Simulizi: Harakati za Jason Sizya

Simulizi: Harakati za Jason Sizya

Hii simulizi ni sisimuzi sana askofu asante sana ni vile tu hulka ya binadamu kutotosheka kirahisi ila leo umetutendea tendo aisee shukrani mkuu wa hii kaya
 
Mimi honestly sioni kama Jason ana mapenzi na mke wake, najiuliza alikua nje mda mrefu hii likizo c ndo angekaa na family abond na mtoto etc kuna namna haya mahusiano hayajabalansi ikwesheni
 
Mimi honestly sioni kama Jason ana mapenzi na mke wake, najiuliza alikua nje mda mrefu hii likizo c ndo angekaa na family abond na mtoto etc kuna namna haya mahusiano hayajabalansi ikwesheni
Haha! Mabaharia kama Jason si wa kuwaamini. Muulize rafiki yake Bob nelly[emoji23][emoji23] ...
 
Simpendi najikuta akipata matatizo nafurahia
 
Haha! Mimi si karani ila jana dada karani aliomba tu kujificha ndani kwangu wakati mvua inanyesha. Mimi ni nani hadi nibishane na serikali[emoji23][emoji23]...

Tuombe Mungu kesho naweza kutupia...
[emoji23][emoji23][emoji23]tutashukuru sana mkuu!..
 
ufukweni mombasa.JPG

248

Watu wengine waliokuwepo eneo la mbele ya hoteli ya Serena Beach Resort katika viunga vya maegesho ya magari na hata kwenye bustani ya maua ikiwa ni pamoja na walinzi wa eneo hilo, hawakuweza kubaini ni nini kilikuwa kimetokea. Lilikuwa tukio la haraka sana na lililonishtua sana. Ila pamoja na mshtuko ule akili yangu ilikuwa inafanya kazi haraka haraka. Mwili ulikuwa bado unanisisimka na damu ilikuwa inachemka na kukimbia kwenye mishipa yangu ya damu.

Niliinuka haraka, baada ya gari lile aina ya Toyota Crown kutoweka, huku nikijitazama kwenye mkono wangu wa kulia uliokuwa na michubuko midogo hasa kwenye eneo la kiko (wengine huita kiwiko) cha mkono. Kisha nikayatembeza haraka macho yangu kutazama huku na kule katika namna ya kuchunguza iwapo kulikuwa na yeyote wa kumtilia shaka, nikagundua kuwa kila mtu kwenye eneo lile alikuwa anaendelea na hamsini zake na hakuna aliyeonekana kunitia shaka.

Hata hivyo nilijionya na kujipa tahadhari kuwa nilipaswa kuwa makini zaidi katika nyendo zangu kwani bado sikuwa na hakika vizuri juu ya adui zangu. Nilishusha pumzi za ndani kwa ndani na kuanza kutembea taratibu kurudi hotelini, mkono wangu wa kuume ukiwa mfukoni, kwenye mfuko wa suruali yangu, na kidole changu cha shahada kikiwa tayari kimetuama vyema kwenye kilimi cha bastola yangu ndani ya mfuko huo.

Wakati nikitembea kuelekea ndani ya jengo la hoteli niliendelea kuwachunguza watu niliopishana nao na hata waliokuwa wanaendelea na shughuli zao ili kubaini kama kulikuwa na mtu yeyote aliyeonekana kufuatilia nyendo zangu. Kisha niliyainua macho yangu kutazama juu ya lile jengo la hoteli, na hapo nikaziona kamera mbili kubwa za ulinzi (CCTV) zilizopandwa mbele ya lile jengo la hoteli. Zilikuwa kamera zenye nguvu kubwa ya kunasa picha za matukio katika mfumo wa video. Nilitambua kuwa kamera zile zingekuwa zimenasa picha za tukio lote lililotokea muda mfupi uliokuwa umepita katika eneo lile.

Na hapo akili yangu ikaanza kufanya kazi mara mbili zaidi katika namna ya kutafuta suluhisho la kadhia iliyonikumba. Hata hivyo kilichoitatiza sana akili yangu ni kuwa nilikuwa bado nipo kizani kuhusu nini kilikuwa kinaendelea nyuma ya pazia kumhusu Rahma wa Singida na kundi lake, japokuwa tangu tulipokutana katika lango la Benki ya NBC, Posta jijini Dar es Salaam hisia zangu ziliniambia kuwa lilikuwepo jambo lisilo la kawaida kwa mwanamke huyo.

Sasa nilitambua kuwa kulikuwa na jambo kubwa na la hatari lililofichika katika mkasa mzima, jambo ambalo Rahma na watu wake hawakutaka lijulikane na walianza kuniona tishio kwenye mipango yao baada ya kugundua kuwa niliwashtukia, na pengine walidhani kuwa tayari nilikuwa nimezipata penyenye za kile walichokuwa wakikifanya.

Hatimaye nikawa nimefika mbele ya jengo la Serena Beach Resort na kuanza kuzipanda ngazi za varanda ile ya hoteli kisha nikaingia eneo la mapokezi. Hapo niliwakuta Wazungu wawili; mwanamume na mwanamke ambao kwa mtazamo tu niliweza kubaini kuwa walikuwa wenzi. Walikuwa wameketi kwenye yale makochi ya sofa huku upande wa pili kukiwa na wanaume wengine wawili na mwanamke mmoja, wote Waafrika na kila mtu alikuwa busy na simu yake au anajishughulisha na mambo yake.

Nilipotupa macho yangu pale kwenye meza ya mapokezi nikamwona mfanyakazi mmoja wa kiume, nikamtambua kuwa ni yule kijana aliyekuwa zamu moja na Merina siku iliyokuwa imetangulia wakati nafika pale Serena Beach Reosrt. Niliwasalimia haraka haraka wale watu niliowakuta pale mapokezi kisha nikaanza kuvuta hatua zangu kueleka kwenye ngazi za kuelekea juu kwenye orofa ya pili kilipokuwepo chumba changu, lakini kabla sijafika mbali nikamsikia yule mfanyakazi wa mapokezi akiniita.

Moyo wangu ukapiga kite kwa nguvu kama niliyeambiwa jambo la kushangaza na la hatari mno. Sikujua ni kwa namna gani hali ile ilinitokea lakini niliziheshimu sana hisia zangu. Nikageuka kumtazama ili nihakikishe kama ni mimi aliyekuwa akiniita, na hapo yule mfanyakazi wa mapokezi akabetua kichwa chake kukubali huku akinionesha bahasha ndogo aliyoishika mkononi kwake.

Taratibu nikapiga hatua zangu kumfuata pale alipokuwa amesimama huku nikimtazama usoni kwa umakini, macho yangu yalikuwa yamefanya kituo kwenye uso wake. Nilipomfikia akanisalimia kwa adabu huku uso wake ukiwa umepambwa na tabasamu la bashasha, halafu akanikabidhi ile bahasha iliyoonekana kuwa na ujumbe ndani yake.

Niliipokea huku nikiendelea kumtazama usoni katika namna ya kumsoma iwapo alikuwa anafahamu chochote kuhusu kilichomo ndani ya ile bahasha. Sikuona tashwishwi yoyote usoni kwake iliyoashiria kuwa alikuwa anajua kilichomo ndani ya bahasha na hivyo macho yangu nikayarudisha kuitazama ile bahasha ambayo juu yake ilikuwa imeandikwa “Jason Sizya, room 204”.

“Ya nini hii?” nilimuuliza yule mfanyakazi wa mapokezi huku nikimtazama usoni kwa udadisi. Akanyanyua mabega yake juu na kuyashusha.

“Sifahamu chochote, mimi nimepewa tu nikupe,” yule mfanyakazi wa mapokezi akaniambia.

“Nani kakupa?” nilimuuliza huku nikigeuza shingo yangu na kuyatembeza macho yangu taratibu kuzichunguza zile sura zilizokuwepo eneo lile kuona kama kulikuwa na yeyote wa kumtilia shaka. Sikumwona na hivyo nikayarudisha tena macho yangu kumtazama yule mfanyakazi wa hoteli.

“Kuna dada mmoja alikuja hapa wakati wewe upo restaurant unastaftahi akaniambia ukitokea nikupe, alisema ukisoma kilichomo ndani utatambua kila kitu,” yule mfanyakazi wa mapokezi aliniambia. Bado uso wake haukuwa na tashwishwi yoyote.

“Yukoje?” nilimuuliza tena huku akili yangu ikihangaika kubashiri angeweza kuwa nani, kwani kwa vyovyote asingeweza kuwa Rahma wa Singida ambaye tulikuwa wote restaurant.

“Ni mweupe, alikuwa amevaa suruali ya jeans ya rangi ya bluu iliyombana na pullneck nyeusi, kichwani alijifunika na mtandio na mweusi na alivaa miwani mikubwa myeusi iliyofunika macho yake. Miguuni alivaa viatu aina ya Travolta,” yule mfanyakazi wa mapokezi alimwelezea huyo dada na hapo hapo kengele ya hatari ikalia kichwani kwangu. Nikaitazama tena ile bahasha iliyokuwa mikononi mwangu.

Akili yangu ikamfikiria Leyla Slim Abdullas, hata hivyo nikaliondoa haraka wazo hilo kwa kujua kuwa sikuwa nimemjulisha Leyla kama nimeingia Mombasa, achilia mbali uwepo wangu katika hoteli hiyo ya Serena Beach Resort. Nililipuuza haraka wazo la kwamba Leyla ndiye aliyeileta ile bahasa. Sasa picha ya Zuena wa Mombasa ikanijia akilini kwangu, nikawaza kuwa huenda ni yeye aliyefika pale hotelini.

Lakini… hebu ngoja kwanza… mbona Zuena alinifahamu kwa jina la Slim Kubanda na si Jason Sizya kama ilivyoandikwa juu ya ile bahasha? Si hivyo tu, niliahidi kumjulisha hoteli ambayo ningefikia lakini hadi muda ule sikuwa nimemjulisha. Hitimisho nililolifika ni kwamba si Leyla wala si Zuena aliyefika hapo kuleta ile bahasha. Sasa… angeweza kuwa nani?

Msichana pekee niliyekuwa na uhakika wa asilimia mia moja kwamba alifahamu vyema uwepo wangu pale Serena Beach Resort, alilifahamu jina la Jason Sizya na nambari ya chumba nilichofikia pale Serena Beach Resort ni Merina peke yake. Lakini asingekuwa Merina kwa kuwa yeye alikuwa mfanyakazi hapo hapo Serena Beach Resort na hivyo huyu kijana wa mapokezi asingeshindwa kumtambua mfanyakazi mwenziwe.

Au labda Merina alikuwa amemtuma msichana mwingine aniletee ile bahasha? Je, ilikuwa na ujumbe gani? Maswali mengi yalianza kupita haraka haraka akilini kwangu na kuzidi kunitatiza.

Nilimtazama yule mfanyakazi wa mapokezi na kushusha pumzi kisha nikamshukuru, halafu nikanyanyua mkono wangu kuitazama saa yangu ya mkononi na nilipojiridhisha na mwenendo wa majira yake nikageuka nyuma na kuyatembeza macho yangu taratibu kuchunguza kama kungekuwa na ongezeko la mtu mwingine eneo lile la mapokezi. Sikumwona mtu yeyote mwingine hivyo nikaamini kuwa hali bado ilikuwa shwari.

Inaendelea...
 
Back
Top Bottom