Kuna watu wanapenda kuwananga walevi wakati ndio walipa kodi wakuu wa Taifa 🤔Mkuu rekebisha tabia zako ulevi sio jambo zuriii
As if ushaweka yote...wonders shall never end...Malizia simulizi ili ujue nini kilijiri
Soma ile Aya ya mwisho kwenye episode ya 61.Story nzuri sanaa ila kwenye simu umetuingiza cha kike,uliporudi home uliangalia saa ya ukutani kisha,saa ya mkononi kisha simu kuhakiki muda, kwabajaji huna simu umeacha pub mtaa wa tatu.
Story nzuri sanaa ila kwenye simu umetuingiza cha kike,uliporudi home uliangalia saa ya ukutani kisha,saa ya mkononi kisha simu kuhakiki muda, kwabajaji huna simu umeacha pub mtaa wa tatu.
JD Lete muendelezo achana nae huyo 😂Soma ile Aya ya mwisho kwenye episode ya 61.
Acha kukurupuka.
Muwe mnasoma kwa utulivu kuepusha kujaza comment ana namba ya kazini hio hampi kila mtu tu,namba alotaka ambayo hutumia kwa watu mbalimbali ndo alosahai pub.Story nzuri sanaa ila kwenye simu umetuingiza cha kike,uliporudi home uliangalia saa ya ukutani kisha,saa ya mkononi kisha simu kuhakiki muda, kwabajaji huna simu umeacha pub mtaa wa tatu.
SULUMU.
Nourhan njoo huku mambo tayariSEHEMU YA SITINI NA MBILI
Kupitia mwanga hafifu wa taa ya nje niliweza kuona namna mke wangu alivyokasirika kuliko maelezo.ikabidi kwa aibu niingie ndani huku nikiwaza mambo mengi sana nikijua nishaharibu.
Nikiwa ndani nilisikia muungurumo wa gari ikabidi nitoke niangalie kupitia upenyo mdogo wa geti ,wakati huo mke wangu na shoga yake Jane wapo nje ya geti wakiongea dizaini kama wanaagana hivi .
Gari lenye namba za usajili wa serikali lilikuwa pale nje, huku madam Jane akipanda na kuondoka huku dereva akionekana ni mgeni maana mke wangu alikuwa akimuelekeza njia.
Mke wangu aliingia na kunikuta getini ,
Yaani una wasiwasiiii eeenh ,
Baba kwani nini kinakusumbua,
Najua ni mlevi ndio,ni miaka mingi unakunywa, lakini mbona kama hii pombe inakupeleka pabaya kwasasa,
Hivi unatambua ni matatizo gani umechuma kwa kumpiga yule mwanamke?
Na kwanini huwa huna njia nzuri ya kuongea na mtu mpaka utumie mikono yako?
Halafu huyu dada wa watu,kakufanyaje mpaka umuite malaya ,wakati alikuja na taarifa nzuri tu eeeh,ila nisikufiche mume wangu,
Kwa hapa umechuma matatizo.
Huna uwezo wa kushindana na mume wa yule dada,niwe mkweli tu kakupita vingi.yaani ni kila kitu.
Kuanzia umri,uchumi,umaarufu na vingine vingi.
Wewe anakujua nani baba,na hata kama unajulikana labda ni kwa waajiri wako tu na baadhi ya majirani.
Hata huo umaarufu ambao huwa unaniambia unao,mbona kama hujulikani maana baadhi ya watu nikiwaeleza kuwa mume wangu ni mtu fulani ,bado huwa nagundua wengi hawakujui,usijivunia kuonekana kwenye TVs na magazeti,wala siyo mafanikio hayo hujawa popular baba yangu.
aliweka kituo mke wangu baada ya kuongea kwa kirefu.
Kwani mke wangu lile gari lililokuja kumchukua yule mwanamke ni la taasisi gani ? niliuliza huku nikihema.
Hebu tuingie ndani kwanza usijifanye mtoto wa mwenzio kama mgeni wakati nipo kwangu.
(Huku tukitembea kuja ndani)
Yule ni mdogo wake na Jane kamfuata dada yake,tumeamua kumpigia ili aje maana usiku huu usafiri tungepata wapi. Halafu naomba niache nipumzike
alijibu kwa kifupi mke wangu.
