Simulizi: Harakati za Jason Sizya

Bishop yupo kwenye taharuki aanze chai au nkate?
Haha! Ni kweli nilikuwa kwenye taharuki lakini sasa hivi akili yangu ina utata[emoji23][emoji23].
Nitarudi baada ya dakika chache...
 

334

Mtafaruku…




Saa 6:15 usiku…

ULIKUWA usiku wa Jumamosi tulivu, Almasi Dilunga aliwasha injini ya gari lake kisha akaliondoa taratibu toka pale kwenye maegesho ya magari ya Maisha Club kulikokuwa na burudani ya aina yake kutoka kwa wanamuziki maarufu wa Bongo Fleva. Hakika nilikuwa nimesuuzika sana kwa burudani waliyoitoa wanamuziki hao hususan Zuchu. Kwa kweli mwanadada huyu alikuwa ameniburudisha vilivyo kwa muziki na uchezaji wake.

Almasi yeye alikuwa mpenzi mkubwa wa muziki wa rhumba na reggae na ndiye aliyetutaka tuondoke hapo Maisha Club na kuelekea Capital Social Club ambako kulikuwa na shoo kabambe kutoka kwa Bendi ya Malaika chini ya mwanamuziki mahiri, Christian Bella.

Nilikuwa nimesafiri kutoka jijini Dar es Salaam hadi jijini Dodoma kwenda kumtembelea rafiki yangu Almasi Dilunga, na vile vile kumpongeza kutokana na nafasi aliyoipata baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Albert Masinde kufanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya (DCs), Wakurugenzi wa Halmashauri (DEDs) na Makatibu Tawala wa Wilaya (DASs).

Hizi zilikuwa teuzi za nne tangu Rais alipoamua kubadilisha sura ya serikali yake kwa kuanza na Baraza la Mawaziri alilolivunja baada ya kutoridhika na mambo yalivyokuwa yakienda ndani ya serikali kufuatia mkasa mzito ulioibuka na kuzua taharuki kutokana na mauaji ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Ummi Mrutu. Mkasa huu ulisababisha kuandikiwa simulizi iliyoitwa ‘Taharuki’.

Ndiyo, ilikuwa taharuki iliyosababisha sintofahamu kwa Watanzania na kunilazimisha kuingia kazini pasipo kupenda, na hatimaye kwa kusaidiana na maofisa wawili wa usalama wenye mbinu maalumu, Komando Luteni Lister na Pamela Mkosamali, tukafanikiwa kuufichua mpango hatari uliokuwa umesukwa kwa ufundi wa hali ya juu na mtandao hatari ambao uliwahusisha baadhi ya mawaziri na wanausalama, wengine wakiwa viongozi katika taasisi za ulinzi na usalama.

Baada ya Rais kulivunja Baraza la Mawaziri na kuunda baraza jipya huku akiwaacha aliyekuwa Waziri Mkuu, Festus Mponjoli na mawaziri watano, aliingia katika awamu nyingine kwa kuwabadilisha viongozi wa taasisi za ulinzi na usalama huku mkurugenzi mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), mzee Rajabu Kaunda akistaafu kwa heshima na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari na Teknolojia wa TISS, David Mshana.

Halafu Rais akafanya mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa (RCs) na Makatibu Tawala wa Mikoa (RASs) na kisha akahitimisha kwa kufanya mabadiliko katika ngazi za wilaya na halmashauri na ndipo Almasi akateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji na kituo chake cha kazi kikawa pale pale makao makuu ya nchini, jijini Dodoma, na hivyo alikuwa akitembelea gari la kifahari aina ya Toyota Landcruiser GX V8 la rangi ya fedha.

Nilikuwa na furaha kubwa sana kwa Almasi kupata nafasi hiyo kwani alikuwa amepita kwenye mlolongo mrefu wa matatizo ya kifamilia yaliyomsababisha kuishi maisha ya msoto mtaani huku akiifanya bangi kuwa mfariji wake mkuu, japokuwa alikuwa msomi mzuri mwenye Shahada ya Uchumi aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Si hivyo tu, Almasi alikuwa na ufahamu mkubwa sana wa mambo mbalimbali duniani yakiwemo ya kisiasa, kiuchumi na hata ya kijamii na alikuwa na uwezo wa kuchambua mambo katika namna ambayo ungetamani usiwe mwongeaji ili ubaki kumsikiliza. Sasa Almasi alikuwa ndiye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, nafasi ambayo kwa wengine ilionekana kuwa Rais alikuwa amempendelea, lakini kwangu niliona Almasi alistahili, ndiyo maana nilikuwa nimempigania kwa kila hali hadi kuipata nafasi hiyo.

Ndiyo… watu wengi waliomfahamu Almasi walimchukulia kama mvuta bangi tu, na kwa wale ambao hawakumfahamu kabla ya uteuzi na baada ya kuteuliwa wakafuatilia wasifu wake, walidhani hakustahili nafasi ile hasa kuachwa Jijini Dodoma, pengine walidhani alistahili kupelekwa kwenye halmashauri za vijijini.

Ukweli ni kwamba nilitambua kipawa na karama ya uongozi aliyokuwa nayo Almasi, niligundua jambo hilo siku ya kwanza tu nilipomfahamu, kwa namna alivyokuwa akiongea alionekana kabisa kuwa alikuwa na vision halafu deep down alionekana ana ule ubinadamu ambao ni nadra sana kuuona karne hii.

Hivyo safari yangu hiyo kwenda Dodoma kipindi hicho ilikuwa na maana kubwa sana japokuwa zilikuwa zimeshapita wiki tatu tangu Almasi ateuliwe na kuapishwa, hata hivyo sikuangalia muda bali nilidhani ilikuwa sahihi si tu kwenda kumpongeza Almasi bali tujipongeze. Naam… sote wawili tulistahili kujipongeza hasa ikizingatiwa kuwa sasa kipele kilikuwa kimempata mkunaji, Almasi alikuwa mmoja wa watu wachache sana wenye maono ingawa bahati mbaya machoni mwa wengi alionekana mtu dhalili, akaishia kuvuta bangi ili asipate msongo wa mawazo.

Pia nilikwenda Dodoma kwa ajili ya kuhakikisha kuna usalama wa kutosha kwa kuwa katika kipindi hicho wageni wengi kutoka Nchi mbalimbali za Jumuia ya Madola walikuwa wakiwasili kwa ajili ya Mkutano wa Nchi za Jumuia ya Madola ambao ulipangwa kufanyika siku ya Ijumaa ya wiki iliyokuwa ikifuata, katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano hapo jijini Dodoma.

Usiku huu Almasi alikuwa amevaa suruali nyeusi ya dengrizi na shati la samawati la mikono mirefu brand ya Levi’s, aliendesha gari mwenyewe baada ya kumruhusu dereva wake akapumzike. Ndani ya gari lile la kifahari tulikuwemo watu wanne; Almasi mwenyewe, mkewe Sofia, mimi na dada wa Sofia aliyeitwa Amanda.

Sofia na Amanda walifanana sana na endapo ungekutana nao usingeweza kuwatofautisha. Nilipomwona Amanda kwa mara ya kwanza nilidhani yeye na Sofia walikuwa mapacha, baadaye ndipo nikagundua kuwa Amanda alikuwa mkubwa akimzidi Sofia kwa miaka miwili.

Kama ilivyokuwa kwa Sofia, Amanda pia alikuwa msichana mrefu, mpana na mwenye umbo la kuvutia, alikuwa binti halisi wa Kiafrika ambaye uzuri wake ulitosha kuudhihirisha utukufu wa Mungu kwenye sanaa ya uumbaji. Alikuwa na kifua chenye ukubwa wa kati, tumbo dogo na rangi yake ya maji ya kunde iliyokuwa na mng’aro wa aina yake, wala hakuhitaji kabisa vikorombwezo vya aina yoyote kuinakshi ngozi yake.

