Simulizi: Harakati za maisha

Simulizi: Harakati za maisha

SEHEMU YA THELATHINI NA TISA

Nilirudi ofisini kwangu nikaendelea na mishe zangu huku akili fulani ikinijia , kiufupi sikuwa mtulivu,

Shabani bwana, Sasa imekuwaje anataka kuuza chombo ya wife wake tena kibabe, hizi ndoa hizi MUNGU atusaidie sana.
Ila hii gari nauza ugomvi wao Mimi haunihusu , kwanza ngoja nimpigie yule mwalimu siku nyingi ananisumbua magari ya taasisi yetu yatauzwa lini ili naye aweze kupata usafiri Sasa ngoja nimpe hii.
Nikampigia simu........

Hello Madam, naitwa Daniel ni yule uliniagiza nikufanyie mpango wa gari ,na nimeshapata,ipo ni nzuri haijatembea kabisa na bei ni rafiki.
Niliongea kwa mbwembwe huku nikiona pale ningepata hela nijuavyo wanawake wengi wakihitaji kitu huwa hawarudi nyuma na huwa si wabishi kwenye kupatana bei kama sisi wanaume.

Mmmh mwanangu,kwanza pole sana mimi nilishapata gari siku si nyingi.halafu pia ile Cruiser uliyomuuzia mume wangu, kipindi kile ilimsumbua sana tena mno si tukashangaa gari gani haipandi milima,muinuko kidogo tu inashindwa!! Kiufupi mwanangu ulivyokuwa unasifia chombo na kilivyo ni tofauti,ilibidi tuingie gharama zingine kufanya overall Engine na gharama zingine kama Pump na vitu vingine vingi .kiufupi Mr alikunyamazia tu lakini alichukia.
alijibu kisha tukaagana huku nikiona aibu fulani hivi

Niliendelea kuwasaka watu nikiwapigiapigia lakini hakuna hata mmoja niliyefanikiwa kumuweka kwenye ramani.

Niliacha mtumbwi wangu pale ofisini ,nikapanda chombo kipya,lengo nikaweke kwenye gereji iliyopo karibu na nyumbani kwangu halafu nitafute wateja taratibu,maana maeneo ya mjini majamaa wengi wangeingia tamaa ili tuanze kuwa na chain ndefu kwenye mgawanyo wa mshiko.
Huyoooo mpaka nyumbani kwangu.

Mke wangu licha ya kuona usafiri mpya ,hakuuliza chochote wala kushughulika na mimi.
Huwa ni mtu wa kuuliza haswa ukiwa na kitu ambacho si chetu lakini siku hiyo akawa kimya nilishangaa sana.

Nikiwa pale nje napekuapekua simu ili nione kama kuna mtu ataweza kuwa na utayari kwa ajili ya lile gari lakini nilichemka.

Baada ya muda kidogo,kuna watu wawili walikuja pale home,
Nawafahamu ni wasumbufu , hawajui kukataliwa ni kama hawakuwa na akili nzuri kwa mtazamo wangu

Vipi wazee ,
Usiku huu mnakuja kwenye majumba ya watu,hampigi simu ,hamtoi taarifa vipi, huu ni muda mtu anahitaji kupumzika baada ya shughuli za kutwa nzima eenh ,hebu jirekebisheni basi nyinyi ni watu wazima hakuna haja ya kusemana kama watoto.

Eeh mna shida gani,hebu tuingie ndani kwanza,niliongea huku nikiwa nishawachoka.

Sasa bro kwanza tusamehe upo sahihi kwa ulichoongea ,na tukiri wazi tumekosea.ila tumekuja kukuomba msaada wa Jersey kwaajili ya timu yetu ambayo ni kama yako eeeh.
Kifupi tumejichanga pale mtaani tumepata kukidhi vitu kadhaa laini tulitaka utusaidie suala la jezi tu .
aliweka kituo yule jamaa.

Ndugu zangu kwanza napenda niwaweke wazi tu kuwa mimi sina hela kama mnavyofikiria pengine muonekano wangu huwafanya watu wadhani nina kitu mimi ni kama nyinyi tu,tunaishi kiujanja ujanja.
Majukumu ni mengi nashindwa hadi kutimiza baadhi ya vitu.