Lakini vipi kuhusu gari limeharibika sana eeh? niliuliza.
Nimesema niache nipumzike ungetaka majibu mazuri ungesikiliza, ikifika asubuhi utajionea mwenyewe, Mimi Sina majibu. alijibu kwa sauti inayoashiria usingizi unamchukua.
Nililala lakini ni moja ya usiku ambao sikupata usingizi kabisa, kwanza niliwaza kuhusu gari kuonekana limeungua, ni gari ambalo hurahisisha mizunguko yake mingi Sasa ikiwa limeungua likaharibikaaa, mmmmh itakuwaje?
Halafu inaonesha huyu Jane ana tagi ubavu Sasa kama kweli mume wake kanizidi vingi kama alivyosema mke wangu itakuwaje?
Nilijiuliza maswali mengi huku uoga ukininyemelea kwa mbali.
Ni saa ngapi usingizi ulinipitia, sikujua ,ila nakumbuka niliamka mapema na kuingia bafuni nikamaliza kusudi langu, nikajiandaa vyema kabisa, huku wakati nikifanya hayo yote mke wangu alikuwa kitandani bado. ni hali ilinishangaza kwasababu si kawaida yake.
Nikaamua kumuamsha na kuvunja ukimya kwanza,
Hilo gari mnasema mliweka gereji gani vile nataka nikalione!
Niliuliza
Asubuhi hii ni gereji gani itakuwa imeshafunguliwa, na hizi gereji za kiswahili ndiyo kabisaaa.wewe nenda kazini ukija utalikuta tu.
alijibu huku akiamka na kukaa kitako.
Niliwasha ngalawa yangu na kuingia mpaka mtaa wa tatu ili angalau nikachukue simu yangu, Cha ajabu nilifika pale nakukuta ni kimya ni duka Moja tu lilikuwa limefunguliwa huku wanafunzi wakiwa ni wengi pale dukani . Nikashuka na kwenda hadi pale huku nikisubiri watu wapungue ili niulize, kweli ikawa vile.
Asalaam aleykum sheikh, nilisalimia vile baada ya kukuta muuzaji ana haiba ya kiostaz.
Akaitiikia huku akinikaribisha vyema.
Samahani kaka, nauliza huyu mwenye hii pub anakaa wapi labda maana nilikuwa namuhitaji.
niliweka kituo.
Samahani kiongozi Mimi mambo wala habari za watu wanaojishughulisha na uuzaji wa pombe usiniulize, labda kama una shida tofauti na hiyo sema. aliongea huku uso wake ukionesha kukasirika.
Nenda kamuulizie huko nyuma ya haya mafremu maana hapa ni kwa wazazi wake. alijibu mama mmoja aliyekuwa pale dukani.
Vipi hana mume yule dada,
Niliuliza hivyo nikiwa nachukua tahadhari.
Hehehehee wewe baba usinichekeshe, yaani asubuhi hii watu hawajapiga hata mswaki nyie tayari mnawaza ngono asubuhi tu loh.na huyu msichana atamaliza watu jamani khaaa!
alileta dharau yule mama.
Halafu wewe jamaa muonekano wako hata haufanani na maongezi yako mdomoni wakati unakuja hapa nilikuona wa maana sana.
alipigilia msumari yule ostaz muuzaji wa pale dukani.
Nilitoka pale kwa aibu huku nikiangalia saa Kila muda nisije kuchelewa kazini. Nikazunguka kule nyuma ambapo geti fulani lililokaa kiswahili lilikuwa wazi huku wanawake zaidi ya sita wakionekana ni wapangaji mle ndani wakinikaribisha mle ndani huku wakiongea maneno fulani wao kwa wao, kama hujazaliwa uswazi unaweza sema wanaongea mambo yao kumbe wanakusema wewe .
Samahani ndugu zanguni namuulizia huyu dada mwenye hiyo pub .
Niliongea mara baada ya kuwasalimia.
Eeeh dada weeeee !!!
Mungu akupe nini mtoto wa mazahouse weweeee.
Watu hawapati usingizi wanaamua kuja asubuhi tu nasema usipojenga mwaka huu hujengi teeeena.alikuwa ni msichana wa kwanza akiongea.