Tofauti kubwa kati yake na Sofia ilikuwa katika nywele, wakati Sofia alikuwa na nywele nyingi alizozisuka, Amanda kwa upande wake alikuwa amezikata na kubakiwa na nywele fupi.

Endelea...
 

335

Usiku huu Amanda alikuwa amevaa kitu fulani hivi very expensive, made by Channel. Kilikuwa kigauni fulani amazing cha rangi ya pink chenye kumetameta na kung’aa kilipomulikwa na mwanga wa taa, kigauni kile kilimbana na kuishia juu kidogo ya magoti yake na kuifanya miguu yake milaini na minene kidogo kuonekana kwa uzuri. Kwa kigauni kile niliweza kuiona michirizi fulani nyuma ya miguu yake, na hapo nikajikuta nikisisimkwa mwili wangu kila nilipomtazama.

Kana kwamba hiyo ilikuwa haitoshi, kigauni alichovaa kilishonwa kwa namna ambayo kiliacha nusu ya kifua chake wazi na hivyo kukifichua kidani cha asili chenye herufi ‘A’ kilichokuwa kimenasa vyema kwenye shingo yake ndefu na kupotelea katikati ya uchochoro wa matiti yake makubwa kiasi yenye chuchu imara zilizotuna na kulisumbua kidogo gauni lake.

Pia kigauni hicho kilikuwa kimeyashika vyema mapaja yake makubwa yaliyoshikiliwa na nyonga pana na nyuma alikuwa amefungasha mzigo mkubwa kiasi, usiochukiza kuutazama, wa makalio na pia kutokana na kigauni chake kubana ilisababisha shanga na mistari ya mkanda wa nguo ya ndani viweze kujichora na kuonekana waziwazi. Ilikuwa ni aina ya zile chupi za vimikanda vya kupita kiunoni na vijitambaa vidogo tu vya kufunika mbele.

Dah, kila nilipokitupia jicho kiuno chake na kuziona zile shanga nilihisi pumzi zikinipaa na mapigo ya moyo wangu kwenda mbio isivyo kawaida. Miguuni Amanda alikuwa amevaa sendo ghali za kike za rangi ya pink na alikuwa amebeba mkoba mzuri wa ngozi ya mamba wa rangi ya pink. Kwa kifupi usiku huu ni kama vile Amanda alikuwa amepanga kunipa tabu baada ya kugundua nilikuwa dhaifu wa vidosho kama yeye!

The attraction was so obvious kiasi kwamba kuna wakati nilijikuta nikimgusa hapa na pale wakati tukipiga soga, pasipo sababu yoyote ya msingi ilimradi tu niuguse mwili wake wenye ngozi laini. Haha, mimi bhana! Kuna wakati nilianza kumhurumia sana Rehema kuwa na mume wa aina yangu, maana… dah… ngoja niachane na hizo nisije nikapoteza lengo ya simulizi yangu.

Sofia pia hakuachwa nyuma, usiku huu alikuwa amevaa gauni zuri refu la rangi nyekundu brand ya Luis Vuitton, lililokuwa liking’aa kila limulikwapo na mwanga wa taa. Shingoni alikuwa amevaa mkufu mdogo wa dhahabu wenye kung’aa na mkononi alikuwa na pochi ndogo nyekundu. Chini alikuwa amevaa viatu vyekundu vya mchuchumio vyenye visigizo virefu. The sisters looked like heaven angels.

Wakati tukielekea Capital Social Club, ndani ya gari la Almasi sauti ya muziki wa reggae remix ya wimbo wa Laura Branagan ilisikika toka kwenye spika za redio iliyofungwa kwenye gari lile, ilikuwa ni full kuinjoi, tuliimba na kucheza wenyewe kama tuliokuwa tumepagawa. Haha!

…You take my self, you take my self control,
You got me livin' only for the night,
Before the morning comes, the story's told,
You take my self, you take my self control,
Another night, another day goes by,
I never stop myself to wonder why,
You help me to forget to play my role,
You take my self, you take my self control…


Hakika ulikuwa ujumbe murua kiasi kwamba mimi na Amanda tulijikuta tukiimba kiitikio hicho utafikiri sisi ndio tulioutunga wimbo huo, ilikuwa ni full kuzungusha kichwa, kurukaruka kwenye viti vyetu na kunesanesa. Tulikuwa kwenye dunia yetu, na kwa muda fulani tulijikuta tukisahau masahibu ya maisha.

Tulifika Capital Social Club saa sita na dakika arobaini za usiku na Almasi akaliegesha gari lake kwenye maegesho maalumu ya ukumbi wa Club. Capital Social Club ilikuwa moja ya kumbi mpya na za kisasa kabisa kuwahi kujengwa jijini Dodoma. Tulipoingia ndani tulikuta ukumbi ukiwa umefurika watu. Wanamuziki wa bendi ya muziki ya Malaika walikuwa wanatumbuiza jukwaani.

Tulianza kutafuta sehemu nzuri ili tukae, mara tukamwona mwanamume mmoja ambaye baadaye nilikuja kumtambua kuwa meneja wa ukumbi ule akitujia haraka baada ya kumtambua Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Almasi Dilunga, akatujulia hali na kututafutia sehemu nzuri, tukaketi tukitazama onesho la Malaika Band huku taratibu tukipata bia na mvinyo.

Sofia, ambaye nilikuwa nikimtania kwa kumwita ‘Mama Kijacho’, alikuwa anakunywa sharubati. Wakati tulipokuwa tukipata vinywaji vyetu taratibu sikusahau wajibu wangu. Muda wote macho yangu yalikuwa makini, nilijitahidi kumsoma (kama scanner) kila mtu aliyekuwepo mahali hapo kujua kama kulikuwa na mtu aliyenitia wasiwasi. Hata kama katika nyakati za furaha kama hizo bado ule ‘u-Jason Sizya’ katika fikra zangu uliendelea kuwepo na ndiyo ulionifanya kumtazama kila mtu ndani ya ule ukumbi wa starehe kwa jicho la ziada.

Mara akapanda mwanamuziki Christian Bella na kuimba wimbo wa peke yake ambao kwa wakati huo ulikuwa gumzo ukitamba kwenye vituo mbalimbali vya redio na runinga, na hapo ukumbi mzima ukalipuka kwa shangwe. Sofia alishindwa kujizuia na kunishika mkono akiniomba twende jukwaani tukacheze, kwa kuwa mumewe Almasi hakupenda mambo ya kucheza cheza, yeye alipenda kusikiliza tu.

Wimbo ule ulipoisha tukarudi mezani lakini kabla hatujakaa ukapigwa wimbo mwingine wa taratibu ambao pia ulikuwa unatamba kwenye vyombo mbalimbali vya habari. Wimbo huu ulinifanya nisisimkwe mwili wangu kutokana na ujumbe uliokuwemo kwenye wimbo ule. Ulikuwa wimbo wa ujumbe wa mapenzi na kwa kweli Christian Bella alikuwa ameimba kwa hisia sana na kuutendea haki wimbo huo.

Nilishindwa kujizuia na kumshika mkono Amanda, nikamwinua nikimwomba twende jukwaani tukacheze. Amanda hakuwa na pingamizi, huwenda hata yeye aliisubiri nafasi hiyo. Tukawa tunacheza na kwa jinsi tulivyokuwa tukiendana watu wengi mle ukumbini walijikuta wakitwangalia sisi tu, kupitia macho yao, nilitambua kuwa wapo waliotwangalia kwa kuvutiwa na sisi, na wengine walisumbuliwa na wivu!