Halafuuu mnamkumbuka yule mzee Mhindi mswahili mwenye Land Rover?niliuliza

Si yule alikuwa anasimama pale uwanjani ukawa unaongea naye mara nyingi huku akionesha anapenda mpira? waliuliza na wao.

Yes ni yule yule ,
Yule mzee ana hela sana tena mkiongea naye kwa adabu na utulivu atawaelewa.ni shabiki mwenzangu wa Arsenal ya Uingereza,yaani timu yetu licha ya kufanya vibaya kwa misimu kadhaa lakini tutakufa nayo.
Ila kwa suala la pesa nipo vibaya nisiwadanganye.niliweka kituo.

Aaaaaah bro muogope Mungu Brevis ina maganda kabisa hii halafu unasema upo vibaya ,na umeikata lini hii ? Aliuliza yule jamaa mwingine.

Huwezi amini hii siyo yangu kuna jamaa kanipa inasukumwa hii,watu wanataka kufanya mambo mengine tena.niliongea huku tukiizunguka .

Ok sawa kuna demu anataka gari ya mkononi kama hii tena alisema anataka chombo isiwe na matatizo,hii ingemfaa sana hii.

Ana hela ?mimi wanawake wengi nawajua wanalialia sana kwenye biashara wanatakaga kuonewa huruma kila eneo.nilitahadharisha.

Demu yupo vizuri,
tena kama vipi tukupe namba zake muongee wenyewe kwa muda wenu .
Sisi hatutaki shilingi mia yako,ila tunakuombea ufanikishe ili utununulie Jersey tu basi.waliongea huku tukipeana tano na kucheka kisha wakaondoka.

Kwani mume wangu hawa siku zote huwa wanafuata nini hapa? Aliuliza mke wangu.

Si wale watu wa michezo,yaani ni wasumbufu kama nini ,mtu hata ukatae jambo hawajui.nilijibu.

Siku nyingine muwe mnaongelea mambo yenu sehemu nyingine, siyo hapa ,nyumba inakuwa na makelele kama wodi ya watoto,watu mnacheeeka mnagonga mikono hamjui kama ni kero kwa wengine.
Mambo yenu sitaki ndani mwangu leo iwe mara ya kwanza na ya mwisho.aliweka kituo.

Nisamehe mke wangu wala usijali hata hivyo niliwaambia na mimi kwanini waje bila kupiga simu,nilijibu.

Na hiyo gari ni ya nani?
Aliuliza.

Ni ya mshikaji wangu fulani nimeazima yangu imeharibika nimeiacha ofisini .nilidanganya.

Babaaaa wewe una matatizo kama nini,na nimewasikia vizuri kuwa unauza hilo gari sasa kuwa na tahadhari na hiki chombo sitaki kilale
Hapa,na sijui kwanini huwa hukomi tu ,mtu una matatizo chungu mzima lakini bado hujifunzi,huwazi.
akionesha kuchukia.

Sasa usiku huu mimi chombo nitapeleka wapi usiku huu ,subiri asubuhi mimi naondoka nayo wala usijali.nilijibu kisha mambo mengine yakaendelea.

Asubuhi na mapema nilipokea simu kutoka kwa Lewis akinitaarifu jambo.

Shalom mtumishi ,kwanza namshukuru Mungu kwa kutupa kibali tena cha kuongea kwa mara nyingine hakika atukuzwe Mungu.aliongea Lewis ambaye ni mchungaji.

Eeeh kaka nipe taarifa kwanza maana simu yako ni muhimu nilikuwa naisubiri.niliongea kwa sauti ya chini.

Ndugu yetu siku ya leo ataletwa tena mahakamani kwa mujibu wa kanuni sheria akitokea gerezani,
Kwa hiyo sisi ndiyo tunajiandaa kwenda huko muda si mrefu.hivyo tulitaka kujua kama utaungana na sisi kwakuwa ulionesha nia ya kutaka kuwa karibu na sisi . aliweka kituo akinisikiliza.

Hapana mimi huko sitakuja ila nitakuwezesha chochote kitu kwakuwa kwasasa najua mambo yenu mengi yamesimama hayaendi .niliongea huku nikifanya kama nilivyoahidi huku nikingoja feed back kutoka kwa Pastor Lewis.

Nikiwa ofisini nilipiga namba fulani ambayo nilipewa na jamaa zangu ,simu ikapokelewa.

Nani mwenzangu,sauti upande wa pili ilisikika.