Sema dada yetu nyota imewaka tuache masikhara wewe mtu na suti yake saa kumi na mbili za asubuhi yupo kwenye majumba ya watu , huyu mganga wako ni kiboko aisee.
ni maneno yalichukiza ila sikuwa na jinsi wanawake wale ukiwachokoza ni aibu utapata.
Mara yule dada wa ile pub alitoka na kanga yake ambayo kwa makusudi imevuka kwenye magoti yaani maungo yake yalionekana sehemu kubwa.
Karibu kaka, karibu sana.
alinikaribisha huku akija huku nje ili tuwe huru kuongea.
Samahani dada yangu Jana nimesahau simu yangu hapa vipi uliiona? niliuliza.
Hee! wee vipi, ulisahauuuu?
au ulinipa?
wewe si ulisema nichukue tu , ukadai utanunua nyingine siyo wewe?
Sema hata hivyo Mimi mwenyewe nililewa maana si kwa bia zile ulizotupiga, nilisahau kama hata laini hujatoa acha simu isumbue weeee
yaani Kuna wale mashoga zangu sijui kama wameamka, loh weee mbaba Mungu akuweke una pepo ya peke yako. aliongea kwa kunisifia yule dada.
Samahani labda nililewa kama hiyo simu ipo nipe nataka kuwahi kazini.
Yule dada aliingia ndani Kisha akanipa simu yangu.huku nikikutana na missed calls kama mvua.
Sasa swaiba? Nipe hata hela nikapate mchemsho maana siyo kwa hii hangover. aliniomba hela eti.
Wewe Mimi Sina hela nawahi kazini ujue baadaye nitakutafuta.
Nilijibu huku nikitoka kwa spidi maana jua nalo lilikuwa limetoka sana .
Jifunze,
Elimika,
Burudika.
Loading............
Shusha vitu shusha mkuu.....story imenoga aseeeSEHEMU YA SITINI NA MBILI

Tunaelimika Sana pombe sio kitu kizuri asee......SEHEMU YA SITINI NA TATU.
Nikiwa nahemea juujuu nilifika ofisini nikiwa nimechelewa kwelikweli.
Nikakutana na boss getini .
Yaani ulikuwa mkosi wa aina yake.
Daniel ndiyo unafika?
aliuliza huku akiwa anashusha miwani yake.
Ndiyo boss ni foleni tu hakuna kitu kingine si unajua tunaoishi pembeni ya mji. Niliongea huku nikijipendekeza.
Siku nyingine jitahidi bwana , maana Kuna watu wamekuja tumeongea nao wameshaondoka, hivi kwa mfano wangekuhitaji?
Huoni kama unaiaibisha taasisi!
acha hizo Daniel.ila Mimi nasafiri naenda Mkoa X nadhani kurudi ni baada ya siku mbili hivi. aliniambia boss.
Kwanza nilifurahi kuona kaongea na Mimi kirafiki , pili Kila akipata nafasi ya kusafiri Kila mmoja hufurahi kutokana na alivyo, alikuwa anaogofya si mchezo.
Naam, baada ya kupunguza majukumu kadhaa nikaamua kuwacheki watu wa muhimu ambao walinitafuta ile jana pindi simu ikiwa kwa yule dada,
huku namba ngeni ambayo ilipiga mara mbili tena usiku sana nikiipiga lakini haikupokelewa.
Kuja huku inbox nikakuta Kuna meseji nyingi za kawaida, ila Kuna meseji moja hii ilinitisha zaidi,
Ilisomeka hivi,
Habari Mr Daniel, hope u mzima.
Naomba tu kujua mke wangu kakukosea nini kiasi Cha kumdhalilisha!
Lakini najua wewe una akili timamu najua ipo sababu ya msingi ambayo huenda ilipelekea wewe kufanya uliyofanya. Nimeamua kuahirisha shughuli zangu ili tuje tuongee kiume . Sitaki kukuhukumu kabla sijajua ukweli. "
Ilikuwa meseji moja ilinisisimua na kunitisha huku tumbo likikoroga, wakati huo huo simu toka kwa mke wangu iliingia.....
Eenhee niambie wife umeshindaje? Nilisalimia kwa upole.
Mimi niko salama salimini ila asubuhi nilipokea simu kutoka kwa Jane kuwa anaumwa na hata hivyo tumempeleka kituo cha afya , kusema ukweli ulimuumiza sana mwanamke wa watu yaani mashavuni Kuna alama za vidole kabisa , jamani mume wangu kwani ilikuwaje ile jana?
Ndugu wa Jane wapo hapa wengine wanatamani wafike ofisini kwako ila nimewaficha maana watakudhalilisha, haya kingine tumesikia mume wake anayefanya kazi huko mkoani naye ameshafika na amemuona mkewe alivyoumizwa.
Ubavu wake wa kulia anadai unamsumbua baada ya kumpiga mateke bila hata huruma.
Ila Daniiiiii, mume wangu ninayaongea haya mara nyingi ila sijajua kwanini huwa hunisikii. aliweka kituo mke wangu.
Kwahiyo wameenda polisi si ndiyo?
Niliuliza kwa sauti ya uoga.
Sasa angetibiwa vipi bila PF3 na lile ni shambulio? kifupi mume wangu una kesi tayari. alinitisha mke wangu.
Naomba unielekeze lilipo gari nikalione ili nijue tunafanyaje. Nilimwambia.
Mke wangu alinielekeza huku akiambia niwe makini maana ndugu kwa upande wa Jane wanechachamaa huku baadhi wakiwaza kulipa kisasi, mke wangu alinitahadharisha.
Saa nane mchana nilichukua gari la ofisini nikaingia nalo mtaani huku nikielekea mahali ilipo gereji husika, na kuingia mle ndani huku vijana wake wakija kwa pupa wakidhani labda nimekuja kutengeneza gari,.
Tukasalimiana huku nikiwaambia Kuna gari ililetwa na mke wangu Jana yake hivyo nataka nione hali yake,.
Niliruhusiwa huku nikishangaa gari mbona ni nzima Mimi nilidhani imebaki chuma chakavu.
Tulifunua boneti hapo nikagundua kweli imeharibika maana nyaya zote ziliungua na bahati nzuri wasamaria waliwahi kuzima na mchanga
Sasa fundi, hii itapona kweli maana inatisha ujue niliuliza kwa hali ya kuikatia tamaa.
Kwanini isipone , hapa ndiyo mahala pake na hii shock imetokea kutokana na kupeleka kwa mafundi umeme wa bei rahisi wewe ona mwenyewe, huu ufungaji wa waya, ni fundi gani atafanya hivi, au ni wewe mwenyewe bro, eeh unaweza kukikosa chombo kwa ubahili wa hela ndogo tu.hapa Kuna mafundi wenye vyeti vyao pia Mimi ndiye C.E.O hapa. alifafanua yule fundi aliyeonekana ni muongeaji mzuri.
Kwahiyo unanihakikishia litapona si ndiyo? Niliuliza.
Hapo wewe na ulivyojipanga tu
Kuna gari mbovu zaidi ya hili na zimepona ziko barabarani, na shukuru Mungu watu walizima mapema pengine ingeisha kabisa ohoooo. Lete pesa vijana waingie mzigoni. aliongea yule fundi kwa mbwembwe.
Mimi Sina pesa kwa leo ila naomba nipe siku tatu tu nijipange nitakuja tuianze hii kazi. nilimwambia ukweli.
Ziwe siku tatu kweli,
Wengi mna tabia ya kuacha gari Kisha mnapotea, hapa siyo parking jamani, magari yanatakiwa yapungue yaingie na kutoka eneo lenyewe dogo hili . Lakini hata hivyo tupo ubaoni tu bro na hii ni miongoni mwa kazi tuitegemea, acha hata ya kijiwe basi. (Akinitaka niwaachie pesa)
Nipe namba yako nitakurushia jioni ili muianze kazi kabisa kesho.
Niliongea Kisha tukaagana. Huku nikiwa makini sana mtu akiniwashia taa tu pengine kuomba njia Mimi naona labda ni ndugu zake Jane, hakika alivuruga kichwa changu.
Nilimpigia wife simu kwamba achague nguo kadhaa Kisha aniletee maeneo ya mjini.