Japokuwa ulikuwa muziki wa rhumba la taratibu wenye ujumbe wa mapenzi lakini nilijikuta mikono yangu ikienda kwenye hips za Amanda, nikagusagusa shanga zake wakati nikizipapasa taratibu nyonga zake kisha nikamkumbatia huku mapigo yangu ya moyo yakizidisha kasi. Na hapo pumzi zangu zikanipaa na kuwa zile za kukimbizwa na mbwa. Nikajiuliza kama kumgusa tu ilinifanya nijisikie hivi, vipi kuhusu mchezo katika uwanja wa sita kwa sita?

Mkono wangu wa kushoto ukapanda kuelekea shingoni kwake, ukiwa njiani kuelekea huko ukajikwaa kwenye titi lake la kulia lililosimama dede na ambalo ni kitambaa laini tu cha gauni alilovaa ndiyo kililizuia lisinipanguse nyama kwa nyama.

Kabla sijaufikisha mkono wangu kwenye shingo yake nikabadili uelekeo na kuupeleka kwenye kidevu chake, nikakishika kidevu chake kisha nikakiinua taratibu, tukawa sasa tunaangaliana uso kwa uso. Nikashindwa kujizuia na kumpelekea midomo yangu… naye bila ajizi akaniletea ya kwake. Dah, midomo yetu ilipogusana tukabusiana kwa namna ambayo ilinifanya nihisi msisimuko wa ajabu.

Endelea...
 

336

Ukweli nilishawabusu wanawake wengi ila busu la Amanda lilikuwa lina ladha ya tofauti sana. Ilikuwa ladha fulani ambayo sikuweza hata kuielezea, soft touch and innocent. Midomo yetu ilikuwa inasuguana tu na hapo nikajikuta napata ladha mchanganyiko! Chumvi si chumvi, sukari si sukari, chachu si chachu, chungu si chungu… haha!

Kisha nilimsikia Amanda akitoa miguno fulani iliyoashiria kuwa alikuwa katika hatua ambayo lolote lingeweza kufanyika. Na mara akaizungusha mikono yake nyuma ya shingo yangu na kulaza kichwa chake kifuani kwangu. Akilini kwangu nikapanga kuwa lazima nikajilie vyangu tukirudi nyumbani, maana hali ile ilimaanisha kuwa nilikuwa nimepewa ruhusa pasipo hata kutamka neno. Niliwaza huku nikifurahia bahati yangu.

Dah, wimbo tuliokuwa tunacheza ukawa umeisha na sasa walianza kupiga wimbo mwingine ambao mapigo yake na hata uchezaji wake ulikuwa wa haraka. Tukaamua kurudi kwenye viti vyetu kuketi.

Kisha Amanda aliniaga na kuinuka akaelekea maliwato na baada ya dakika takriban tano alirudi kuketi, lakini alionekana kama alikuwa na mawazo mengi. Hakuwa na ule uchangamfu aliokuwa nao kabla. Kwa kuwa nilijua kumsoma mtu haikuwa kazi ngumu kugundua kuwa Amanda hakuwa sawa. Muda huo ilikuwa imeshafika saa nane na nusu za usiku

“Vipi Amanda, kuna tatizo lolote?” nilimuuliza kwa sauti ya chini huku nikimtazama usoni kwa udadisi.

“Hakuna tatizo. I’m okay,” Amanda alinijibu huku akijilazimisha kutabasamu.

Nilitaka kuendelea kumsaili lakini nikaamua kupuuzia hali ile baada ya kuhisi kulikuwa na mtu mahali alikuwa akinitazama. Nikayazungusha macho yangu kutazama mle ukumbini. Mara nikamwona mtu mmoja miongoni mwa watu waliokuwa mle ukumbini akinitazama kwa jicho la wizi katika namna ambayo ilinitia shaka sana.

Alikuwa ameketi kwenye meza ya tatu tu kutoka ilipokuwa meza yetu na kilichonishtua na kunifanya nivutiwe zaidi na mtu huyo ni namna ambavyo macho yake yalionesha umakini wa kufuatilia nyendo zangu. Sikuwa nimemwona kabla na sikujua alifika kwenye meza hiyo muda gani, jambo hilo likanifanya niwe na tahadhari zaidi.

Alikuwa mwanamume mweusi, mrefu na mwenye mwili uliojengeka, akiwa na misuli imara mwilini iliyoonekana waziwazi na alikuwa amenyoa upara. Alivaa mavazi ambayo kutokana na ukubwa wa mwili wake wenye misuli imara yalionekana kama ambayo hayamtoshi vizuri kwa namna yalivyombana, suruali ya bluu ya dengrizi na fulana nyekundu na miguuni alikuwa amevaa buti za kiaskari. Kwa mtazamo tu niliweza kubaini kuwa alikuwa rika moja na mimi.

Nilipomchunguza vizuri nikagundua kuwa alikuwa amevaa kifaa fulani cha mawasiliano kwenye sikio lake la kulia na alionesha kama alikuwa anawasiliana na mtu au watu fulani ambao hawakuwepo eneo lile. Kengele ya hatari ikalia kichwani kwangu.

“Almasi, unamfahamu mwanaume yule mwenye fulana nyekundu inayombana?” nilimuuliza Almasi huku nikioneshea kwa ishara ya macho yangu kule alikoketi yule mtu. Almasi, Sofia na Amanda kwa pamoja wakayapeleka macho yao kumtazama yule mwanamume kisha wakayarejesha macho yao kunitazama, na hapo Almasi akatikisa kichwa chake kukataa.

Hata hivyo niliweza kuona chembe fulani za hofu kwenye nyuso zao. Kwa kuwa sikutaka wahofie hivyo nikafanya namna ya kuwafanya wapuuzie jambo hilo, “Angalia tu usije ukanenepa ukawa kama mtu huyo!” nilimwambia Almasi huku nikicheka.

Alamsi akatabasamu na kuzungusha macho yake kutazama juu. “Kwa nini umenifikiria hivyo?”

Nikatabasamu. “Kwa nafasi yako ya sasa usipokuwa makini unaweza kujiachia na kuwa hivyo.”

“Dah, hata nijiachie vipi bado siwezi kuwa kama huyo jamaa. Huu mti mkavu bwana,” Almasi alisema na kuwafanya Sofia na Amanda wacheke.

Sasa nilikuwa nimefanikiwa kuiondoa hofu kwa akina Almasi lakini nilibakiwa na jambo moja, kuwaondoa eneo lile salama kabla jambo baya halijatokea. Nikahisi kibofu changu cha mkojo kilikuwa kimejaa na hivyo nilitakiwa kwenda haja ndogo kwani ule mvinyo niliokunywa ulikuwa umekijaza kibofu changu. Nilipanga kuwa pindi nikitoka maliwato tuondoke. Niliinuka na kuelekea eneo la maliwato.

Ili kufika yalipo maliwato ilimbidi mtu atoke kwanza nje ya ukumbi ule wa starehe, lakini akiwa bado ndani ya jengo lile la Capital Social Club, na kisha ashike ukumbi (corridor) mwembamba mrefu upande wa kushoto na baada ya kufika mwisho wa ukumbi ule akate tena kushoto na baada ya hatua zisizozidi kumi aingie kulia.

