Christian ndio ilikuwa chachu kubwa ya mapenzi yao.

walivyohama katika nyumba yao ya kupanga walianza rasmi kuishi maisha ya mke na mume Adam hakuwa na amani hata kidogo na familia ya Reshmail hasa baada ya kukuta katika nyumba hiyo ndogo waliyohamia magazeti yaliyobandikwa kama mapambo likisema;

?imani za kishirikina zamwondoa mheshimiwa Manyama bungeni? alitamani sana kuisoma habari hiyo kiundani iliyotoka takribani miaka mitano iliyopita lakini ilikuwa imeandikwa inaendelea ukurasa wa pili anbao haukuwepo pale ukutani

?Au walikuwa wanataka kunitoa kafara? Mungu wangu!! Niliwakosea nini mimi? alijiuliza Adam wakati wakiingiza yao ya Rambo ndani ya chumba hicho kimoja kilichotenganishwa na pazia kufanya sebule na chumba

Hisi hizo mbaya zikamfanya Adam aamue kuanzisha rasmi uhusiano na mwanamke ambaye amezaa naye mtoto pia aliyeokoa maisha yake bila kutarajia mwanamke ambaye hajawahi kumkwaza,mwanamke mpiganaji anayempa furaha tele kila siku

?Bite nataka uwe mke wangu?

?Mh!! Niwe mkeo mara ngapi mimi mkeo tayari jamani? alijibu Bite huku akichezea ndevu za Adam ikiwa ni siku ya pili tu tangia wahamie katika makazi hayo mapya

?una utani wewe mbona ulikuwa hujaniambia wala sijawahi kusikia ukiniita mume wako?

?sio lazima nikwambie tayari nina mtoto wako halafu humu ndani kuna kitanda kimoja tena kidogo tu,ulidhani chako mwenyewe!!!? aliuliza Bite kisha wote wakacheka huku wakikumbatiana na kuangukia kitandani

**** *******?
 
SEHEMU YA 57



Maisha ya Reshmail jijini Dar-es-salaam yalikuwa yamebadilika sana akiwa anasubiri wakati baba yake akimtafutia kazi itakayompendeza alifurahia mara zote na Christian huku akiwa amewabadili watu wote wanaomfahamu kwa ukaribu kutokea kumwita Reshmail na sasa walimwita mama Christian na alikuwa amejivika pete ya ndoa katika kidole chake cha shahada ikwa na jina Adam na nyingine ndogo akiwa amemvisha Christian ikiwa imeandikwa Reshmail.

Hakuwa mtu wa kulialia tena wala msongo wa mawazo haukumsumbua tena aliamini nafasi ya Adam ilikuwa imezibwa vyema na Christian ambaye alikuwa Adam mpya kwake. Walilala wote, walicheza wote na kusimuliana mambo mbalimbali.alipoenda kusalimia rafiki zake walienda wote Christian mkono wa kulia.

Harakaharaka Christian alijikuta akimpenda mno Reshmail kuliko hata ilivyokuwa kwa mama yake mzazi,maisha ya kifahari ya kwao Reshmail yalimfanya Christian anawiri sana ungewakuta wakicheza bustanini kama vile wanalingana umri walibembea pamoja na kupigana kiuongouongo,kwa ufupi waliishi maisha ya kusisimua kwa kila aliyewaona.

Akiugua Reshmail ni Christian atamuuguza kwa kukaa pembeni yake bila kutoka nje hadi apone hivyo hivyo kwa Reshmail abaye alimwogesha na kumlisha.

Wakati huo Reshmail ndio alikuwa mwalimu wa Christian akimfundisha kusoma na kuandika jambo ambalo hata baba yake alilipenda na Christian alikuwa mtu anayeelewa haraka akifundishwa ,reshmail alifurahia sana.

Baada ya kukaa na Christian mwezi sita reshmail kwa mara nyingine Iringa kwa rafiki yake jambo kubwa lililompeleka huko ni harusi ya rafiki yahe huyo ambapo alitarajiwa kuwa matron wa kipenzi chake hicho.

?shoga shughuli kesho kutwa hata haujaonekana jamani au ndio mambo yetu yale haja ya kufanyiwa make up?.? Aliuliza kiutani.

Eve katika simu alipokuwa anaongea na Reshmail.

?Kesho asubuhi na mapema nakujua ,mume wangu alikuwa na mafua ndio tatizo si unajua tena.?alijibu Reshmail.

Haya mume huyo anavyoringiwa shauriro ?alijibu Eve .Christian alikuwa amependekezwa kuwa bwana harusi mdogo pamoja na Loyce (mtoto wa kaka yake Benny).

