Simulizi: For You

Simulizi: For You

FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO

★★★★★★★★★★★★★★★★★


"Hey, kama umemaliza, nakuomba utupishe," Luteni Michael akamwambia Lexi.

"S..sawa..." Lexi akajibu.

"Nitakutafuta baadae Lexi, sawa?" Nora akasema.

"Haya..."

Lexi akajibu na kuanza kuondoka. Wasiwasi ulikuwa umemwingia na wazo moja tu likawa akilini mwake; akitoka hapo, ni moja kwa moja kumtafuta Oscar ili amfiche.

"Subiri!"

Sauti hiyo ikamfanya Lexi asimame, lakini hakugeuka nyuma. Ilikuwa ni Mario. Mwanajeshi huyu akaanza kumfata Lexi mpaka aliposimama, huku wengine wakimwangalia. Akafika usawa wa uso wake akimtazama kwa umakini.

"Niangalie," Mario akasema.

Lexi akamgeukia.

"Tulishawahi kukutana mimi na wewe?" Mario akauliza.

Lexi akatikisa kichwa kukataa.

"Mario unafanya nini? We... em' nenda," Mishashi akamwambia.

Lexi bila kukawia akaondoka haraka.

"Kuna mambo ya muhimu hapa, halafu we unakaa kuzitafutia tu balehe zako watoto," Mishashi akamwambia.

"Hamna bwana... huyo dada kama vile nilishawahi kumwona," Mario akasema.

"ACP, walinde uwapendao dhidi ya fataki," Hussein akamwambia Nora.

Nora na Luteni Michael walikuwa wamezama na Bobby kutafuta utambulisho wa "Erick," nao wakapata kujua kwamba mwanaume mwenye sura hii alikuwa anaitwa Oscar Amari, kijana fulani mfanyabiashara tu jijini hapo. Bila kukawia wakaanza kutafuta alipokuwa wakati huu, kwa njia zile zile kama walivyofanya kwa Kevin Dass.

Baada ya kujua, Luteni Michael akawaamuru Mishashi, Vedastus, Hussein, Alex na Omari waende pamoja naye kumkamata mwanaume huyo, halafu Bobby, Mario na ACP Nora wabaki hapo hapo pamoja na Nathan Masunga, na kumwambia Samuel, yule mchoraji, aondoke tu kwa kuwa msaada wake ulitosha. Nora akamwomba Luteni Michael aende pamoja nao, lakini Luteni akasisitiza kwamba ACP alipaswa kubaki hapo ili awe salama. Bila kukawia wanaume hao wakaondoka hapo kwenda kumkamata Oscar.



Giza lilikuwa limeshaingia ikiwa ni saa moja sasa. Lexi alikuwa akiendesha gari lake kwa spidi zote, huku akiwa ameunganisha kifaa kile maalum kumtafuta Torres ili amjulishe Oscar kwa njia salama kwamba alikuwa hatarini. Lakini Torres akawa hajibu, kwa sababu ni ndani ya muda huo ndiyo alikuwa anakula utamu wa LaKeisha huko "chini."

Lexi alichoka. Alijua kama angewatafuta wengine kwa njia ya kawaida (kutia ndani Oscar) na kuwapa ujumbe huo, ingekuwa hatari. Pia, sikuzote Mess Makers walikuwa na vifaa vya ufatiliaji endapo shida ingetokea kwa mmoja ili kuwapa "signal" wengine waje kutoa msaada, kama kipindi kile Kevin alivyofanya, lakini kwa wakati huu Oscar hakujua kwamba shida ndiyo ilikuwa inamfata, kwa hiyo hangeweza kuwasha hiyo signal mpaka impate, na kwa kuwa Lexi aliijua tayari, hakutaka impate mapema.

Kwa hiyo alichofanya, akawasha ya kwake aliyokuwa ameifichia ndani ya pete aliyovaa kwenye kiganja cha mkono wa kulia, ili wenzake wafikiri yeye ndiyo yuko kwenye shida, na kokote alikokuwa wangewahi kutoa msaada. Kwa wakati huu, ni Mensah, Victor, na Oscar ndiyo waliokuwa Dar, hivyo Lexi akafika maeneo fulani yaliyokuwa na miti mingi pembezoni na kuirusha pete yake yenye kifaa kile cha ufatiliaji kwa nguvu sana kuelekea huko, huku akiwa bado mwendoni. Nia yake ilikuwa ni kwamba, ikiwa Oscar na wengine wangetambua Lexi amewasha signal yake na kuanza kwenda kutoa msaada, basi wangeenda mpaka sehemu hiyo alipokirusha, hii ikimaanisha kwamba kokote Oscar alipokuwa, angeondoka, kwa hiyo Luteni Michael na wenzake wangekuta hayupo kule walikomfatilia.

Lakini bado Lexi hakuwa na uhakika sana kama jambo hilo lingekuwa na matokeo yenye faida sana, kwa hiyo bado akaamua tu kwamba angekwenda kule alikojua Oscar aliishi jijini humo kuangalia kama yupo ili awahi kumtorosha, na kama asingemkuta, basi ingekuwa imekula kwao. Akaendesha gari lake mpaka kwenye hoteli aliyokaa (yeye Lexi) na kuchukua nguo zake zile maalumu kwa ajili ya mapambano, kisha akarejea kwenye gari na kuondoka, akipanga kuzivaa ndani ya gari lake mbele ya safari kwa sababu alijua Luteni Michael na wengine wangekuwa wameshaanza mwendo kumfata Oscar.


★★★★


"Mmm... aaah... aaahh... tam beibyyy...aiiyyaah.. ssss... ooaah...."

Hizo zilikuwa ni sauti za kimahaba kutoka kwa mwanadada mmoja mrembo, ambaye alikuwa akipewa penzi motomoto na kijana mmoja mtundu sana, ambaye hakuwa mwingine ila Oscar mwenyewe.

Ilikuwa ni saa ya raha tu kwake, akiwa na mpenzi wake wa huku Dar es Salaam akimpa show ya uhakika. Nasema mpenzi wa Dar kwa sababu Oscar alikuwa na mpenzi kila mkoa aliowahi kukanyaga, ili kama kungekuwa na mission hapa na pale, basi asingeondoka sehemu hiyo bila kuitia alama. Lakini mwanadada huyu aliyekuwa naye ndiyo aliyekuwa wa karibu zaidi kwake kwa sababu ya Oscar kukaa Dar muda mwingi kuliko mikoa mingine, na hapa walikuwa wametoka kuangalia mechi pamoja na kuja kuliwazana kimahaba katikati ya tano kwa sita.

Oscar pia alikuwa akikaa kwenye chumba cha hoteli ya kifahari upande mwingine wa jiji. Mpenzi wake huyu alikuwa mwanadada mwenye miaka 23, naye alikuwa binti wa matawi ya juu pia. Uhusiano wao ulianza hasa kwa kuwa Oscar alikuwa mwenye swagger nzuri, na hawakuwahi hata kukaa kuzungumzia maisha ya familia zao wala nini na kufurahia tu "company" ya mmoja na mwenzake kinamna hiyo. Binti huyu angemtafuta Oscar na kutumia muda pamoja naye, kisha angelambwa viwili vitatu na kurudi kwao. Alimkubali sana Oscar, huku jamaa yeye akichukulia uhusiano huu kuwa "poa tu" maana alikuwa aina ya kijana unayeweza kumwita "playboy."

Baada ya kumridhisha mrembo wake, Oscar akalala pembeni, naye binti akakilalia kifua chake. Story mbili tatu zikafuata, kisha wote wakanyanyuka kwenda kujimwagia huku wakitaniana. Lakini kwanza, Oscar akaona ni vyema akiangalia kifaa chake kilichounganishwa kwa Torres ikiwa jamaa alikuwa amemtafuta, lakini hakukuta kitu. Akaghairi hata kuangalia kifaa kingine kuona kama kuna yeyote kati ya wenzake aliyetoa signal ya kuomba msaada kwa vifaa vyao vya ufatiliaji baada ya mpenzi wake kumshurutisha awahi bafuni ili waoge wote. Ikiwa tu angekiangalia, angetambua kwamba signal ya Lexi iliwashwa, lakini hiyo ikampita.



Ni wakati huu huu ndiyo Torres alikuwa amemaliza kumfikisha LaKeisha kwa mara ya nne kule "chini" kwenye maficho yao, na bado eti mwanamke huyo akataka waendelee. Torres akamtania kwa kusema hakutumia Viagra siku hiyo kwa hiyo hapo ndiyo walikuwa wamemalizana, naye LaKeisha akabaki akihisi furaha sana. Alikubali muziki wa Torres, hata akajiuliza ni kwa nini jamaa alikuwa anambania hivyo muda wote huo. Hapo ndiyo akajua kweli mambo mazuri hayahitaji haraka.

Torres akamwacha LaKeisha kitandani ili kwenda kuangalia kwenye mitambo yake mambo yoyote mapya, naye akaghafilika sana baada ya kukuta mapya mengi yenye kushtua. Lexi alikuwa amemtafuta kwa muda mrefu, naye akasikiliza maneno yake yote kwa makini na kuchoka hata zaidi. Akaangalia muda tokea jumbe hizo zilipoingia mpaka wakati huu, pale Oscar alipokuwa, na umbali kutokea kule Lexi aliposema Luteni Michael na wenzake walikuwepo, naye akapiga mahesabu ya haraka na kuona kweli alikuwa amemponza mwenzie.

Kwa wasiwasi mwingi akaanza kumtafuta Oscar kupitia kifaa kile salama, lakini hakujibu. Akawatafuta wengine, yaani Mensah, Victor na Kendrick pia, na kuwaambia yanayoendelea. Mensah na Victor wakasema kwamba walipata signal ya Lexi na walikuwa wakielekea kule alikokuwa, lakini Torres akawaelewesha kila kitu kwa kuwaambia Lexi alifanya hivyo kama njia mbadala, kwa sababu aliyekuwa hatarini zaidi ni Oscar. Kendrick alikuwa Geita akipanga mambo fulani kisiri kwa ajili ya timu yao, naye akakazia kwa Victor na Mensah kwenda alikokuwa Oscar ili wasaidie pia.



Oscar alipokuja kumaliza kuoga na kuvalishana nguo na mpenzi wake, akapata sasa kuiona signal ya Lexi ya kifaa chake cha ufatiliaji. Akashangaa sana, kisha akachukua kile kingine kwa ajili ya kuwasiliana na Torres na kukuta ametafutwa muda si mrefu. Akasogea pembeni ili kumpigia Torres, lakini kikaanza kuita kabla ya yeye kupiga. Alipopokea, Torres alisema neno moja tu lililomwelezea kijana huyu mambo mengi mno:

"Run!"

Alipaswa kukimbia haraka sana.

Bila kuuliza chochote, Oscar akaifata simu yake ya kawaida na kuitolea laini zake mbili, kisha akaikanyaga-kanyaga simu hiyo na kuzivunja laini zote, naye akaenda kuzitupa ndani ya choo cha kukaa humo bafuni. Akatoka na kuwasha kifaa chake cha ufatiliaji, kisha akaanza kubeba vifaa hivyo, nguo zile maalum kwa ajili ya mapambano, na pesa zake zote, na kuziweka ndani ya begi dogo la mgongoni kisha kulivaa. Binti akawa anamshangaa kwa sababu aliona ni kama mpenzi wake anataka kukimbia.

Akamuuliza tatizo lilikuwa ni nini, naye Oscar akamwambia hivi, "Haunijui, haujawahi kuniona, hukuwahi kuja kwenye chumba hiki, na haujui niko wapi. Yeyote atakayekuuliza chochote kuhusu mimi, kataa kwamba unanijua. La sivyo Aste, maisha yako yanaweza yakawa hatarini."

Binti akashindwa kumwelewa kabisa. Oscar akambusu tu mdomoni na kumwambia aondoke hapo upesi, kisha yeye akatangulia kuondoka. Alikwenda mpaka kwenye lifti (elevator) na kuingia, kisha akaanza kushuka chini akitumaini kuondoka hapo kabla ya waliomtafuta kufika. Alipotoka ndani ya lifti kule chini, akaanza kutembea upesi kuelekea sehemu ya kutokea kwenye jengo hilo la hoteli, lakini kasi yake ikakatizwa baada ya kuwaona wanaume waliokuwa ndiyo wameingia tu hapo. Alimtambua haraka yule aliyetangulia mbele, naye alikuwa ni Luteni Michael.

Oscar akaanza kurudi nyuma kuelekea lifti tena, lakini Alex akamwona na kumtambua, naye akawaonyesha wenzake haraka. Wote wakaanza kumkimbiza, Hussein akiwa mbele kutokana na kuwa mwenye kasi zaidi, lakini hakufanikiwa kumfikia kabla milango ya lifti haijafunga na Oscar kuanza kurudi juu tena. Watu waliokuwa sehemu hiyo wakawa wanashangaa kwa kutoelewa yaliyoendelea, lakini kwa kuona tu wanajeshi wale wakiwa wameshika bastola mikononi wengi wakaanza kukimbilia upande mwingine.

Luteni Michael akamwambia Alex abaki hapo chini kuangalia Oscar angeishia ghorofa ya ngapi ili awajulishe kwa sababu walitaka kupanda ngazi, na ili kuzilinda sehemu hizo mbili za lifti ikiwa Oscar angerudi chini tena, kisha Luteni Michael pamoja na wengine wakaanza kupandisha ngazi upesi kuelekea juu. Hoteli hii ilikuwa na ghorofa 13, naye Alex akaendelea kuangalia namba kwa nje zikiendelea kupanda tu, 4... 5... 6... 7....

Lakini Oscar akiwa ndani ya lifti hiyo huku wasiwasi ukiwa umemjaa, akashtushwa na kishindo kutokea juu yake, na baada ya kuangalia akaona mlango mdogo wa juu ukifunguka na mtu fulani akiingiza mkono wake kumpa yeye ili apande. Alipomwangalia, hakumwona uso kwa sababu ya kificha uso chake, lakini akatambua ni mwenzake kwa kuwa alikuwa amevaa nguo zile maalumu kwa ajili ya mapambano ambazo kila mmoja wao alikuwa nazo, na kwa haraka akajua ni Mensah kwa sababu nguo yake ilikuwa na mstari mwekundu shingoni. Ya Lexi ilikuwa na mstari wa njano, Torres wa zambarau, LaKeisha wa pink, Victor wa kijani, Kevin wa samawati, na Oscar mweupe.

Upesi Oscar akampa mkono wake, naye Mensah akamvuta kumpandisha kwa juu huku lifti ikiendelea kupanda. Oscar akamuuliza imekuwaje mpaka mambo yakawa hivi, lakini Mensah akasema hawakuwa na muda wa kuongea sasa. Hivyo wakaendelea kusubiri mpaka lifti ifike mwisho, na baada ya kusimama, wakaanza kupanda kamba nene zilizoishikilia lifti na kuelekea juu kabisa ili watokee kwenye dari la juu la ghorofa. Kwa kuwa lifti ilipofika mwisho ilifungua milango, hapo nje tayari Luteni Michael na wenzake walikuwepo na bastola zao wakiwa wamezielekezea humo, lakini wakashangaa kutomwona Oscar humo.

Luteni Michael akamuuliza Alex kwa vifaa vyao ikiwa Oscar alirudi chini labda, lakini Alex akakanusha. Wakiwa wanajiuliza ilikuwaje, Luteni Michael akamwambia Hussein aanze kurudi chini kwa kasi yake ili kuona tu kama Oscar angepatikana huko, halafu yeye pamoja na Mishashi, Vedastus na Omari waelekee juu ya ghorofa kabisa kwa kuwa nafasi za kumkuta huko zilikuwa kubwa zaidi. Hussein akachomoka upesi kuelekea chini, naye Luteni Michael na wenzake wakaanza kuelekea juu kupitia ngazi fupi za mwisho.

Upande wa kule juu, Oscar na Mensah tayari walikuwa wamepanda na kuanza kuelekea sehemu ambayo Mensah aliitumia kupanda juu ya jengo hilo kwa nje wakati anakuja. Alikuwa ametumia vifaa fulani viwili vyenye nguvu kali sana ya sumaku kupanda (kama mtu anayetambaa vile, lakini ukutani) kupitia chuma la bomba nene upande wa nyuma wa jengo hilo, hivyo wakati wa kushuka wangeshikana mikono miwili na kutumia mikono mingine kushika vifaa hivyo ili kushuka chini kwa pamoja.

Kwa kudhani kwamba walikuwa wamemchengua Luteni Michael na wenzake, wakafika hapo na kuanza kujiandaa kushuka pale sauti ya risasi iliposikika kutokea nyuma yao.

"Tulieni hivyo hivyo!"

Sauti ya Luteni Michael ikasikika vyema kutokea nyuma yao kwa umbali mfupi. Oscar akafumba macho na kutukana kichini-chini kwa kuwa alijua hapa walikuwa wamekwisha. Kwa kujiamini, Mensah akageuka nyuma, akiwa bado haonekani sura yake, naye Oscar vilevile akageuka. Sasa wakawaona wanajeshi wale wakiwa wanawakaribia huku bastola wakizielekezea kwao.

"Mikono juu," Luteni Michael akawaamuru.

Oscar akanyanyua mikono yake, lakini Mensah hakunyanyua.

"We ndiyo una kiburi eti?" Luteni Michael akamuuliza.

Kufikia wakati huu, Vedastus, Mishashi na Omari walikuwa wamewakaribia zaidi, nao walipowafikia wakawapiga miguuni na kuwafanya wapige magoti. Vedastus na Omari ndiyo wakaanza kushughulika kuwafunga kwa pingu mikononi kwa kuirudisha mikono nyuma, huku Mishashi akiwa bado amewaelekezea bastola.

"Hii siku ya bahati sana kwetu. Wawili kabisa!" akasema Omari.

"Hebu mtolee hiyo mask," Luteni Michael akamwambia Vedastus.

Vedastus alikuwa tu ndiyo ameushika upande wa pembeni wa kificha uso cha Mensah, pale aliposhtushwa na sauti ya maumivu kutoka kwa Luteni Michael. Wote wakamwangalia na kumwona amedondoka chini, akiwa amepoteza fahamu, lakini mtu aliyempiga hawakumwona. Ghafla tu akatua mtu fulani hapo na kurusha visu viwili vikali kwa kasi sana vilivyowapata Vedastus na Omari sehemu za mabegani kwa pamoja. Mishashi akaelekeza bastola kwake, lakini mtu huyo akamwahi na kumpiga mikononi kwa njia fulani iliyofanya mikono ya Mishashi ilegee, kisha mtu huyo akampiga ngumi za kasi sehemu ya pembeni ya nyonga, katikati ya kifua na pembeni ya shingo, naye Mishashi akaanguka na kutulia tuli!

Jambo hili liliwashtua sana Mensah na Oscar, kwa sababu hawakuweza kumtambua mtu huyo. Alivaa nguo nyeusi mwili mzima, na uso wake ulifunikwa kwa kitu kama kofia iliyotokea nyuma ya mgongo wake (kama yale masweta yenye kofia/hood). Mdomo wake ulizibwa kwa barakoa ngumu nyeusi yenye mchoro mweupe wa meno ya simba, na kuzunguka kiunoni kwake kulikuwa na mkanda wenye visu vidogo vidogo.

Mensah na Oscar wakasimama, huku bado mikono yao ikiwa imefungwa kwa nyuma. Hawakuweza kumtambua hata kidogo. Alikuwa mgeni kabisa kwao. Vedastus na Omari wakajitahidi kunyanyuka na kuvitoa visu vile mabegani mwao, na ile tu walipokuwa wanataka kumpiga mtu huyo kwa risasi, akaruka sarakasi nyingi kuwaelekea na kuzipiga bastola zao kwa miguu. Kisha akaanza kuwapiga wawili hao kwa kasi sana na kwa kuwachanganya mno. Wote wakaanguka chini na kutulia tuli!

Mtu huyo akamgeukia Oscar, ambaye alikuwa upande wa kulia akimwangalia kimaswali, naye akamwangalia na Mensah, ambaye alikuwa kushoto kwake. Oscar na Mensah wakaangaliana, kisha baada ya kupeana ishara, wakamfata hivyo hivyo wakiwa wamefungwa ili wamshambulie. Walijitahidi kupigana naye kwa kupokezana mitindo ili kuweza kuiwekea miili yao mihimili mizuri, lakini mtu huyo akawashinda ujanja.

Oscar kwa sababu ya wepesi wake alifanikiwa kuirudisha mikono yake iliyofungwa kwa mbele kwa kuikunja miguu yake, kisha akambana mtu huyo kwa pingu sehemu ya shingo akitaka kumnyonga. Lakini mtu huyu akaigeuza nguvu ya Oscar dhidi yake mwenyewe na kumpiga ngumi zake zile za kasi, naye Oscar akadondoka chini. Mensah ndiyo bado alikuwa mzito kutokana na mikono yake kuwa kwa nyuma bado, lakini akaendelea kujitahidi kurusha chochote alichoweza.

Mtu huyo akafanikiwa kumpiga Mensah kwa njia iliyomfanya aishiwe nguvu, kisha akaanza kumfata ili ammalize. Oscar akamwahi na kuchomoa kisu chake kimoja ili amchome, lakini mtu huyo akamkwepa na kumpiga ngumi mbili za kasi katikati ya shingo yake, naye Oscar akajishika shingoni akihisi maumivu makali. Bila Oscar kutazamia, mtu huyo akakishika kichwa chake alipokuwa ameinama huku ameishika shingo bado, na kujiviringisha kwa sarakasi nyuma ya mgongo wake huku bado akiwa amekishika kwa nguvu, na hapo akawa amemnyonga Oscar!

Mwili wake ukadondoka chini kama mzigo mzito, huku kichwa chake kikiwa kimegeukia mpaka nyuma ya mgongo wake kabisa!

Mensah bado alihisi kama nguvu imemtoka, lakini aliona vizuri sana jambo lililompata mwenzake. Alihuzunika sana. Mtu huyu asiyejulikana akaanza kumfata na Mensah ili ammalize pia, na ile anataka tu kumshika, mkono wake ukavutwa nyuma kwa nguvu sana na kushtukia anapigwa teke lililompata sehemu ya taya na kusababisha aangukie pembeni. Mensah alipomwangalia aliyempiga adui huyo, akatambua ilikuwa ni Lexi, akiwa ndani ya nguo zake za mapambano.

Mtu yule akajinyanyua kwa sarakasi na kukaa mkao wa kupambana, huku Lexi akiwa anamwangalia kwa hasira sana ndani ya mask yake. Wawili hawa wakaanza kufatana, na mkono ukaanza. Mtu huyo alifikiri angeweza kumlainisha Lexi kama alivyofanya kwa wengine, lakini alikuwa amekosea sana. Lexi aliyazuia mapigo yake yote na kumfumua yeye kisawasawa. Alijua vyema jinsi ya kupigana, hivyo alijilinda dhidi ya adui huyu na kujaribu kumlipizia kisasi Oscar. Ingawa hivyo, bado adui huyu alionekana kuwa mzoefu sana na kufanikiwa kukwepa pia mapigo ya Lexi yaliyoelekea kumuua. Wote walitumia njia zote walizoweza, lakini ikawa ngoma droo.

Ni wakati huu Luteni Michael ndiyo akaanza kurejewa na fahamu, naye akawa anawaona kwa mbali wawili hao walipokuwa wanapigana. Akaiokota bastola yake na kujitahidi kuunyanyua mkono wake uliokuwa hauna nguvu sana na kuielekeza kwa Lexi, akiwa bado amelala hapo chini, kisha akafyatua risasi iliyompiga mgongoni. Ijapokuwa Lexi aliweweseka kidogo baada ya risasi hiyo kumpata, ikawa imedunda kutokana na nguo ya Lexi kuwa 'bulletproof.' Hii ikafanya adui yule asiyejulikana aanze kuruka masarakasi yake mpaka kwa Luteni Michael na kuipiga bastola pembeni, kisha akakimbilia upande uliokuwa na nyaya nene aliyotumia kufikia huko juu na kuirukia, naye akatokomea kutoka hapo.

Lexi akamtazama Oscar pale chini. Aliingiwa na simanzi nzito sana kumwona rafiki yake akiwa mbali na uhai. Luteni Michael akawa anajaribu kujinyanyua, lakini viwiko vya mikono yake vilikuwa legevu sana kiasi kwamba akawa anashindwa. Akawaona vijana wake watatu pale chini wakiwa wamelala tuli tu. Akajiuliza ni kwa nini Hussein na Alex hawakuwa wamefika huku juu tokea muda ule alipopiga risasi hewani kuwazuia Oscar na mwenzake wasitoroke, kwa kuwa walitakiwa kuwa msaada mkubwa kwao.

Lexi akamfata Oscar pale chini, akapiga magoti huku akiangalia kichwa cha kijana huyu kikiwa nyuma ya shingo yake, naye akadondosha chozi la huzuni ndani ya mask yake. Sauti za ving'ora vya magari ya polisi zikaanza kusikika zikija kutokea kule chini.