Nami nilipitia njia hiyo hiyo, na wakati nikitembea kuelekea maliwato ya ukumbi ule nilijikuta nikivutiwa na ubora wa ukumbi ule. Hakika mikono ya mafundi ujenzi ilikuwa imeitendea haki taaluma yao. Kila eneo la ndani ya Club ile lilivutia kulitazama na kuta zake zilikuwa safi na zilizonyooka vizuri na kupambwa kwa nakshi tofauti za kupendeza.

Mwanga wa taa za mle ukumbini uliakisiwa vizuri na marumaru za kisasa zilizokuwa sakafuni na kutengeneza mandhari fulani nzuri iliyovutia sana kutazama. Hata hivyo bado nilikuwa makini sana kumtazama kila mtu aliyekuja nyuma yangu au hata niliyepishana naye.

Baada ya kuingia upande wa kulia nikawa nimefika sehemu iliyokuwa na milango miwili. Mlango mmoja ulikuwa kwa ajili ya kuingia sehemu ya maliwato ya wanawake na mlango mwingine ulikuwa ni kwa ajili ya kuingia sehemu ya maliwato ya wanaume.

Niliufungua ule mlango wa maliwato ya wanaume na kuingia na hapo nikawa nimetokezea kwenye ukumbi mpana uliotazamana na milango sita ya vyoo. Milango miwili ilikuwa wazi huku mingine minne ikiwa imefungwa. Hata hivyo hakukuwa na dalili za uwepo wa mtu yoyote mle ndani ya vyoo. Watu wawili waliokuwa wakijisaidia haja ndogo walimaliza na kutoka, nikabaki peke yangu.

Vyoo vyote vilionekana visafi na kwenye ule ukuta wa ukumbi uliokuwa ukitazamana na ile milango ya vyoo kulikuwa na kioo kipana cha kujitazama, na pembeni ya kioo kile kulikuwa na masinki sita ya ukutani kwa ajili ya haja ndogo pamoja na mifereji midogo ya chini iliyojengewa vizuri kwa marumaru kwa ajili ya kukusanya maji taka na kuyasafirisha nje.

Kutokana na tahadhari niliyojiwekea, sikutaka kujisaidia haja ndogo pale kwenye masinki ya ukutani, na badala yake nilichagua choo kimoja kilichokuwa mwishoni mwa ile korido kisha nikafungua mlango na kuingia ndani halafu nikaufunga mlango na kufungua zipu, nikajisaidia haja ndogo.

Wakati nilipokuwa namalizia nikaanza kuhisi kuwa mle ndani kwenye ule ukumbi wa maliwato kulikuwa na mtu aliyekuwa akitembea. Hilo kwangu halikuwa jambo la kushangaza kwa kuwa eneo lile la maliwato lilikuwa likiingiwa na kila mtu, ila kilichonivutia zaidi ni namna mtu huyo alivyokuwa akitembea taratibu na kwa tahadhari kama ambaye hakutaka nigundue kuhusu uwepo wake mle maliwato. Alikuwa kama akivikagua vile vyoo.

Endelea...
 

337


Nikiwa nimeanza kuhisi jambo baya sikutaka kumshtua mtu yule hivyo nikaifunga taratibu zipu ya suruali yangu na kutulia huku masikio yangu yakifanya kazi ya ziada kusikiliza hatua za mtu yule. Hatimaye ile sauti ya hatua za yule mtu ikakoma na eneo lote la vile vyoo likawa kimya. Niliendelea kuyatega masikio yangu na kwa kweli sikuweza kuhisi kitu chochote eneo lile.

Baada ya kitambo kirefu cha kusubiri nilipatwa na hisia kuwa kulikuwa na mtu aliyekuwa amesimama nje ya ule mlango wa choo changu. Ili kuhakikisha niliyapeleka macho yangu haraka kutazama chini ya ule mlango sehemu kulipokuwa na uwazi mdogo kati ya ule mlango na sakafu ya kile choo. Nikaona kitu kama kivuli cha miguu ya mtu.

Sasa nilijua kuwa sikuwa salama tena. Hata hivyo sikutaka kuendelea kubakia mle chooni kwa muda mrefu jambo ambalo lingewapa wasiwasi mkubwa akina Almasi, hivyo nikaamua kufanya jambo la kumshtukiza yule mtu aliyekuwa amesimama nje ya choo changu kwa kuufungua ghafla ule mlango na kisha nikajirusha nje na kutua kwenye ule ukumbi kama paka. Bastola ilikuwa tayari mkononi kwangu.

Na hapo nikamwona yule mwanamume mweusi, mrefu na mwenye misuli imara mwilini akiwa ameshika bastola yake mkononi tayari kwa shambulizi. Nikawahi kuupiga teke mkono wake wenye bastola kwa nguvu zangu zote na hivyo kuifanya ile bastola yake imtoke na kuanguka sakafuni. Hata hivyo yule mtu alikuwa makini sana, akaniwahi kwa kutupa ngumi mbili zenye kasi ya umeme. Nikazikwepa na hivyo zikakata upepo.

Kisha akaachia pigo maridadi kwenye mkono wangu ulioshika bastola na ile bastola ikanitoka na kuanguka sakafuni. Sasa tukawa tunatazamana tukiwa mikono mitupu, kilichofuata hapo ilikuwa ni makabiliano ya ana kwa ana. Nikaachia pigo moja maridadi la ngumi lililomkosa na kukata hewa bila majibu.

Nilipotupa pigo la pili akawa amechelewa kidogo na hivyo ngumi yangu makini ikaitandika shingo yake na kumfanya agune kwa maumivu makali ambayo kwa vyovyote yalisambaa haraka mwilini mwake. Sasa akacharuka na kuniletea mapigo mawili ya ngumi kavu za tumboni zilizolikoroga tumbo langu. Japokuwa nilikuwa nimejitahidi kuyadhibiti mapigo yale lakini sikufanikiwa kwani yule mtu, japo alikuwa na mwili mkubwa, alikuwa mwepesi na fundi sana wa mapigano.

Kisha alitupa pigo la teke huku macho yake yakionesha kudhamiria kuzipasua korodani zangu, nikalipangulia chini kwa mikono yangu imara na kumfanya yule mtu apoteze mhimili na kupepesuka kidogo, hata hivyo alikuwa mwepesi sana alipopata mhimili wa ukuta akarusha pigo jingine la ngumi ya chembe ya moyo.

Mara hii nilikuwa mtulivu na makini hivyo nikaipangua ngumi ile kama mchezo kisha nikarusha teke lakini liliishia kudakwa na yule mtu, nikaona kabisa kuwa alikuwa anaenda kuuvunja mguu wangu, nikarusha teke la mguu mwingine uliobakia chini na teke hilo likatua kwenye korodani zake na hapo yule mtu akatoa mguno wa maumivu makali huku akibweka kama mbwa mwizi. Sote tukapiga mweleka, lakini yule mtu hakuonekana mtu wa kukata tamaa mapema.

Alirusha miguu yake kwa samasoti ya chini na kusimama haraka tayari kwa kuniletea mashambulizi, nikamuwahi na pigo jingine la teke la mzunguko lenye kasi lakini yule mtu aliwahi kuliona hivyo akalikwepa kwa kusogea kidogo pembeni na hapo pigo lile la teke likapita bila shabaha na kukata upepo.

Upesi nikajitanua na kuchana msamba kisha nikajizungusha na kumchota miguu yule mtu, nikamsomba kimo cha mbuzi na kumtupa chini kama gunia. Yule mtu akatokwa na ukelele wa maumivu huku akinitukania mama yangu, halafu upesi akawahi kusimama na hatimaye tukawa tunatazamana ana kwa ana. Nikajikuta nikiangaliana na macho yaliyobeba ghadhabu kubwa, yakitoa cheche za moto.

