SEHEMU YA KUMI NA MBILI
Sasa Jax hizi karatasi naziona zina jina na picha zisizo zako, lakini pia kuna saini nyingi sana humu, mihuri sijui vikorokoro kibao, halafu naona ni madini aina ya Rubi? Mimi nikadhani dhahabu au Almasi? niliuliza
Kwanza akacheka sana Kisha akafafanua,
Daniel bwana, eti Almasi,
Hiyo hatuiwezi bwana, tungefikia kujadili habari za hiyo kitu, tungeongelea hapa, ok ila umeuliza swali zuri,
Sasa bwana Dani hapa tunaongelea Rubi kwasababu ndiyo aina niliyoagizwa na tajiri ambaye yeye yupo hapa hapa mjini.alifafanua.
Je,Mimi Daniel nawezaje kuijua kuwa hiyo ndiyo Rubi na hii siyo? niliuliza
Kisha akaniashiria tuingie kwenye gari lake huku akifungua mkoba na kutoa vidude fulani vyenye rangi tofauti tofauti,
Hapa nina aina tatu za madini , hizi chenga chenga ni dhahabu, ukisikia dhahabu ghafi ndiyo hii, na hii ni fake yake usione ni kama zinafanana laini Kuna utofauti mkubwa na kizuri zaidi ni kwamba usiwaze kwakuwa utakuwa na Mimi basi Kila kitu kitakaa sawa. alifafanua mshikaji wangu aliyeitwa Justini au Jax.
Je, tunapataje sasa haya madini yaani tunanunua kwa nani? niliuliza
Ewaaaah swali zuri kwanza kuna zaidi ya mikoa minne ambayo Mimi naifahamu, tunaweza kupata lakini ni kwa baadaye, kwasasa Kuna mtu atatuletea mwenyewe, yaani Kuna jamaa mmoja anaitwa Hussein, yupo hapa hapa yeye alisema Mimi nimtafutie soko lilipo, Sasa nikawaza kuliko nimuoneshe tajiri ni vyema nikakutafuta wewe kwanza ili tuwe tunanunua kwa bei kadhaa na tunauza kwa bei hii.
Ni pesa nzuri tutatengeneza Dani, hebu fikiria tupo tu mjini mtu anakuletea madini, Kuna watu wapo machimboni huko wamewekeza hela ndefu na bado hawana uhakika wa kurudisha hata nusu hasara.aliweka kituo.
Dah sawa bwana ila sijajua tunaanza na mtaji wa shilingi ngapi maana haya ni madini kaka, niliuliza.
Siyo hela nyingi kwasababu Gram moja ya Rubi ni .....na Gram moja ya dhahabu ni .........na unaanza kidogo kidogo hata grams hamsini unapeleka kwa tajiri hata kumi tu unapeleka halafuuuu....
Japokuwa sisi tumelenga Rubi lakini lazima tujue bei zote za aina ya madini na pia anaweza kutokea tajiri mwingine wa dhahabu na vitu vingine
alifafanua
Hela ya hizo grams alizonitajia kiukweli nilikuwa nayo, ila uoga na moyo kukataa vilishika nafasi yake, huku tamaa ikiwa kwenye kiwango kikubwa faida ilikuwa inakuja kama mara mbili hivi, hivyo nilishachanganyikiwa.
Sasa Jax tunapaswa
Tuanze na grams ngapi kwanza, na nakutegemea maana kumbuka hii biashara Mimi sijui chochote. niliuliza
Grams hamsini ingekuwa poa ila si vitu vinapatikana kirahisi , halafu tunatakiwa kuishia grams hamsini tuhata kama ukikuta ana kilo moja lakini pia unadhani ni nyanya hizo dani huyo jamaa yangu Hussein aliniambia ndiyo kwanza ana grams thelathini....................
Si mbaya hizo twende tuwachukue,na kwakuwa tunaanza hicho ni kiwango kikubwa sana , nataka niile faida yake kwanza ndipo naweza shawishika zaidi. niliongea huku nikiwa na hamu sana na hiyo biashara.
Huu ni mzani na hivi ndivyo unavyosoma Mimi nishawahi jaribu kufanya hii kitu sina ugeni nacho,
Wala usiseme Jax Mimi na wewe tulikutana club fulani kwa mara ya kwanza nilikuwa naogopa hata kukusogelea , ulikuwa na mawe kaka na hivi ilikuwaje ukaporomoka maana wewe hujafikisika Bali umeporomoka, niliuliza.
Nilichukua hela ya mkopo Kisha nikamiliki shimo la dhahabu huko mkoani XX , mwanzo nilipata faida sana tu ila baadaye weeeeeeeh
Tena tuache hizi habari, Jana tu nimepita kwenye nyumba niliyouzaga kwa lazima imeniuma sana. na ndiyo maana nimekwambia tunatakiwa kuishia grams hamsini tu hata kama ni zaidi ya hapo,unauza kwanza ndipo unaendelea na mishe zingine. Lakini kumbuka Mimi kwasasa hela Sina na ningekuwa nayo nisingekushirikisha, unaona gari yangu inatoa Moshi hiyo nakosa hata hela nikafanye overall engine , Sina kitu Dani. alifafanua
Kisha tukaagana
Wakati nipo nyumbani niliwaza sana kuhusu mchongo wa ishu ya madini, ni kitu huwa nakisikia kwa watu tu kuwa wanafanya lakini safari hii nikawa nina hamu ya kutaka kujua habari zake ,
Kwanza ngoja nijaribu ila nitakuwa makini kuliko umakini wenyewe, maana haya mambo huwa yana mlolongo mrefu sana, niliwaza huku nikiona ni fursa nzuri kujiongezea kipato.
Siku tatu baadaye rafiki yangu Jastini alinipigia simu kuwa tukutane mahali,
Nikawasha chombo changu Kisha nikamkuta yupo sehemu katulia anakunywa Juisi fulani.
Yaani Jax siamini kama ni wewe ambaye ulikuwa unakesha kwenye mabaa ukilewa sana , Leo hii wewe wa kunywa juisi. niliongea kiutani
Ni vitu vinawezekana hata wewe siku ukiacha pombe , utagundua siyo ajabu kuacha pombe, na hata Mimi nakushauri rafiki yangu wa damu na wa kweli acha pombe, ni kitu ambacho ukitumia wala hupati faida yeyote na ukiacha hupati hasara yeyote chaguo ni lako.
alifafanua
Wewe umeacha au umepumzika?ila hebu tuachane na hayo,
enhee hapa tunamngoja nani Sasa, niliuliza.
Hapa namsubiri jamaa yangu anaitwa Hussein ni afande wa jeshi la polisi aliniambia tukutane saa kumi hii nadhani yupo njiani maana nimetoka kuongea naye muda si mrefu. alinijibu
Afande tena? mimi hao majamaa wamenikalia kushoto kweli yaani , yaani hata nikiwa kwenye sehemu ya starehe akija tu, huwa nahama hiyo sehemu, huwa sitaki kukaribiana nao au kuwa na mazoea nao Sasa kushirikiana kwenye hii ishu tenaaaa.nilinyong'onyea ghafla.
Tatizo lako ndiyo hilo Dani, unapenda sana matabaka, mbona nyumbani kwako Kuna jirani yako ni askari, unataka kusemaje. aliuliza Jax
Yule si jirani tu, tunaonana tunasalimiana imetoka Sina mazoea naye , Wala hata yeye hana time na mimi, tatizo Hawa majamaa wanakuwaga wachunguzi, wapelelezi na uspy mwingi, binafsi huwa sipendi kuwa na ukaribu ila haina shida Kwani tunafanya biashara haramu , si tutafuata sheria? niliweka kituo
Ndiyo hapo Sasa jiulize unakuwa na wasiwasi gani, tufanye kazi bwana acha mawazo potofu. aliongea yule mshikaji wangu huku kwa siku hiyo na Mimi nikiwa nakunywa soda, sikutaka kugusa pombe maana ningepoteza umakini.
Enheeee mtu mwenyewe ndiyo huyu na hii ni pikipiki yake naijua .
Yule Hussein alipaki pikipiki yake Kisha akavua lile kofia lake, lahaulaaa ni yule askari niliyewahi kukutana naye njiani. Tukasalimiana huku nikikosa amani.
Itaendelea....................