335
Usiku huu Amanda alikuwa amevaa kitu fulani hivi
very expensive,
made by Channel. Kilikuwa kigauni fulani
amazing cha rangi ya
pink chenye kumetameta na kung’aa kilipomulikwa na mwanga wa taa, kigauni kile kilimbana na kuishia juu kidogo ya magoti yake na kuifanya miguu yake milaini na minene kidogo kuonekana kwa uzuri. Kwa kigauni kile niliweza kuiona michirizi fulani nyuma ya miguu yake, na hapo nikajikuta nikisisimkwa mwili wangu kila nilipomtazama.
Kana kwamba hiyo ilikuwa haitoshi, kigauni alichovaa kilishonwa kwa namna ambayo kiliacha nusu ya kifua chake wazi na hivyo kukifichua kidani cha asili chenye herufi ‘A’ kilichokuwa kimenasa vyema kwenye shingo yake ndefu na kupotelea katikati ya uchochoro wa matiti yake makubwa kiasi yenye chuchu imara zilizotuna na kulisumbua kidogo gauni lake.
Pia kigauni hicho kilikuwa kimeyashika vyema mapaja yake makubwa yaliyoshikiliwa na nyonga pana na nyuma alikuwa amefungasha mzigo mkubwa kiasi, usiochukiza kuutazama, wa makalio na pia kutokana na kigauni chake kubana ilisababisha shanga na mistari ya mkanda wa nguo ya ndani viweze kujichora na kuonekana waziwazi. Ilikuwa ni aina ya zile chupi za vimikanda vya kupita kiunoni na vijitambaa vidogo tu vya kufunika mbele.
Dah, kila nilipokitupia jicho kiuno chake na kuziona zile shanga nilihisi pumzi zikinipaa na mapigo ya moyo wangu kwenda mbio isivyo kawaida. Miguuni Amanda alikuwa amevaa sendo ghali za kike za rangi ya
pink na alikuwa amebeba mkoba mzuri wa ngozi ya mamba wa rangi ya
pink. Kwa kifupi usiku huu ni kama vile Amanda alikuwa amepanga kunipa tabu baada ya kugundua nilikuwa dhaifu wa vidosho kama yeye!
The attraction was so obvious kiasi kwamba kuna wakati nilijikuta nikimgusa hapa na pale wakati tukipiga soga, pasipo sababu yoyote ya msingi ilimradi tu niuguse mwili wake wenye ngozi laini. Haha, mimi bhana! Kuna wakati nilianza kumhurumia sana Rehema kuwa na mume wa aina yangu, maana… dah… ngoja niachane na hizo nisije nikapoteza lengo ya simulizi yangu.
Sofia pia hakuachwa nyuma, usiku huu alikuwa amevaa gauni zuri refu la rangi nyekundu
brand ya
Luis Vuitton, lililokuwa liking’aa kila limulikwapo na mwanga wa taa. Shingoni alikuwa amevaa mkufu mdogo wa dhahabu wenye kung’aa na mkononi alikuwa na pochi ndogo nyekundu. Chini alikuwa amevaa viatu vyekundu vya mchuchumio vyenye visigizo virefu.
The sisters looked like heaven angels.
Wakati tukielekea Capital Social Club, ndani ya gari la Almasi sauti ya muziki wa
reggae remix ya wimbo wa Laura Branagan ilisikika toka kwenye spika za redio iliyofungwa kwenye gari lile, ilikuwa ni
full kuinjoi, tuliimba na kucheza wenyewe kama tuliokuwa tumepagawa. Haha!
…You take my self, you take my self control,
You got me livin' only for the night,
Before the morning comes, the story's told,
You take my self, you take my self control,
Another night, another day goes by,
I never stop myself to wonder why,
You help me to forget to play my role,
You take my self, you take my self control…
Hakika ulikuwa ujumbe murua kiasi kwamba mimi na Amanda tulijikuta tukiimba kiitikio hicho utafikiri sisi ndio tulioutunga wimbo huo, ilikuwa ni
full kuzungusha kichwa, kurukaruka kwenye viti vyetu na kunesanesa. Tulikuwa kwenye dunia yetu, na kwa muda fulani tulijikuta tukisahau masahibu ya maisha.
Tulifika Capital Social Club saa sita na dakika arobaini za usiku na Almasi akaliegesha gari lake kwenye maegesho maalumu ya ukumbi wa Club. Capital Social Club ilikuwa moja ya kumbi mpya na za kisasa kabisa kuwahi kujengwa jijini Dodoma. Tulipoingia ndani tulikuta ukumbi ukiwa umefurika watu. Wanamuziki wa bendi ya muziki ya Malaika walikuwa wanatumbuiza jukwaani.
Tulianza kutafuta sehemu nzuri ili tukae, mara tukamwona mwanamume mmoja ambaye baadaye nilikuja kumtambua kuwa meneja wa ukumbi ule akitujia haraka baada ya kumtambua Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Almasi Dilunga, akatujulia hali na kututafutia sehemu nzuri, tukaketi tukitazama onesho la Malaika Band huku taratibu tukipata bia na mvinyo.
Sofia, ambaye nilikuwa nikimtania kwa kumwita ‘Mama Kijacho’, alikuwa anakunywa sharubati. Wakati tulipokuwa tukipata vinywaji vyetu taratibu sikusahau wajibu wangu. Muda wote macho yangu yalikuwa makini, nilijitahidi kumsoma (kama
scanner) kila mtu aliyekuwepo mahali hapo kujua kama kulikuwa na mtu aliyenitia wasiwasi. Hata kama katika nyakati za furaha kama hizo bado ule ‘u-Jason Sizya’ katika fikra zangu uliendelea kuwepo na ndiyo ulionifanya kumtazama kila mtu ndani ya ule ukumbi wa starehe kwa jicho la ziada.
Mara akapanda mwanamuziki Christian Bella na kuimba wimbo wa peke yake ambao kwa wakati huo ulikuwa gumzo ukitamba kwenye vituo mbalimbali vya redio na runinga, na hapo ukumbi mzima ukalipuka kwa shangwe. Sofia alishindwa kujizuia na kunishika mkono akiniomba twende jukwaani tukacheze, kwa kuwa mumewe Almasi hakupenda mambo ya kucheza cheza, yeye alipenda kusikiliza tu.
Wimbo ule ulipoisha tukarudi mezani lakini kabla hatujakaa ukapigwa wimbo mwingine wa taratibu ambao pia ulikuwa unatamba kwenye vyombo mbalimbali vya habari. Wimbo huu ulinifanya nisisimkwe mwili wangu kutokana na ujumbe uliokuwemo kwenye wimbo ule. Ulikuwa wimbo wa ujumbe wa mapenzi na kwa kweli Christian Bella alikuwa ameimba kwa hisia sana na kuutendea haki wimbo huo.
Nilishindwa kujizuia na kumshika mkono Amanda, nikamwinua nikimwomba twende jukwaani tukacheze. Amanda hakuwa na pingamizi, huwenda hata yeye aliisubiri nafasi hiyo. Tukawa tunacheza na kwa jinsi tulivyokuwa tukiendana watu wengi mle ukumbini walijikuta wakitwangalia sisi tu, kupitia macho yao, nilitambua kuwa wapo waliotwangalia kwa kuvutiwa na sisi, na wengine walisumbuliwa na wivu!
Japokuwa ulikuwa muziki wa rhumba la taratibu wenye ujumbe wa mapenzi lakini nilijikuta mikono yangu ikienda kwenye
hips za Amanda, nikagusagusa shanga zake wakati nikizipapasa taratibu nyonga zake kisha nikamkumbatia huku mapigo yangu ya moyo yakizidisha kasi. Na hapo pumzi zangu zikanipaa na kuwa zile za kukimbizwa na mbwa. Nikajiuliza kama kumgusa tu ilinifanya nijisikie hivi, vipi kuhusu mchezo katika uwanja wa sita kwa sita?
Mkono wangu wa kushoto ukapanda kuelekea shingoni kwake, ukiwa njiani kuelekea huko ukajikwaa kwenye titi lake la kulia lililosimama dede na ambalo ni kitambaa laini tu cha gauni alilovaa ndiyo kililizuia lisinipanguse nyama kwa nyama.
Kabla sijaufikisha mkono wangu kwenye shingo yake nikabadili uelekeo na kuupeleka kwenye kidevu chake, nikakishika kidevu chake kisha nikakiinua taratibu, tukawa sasa tunaangaliana uso kwa uso. Nikashindwa kujizuia na kumpelekea midomo yangu… naye bila ajizi akaniletea ya kwake. Dah, midomo yetu ilipogusana tukabusiana kwa namna ambayo ilinifanya nihisi msisimuko wa ajabu.
Endelea...