Nilijitambulisha huku nikisema shida yangu .

Samahani wewe ni dalali?
aliuliza yule dada ambaye sikuwa nimemuona.

Mimi siyo dalali na hizo siyo kazi zangu,bali kuna jamaa yangu kakwama na hayupo hapa yupo mbali hivyo kaniambia nimsaidie kutafuta wateja nilijibu

Ok ok safi,nataka gari ya maana iwe nzima ,sitaki chombo kiwe kinasumbua kila mara tutagombana ujue na kama una nafasi leo leo nakuja nione.aliongea huku nikigundua anaonekana mchangamfu sana.

Wewe ukiiona tu naamini utaipenda
Iko vizuri sana.nilijibu huku nikigonga meza nikitambua maisha lazima yaendelee.

Niliwahi kutoka huku tukiwasiliana na yule dada kila mara ili tukutane aone chombo kisha tufanye biashara.

Saa kumi na moja nilikuwa kwenye gereji tulivu isiyokuwa na makelele sehemu ambapo napaamini huku nikimngoja yule mgeni wangu

Nilishangaa akija na watu watatu wengine yeye wanne, wanawake wenzie wawili na mwanaume mmoja kutoka na mavazi yake nilijua huyu ni fundi maana alikuwa anatoka kwenye kampuni fulani ya motors . tulisalimiana huku akionekana si haba pesa ndogo ndogo hazimpigi chenga maana kuanzia mkoba ,nguo zake viatu na Cheni ndogo ya silver aliyovaa shingoni ilikuwa si haba unaweza kupata kiwanja pembeni ya mji huku Uwepo wa Convoy ya watu sikupenda mimi nilijua anakuja mwenyewe.

Naitwa Neema jina nililopewa na wazazi wangu, ila hapa mjini naitwa
Grace , maana ni ileile usijali kaka yangu . Dada alikuwa muongeaji kupita maelezo

Sasa kaka Daniiii hii gari ni mpya mimi nitaiweza kweli? Mimi nilitaka ile very cheap niwe na afford bei lakini hiiiiii no no no no.aliongea kwa kujishauwa yule dada

Lakini wale mashoga zake walidai anisikilize huenda tutaelewana ,kisha baada ya kumtajia bei ndipo alipopata nguvu ya kuizunguka kuiangalia vizuri huku nikifungua milango kwa mbwembwe ili awe na imani na amani nayo

Mmmmmh whaaat, ni kweli au macho yanguuuuu,mbona kama hii gari naifahamu,hii si gari ya mama Moo hii,yes ni yenyewe bwaanah, ni wiki moja imepita alinikuta maeneo ya kiluvya akanipa lift.alishtuka yule dada akiongea kwa kubana pua huku mimi nikishangaa .

Mama Moo ni nani wewe dada,
Hii gari kanipa mshikaji wangu anaitwa Shabani na yupo Mkoa Sasa hivi kaniambia nimuuzie.
Niliongea kwa kujiamini .

Sasa Shabani si ndiye mume wa mama Moo . Kisha akawageukia
Wale wenzie , jamani
Ile habari ya ugomvi wa shoga yangu aliyenyang'anywa gari na mumewe juzi niliyowaambia Sasa gari ni hii ,

Shabani anafanya biashara ya mazao yaani nafaka zote, Sasa kwakuwa anakuwa ofisini kwake kwahiyo show nzima huwa anasimamia mkewe,Sasa baada ya mke kununua gari Shabani alishtuka ndipo alipoichungulia account na kukuta Haina kitu na mwanamke kajenga nyumba kuuuuubwa wapi huko sijui ,na pia akajizawadia na gari

hii gari wala si ya muda mrefu mimi ndiye nilimshauri anunue baada ya kuwa kakamilisha ujenzi wa nyumba yake aliyojenga bila mumewe kujua.

Kumbe ndiyo maana shoga yangu Leo mnyooonge , kwenda polisi anashindwa ,gari hajui ilipo na Shabani kaenda Mkoa kufuata mazao safari kaenda mwenyewe, Sasa shoga yangu yupo katikati. Hajui afanyaje.

Weeeee tuondoke jamani hii gari ya moto , kaka Mimi biashara nimeshindwa kama ni hii gari tafuta mteja mwingine. Aliongea yule dada huku wakigonga mikono na mashoga zake wakiingia kwenye gari la kampuni aliyotoka yule fundi wakaishia huku nikishika tama nisijue Cha kufanya.

