Simulizi : Facebook Imeharibu Maisha Yangu

SEHEMU YA 61

?Chriss??.Christian??Christian wanguuuu!!! Jamani ni mwanangu..ni mwanangu huyu? alipiga kelele mwanamke huyu, alikuwa ni Bite na tayari akili yake imemgundu Christian,watu wote waliamini amechanganyikiwa lakini alikuwa anasisitiza bado kwa maneno hayohayo.

Hakika mbele yake alikuwepo mwanaye waliyepotezana zaidi ya nusu mwaka sasa na dalili za kumpata zilikuwa zimeanza kufifia.

Mayowe yake yalivyozidi yakapoteza usikivu pale ukumbini na kila mtu kuanza kujiuliza kulikoni eneo lile

?mama mama mama,huyu ni mwanangu?..Christian jamani? Bite kwa sauti ya juu sana akaanza kumwambia Eveline ambaye alikuwa amekodoa macho kuangalia anachofanya Bite pale mbele

?kuna nini jamani? Reshmail alishindwa kujiuliza akamvagaa Eve na kumuuliza

?huyu ni Christian,mtoto wangu jamani mtoto wangu kabisa? alisisitiza Bite.

Nguvu zilimwisha Reshmail japokuwa hakuzimia lakini alianguka chini,alishuhudia kila kitu lakini hakuweza kuzungumza,ulikuwa mshtuko wa hali ya juu sana haikuwa sherehe tena bali kasheshe,huku Bite na mayowe yake huku Reshmail akiwa chini.

Wapiga picha hawakuwa mbali walilichukua hili tukio kikamilifu tayari kwa kuuza katika vyombo vya habari.

Mwanamama mwenye nguo nyeusi alikuwa anapambana kupenya katika msitu mkubwa wa watu pale ukumbini,mwanzoni hakuwemo kwenye sherehe

?vimama vya Kiswahili navyo,hapo umbea tu ndo amefata humu,akipigwa hapo au akikanyagwa atamlalamikia nani?
 
SEHEMU YA 63

?Adaam??Adaaaam!!!? alipiga kelele kali zaidi wakati huuu Reshmail. Adam alikuwa amejivua baibui kwa upande wa usoni, akiwa hajapewa jibu lolote reshmail palepale alifika Bite,

?Adam! Umefikaje hapa mume wangu?si ulisema hauji?? Bite aliuliza

?nini? Nani? Umemwitaje? Na huyu ni??.? Hakuweza kumalizi kauli yake wakati huu,mawazo yakauzidi nguvu ubongo wake akazimia palepale.

Wakati huo Chriss alikuwa analia tu hajui kinachoendelea, Eve na Benny walikuwa wanahaha huku na huko bila kukumbuka kwamba alikuwa na shera safi kabisa tena ya gharama za juu kabisa, Benny ndio alikuwa kama tahira hajui hata pa kuanzia alikuwa ameshtuka sana.

Ilikuwa kama vita vile lakini hakuna hata aliyejeruhiwa wala aliyekuwa anapigana vilikuwa si vita vya risasi bali vita vya mapenzi.

Wageni waalikwa waligeuza tukio hilo kuwa kama filamu ya kusisimua lakini waliyokuwa wameianzia katikati bila kujua ilianzia wapi na inaenda wapi.,nani nyota wa filamu na nani adui.

***

Ni katika nyumba ya Eveline. Reshmail akiwa mbele ya Beti amepiga magoti akilia kwa uchungu
 
SEHEMU YA 64

?Bite wewe ni mwanamke mwenzangu nionee huruma kwa haya niliyopitia,nimeteseka sana, nimedhalilishwa kwa ajili ya Adam, ni kwa ajili yake hadi leo mimi ni bikra, kwa ajili yake familia yake imetuchukia,kwa ajili ya Adam baba yangu haeshimiki tena mtaani kwetu,Bite sitamani mwanaume yeyote yule,ukininyan?ganya Adam na Christian mimi nitakufa Bite, ni furaha gani utaipata kwa kifo changu kwa ajili ya upendo?, sitajali huyu mtoto uliyezaa nae wala sitaumizwa na ujauzito wake uliombebea, ninakuomba Bite niache na mimi nipate furaha japo kidogo tu katika siku zangu zilizobaki hapa ulimwenguni, nisaidie niweze kurudisha upendo uliogeuka chuki kati ya familia yangu na Adam. Bite uamuzi upo mikononi mwako,ukikataa utaniumiza sana na nina uhakika nitakufa na pendo langu kwa Adam?