?He unatoka mume wangu asiuze sura,na jinsi alivyoandaliwa huku Dar es salaam ,utachoka mwenyewe na simtoi mpaka siku ya shughuli,atakayeruhusiwa kumuona ni bibi harusi mdogo(Loyce) peke yake wakati wa kujifunza,sitaki mwingine amuone mpaka siku yenyewe?alijibu Reshmail kwa furaha.
 
SEHEMU YA 58

?Haya umeshindwa ambao hatuna waume tunalo,alijibu Eve kisha wakaagana.

Asubuhi ya siku iliyofuata majira ya saa nne asubuhi tayari Reshmail,Christian,mpambaji pamoja na dereva walikuwa ndani ya gari la baba yake (Resh)taratibu safari ya Iringa ikaanza.

?Usitupeleke kwa kasi sawa eeh,alitoa malekezo Reshmail na kukubaliwa na dereva kwa sababu hawakuwa na haraka yeyote ila mbele yao yalikuwa bado masaa mengi sana kabla ya harusi kufanyika.

Kwa mwendo wa kinyonga kabisa gar lilifika mbele ya nyumba ya Eve majira ya saa nne usiku na hakuna aliyekuwa ameschoka sana.Shamrashamra zilikuwa kubwa sana maeneo ya pale kwa Eve kelele zilizidi alipofika Reshmail, na kama alivyoaahidi kweli alishuka yeye peke yake kutoka katika gari akifuatiwa na dereva,urembo wake utadhani alikuwa amepembwa tayari kuingia ukumbini.

?Shoga tabia gain hiyo kupendeza kuliko bibi harusi??aliuliza eve kiutani baada ya Reshmail kuingia katika chumba ambacho Eve alikuwa amehifadhiwa akiwa na wapambaji wake.

?Hebu acha utani wako,kila mara unadhani tuko shuleni?mwone,?alijibu Reshmail,Eve akajiziba mdomo kwa aibu huku akiwatazama wapambaji wake waliokuwa wamejizuia kucheka lakini uvumulivu ukawashinda wakacheka kwa nguvu.

Chumba kile kikageuka kijiwa cha story kati ya Reshmail na Eve ,stori zingine zilikuwa juu ya mume wa Reshmail (Christian),shoga hadi pete?

?Sina utani mie mbona??alijibu Resh huku wapambaji wakiwa hawajui hata kinachoongelewa.

?Mama kuna mtu anataka kukuona,ilikuwa ni sauti ya kike ikimueleza Eve.
?Heh!!ushazaa na wewe??aliuliza kiutani Reshmail.Mh!!niringe huyu ni msaidizi wangu tu wa kazi anaitwa Bite,nampenda naye ananipenda pia.

?Sio kama mimi na Christian ?alidakia Reshmail ambaye tangu aingie chumba kilitawaliwa na vicheko.

?Bite humuwezi huyu anaitwa mam Christian ni rafiki yangu tangu utotoni.

?Nafurahi kukufahamu mama Christian hata mimi.

Alitaka kuondelea kuongea Bite akakatishwa na Eve.

?Anayetaka kuniona nani huyo tena?,mwambie nina mgeni" Bite akajiondokea bila kumalizia kauli yake.

Sherehe ilifana kuanzi kanisani lakini mambo yote yalikuwa saa mbili usiku maharusi wadogo walipokuwa wametangulia mbele wakifuatiwa na wana ndoa wenyewe(Eveline na Benjamin)huku nyuma yao Reshmail na Fredrick wakifunika kila kitu kwa pale mbele Christian aliteka macho ya watu huku kamera zimemulika yeye.
 
SEHEMU YA 59


Tabasamu lake pana la wakati wote lililoonyesha vishimo katika mashavu yake yote lilisababisha watu wengine wahisi huenda sio kutoka Tanzania , suti yake iliyoendana kabisa na mwili wake na viatu vyake pia jinsi mkono wake ulivyokuwa umemshika kiustadi Loyce (bi harusi mdogo) ulimfanya MC ashindwe kukaa kimya ?nani mwenyewe harusi,wa mbele,nyuma au kati? aliuliza kwa mbwembwe

?mbeleeeeeeeee!!!.......nyumaaaaa!!!!? ndio majibu yaliyosikika kutoka kwa wengi

?hayaa wageni waalikwa wanasema maharusi wa katikati wamefunika sana? alidanganya MC aliyefahamu wazi Christian na Reshmail wameteka macho ya watu wengi pengine kuliko maharusi wenyewe.

Picha zilipigwa kwa wingi lakini Christian hakuonyesha wasiwasi wowote ?mh!! Katoto kazuri halafu kajanja hako? wanawake walikuwa wakinon?gonezana huku wakimtazama Christian anavyozidi kusonga mbele

?wamekatoa nje,baba yake ni mreno? alidakia mama aliyesifika kwa umbea pale mtaani aliyejulikana zaidi kwa jina la mama mwingi.hata hawakuhangaika kujibishana nae kwani walishamzoea

Taratibu kabisa kwa mwendo wa kunyata jozi hizi tatu za kuvutia ziligawanyika huku jozi mbili za wakubwa zikienda katika meza kubwa kabisa na watoto wakienda katika meza yao ndogo iliyokuwa akimeremeta soda na vinywaji vingine baridi,

?kusema ukweli sherehe imependeza,siongei kama MC bali kama ndugu Kidagaa Peter Kubalunga wengi wananiita MC K.P? alichombeza Msema Chochote (MC) na kushangiliwa sana na umati mkubwa uliohudhuria sherehe hiyo


********** ************ ********

?Dah!! Umependeza kweli sitaibiwa huko na wajanja,hebu ona ona mgongo wako utadhani huna mamba ulivyopendeza,ona kifua chako mpenzi wangu hapana nitaibiwa mke mie? Adam alikuwa akimtania Bite huku akim funga zipu yake ya mgongoni

?Acha wivu mwanaume wewe,kaa ndani usubirie ya kwako aniibe nani wataishia kutamani tu!!? alijibu Bite huku akimun?gunya midomo yake ili lipstick aliyopakaa ikae vizuri zaidi na kioo kikiwa mbele yake

 
SEHEMU YA 60

?Nakupenda sana mke wangu,tambua hilo niliamua toka moyoni mwangu na wala sijutii hata kidogo najionamwenye bahati sana? Adam kwa sauti ya chini iliyomaanisha anachokisema alimwambia Bite ambaye alitulia tuli akamtazama Adam kisha akamkumbatia na kumbusu.

?nakupenda pia nakupenda sana? Bite akamwambia Adam halafu akatoka nje na kupanda teksi iliyokuwa inamsubiri kwa nje na kuondoka,Adam hakuthubutu kutoa hata pua yake nje kwani bado alikuwa na uoga wa kurejea mikononi mwa watu wabaya

Majira ya saa tatu na nusu Bite tayari alikuwa mlangoni akionyesha kadi yake ya mwaliko kwa watu wa ulinzi kisha mwanadada kutoka kamati ya maandalizi akamwongoza Bite kuelekea katika upande ambao ndugu zake na mwanamke walikuwa wamekaa,eneo la chini ya meza ya bwana na bibi harusi mdogo.Bite alikuwa tayari kama ndugu wa damu kwa Eveline walitokea kuheshimiana sana na hawakuwahi kuingia katika malumbano makubwa sana.

Amani ilitoweka katika meza ya bwana na bibi harusi wadogo,Christian alikuwa amekosa utulivu mara kwa mara alikuwa ananyanyua shingo yake aweze kuona kitu Fulani ambacho hakuna aliyefahamu ni nini kimemsibu

?Au kanaumwa tumbo?? alijiuliza matron huku akienda kwenye ile meza kumsikiliza Chriss ana shida gani.

?Chriss ni nini baba umekuwaje?? alimuuliza baada ya kumfikia

?nataka kwenda kwa mama? alijibu kwa sauti iliyojaa manun?guniko sana

?subiri kidogo mtoto mzuri nitakupeleka sawa? matron alimdanganya Chriss huku akiamini shida yake ilikuwa kwenda kwa Reshmail,kidogo Chriss alitulia japo bado hakuwa na katika hali ya uchangamfu kama awali

Muda wa kutoa zawadi ulipofika maharusi wote katika jozi tatu walitakiwa kuwa mbele ya umati kwa ajili ya kupokea zawadi zao.Christian na Loyce waliwekewa viti wakakaa wakati Eve,Benny,Reshmail na Fredrick walisimama wima kupokea heshima hizo

?heee! We mtoto vipi? Jamani huyu mtoto kulikoni? yule mwanamke aliuliza baada ya kushikwa gauni lake na Christian alipotaka kuondoka baaba ya kutoa zawadi.

Bahati mbaya muziki ulikuwa umezimwa hivyo ukumbi mzima ulishuhudia tukio hili la kushangaza

?mamaaaa!! Mamaaaa!!? Chriss alimpigia kelele alipotaka kuondoka
 
Back
Top Bottom