"Hey.... we have to go..."

Mensah akasikika akimwambia hivyo, naye Lexi akafumba macho na kunyanyuka. Alipokuwa anaanza kumfata Mensah, akasimama, kisha akamwangalia Luteni Michael pale chini. Luteni yeye alijua anaangaliwa lakini sura ya aliyemwangalia hakuiona, hivyo akabaki kumtazama tu pia kama anasubiri afanye jambo fulani. Lexi alikuwa na hasira siyo mchezo, lakini hakukuwa na muda wa kuzimalizia hapa. Akalifata begi la Oscar na kulichukua, kisha akamfata Mensah na kuzifungua pingu mikononi mwake, akamsaidia kunyanyuka, nao wakaondoka hapo kupitia njia ile ile ya Mensah. Ilibidi tu Mensah ajikaze kushuka hivyo hivyo ingawa alihisi mwili wake hauna nguvu, lakini wakafanikiwa kuondoka huko.

Luteni Michael akaachwa hapo anazikusanya nguvu zake ili anyanyuke. Alikuwa akijiuliza mtu huyo alimpiga jinsi gani mpaka kufanya nguvu zake zimtoke. Akiwa anajibebabeba, wakafika maaskari hapo na mabunduki yao, wakamfata na kumsaidia kunyanyuka, naye Luteni Michael akawaambia wawaangalie wenzake kama walikuwa bado wamepoteza fahamu.

Lakini ukweli ukawa ni kwamba, Mishashi, Vedastus, na Omari, hawakuwa hai tena. Luteni Michael alihuzunika sana. Akafumba macho yake na kukaa chini tena. Maaskari wenyewe wakaendelea kufanya yao juu hapo kama kuiondoa miili ya maiti, ikiwa ni saa 3 ya saa 4 usiku sasa, na kwa sababu ya msiba huu uliokuwa umewapata wenzake, Luteni Michael aliacha hata kukaza fikira kuwaambia maaskari kwamba maadui walitorokea kupitia wapi, na wawazungukie wapi.



Baada ya muda fulani, waandishi wa habari kutoka vyombo kadhaa wakawa wamefika, nao wakaanza kuhojiana na maaskari. ACP Nora na Mario wakawa wamefika pia sehemu hiyo. Walijiunga na Alex na Hussein ambao nao walikuwa wamepoteza fahamu tokea muda fulani nyuma. Kujua kwamba Vedastus, Omari, na Mishashi hawakuwa hai kuliwatia simanzi pia. Wakawa wanamuuliza Luteni Michael ni nini kilitokea.

"Mlikuwa wapi?" Luteni Michael akawauliza Alex na Hussein.

"Luteni... sisi... mimi nilipofika chini sikuona lolote lile la ajabu kutokea juu, nilimkuta tu Alex pale. Ndiyo kidogo tu tukasikia mlio wa risasi..." Hussein akasema.

"Watu wakaanza kukimbia ovyo ovyo. Tukaanza kupandisha juu. Lakini tulipofika ghorofa fulani akatokea mmoja wao, akapambana nasi... akafanya tukapoteza fahamu..." Alex akamwambia.

"Huyo mmoja wao mlimwona sura?" akauliza Mario.

"Hapana... kuna... mask fulani wanavaa," akasema Hussein.

"Kwa hiyo, ni kwamba Mess Makers wamemuua huyu Oscar kwa sababu tulimtambua au?" akauliza Mario.

"Na ni kwa nini wamuue Veda, Misha, na Omari halafu wewe wakuache?" akauliza Nora.

"Kulikuwa na mtu mwingine hapa... na yeye siyo mmoja wao," akasema Luteni Michael.

Wote wakamwangalia kwa umakini.

"Alikuwa anapigana nao... lakini na yeye sikumwona... yaani... hii inachosha sana," akasema Luteni Michael.

Kifaa cha mawasiliano cha Mario kikaita, naye akasogea pembeni, akapokea na kuongea na Bobby.

"Luteni... Bobby anasema Kanali Oswald anakutafuta," Mario akamjulisha baada ya kurejea.

"Yuko wapi?" Luteni Michael akauliza.

"Amefika jengoni," Mario akasema.

"Tunapaswa tukupeleke kwanza hospitali," Nora akamwambia Michael.

"No. Tunaenda huko huko. Kanali nilikuwa nimeshamwambia kuhusu hii ishu na kumwahidi ningemletea matokeo mazuri leo leo kama exchange ndogo ya msaada wake kwa ile hacking aliyofanya Bobby..." Luteni Michael akamwambia.

"Kwa hiyo... sasa matokeo siyo mazuri... atafanya nini?" akauliza Hussein.

"Ndiyo twende ukajue," Luteni Michael akamwambia na kuanza kuondoka.

Nora, Hussein, Mario na Alex wakabaki kuangaliana, kisha nao wakaondoka hapo pia wakimfata Luteni Michael.

Mwili wa Oscar ulipelekwa kuhifadhiwa, vile vile na miili ya wanajeshi wale watatu. Timu ya Luteni Michael haikuwa na wanajeshi wa ovyo ovyo tu, walikuwa ni watu aliofanya nao kazi kwa ukaribu na kwa muda mrefu, hivyo aliwathamini sana. Vifo vya hawa watatu vilimpa pengo kubwa sana ambalo ingechukua muda mrefu kuja kuliziba. Alijilaumu pia, kama ilivyo kawaida ya mtu akifiwa, kwa kuhisi ni kama hakufanya mengi kuweza kuokoa maisha ya wenzake.

★★

Walipofika kule kwa Bobby, walimkuta Kanali Oswald Deule akiwa hapo, naye akamuuliza Luteni Michael zawadi yake ilikuwa wapi. Luteni akamweleza kila kitu, na kuomba samahani kwa kuwa mpango wake ulikuwa ni kumkamata Oscar akiwa hai, lakini sasa angempatia Oscar aliyekufa. Akamwambia kama alitaka kuwapa adhabu yoyote ile angeikubali tu, hata kama akiondolewa kwenye mission hii, kwa kuwa alihisi ni kama amepoteza muda mwingi tokea walipoanza msako huu bila kuleta matokeo yoyote mazuri.

Lakini kwa kushangaza, Kanali Oswald akamwambia asifikiri hivyo, na kwamba kiukweli kazi waliyokuwa wameifanya ilikuwa nzuri, na walitakiwa kuendelea. Wote hapo walidhani labda Kanali Oswald angewaambia waweke kituo kikuu katika msako huu, lakini ikawa tofauti. Kanali akamwambia Luteni Michael alielewa kwamba amepoteza watu muhimu kwake, kwa hiyo angetarajia aendelee na mgawo huu ili awalipizie na kisasi. Hakuna mtu mwingine aliyeweza kufika hadi kwenye hatua ya kumkamata Kevin Dass na Oscar Amari isipokuwa Luteni Michael na timu yake, hivyo Kanali Oswald akawaambia wangeendelea na kazi zaidi baada ya kufanya msiba kwa ajili ya wanajeshi wake. Akamwahidi pia kwamba msiba huu ungefanywa kitaifa ili kuwaenzi wanajeshi hao, na ili kuwaonyesha watu jinsi Mess Makers walivyo watu wabaya sana.

Baada ya hayo, Kanali Oswald akamwita Luteni Michael pembeni ili waongee. Alimkumbusha kwamba kwenye msako huu, alipaswa kuwa mwangalifu sana ili Nora asiingie kwenye matatizo kwa maana alijua baba yake ni nani. Lengo la Nora kuwa hapo lilikuwa wazi; kuwasaidia tu kuwapata maadui, lakini kwenye suala la kuwafuata maadui alipaswa kumweka Nora pembeni. Luteni Michael akamhakikishia kwamba Nora angekuwa salama kwa sababu hata leo alimwacha nyuma kabla ya kwenda kwa Oscar, kwa kuwa alijua umuhimu wake. Akamshukuru kwa uelewa wake, naye Kanali Oswald akaondoka hatimaye.


★★★★


Lexi na Mensah walikuwa wamefanikiwa kutoka eneo lile na kuondoka jijini hapo haraka sana. Sehemu waliyokuwa wakielekea haikuwa nyingine ila kule "chini," mafichoni kwa timu yao nzima. Victor pia alijiunga nao njiani, kwa sababu upande wa jiji la Dar es Salaam alikokuwa ilikuwa ni mbali, na ndiyo sababu hakuwahi kufika kule Oscar alipokuwa kama alivyowahi Mensah. Walikuwa kimya tu kwa masaa kadhaa wakiwa mwendoni mpaka wanafika kule. Tayari taarifa za kifo cha Oscar zilifikia screen za Torres, ambaye alihuzunika sana. LaKeisha na Kevin waliachwa na simanzi kuu pia kwa kumpoteza mwenzao.

Baada ya Lexi na wengine kufika huko, LaKeisha alimpokea Lexi kwa kumbatio huku akilia sana. Wanaume walikaa tu pembeni wakiwa kimya, bila kutazamana hata kidogo. Lexi alikuwa anatokwa na machozi bila kutoa sauti yoyote, naye akaelekea sehemu yenye chumba pamoja na Lakeisha ili kumtuliza. Alijitahidi kumbembeleza huku naye akiumia sana moyoni. Kulikuwa na hali fulani ya utengano wa kihisia ndani ya kundi hili kwa sababu ya kifo cha mwenzao, na muda ukasonga wakiendelea kuwa hapo bila kufanya lolote zaidi ya kusikitika sana.

★★

Ilifika asubuhi, na boss wao, yaani Kendrick Jabari, akawa amefika huko pia. Aliwakuta vijana wake wakiwa wameketi kwenye chumba cha pamoja, na baada ya LaKeisha kumwona akamfata na kumkumbatia huku analia. Kendrick alikuwa na uso ulioonyesha utulivu tu, naye akambembeleza mwanamke huyo na kwenda kuketi pamoja naye.

Wote walikuwa wamevaa T-shirt nyeusi, isipokuwa Kendrick, aliyefika akiwa amevaa suti yenye rangi ya kijivu. Akaomba aelezewe kila kitu, naye Mensah akamsimulia aliyojionea. Torres pia akaongea, na mwanaume huyo akaeleza mambo yote yaliyotokea kwa upande wake, akisema ni kutokuwa kwake makini ndiyo kulisababisha mambo yote hayo kutokea. Akamwomba Kendrick ampe adhabu kwa sababu hiyo, naye Mensah, Kevin, LaKeisha pamoja na Victor wakasema hivyo hivyo pia kwa kuwa waliona ni kama na wao hawakuwa makini vya kutosha.

Kendrick akamwangalia Lexi. Alikuwa amekaa tu kimya bila kumtazama, huku akipigapiga kidole chake kimoja juu ya meza, naye Kendrick akasimama na kuanza kuondoka hapo. Wengine wakawa wanamwangalia tu mpaka alipokaribia sehemu ya kutokea, kisha akasema, "Nifate," bila kugeuka kumtazama yeyote kati yao, naye akatoka. Kila mmoja wa vijana hawa akamtazama Lexi, wakielewa Kendrick alimaanisha yeye, naye akanyanyuka na kumfuata Kendrick.

Alifika alipokuwa na kumkuta amesimama tu, hivyo akaenda mpaka karibu na kusimama pembeni yake.

"Ni nani aliyemuua?" Kendrick akauliza.

"Sijajua," Lexi akasema.

"Kivipi? Si ulipigana naye?"

"Alificha sura. Huyu hakuwa askari wala... yaani... alikuwa tofauti...."

Kendrick akashusha pumzi.

"Unaonaje? Itakuwa sahihi nikiwapa adhabu hawa?" Kendrick akauliza.

"Wamekosa nini kwani?" Lexi akauliza pia.

"Kama wangekuwa hawajakosea, wasingeomba adhabu..."

"Itasadia nini? Kumrudisha Oscar?"

Kendrick akamwangalia na kuuliza, "Kwa hiyo unataka nifanye nini?"

"Sitaki ufanye chochote uncle. Nataka tu nimshike huyo mpumbavu aliyemuua mimi mwenyewe..."

"Huyu Nora ameshaanza kuwa tatizo kubwa sana. Tunahitaji kumng'oa," Kendrick akasema.

"Uncle... yule yupo kufanya kazi aliyopewa, kama huyo Michael na wengine tu. Hawakuwa na nia ya kumuua Oscar... aliyemuua ni mtu mwi...."

"Lakini ni kwa sababu yake ndiyo maana wameweza kumfikia!" Kendrick akamwambia kiukali.

Lexi akaangalia chini kwa huzuni.

"Umenifundisha kutoongozwa na hisia kwenye kuamua mambo ili nifanye maamuzi yaliyo sahihi. Wakati huu ni mgumu kwetu sote uncle, kwa hiyo nakuomba tafadhali tuliza kwanza akili. Mimi pia nahitaji hilo. Kwa ajili ya Oscar... please uncle..." Lexi akasema kwa hisia.

Kendrick akabaki kumtazama tu, kisha akaangalia pembeni tena.

Wawili hawa wakaendelea kusimama hapo, bila kujua kwamba Kevin alikuwa amejibanza umbali mfupi kutokea hapo akiwasikiliza. Jamaa akatoka hapo na kwenda kuketi sehemu ambayo alikuwepo Victor akipata chakula kidogo.

"Vipi? Mbona sura ngumu?" Victor akamuuliza.

"Mimi huwa nashindwa kuelewa, basi tu," Kevin akasema.

"Mpaka leo bado hujaelewa nini?" Victor akauliza.

"Si huyu Lexi... sijui yukoje..."

"Amefanya nini, ongea point basi..."

"Hivi ni kwa nini yeye ndiyo anatuongoza sisi? Mm? Ningetarajia kwa mtu kama Torres au wewe na kipaji chako labda hata ndo' ungekuwa mbele yetu, lakini eti na wewe unapewa maagizo na hako kasichana unakokazidi umri..."

"Kwani wewe... ahah... shida yako ni umri tu, au bado roho inakuuma kwa sababu ulimtokeaga akakupiga chini?"

"Siyo hivyo. Me naona mambo yake hayajakaa sawa. Hapa juzi hao mafala walinishika akanikalisha tu hapa, sa'hivi Oscar ameenda... boss anamwambia tumshughulikie huyo Nora eti anakataa. Me nakwambia wote humu ndani mtakufa kwa sababu yake," Kevin akasema.

Victor akaweka chakula chini.

"Naomba unisikilize. Tena unisikilize kwa makini sana. Bila huyo msichana sasa hivi usingekuwa hapa, elewa hilo. Ametuongoza vizuri sana tokea wakati ambao haukuwahi fikiri kuna watu kama sisi, vizuri kuliko hata Raisi wa nchi hii anavyodanganya kufanya. Hii kitu ya Oscar.... Kevin, hatukuiona inakuja. Siyo kwamba kwa sababu kuna mambo tunayafanya vizuri hiyo imaanishe sisi ni wakamilifu, NO! Makosa yatatokea tu, upende usipende. Ikiwa boss angekuwa amekupa wewe ndiyo utuongoze sisi, haki ya Mungu nakwambia tungekuwa tunanyea debe sa'hivi, ohooo!" Victor akasema.

Kevin akawa anayasikiliza maneno yake lakini kwa kukerwa.

"Heshimu kilichowekwa, acha kulalamika-lalamika. Lexi akiona hapa inafaa, inafaa. Akiona jambo halifai, ujue kweli halifai. Alikwambia ukae huku, mpaka sasa hivi uko salama. Ungekuwa nje kama Oscar...." Victor akaishia hapo na kumwangalia tu usoni.

Akabeba chakula chake na kujiondokea tu, akimwacha Kevin bado akiwa anaona kama vile mambo yote yaliyotokea yalikuwa ni makosa ya Lexi, na kulipaswa kufanywe jambo fulani ili kurekebisha hayo yote.



Kendrick na Lexi walijiunga na Lakeisha pamoja na Torres, wakijadiliana kuhusu njia ambayo Luteni Michael na ACP Nora walitumia kumpata Oscar. Lexi akawaambia kwamba alimwona mwanaume yule aliyefanya kazi benki kuu pamoja nao, yaani Nathan Masunga, naye Torres akatambua sasa kwamba walimpata Oscar kwa njia hiyo. Akawakumbusha kuwa Oscar alitumia jina bandia la Erick kipindi kile wanajipanga kuiba pesa zile, na alimlipa jamaa ili siku hiyo asiende kazini. Torres akawa anaona sasa kwamba kiukweli ACP Nora alikuwa mwerevu kupita maelezo mpaka kufikiria njia hiyo ili kugundua ukweli, na bado akawa anajilaumu kwa kukosa kuwa makini siku ya jana.

Kendrick akasema kwamba kuanzia sasa mambo yangetakiwa kuwa sawa zaidi. Aliwataka wawe makini hata zaidi ili watimize yale waliyotaka kuyatimiza kwa wakati mwafaka. Baada ya hapo, Kendrick akaondoka huko "chini" ili kurudi Geita haraka.

LaKeisha akaongea na Lexi, akimwambia kilichotokea baina yake na Torres. Lexi akamwambia ilikuwa ni sawa, na ijapokuwa wakati huu walikuwa kwenye huzuni, alifurahia kwa ajili yake. Akampa ushauri kwamba asimwache Torres maana ni mwanaume mzuri sana, kisha naye Lexi akaenda kwa Torres, ambaye alimpatia kifaa kingine cha ufatiliaji, halafu akaondoka sehemu hiyo ya maficho.

Torres alimfanyia vipimo Mensah kuelewa ni njia gani adui yao mpya aliitumia kumpiga bila kutumia nguvu nyingi mpaka mwanaume huyu akaishiwa nguvu kabisa, lakini bado hakuweza kuelewa. Kwa hiyo sasa Mess Makers wakawa na adui mpya asiyefahamika, na pengo kubwa sana kwenye timu yao lililoachwa na kijana Oscar.


★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★

WHATSAPP +255 787 604 893
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA

★★★★★★★★★★★★★★★★★


Taarifa za kuuawa kwa Oscar ziliwafikia viongozi wale wafisadi na waovu, yaani Raisi Paul Mdeme, Jenerali Jacob Rweyemamu, Luteni Jenerali Weisiko, na wale wengine kwenye muungano wao wenye kufanya na kuficha maovu. Raisi Mdeme alikasirishwa kwa kadiri kubwa na kuwajulisha wawili hao kuwa nafasi kama hiyo ilitakiwa kuwa yenye matokeo mazuri, yaani Oscar akamatwe akiwa hai ili waweze kumbana vyema kusema wenzake wako wapi. Mdeme alichoambiwa ni kwamba, wakati walipofanikiwa tu kumkamata Oscar, wenzake walitokea na kumuua ili asije kuwafichua, kisha wakatokomea. Kwa hiyo Raisi huyu akawaambia wakuu hawa wa kijeshi wahakikishe watu wao wanafanya mambo kwa umakini zaidi ili kupata matokeo aliyotaka.

Lakini Mdeme alifichwa ukweli muhimu na Jenerali Jacob pamoja na Weisiko. Kumbuka wawili hawa walikubaliana kwamba hawangeruhusu yeyote kati ya watu kutoka kundi la Mess Makers akamatwe na watu ambao hawakujua siri zao (watu kama Luteni Michael na timu yake), ijapokuwa Raisi Mdeme yeye alichukulia mambo kijuujuu tu na kulazimisha watumie njia hiyo kuwakamata (yaani timu ya Luteni Michael na ACP Nora), kwa hiyo Jenerali Jacob na Luteni Jenerali Weisiko waliamua kwamba wangeiweka "silaha" fulani muhimu ya Weisiko kuifatilia timu ya Luteni Michael, ili wakiwakaribia tu Mess Makers, "silaha" hiyo iwe ya kwanza kuwashika na kuwanyonya ukweli, la sivyo iwaue kabla ya Luteni Michael na wengine kuupata.

Silaha hiyo, ndiyo yule mtu asiyefahamika ambaye alimuua Oscar usiku ule, pamoja na wanajeshi wale watatu wa timu ya Luteni Michael.

Kwa hiyo, "silaha" hiyo, au "silaha" huyo, alirudi kwa Weisiko na kumwambia hakufanikiwa kumkamata Oscar kwa wakati, kwa hiyo akamuua. Baada ya Weisiko kuwa amemjulisha Jenerali Jacob juu ya hilo, akampongeza kwa kazi hiyo na kumwambia aendelee kuwa chonjo nao kwa sababu bado Luteni Michael na timu yake wangeendelea na msako huo, hivyo "silaha" angepaswa kuwa karibu endapo wangefanikiwa kuwapata Mess Makers ili awepo kufanya yake.

Jenerali Jacob na Weisiko wakaendelea kuwa na ukaribu wao ambao tokea zamani uliwapa nguvu, huku Raisi Mdeme akidhani bado wanafuata tu njia yake kwa utiifu, kumbe ni wanafiki wakunjufu.


★★★★


Maandalizi kwa ajili ya msiba wa wanajeshi wale watatu, Mishashi, Vedastus na Omari, yalikamilika na kufanyika siku mbili baada ya kuuawa kwao. Wangepatiwa heshima na utambuzi mkubwa nchini kwa kuwa walionekana kama wajitoaji muhimu kwa nchi yao mpaka kufikia kifo kwenye vita hii iliyokuwa ikiendelea baina ya serikali na Mess Makers. Wanafamilia, marafiki, viongozi mbalimbali wa usalama wa taifa pamoja na makamu wa Raisi wangekuwepo hapo, na vyombo vya habari vilirusha kipindi maalumu cha kuwaaga "wazalendo" hao.

Luteni Michael alikuwa mwenye hasira sana kutokana na jambo lililowapata watu wa timu yake, na aliona ni kama msiba huu ulikuwa ni matangazo tu yasiyokuwa na maana yoyote kwa sababu aliamini njia sahihi ya kuwaenzi watu wake hao ilikuwa ni kuwakamata Mess Makers. Alikuwa anataka kuwaua yeye mwenyewe, lakini pia alielewa kazi yake ilimtaka kuwakamata wakiwa hai kwanza. Ijapokuwa wengine wangekwenda msibani, yeye alikuwa akifanya utafiti peke yake wa matukio ya usiku ule ili abaini mambo haraka, na hivyo kuweza kuwalipizia kisasi watu wa timu yake.

Maneno mengi sana yalisemwa kuhusu jinsi ambavyo Mess Makers wameendelea kuua watu wasio na hatia na uhakika wa kuwakamata. Picha ya Oscar ilitumiwa kama onyesho la mafanikio katika kulikaribia kundi la Mess Makers, kwamba muda si mrefu wote waliokuwa pamoja naye wangekamatwa, kisha aidha kufungwa au kupewa hukumu ya kifo kutokana na mabaya waliyoiletea nchi.

Baada ya pindi maalumu za msiba kuisha, ACP Nora alijiunga pamoja na Mario, Hussein, Alex, na Bobby, kwenda kwa Luteni Michael ili kuendelea na utafiti. Ilikuwa bado ni kwenye jengo lao lile lile, nao wakaanza kujadiliana naye kuhusu hatua ambazo zingefuata. Nora tayari alikuwa ameyarudisha mafaili yale yenye taarifa za watu waliojeruhiwa kwenye bomu kwa daktari Shani, naye alimshukuru kwa hillo na kumpa pole ya msiba wa rafiki zake. Luteni Michael alionekana wazi kuwa amevunjika moyo ijapokuwa hakukata tamaa. Wengine walijitahidi kufuata maagizo yake na kuangalia kila njia mpya ya kubaini lolote kuhusu Mess Makers, lakini wakashindwa kupata lolote lenye kuwasaidia.

Kwa hasira nyingi, Luteni Michael alianza kupiga vitu kwa nguvu na kurusha maboksi yenye vifaa mbalimbali chini. Alihisi ni kama sasa wasingeweza kuwapata watu hao maana walijificha kwa njia iliyokuwa ngumu sana kufichua. Akawaambia wanajeshi wake pamoja na Nora waondoke tu na kwenda kupumzisha akili na mwili mpaka muda fulani ambao ungefaa siku ya kesho ili wajadili mambo kwa njia nzuri zaidi. Hakuwaambia hakuwa sawa kihisia, ila wote walielewa hiyo ndiyo iliyokuwa sababu.

Wanajeshi wa timu yake wakaondoka tu, na hapo akabaki Luteni Michael na Nora pekee.

"ACP... nafikiri umenisikia niliposema mnaweza kwenda. Mbona umebaki?" Luteni Michael akauliza huku akisoma jambo fulani kwenye makaratasi.

"Siyo makosa yako," Nora akamwambia kwa sauti yenye kujali.

"Nini?"

"Kilichowapata... siyo makosa yako," Nora akasema.

Luteni Michael akamtazama kiufupi, kisha akasema, "Nenda karukeruke kidogo popote ujuapo ili ukirudi ufanye kazi kwa njia ambayo itasaidia makosa mengine yasitokee. Ondoka... kapumzike ni usiku sasa."