Kilio kilimzuia kuendelea kuongea,lakini na yeye mgongoni mwake alilowanishwa kwa machozi ya Bite yaliyokuwa yanatililika muda wote wakati Reshmail anaongea,kwa hali halisi alimwonea huruma lakini pia kwa dhati kabisa aliwapenda Adam na Christian. Eve na mumewe Benny walikuwa watazamaji,wenyewe hawakuwa na uwezo wa kutoa maamuzi yoyote yale.

Christian alikuwa ametulia kwenye kochi, hali ya utulivu aliyokuwa nayo ilipita siku zote.

?Adam tulipokutana unapajua,yote tuliyofanya unayajua,upendo wangu kwako nadhani unautambua pia??labda sikupangwa kuwa wako milele ndio maana aliyepangwa amejitokeza wakati muafaka,asante kwa zawadi ya penzi lako,asante kwa mtoto na huu ujauzito hii ni heshima kubwa kwako milele,neno gumu ninaloweza kulisema sasa ni kuwa kwa moyo mmoja nakuruhusu uendelee na Reshmail,nayasema haya mbele ya mama yangu Eveline?

Alizungumza Bite kisha akashindwa kujizuia kuangua kilio kikuu kilichoamsha hisia za kila mtu pale ndani wote wakadondosha machozi yao. Adam,Reshmail na Bite wote kwa pamoja wakakumbatiana huku machozi yao yakitua juu ya Christian aliyekuwa katikati yao,ilikuwa ni picha ya kusisimua na kuumiza sana.

****** *****
 
SEHEMU YA 65 .......... MWISHO

Kilikuwa kikao kikubwa cha familia yao Reshmail,watu wote muhimu walikuwemo kasoro mama wa familia hiyo aliyesusia kikao,mzee Manyama,Reshmail,Eve,Benny,Bite,na Paskalina walikamilisha kikao hichi,Christian alikuwa bustanini akibembea.

Reshmail alikuwa anatoa siri nzito nzito za kushangaza ambazo kwa namna kubwa kabisa zilitoa taswira ya mambo yaliyokuwa yamefichika kwa muda mrefu,uhusiano wa kimapenzi kati yake na mama yake mzazi ulimwacha kila mtu mdomo wazi,Reshmail aliomba msamaha kwa hilo na alieleweka na kusamehewa. Ni katika usimuliaji wa upande wa Bite kuhusu ngome ya vigogo iliyoleta fikra za mazingira ya kupotea kwa kadi yake ya benki katika mazingira ya utata mkubwa,Benny hakuongea neno kwani yeye alikuwa kama mgeni tu katika mkutano huo.

Mzee Manyama alikuwa kimya akimtafakari mkewe kwa maovu aliyoifanyia familia yake,kwa mateso aliyompa Adam na kwa uvunjifu wa amani aliouleta baina ya familia hizi mbili,kwa fedheha aliyomletea na kumvunjia heshima yake bungeni na hata mtaani,akiwa mwingi wa hasira alisimama bila kuaga na kuelekea chumbani,kwa hali aliyokuwa nayo Reshmail aliamua kumfata kwa nyuma ili asije kufanya jambo baya huko anapoenda,hasira yake ilipokelewa na na mwili wa mkewe ukiwa sakafuni,tayari alikuwa maiti.

?ulistahili hukumu hii? bila kushtuka alisema mzee Manyama huku akimpisha Reshmail aingie humo ndani.