Kutukaniwa mama yangu kulinitia hasira, nikaamua nimfundishe adabu ili siku nyingine aheshimu wa wazazi wa wenzake, nikajifanya kama nilitaka kuikimbilia bastola yangu iliyokuwa sakafuni na hivyo nikafanikiwa kumpumbaza yule mtu, kwani akili yake ilikuwa katika kunizuia nisiifikiie ile bastola. Na hapo nikamwingia na ngumi tatu kali za uso kabla sijajirusha juu juu na kumtandika kichwa kikali sana yule mtu kilichomtupa chini.

Akanyanyuka haraka huku akinijia kama nyati aliyejeruhiwa. Akakutana na teke la mzunguko lililombwaga kifudifudi. Kisha nikawahi kumkwida ukosi na kumwinua. Nikamzungusha na kumnyuka ngumi tatu za mfululizo. Na hapo nikamwona akikung’uta kichwa chake kuondosha ulevi na nyota ambazo bila shaka zilizomzonga usoni.

Kisha akasimama huku akijizatiti, huenda ni baada ya kukumbuka yeye ni nani na alikuwepo pale kwa lengo gani. Akanijia tena kama mbogo! Akarusha ngumi, akarusha teke. Vyote viliambulia patupu. Akajirekebisha na kujaribu kujiweka sawa. Akarusha ngumi, akarusha teke na kujikuta akikata tena hewa na kuzidi kujichosha.

Sikutaka kumchelewesha, nikajizungusha na kumfumua teke la juu kwa juu. Akapepesuka. Nikamfumua teke la usoni. Akadondoka kama gunia la mahindi. Sasa alikuwa amejifunza adabu na kutambua kuwa mimi mama yangu alikuwa na thamani kubwa, pia alijua sikuwa saizi yake na hivyo akachupa ili aiwahi bastola yake iliyokuwa sakafuni. Alipotua tu sakafuni na kuishika bastola yake na mimi nikawa nimetua na kumkanyaga kwa nguvu kwenye uti wa mgongo. Nikasikia sauti ya mfupa ukilia ‘ko!’.

Yule mtu akapiga yowe na kuiachia ile bastola huku akirudi chini kifudifudi. Sauti ile ya mvunjiko ilikuwa na maana kuwa nilikuwa nimemvunja mfupa wa kiuno na kwamba asingeweza tena kuinuka katika maisha yake yote, wala kuketi, wala kuchutama. Na wala asingeweza kutambaa. Kwa maisha yake yote yaliyobakia angekuwa mtu wa kubebwa na kugeuzwa tu kama maiti. Kisha nikaziokota bastola zote mbili, yangu na yake halafu nikamsogelea.

“Wewe ni nani na ni kitu gani unahitaji kutoka kwangu...?” nilianza kumhoji huku nikiwa mtulivu kabisa. Lakini yule mtu alikuwa jeuri. Hakutaka kunijibu na badala yake alinitazama kwa macho yake yenye ghadhabu.

“Nakuuliza, wewe ni nani na una shida gani na mimi?” nilimuuliza tena yule mtu lakini hakunijibu na badala yake akaanza kugugumia maumivu na hapo nikamchapa makofi mawili ya nguvu usoni kumuweka sawa.

“Nakuuliza wewe una shida gani na mimi mbona tunafuatana fuatana hadi chooni?” nilimuuliza tena yule mtu huku nikiwa nimekasirika.

“Mimi nilikuwa sikufuati wewe bwana,” yule mtu aliongea kwa hofu huku akilalama kwa maumivu.

“Sasa kwa nini uje mlangoni kwangu kunisubiria, inamaana vyoo vyote humu ndani vina watu?” nilimuuliza huku nikimtazama kwa hasira.

“Unanionea bure tu mimi sifahamu chochote,” yule mtu alilalamika. Kisha Katika hali ya kushangaza, nikamwona akilainika na kuanza kuvuja damu nyingi mdomoni.

Endelea...
 

338

Nikashangazwa sana na hilo tukio, na nilipomkagua na macho yangu sikuona kama alikuwa na mushkeli popote pale. Mbele ya macho yangu nilimwona yule mwanamume akikata pumzi na kisha ulimi ukatoka mdomoni mwake na kudondokea chini! Alikuwa ameunyofoa ulimi wake kwa kutumia meno!

Shit!” nilijikuta nikilaani na kisha nikaanza kumfanyia upekuzi wa haraka haraka yule mtu pasipo kupata kitu chochote cha maana toka kwake.

Muda huo kulikuwa na watu nje ya ule ukumbi wa vyooni walikuwa wanagonga mlangoni, na hapo nikagundua kuwa yule mtu alikuwa ameufunga ule mlango wa kuingilia kwa ndani ili kuzuia watu wasiingine. Sikutaka ule mwili ukutwe pale kwenye ukumbi, haraka nikamvuta hadi kwenye choo cha mwisho kabisa na kumuegemeza kwenye mlango wa kile choo na kuufunga. Na hapo akawa ameulalia mlango na kuuzuia usiweze kufunguka kwa urahisi. Ile bastola yake niliiacha mle mle chooni nilimomfungia.

Kisha nikamwaga maji mengi kwenye zile damu na kuyasukuma yale maji kwenye mojawapo ya mifereji midogo ya chini iliyojengewa vizuri kwa marumaru kwa ajili ya kukusanya maji taka na kuyasafirisha nje, nilipohakikisha nimeondoa ushahidi nikaenda kufungua komeo la ule mlango wa kuingilia kwenye ukumbi wa vyoo na kutoka haraka huku nikipishana na watu kadhaa waliokuwa wakinitazama kwa hisia mchanganyiko, wapo walionitazama kwa mshangao, na baadhi yao walinitazama kwa hasira na walikuwa wanatoa matusi ya waziwazi lakini sikuwajali.

Nilitoka nje kabisa ya jengo la Capital Social Club na kukuta kulikuwa na watu kadhaa, wake kwa waume waliokuwa na mambo yao. Pia kulikuwa na madadapoa kama wote waliokuwa mawindoni. Biashara za ufuska na ufisadi zilikuwa zikiendelea mtindo mmoja. Magari hasusan teksi, yaliwasili na kuondoka kila dakika.

Ukweli pale Capital Social Club palikuwa mahali pa aina ya pekee katikati ya Jiji la Dodoma, mahali palipopendwa na watu mchanganyiko kuanzia vijana wa kazi, wakora, mapusha, madadapoa na kadhalika. Wakati nikitembea kuelekea sehemu ya maegesho ya magari nikamwona dadapoa mmoja akinijia haraka… Hapana, huyu hakustahili kuitwa dadapoa, labda niseme mamapoa. Alikuwa mwana mama wa makamo aliyekuwa amejiremba kwa wanja na rangi na nywele za bandia ili aonekane bado binti.

Yule mamapoa alinijia haraka huku akiachia tabasamu hata hivyo niligundua kuwa tabasamu lake lilikuwa la kuulaani na kuukashifu umri wake mwenyewe, huku likiutukana ujana na urembo wa wale madadapoa wenzake walioonekana vijana. Nilipojaribu kumlinganisha na Amanda nikamwona kama takataka fulani, nikamkata jicho la dharau kama niliyekuwa natazama kinyesi nilichokikanyaga uchochoroni. Akanywea na kubadili uelekeo.

Nikavuta hatua zangu kuelekea kwenye maegesho ya magari huku nikimtumia ujumbe mfupi wa maandishi Almasi, kwenye simu yake, kumtaka yeye na wengine watoke haraka nje kwani kulikuwa na tatizo kubwa lililokuwa limetokea. Nia yangu ilikuwa kuwaondoa eneo lile kabla ile maiti kule chooni haijagundulika.

Wakati nikisimama pale kwenye maegesho kando ya gari tulilokuja nalo nikahisi kulikuwa na mtu mwingine aliyekuwa amesimama eneo lile. Haraka nikageuka na kumwona mwanaume mmoja mrefu aliyekuwa amesimama pembeni ya gari aina ya Toyota Harrier la rangi nyeusi, ambalo lilikuwa limeegeshwa takriban hatua tano tu kutoka kwenye gari letu.

Mtu yule alikuwa amevaa suruali ya kadeti ya rangi ya nyeusi na shati jeupe la mistari ya bluu la mikono mirefu. Kichwani alivaa kofia nyeusi ya kapelo na miguuni alivaa buti ngumu za ngozi.

“Vipi, Jason?” yule mtu aliniuliza huku akiachia tabasamu. Sauti yake ilikuwa nzito.

Nilishtuka sana kuona yule mtu alikuwa akinitambua lakini mimi sikuwa na kumbukumbu naye. Kengele ya tahadhari ikalia kichwani kwangu. Nilijitahidi kumtazama kwa umakini lakini sikuweza kumtambua kabisa na wala sikukumbuka kama niliwahi kumwona popote.

“Sijui naongea na nani tafadhali? Maana sura yako ni ngeni!” nilimuuliza yule mtu huku nikimtazama kwa umakini mkubwa.

“Dah, inamaana sura hii umeisahau?” yule jamaa aliniuliza huku akiendelea kutabasamu. Muda huo alikuwa anapeleka mkono wake kiunoni, nikawa makini zaidi.

“Si vibaya kama utanikumbusha wewe ni nani?” nilimuuliza huku nikiwa makini na nyendo zake baada ya kuona mkono wake ukiwa umetulia kiunoni ukiwa umekamata bastola kwa uficho, kisha akaanza kupiga hatua kunisogelea taratibu.

Okay, isiwe kesi… Naitwa Kas…” yule mtu alianza kusema huku akinikaribia lakini kabla hajanifikia wala kumalizia sentensi yake nikamshuhudia akirushwa hewani kimo cha mbuzi na kuanguka chini kisha akatulia.

Haraka sana nilijirusha kando na kuficha kwenye gari letu huku nikiyazungusha macho yangu kutazama huku na kule, sikuona kitu. Nikaitoa bastola yangu kiunoni na kuishika vyema mkononi tayari kwa lolote huku nikianza kunyata, nikazunguka upande wa pili wa lile gari kuhakiki usalama zaidi kwa sababu nilikwisha hisi mahala hapo hapakuwa salama.

Kisha niliendelea kunyata hadi nilipotokea upande ule ule alioanguka yule mtu, nikamchunguza vizuri na kuyaona matundu mawili ya risasi kifuani kwake, na hapo nikagundua kuwa muuaji alikuwa ametumia bastola yenye kiwambo cha kuzuia sauti. Kando yake nikaiona bastola aina ya Revolver.

“Huyu mtu ni nani, na nani aliyemuua kwa kutumia bastola yenye kiwambo cha kuzuia sauti?” nilijikuta nikiuliza bila kupata majibu. Kitu kimoja tu nilichokifahamu kwa wakati huo ni kwamba eneo lile halikuwa salama hata kidogo. Ilionesha wazi kuwa kulikuwa na jambo zito sana lililokuwa linaendelea pale. Nikawa makini huku bastola yangu ikiwa tayari kwa lolote, maana niilikwisha anza kuisikia harufu ya damu eneo hilo.

Nikakumbuka kuwa mchezo ulianza kwa yule bonge la mtu kunifuata kule chooni akikusudia kuniua lakini nikamuwahi, na sasa mtu mwingine ambaye pia alikuwa na bastola akauawa kimya kimya mbele yangu na sikujua alikuwa nani na alitaka kuniambia nini! Tayari hali ile ilikwisha washa taa ya hatari kichwani kwangu.

Nikahama eneo lile na kunyata hadi kwenye gari la tatu kutokea lilipokuwa limeegeshwa gari la Almasi na kisha nikanyuka ili niondoke haraka toka eneo lile halafu niwasiliane na akina Almasi kuwatahadharisha na hali ile, hata hivyo nilikuwa nimestaajabishwa sana kwa kutokuwaona akina Almasi wakitoka nje hadi muda huo japokuwa nilikuwa nimewatumia ujumbe kuwataka watoke haraka kwa kuwa kulikuwa na tatizo.

Nikiwa natakafari huku nikianza kupiga hatua haraka kuondoka eneo lile la maegesho ta magari mara nikasikia mvumo mkali wa risasi, ambayo nilitambua mara moja kuwa ilitoka kwenye bunduki kubwa aina ya SMG, ikipita karibu kabisa na sikio langu.

Endelea...
 

339

Nikajirusha chini na kuanza kutambaa kama nyoka huku mwili ukinisisimka na kijasho kikianza kunitoka. Halafu nikaenda kujibanza nyuma ya gari moja jeupe aina ya Noah huku nikijiuliza ni nani aliyerusha risasi ile ambayo kwa vyovyote ilikusudiwa kuniua? Je, mtu huyo alikuwepo wapi na alikuwa na tofauti gani na yule aliyemuua yule mtu mbele yangu?

Nikiwa nimejificha niliangaza macho yangu huku na huko kutazama kwa makini lakini sikumwona mtu mwenye bunduki au wa kumtilia shaka isipokuwa niliona kila mtu aliyekuwepo pale nje ya Capital Social Club alikuwa amekumbwa na taharuki baada ya kusikia mlio wa risasi.

Sasa akili yangu ikaanza kufanya kazi haraka haraka maana hali ya eneo lile haikuwa shwari kabisa. Nikakumbuka kanuni isemayo ‘nyoka aliyejificha ni mbaya zaidi kuliko aliye sehemu ya wazi’ hivyo nilitambua kuwa nilipaswa kuwa makini zaidi kwa kuwa sasa nilikuwa napambana na mtu au watu waliokuwa mafichoni tofauti na kule chooni nilikopambana na mtu tukiwa ana kwa ana.

Pia hali ile ilinipa ujumbe kuwa kama nilidhani yule niliyepambana naye chooni alikuwa peke yake sasa hii ilikuwa ishara kuwa walikuwepo wengi, tena walioanza kunitatanisha kwa kuwa sikujua walikuwa wakileta mashambulizi kutokea upande upi!

Wakati nikijiuliza maswali haya nikasikia milio mingine mfululizo ya risasi kulekea kule nilikokuwa nimejificha na kutawanya vioo vya lile gari aina ya Noah lililokuwa limenificha. Wakati huo nilikuwa nimejilaza chini ya uvungu wa gari hilo.

Milio ile ya risasi ilizidi na kuwafanya watu waliokuwa maeneo ya karibu wapatwe na taharuki kubwa na kukimbilia ndani ya ukumbi na hali ile ikawa ni sawa na kupeleka taarifa juu ya vurumai ile iliyokuwa ikiendelea pale nje. Watu wakaanza kutoka ndani ya ule ukumbi kwa lengo la kutaka kushuhudia. Waswahili bhana, hawakujua hatari kitu gani! Huenda walidhani kulikuwa na tukio la ujambazi uliotaka kufanyika na hivyo kulikuwa na mapambano kati ya polisi na jambazi!

Kitendo cha watu wengi kujitokeza kushangaa kikafanya risasi zikome ghafla na hapo nikaanza kujivuta taratibu na kutoka chini ya uvungu wa lile gari aina ya Noah, kisha nikawa natambaa chini haraka kama nyoka nikihama toka gari moja hadi katika gari lingine na nilipofika kwenye gari aina ya Toyota Prado TX lililokuwa mbali kidogo na lile gari aina ya Noah, nikiwa bado natambaa nikahisi kuguswa na kitu cha baridi kisogoni ambacho moja kwa moja nilitambua kuwa ulikuwa ni mtutu wa bunduki aina ya SMG.

Mwili wangu ukaingiwa na baridi. Nikajua kabisa kuwa kama mimi ndiye niliyekuwa mlengwa wa mashambulio yale na tayari nilikwisha patikana. Nikatulia, sikutikisika wala kuinua mkono wangu uliokuwa umeshika bastola maana unapotokewa na hali kama ile ya kuwekewa mtutu kichwani hutakiwi kufanya jambo lolote lile kwa pupa. Inabidi utii kila utakachoambiwa.

“Weka silaha yako chini na uinuke taratibu,” sauti kavu ya kiume iliniamrisha.

Nikaiweka chini bastola yangu na kusimama nikiwa nimenyoosha mikono yangu juu. Ghafla nikamshuhudia yule mtu aliyeniwekea mtutu kisogoni akirushwa juu na kuanguka kwa kishindo nyuma yangu. Nikageuka haraka na kumshuhudia akitikisika mara mbili tu na kutulia huku roho yake ikiwa mbali na mwili. Kichwa chake kilikuwa kimefumuliwa na risasi iliyotoka kwenye bastola yenye kiwambo cha kuzuia sauti.

Nikaruka haraka na kuinyakua bastola yangu iliyokuwa chini huku nikijibanza nyuma ya lile gari aina ya Toyota Prado TX. Nikaangaza macho yangu kila upande lakini sikuona mtu yeyote pale karibu na mahala nilipokuwa. Nilichoweza kushuhudia ni watu waliokuwa wakitazama huku na huko kwa hofu.

Sasa hali ilikuwa ya utata, ilizidi kunitatanisha kwani nilihisi kulikuwa na wauaji tofauti; mmoja akitumia bastola yenye kiwambo cha kuzuia sauti na alikuwa akiua watu wote waliojaribu kunisogelea, na mwingine… alikuwa akitumia bunduki kubwa aina ya SMG, na huenda muuaji huyo ndiye yule aliyeuawa wakati akiwa ameniwekea mtutu wa bunduki kichwani.

Nikiwa katika mawazo hayo ghafla kukasikika kishindo kizito kilichofuatiwa na mlipuko mkubwa. Nikajitupa chini na kuanza kutambaa haraka kama nyoka nikitoweka eneo lile, muda huo macho yangu yalikuwa makini kutazama kila upande, hasa kule kulikotokea mshindo ule na hapo nikaliona gari moja aina ya Jeep lililokuwa katika eneo lile la maegesho likirushwa angani na kusambaratika. Lilipoanguka chini likasababisha moto mkubwa uliosambaa kwenye magari mengine yaliyokuwa katika maegesho.

Kitendo kile kilisababisha mvurugano wa watu katika eneo lile. Watu walianza kutawanyika ovyo kila mtu alikuwa akijaribu kuyaokoa maisha yake. Nami nikapata upenyo wa kuondoka haraka eneo lile huku akili yangu ikianza kuwafikiria akina Almasi, Sofia na Amanda kwani sikujua walikuwa wapi muda huo. Muda wote nilikuwa makini kumtazama kila mtu.

Nilifanikiwa kutoka kwenye geti la kuingilia pale Capital Social Club na wakati naanza kuvuka barabara ili nielekee upande wa pili wa barabara mara ukatokea mlipuko mwingine mkubwa zaidi na uliolitikisa eneo lote la Capital Social Club. Pamoja na ujasiri wangu lakini hali ile ilinitia hofu. Sikutaka tena kuzubaa eneo lile, nilitimua mbio na nilikuja kujishtukia nikiwa mbali na Club ile.

Nikasimama na kutazama kule Capital Social Club. Sasa eneo la Club ile lilikuwa limegeuka kuwa uwanja wa vita, ilikuwa ni kizaazaa cha aina yake. Magari yalikuwa yakiwaka moto. Wakati nikiwa mbali na lile eneo nilianza kujiuliza iwapo akina Almasi walikuwa wamesalimika kwani nilikuwa nahofia usalama wao. Kwa kweli nisingejisamehe endapo wangekuwa wameuawa kwa kuwa ningeonekana kuwa nilishindwa kuwalinda. Kisha nikakumbuka kuitazama saa yangu na kugundua kuwa ilikuwa imefika saa tisa na dakika arobaini na tano za usiku.

Mara simu yangu ya mkononi ikaanza kuita, nikaitoa haraka nikitumai kuliona jina la Almasi, nilidhani huenda walikuwa wakinitafuta kujua kama nilisalimika katika mkasa ule wa kutisha. Lakini nilipoitazama vizuri simu yangu nikagundua kuwa mpigaji alikuwa mwanadada Aziza Msojo, katibu muhtasi wa mkuu wangu katika kikosi maalumu cha siri kinachoshughulika na operesheni hatari ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa.

Nilijikuta nikishanga sana. Akili yangu iliniambia kuwa tayari taarifa za tukio lile la risasi na bomu pale Capital Social Club zilikwisha fika kikosini kwangu, na hivyo walitaka kuhakikisha toka kwangu.

Kwa takriban miezi mitatu sasa nilikuwa nimehamishwa kutoka ofisi yangu ya mwanzo yaani Taasisi ya SPACE na kupelekwa katika kikosi maalumu cha siri kilichoshughulika na operesheni hatari, kikosi hiki kilitambulika kwa jina la ‘The Special Operation Group’ au SOG kwa kifupi, na kilisheheni maofisa wenye mbinu na ujuzi wa hali ya juu.

Endelea...
 

340

Uteuzi wa maofisa wa kikosi hiki ulizingatia vigezo muhimu hususan uwezo wa kukusanya na kuchambua taarifa, uwezo wa kujilinda na kupambana na adui, na uzoefu wa kufanya kazi katika mazingira magumu na ya hatari. Wengi wa maofisa ndani ya kikosi hiki walikuwa ni makomando kutoka jeshini kama Luteni Lister na Daniella Palangyo. Na kwa kufanya mambo kuwa mepesi na yenye ufanisi mkubwa kikosi hiki kilikuwa cha watu wachache tu kwa kila operesheni.

Huyu Daniella Palangyo alikuwa komando katika Idara ya Ujasusi jeshini (Millitary Intelligence) na kwa mara ya kwanza nilikutana naye katika operesheni hatari nikidhani alikuwa mmoja wa wanamtandao hatari wa kigaidi waliomuua Waziri wa Mambo ya Ndani Ummi Mrutu na kusababisha taharuki kubwa (kama ilivyosimuliwa katika mkasa uliopewa jina la Taharuki).

Baada ya kumaliza kazi ndipo nilikuja kugundua kuwa Daniella alikuwa na msaada mkubwa sana kwangu na kwa Idara ya Usalama wa Taifa akifanya kazi kama ofisa kifuniko kwa kumtumia askari wa Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Sajenti Mambo ili kunifikishia ujumbe wa kutusaidia kujua kile kilichokuwa kikiendelea ndani ya mtandao huo hatari na hatimaye tukafanikiwa kuzuia mpango hatari ulioandaliwa na mtandao huo ili kuleta taharuki nchini.

“Hallo!” hatimaye nilisema kwa sauti ya kichovu baada ya kuipokea simu na kuiweka kwenye sikio langu la kushoto.

“Hallo, Jason, hujambo?” Aziza aliniuliza kwa sauti iliyokuwa na hofu kidogo.