Nora akamwangalia tu kwa huruma kiasi. Alielewa mwanaume huyo alikuwa kwenye hisia kali za hatia ijapokuwa alijitahidi kuonyesha yuko imara. Kwa kuelewa kwamba alichohitaji ilikuwa ni kuachwa peke yake, akaridhia tu kwamba kumwacha kwanza ilikuwa jambo la busara.

"Okay. Nikirudi bila shaka nitakuwa nimepata jambo lingine la kufanyia kazi. Usiku mwema," Nora akasema, kisha akaanza kuondoka.

Luteni Michael akamtazama tu mpaka alipotoka ndani ya jengo, naye akaketi kiuchovu na kufunika uso wake kimasikitiko. Alijisikia vibaya kutokana na yote yaliyotokea, lakini hata zaidi alijihisi vibaya kwa kumsemesha Nora kwa njia ambayo hakuona inafaa. Kufikia wakati huu alikuwa amejenga upendezi mwingi kumwelekea mwanamke huyo ijapokuwa hakuonyesha wazi jambo hilo, na sasa akawa anafikiria huenda ingempa faraja kwa kadiri fulani kama angefunguka kwake. Akanyanyuka na kwenda mpaka nje kwenye gari lake, akiwa ameamua kumfuata Nora kule kule kwenye chumba chake cha hoteli ili aongee naye. Hakujua itikio la mwanamke huyu lingekuwaje, kwa hiyo alijiweka tayari kwa lolote na kuiridhisha nafsi yake kuwa angekubali matokeo; mazuri au mabaya.

Aliendesha gari lake mpaka maeneo ilipokuwepo hoteli alikopanga Nora, lakini aliishia mbali kidogo kuifikia baada ya kukuta kundi la watu nje hapo wakionekana kama wamezunguka tukio fulani. Akashuka na kwenda pale ili kujua ni nini kilikuwa kinaendelea, naye akalikuta gari la Nora likiwa limeegeshwa upande huo na mlango wa mbele ukiwa wazi. Walinzi wawili wa jengo la hoteli hiyo walikuwa wakizuia mtu yeyote asiliguse gari hilo mpaka polisi wafike, naye Luteni Michael akawakaribia na kuwauliza nini kilikuwa kimetokea.

Walimweleza kwamba wakati ACP Nora alipokuwa tu amefika hapo, lilikuja gari fulani kama hiace lenye rangi nyeusi, na wanaume kadhaa wakashuka na kumkamata Nora kisha kumwingiza ndani yake kwa lazima, na kutokomea kusikojulikana. Luteni Michael aliwauliza kiukali walikuwa wanafanya nini mpaka wakaruhusu mtu anatekwa kirahisi sana, nao wakamwambia walikuwa kwenye kazi zao hivyo hawakuweza kutenda kwa uharaka kwa sababu watu hao walishtukiza sana.

Baadhi ya walioshuhudia jambo hilo walikuwa wanasema Nora alishuka, kisha wanaume hao wakaja haraka na kuanza kumvuta kwa nguvu lakini akawa akijitahidi kujinasua, ndiyo wakampiga na kumfanya apoteze fahamu, kisha wakamwingiza na kuondoka naye. Luteni Michael alikasirika sana, huku hofu ikimpanda kwa wakati huo huo. Akauliza ulikuwa umepita muda mrefu kadiri gani tokea jambo hilo lilipofanyika, na washuhuda wakasema zilikuwa zimepita kama dakika 25 hivi.

Upesi Luteni Michael akampigia Bobby na kumjulisha yaliyotokea, naye akamwambia atumie utaalamu wake kufatilia Nora alikopelekwa kisha amwongoze ili aende huko. Bobby akakubali na kusema angewaambia na wengine ili wachangamke kwenda kumuunga mkono na kumpatia dada wa watu msaada. Mambo yalikuwa yanazidi kwenda vibaya upande wa Luteni Michael aisee. Alikuwa tu ametoka kuwapoteza watu muhimu sana ambao alifanya nao kazi kwa miaka mingi, na sasa ikiwa angempoteza mwanamke aliyekuwa ameanza kumpenda, asingejisamehe kamwe.

Akaondoa gari kwa kasi sana kuelekea upande ambao Nora angekuwepo.


★★★★


Ikiwa ni saa nne ya saa tano usiku sasa, Nora aliamka akihisi maumivu makali kichwani kwake. Alihisi pia kama yuko mwendoni, na kwa haraka akatambua alikuwa ndani ya gari. Alipoanza kuangalia ndani hapo, akatambua alikuwa katikati ya wanaume kadhaa walioketi siti za kando huku wakiongea mambo yasiyoeleweka kwake. Alihisi kizunguzungu kikali pia, akiwa kama ametoka kunywa pombe iliyomlewesha kupita maelezo.

Gari lilisimama hatimaye, naye Nora akahisi aliposhikwa na kuanza kutolewa nje. Maumivu kichwani yalikuwa makali, lakini akajitahidi kukisawazisha kidogo na kukaza meno yake ili atafute njia ya kutoroka. Wanaume wawili waliokuwa wamempa egamio ili atembee walikuwa wakisema kwamba wenyewe ndiyo wangeanza kwanza, tena kwa matundu yote mawili kwa wakati mmoja!

Nora akatambua kwamba hawa watu walikuwa na nia ya kumbaka, lakini kutokana na jinsi walivyokuwa wamemkamata ilionyesha walikuwa wamejipanga sana, hivyo labda nia yao nyingine baada ya kumfanyia ubaya huo ilikuwa ni kumuua. Wazo la kwamba huenda walikuwa ni Mess Makers ndiyo wanafanya hivi ili kulipa kisasi kwa ajili ya kifo cha mwenzao lilimwingia, naye akaona ilikuwa lazima atoroke haraka kwa sababu maisha yake yalikuwa hatarini.

Kwa kasi, akajinasua na kuwapiga wanaume hao wawili sehemu zao za siri na kuanza kujitahidi kukimbia. Wale wengine walikuwa wametangulia mbele kidogo, hivyo wakaanza kumkimbiza haraka na kufanikiwa kumshika. Alikuwa anajitahidi kurusha ngumi na mateke ili kujinasua kwa uwezo wake wote, lakini mmoja wa wanaume hao akampiga ngumi kwa nguvu sana tumboni na kumfanya Nora alegee mno. Alihisi kuishiwa nguvu, akaanguka akiwa analia kwa maumivu. Wanaume hao wakaanza kucheka na kuwatania wenzao waliopigwa na Nora, kisha wakamnyanyua mwanamke huyu juu na kuanza kumpeleka ndani ya jengo lililokuwa hapo.

Nora alijitahidi sana kujikaza kutokana na maumivu aliyohisi kichwani na tumboni, na kwa haraka akagundua kwamba hapo alikuwa ametekwa na wanaume saba. Walimwingiza ndani ya jengo hili ambalo lilikuwa ni ghorofa linalofanyiwa ujenzi, likiwa limefunikwa kwa neti ndefu za kijani kulizunguka kutokea juu mpaka chini kwa nje, na mbao za kupandia juu za mafundi zilikuwepo bado. Walimpeleka mpaka kwenye ghorofa ya nne, kukiwa na giza, lakini mwanga hafifu wa taa za kutokea jijini ukifanya vitu vionekane kwa mbali. Pembeni mwa jengo hili ulikuwa ni mnara mrefu wa mtandao wa Vodacom, hivyo kufikia ghorofa ya nne ya jengo hili ilikuwa ni kama wamefikia nusu ya mnara huo.

Wanaume wawili waliokuwa wamembeba Nora, wakamshusha na kumweka tu chini, kisha wakarudi nyuma kusimama na wenzao huku wakimwangalia kwa hila. Nora akawa akijivuta-vuta chini hapo kwa kurudi nyuma, akiwa na hofu kwa kadiri fulani. Mmoja wao akamsogelea na kuchuchumaa karibu yake, kisha akamshika kwenye goti la mguu, naye Nora akaikunja miguu yake na kujirudisha nyuma tena.

"Usigope mrembo... sisi hatutakuumiza. Tunataka tu kucheza," mwanaume huyo akasema.

"Mnataka nini? Nani amewatuma? Nyie ni Mess Makers?" Nora akauliza kwa sauti tetemeshi.

"Ndiyo... sisi ni Mess Makers..."

Mwanaume huyo akasema hivyo na kufanya wenzake wacheke.

"Wewe mtoto mzuri namna hii unafanya nini polisi? Hizo kazi ungewaachia wale wanawake wanene tu ndiyo huwa zinawafaa... wewe ungekuja kwangu tu..."

"Nisikilize. Mimi ni askari. Unajua mtapatwa na mambo mabaya mkinifanyia ujinga. Naomba mniachie..." Nora akasema kwa ujasiri.

"Unataka tukuachie? Sawa. Tutakuachia. Lakini lazima kwanza tucheze..."

Mwanaume huyo akamwambia hivyo na kumshika sehemu ya paja. Nora alipojirudi nyuma, akagusa kitu alichotambua kuwa ni mbao, naye akatulia kidogo.

"Hapa tuko wengi, na hauna ujanja. Ikiwa wewe ni mtu mwenye akili kama wanavyokutangaza, utajiachia kwetu tufanye yetu. Baada ya hapo labda ndiyo tutakuachia," mwanaume huyo akamwambia.

"Kweli?" Nora akauliza.

Wanaume wale wengine wakacheka.

"Ndiyo kweli kabisa..."

"Kwa hiyo... mnataka... niwape... nyie wote?" Nora akauliza.

"Vyovyote utakavyopenda mrembo..."

"Lakini mko wengi," Nora akasema.

Wote wakacheka sana.

"Basi tutafanya mmoja baada ya mwingine..."

"Lakini... kama ndiyo hicho mlichokuwa tu mnataka... si mngechukua slay queen huko, kwa nini mimi?" Nora akauliza kijanja.

"Sikia. Wewe hapa ulikuwa ni kufa tu. Lakini sisi tunakuonea huruma. Acha maswali, anza kuvua nguo. La sivyo tutakutupa kutokea hapa mpaka chini, umeelewa?"

Nora sasa akawa ametambua kuwa hawa walikuwa wametumwa na mtu fulani kumfanyia ubaya, siyo kwamba labda wao ndiyo walikuwa wana nia mbaya naye moja kwa moja.

"Nani amewatuma?" Nora akauliza.

"Hujanisikia? Nimekwambia..."

"Okay, okay, nimeelewa. Naombeni tu nwelewe kwamba nina maumivu maana mmenipiga kichwani na tumboni, kwa hiyo inabidi nijiandae," Nora akasema.

"Dah, hivi huyu demu yuko serious kweli?" mmoja wa wale wanaume akauliza.

Yule mwanaume aliyekuwa karibu na Nora akamgeukia mwenzake ili atoe jibu, na hapo hapo Nora akavuta ubao ule na kumtandika nao sehemu ya mgongoni. Mwanaume huyo akatoa sauti ya maumivu kidogo na kuangukia pembeni, naye Nora akajitahidi kusimama huku akiwa ameushika ubao ule. Wale sita wengine wakaanza kumzunguka polepole huku yeye akirudi kinyume-nyume, akiwaonyeshea ubao kuwa yeyote akimsogelea atampiga.

"Bado una kiburi kumbe?" mmoja akasema.

"Kaeni mbali nami. Nitawaua wote," Nora akasema kwa ujasiri.

"Basi anza na mimi..." mwingine akasema na kumfata kwa kasi.

Nora akampiga na ubao huo kwa nguvu begani, na mwingine alipomsogelea akampiga tumboni. Hapo hapo mwingine akawa amemshika kwa nguvu, nao wakaanza kurudi ovyo ovyo nyuma kwa sababu ya Nora kujaribu kujinasua. Mwanaume huyo akamsukuma kwa nguvu mpaka sehemu ya ukutani na kufanya Nora ajibamize uso wake kwa nguvu, naye akaanguka chini huku wanaume hao wakimcheka.

"Tunapenda sana wanawake wanaojua kupambana..." mmoja wao akasema.

Yule mwanaume aliyekuwa amepigwa kwa ubao mara ya kwanza akawasukuma wenzake pembeni ili awe wa kwanza kumtendea Nora vibaya kimwili, na wenzake wakawa wamemzingira Nora ili asiponyoke. Mwanaume huyo akatoa bastola kutoka nyuma ya kiuno chake na kumwonyeshea Nora, kisha akampa mwenzake na kutoa ishara kwa wengine kwamba wamshikilie Nora ili amwingie kwa nguvu kimwili.

Wanaume watano wakamfata Nora, wakamshika na kumlaza chini kwa nguvu, wawili wakiwa wameishika mikono yake na wengine kuisambaza miguu yake. Mmoja wao alikuwa akiivuta suruali yake Nora ili kuitoa yote, huku mwanamke huyu akipiga kelele za kuomba msaada na machozi yakimtoka. Yule aliyekabidhiwa bastola akatoa kitambaa na kwenda kumfunika mdomo kwa nguvu, kisha akakifunga nyuma ya shingo yake. Nora alikuwa akilia kwa hisia sana, na hatimaye wanaume wale wakafanikiwa kuitoa suruali yake yote, wakimwacha na chupi nyeupe tu.

"Wow! Mtoto msafi wewe! Yaani unanukia kila kona siyo kama yale manyanya ya traffic yanayonuka mijasho tu," mwanaume huyo akasema huku akifungua suruali yake, na wenzake wakawa wanacheka.

Mwanaume mmoja akataka kuitoa na chupi ya Nora, lakini huyu aliyetaka kuanza kumwingia akamzuia.

"Nataka niitoe mwenyewe, wewe shika mwili huo asifurukute," mwanaume huyo akasema.

Nora akawa analia tu huku anatikisa kichwa kumwonyesha mwanaume huyo kwamba asifanye hivyo, naye jamaa akawa amemaliza kuitoa suruali yake na kuvua boxer pia. Akawa anaitingisha-tingisha kichokozi mashine yake iliyosimama kumwelekea Nora, na wenzake wakawa wanacheka.

"Ila bro, faster. Hatuna muda mwingi wa kupoteza," mmoja wa wale wanaume akamwambia.

Jamaa akaanza kumkaribia Nora ili afanye yake, pale kishindo fulani kilipotokea sehemu ya nje upande ambao ulikuwa na mbao za mafundi za kupanda juu. Wote waliangalia upande huo, lakini ni upande ambao walikuwa wameupa visogo ndiyo akatokea mtu fulani aliyeingia kwa kasi sana na kupita katikati yao mpaka sehemu ya pembeni, akijiviringisha chini na kunyanyuka juu; akiwa amesimama kwa kuwapa mgongo.

Wote walishtushwa na hilo, lakini kilichofuata kuwashtua hata zaidi ni sauti ya kilio cha maumivu kutoka kwa yule jamaa aliyetaka kumwingia Nora kinguvu. Walipomwangalia, wakakuta hana uume! Yaani ulikuwa umekatwa kabisa na kubakiza damu tu zilizoruka-ruka kama maji kwenye bomba lililopasuka. Mtu huyo aliyeingia hapo ghafla alikuwa amepita na uume wa jamaa kwa kutumia kisu kwa kasi aliyoingia nayo, na wanaume wale wengine wakamwachia Nora na kubaki kumwangalia mwenzao akilia kwa maumivu sana huku akigaagaa chini.

Nora alijivuta nyuma na kuegamia ukuta, akimwangalia mtu huyo aliyekuwa amesimama huko mbele. Alionekana kuvaa nguo nyeusi mwili mzima na kificha uso kichwani kilichoacha sehemu ndogo tu ya mdomo wake. Kwa haraka akawa amemtambua mtu huyo, kwamba ndiye yule ambaye alikuja na wenzake kumwokoa Kevin Dass usiku ule walipofanikiwa kumkamata kule Mwanza. Wale jamaa wengine wakajiweka tayari kimapambano, huku yule aliyekuwa amekabidhiwa bastola na huyu aliyekatwa uume akiitoa na kumnyooshea mgeni aliyeingia.

"Unasubiri nini? Mpige risasi!"

Mmoja wao akasema hivyo kwa sauti, na hapo hapo jamaa akaanza kufyatua risasi kuelekea sehemu za mgongo na hata miguu ya mtu huyo. Alipiga risasi kama 9 hivi, kisha bastola ikawa tupu. Wanaume wote walibaki kushangaa tu mtu huyo akiwa amesimama tuli wakati alikuwa ametoka kumiminiwa risasi mwilini, lakini Nora alielewa wazi kwamba nguo aliyovaa ilizizuia risasi hizo. Kisha mtu huyo ambaye hakufahamika kwa yeyote ndani hapo, akakitupa kisu alichokuwa amekishika, naye akajisawazisha na kuwatazama kwa utayari.

Wanaume wale wakaambiana kwa kuamrishana kuwa wamfate na kummaliza kwa mikono yao wenyewe, kwa kuwa alikuwa peke yake, hivyo ikaonekana kwamba wangemshinda nguvu. Kichwa kichwa tu wakaanza kumfata kwa kasi ili wamshambulie, lakini akawakwepa kwa mitindo ya sarakasi na kuingia katikati yao, kisha kutokea mpaka sehemu ambayo Nora alikuwa amejiegesha. Wanaume wale waligeuka nyuma, na mmoja akamwahi mtu huyo ili ampige, lakini akaikunja-kunja mikono yake na kuivuta kwa nguvu sana pande mbili tofauti, kitu kilichofanya aivunje-vunje mifupa yake kuanzia mikononi mpaka mabegani. Jamaa akatoa kilio cha maumivu kwa kulemazwa mikono sasa, na mtu huyo akamsukuma pembeni kama mzigo wa uchafu.

Wengine wawili wakamrukia, lakini mtu huyo alikuwa na njia fulani ya kukwepa ambayo ilimstaajabisha sana Nora. Akavipigisha vichwa vyao kwa nguvu sana uso kwa uso na kufanya wavunjane pua, na wakati huo huo mwingine aliyemkaribia akamtandika teke shingoni kwa kuruka sarakasi ya nyuma, na alipotua akaisambaza miguu yake chini kwa msamba na kuizungusha ili amkate mtama jamaa mwingine.

Aliwachangamkia kwa kasi sana wanaume hao na kuwapiga kwa kuwachanganya mno, na mmoja wao akakiokota kisu kile ambacho mtu huyo alikitupa chini, kisha akamfata ili amchome lakini akaambulia kuzungushiwa mkono wake yeye mwenyewe na kujichoma mdomoni. Wengine hawakuwa hata na muda wa kushangaa, na tayari mtu huyo akawa amemchana sehemu ya kitovu mwanaume mwingine na kufanya utumbo wake mwingi umwagike chini.

Nora alihofishwa kwa kiasi kikubwa na mauaji hayo yaliyotokea mbele yake. Wanaume wawili wakamkamata mtu huyo na kumng'ang'ania kwa nguvu, kisha yule aliyebaki akaanza kumfata ili amwangamize, lakini mtu huyu akainyanyua miguu yake juu na kudunda kwenye kichwa cha jamaa aliyekuwa anamfata na kujibinulia nyuma ya wale waliokuwa wamemshikilia, nao wakajitoa kwake kwa kukosa mhimili mzuri.

Walipojisawazisha tu, mmoja akashtukia anapigwa ngumi ya tumboni, lakini maumivu yalikuwa ni makali sana kwa sababu mkono wa mtu huyo uliompiga ulikuwa bado na kisu kile, kwa hiyo kiliingizwa mpaka ndani ya tumbo lake kama vile kupigilia msumari wote ndani ya ukuta. Akaanguka chini akiwa amejishika tumbo bila kutoa sauti yoyote kwa kuhisi maumivu makali yaliyofanya koo yake ikaze, na yule wa pembeni akamrukia mtu huyu ili ampige kichwani kwa uchuma wa bastola ile tupu aliyoiokota chini, lakini mtu huyu akamkwepa na hapo hapo kukishika kichwa chake na taya kwa kuizungushia mikono yake kinyume, halafu akaivuta mikono kwa nguvu na kufanya shingo ya jamaa inyongwe kwa njia iliyofanya uso wake ugeukie mpaka mgongoni!

Mwanaume huyo akadondoka chini na kuanza kushtuka-shtuka mwilini sana, naye Nora akawa akisikia jinsi mtu huyo aliyemnyonga jamaa alivyopumua kwa nguvu.

Kisha mtu huyu akamwangalia yule jamaa mwingine aliyebaki, ambaye alikuwa kasimama tu akionekana kuogopa. Akaanza kurudi nyuma na kugeuka ili akimbilie sehemu iliyokuwa kwa ajili ya mlango ili atoroke, lakini mtu huyu akaokota bastola ile na kumponda kwa nguvu sana nyuma ya kichwa chake, kitu kilichofanya jamaa aweweseke na kujigonga ukutani. Mtu huyo akamfata pale chini, na bila kukawia akamkanyaga nyuma ya shingo na kuikandamiza kwa nguvu sana mpaka ulimi wote wa mwanaume huyo ukatoka nje ya mdomo wake!

Nora alikuwa ameghafilika haswa. Alipatwa na mshtuko mkubwa sana kiasi kwamba alikuwa ametulia tuli tu kama vile hayuko hapo. Mtu huyo akageukia upande wa Nora, naye Nora akatambua kwamba alikuwa anawaangalia wanaume wale waliolala pale chini. Kati ya wanaume wote saba, ni wawili tu ndiyo bado walikuwa hai; yule aliyekatwa uume, na yule ambaye alivunjwa mikono mapema kabisa. Mtu huyo akaanza kutembea kumwelekea yule aliyemvuja mikono, naye jamaa alipoona anafuatwa, aliingiwa na nguvu fulani mpya iliyomfanya anyanyuke hivyo hivyo huku mikono yake ikiwa imelegea kama mikono ya mashati ya Brother-K, naye akawa anarudi kinyume-nyume kwa kuogopa sana. Mtu huyo akawa anamfata taratibu tu, akijua kwamba woga wa mwanaume huyo ulimaanisha kifo chake mwenyewe kwa sababu alikuwa anarudi nyuma bila kutambua kwamba alielekea sehemu yenye uwazi mwishoni mwa chumba hicho, na kufikia hapo mwishoni jamaa akaanguka mpaka kule chini bila hata kusukumwa!

Hiyo ikamwacha mzee wa uume-mkato pale chini, akiwa anaugulia maumivu tu huku damu nyingi ikiwa imemtoka, na mtu huyo akamfata mpaka hapo na kuchuchumaa karibu yake. Jamaa akaomba apelekwe hospitali eti, akisema yeye hana makosa kabisa. Mtu huyu akatoa kitu fulani kutoka kwenye nguo aliyovaa, kisha akamziba pua jamaa kwa vidole na kumwekea kitu hicho mdomoni mwake. Akaiachia pua yake, naye jamaa akaanza kutetemeka sana huku akiwa kama anataka kukohoa lakini anashindwa. Ilikuwa ni sumu ndogo tu kama kidonge ambayo ilienda kukatakata ogani ndani ya mwili wa jamaa, kifo cha taratibu chenye maumivu ambacho angekisikilizia vizuri kabisa.

Mtu huyo akasimama na kuanza kumfata Nora mpaka alipokaa. Nora alikuwa hata hajatoa kitambaa kile ambacho wale wanaume walitumia kuufunga mdomo wake ijapokuwa mikono yake haikuwa imefungwa. Yaani ni kama nguvu zilikuwa zimemwishia kutokana na yote yaliyokuwa yamefanyika kufikia sasa, naye akabaki kumwangalia tu mtu huyo kama anasubiri zamu yake ya kuuawa ifuate. Mtu huyu akachuchumaa karibu na Nora, akionekana kama anamwangalia.

Kwa ukaribu huo, Nora aliweza kuiona vyema sehemu ya usoni ya mask aliyoivaa, ikiwa kama nguo fulani ngumu sana yenye kitu kama vioo vya miwani nyeusi (tinted), na ni sehemu ya mdomo wake tu ndiyo iliyokuwa wazi, lakini kuanzia kidevuni kuelekea chini palifunikwa vyema kama mwili wake wote. Mdomo wa mtu huyu ulipakwa rangi nyeusi, hivyo haingekuwa rahisi kuukariri, lakini kama ni kitu kimoja alichotambua Nora ni kwamba mtu huyu alikuwa mweupe. Ulikuwa weupe wa pembeni kuzunguka midomo yake, ulioonekana vizuri gizani hapo na kumfanya Nora adhani huenda ni mzungu, lakini kihalisi, ilikuwa ni Lexi.

Kishindo alichokuwa ameingia nacho hapo kilikuwa ni balaa!

Alipomtazama Nora, aliona jinsi alivyoogopa ingawa alijikaza sana kuonyesha ujasiri wake, naye akamsogelea usoni na kupeleka mikono yake karibu na uso wake. Nora aligeuzia shingo pembeni akifumba macho yake kwa nguvu sana kwa kudhani angeumizwa, lakini Lexi akakishika kitambaa kilichomfunga mdomoni na kukifungua kutokea nyuma ya shingo yake. Alipohisi kitambaa kimetolewa, Nora akageuka na kumwangalia mtu huyu ambaye hangeweza kutambua ni nani. Lexi akaifuata suruali ambayo alijua ni ya Nora, kisha akamrushia mapajani mwake.

Nora alishindwa kuelewa nini kilikuwa kinaendelea. Alijua wazi kuwa mtu huyo mbele yake ni mmoja wa watu waliojiita Mess Makers, na bila shaka ni huyu huyu ndiye aliyempiga risasi nne mara ya kwanza kule Mwanza lakini akamwacha tu. Leo tena, kwa kufikiri labda wanaume wale saba waliomteka waliagizwa na Mess Makers ili wafanye hayo, isingepatana na akili kwamba mmoja wao angeamua kuwaua wote ili tena amwokoe yeye. Kama siyo Mess Makers waliowatuma watu hao, basi angekuwa ni nani? Na kwa nini mmoja wao ahatarishe uhai wake ili tu kumsaidia yeye? Mambo mengi yalikuwa yanachanganya sana akili yake.

Baada ya kuwa amemrushia nguo hiyo, Lexi akaanza kuelekea sehemu ya mlangoni taratibu, lakini Nora akamwita.

"Hey... subiri..."

Lexi akasimama kwanza. Kisha akamgeukia na kumwangalia alipoketi pale chini, naye Nora akajitahidi kusimama huku bado akihisi maumivu mengi kichwani kwake. Akawa anamwangalia mtu huyo mbele yake huku akipumua kwa njia ya uchovu fulani hivi.

"We... we ni nani?"

Nora akauliza swali hilo, bila kutambua kwamba jibu tayari alilijua.

Lexi akaendelea tu kumwangalia, nao wote wakasikia sauti za gari zikifika nje ya jengo hilo. Nora kwa haraka alijua bila shaka hao walikuwa aidha ni maaskari au Luteni Michael, naye akabaki kumtazama tu mtu aliyekuwa amesimama mbele yake kama vile hajawasikia wanaokuja. Hatua za haraka za kupanda ngazi zilisikika kutokea chini, naye Lexi akaacha kumwangalia Nora na kuanza kuelekea sehemu ile ya wazi kuelekea mbao za mafundi za kupanda. Akaruka na kuanza kupanda moja akienda juu, huku Nora akiachwa na maswali mengi kichwani.

Kutokea nje ya mwingilio wa chumba hicho, sauti ya Luteni Michael ilisikika ikisema kwamba kwa wale waliokuwa ndani hapo, wajisalimishe kwa kuwa walikuwa wamewazingira. Nora akajikaza na kuita kwa sauti, kisha kuwaambia waingie ili kumsaidia haraka. Alitangulia kuingia Luteni Michael, naye alipigwa na butwaa baada ya kuiona miili ya wanaume wale pale chini. Wakaingia wanajeshi wa timu yake pia, Alex, Mario, Hussein na Bobby, na wao vile vile wakashangazwa na waliyoona.

Luteni Michael akamwangalia Nora na kumwona akiwa bila suruali kwa chini, naye akamfata pale upesi na kumuuliza nini kilitokea. Nora akamwambia kichwa kilimuuma sana na tumbo pia, hivyo akamwomba amsaidie kuelekea hospitali kwanza na mambo mengine angemweleza baadae. Luteni Michael akatii na upesi kumbeba Nora mikononi mwake, kisha akawaamuru Bobby na Alex wabaki na kuchunguza mambo hapo, halafu wawatafute mapolisi ili waje washughulike na masalio.

Luteni Michael akiwa amembeba Nora, akifuatwa na Mario pamoja na Hussein, wakaanza kuelekea chini upesi ili kumwahisha ACP hospitalini.



Lexi alikuwa amepanda kuelekea juu mpaka ghorofa ya sita, kisha akapita ndani ya jengo na kurukia upande wa pili wa mbao za mafundi, na kuanza kushuka kuelekea chini wakati ule ambao Luteni Michael ndiyo alikuwa amefika ndani ya chumba kile alichomwacha Nora. Akafanikiwa kurukia upande mwingine wa ukuta uliozungukia jengo hilo, naye akawa katikati ya kokoto nyingi zilizozagaa chini hapo na kujibanza ukutani ili ashushe pumzi kidogo. Lakini alipotazama mnara ule wa Vodacom, akaona kitu fulani kule juu kilichovuta umakini wake. Akajitoa kwenye ukuta huo na kusimama vizuri zaidi ili aangalie kitu hicho, naye akatambua ilikuwa ni mtu.

Kulikuwa na mtu juu ya mnara huo, akiwa amening'inia kwa njia fulani ya kizembe, lakini Lexi akatambua kwamba alikuwa amejishikiza vizuri, na alikuwa anamwangalia. Hakuuona uso wake, lakini kwa haraka Lexi akajua mtu huyo ndiyo yule aliyetokea siku ile ghafla na kumuua Oscar, yaani silaha ya Luteni Jenerali Weisiko. Aliona kwamba sasa huyu mtu hatari sana alikuwa anamfatilia aidha Nora au yeye, lakini sanasana Nora kwa sababu kwa yeye Lexi haingekuwa rahisi kujua njia zake. Alitamani kumfata hapo hapo juu, lakini akafikiria hali zilizowazunguka wakati huu, hivyo akaamua kuachana naye tu na kujiahidi kwamba wangekutana tu tena, na kwa wakati huo hangemwacha salama.

Lexi akaondoka sehemu hiyo upesi kuelekea upande mwingine, na "silaha" huyo wa Weisiko akajisawazisha vizuri hapo juu na kumsindikiza tu Lexi kwa macho, akiwa ameona vizuri sana kila kitu kilichotokea kwenye jengo lile tokea Nora alipoletwa na wanaume wale mpaka Lexi alipowaua, naye akashuka kutoka juu ya mnara huo kwa kamba ndefu na kutokomea kusikojulikana.



★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★

WHATSAPP +255 787 604 893
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA

★★★★★★★★★★★★★★★★★


Nora alifikishwa hospitalini haraka sana kupatiwa huduma za kitiba. Alivaa suruali yake wakati wakiwa mwendoni, hivyo kufikia sasa hakuwa ameachwa mtupu kwa chini. Matabibu walimsaidia, na baada ya muda fulani daktari akamjulisha Luteni Michael kwamba Nora angekuwa sawa tu kwa kuwa walifanikiwa kuzuia damu isivujie ndani ya tumbo lake na kumpa dawa ambazo zingetuliza maumivu ya kichwa chake. Luteni Michael akaomba kumwona ili waongee, lakini daktari akamwambia kuwa kwa wakati huo Nora alikuwa amekwishalala, hivyo ingempasa asubiri mpaka kesho ili kuongea naye.

Baada ya daktari kuwaacha, Mario akamwambia Luteni Michael kwamba aliwasiliana na Bobby kutokea kule walipomwacha na Alex, naye alikuwa amesema miili ile ya wanaume waliouawa jengoni pale iliondolewa hatimaye. Luteni Michael akamwambia Mario amwambie Bobby ahakikishe kwamba watu wa vyombo vya habari hawahusishwi na tukio hilo kwa sababu hakutaka gumzo mapema sana wakati tu walikuwa wametoka kwenye msiba. Kama ni taarifa ambayo maaskari walipaswa kutangaza ilikuwa ni vifo vya wanaume hao, na lawama waielekeze kwa Mess Makers kama kawaida yao, lakini masuala ya ACP Nora kutekwa hakutaka yasambazwe kokote.

Luteni Michael alijua vizuri kivumbi ambacho kingetokea endapo Jenerali Jacob angesikia kuwa binti yake aliwekwa hatarini, kwa kuwa Michael aliahidi kumlinda akiwa chini ya uongozi wa Kanali Oswald pia. Lakini ukweli wa jambo hilo haungeweza kufichwa kwa Jenerali Jacob kama walivyolenga, kwa sababu alizipata taarifa hizo kutoka kwa Luteni Jenerali Weisiko, ambaye pia alikuwa amezipata kutoka kwa "silaha" wake yule aliyeona kila kitu kilichotokea akiwa juu ya mnara.

Luteni Michael akawaambia Mario na Hussein wabaki hapo hospitalini ili kumpa ulinzi Nora mpaka atakapoamka, naye angeondoka kwenda kufanya uchunguzi wa kina pamoja na Bobby. Wanaume hao wakatii na kubaki hapo, wakimsindikiza Luteni kwa macho alipoondoka hospitalini.


★★★★


Asubuhi iliyofuata, tayari vyombo kadhaa vya habari vilikuwa vimeshatangaza kuhusu tukio la usiku uliopita kwenye habari muhimu za asubuhi. Kwa sababu hakukuwa na mashuhuda wengine wa tukio, suala hilo lilielezewa na mapolisi tu, waliosema kwamba wanaume hao saba walikuwa ni wajenzi wa jengo hilo wenye familia bila shaka, lakini Mess Makers wakawaua bila sababu yoyote kwa kutaka jambo fulani kutoka kwenye jengo hilo. Ukweli ukafichwa kuhusiana na ACP Nora kutekwa na kukaribia kuuawa.

Nora akaamka hatimaye asubuhi hii kwenye mida ya saa 3, naye akatambua kuwa bado alikuwa kwenye kitanda cha hospitali. Alikuwa kwenye chumba cha peke yake, naye akageuza shingo yake upande mwingine na kumwona Mario akiwa ameketi kwenye kiti huku ameinamisha kichwa chake, na mikono kuikunjia kifuani. Alipomtazama vizuri, akatambua alikuwa amesinzia, mara kwa mara kichwa chake kikikaribia kudondokea mbele. Akamwonea huruma kiasi kwa sababu alijua hakulala usiku mzima na hivyo bila shaka alikuwa amechoka. Alipojishika kichwani, alitambua kuna plasta kubwa iliyogundishwa pembezoni mwa paji la uso wake, naye akaanza kutafakari mambo yote yaliyotokea usiku wa jana.

Picha kamili ya mauaji ya wanaume wale ilimrudia. Kihalisi, aliwaza kwamba hata yeye angewaua watu hao kwa mambo waliyotaka kumfanyia, lakini hakuwaza kamwe kwamba kuna mtu ambaye angewaua kwa njia ile iliyomwogopesha sana. Lakini tena mtu huyo alikuwa ni mmoja wa Mess Makers. Swali kuu kichwani kwake lilikuwa ni nini kilichomfanya mtu huyo amsaidie wakati yeye Nora ni sehemu kubwa kwenye mipango ya kutaka kulikamata kundi lao na kuliangamiza. Alipatwa na hisia fulani isiyoeleweka kila mara alipokumbukia jinsi mtu huyo alivyomtolea kitambaa mdomoni na kumrushia suruali ili avae; alikuwa anataka kuthibitisha nini? Kwamba Mess Makers si watu wabaya? Haikuingia akilini hata kidogo.

Alipohisi haja ndogo, Nora akajinyanyua taratibu na kuketi. Alihisi maumivu ya kichwa kwa mbali, naye akatambua kwamba alifungwa kwa bendeji tumboni. Nguo aliyokuwa amevalishwa kwa sasa ilikuwa "gauni ya mgonjwa," naye akashuka kutoka kitandani na kujaribu kusimama chini, lakini kizunguzungu kikamwangushia kitandani tena. Akachekea kwa chini kidogo, kisha akajitahidi kukikaza kichwa ili kizunguzungu kisimvae tena, lakini ni hapa ndiyo Mario akashtuka kutoka kwenye usingizi wake wa kuonja.

"ACP... unafanya nini, hutakiwi...."

Mario akasema hivyo na kwenda kumshika alipokuwa anajitahidi kusimama.

"Hutakiwi kutoka kitandani ACP..."

"Mario, sijikojoleagi kitandani. Nisaidie nielekee toilet," Nora akasema.

Mario akatii na kumpa egamio ili waelekee kwa choo, akimuuliza kama anahisi maumivu mengi, lakini Nora akakanusha. Akafanikiwa kumpeleka kupata haja ndogo, kisha akamrudisha tena kwenye chumba chake na kumwacha ili akamwambie daktari kwamba mgonjwa wake kaamka.

Nora alipouliza wengine walikuwa wapi baada ya Mario kurudi, akamwambia walikuwa wakiendelea na kazi, na ni yeye pamoja na Hussein ndiyo walioachwa kumlinda, lakini Hussein alitoka kidogo kwenda kufata vyakula kwa ajili yake. Daktari akafika kumwangalia Nora, naye akasema angehitaji kuendelea kuwa hospitalini hapo kwa siku mbili zaidi, lakini Nora akakataa. Akasisitiza kwamba alitakiwa kurudi kufanya kazi kwa sababu hakujisikia kuwa mgonjwa kama daktari alivyosema alihitaji uangalizi.

Daktari akamwambia kwamba akiondoka kabla ya wakati huenda akaisababishia afya yake madhara, lakini Nora akasema kama ni hivyo wampe tu dawa za kwenda nazo hata kama atazitumia mwaka mzima, lakini hangekaa hospitali kwa siku mbili zaidi. Mario naye akajaribu kumsisitiza asikilize ushauri wa daktari, lakini Nora akagoma. Ni hapa ndipo Hussein akaingia humo, huku nyuma akifuatwa na Luteni Michael.

Daktari akawaeleza hali, naye Luteni Michael akamshukuru na kumwomba aende tu ili aongee na mgonjwa.

"Jamani, acha kuniita mgonjwa, naonekana kama naumwa?" Nora akamwambia Luteni Michael wakati daktari alipoanza kuondoka.

"ACP... unatakiwa kumsikiliza daktari. Kama afya yako hairuhusu kuondo...."

"Luteni niko sawa. Hayo ni maneno ya doctor tu lakini najua niko sawa. Kichwa kitapona ni pain killer tu na hakuna shida tena. Siwezi kukaa me hapa kwa siku mbili zaidi nimebung'aa tu," Nora akasema kwa uhakika.

"Kubung'aa ndiyo nini?" Mario akauliza.

"Kukodoa macho. Angalia kwenye dictionary utalikuta hilo neno," Hussein akamtania.

"ACP... nimeshapoteza watu muhimu kwenye suala hili, na wewe ni muhimu zaidi. Sitahatarisha uzima wako...."

"Hauhatarishi chochote Luteni. Huu ni mwili wangu. Please, please, niondoeni kwenye hii sehemu. Tafadhali," Nora akasema.

"Haupendi hospitali eeh?" Hussein akamuuliza.

"Sitaki tu kukaa hapa," Nora akajibu.

"Okay. Basi tutaongea na madaktari wakuachie mapema, lakini tunahitaji kuhakikisha uko vizuri sana," Luteni Michael akasema.

"Niko vizuri Luteni, na nikitoka hapa nataka tuendelee na kazi," Nora akasema.

Luteni Michael akaangaliana na vijana wake tu, kwa kuwa ilionekana hakukuwa na cha kumzuia Nora kufanya alichotaka. Hussein akaanza kufungua vyakula mbalimbali na kuweka chai pia ili ampatie ale.

"Tunaweza kuongelea kuhusu ni nini kilitokea jana usiku?" Luteni Michael akamuuliza.

"Yah. Aam... nilikuacha pale muda ule...."

"Yeah nakumbuka..." Luteni Michael akamalizia kimkato.

"Nilipofika tu... nje ya geti... akaja mwanaume mmoja... mmoja wao hapo kabla sijajua ni nani na... alikuwa anaomba nishushe kioo kama anataka msaada. Nilipomsikiliza akaniambia kwamba kuna mtoto wa rafiki yake anapigwa vibaya nyumbani siyo mbali na hapo... kwamba alijua mi ni askari halafu.... Nikashuka ili nianze kumfata, ndiyo hapo hapo gari likaja mbele yetu kwa kasi. Sikujua kilichoendelea tena ghafla yaani...."

"Nafikiri kulikuwa na mwingine aliyekuja nyuma yako akakupiga kichwani," Luteni Michael akasema.

"Ndiyo, inawezekana. Niliamkia jengoni kule. Walikuwa wanataka kunibaka, kisha waniue. Lakini..." Nora akaishia hapo tu na kuonekana anatafakari jambo fulani.

"Nini kikafuata?" Luteni Michael akauliza.

"Kuna mtu aliingia... akaanza kupigana nao," Nora akasema.

"Nani?" akauliza Hussein.

"Sifahamu. Sikuweza kuuona uso wake," Nora akajibu.

"Kwa hiyo... alifika tu paap... akapigana nao na kuwaua wale wote saba? Yeye mwenyewe?" akauliza Hussein.

"Alionekanaje? Alikuwa mwanaume au mwanamke? Alivaa vipi? Na alipigana nao vipi?" Luteni Michael akauliza.

"Kila kitu kilitokea haraka sana na... kulikuwa na giza kwa hiyo... sikuona mambo mengi vizuri," Nora akadanganya.

"Atakuwa nani sasa? Jamaa amewaua vibaya sana wale wachizi... tena yaani kama vile siyo mtu wa nchi hii. Au labda ni yule aliyemuua Oscar?" akauliza Mario.

"Labda ni Super Mario," akasema Hussein kiutani.

"Hivi we hauwezi kuacha kuniandama? Unanionaga kama sijaenda shule eti?" Mario akamwambia Hussein.

Wawili hawa wakaanza kubishana kama kawaida yao. Luteni Michael akawa anamwangalia tu Nora kiudadisi, akihisi kwamba kuna jambo alificha.

"Hussein hiyo chai itapoa. Em' mpe dada basi," akasema Mario.

"Mario, Hussein, naombeni mtupishe mara moja," Luteni Michael akawaambia.

Wawili hao wakatoka ndani ya chumba hicho baada ya Hussein kumsogezea Nora kiamsha kinywa karibu.

"ACP... nini kilitokea? Niambie tafadhali. Nahisi ni kama hausemi kila kitu," Luteni Michael akamsemesha.

"Nimekwambia kila kitu... ingawa ni kifupi lakini, ndiyo mambo yalivyokuwa," Nora akasema.

"Kwa hiyo, ni kama hatuna jambo lingine la kutoa kutokana na haya yote? Umetekwa jana ACP.... hatuwezi kubung'aa kama unavyosema, ni lazima tujue kila kitu ili tuyamalize matatizo haya haraka. Ikiwa utaficha jambo fulani haitasaidia... na kiukweli ni kama tumepoteza mwelekeo ACP... Usifiche lolote. Sisi ni timu. Sema kila kitu tusaidiane," Luteni akamwomba.

"Unataka kusikia nini? Kwamba niliuona uso wake? Sikuuona Luteni... aaghh..." Nora akasema kimkazo na kufanya kichwa chake kiume.

"Okay, okay, basi inatosha usi... usijiumize. Samahani," Luteni Michael akamwambia kwa kujali.

"Nahisi njaa Luteni. Wacha nile kwanza, then nikitoka tutajadili mambo kwa kina. Sawa?" Nora akaomba.

"Okay. Haina shida. Sisi tutakuwa hapo nje. Pata chai kwanza," Luteni akasema.

Luteni Michael akamwangalia kwa sekunde kadhaa, kisha akatoka ndani ya chumba hicho pia. Nora akashusha pumzi na kufumba macho yake, naye akaegamia tu mto na kuanza kutafakari vitu tena. Lakini akaamua kutokazika sana kimawazo, na njia nzuri ya kurejesha nguvu ili awahi kuondoka ingekuwa ni kula, hivyo akavuta chakula alichowekewa na kuanza kula taratibu.


★★★★


Lexi alikuwa ameshaondoka Dar es Salaam na kwenda mpaka kule kwenye nyumba yao ya maficho, kule walikopaita "chini." Alifika na kwenda mpaka kwa Kendrick Jabari, ambaye alikuwa ameketi tu kwenye kiti chake huku akivuta sigara, na pembeni alikuwepo LaKeisha, Mensah, Victor, na Kevin.

"Lexi!"

LaKeisha akaita kwa shauku baada ya kumwona, lakini Lexi akafika tu hapo na moja kwa moja kumfata Kendrick, kisha akaikwapua sigara yake na kuirusha pembeni kwa hasira. Wengine wakawa wanamwangalia kimaswali sana wasielewe nini kilikuwa kinaendelea mpaka Lexi amzingue "boss" wao kiaina, lakini Kendrick akawa anaangalia tu chini kiutilivu.

"Lexi... nini unafanya?" Mensah akauliza.

"Saba? Really uncle? Ni akili mbovu kiasi gani iliyokufanya ufikie uamuzi huo?" Lexi akamuuliza Kendrick kwa hasira.

Wengine wakawa hawaelewi alichomaanisha na kubaki kuangaliana tu.

"Lexi... nini sweety? Nini... kinaendelea?" LaKeisha akauliza.

Lexi akabaki tu kumtazama Kendrick. Mwanaume huyu akashusha pumzi na kumtazama usoni "binti yake," naye aliona hasira tupu tu machoni mwake.

"Ulijuaje?" Kendrick akauliza kiutulivu.

"Nina njia zangu," Lexi akasema.

Kendrick akatikisa kichwa na kusema, "Ni Torres."

"Uncle, what you did was wrong. Hivyo siyo tunavyo-roll," Lexi akasema.

"Ku-roll kivipi?" Kendrick akauliza.

"Unawezaje kuagiza wanaume saba wamkamate mwanamke defenseless wam...."

"Na wewe unawezaje kuingilia mipango yangu? Nani amekuruhusu?" Kendrick akamuuliza kiukali.

Wengine wote wakabaki kushangaa.

"Sikuhitaji ruhusa ya mtu yeyote kufanya jambo lililo sahihi," Lexi akasema kiukali.

"Sahihi? Kuwaua wanaume saba ni sahihi?" Kendrick akauliza na kusimama.

"Boss, Lexi... what's going on?" Mensah akauliza

"Ni ndoto gani ya kitandani iliyokufanya ukaingilia mipango yangu, huh?" Kendrick akauliza kwa hasira.

"Kama kumbaka mwanamke asiye na hatia na kumuua...."

"Asiye na hatia? Asiye na hatia? Huyo mwanamke ndiyo sababu hatuna Oscar tena hapa. Umewaua watu ambao wangelimaliza tatizo hili ili iweje? Aje kufanya tusiwe na Keisha, au Mensah, au Victor hapa tena? Eeh? Una matatizo gani?"

"Siyo yeye aliyemuua Oscar..."

"I DON'T CARE!"

"I DO! Why? Kwa sababu sisi hatutakiwi kuwa kama wao. Fanya mambo namna hiyo unakuwa hauna utofauti na Jacob wala Weisiko!" Lexi akasema kwa hasira.

"Unasemaje?"

Kendrick akauliza kiukali na kuanza kumfata Lexi.

"Boss, boss, boss, boss, boss...." Mensah na Victor wakamwahi ili asimfanyie jambo baya Lexi.

"Mwacheni," Lexi akasema.

Mensah na Victor walikuwa katikati yao kumzuia Kendrick kumfata Lexi.

"Nimesema mpisheni!" Lexi akawaamuru.

Mensah akapisha taratibu, naye Victor akasogea pembeni pia. LaKeisha alikuwa ameingiwa na hofu, huku Kevin akiwaangalia kwa umakini tu.

"Njoo," Lexi akamwita Kendrick.

Kendrick akabaki amesimama tu, akitambua kwamba alikuwa ameziruhusu hasira zake zimwongoze vibaya na kutishia kumpiga Lexi.

"Fanya chochote unachotaka juu yangu, lakini kamwe usiumize watu wasio na hatia. Yote tunayofanya, tunayafanya tukiwa na lengo moja... la pamoja, lakini hili ulilofanya lilikuwa ni tendo lenye ubinafsi... wala siyo kwa ajili ya Oscar. Ninajua ulifanya hivyo ili kumkomoa Jacob kwa sababu Nora ni mwanae. Naomba ujue hili uncle. Ukitenda kwa unyama kwa mtu asiye na hatia kwa sababu tu ya kibinafsi, basi mimi siwezi kukufuata tena..." Lexi akasema kwa hisia.

"Lexi!" akawa amefika Torres hapo na kuita hivyo.

"Torres, what the f(...) is going on?" akauliza Mensah.

"Boss, Lexi, tafadhali... tukae chini tusuluhishe mambo kama familia. Tusiwe na conflict over jambo hili kwa sababu... look... najua in perspective, boss tunaweza ku-differ... na...."

Torres akaendelea kuongea kwa njia ya kutafuta suluhu, naye Kendrick akawa tu anamwangalia Lexi kwa hisia akitafakari maneno yake. Lexi pia alikuwa anamtazama kwa hisia, kisha kabla hata ya Torres kumaliza kuongea, Lexi akaondoka sehemu hiyo haraka sana. LaKeisha akamfata upesi ili kujua tatizo lilikuwa ni nini, naye Kendrick akawaambia wengine wampishe kwa sababu alitaka kuwa mwenyewe.

Baada ya wote kuondoka sehemu hiyo, Kendrick akaketi na kubaki anamfikiria sana Lexi. Hakupenda hata kidogo kumwona akiudhika hasa kwa sababu alimpenda kama mwanae wa kumzaa, lakini kwa upande mwingine alikuwa amekasirishwa sana na uamuzi wake wa kuingilia mpango wake wa kuwatuma watu wale ili wamfedheheshe mtoto wa adui yake. Kitendo alichofanya Lexi kilikuwa kimeikorofisha sana nafsi yake, na hii ikaanza kujijenga kuwa sababu kubwa ya mgogoro kati ya wawili hawa.

Ijapokuwa LaKeisha alijaribu kumzuia Lexi asiondoke na amwambie kila kitu kilichotokea, Lexi alikuwa amefadhaika sana na kutoweza kuongea lolote lile. Akamwambia tu LaKeisha alihitaji kuondoka na kurudi Dar, lakini akamhakikishia kuwa bado alikuwa pamoja naye. Baada ya Lexi kutembea, ikabidi LaKeisha na wengine wakae na Torres ili awaelezee yaliyokuwa yametoka kutendeka.

Torres aliwaweka wazi sasa kuwa alijua kuhusu mpango wa kisiri wa Kendrick wa kuagiza watu wale saba wamteke ACP Nora ili wamtendee vibaya kimwili, kisha waache ujumbe kwenye mwili wake ulioelekezwa kwa Jenerali Jacob ili kumuumiza kihisia; kama kumkomoa. Aliwaambia kwamba Kendrick alimtumia yeye (Torres) kuwalipa wanaume hao kwa njia isiyo ya moja kwa moja (yaani bila kujua wanalipwa na nani) ili wafanye kazi hiyo, kisha wangeongezewa pesa zaidi kazi hiyo ikikamilika. Wanaume wale saba walikuwa watu wabaya ambao walijikusanyia pesa kwa kutenda mambo maovu, hivyo kwa msaada wa Torres, Kendrick ndiyo alifanikiwa kuwapata na kuwaongoza kisiri kufanya jambo hilo.

Lakini baadae Torres aliongea na Lexi kumjulisha alichofanya Kendrick, na ndiyo Lexi akaamua kwenda kumsaidia Nora. Torres akaweka wazi kuwa alimwambia Lexi kama kumfahamisha tu, siyo kwamba alitegemea angefanya jambo alilofanya. Sasa Torres akawa hana uhakika kama "boss" wao huyo angeendelea kumtumaini kwa sababu ilionekana alifanya usaliti kwake, lakini kihalisi ni dhamiri yake tu ndiyo iliyomsumbua kutokana na kitendo hicho cha boss wao kuwa kibaya sana.

Kevin, Victor na Mensah wakamwambia Torres angetulia tu na kutomwambia Lexi kwa sababu hawakuona faida yoyote ya kumsaidia mwanamke yule, lakini LaKeisha akawarekebisha kwa kusema jambo aliloagiza boss wao halikuwa jambo zuri kiuweli. Vipi kama ingekuwa ni dada zao, au mtoto wa kike wa Victor? Akashauri tu kuyaweka hayo pembeni kwanza ili wajaribu kusaidia kuweka mambo sawa baina ya Lexi na boss mkubwa. Wawili hao ndiyo waliokuwa nguvu kuu ya timu hii, hivyo kama wangetofautiana namna hii kwa muda mrefu basi mambo mengi yangeharibika.

Vijana hawa wakatawanyika baada ya mazungumzo yao mazito kuelekea suala hilo. Lakini hawakujua kuwa ni Kevin ndiye aliyempa Kendrick wazo lile la kuwaajiri wanaume wale saba ili wamfanyie Nora ukatili ule. Jamaa alikuwa ameongea na Kendrick na kumpa ushauri huo tokea wakati ule alipoona ni kama Lexi hajui jinsi ya kufanya mambo vizuri, naye Kendrick aliona kweli ingekuwa sahihi kufanya hivyo bila Lexi kujua ili amwondoe Nora, aliyemwona kama kisababishi cha kifo cha Oscar. Kwa hiyo hapa Kevin alikuwa akiigiza kama vile mambo haya yote ni mapya kwake, kumbe ni yeye ndiye aliyesababisha sasa Lexi na Kendrick wakatofautiana.

Kevin akajaribu kumfata Kendrick ili waongee kifaragha, lakini bado mwanaume huyo hakutaka kuzungumza na yeyote. Akamwacha tu, na ijapokuwa mpango ule wa kumwondoa Nora haukufanikiwa kwa sababu ya Lexi, ikamridhisha kuwaza kwamba utofauti wa wawili hawa ungefanya Lexi awekwe pembeni kuanzia sasa ili yeye aweze kuendelea kumshawishi Kendrick kijanja kufanya mambo kwa njia aliyotaka.


★★★★



IKULU


Kundi la kufanya maovu la Raisi Paul Mdeme lilikutana tena kwa pamoja Ikulu. Walikuwa wanataka kuzungumzia mambo yote yaliyofanyika tokea mara ya mwisho walipokutana hapo, na kwa sababu hayakuwa mambo mazuri, hali iliyokuwepo kati yao pia haikuwa nzuri. Salim Khan, yule milionea, kama kawaida alikuwa akilalamika kwamba mambo yote aliyotabiri kutokea yangetokea, hasa kwa sababu Mdeme aliwahakikishia mzigo wake wa dhahabu ungefika na kuutumia kwa njia fulani, lakini Mess Makers walifanikiwa kuuiba pia.

Ingawa Mdeme alisema walipiga hatua katika msako wao wa wezi wale, bado haikuwa na faida yoyote kwa wanzake kwa sababu mambo yao mengi yaliharibika kwa kuwa hawakupata "support" nzuri kama ilivyokuwa mwanzoni. Salim Khan aliongea na kuongea, naye akamkumbusha Luteni Jenerali Weisiko kwamba alimwambia kama mpango ule ungeharibika basi angemkata kichwa kwa sababu alimwonyesha jeuri, na hilo likamkasirisha sana Weisiko.

Katika maongezi yao wote, Jenerali Jacob alikuwa kimya tu wakati wote, na wengine wakataka kujua aliwaza nini.

"Mnataka niseme nini? Na mimi nianze kulalama kama mtoto anayedai pipi? Itasaidia kufanya mambo yawe shwari?" Jenerali Jacob akaongea.

"Unataka kusema nini?" Gavana Laurent Gimbi akamuuliza.

"Salim aache utoto!" Jenerali Jacob akasema.

"Unasemaje?" Salim akauliza kiukali.

"Unajua ukifunga ndoa, shangwe na furaha, au tabu na mateso ni vitu vya lazima. Wewe umefurahia raha kwa miaka mingi, sasa tabu zimeanza unataka kujifanya kama vile sikuzote tulikuwa kile ambacho kimekupa raha kwa muda huu wote. Grow up. Kuwa kama mwanaume, acha kuongea sana, fanya vitendo. Ikiwa wewe ndiyo mwenye pesa zaidi nchini, onyesha nguvu yako na siyo kukaa tu nyuma ya mgongo wa mtu!" Jenerali Jacob akasema.

Luteni Jenerali Weisiko akatabasamu kwa kiburi baada ya kuona Jenerali amempausha mwanaume huyo.

"Mgongo wa mtu? Unamaanisha mimi nabebwa na Mdeme tu, si ndiyo?" Salim akauliza.

"Unajua mwenyewe!" Jenerali Jacob akasema kwa kukerwa.

Wengine wakamshangaa. Hata Mdeme alikuwa akijiuliza ni kwa nini Jenerali Jacob alikuwa mwenye hasira sana.

"Jamani... naona sisi sote tuko high sana. Tutaongea wakati mwi...."

"Wakati gani Eliya?" Waziri Mkuu Yustus Kagame akamkatisha Makamu wa Raisi.

"Kwa hiyo Jenerali... umeamua kunitukana leo, si ndiyo?" Salim Khan akamwambia.

"Aagh... halafu nilikuwa nakuona wa maana kweli, lakini mambo yako ya kitoto sana mwanangu," Weisiko akamwambia Salim.

Salim Khan akasimama na kumfata Weisiko, naye Weisiko akasimama pia.

"Ah-aaah mambo gani haya tena?" akauliza Yustus.

Salim Khan alikuwa na mwili mnene na mrefu pia, hivyo alikuwa mwenye nguvu na alitaka kumwonyesha Weisiko kuwa hakuogopa mwanajeshi.

"Kwa hiyo mkipigana tatizo ndiyo litaondoka?" akauliza Raisi Paul Mdeme.

"Huyu mbwa mchanga tuliyemfuga na kumfundisha jinsi ya kutafuna nyama leo anajifanya kutubwekea sisi... unacheza na moto Weisiko!" Salim akamwambia akiwa karibu na uso wake.

"Sijali una nguvu kiasi gani kaka. Hili tatizo siyo lako peke yako, limetuathiri sisi wote. Ungekuwa na busara kweli ungetafuta njia za kusuluhisha badala ya kujibweteka tu ukisubiri mheshimiwa Raisi ndiyo afanye kila kitu kama vile unamlipa," Weisiko akamwambia.

"Unajuaje kwamba simlipi?" Salim akauliza.

"Analipwa na serikali," Weisiko akajibu.

"Ahahahah... serikali gani? Hii hii ya trilioni 20?" Salim akasema kikejeli.

"Inatosha! Nionyesheni heshima mkiwa hapa!" Mdeme akaamuru.

Salim akaifata meza ya Mdeme na kuweka mikono yake juu ya meza, huku akimwangalia usoni kwa hasira.

"Mambo yote ambayo yametokea ni makosa yako. Hakuna yeyote anayepaswa kulipa ila wewe. Kuanzia sasa, sitaki tena kufanya lolote na nyie. Kivyangu, kivyenu," Salim akasema.

Wengine wakashangaa, isipokuwa Jenerali Jacob na Luteni Jenerali Weisiko. Wakaanza kumwambia asiongee namna hiyo kwa sababu ya hasira tu, lakini Salim akaonekana hatanii. Akamsogelea tena Weisiko usoni.

"Tutaonana," Salim akamwambia.

Weisiko alikuwa anamtazama kwa hasira kuu moyoni. Salim akaondoka hapo, akiwa amejitoa kwenye kundi hili kwa sababu ya tofauti zao kutokana na mambo yote haya. Mdeme akawa anamwangalia sana Weisiko, kama vile anamlaumu kwa kilichotokea.

"Mheshimiwa..."

"Shut your mouth!" Mdeme akamkatisha Weisiko.

Weisiko akatulia. Wengine walimwangalia Mdeme kwa wasiwasi kiasi, lakini Jenerali Jacob alikuwa ameangalia pembeni tu.

"Eliya, Yustus, Gimbi..." Mdeme akaita.

Watatu hao wakaitika.

"Mnaweza kwenda. Nahitaji kuongea na hawa wawili," akasema Mdeme.

Makamu wa Raisi, Waziri Mkuu, na Gavana wa Benki Kuu wakanyanyuka na kuondoka kama walivyoamriwa. Wakabaki wazee wa kazi hapo. Mdeme alikuwa akimtazama sana Jacob, naye aliona bado alikuwa kwenye hasira.

"Una shida gani wewe? Kwa nini umeongea vitu vikali namna ile?" Mdeme akamuuliza Jenerali Jacob.

"Nilikuwa najaribu kutetea upande wako, halafu me ndo' mbaya?" Jenerali Jacob akamuuliza.

"Unajua Salim ni nani... kashifa kwake hazitasaidia kwa sababu bado tunamhitaji..."

"No. Unamhitaji wewe. Mimi sijawahi kumhitaji. Nimekuwa nikifuata mambo yote uliyoniagiza kufanya tokea tulipoanza hii ishu, lakini mimi siyo mbwa wa mtu. Sisi sote hapa tuna dignity kaka... siwezi kukaa kuangalia tu mtu anatufokea kama vile sisi watumwa wake," Jacob akasema.

"Jacob, kumbuka ni kwa msaada wake ndiyo...."

"Huo msaada wake ungefanikiwa bila sisi kuhusika? Tusingetumia vijana wetu kwenye kila kitu tulichofanya, mngekuwa mlipo?" Jenerali Jacob akamwambia.

"Jacob! Unathubutu vipi kunisemesha namna hiyo? Umesahau sehemu yako?" Mdeme akasema kiukali.

"Naijua vizuri sehemu yangu, na ndiyo maana ninaongea. Nilikwambia kuwaendekeza hao Mess Makers ni hatari, lakini kwa sababu ya woga wako ukakifanya kichwa chako kiwe kigumu. Mimi sitakaa kupelekeshwa na Salim kama vile ananimiliki. Wewe si umeshaagiza mambo yafanywe namna unayotaka, basi tuyaache namna hiyo hiyo," Jenerali Jacob akaongea.

Raisi Paul Mdeme akawa anamtazama kimaswali sana.

"Ikiwa tumemaliza hapa, niruhusu niondoke.... mheshimiwa," Jenerali Jacob akasema.

Kisha akanyanyuka na kuanza kuondoka, akifuatwa na Weisiko.

"Una hasira na mimi kwa sababu ya kilichompata Nora, sivyo Jacob?" Mdeme akauliza hivyo.

Majenerali wakasimama na kumgeukia.

"Unanilaumu kwa kilichompata mtoto wako... kwa sababu mimi ndiyo nilimwingiza kwenye mission hiyo... ndiyo maana leo umeamua kunionyesha wazi hasira yako," Mdeme akamwambia.

"Ninaweza kuwa na uhusiano usioeleweka na mwanangu, lakini nampenda sana. Tokea mwanzo nimekuwa nikifuata kila kitu unachosema Mdeme, lakini inapokuja kwenye suala la damu yangu... sitakuwa mzuri," akasema Jenerali Jacob.

Mdeme akasimama na kumfuata mpaka karibu.

"Najua nimekosea ndugu yangu. Ni makosa yangu kwamba nimemwingiza Nora matatizoni... na kwa hilo naomba unisamehe. Nakutegemea sana Jacob. Wewe ndiyo nguvu yangu. Siko radhi hata kidogo kukupoteza," Mdeme akamwambia.

Jenerali Jacob na Weisiko wakatazamana.

"Ikiwa unataka... nitamwondoa Nora katika msako huu. Akae tu pembeni ili awe salama kwa sababu... hata mimi kiukweli sijajisikia vizuri baada ya kujua kilichompata. Namwona kama binti yangu pia," Mdeme akasema.

"Nora hatakubali kuacha hii ishu, tena hasa baada ya kilichotokea. Unajua jinsi alivyo na king'ang'anizi," Weisiko akamwambia Jenerali Jacob.

"Basi nitaagiza arudishwe kabisa Dodoma... yaani asihusike hata kidogo na...."

"Hapana," Jenerali Jacob akamkatisha Mdeme.

Mdeme akamtazama tu kwa umakini.

"Najua Nora ni wa muhimu katika hili. Atapaswa kuendelea na kazi yake, lakini nitataka awekwe mbali na action zozote za kuwafuata watu hawa," akasema Jenerali Jacob.

"Usijali Jacob. Nitafanya mpango. Natumaini mambo kati yetu yataendelea kubaki sawa kijana wangu," Mdeme akamwambia.

"Na huu uzee unamwita kijana? Acha kumdekeza sana mheshimiwa," Weisiko akatania.

Mdeme akatabasamu na kusema, "Salim mniachie mimi, nitadili naye. Endeleeni tu na kazi. Ninajua wakati huu matokeo yatakuwa mazuri."

Viongozi hawa wa jeshi wakatikisa vichwa vyao kukubali, naye Luteni Jenerali Weisiko akapiga saluti ya heshima, kisha wakatoka kwenye ofisi yake.



Wakiwa bado wanaelekea nje, Weisiko akamuuliza Jenerali Jacob, "Tuna uhakika Mdeme atafanya mambo yawe sawa, au tuendelee na mambo yetu kisiri?"

"We unaonaje?" Jenerali Jacob akamuuliza.

"Mimi ninafata chochote unachochagua General," Weisiko akamwambia.

"Tunaendelea Weisiko. Hatutaruhusu siri zetu zivuje. Hawa jamaa wanatuchezea mchezo wa kuzungusha sana, wakifikiri sikuzote faida itakuwa kwao, ila tutahakikisha wanakwisha wote," akasema Jenerali.

"Na Salim?" Weisiko akauliza.

"Kwa hizo dharau? Unajua cha kufanya," akajibu Jenerali Jacob.

Weisiko akaachia tabasamu la kuridhika baada ya kusikia kauli hiyo. Wawili hao wakaondoka jengoni hapo hatimaye ili kwenda kufanikisha mipango yao.


★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE

★★★★★★★★★★★★★★★★★


SIKU ILIYOFUATA


Kama ni habari mpya ya jiji siku hii iliyokuwa na ulingano na Mess Makers, basi ilikuwa ni kile alichofanya Salim Khan. Milionea huyo alikuwa amejiondoa katika mambo YOTE aliyowekeza pesa zake kwenye miradi ya serikali, haijalishi zilikuwa ni sekta gani; zote. Kwa muda wote ambao Mess Makers walikuwa wakiwapa shida yeye na kundi lake, Salim Khan ndiye aliyekuwa akimsaidia sana Raisi Paul Mdeme kwa masuala hayo, lakini tokea walipokosana kwa sababu ya viburi vyao, sasa akawa ameamua kuwaonyesha wazi kwamba hakuwa akitania aliposema yeye na wao ni basi.

Watu wengi sana walikuwa na maswali kuhusu uamuzi wa tajiri huyo, na wale waliokuwa wanamfanyia kazi wakavijulisha vyombo vya habari kwamba Salim Khan angeeleza sababu zake kwenye mahojiano maalum siku ya kesho, hivyo wangepata majibu waliyohitaji.

Raisi Paul Mdeme alijitahidi sana kumtafuta ili waongee, lakini Salim alimkwepa tu. Alijua uamuzi wake huo ungemuumiza sana, hivyo kufikia hapa alishindwa kujua angefanya nini. Mess Makers walikuwa wamemwibia matrillioni ya pesa, wakaiba na dhahabu zake, bado watu waliowekwa kuwafatilia hawakuwa wamewakamata, na sasa tena Salim alikuwa ameanza kuleta zengwe. Akaona amtafute Jenerali Jacob kwa simu ili wazungumze kuhusu ni nini ambacho wangefanya sasa.

"General... Salim anataka kuharibu mambo. Itakuwaje kama kwenye hayo mahojiano akisema kila kitu ambacho tumefanya?" Mdeme akasema.

"Hawezi," Jenerali Jacob akajibu.

"Unajuaje?"

"Atakuwa na mambo mengi ya kupoteza ikiwa ataropoka chochote kuhusu sisi. Anachotaka tu ni umati wa kumfuata... ndiyo sikuzote anachoangalia..."

"Nimejaribu kumtafuta, hanijibu. Yaani ni kama amekuwa mwendawazimu..."

"Anafanya hivyo ili kutukomoa, na kwa sababu pia anajua hatuwezi tukamfanya lolote..."

"Kwa hiyo tunatakiwa tu kukaa na kumwacha atambe? Maswali yakija kugeuziwa kwangu itakuwaje?"

"Mheshimiwa Raisi... mimi ni mwanajeshi. Mambo ya siasa huwa...."

"Oh, come on Jacob! Acha kujifanya modest sana katika hili. Ninajua hauwezi kukaa tu ukasubiri Salim atende kama mwehu. Niambie. Unawaza nini?"

"Okay. Ninawaza.... kumuua," Jenerali Jacob akasema kwa uhakika.

"Come again?!" Mdeme akashangaa.

"Yeah," Jenerali Jacob akasema.

"General... unajua unachokisema? Hebu tuache masihara basi!" Mdeme akamwambia.

"No, wewe ndiyo uache masihara. Acha kunyong'onyea mbele ya mtu eti kisa amewahi kukupa mia mbili. Salim anakutusi vibaya sana Mdeme, kwamba pamoja na kwamba wewe ni Raisi lakini hauwezi kumfanya kitu. Nilikuwa nikisubiria unipe amri hii lakini inaonekana mambo yamekuwa mengi sana kwako mpaka unasahau tulipotoka. Kumbuka tulitumia njia zipi kuwaondoa wale wote waliokuwa vikwazo kwetu. Salim sasa ni kikwazo kwetu Mdeme. Ni lazima aondolewe!" Jenerali Jacob akasema kwa mkazo.

"Lakini General, Salim siyo kama wengine. Hatuwezi tu ku...."

"Hatuwezi? Umeweka wingi! Hiyo inamaanisha unaniunga mkono, siyo?"

"General... Salim akifa kwa wakati huu haitakuwa nzuri kwangu. Kwa jinsi mambo yalivyo watu wanaweza wakafikiri moja kwa moja kwamba mimi ndiyo nimemuua... haitakuwa nzuri Jacob," Mdeme akasema.

"Usijali kuhusu hilo. Kila kitu kitakwenda kulingana na mpango..."

"Unamaanisha... yaani umeshapanga jinsi ya... kumuua Salim?"

"Ndiyo..."

"Halafu nini kitafuata baada ya hapo?"

"Ndiyo maana nimekwambia kwamba kila kitu kitakwenda kulingana na mpango niliouweka. Sikuzote nimejitahidi kukulegezea mambo kaka, lakini hauonyeshagi shukrani vya kutosha. Unawafurahia zaidi watu ambao wanakuja kukugeuka wakati sisi tulio waaminifu unatuweka tu pembeni kama akiba ya mchele..."

"Jacob... siyo hivyo. Ni kwamba tu...."

"Haina haja ya kujikwarua sana. Wewe kaa kwa kutulia. Kila kitu kikikamilika, utakuja kunishukuru. Just play along," Jenerali Jacob akasema.

Kisha akakata simu na kumwacha Mdeme akiwaza mengi sana. Hakuwahi kufikiria angekuja kulazimika kuchukua uamuzi huu; kuua mtu aliyemwona kama rafiki kwa muda mrefu sana, hata ijapokuwa wote walitenda mambo mabaya. Lakini akaamua kuyaacha mambo mikononi mwa Jenerali Jacob, akiamini mwanaume huyo alijua akichokuwa anakifanya.


★★★★


ACP Nora alikuwa akijiandaa kuondoka hospitalini. Luteni Michael alikuwa ameongea na madaktari kwa niaba yake siku iliyopita na kuwaambia Nora alitaka sana kuondoka, nao wakamwambia kwa kuwa alisisitiza basi angeondoka wakati huu. Ikiwa ni mida ya saa 6 mchana tayari, akawa amemaliza kuvaa nguo zingine nadhifu ambazo Mario alisaidia kumletea hapo, na sasa akawa anajiandaa kuondoka ndani ya chumba hicho hatimaye, huku Mario na Hussein wakiwa nje wanasubiri.

Lakini kabla hajauendea mlango, ukagongwa, na sauti ya Luteni Michael akiuliza kama ilikuwa sawa kuingia ikasikika. Kulikuwa na muuguzi wa kike ndani hapo pia ambaye alikuwa anamsaidia Nora kwa mambo kadhaa, naye akasema kwa sauti kubwa kiasi kwamba Luteni Michael angeweza kuingia. Luteni Michael alipoingia, Nora aliachia tabasamu dogo, lakini likafifia baada ya wengine waliomfuata nyuma yake kuingia.

Ilikuwa ni Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Donald Ngassa, akiwa pamoja na yule msaidizi mkuu wa mambo ya ndani yaliyohusiana na Jeshi la Polisi, Principal Secretary Joachim Uwesu. Kwa kuangalia uso wa Luteni Michael, Nora angeweza kuhisi kwamba jambo waliloleta hapo halikuwa na uzuri kwake. Akapiga saluti ya heshima kuwaelekea, lakini IGP Donald akamwambia ajiweke tu sawa. Muuguzi yule akawapisha na kuondoka.

"Unajisikiaje binti yangu?" IGP Donald akamuuliza.

"Niko sawa mkuu. Tayari kurudi kazini," akasema Nora.

"Habari za muda ACP?" Secretary Joachim akamsalimu.

"Ni nzuri tu Joe. Unaendeleaje?" Nora akarudisha salamu pia.

"Vizuri zaidi yako," akajibu Joachim, naye Nora akatabasamu.

"Unajua ulikuwa unatakiwa kuendelea kukaa hospitalini ACP... kwa nini unang'ang'ania kuondoka?" IGP Donald akamuuliza.

"Kukaa hapa hakuna utofauti na kukaa gerezani. Na tafadhali naomba mwache kunitendea kama vile ndiyo nimetoka kutotolewa... mnaweza kunichangia sasa hivi na wote nikawakunja," Nora akatania.

Wawili hao wakacheka kidogo.

"Mmekuja kunitembelea tu, au kuna mapya?" akauliza Nora.

"Vyote. Kwanza... pole kwa yote yaliyokupata dada. Ni mambo yenye kusikitisha sana, na tunaelewa ni jinsi gani ilivyo ngumu kwako," akasema Secretary Joachim.

"Ahah... Joe ukishagaanza kuzunguka sana wote tunajua tu kwamba bomu linakuja," Nora akasema.

"Ah... Nora ameshaanza. Sikuzote ananifikiria kama vile mtu aliyeficha kisu nyuma ya mgongo wake," Joachim akasema.

IGP Donald akatabasamu.

"Kwa hiyo, mapya ni yapi?" akauliza Nora.

"Siwezi kusema ni mapya ila... unajua kiukweli kama ingekuwa ni mimi ndiyo nimepatwa na mambo hayo yote yaliyokupata, ningeahirisha uchunguzi huu kwa sababu tayari najua kuna watu wameniwekea target kwa nyuma," akasema Secretary Joachim.

"Hata me ningefanya hivyo, kama ningekuwa wewe," akajibu Nora.

"Ahahahah... usijifanye Alexander the Great," Secretary Joachim akasema.

"Kwa hiyo unasema kwamba... nimeondolewa kwenye hii mission?" Nora akauliza.

"Oh Nora, hatutafanya hivyo. Najua unavyopenda kazi yako na... kiukweli tunakuhitaji sana. Wewe ni wa muhimu katika hili hakuna asiyejua. Na ndiyo sababu hatuwezi kuruhusu chochote kibaya kikupate. Lakini pia najua huwa haupendi walinzi," akasema Secretary Joachim.

"Yeah... kabisa..." akasema Nora.

"Kwa hiyo ni muhimu tutumie njia fulani kukulinda...."

"Joe... tafadhali acha kuzunguka sana just... tell me," Nora akamkatisha.

"Okay. Kuanzia sasa utapaswa kufanya uchunguzi wako wote... mbali na timu ya Lieutenant Michael," Secretary Joachim akasema.

Nora akamtazama Luteni Michael kimshangao, lakini yeye alikuwa anamwangalia kwa njia ya kawaida.

"Unamaanisha nini... mbali?" Nora akauliza.

"Tunakupa ofisi yako maalum huku, utakuwa unafanya kazi zako za utafiti huko, kisha zinatumwa kwa Luteni ili wazishughulikie," akasema IGP Donald.

Nora akakunja uso kimaswali.

"I don't... yaani... nifanye kazi na watu ndani ya jiji moja bila kuonana nao, ndiyo unachosema?" akauliza.

"Yeah," akajibu IGP Donald.

"Kwa nini?" Nora akauliza.

"Kama nilivyosema... ni ili kukulinda," akasema Secretary Joachim.

"Luteni Michael amekuwa akinilinda vizuri tu mbona? Na... sihitaji ulinzi mimi. Sihitaji kupewa ofisi, sihitaji chochote... nitakuwa sawa. Huwezi kunitenganisha na timu hii. Nachotaka hata zaidi sasa ni kurudia kazi hii nikiwa nao kwa kuwa tumetoka mbali... nimewazoea... sitaweza kufanya kazi bila kuonana nao," Nora akawa anaongea kwa hisia.

"Basi ACP, tafadhali jitulize. Unapaswa kujitahidi tu kuyaona mambo kwa njia pana zaidi. Hii itakuwa nzuri kwako. Unaweza ukawa subject wa tukio lingine kama lililokupata kwa sababu hauna uangalizi maalum," IGP Donald akamwambia.

"Hivi kweli... Luteni... does this make sense?" Nora akamuuliza Michael.

Lakini Luteni Michael akabaki kimya tu.

"Nora... tafadhali kubali hili. We are just looking out for you. Tafadhali nakuomba just... please... nakuomba kama rafiki. Ni muhimu sana kwako," Secretary Joachim akamwomba.

"Na kama nikikataa?" Nora akauliza.

"Basi... ni kwamba hautapaswa kujihusisha na kesi hii... utapaswa kurudi kwenye post yako Dodoma," IGP Donald akasema.

"Unbelievable!" Nora akasema kimshangao.

"Nora please... tunakuhitaji, just do this, hakuna ugumu wowote... ni kwa ajili yako," Joachim akamsihi.

"Luteni..." Nora akamwita kama anamhitaji amuunge mkono.

"Wako sahihi ACP. Ni bora iwe hivi... ili uwe salama zaidi," Luteni Michael akamwambia.

Nora akarudi sehemu ya kitanda na kuketi, huku akitikisa kichwa taratibu kwa kutoamini.

"Ni General wenu ndiyo amefanya haya yote, siyo?" Nora akauliza bila kuwatazama.

IGP Donald na Secretary Joachim wakaangaliana, kisha Joachim akasogea usawa wa Nora.

"Hapana, ni mheshimiwa Raisi. Alijisikia vibaya sana kwa kilichokupata ndiyo maana akatoa agizo hili," Joachim akasema.

"Angekuwa amenipigia simu kuniambia," Nora akasema.

"Ana mambo mengi kama unavyojua, ndiyo maana tuko hapa," IGP Donald akamwambia.

Secretary Joachim akatoa karatasi fulani jeupe na kumpatia Nora.

"Sign tu hapo kuthibitisha kwamba umekubali," Secretary Joachim akasema.

"Nina uhakika gani hiyo siyo bogus treaty?" Nora akauliza.

"Ahahah... unaweza kuisoma ukihitaji. Lakini hata wewe unajua blah, blah, blah, ni nyingi hapo," Secretary Joachim akamwambia.

Nora akamtazama Luteni Michael kiufupi. Luteni aliona kwenye macho ya mwanamke huyu kwamba kweli hakutaka kufanya hivyo, lakini kwa sababu alikuwa chini ya hali iliyomlazimu kutenda kupatana nayo, hakukuwa na jinsi. Nora akaichukua karatasi hiyo, naye Secretary Joachim akampatia kalamu ili atie sahihi.

"Kuna air condition nzuri kwenye hiyo ofisi?" Nora akauliza kiutani.

"Ahahahah... chochote kwa ajili yako Malkia," Joachim akamwambia.

Nora akatia sahihi yake, kisha Secretary Joachim pamoja na IGP Donald Ngassa wakamuaga na kumwambia kwamba walikuwa wamefanya mipango ya kumbadilishia hoteli ya kukaa ili awe sehemu mpya na salama, hivyo angepaswa kwenda kupumzika leo, halafu kesho ndiyo angepelekwa kwenye ofisi yake mpya ili aendelee na kazi. Nora bado alipingana sana na mambo hayo yote, lakini kama ingemhitaji kuyafuata tu ili kuendelea na kazi aliyopewa, basi angefanya hivyo. Alikuwa amekwishazoea kufanya kazi bega kwa bega na timu ya Luteni Michael, lakini kuanzia sasa ingekuwa ni kurushiana mawe mbali kwa mbali.

"Eti wako sahihi ACP... Kweli na wewe unakubaliana na huu upuuzi?" Nora akamwongelesha Luteni Michael.

"ACP..."

"Well, hakuna jinsi now. Tutapaswa kufanya kazi kama vile hatujuani na... kama vile hatujapitia mambo mengi pamoja," akasema Nora, akionekana kuudhika.

Akanyanyuka ili aanze kuuelekea mlango, lakini Luteni Michael akamshika mkononi kumzuia.

"Nora..." Luteni Michael akamwita kwa sauti yenye hisia.

Nora alipomwangalia, akatambua kuwa Luteni Michael alikuwa akimwonyesha hisia fulani hivi mpya, na hili likavuta umakini wake.

"Leo ndiyo kwa mara ya kwanza umeniita kwa jina langu. Hii yote kuni-please kwamba jambo hili lote ni sahihi?" Nora akauliza.

Luteni Michael akamsogelea karibu zaidi. Nora akabaki kumtazama kama ameduwaa.

"Siyo rahisi kwangu pia Nora. Nilikuwa napenda sana ukiwa karibu yangu. Bado natamani hilo. Lakini siwezi ku... kujua nitafanya nini kama na wewe ukipotea kwa sababu ya kuwa nasi muda mwingi... siwezi kujisamehe kama utapatwa na lolote baya Nora..." Luteni Michael akaongea kwa hisia.

Nora akawa anajiuliza sababu ya Luteni Michael kumwambia haya yote ni nini, lakini lile wazo lile, halikuwa mbali sana akili yake.

"Luteni...."

"No... niite Michael," Luteni Michael akamwambia.

"Unataka kusema nini?" Nora akauliza.

Luteni Michael akaona amjibu kwa vitendo. Akaanza kuusogelea mdomo wa Nora taratibu, naye Nora akatambua kuwa jamaa alitaka kumbusu. Michael alipokuwa ameukaribia zaidi mdomo wa Nora, mwanamke huyu akainamisha uso wake na kupiga hatua chache nyuma. Hii ikamuumiza sana Luteni Michael.

"Luteni.. hhh... Michael... samahani ila...."

Nora akakatishwa baada ya mlango wa chumba hicho kufunguliwa. Wakaingia Mario na Hussein.

"Tulikuwa tumewasindikiza hao wawili mpaka kwenye gari... ahah... Secretary Joachim ni mcheshi," akasema Mario.

"Lakini ACP... ni kweli eti sasa hivi hautaambatana nasi?" akauliza Hussein.

"Ndiyo. Ndiyo inavyoonekana," Nora akajibu huku akijaribu kupotezea kilichokaribia kutokea baina yake na Luteni Michael.

"Dah! Itakuwa ngumu kutokukuona tena," Mario akasema.

"Lakini hata kukutembelea si itakuwa poa?" Hussein akauliza.

"Ndiyo. Mnaweza kunitembelea... ila sijui sana," akasema Nora.

"Tutaku-miss. Hasa Luteni," akasema Mario.

Nora akamtazama Luteni Michael, ambaye alikuwa anamwangalia kwa hisia pia.

"Na sisi tumeongezewa jamaa wengine kwenye timu yetu. Ila hawataweza kuwareplace wenzetu waliopotea... never," akasema Hussein.

"Wamekuja wangapi?" Nora akauliza.

"Watano. Special unit toka JKT," akasema Hussein.

"Okay. Nadhani sote tu tukiendelea na kazi... hata kama tutakuwa tumetenganishwa... tutafanikiwa tu," akasema Nora huku akimtazama Luteni Michael.

"Yeah... ACP yuko sahihi," Luteni Michael akasema.

Kwa kuwa hali kati ya hawa wawili ilikuwa imejivuruga kwa njia ambayo haikutazamiwa, Nora akaona tu aanzishe mwendo ili kuondoka hospitalini hapo. Wanajeshi hao watatu wakamsindikiza, huku Mario akimwambia alilileta na gari lake Nora pia. Luteni Michael akapendekeza amwendeshe mpaka kwenye hoteli mpya ambayo angekaa ikiwa hakuwa na nguvu za kutosha, lakini Nora akasema angekuwa sawa tu kuendesha ili kujipa nguvu zaidi. Ingawa hivyo, Mario na Hussein wangetakiwa kumsindikiza ili kuhakikisha anafika salama, naye Luteni Michael angeelekea kule jengoni kwa timu yake.

Wakaachana muda mfupi baada ya hapo, naye Luteni Michael akabaki tu akitafakari sana kuhusu itikio la Nora ndani ya chumba kile. Mwanzoni alipofikiria kumwambia hisia zake, alikuwa tayari kwa lolote lile ambalo lingetokea, lakini leo baada ya Nora kukwepa hisia zake, bado alikuwa akitaka sana kurekebisha hali hiyo ili ampate mwanamke huyo. Akaingia tu kwenye gari lake akiwa anafikiria ni nini kifuate kuhusiana na jambo hilo.



Baada ya Nora kufika hotelini na kusindikizwa na Mario pamoja na Hussein mpaka nje ya mlango wa chumba chake kipya, wawili hao wakamuaga na kusema ahakikishe anafunga mlango kwa ndani. Walikuwa wameongea naye kuhusu mambo mengi, kutia ndani suala la Salim Khan kuitimulia vumbi serikali na kusema kama kweli jamaa alikuwa ameamua kufanya aliyoyafanya basi na wao wangeacha kazi yao na kwenda kucheza tu mpira na timu ya Yanga. Hii ilikuwa ni njia yao ya kumtania, naye Nora alifurahia sindikizo lao na kuagana nao vizuri. Alipoingia kwenye chumba chake, alipendezwa na mandhari safi na mpangilio mzuri wa vitu, na vingi vilikuwa vya gharama. Akaelekea kitandani na kuketi ili kutafakari mambo kwa ufupi.

Kumbukumbu za mambo yote yaliyotokea usiku ule aliotekwa, zilimfanya ahisi ni kama yale yote aliyoona yalikuwa kwenye ndoto ya kutisha, lakini alijua wazi ilikuwa ni mambo halisi. Bado mtu yule aliyetokea ghafla kumwokoa alizunguka sana kichwani kwake, fikira ya kwamba ni adui aliyeokoa uhai wake ilimtatiza sana. Lakini tena, akaituliza tu akili yake na kuamua kwamba asitafakari mambo yenye kuvunja sana moyo kwa muda huo, bali ajaribu kujipa wakati wa kutosha kuijaza nguvu akili yake ili kufikia kesho kazi zianze.

Njia nzuri iliyokuja haraka kuliko zote akilini mwake, ilikuwa ni Lexi. Akafikiria ampigie simu ili kuongea naye, na labda hata aonane naye. Zilikuwa zimepita siku kama tatu bila kuonana naye, na akikumbukia mambo yalipoishia baina yao, akajawa na hamu kubwa zaidi ya kutaka kumtafuta. Akachukua simu yake na kumpigia, naye akapokea.

"Hey..." Nora akasema.

"Hey..." Lexi akasikika.

"Mbona kimya?" Nora akauliza.

"Mimi, wewe?" Lexi akauliza pia.

Nora akatabasamu na kusema, "Wewe."

"Hakuna. Ni wewe ndiyo umeona unichunie," Lexi akasema.

"Sijakuchunia wala. Nili..patwa na matatizo," Nora akasema.

"Matatizo gani?"

"Nilitekwa..."

"Wewee.... lini?"

"Juzi..."

"Eh! Uko sawa lakini mheshimiwa?"

"Ndiyo niko sawa..."

"Pole sana jamani. Kwa hiyo... eh... yaani hata nimekosa la kusema..."

"Usijali... nitakuwa sawa..."

"Nimeona kwenye habari, mlimkamata mmoja wao... anaitwa Oscar eeh? Ndiyo maana wakakuteka eti?" Lexi akauliza kama vile haujui ukweli.

"Hapana Lexi... sijui sana. Tafadhali... tusiongelee hayo..." Nora akamwomba.

"Okay sawa mheshimiwa. Uko wapi sasa hivi?" Lexi akauliza.

"Niko hotelini... napokaa..."

"Oh, okay. Unahitaji kupumzika..."

"Nahitaji kukuona..." Nora akasema kwa hisia.

Lexi akiwa upande wa pili, alifumba macho baada ya Nora kusema hivyo. Bado alikuwa na wakati mgumu pia baada ya kilichotokea baina yake na Kendrick kuhusiana na suala zima la kumteka mwanamke huyo. Ijapokuwa alihisi hatia sana kwa kilichompata Nora, alijua bado angetakiwa kuwa makini kwa sababu yeye bado alikuwa adui yake.

"Aam... unahitaji kuniona?" Lexi akauliza.

"Ndiyo..." Nora akasema.

"Lakini..."

"Please..." Nora akamwomba.

"Okay. Uko hoteli gani?" Lexi akauliza.

"Hyatt Regency," Nora akasema.

"Wow! Halafu ulikuwa unaniita mimi mtoto wa kishua!" Lexi akasema.

Nora akacheka kwa sauti ya chini.

Lexi akamwambia angefika hapo muda si mrefu sana, nao wakaagana baada ya hapo.

Nora sasa akajihisi kama vile alikuwa ameanza kuutua mzigo mzito wa mawazo baada ya kuongea na Lexi. Akaona ampigie na mdogo wake, Asteria, ili kumjulia hali, lakini kwa sababu fulani hakupokea simu yake mara nne kabisa. Hivyo Nora akaweka tu simu yake pembeni na kubaki hapo kwenye chumba chake akimsubiri kwa hamu Lexi, akitarajia mambo mengi sana.



Ilipita kama nusu saa hivi, naye Lexi akampigia Nora kumjulisha kwamba tayari alikuwa nje ya jengo hilo la hoteli. Nora akamwelekeza namba ya chumba chake, kilichokuwa kwenye ghorofa ya 7 kabisa, naye Lexi akaanza kupanda huko juu. Hoteli hii ilikuwa ya kifahari sana, ikiwa na vitu vingi vya gharama na vyenye ubora wa hali ya juu. Chumba kwa kulala usiku ilikuwa ni laki nne, sasa fikiria Nora alikuwa analipa kiasi gani kukaa hapo kwa muda wote ambao angeendelea kuwapo!

Baada ya Lexi kufika nje ya mlango wa chumba cha Nora akaugonga, naye Nora akafungua. Walipeana tabasamu lenye hisia huku wakiangaliana sana. Lexi alikuwa amevaa nguo fulani nyekundu kwa juu yenye mikono mirefu kufunika mpaka viganja ikiacha vidole vichache wazi, suruali nyeupe ya jeans laini, na sneaker nyekundu kwa chini. Kichwani kwake alivaa kofia nyeusi yenye maandishi "TMT," akionekana kama muhuni wa genge fulani hivi.

Nora akamkaribisha ndani, naye akapita na kuelekea sehemu yenye sofa. Vitu vingi hapo vilikuwa vizuri sana kutazama, na baada ya Lexi kugeuka akakuta Nora amesimama karibu naye huku anatabasamu. Yeye pia akatabasamu, kisha Nora akaichukua kofia yake (Lexi) na kuivaa yeye. Lexi akatabasamu kwa furaha, kisha akamkumbatia Nora. Nora alijihisi vizuri sana baada ya Lexi kufanya hivi, naye akazungusha mikono yake mgongoni kwake kurudisha kumbatio hilo pia.

"Mbona hauongei sana leo?" Nora akauliza.

"Nimefurahi tu kuona unaendelea vizuri mheshimiwa," Lexi akasema.

Wakaachiana taratibu, lakini Nora akaendelea kuvishikilia viganja vya Lexi kwa chini.

"Kirefu cha TMT?" Nora akauliza huku anaipiga kofia kwa kidole.

"The Money Team," Lexi akajibu.

"Ahahahah... unapenda sana hela eeh?" Nora akauliza.

"Kupita msosi," Lexi akasema.

Nora akaendelea kumwangalia kwa hisia.

"Nime... nimekumiss," Nora akamwambia.

Lexi akachekea kwa chini.

"Nini?" Nora akauliza.

"Hii yote... siyo ajabu kwako?" Lexi akauliza pia.

"Kwa nini iwe ajabu?"

"Ahahah... ulishawahi kuiona movie ya Deadpool 2?" Lexi akamuuliza.

"Deadpool... Marvel?"

"Yeah..."

"Ndiyo... nimeziangalia zote..."

"Well, kulikuwa na hali tete wakati Wade anamwomba Cable wakumbatiane..."

"Ahahahah... pelvis to pelvis?" Nora akamkatisha.

"Hahah... kumbe unajua..."

"Acha zako Lexi... Deadpool ni chizi," akasema Nora huku akiendelea kucheka.

"Na sisi je?" Lexi akauliza.

Nora akaweka umakini kiasi.

"Sisi...." Nora akaishia tu hapo.

"Waliokuteka walikuumiza sehemu gani?" Lexi akabadili mada ghafla.

"Lexi... nilikwambia tusiongelee hayo leo..." Nora akasema.

"Sorry. Unataka tuongelee nini?" Lexi akauliza.

"Mimi... na wewe..." Nora akasema na kumsogelea karibu zaidi.

"Pelvis... to pelvis," Lexi akatania.

Nora akatabasamu kwa hisia.

Hali hii mpya ilikuwa ikimfurahisha sana Nora, lakini Lexi alikuwa akijitahidi kuzizuia hisia zake kumwelekea mwanamke huyu, na ukweli ni kwamba alikuwa ameanza kuvutiwa na Nora. Kwa hiyo alijihisi vibaya kwa kadiri kubwa kwa sababu haikutakiwa kuwa hivi; mpango kutokea mwanzo ulikuwa ni kumpeleleza Nora ili kupata taarifa muhimu kutoka kwake, lakini sasa kuingiza hisia ingesababisha ajihisi mwenye hatia kwa sababu alijiona mnafiki. Ila ukitegemea na jinsi yeye na Kendrick walivyotofautiana kutokana na mwanaume huyo kumfanyia ubaya Nora, ni kama ndiyo nguvu ya kumkaribia zaidi mwanamke huyu iliongezeka.

Nora akaigeuzia kofia upande wa nyuma ili isizuie uso wa Lexi alipokuwa akimkaribia zaidi, na moja kwa moja Lexi alijua Nora alitaka ambusu kama wakati ule wako ufukweni. Nora akaizungushia mikono yake kiunoni kwa Lexi, miili yao ikiwa karibu zaidi sasa, kibofu kwa kibofu, na walipotaka tu kupiga busu mlango ukagongwa.

"Aagh... hivi ni kwa nini hiyo huwa lazima itokee?" Nora akauliza kwa kukerwa.

"Ahahah... nenda kaangalie ni nani," Lexi akamwambia.

"Usikimbie," Nora akasema kiutani.

Kisha akamwachia na kuuelekea mlango. Alishangazwa kiasi baada ya kukuta ni Luteni Michael ndiye aliyefika hapo.

"Luteni..." Nora akaita.

Lexi alikuwa ametazama pembeni aliposikia Nora akisema hivyo, na macho yake yakakaza kwa kuhisi hasira. Sababu ilikuwa ni kwamba usiku ule Oscar alipokufa, Luteni Michael alikuwa pale, hivyo kwa njia fulani ilikuwa ni kama Lexi alimchukia kwa kuhisi ni kama yeye ndiye aliyesababisha mwenzake asiweze kujilinda vizuri kwa kuwa aliamuru afungwe pingu. Akakunja ngumi akizizuia hisia zake, bila kugeukia upande wao.

"Nora... tunaweza kuongea?" Luteni Michael akamwomba.

"Luteni...."

"Nilikwambia niite Michael..."

"Okay. Michael. Kuna jambo lolote jipya? Ungenipigia tu simu, si ulikuwa umeenda kule..."

"Nakupenda..."

Nora akabaki kumtazama tu kwa njia ya kawaida, kama vile katafunwa na butwaa zito. Lexi aliyasikia maneno hayo, naye akapandisha nyusi zake huku akiachia tabasamu kwa mbali.

"Nakupenda Nora. Ndiyo jambo jipya nililokuja kukwambia," Luteni Michael akanena kwa hisia.

"Michael... aam..."

"Siyo lazima unijibu leo. Najua nimekushtukiza kule hospitalini, na... nilikuwa nataka sana kukwambia hivi kwa muda mrefu nyuma ila... Nora nimekupenda. Ninaomba unipe nafasi kwenye moyo wako," Luteni Michael akamwambia.

Lexi akachekea kwa chini akiwaza ni jinsi gani jamaa alivyokuwa anajitafutia kuvunjika moyo mapema sana.

"Michael... ona... mimi... sijui nisemeje... kiukweli siko tayari kuwa kwenye mahusiano na mwanaume yeyote kwa sasa. Am so sorry," Nora akamwambia ukweli.

"Kwa nini?"

"Nina sababu zangu..."

"Sababu gani?"

"Michael!"

"Kama haujanipenda niambie tu dada yangu, sitaki kukaa nikisubiri kwa sababu nitaendelea kuumia..."

"Michael sisi siyo watoto... najua unaelewa ninachomaanisha..."

"Hapana, labda unieleweshe vizuri..."

Lexi akawaza; huyu jamaa vipi? Mbona kama analazimisha vile?

"Seriously? Luteni... tumetoka tu kutenganishwa kwa sababu apparently wewe ni hatari kwangu, si ndiyo? Hivyo nahitaji kuwa salama. Na wewe ukatia tiki kwamba ni sahihi..."

"Ni kitu ambacho kiko nje ya uwezo wangu, lakini kuwa nawe ninaweza. Kuwa pamoja nawe haitakuwa kama kazi Nora..."

"Luteni tafadhali... ni kama nilivyokwambia. Samahani sana..."

"Ona... samahani pia kwa kuwa nimepitiliza sana kihisia na... Nora... hii ndiyo mara yangu ya kwanza kufunguka namna hii kwa...."

Wakati Luteni Michael akiendelea kumwaga maneno yake ya moyoni, Lexi akaona achokoze.

"Mheshimiwa, ni nani, mbona umekawia?" Lexi akauliza.

"Aa... nakuja..." Nora akasema.

"Nani huyo?" Luteni Michael akauliza.

"Ni rafiki yangu..."

"Rafiki? Yaani umetoka hospitalini, sasa hivi unaniambia unahitaji kupumzika kumbe kuna mtu ndani?" Luteni Michael akauliza.

"Ish! Luteni una haki gani ya kuniuliza mimi maswali hayo? Umenioa?" Nora akauliza akiwa ameudhika.

"Kuna tatizo?" Lexi akasikika akiuliza.

Luteni Michael akampita Nora na kuingia mpaka ndani. Nora alishangazwa sana na jambo hilo.

"Lieutenant Michael! What do you think you're doing?" Nora akamuuliza kiukali.

Luteni Michael sasa akawa anamtazama Lexi uso kwa uso. Lexi hakuonyesha woga wa aina yoyote kumwelekea kwa jinsi alivyokuwa akimtazama.

"Kwa hiyo... kumbe huyu ndiyo 'rafiki' yako? Ninge-guess kumbe mara ya kwanza nilipomwona," Luteni Michael akamwambia.

"Michael, nakuomba uondoke..." Nora akasema.

"Bro, kuna shida gani?" Lexi akamuuliza Luteni.

"Usiniite bro, nitakuwasha sasa hivi!" Luteni Michael akamwambia kiukali.

"Michael!" Nora akamwita kwa hasira.

"Nakuomba ujaribu," Lexi akamwambia Luteni Michael bila kuogopa.

Luteni Michael na Nora wote wakamwangalia Lexi kimshangao kidogo.

"Unasemaje?" Luteni Michael akamuuliza.

"Nataka ujaribu kuniwasha!" Lexi akamwambia kiutulivu kabisa.

Luteni Michael akakunja uso kwa hasira, naye Nora akaingia katikati ya wawili hao.

"Luteni... naomba uondoke sasa hivi..." akamwambia.

"Nora... unanifukuza namna hiyo ukiwa na huyu mtu usiyemjua kabisa?" Luteni Michael akauliza.

"Unajuaje simjui? Na kwani mimi nilikuita hapa?"

"Unapaswa kuwa makini na watu unaowaingiza kwenye maisha yako Nora..."

"Get out..."

"Huyu mwanamke ulimleta mpaka kwenye condo letu, na sasa hivi ananichallenge ki...."

"Get out!" Nora akafoka.

Luteni Michael akamwangalia tu kwa ufupi, kisha akamtazama na Lexi kwa umakini, naye akaondoka hapo akiwa amevunjika sana moyo. Nora akamgeukia Lexi na kukuta ametazama pembeni.

"Lexi... samahani..."

"No... usiombe samahani. Niko sawa," Lexi akamwambia.

"Yaani... nashindwa kuamini Luteni Michael kati ya watu wote amefanya kitu kama hicho... sijui tu amekuwaje..."

"Usha'sikia kitu kinaitwa wivu wa mapenzi?" Lexi akatania.

Nora akatabasamu na kutikisa kichwa kwa kusikitika.

Lexi akamwangalia kwa sekunde kadhaa, kisha akaanza kusema, "Sikia... kuna kitu nataka nikwambie. Kiukweli..."

"Lexi... tafadhali usiongelee jambo lolote lenye kuvunja moyo. Watu wananisumbua, Michael tayari ameanza kuwa kikwazo kwangu... please just... tuigize kwa leo kwamba hakuna matatizo. Nahitaji sana kuituliza akili yangu. Utanisaidia?" Nora akamwambia kwa upole.

Lexi akashusha pumzi, kisha akatikisa kichwa kukubali.

"Okay, kwa hiyo... ungependa tufanye nini?" Lexi akauliza.

"Anything you want," Nora akajibu.

"Okay. Unaonaje tukienda kutembea? Say... labda shopping?" Lexi akasema.

"Ahahahah... nawe unafanyaga shopping?"

"Yeah. Huwa nafanya shopping kubwa asikwambie mtu... au, bado hauko fit ku..."

"Nipe dakika tatu nibadili nguo," Nora akasema huku akielekea sehemu yenye begi lake la nguo.

Lexi akawa anamwangalia kwa huzuni sana. Ilikuwa kidogo tu amwambie ukweli kuhusu yeye, ijapokuwa hakujua hiyo ingemwacha wapi. Lakini tena, fikira ya kwamba angewaponza wenzake kwa sababu tu ya hisia zake ikamfanya aliondoe wazo la kutaka kumwambia jambo hilo, na badala yake afurahie muda huu pamoja naye, haijalishi ungekuwa mfupi kadiri gani.


★★★★


Luteni Michael alirudi kwa timu yake akiwa ameudhika sana. Akafika na kukaa karibu na Bobby, ambaye kwa haraka aligundua kwamba kuna kitu kilimtatiza Luteni wake. Wanajeshi wale watano waliokuwa wameongezwa na Kanali Oswald kwenye timu hii waliitwa Rachel (36), Tariq (42), Manengo (40), Aliyah (30), na Zachary (39). Wanne walikuwa watanzania asilia, isipokuwa Tariq, ambaye alikuwa na asili ya uarabu, lakini alikuwa mswahili sana. Wote walikuwa na mafunzo mazuri ya kijeshi, na toka walipofika walikuwa wakisaidiana na "wenyeji" kama Alex, Mario na Hussein, katika kufatilia mambo kadha wa kadha.

Tokea usiku ule ACP Nora alipotekwa, wanajeshi hawa kwa pamoja walikuwa wanatafuta uwezekano wa kupata "server" zozote ambazo zilikuwa zimefichika nchini (aina fulani za kompyuta au programu za kompyuta zenye uwezo wa kupata taarifa na kuingia sehemu yoyote hususa kwenye mtandao). Walikuwa wakitafuta hizi kwa sababu waliona kwamba Mess Makers walikuwa wanapata taarifa nyingi na kufanya mambo mengi kitaalamu, hivyo bila shaka kungekuwa na pazia linalowaficha kitaalamu pia; teknolojia. Manengo pia alikuwa mtaalamu kwenye masuala ya teknolojia kama Bobby, na ni yeye ndiyo alitoa wazo hilo walilokuwa wakilifanyia kazi. Walitaka kujua ziko wapi hizo server ambazo Mess Makers walitumia na kama wangezipata, basi wangewapata wao.

Lakini kiukweli ilikuwa ngumu sana kufanikiwa katika hili kwa sababu ni kama Torres aliweka ukuta wenye nguvu sana kwenye mitambo yake ili usiweze kuvunjwa kirahisi. Mara zote ambazo timu ya Luteni ilikuwa ikikaribia kupata sehemu (location) yao, Torres angegeuza upande waliokuwa kwa kuwachanganya sana. Wangeona mara server hizo ziko Sweden, wakati huo huo ziko Sumbawanga, mara Cairo, yaani walishindwa kujua ipi ni halisi na ipi ni ya uwongo. Chanzo kikuu cha mitambo yake Torres alikificha kwa ustadi sana, ustadi ambao ulikuwa mtata sana kwa wataalamu hawa wa kijeshi kuufikia.

"Mmepata lolote lingine?" akauliza Luteni Michael.

"Hapana. Hizi zingine zinazojitokeza sehemu nyingi zinachanganya bado. Siyo rahisi kugundua ipi ni original au fake maana...." Manengo akaishia tu hapo.

"Kwa hiyo jamaa na wenyewe wamekuwa kama Cypher?" akasema Mario kiutani.

"Cypher ndiyo nini?" akauliza Luteni Michael.

"Ni kwenye... Fast and Furious..."

"Fast and Furious ndiyo nini?" Luteni Michael akauliza kiukali.

Wanajeshi wengine wakabaki kumtazama tu. Mario akabaki kimya.

"Luteni, alikuwa anatania tu," Bobby akamwambia.

"Sihitaji masihara kwenye kazi. Inaeleweka?" Luteni Michael akasema.

"Ndiyo mkuu," akajibu Mario.

"Labda mtu anayekuwa anawapa info hayuko nchini. Maana tungekuwa tumeshaikamata engine yao mapema sana," Aliyah akasema.

"Labda hata Marekani?" akauliza Mario.

"Labda hata Ujerumani," akasema Alex.

"Au labda ni mtu fulani tu anatuzunguka hapa hapa. Bobby... unamkumbuka yule dada aliyekuja humu siku ile?" Luteni Michael akamuuliza.

"Dada?" Bobby akauliza pia.

"Yule rafiki yake na ACP?" akauliza Alex.

"Ndiyo. Yule mwanamke siyo. Kuna jambo fulani kuhusu yeye ambalo haliko sawa. Kama vile anajua kitu, au anaficha kitu," akasema Luteni Michael.

"Ndiyo nani?" Rachel akauliza.

"Ni rafiki yake ACP Nora Lois. Lakini Luteni, anahusianaje na mambo haya sasa?" Bobby akamuuliza.

"Huyo mwanamke mara ya mwisho kuonana naye amenichallenge kabisa. Ananiambia nijaribu kumpiga kama naweza!" Luteni Michael akasema.

Wengine wakaanza kuangaliana kimaswali, isipokuwa Hussein, ambaye muda wote alikuwa anatazama sehemu moja.

"Kisa?" akauliza Alex.

"Mwanamke kukupa challenge inamaanisha ni mmoja wa Mess Makers?" akauliza Zachary.

"Siyo hivyo. Fikiria mara ya kwanza alikuja tu humu na kuingia... bila kuogopa chochote akaingia ndani humu. Ndiyo hiyo siku tulikuwa tumempata Oscar Amari, halafu ghafla kuna watu huko wakatokea kumsaidia. Unadhani walijuaje kwamba tungemfata?" Luteni Michael akasema.

"Kwa sababu wana njia zao nyingi hawa jamaa... kama ilivyokuwa Mwanza," akasema Alex.

"No, Alex. Mwanza Kevin Dass aliwasha tracker baada ya kutuona, na hata wenzake wakaja baadae sana. Huyu Oscar hakuwa na njia ya kujua tumeanza kumfata isipokuwa kuwe na mtu alimwambia mpaka kufanya wenzake wafike kabla hatujamshika. Think," akasema Luteni Michael.

"Kwa hiyo... huyo mwanamke... alipofika hapa aliona picha ya Oscar, akaenda kumwambia... labda kwa njia fulani lakini siyo simu, si ndiyo? Kwa hiyo yuko na Nora ili kupata taarifa muhimu kutoka kwetu, ndiyo unachosema Luteni?" Bobby akamwambia.

"Ndiyo ninachofikiri. Nyie mnaonaje?" Luteni Michael akawauliza.

"Inawezekana ikawa kweli. Kwa nini kwanza mliruhusu mtu aingie humu?" Tariq akaongea.

"Kaliingia tu utafikiri ni kwake humu. Nani anakakumbuka sura vizuri? Eeh? Alex?" Mario akauliza.

Alex akatikisa kichwa kukataa.

"Bobby?"

Akakataa pia.

"Hussein?"

Kimya.

"Oya, vipi?" Mario akamuuliza.

"Eeh? Yah... yeah namkumbuka... lakini mkiniambia tumchore siwezi," Hussein akajibu huku akiendelea kutazama sehemu ile akiwa anachezea ndevu zake laini taratibu.

Mario alipomtathmini vizuri, akatambua Hussein alikuwa analitazama kalio kubwa kiasi la Aliyah lililokuwa ndani ya suruali ngumu ya kardet, naye Aliyah alikuwa ameshatambua hilo ila akawa anapuuzia tu. Mario akatikisa kichwa kwa kukerwa.

"Hatuna muda wa kuanza kuita mchoraji. Manengo, search simu ya ACP utafute namba yenye jina 'Lexi,' kisha check usajili wa mtu huyo uangalie background zake zote. Naenda nje mara moja," Luteni Michael akasema huku akinyanyuka.

"Lakini Luteni... ACP... sidhani atafurahi kujua ikiwa..." Bobby akasema.

"Kwani ni lazima ajue?" Luteni Michael akauliza.

Wote wakakataa.

"Fanya hivyo. Mario, Hussein, mko nami," akasema Luteni Michael huku akiondoka.

Manengo akaanza upesi kazi aliyopewa. Mario akaanza kumfata Luteni Michael, naye Hussein akawa anarudi kinyume-nyume huku anamwangalia Aliyah. Aliyah alikuwa anamtazama pia kwa njia ya kutopendezwa, naye Hussein akamrushia busu kwa ishara ya mdomo huku akiwa amelegeza macho. Hii ikafanya baadhi ya waliobaki hapo kucheka kidogo, huku Aliyah akitabasamu kwa mbali na kutikisa kichwa.

"Hivi huyo jamaa anakuwaga makini kweli?" Zachary akauliza.

"Achana naye huyo, masihara huwa ndiyo fani yake," Bobby akasema.

"Hussein anaonekana kupenda sana masihara. Angalieni isije ikawa-cost," akasema Rachel.

"Yeah, toka tumefika amekuwa akifanya vitu kama teenager. Ana miaka mingapi?" akauliza Zachary.

"Acha kujaji sana Zach," Tariq akaongea.

"Ndiyo fani yake," Manengo akasema kiutani.

"Ana miaka 32. Na hapana.
Mambo anayofanya ni sehemu tu ya utu, ila kikazi yuko vizuri mno. Hussein naweza kusema labda ndiyo kijana makini zaidi kuliko wote humu ndani," Alex akamwambia Zachary.

"Kweli?" Rachel akauliza.

"Yeah. Baada ya kujuana naye vizuri mtaona hilo," akasema Alex.

"Siyo fair kwa Mario kutania ila ni fair kwa Hussein kutania, ndiyo unachosema?" Aliyah akauliza.

"Hamna. Luteni kuna kitu tu kinamsumbua. Huwa hayuko hivyo sikuzote. Amekuwa namna hiyo tokea...." Alex akaishia tu hapo.

"Tokea vifo vya wenzenu... inaeleweka. Naomba tusizungumzie hayo tena. Ila Aliyah sasa hivi una kupe mkiani kwa hiyo kuwa macho," Tariq akaongea kwa utani.

Wengine wakacheka kidogo, wakijua alimaanisha Hussein.

"Anyway, tunaweza kuendelea na mambo mengine...." akasema Bobby.

Wanajeshi hawa wakaungana na Manengo katika utafiti wake mpya.


★★★★


Lexi pamoja na Nora walielekea katikati ya jiji kutafuta viburudisho mbalimbali. Nora alifurahia kwelikweli uwepo wa Lexi karibu yake. Walikwenda kupata msosi wa nguvu pamoja, wakaangalia mechi ya alasiri pamoja, kisha wakaamua kwenda 'supermarket' ili kununua vitu vingi kwa ajili yao wote. Kwa wale ambao wangewaangalia, waliwaona kama dada wenye undugu tu wakiwa kwenye matembezi, lakini ndiyo walikuwa kwenye mwanzo wa pendo lao jipya.

Wakati wawili hawa walipokuwa wakielekea sehemu ya malipo kwenye supermarket hiyo, walikuwa wakiongelea mambo mengi yenye kufurahisha sana, na Nora alishindwa kujizuia kucheka mno kwa jinsi Lexi alivyokuwa na story nyingi za kuchekesha. Wakawa wamefika kwenye meza ya mahesabu, na mhudumu akawa anatoa bidhaa kupima bei (wanajua wenyewe wanavyofanyaga), huku Lexi akimsimulia Nora vichekesho fulani.

"Ahahahah... kwa hiyo hakurudi tena?" akauliza Nora.

"Hakuonekana kabisa!" Lexi akasema.

"Okay. Nyingine..."

"Mh... mheshimiwa haujachoka kucheka?" Lexi akauliza.

"Aahh... bado..."

"Ahahah... okay. Aam... kulikuwa na mwalimu mpya wa dini aliyehamia kwenye shule nyingine katikati ya muhula. Alipewa darasa la 6... nafikiri, ili afundishe hilo somo. Kwa hiyo kwenye kipindi chake cha kwanza akataka kujua wanafunzi walikuwa wanajua mambo mengi kadiri gani kuhusu mada walizojifunza kabla ya yeye kufika. Akaamua kuanza na mada ya mwisho ambayo mwalimu aliyepita aliishia kuwafundisha...."

"Mm-hmm..." Nora akamuasa kuendelea.

"Akawasalimu. Halafu akawauliza, 'Ni nani aliyeangusha kuta za Yeriko?'"

Nora akaanza kucheka kwa sauti ya chini kabla hata Lexi hajaendelea.

"Ahahah... ikapita dakika moja darasa zima likiwa kimyaaa. Wanafunzi wote walikuwa wanamwangalia tu. Kwa hiyo akachagua wale waliokaa madawati ya mbele waanze kujibu. Akaanza Amosi: 'Mwalimu mimi ni mgeni hapa, nilianza tu shule wiki iliyopita.' John: 'Mwalimu mi siku hizo kuta zilipovunjika sikuja shule, haki ya Mungu...'"

Nora akaendelea kucheka, na mhudumu yule wa mahesabu akawa anacheka pia.

Lexi akaendelea, "Mary akasema, 'Sir, mimi niliupita tu nikakuta umeshavunjwa, hata sikuugusa...'"

"Jamani..." Nora akasema huku akitabasamu.

Lexi akaendelea, "Mwingine akasema, 'Mwalimu yaani tena mimi ndo' kabisaaa hata sikujua kama umevunjika! Ndo najua sahivi.' Mwalimu akashangaa sana na kukasirika mno. Akaenda kwenye ofisi ya mkuu kumweleza kilichotokea. Mkuu akamwambiaje, 'Pole sana kuhusiana na hilo. Unajua watoto walivyo watukutu saa nyingine wanakuwa wanaharibu tu vitu vya watu afu wanakataa. Lakini usihofu, tutalitatua suala hili. Andika tu gharama yote inayohitajika ili kuutengeneza huo ukuta, halafu kwenye kikao kinachofuata tutalizungumzia hilo suala na wengine.'"

Nora pamoja na mhudumu yule wakawa wanacheka.

"Mwalimu mkuu na yeye walewale tu," akasema Nora.

"Acha kabisa," Lexi akasema.

"Kwa hiyo ikawaje?" Nora akauliza.

"Teacher wa dini akaacha kazi siku hiyo hiyo!" Lexi akamwambia.

Nora akacheka tena.

"Hiyo ni nzuri sana. Niliisomaga zamani sijui wapi..." yule mhudumu akawaambia.

"Eeh.. mimi pia. Kwenye mavitabu ya jokes... ya kiingereza," akasema Lexi.

"Eee ndiyo, ya kiingereza," mhudumu akahakikisha.

"Ahahah... basi mimi sikuwahi kufuatilia sana jokes yaani... sikujua ni nzuri sana mpaka...."

Nora alipokuwa anaendelea kuongea hivyo, Lexi akahisi nguo yake inavutwa kwa nyuma, naye akageuka upesi akifikiri kuna mtu anataka kumwibia. Lakini hakukuwa na mtu mzima hapo, bali msichana mdogo aliyekuwa anamwangalia kwa makini. Lexi akatabasamu na kuchuchumaa, akimtazama kirafiki. Nora alipomwangalia Lexi na msichana huyo, akakunja uso wake kimaswali.

Msichana huyu alikuwa amevalia gauni la mtindo wa jeans ya samawati, ambalo liliishia magotini, na viatu vya rangi ya pink vyenye manyoya. Alikuwa mweupe, na nywele zake zilisukwa kwa mtindo wa mabutu makubwa kuzunguka kichwa chake. Kwa kumwangalia, kadirio la umri wake ingekuwa ni kati ya miaka mitano mpaka saba. Kilichomshangaza Nora ni kwamba macho ya msichana huyo yalifanana kabisa na macho ya Lexi, lakini Lexi hakuwa ametambua hilo.

"Hi, mambo?" Lexi akamsalimu.

"Poa," akajibu msichana huyo.

"Nambie mrembo. Umekuja kununua nini?" Lexi akamuuliza.

"Soseji, sneakers, diapers, na mavitu mengi," akajibu.

"Ahahahah... hizo diapers ni kwa ajili yako?" Lexi akauliza.

"No. Ni za mama," kakajibu na kuwafanya watatu wale wacheke.

"Mama yuko wapi?" Nora akauliza.

"Yupo huko... najificha asinione," akajibu.

"Kwa hiyo unamsumbua mama yako makusudi ili akutafute?" Nora akauliza.

"Ndiyo. Mpaka aninunulie ice cream," kakajibu.

"Aaaa... hapo umefanya la maana," Lexi akamwambia.

"Dada, unafanana na huyo mtoto, ni ndugu yako?" mhudumu wa mahesabu akamuuliza Lexi.

"Nini?" Lexi akauliza.

"Nilifikiri ni mimi tu labda, kumbe na wewe umeona?" Nora akaongeza.

"Ndiyo, mnafanana," mhudumu akamwambia tena Lexi.

Lexi akatabasamu tu na kumwangalia huyo mtoto.

"Eti ni kweli tunafanana?" Lexi akamuuliza kirafiki.

"Ndiyo. Mama aliniambia umekufa lakini leo nimekuona," mtoto huyo akajibu.

Lexi na Nora wakakunja sura zao kimaswali. Wakaangaliana kama kuulizana mtoto alikuwa anaongea nini huyu, kisha Lexi akamtazama tena msichana huyo.

"Unaitwa nani?" akamuuliza.

"Alexa," mtoto akajibu.

Lexi akashangaa.

"Alexa? Jina lako linataka kuendana kidogo na la huyu. Anaitwa Lexi. Alexa na Lexi," Nora akamwambia kwa shauku.

Lexi akawa bado anamwangalia mtoto huyo kimaswali.

Simu ya Nora ikaanza kuita, naye akasogea pembeni kidogo kupokea. Mhudumu wa mahesabu akamwambia Lexi gharama ya vitu walivyonunua, naye akanyanyuka ili alipie. Lakini, kutokea nyuma yake, alianza kusikia sauti ya mwanamke ikiita jina la 'Alexa,' naye Alexa akacheka kidogo na kujificha karibu na miguu ya Lexi; akiing'ang'ania. Lexi alikuwa ameangalia mbele tu, kwa sababu ya mapigo yake ya moyo kukimbia kwa kasi sana baada ya msisimko mkubwa kuuvaa mwili wake. Aliifahamu sauti hiyo vizuri sana.

"Hivi wewe, nimeshakwambia nini kuhusu... mmm?"

Mwanamke huyu akasikika akiongea hivyo nyuma ya Lexi, naye Alexa akawa anacheka huku akimpiga chenga kwa kwenda huku na huku usawa wa miguu ya Lexi.

"Dada samahani sana... watoto kama ujuavyo..."

Mwanamke huyo akamwambia Lexi hivyo akihofia labda hakupenda mchezo aliokuwa anafanya Alexa. Lakini Lexi alipogeuka tu kumtazama, mkoba aliokuwa ameushika mwanamke huyu ukamponyoka kutoka mkononi mwake na kudondoka chini, akiwa anamwangalia Lexi kwa mshangao. Lexi alikuwa anamtazama kwa umakini sana, huku machoni chozi likijaa haswa, na mwanamke huyo akaonekana akianza kutetemeka midomo.

"Ss... Xander?!" mwanamke huyo akaita kwa sauti yenye kutetemeka.

Lexi akadondosha chozi huku akihisi mkono wake umeishiwa nguvu.

"Valentina," Lexi akasema kwa hisia.



★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA

★★★★★★★★★★★★★★★★★


Nora akawa amemaliza kuongea na aliyempigia na kurudi usawa wa Lexi. Alikuwa anataka amsemeshe jambo fulani, lakini akasitisha baada ya kuona Lexi alikuwa anadondosha chozi. Akamwangalia na Valentina, ambaye alikuwa anadondosha machozi pia huku Alexa akimuuliza nini tatizo.

"Lexi... what's wrong?" Nora akamuuliza.

Lexi akajifuta chozi haraka.

"Hamna kitu. Niko sawa," Lexi akajibu.

Valentina pia akajifuta machozi na kumwambia binti yake alikuwa sawa, naye akaendelea kumtazama Lexi. Nora alikuwa anawaangalia wawili hawa kimaswali sana.

"Mnafahamiana?" Nora akauliza.

"Ndiyo ni... rafiki yangu wa zamani. Ni kitambo sana. Sikudhani ningekuja kumwona... tena," Lexi akamwambia.

"Ooh... sawa. Habari yako dada? Naitwa Nora," Nora akamsalimu Valentina.

"Ah... safi. Naitwa Va..Valentina," yeye pia akajitambulisha huku bado akimtazama Lexi.

"Lexi... kuna dharura imetokea. Mdogo wangu... nahitaji kwenda kumwona ila..."

"Usijali Nora. Wewe nenda tu," Lexi akamwambia.

"Lakini vipi kuhusu..." Nora akauliza huku akiangalia vitu walivyonunua.

"Usijali. Nitavipeleka kwa apartment yako. Sijui kama funguo una..."

"Oh, no, tunaacha. Nitawapigia kuwajulisha unazichukua. Asante, ngoja niwahi. Nita... nitakukuta siyo?" Nora akaongea haraka.

"Yeah... utanikuta," Lexi akamwambia huku akimtazama Valentina.