*** ******* *****

Mapema baada ya mazishi ya mama yake mzazi Reshmail akiongozana na Adam katika gari ya baba yake,dereva akiwa Adam walifunga safari ya kwenda Mwanza kwa wazazi wake (Adam).

?utabaki ndani ya gari nitatangulia mimi najua watakuwa wakali hao lakini wakikuona ndipo mzizi wa fitna utakapokuwa umekatwa? Reshmail alimpa maelekezo Adam ambaye alikubali kwa ishara ya kutikisa kichwa.

Gari ilipaki nje kidogo ya nyumba ya kina Adam,kama walivyoelewana akashuka Reshmail akiwa amependeza sana,akaifunga gari kwa kutumia rimoti aliyoshuka nayo na kwa mwendo wa kunyata akaanza kuusogelea mlango akausukuma akaingia ndani,kupitia kwenye kioo Adm lishuhudi Reshmail akitoweka machoni pake.

?umefata nini hapa we mchawi Adam hajakutosha unamtaka na Rosemary ngoja sasa?.Rose!!!!?

Aliita mama Adam,Reshmail akiwa anatabasamu kwani alijua ni muda mfupi wote watakuwa na furaha kubwa.

Akiwa bado hajaanza kuongea alishuhudia mama Adam akimfuata na kisu huku Rosemary akifika pale na mwiko mkubwa,wakati huu akili yake ilifanya kazi haraka akaanza kukimbia lakini nguo yake ndefu ilimsaliti baada ya kunasa kwenye geti la kutokea nje.

Kwa macho yake mawili Adam alishuhudia Reshmail akiwa chini huku watu wawili wakimshambulia kwa fujo,alijaribu kufungua mlango lakini ulikuwa umewekwa ?loki? sauti yake haikuweza kusikika nje alipigapiga vioo vya gari lakini hakuna aliyemsikia.

Alishuhudia damu nyingi sana ikiruka juu. Kwa akili ya haraka haraka akakumbuka kushusha kioo akatokea dirishani

?mamaaaaaaaaaaaaaaa!!!? Adam akaita kwa nguvu palepale mama yake akageuka na kudondosha kisu alichokuwa nacho,

?Adam mwanangu ni wewe!!!?

Alisema mama Adam huku aimfuata Adam ambaye hakumjali bali alifika alipokuwa Reshmail

?Reshmail,Reshmail?

? mama na dada mmemuua mke wangu jamani mamaaaa!!? alilia Adam baada yakuona hajibiwi kitu.

?A.d?.am!! ninaku?.fa mume wangu?.ninakufa kwa furaha?..ni..meku..rudish?sha kwenu?naku?panda..sana?

Reshmail aliongea kwa kujiumauma huku akivuja damu,raia wengine walikuwa katika harakati za kutafuta msaada lakini msaada mkubwa uliopatikana ni wa polisi waliowatia nguvuni mama Adam na mwanae Rosemary huku roho ya Reshmail ikimaliza muda wake palepale Igoma jijini Mwanza.

kama usingekuwa ujasiri wa Adam basi tukio lile lingegharimu maisha yake,tayari mama mkwe amepotea,na sasa mpenzi wake Reshmail,mama na mdogo wake wakitupwa jela kwa kesi ya mauaji.

**** **** **** *****

?mapenzi yamenipotezea muda wangu nimekuwa mfungwa miaka mitano, mapenzi yameivunja vunja familia yangu, mwanamke niliyempenda ametoweka tayari tena mbele ya macho yangu,ni heri niisome hii sheria vizuri zaidi ili ikiwezekana siku moja niwatetee ndugu zangu walioko gerezani hao pekee ndio furaha yangu, kamwe siwezi kuhangaika tena na watoto wa hapa chuoni hata siku moja sidhani kama wana maana sana kwangu nikithubutu tena huenda yatakuwa makubwa zaidi ya awali.?

Alimaliza simulizi yake Adam.

MWISHO
 
Bonge la story... Safi sana...

Chapter Closed...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom