Bishop Hiluka
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 7,147
- 14,699
- Thread starter
- #921
333
Mpambano mwingine…
Saa 7:00 usiku…
MVUA kubwa ilianza kunyesha sambamba na upepo wa wastani na hivyo kuifanya sehemu kubwa ya Jiji la Dar es Salaam kwa wakati huo wa usiku kutawaliwa na hali ya baridi. Hii ilitokea muda mfupi tu tangu tulipofika kwenye nyumba za maofisa wa Usalama wa Taifa eneo la Makumbusho, nyumbani Pamela.
Tulipofika hapo Pamela hakutaka niondoke kama alivyoniambia hapo awali kuwa nimpitishe kisha ndiyo nielekee nyumbani kwangu Upanga, na badala yake kupitia ushawishi wake kama mwanamke tukajikuta tukitumbukia tena kwenye mtego mwingine wa mapenzi mazito.
Yalikuwa mapenzi motomoto yaliyonifanya nitamani kuitangazia dunia kuhusu utamu wa mwanamke huyo. Pamela alikuwa mwanamke mtundu sana aliyejua jinsi ya kucheza vizuri na hisia za mwanaume na kwa kweli aliniwezea sana na kunifanya nisahau mikasa yote niliyokuwa nimekumbana nayo katika harakati za kumsaka Bosco Gahizi na wenzake.
Mara tu tulipoingia nyumbani kwake tukaanzia bafuni tulikokwenda kuoga ili kutoa uchovu na kuipoza miili yetu na tukiwa huko bafuni Pamela akaanza vitimbi vyake vya hapa na pale. Wakati tukioga kwenye bomba la mvua alinivuta na kunikumbatia huku akiipitisha mikono yake nyuma ya shingo yangu na kufanya joto kali la mwili wake linipe faraja kubwa.
Nilishindwa kuvumilia, nami nikazungusha mikono yangu kumshika kiunoni kisha nikawa nakiminya minya kiuno chake. Tukatazama machoni kisha tabasamu maridhawa likachomoza kwenye nyuso zetu. Kisha Pamela akapeleka mkono wake kwenye malighafi zangu na kuanza kuzitomasa kwa namna ya kunipandisha mdadi halafu akaanza kunichua taratibu mshumaa wangu katika namna ya kuamsha vilivyolala, kwa kweli sikuweza kukivumilia kitendo kile, nikaamua kumpelekea moto huko huko bafuni.
Na tulipomaliza ngwe moja tukaoga na kisha tukaelekea chumbani ambako sasa kila mmoja alikuwa amempania mwenzake, maana tulipoingia tu chumbani Pamela akaanza uchokozi, nikambeba na kumtupia kitandani huku wote tukiangua vicheko hafifu vya mahaba. Kisha kama watu tuliopandwa na wazimu wa mapenzi tukaingia mchezoni na muda mfupi uliofuata tulijikuta tukimezwa na ulimwengu wa huba. Ilikuwa ni kama sinema ya kusisimua yenye kila aina ya vionjo vya kumtoa nyoka pangoni.
Tulikuwa kwenye ulimwengu mzito wa mapenzi na dunia ilikuwa kama kisiwa cha raha kwa ajili yetu. Tukizisahau shida zote. Pamela alikuwa amezitendea vyema hisia zangu na raha tuliyoipata macho yetu hayakuweza kutazama. Muda huo hatukukumbuka kitu kingine chochote isipokuwa kuivunja amri ya sita, huku mapenzi yakionekana kunoga kwa namna yake na miguno ya mahaba ikihanikiza kila mahali mle chumbani.
Tulivingirishana kwa sarakasi za aina yake pale kwenye uwanja wa sita kwa sita huku mechi yetu ikitawaliwa na rafu za kila aina kwa kuwa mchezo wetu haukuwa na refa wala kamisaa, na kila mtu alijaribu kuonesha ufundi wake pasipo kujali kama alikuwa anafuata sheria za mchezo au la.
Nilicheza sana rafu kwa kuwa nilikuwa nimegundua hila ya Pamela kuwa aliamua kutumia utundu wa hali ya juu ili kunifanya niongee lugha aliyoitaka, kwani Waswahili husema kuwa “kichwa cha chini kikisimama cha juu huwa hakifanyi kazi sawa sawa.”
Tulipambana kwa takriban saa nzima na hatimaye mchezo wetu ulifika tamati huku wote wawili tukiwa hoi kabisa, kila mmoja wetu akionekana kutosheka na mwenzake.
_____
Saa 3:30 asubuhi…
Nilishtuka toka katika usingizi wa fofofo na kuyafumbua macho yangu taratibu kisha nikayatembeza mle chumbani kuangalia huku na kule nikijaribu kusikiliza kwa umakini. Sikujua kitu gani kilikuwa kimenishtua na kuukatisha ghafla usingizi wangu uliokuwa umenichukua ghafla! Ilikuwa ni siku nyingine na muda huo tulikuwa bado tumelala.