Kweli baada ya masaa mawili na nusu hivi jua likielekea kuzama alikuja maeneo fulani akiwa na uso uliosawajika.
Mume wangu ni afadhali ungenipiga Mimi mwenyewe, Mimi ningekuvumilia si kwasababu nakupenda sana, ila ni kwasababu ni mzazi mwenzangu, baba wa watoto wangu, ni rafiki yangu, nimekuzoea lakini hali si hali , ndugu zake Jane baadhi wanasema lazima wakupige ili wakukomeshe ingawaje mumewe anakataza akidai Sheria itafuata mkondo na kutokana na sababu ile mume wake amekasirika sana , Tena anadai ana hamu akuone wewe ni mtu wa dizaini gani. eeeh. aliongea mke wangu.
Haina shida ila Mimi nasafiri naenda mkoani nitarudi baada ya wiki. Ila kitakachojiri utaniambia na waeleze kuwa nimesafiri au wanipigie simu.
niliongea kwa kujiamini kimwili ila uoga ulichukua sehemu kubwa.
Wapi tena?
Yaani unaniachia msala si ndiyo?
alihoji mke wangu.
Nakuachia msalaaa au naenda kazini?
Ina maana hujui kama kazi zangu ni za kusafiri safiri?
Kwahiyo niache safari nianze kumfikiria Jane?
Wewe niache niende nikirudi tutayajenga tu , najua nimekosea tutaombana msamaha Kila kitu kitakaa sawa tu. niliongea kwa msisitizo mke wangu akawa hana namna akakubali kishingo upande.
Kwahiyo hata hurudi nyumbani unaondokea huku huku mume wangu? aliuliza kwa sauti ya chini yenye huruma.
Ndiyo hivyo haya hivyo nimechelewa naenda Mkoa wa mbali na inabidi kesho niingie kazini na hakikisha yule kijana haondoki pale nyumbani, mpaka nikirudi mwambie kama ni malipo nitamuongezea maana mwanaume ni mwanaume tu.
Mke wangu alinitakia safari njema huku akitafuta taxi na kuondoka.
Sikuwa na safari ya mkoani Wala Nini ila nilikuwa naogopa kuja kudhalilika mbele ya mke wangu, nikaona njia rahisi ni kutoka nyumbani kwa muda.
Nilirudisha gari la ofisi nikachukua langu na kwenda kutafuta lodge ya bei nafuu ili nikae kwa muda wa wiki nzima nikijua wale jamaa hasira zitawashuka tu, kwenda wakiwa wa moto ni sawa na mbwa kuingia mdomoni mwa chatu.
Simu zilikuwa nyingi za vitisho kutoka kwa ndugu wa Jane huku wale wajuba wakionesha ni wababe si mchezo, ila niliwaambia nimesafiri nikirudi tutayajenga.
Simu pekee iliyonitisha zaidi ni ya mumewe Jane, baada ya kuniambia kuwa atafika ofisini kwangu hata kama sipo ataeleza tabia zangu zote ambazo kazisikia toka kwa baadhi ya majirani , na kwa cheo chake atahakikisha nafukuzwa kazi , akinishauri ni vyema tuonane tumalize. Lakini Daniel sikuwa tayari kuonana na wale jamaa kwa muda ule. Maana wangeniweka ndani (lockup) au kunipiga wanikomeshe.
Usiku niliongea na mke wangu huku akionesha ni mwenye huzuni, hata Mimi pia nilikuwa ni mwenye huzuni mno nikiwaza Sasa haya ni maisha gani tena!
Huwezi amini hata nikiyaona magari ya kusafirisha pombe mwili ilikuwa inasisimka ni kipindi pombe niliona ni zaidi ya shetani. Je, kwenye jiji la wenye unaweza kujificha?
Nini kitajiri , usikose sehemu ijayo.
Jifunze,
Elimika,
Burudika.
Itaendelea..............
Samson haukomi jamani ukimaliza hilo utafata lingine.SEHEMU YA SITINI NA TATU.

Nimecheka Sana kuishi kama dikidiki😂Hakuna kitu kibaya kama kutafutwa na watu ,nlipataga ka msala fulani aisee sitakuja sahau nlikuwa naishi ka digidigi maisha haya hapana aisee