Jifunze,
Elimika.
Burudika.

Itaendelea......................
 
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
Sasa Jax hizi karatasi naziona zina jina na picha zisizo zako, lakini pia kuna saini nyingi sana humu, mihuri sijui vikorokoro kibao, halafu naona ni madini aina ya Rubi? Mimi nikadhani dhahabu au Almasi? niliuliza

Kwanza akacheka sana Kisha akafafanua,

Daniel bwana, eti Almasi,
Hiyo hatuiwezi bwana, tungefikia kujadili habari za hiyo kitu, tungeongelea hapa, ok ila umeuliza swali zuri,
Sasa bwana Dani hapa tunaongelea Rubi kwasababu ndiyo aina niliyoagizwa na tajiri ambaye yeye yupo hapa hapa mjini.alifafanua.

Je,Mimi Daniel nawezaje kuijua kuwa hiyo ndiyo Rubi na hii siyo? niliuliza

Kisha akaniashiria tuingie kwenye gari lake huku akifungua mkoba na kutoa vidude fulani vyenye rangi tofauti tofauti,
Hapa nina aina tatu za madini , hizi chenga chenga ni dhahabu, ukisikia dhahabu ghafi ndiyo hii, na hii ni fake yake usione ni kama zinafanana laini Kuna utofauti mkubwa na kizuri zaidi ni kwamba usiwaze kwakuwa utakuwa na Mimi basi Kila kitu kitakaa sawa. alifafanua mshikaji wangu aliyeitwa Justini au Jax.

Je, tunapataje sasa haya madini yaani tunanunua kwa nani? niliuliza

Ewaaaah swali zuri kwanza kuna zaidi ya mikoa minne ambayo Mimi naifahamu, tunaweza kupata lakini ni kwa baadaye, kwasasa Kuna mtu atatuletea mwenyewe, yaani Kuna jamaa mmoja anaitwa Hussein, yupo hapa hapa yeye alisema Mimi nimtafutie soko lilipo, Sasa nikawaza kuliko nimuoneshe tajiri ni vyema nikakutafuta wewe kwanza ili tuwe tunanunua kwa bei kadhaa na tunauza kwa bei hii.

Ni pesa nzuri tutatengeneza Dani, hebu fikiria tupo tu mjini mtu anakuletea madini, Kuna watu wapo machimboni huko wamewekeza hela ndefu na bado hawana uhakika wa kurudisha hata nusu hasara.aliweka kituo.

Dah sawa bwana ila sijajua tunaanza na mtaji wa shilingi ngapi maana haya ni madini kaka, niliuliza.

Siyo hela nyingi kwasababu Gram moja ya Rubi ni .....na Gram moja ya dhahabu ni .........na unaanza kidogo kidogo hata grams hamsini unapeleka kwa tajiri hata kumi tu unapeleka halafuuuu....
Japokuwa sisi tumelenga Rubi lakini lazima tujue bei zote za aina ya madini na pia anaweza kutokea tajiri mwingine wa dhahabu na vitu vingine
alifafanua

Hela ya hizo grams alizonitajia kiukweli nilikuwa nayo, ila uoga na moyo kukataa vilishika nafasi yake, huku tamaa ikiwa kwenye kiwango kikubwa faida ilikuwa inakuja kama mara mbili hivi, hivyo nilishachanganyikiwa.

Sasa Jax tunapaswa
Tuanze na grams ngapi kwanza, na nakutegemea maana kumbuka hii biashara Mimi sijui chochote. niliuliza

Grams hamsini ingekuwa poa ila si vitu vinapatikana kirahisi , halafu tunatakiwa kuishia grams hamsini tuhata kama ukikuta ana kilo moja lakini pia unadhani ni nyanya hizo dani huyo jamaa yangu Hussein aliniambia ndiyo kwanza ana grams thelathini....................

Si mbaya hizo twende tuwachukue,na kwakuwa tunaanza hicho ni kiwango kikubwa sana , nataka niile faida yake kwanza ndipo naweza shawishika zaidi. niliongea huku nikiwa na hamu sana na hiyo biashara.