“Sijambo. Vipi mbona tunapigiana simu saa hizi?” nilimuuliza Aziza kwa wasiwasi kidogo nikitaka kujua kama sababu ya yeye kunipigia simu usiku huo ilikuwa ni taarifa za mkasa uliotokea punde jijini Dodoma.

“Ukiona hivyo jua mambo si shwari. Mimi nipo hapa ofisini saa hizi, Kanali Mjaka anakuhitaji ofisini haraka sana,” Aziza alisema.

Nilishangaa sana. Sikushangaa kwa kusikia kuwa Aziza alikuwa ofisini muda ule wa saa kumi za usiku kwa sababu nilizifahamu vyema kazi zetu, hatukuwa na muda maalumu wa kuingia wala kutoka ofisini, bali nilishangazwa na kitendo cha mkuu wangu kunitaka haraka sana niwe jijini Dar es Salaam wakati alifahamu kuwa nilikuwepo Dodoma na uwepo wangu jijini humo ulikuwa muhimu mno kwa kipindi hicho.

“Kuna taarifa gani huko Dar, si unajua mimi nipo huku Dodoma?” nilisema na kushusha pumzi.

“Hebu subiri kidogo,” Aziza alisema kisha kukawa kimya, sikujua kama alikuwa akitafakari jibu la kunipa au alikuwa anawasiliana na bosi wake.

Nilianza kupatwa na wasiwasi juu ya hali ile. Pia akili yangu ilianza kufanya kazi haraka nikitakafari jambo gani ambalo lingeweza kufanya niitiwe haraka kule ofisini jijini Dar es Salaam wakati nilikuwa nimepewa kazi ya kufanya jijini Dodoma? Hata hivyo sikuweza kupata jibu la haraka haraka ingawa moja kwa moja nilijua kuwa kama niliitiwa kazi basi ingekuwa operesheni hatari ambayo ingenilazimu kuachana na shughuli nyingine zote ili kuishughulikia haraka.

Dah! Sasa nilihisi mwili wangu ukinyong’onyea zaidi kwani ni miezi mitatu tu ilikuwa imepita tangu nitoke kwenye operesheni hatari iliyonifanya mara kadhaa nijikute nikiponea katika tundu la sindano ingawa mwishoni nilisaidia kuusabaratisha mtandao hatari wa kigaidi, operesheni ambayo ilipewa jina la ‘Taharuki’. Ni matokeo ya operesheni ile yaliyowafanya wakuu wa Idara ya Usalama wa Taifa kuona ninafaa kuhamishiwa katika kikosi hiki maalumu cha SOG.

Kabla kumbukumbu za operesheni ile hatari hazijafutika akilini kwangu, sasa nilikuwa ninaitiwa kazi nyingine ya hatari. Hii ndiyo adha tuliyokuwa tikiipata maofisa tuliokuwa tukifanya kazi katika idara hizi za ujasusi.

“Jason!” sauti nzito ya mwanamume ilinizindua toka kwenye mawazo yaliyoanza kuiteka akili yangu. Mara moja nikagundua kuwa sasa nilikuwa naongea na mkuu wa SOG, Kanali Othman Mjaka.

Kitendo cha kuisikia sauti adimu ya Kanali Othman Mjaka kikanifanya nimeze funda kubwa la mate kuutuliza moyo wangu huku nikianza kuhisi kulikuwa na jambo lisilo la kawaida. Moyo wangu ulipiga kite kwa nguvu na hapo kijasho chembamba kikaanza kunitoka.

“Ndiyo, mkuu,” nilisema kwa sauti tulivu ya unyenyekevu huku nikiilamba midomo yangu iliyokuwa imekauka.

“Sikia… kuna ndege maalumu itaondoka hapo Dodoma saa kumi na moja na nusu alfajiri hii kuja huku Dar. Fanya uwezavyo ufike airport kabla ya saa kumi na moja na umtafute rubani wa ndege hiyo anayefahamika kwa jina la Kapteni Saul Luvanda,” Kanali Mjaka aliniambia.

“Sawa, mkuu,” niliitikia kwa unyenyekevu huku mapigo ya moyo wangu yakienda mbio.

“Nakuhitaji hapa ofisini kabla ya saa moja kamili za asubuhi, hivyo ukiachwa na ndege hiyo utafute namna yako ya kufika hapa ili muda huo uwepo hapa,” Kanali Mjaka alisema na nilipotaka kujibu nikagundua kuwa simu ilishakatwa. Nikabaki na mshangao.

Nilikumbuka kuitazama saa yangu ya mkononi, nikagundua kuwa zilibaki dakika saba tu kutimia saa kumi kamili za alfajiri. Sasa sikuwa na muda wa kupoteza, kwa hali ilivyokuwa nisingeweza kwenda nyumbani kwa Almasi kuchukua begi langu na kisha niwahi airport, isitoshe sikujua kama Almasi na wenzake walikuwa wamesalimika kwenye tukio lile la kigaidi, hivyo nikalazimika kuianza safari yangu ya kuelekea kiwanja cha ndege ili kumtafuta Kapteni Luvanda kama nilivyoelekezwa na mkuu wangu.

Hata hivyo bado akili yangu iliendelea kusumbuka kuhusu Almasi na wengine maana sikuwa na taarifa zao, hakika nilikuwa kwenye sintofahamu maana kila nilipojaribu kumpigia simu Almasi simu yake haikuwa ikipatikana!

* * *

Ni utata mtupu! Nini kipo nyuma ya mashambulizi haya? Jibu utalipata hapa hapa, endelea kufuatilia...
 
Utata ni mwendelezo wa visa na mikasa katika Harakati za Jason Sizya... ni kisa kinachozidi kumchambua Jason Sizya na harakati zake...

SAFARI YA BUZWAGI ilianza kama utani wakati Jason aliposhindwa kuidhibiti zipu yake na kuuonesha ufuska wake kwa kubanjuka hata akiwa safarini, chuki na ghadhabu ya Jameela ikaibuka na kusababisha mauaji kwa sababu tu Jason alisababisha pale alipofunga safari akidai NARUDI BUZWAGI, misukosuko ikampata na kutaka kumtia uchizi katika FUNGATE, halafu sintofahamu ikaibuka wakati akijikuta katika dunia nyingine ya kufikirika, dunia ngeni na yeye akiwa mgeni kabisa lakini mwenyeji wake akamwona kuwa hakuwa mgeni wa kawaida bali ni MGENI MWEMA, na hatimaye akaja kuianza safari nyingine ngumu katika maisha iliyokuja kuzua mambo ya hatari yaliyoishia UFUKWENI MOMBASA, kabla haijazuka TAHARUKI iliyomfanya Jason kuponea tundu la sindano mara kadhaa baada ya kuibua uvundo kutoka kwa mtandao hatari na kisha kudhani ameshamaliza kazi, na sasa anajikuta katika UTATA...

Hii ni zawadi nyingine ya aina yake kutoka kwa mwandishi anayejaribu kuunda dunia ya Jason Sizya. Naamini mtafurahi[emoji120][emoji120]...
 
Hajasusa mtu hapa mida ndio hii Bishop Litro si unaona uvumilivu wangu na mibange nimeukwaa uDED? siku ya kwanza tu kula bata nakutana na "UTATA"
 
Hajasusa mtu hapa mida ndio hii Bishop Litro si unaona uvumilivu wangu na mibange nimeukwaa uDED? siku ya kwanza tu kula bata nakutana na "UTATA"
 
Nipo shamba hapa naisubiria Bishop huku nilipo imegonga Mvua nusu ya usiku wote ngoja nione kama Moto umezimika kule Mlimani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…