Nilipotupa macho yangu kando nikagundua kuwa hata Pamela pia alikuwa bado amelala fofofo. Kwa mbali nilisikia sauti hafifu ya mkoromo wake wa uchovu. Nikaitupia jicho saa yangu ya mkononi na kushtuka. Muda huo miale ya jua la asubuhi ilikuwa inapenya dirishani na kutuama pale kitandani tulipolala.
Kwa mara kwa kwanza tangu nianze harakati za upelelezi kuhusu tukio la kigaidi lililosababisha kuteketea kwa jengo la Alpha Mall nilikuwa nimelala usingizi mtamu sana wa kueleweka kiasi cha kuchelewa kuamka.
Hakika penzi zito la Pamela lilikuwa limeamsha ari mpya nafsini mwangu na kupitia ukaribu ule kitu fulani kilikuwa kimeanza kujengeka moyoni mwangu. Hata hivyo tumbo langu lilikuwa dhaifu sana kwa njaa. Njaa ilikuwa inauma sana utadhani nilikuwa na vidonda tumboni na kichwa changu kilinivangavanga sana.
Kichwa kilikuwa kizito sana mithili ya mtu aliyekuwa ametwishwa kiroba cha mchanga na nilihisi kuchoka mno, kichwani nilikuwa na mawenge ya usingizi yaliyonipa hali ya kutaka kuendelea kulala. Pilika pilika za siku iliyotangulia, pombe kali na ukichanganya na mahaba mazito basi hali ikawa si hali.
Hata hivyo, akilini mwangu niliutaka utulivu kwa gharama yoyote ile japo nipate kupumzisha mwili na kupata japo lepe la usingizi. Nilichotamani ni kulala tu mpaka pale ambapo mwili wangu ungeniruhusu kuamka. Niliuhisi uzito wa kichwa changu na mawenge ya usingizi yakinitesa na hivyo hali hiyo ilikuwa inanipa hali ya kutaka kuendelea kuuchapa usingizi. Lakini sasa nilijikuta nimeamka na sikujua nini kilikuwa kimeniamsha.
Nikayatega masikio yangu kwa umakini kusikiliza na hapo nikagundua kuwa sauti ya simu yangu ya mkononi iliyokuwa ikiita kwa fujo ndiyo iliyonishtua kutoka usingizini. Nikaitazama na kuiona namba ngeni, nikataka niipuuzie lakini hisia zangu zikaniambia kuwa ilikuwa simu muhimu sana. Nikaipokea na kuipeleka sikioni.
“Hallo!” nilisema kivivu vivu na kushusha pumzi ndefu.
“Jason!” sauti ya mkurugenzi mkuu iliita kutoka upande wa pili wa simu. Nikashtuka sana na kujikuta nikiinuka toka pale kitandani na kuketi kitako.
“Naam. Shikamoo, mkuu!” nilisalimia kwa unyenyekevu mara tu nilipogundua kuwa nilikuwa naongea na mkurugenzi mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa aliyeamua kunipigia simu moja kwa moja.
“Marahaba, Jason, habari za tangu usiku?” mkurugenzi mkuu aliniuliza kwa upole kama mzazi anayeongea na mwanawe wa kwanza, mara tu baada ya kumuoza mke.
“Salama, mkuu,” nilimjibu mkurugenzi mkuu kwa unyenyekevu.
“Sasa ni hivi… Mheshimiwa Rais anakupongeza sana kwa kazi uliyoifanya ambayo imetusaidia kuubaini mtandao hatari wa kihalifu, yeye pia anakubali sana uwepo wako katika idara nyeti kama hii… nimetoka kuzungumza naye sasa hivi na kuna jambo ameniambia…” mkurugenzi mkuu alisema na kunyamaza kidogo kuruhusu mate yapite kohoni mwake.
Muda huo huo nikamwona Pamela akishtuka na kunitazama usoni kwa aibu, alipogundua kuwa nilikuwa naongea na simu akajiinua na kusogea karibu yangu ili asikie.
“…Waswahili wanasema ‘mcheza kwao hutunzwa’. Hivyo wewe na wenzako Luteni Lister na Pamela mnatakiwa leo saa saba mchana muwepo Ikulu kuonana na Mheshimiwa Rais, ana mambo mazuri ya kuongea nanyi. Naomba mwambie na Pamela, najua uko naye,” mkurugenzi mkuu alisema.
Pamela ambaye muda huo alikuwa ameweka sikio lake kwenye simu yangu kusikiliza akashtuka sana na kuweka kiganja cha mkono wake mdomoni kuziba mdomo kwa woga, huku akinikodolea macho.
“Sawa mkuu. Nashukuru sana kwa taarifa hii, nashukuru sana sana…” nilisema kwa unyenyekevu. Haha…! niligundua kuwa mkurugenzi mkuu alishakata simu wakati nikiendelea kushukuru. Kisha mimi na Pamela tukatazama na kucheka.
Huu ni mwisho wa Msimu wa Sita kwenye mfululizo wa Harakati za Jason Sizya. Usikose Msimu wa Saba katika mkasa uitwao “Utata”.