Huu ni mzani na hivi ndivyo unavyosoma Mimi nishawahi jaribu kufanya hii kitu sina ugeni nacho,

Wala usiseme Jax Mimi na wewe tulikutana club fulani kwa mara ya kwanza nilikuwa naogopa hata kukusogelea , ulikuwa na mawe kaka na hivi ilikuwaje ukaporomoka maana wewe hujafikisika Bali umeporomoka, niliuliza.

Nilichukua hela ya mkopo Kisha nikamiliki shimo la dhahabu huko mkoani XX , mwanzo nilipata faida sana tu ila baadaye weeeeeeeh
Tena tuache hizi habari, Jana tu nimepita kwenye nyumba niliyouzaga kwa lazima imeniuma sana. na ndiyo maana nimekwambia tunatakiwa kuishia grams hamsini tu hata kama ni zaidi ya hapo,unauza kwanza ndipo unaendelea na mishe zingine. Lakini kumbuka Mimi kwasasa hela Sina na ningekuwa nayo nisingekushirikisha, unaona gari yangu inatoa Moshi hiyo nakosa hata hela nikafanye overall engine , Sina kitu Dani. alifafanua
Kisha tukaagana

Wakati nipo nyumbani niliwaza sana kuhusu mchongo wa ishu ya madini, ni kitu huwa nakisikia kwa watu tu kuwa wanafanya lakini safari hii nikawa nina hamu ya kutaka kujua habari zake ,

Kwanza ngoja nijaribu ila nitakuwa makini kuliko umakini wenyewe, maana haya mambo huwa yana mlolongo mrefu sana, niliwaza huku nikiona ni fursa nzuri kujiongezea kipato.

Siku tatu baadaye rafiki yangu Jastini alinipigia simu kuwa tukutane mahali,
Nikawasha chombo changu Kisha nikamkuta yupo sehemu katulia anakunywa Juisi fulani.

Yaani Jax siamini kama ni wewe ambaye ulikuwa unakesha kwenye mabaa ukilewa sana , Leo hii wewe wa kunywa juisi. niliongea kiutani

Ni vitu vinawezekana hata wewe siku ukiacha pombe , utagundua siyo ajabu kuacha pombe, na hata Mimi nakushauri rafiki yangu wa damu na wa kweli acha pombe, ni kitu ambacho ukitumia wala hupati faida yeyote na ukiacha hupati hasara yeyote chaguo ni lako.
alifafanua

Wewe umeacha au umepumzika?ila hebu tuachane na hayo,
enhee hapa tunamngoja nani Sasa, niliuliza.

Hapa namsubiri jamaa yangu anaitwa Hussein ni afande wa jeshi la polisi aliniambia tukutane saa kumi hii nadhani yupo njiani maana nimetoka kuongea naye muda si mrefu. alinijibu

Afande tena? mimi hao majamaa wamenikalia kushoto kweli yaani , yaani hata nikiwa kwenye sehemu ya starehe akija tu, huwa nahama hiyo sehemu, huwa sitaki kukaribiana nao au kuwa na mazoea nao Sasa kushirikiana kwenye hii ishu tenaaaa.nilinyong'onyea ghafla.

Tatizo lako ndiyo hilo Dani, unapenda sana matabaka, mbona nyumbani kwako Kuna jirani yako ni askari, unataka kusemaje. aliuliza Jax

Yule si jirani tu, tunaonana tunasalimiana imetoka Sina mazoea naye , Wala hata yeye hana time na mimi, tatizo Hawa majamaa wanakuwaga wachunguzi, wapelelezi na uspy mwingi, binafsi huwa sipendi kuwa na ukaribu ila haina shida Kwani tunafanya biashara haramu , si tutafuata sheria? niliweka kituo

Ndiyo hapo Sasa jiulize unakuwa na wasiwasi gani, tufanye kazi bwana acha mawazo potofu. aliongea yule mshikaji wangu huku kwa siku hiyo na Mimi nikiwa nakunywa soda, sikutaka kugusa pombe maana ningepoteza umakini.

Enheeee mtu mwenyewe ndiyo huyu na hii ni pikipiki yake naijua .
Yule Hussein alipaki pikipiki yake Kisha akavua lile kofia lake, lahaulaaa ni yule askari niliyewahi kukutana naye njiani. Tukasalimiana huku nikikosa amani.

Itaendelea....................
Wacha niweke nukta jua limekuwa kali.
 
Back
Top Bottom