Nora akamwangalia kwa ufupi Valentina, kisha akawaaga kwa pamoja na kuondoka.

Kwa kuwa walitumia gari la Lexi kwenye matembezi yao, Nora akalichukua ili kwenda alikokuwa mdogo wake, naye Lexi angechukua taxi ili impeleke hotelini kwa Nora baadae. Lexi na Valentina wakabaki hapo wakiwa wanatazamana kwa hisia sana. Kisha Lexi akakusanya vitu vyake vilivyowekwa kwenye mifuko sasa na kusogea pembeni bila kumsemesha Valentina lolote. Alexa akawa anamwambia mama yake manano mengi kama 'huyu si ndiyo yule uliyenionyesha kwenye picha' na 'si ulisema amekufa,' naye Valentina akawa hawezi kujibu lolote lile na kubaki kumwangalia tu mtu aliyedhani kweli alikufa.

Lexi akamwonyesha Valentina ishara ya kichwa kuwa amfate, kisha akaanza kuondoka hapo bila kusema lolote. Valentina akajituliza na kumshika mkono mwanae, nao wakaenda sehemu ambayo aliacha kifaa cha kubebea vitu alivyonunua na kuanza kuvipeleka kwenye mahesabu. Mapigo ya moyo ya mwanamke huyu yalidunda kwa kasi sana, akiwa na maswali mengi na matarajio yaliyopita kiasi. Baada ya kumaliza kulipia, naye akabeba mifuko iliyowekewa vitu vyake na kuanza kuelekea nje.

Alipotoka tu, akatazama huku na huku akimtafuta Lexi, naye Alexa akamwonyesha kwa kidole kwamba 'yule pale,' kana kwamba alijua mama yake alikuwa anamtafuta. Valentina akamwona Lexi akiwa amesimama nyuma ya gari fulani huku mifuko yake ikiwa chini, naye akaanza kuelekea sehemu hiyo huku Alexa akitangulia mbele. Lexi akanyanyua mkono wake mmoja kumwonyesha Alexa 'ice cream' ya maziwa na chokoleti iliyofunikwa kwa karatasi lake, naye Alexa akaanza kumkimbilia huku anafurahi. Akafika tu usawa wake na kuikwapua, kisha akaanza kuifungua na kulamba. Lexi akawa anamwangalia mtoto huyu huku anatabasamu, na baada ya Valentina kufika hapo karibu, wakatazamana kwa mara nyingine.

Valentina sasa alikuwa mtu mzima hata zaidi, mwenye miaka 38, lakini mwonekano wake bado ulikuwa mzuri kama wa kijana mdogo. Alipendeza. Wakati huu alikuwa amevaa blauzi nyepesi ya njano yenye uwazi katikati ya kifua chake, na suruali yenye rangi ya maroon iliyombana vyema. Uso wake mzuri ulipendezeshwa kwa make up ya kadiri, naye Lexi akatambua kwamba mwili wa Valentina ulikuwa umeongezeka kiasi, yeye hasa akifurahia zaidi hips zake. Akamshusha mpaka kwenye hips hizo na kutazama hapo zaidi, kwa njia ya uchokozi tu.

"Xander... au... I dont... sielewi... nini kinaendelea?" Valentina akasema.

Lexi akaona kwamba bado Valentina alikuwa na upole wake ule ule.

"Nitakueleza Valentina. Usijali," Lexi akamwambia.

Valentina akaendelea kumwangalia tu usoni. Lexi akamtazama Alexa kwa umakini, kisha akamwangalia na mama yake pia. Valentina akaangalia tu pembeni kwa kuwa alielewa Lexi alichokuwa anauliza. Lakini ilikuwa ni ngumu kiasi kumjibu kwa ishara hasa ukitegemea tayari na yeye alikuwa na maswali mengi ya kuuliza.

"Umenenepa," Lexi akamwambia.

"Tunamwitaga bonge nyanya," Alexa akasema.

Lexi akacheka na kuuliza, "Wewe na nani mnamwitaga hivyo?"

"Na baba," Alexa akajibu.

Lexi akamtazama Valentina, naye akamwangalia. Kisha akaangalia kiganja chake cha kushoto na kuona pete.

"Alexa, shika funguo. Tangulia kwenye gari, nakuja," Valentina akamwambia.

Alexa akazipokea.

"Asante kwa ice cream aunty. Tutaonana tena unipe nyingine, si eti?" Alexa akamwambia Lexi.

"Hmmm... ningependa kama ungeendelea kuwa unamsumbua mama, ila sawa. Tuna dili," Lexi akamwambia.

Alexa akacheka na kuanza kuelekea kwenye gari lao.

"Aunty?" Lexi akamuuliza Valentina.

"Angalau nilimwambia kukuhusu," Valentina akasema.

"Mimi kama mwanamke au mwanaume?"

"Xander huyo ni mtoto. Angeelewa vipi kilichowapata nyie, si angeniona mwendawazimu?"

"Mmm... sawa. Naona kweli ume-move on. Unapendeza sana Valentina," Lexi akamwambia.

"Ona... nahitaji kwenda. Namba zangu hizi hapa..." Valentina akasema huku anampa kadi ndogo.

"Kirefu cha Alexa ni nini?" Lexi akauliza.

Valentina akamwangalia tu.

"Ilikuwaje... ilikuwaje uka..."

"Xander... kama wewe tu ulivyoniambia utanieleza... mimi pia nitakueleza, lakini si sasa. Tutaonana. Usiache kunitafuta," Valentina akasema.

"Na wewe usimwambie yeyote kuhusu mimi kuwa hai. Utaweza?" Lexi akauliza.

Valentina akatikisa kichwa kukubali ijapokuwa hakuelewa ni kwa nini.

Horn za gari fulani zikaanza kupiga sana, naye Valentina akatikisa kichwa huku akiondoka. Lexi akatabasamu akijua ilikuwa ni Alexa ndiyo anamwambia mama yake awahi eti, lakini tabasamu lake likageuka na kuwa simanzi nzito. Kitu alichokuwa amegundua wakati huu ni kitu ambacho hakuwahi kutazamia kabisa kwenye maisha yake kwamba kingekuja tokea. Alikuwa na mtoto. Akainamisha kichwa chake kwa kusikitika, kisha akabeba tu mizigo yake na kuelekea sehemu ya barabara. Akaita taxi moja, naye akaingia na kuanza kuelekea hotelini kwa Nora.


★★★★


Nora alikwenda mpaka kwenye nyumba ya mdogo wake, Asteria. Muda ule wakati yuko supermarket, alikuwa amepigiwa simu na rafiki ya mdogo wake ambaye alimjulisha kwamba hali ya Asteria kwa siku chache zilizopita haikueleweka. Alikuwa nyumbani tu, akinywa pombe kupita maelezo na kulia huku anafanya fujo nyingi.

Rafiki yake aliitwa Germana (kifupi Gema). Huyu alikuwa ni wale marafiki ambao wanang'ang'ania wenzao wenye pesa ili na wenyewe watoke, lakini alimjali Asteria, na hali hiyo iliyoendelea ilimtatiza sana. Aliamua kumpigia simu Nora kwa sababu sasa Asteria alikuwa amejifungia kwenye chumba chake tangu jana, na kila mara alipomwita hakumjibu. Kwa hiyo aliogopa na kumwambia dada yake ili aje kumsemesha.

Nora alifika na kuelekea ndani kule upesi. Kwa mara ya kwanza kabisa akaingia ndani ya nyumba hiyo. Hangejali tena nini kilifanya asitake kuingia hapo, kwa kuwa mdogo wake alikuwa wa muhimu zaidi kuliko chuki yoyote aliyokuwa nayo kumwelekea baba yao. Akafika getini na kupiga kengele, na baada ya sekunde chache Gema akafungua.

"Eh, afadhali dada... sh'kamoo?" Gema akamsalimu.

"Marahaba. Huyo vipi?" Nora akauliza huku akiingia haraka.

"Yaani hata sielewi kiukweli. Tokea majuzi amekuwa ovyo tu. Sijui mpenzi wake amemwacha... yaani sielewi," Gema akasema.

"Ah... yaani nyie watoto jamani!"

Nora akaongea hivyo kwa wasiwasi huku anapandisha ngazi baada ya kufika ndani.

Nyumba hii ilikuwa ya ghorofa moja, nayo ilikuwa pana yenye vyumba vichache tu lakini maridadi sana. Kwa kijana mdogo kama Asteria kuwa na nyumba tayari ilikuwa ni full kujiachia na kuburudika na marafiki tu hapo, kwa hiyo mpangilio wa vitu mara nyingi ungekuwa shaghaalabaghala mpaka siku yeye na rafiki yake wakiamua kufanya usafi wenyewe. Asteria bado alikuwa anasoma chuo kikuu, mwaka wa pili kwenye kozi ya kilimo. Na mbwembwe zake zote haikujulikana kwa nini alichagua kozi hiyo, ingawa kama ungemuuliza angesema tu anaipenda.

Baada ya Nora kufika nje ya mlango wa chumba cha Asteria, akajaribu kuufungua lakini haukufunguka. Akaanza kumwita sana, lakini hakujibu. Nora akamwambia kwa kumtisha kwamba endapo kama asingefungua basi angeuvunja mlango, na anajua nini kingefuata ikiwa Nora angechukua hatua hiyo.

Zikapita sekunde kadhaa za ukimya, na mlango ukasikika ukifunguliwa kwenye kitasa. Nora akaufungua na kuingia ndani, na hapo akakuta mambo mengi yakiwa yamekaa ovyo ovyo tu. Akamwangalia Asteria kwa ufupi, ambaye alikuwa amevaa khanga moja kutokea kifuani, huku nywele zake zikiwa zimevurugika sana kichwani. Sakafuni kulikuwa na chupa nyingi za pombe, naye Asteria akasimama usawa wa kitanda na kumwangalia dada yake.

Nora alimtazama mdogo wake kwa hisia kali sana. Alitaka kujua ni nini iliyokuwa maana ya haya yote aliyokuwa anafanya.

"Umechanganyikiwa?" Nora akauliza.

Asteria akabaki tu kumwangalia kwa njia fulani kama mtu mwenye usingizi. Gema akaingia ndani hapo pia na kusimama mlangoni.

"Ongea. Nini maana yake?" Nora akauliza tena.

"Kwani unataka nini Nora? We si una kazi huko za kufanya? Niache tu mimi nitakuwa sawa," Asteria akasema.

"Unasemaje? Ndiyo nina kazi za kufanya, na isingekuwa ya huu upuuzi wako ningekuwa sehemu fulani sasa hivi. Utaendelea kujiendekeza mpaka lini? Kua Aste. Unajirarua namna hiyo kwa faida gani? Yote haya kwa sababu ya mapenzi?" akauliza Nora kwa hisia.

"Ndiyo! Nilikuwa nampenda sana. Hauwezi kuelewa ameacha pigo kubwa namna gani ndani ya moyo wangu," Asteria akasema kwa hisia.

"Kwa hiyo... ukifanya haya yote ndiyo atakurudia?" Nora akauliza.

"Hawezi. Lakini kama ni kuendelea nitaendelea tu...."

Nora akamkaribia na kumtandika kofi zito usoni. Asteria akakaa kitandani huku akilia, na kuweka kiganja chake kwenye shavu huku ameinamia kitanda.

"Utaendelea kuwa mpumbavu mpaka lini? Eeh?" Nora akauliza.

"Nimekwambia hauwezi kunielewa," Asteria akasema huku bado analia.

"Nielewe nini? Nielewe nini?" Nora akauliza.

"Amekufa," Asteria akajibu.

Nora akatulia kidogo na kumwangalia tu.

Asteria akamgeukia na kusema, "Wamemuua."

"Nini?" Nora akauliza kimshangao.

Asteria akaendelea tu kulia.

Ikambidi Nora asogee karibu yake na kupiga magoti chini, kisha akamshika mikono na kumwangalia machoni kwa umakini. Gema akaingia na kusogea mpaka karibu.

"Nini kimetokea?" Nora akauliza kwa kujali.

"Yaani hata sielewi. Nilikuwa naye... kidogo tu nashangaa ananiambia... nisimjue tena... hhh... Nikam..nikamtafuta... lakini sikumpata. Ndiyo nikaja kumwona... TV... eti amekufa...." Asteria akasema na kuanza kulia tena.

Nora akahisi vibaya sana kwamba alimpiga mdogo wake wakati alikuwa kwenye maombolezo. Akamkumbatia na kuanza kumbembeleza, huku akijitahidi kuyazuia machozi yake kumwagika. Akapanda kitandani na kukaa, huku kichwa cha Asteria kikiwa kifuani kwake akiendelea kumbembeleza.

"Pole Aste... pole sana dear," akasema Nora.

Asteria akawa anajitahidi kujikaza.

"Ulikuwa unasoma naye?" Nora akauliza.

Asteria akatikisa kichwa kukataa.

"I'm sorry. Sikuwahi hata kukutana naye. Pole sana mdogo wangu," Nora akamwambia.

"Pole Aste. Me mwenyewe sikujua," Gema akasema.

"Lakini Aste, umesema wamemuua. Inamaanisha nini? Nani amemuua?" Nora akauliza.

"Me hata sielewi. Wanasema ameuliwa na wale... Mess Makers," akasema Asteria.

Nora akashangaa. Akanyanyua kichwa cha mdogo wake na kumtazama usoni.

"Boyfriend wako aliitwa nani?" akamuuliza kwa umakini.

"Oscar," akajibu Asteria.

Nora akaangalia chini akiwa amechoka akili. Mbona mchezo huu wote ulikuwa na mizunguko mingi namna hii? Aliwaza sana ni kwa nini mambo mengi yalikuwa yanatokea kwa njia hii tokea kundi la Mess Makers lilipozuka, lakini akakosa jibu. Sasa akawa anajiuliza ikiwa Oscar alikuwa anatoka na mdogo wake kimakusudi au la.

"Huyo Oscar... ulikutana naye wapi?" Nora akauliza.

"Mitaa fulani... zamani," akajibu Asteria.

"Zamani... yaani miaka mingi?"

"Kama miwili..."

"Kwa hiyo mli-date kwa miaka karibia miwili?"

Asteria akatikisa kichwa kukubali.

"Okay. Umesema... mara ya mwisho ulipokuwa naye nini kilitokea?" Nora akauliza.

"Hata sielewi. Tulikuwa wote... sijui nini kikampata akaanza tu kupasua simu, akaitupa chooni, halafu akaniambia nisimwambie yeyote kama ninamjua kwa sababu... maisha yangu yangekuwa hatarini. Sikumwelewa... yaani ni kama alijua kwamba siku hiyo angekufa... hhh... sielewi hao watu walitaka nini kutoka kwake, alikuwa kijana wa kawaida tu..." akasema Asteria kwa huzuni.

"Kwa hiyo ni kama kuna watu wengine wamemuua halafu polisi wakawasingizia Mess Makers?" Gema akauliza.

"Hata sielewi..." Asteria akasema.

Nora alikuwa anawaza mambo mengi, lakini kwa sasa alihitaji kwanza kumtuliza mdogo wake. Akamfuta machozi na kumwambia asiogope kwa sababu kila kitu kingekuwa sawa. Kwa sababu Asteria hakujua ikiwa dada yake alijihusisha na msako wa Mess Makers, Nora akamsihi kwamba afuate ushauri wa mwisho wa mpenzi wake, kwamba asimwambie mtu yeyote kuwa alitoka naye kimapenzi, na ikiwa ingetokea watu fulani wenye vyeo vya usalama wakamuuliza, basi angepaswa kumwambia yeye kwanza ili amsaidie kushughulika nao.

Dada mkubwa akaendelea kukaa hapo na mdogo wake, akimsaidia kuondoa mkazo na kumtia moyo zaidi ili afarijike.


★★★★


Lexi alirejea hotelini alikoishi Nora kwa sasa na kuelekea kwenye chumba chake moja kwa moja. Giza lilikuwa limeshaingia, ikiwa ni saa 1 sasa. Aliweka mizigo pembeni, naye akaketi sehemu ya kitanda akitafakari mambo mengi. Kukutana kwake na Valentina kulikuwa jambo ambalo hakutazamia hata kidogo. Na tena kuongezea utata wa hali hiyo ni kujua kwamba alikuwa na mtoto pamoja naye, ambaye hakujua kumhusu pia. Alianza kuwaza ingekuwa vipi kama kipindi kile mambo yote yale mabaya yasingetokea, inamaanisha labda leo angekuwa pamoja na binti yake na mama yake pia.

Kwa jinsi ambavyo maisha yao yalikuwa yamebadilika, nani angeamini sasa hivi ikiwa angekwenda na kusema yeye ndiyo "baba" wa huyo mtoto, wakati alionekana kuwa mwanamke? Alianza kumkumbukia Alexa, jinsi alivyokuwa mzuri na mashavu yake makubwa, naye akatabasamu kwa hisia. Lakini pia alithamini sana kwamba Valentina hakuficha ukweli kutoka kwake ingawa ndiyo walikuwa tu wamekutana baada ya miaka nane, naye akawa anatazamia kwa hamu kuja kuonana naye tena.

Wakati akiendelea kutafakari hayo, ujumbe wa Nora ukaingia kwenye simu yake, akiuliza kama bado alikuwepo hapo, naye Lexi akajibu kwa kusema ndiyo, ila aliboeka kukaa peke yake. Nora akamwambia angefika muda siyo mrefu; ampe kama dakika 15 tu. Baada ya Lexi kukubali, akafumba macho kwa sekunde chache, kisha akanyanyuka kutoka alipoketi na kwenda kwenye vitu vya Nora. Alianza kupekua vifaa vyake vingi, akitafuta hasa makaratasi au makablasha ili kuona kama angepata jambo lolote lililohusiana na kazi ya Nora ya kuwatafuta Mess Makers.

Alipekua na kupekua lakini hakupata taarifa zozote zenye kuvuta umakini wake. Ndipo akasikia sauti nyuma yake.

"Unafanya nini?"

Macho ya Lexi yakakaza huku akitazama mbele. Alikuwa amechuchumaa, hivyo akasimama akiwa anahisi hasira sana na kugeuka nyuma yake. Ilikuwa ni Luteni Michael.

"Unaingia vipi humu bila hodi?" Lexi akamuuliza.

Nyuma ya Luteni Michael walikuwa ni Mario na Hussein.

"Hodi siyo kitu ambayo wewe unajali, kwa hiyo tusipotezeane muda. Nataka useme unafanya nini ndani hapa," Luteni Michael akamwambia.

"Siwezi kukwambia nafanya nini hapa mpaka uniambie kwa nini hujapiga hodi," Lexi akasema.

Hussein akatabasamu na kusema, "I like you."

"Asante. Mimi pia," Lexi akamwambia.

"Mnaona jinsi hicho kiburi kilivyojaa usoni kwake? Nani ameshawahi kuwafanyia hivyo akijua kabisa nyinyi ni nani?" Luteni Michael akawaambia wenzake.

"Kwa hiyo kwa sababu wewe ni mwanajeshi ndiyo napaswa kutetemeka sanaaa? Cheo ulichonacho hakipaswi kuogopwa. Wewe upo kwa ajili ya wananchi, siyo kwa ajili ya kuogopwa," Lexi akamwambia kwa ujasiri.

Luteni Michael akamtazama kwa hasira.

"Kaa kimya, mshenzi wewe! Unaongea na sisi namna hiyo, nitakupasua sasa hivi!" akasema Mario.

"Oya, ndo' nini sasa? Swagger gani hizo kama makoplo, tena wale masharobaro wa chihaya?" Hussein akamwambia Mario kiutani.

"Em' niache na we naye," Mario akasema.

Luteni Michael akamsogelea Lexi karibu zaidi. Lexi hakuonyesha woga wowote ule na kumwangalia tu usoni kwa njia ya kawaida.

"Wewe ni nani?" Luteni Michael akamuuliza.

"Naitwa Lexi," akajibu.

"Wenzako wako wapi?"

"Wakina nani?"

"Kama unajali sura yako, ongea kila kitu sasa hivi. La sivyo nitakuumiza," Luteni Michael akamwambia kiutulivu.

"Hivi wewe una shida gani? Unanitaka nini mimi? Au hii yote ni kwa sababu ya Nora? Kwa sababu amekukataa?" Lexi akamwambia.

Mario na Hussein wakaangaliana kimaswali.

"Ninakupa sekunde...."

"Hata usijisumbue. Kama unataka kunipiga anza. I dare you," Lexi akasema.

Luteni Michael akakunja ngumi kwa kuhisi hasira kali sana. Mario na Hussein wakawa wametulia tu wakisikilizia nini kingefuata. Luteni Michael akamsogelea Lexi mpaka karibu kabisa na mdomo wake akimwangalia kwa hasira, naye Lexi akanyanyua kidevu juu akimtazama bila hofu.

"Sababu moja inayofanya nisikuue hapa hapa sasa hivi ni kwamba haitaonekana kuwa haki, lakini hiyo haimaanishi siwezi kukutia dole. Hiki kiburi chako kitakwisha leo leo," Luteni Michael akamwambia hivyo.

Kisha akaishika sehemu ya Lexi ya siri na kuiminya kwa nguvu. Lexi alikasirika sana! Akampiga kichwa cha pua na kufanya Luteni Michael arudi nyuma kidogo. Kisha mwanaume huyo akamfata Lexi tena na kumpiga kofi zito usoni, naye Lexi akadondokea kitandani akikunja ngumi kwa kuhisi hasira kali. Mario na Hussein wakawa wanamwambia Luteni wao asimfanyie mwanamke huyo jambo lolote baya, lakini Luteni Michael akamfata kitandani hapo na kumshika shingoni kisha kumvuta kuelekea uso wake.

"Unajifanya mbabe si ndiyo? Sasa ngoja nikuonyeshe!" Luteni Michael akamwambia.

Kisha akamvuta na kumsukuma upande ambao Mario na Hussein walikuwa wamesimama, naye Hussein akamwahi na kumdaka kabla hajaanguka chini vibaya.

"Asante..."

Lexi akamwambia hivyo Hussein, naye Hussein akamwonea huruma kiasi.

"Mwachie," Luteni Michael akamwamuru Hussein.

"Luteni... hivi unavyofanya siyo sawa. Hata kama angekuwa mmoja wa Mess Makers, huyu ni mwanamke, hupaswi kumpiga hivi. Na vipi ACP aki...."

"Nimesema mwachie!" Luteni Michael akamwambia kiukali huku amemnyooshea kidole.

Hussein akamwachia Lexi na kusimama, ambaye pia akasimama na kumgeukia Luteni Michael.

"Unataka kupigana? Come to me," Luteni Michael akasema.

"Oh, no. By all means, ring's yours (hapana... kwa mambo yote, ulingo ni wako)," Lexi akasema kwa ujasiri.

Luteni Michael akatabasamu na kuwaambia wenzake, "Hivi mnaweza kuamini kabisa mwanamke huyu ananichallenge mimi?"

"Kwani wewe ni nani? Wewe ni binadamu kama wengine tu. Hakuna chochote kilicho chenye ubora kuhusu wewe kinachopita kile cha mtu anayekaa kuombaomba pesa barabarani. Tena naweza kusema hata mtu wa namna hiyo ni bora kuliko wewe, kwa sababu ijapokuwa ana hali ngumu, angalau anajua anapotakiwa kuwa. Wewe je? Unajua unapotakiwa kuwa? No. Kwa sababu unafuata tu kila unachoambiwa na viongozi wako kama mbwa!" Lexi akasema.

Luteni Michael akamfata na kwa hasira akampiga ngumi usawa wa mdomo wake. Mario na Hussein wakashangaa sana na kusogea pembeni, kwa kuwa Lexi alianguka na kuanza kutambaa kuelekea mlangoni taratibu. Luteni Michael akamfata na kuzishika nywele zake kwa nguvu, akimvuta kumsimamisha juu. Kisha akamsogelea sikioni kwake huku mkono mmoja akiuweka kwenye shingo yake.

"Nani unamwita mbwa, malaya wewe? Umekosa mwanaume wa kukupa watoto ukahamia kwenye mashine za usagaji, si ndiyo? Sasa kuanzia leo uta...."

Kabla hajamaliza kuongea, mlango wa kuingilia ndani ya chumba hiki ukafunguka. Ilikuwa ni ACP Nora! Alifika tu ndani hapo na kukuta Lexi akiwa ameshikiliwa namna hiyo, huku uso wake ukionyesha maumivu. Alichoka! Luteni Michael akashtuka moyoni, naye akamwachia Lexi, ambaye alidondoka chini huku akipumua kwa nguvu. Yaani Nora alishindwa hata kuongea, alishindwa hata kujongea, alishindwa kuelewa nini kilikuwa kinaendelea. Mario na Hussein wakatazamana kama kuambiana 'haya sasa,' naye Lexi akamtazama Nora usoni huku mdomo wake ukitoa mchirizi wa damu.



★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
Back
Top Bottom