Simulizi: Harakati za maisha

Simulizi: Harakati za maisha

We m

A

We mavi nitolee ushamba wako wa ileje hapa mi nachangamsha genge tu tatizo u think et niko siriaz?! Smh wanaume tukiongea jifunze kukaza kanga kifuani usubiri haki yako usiku mbwa wahed matus ya mikoani et shobo nani bado anatumia hilo neno la 90s ukute hapo umekuja kurisit mitihani kwa shemeji unapanga foleni na dadako kuukali msengerema wewe mazafanta
Poor you.
 
Mtu umejoi juzi af unaninukishia mdomo legend naeweza kukuzaa huku napigana gaza sometimes sio must kuonesha ushamba
Wanasema mjinga mpuuze yaani Kuna maneno mtu akiongea namcheka namdharau namuona mpuuzi wa mwisho. Umeona majibu ya Jack Daniel ndo mwanaume wa kisawasawa anavyo jibu una type eti we mavi 😂🤣 eti legend,legend my foot.
 
Wanasema mjinga mpuuze yaani Kuna maneno mtu akiongea namcheka namdharau namuona mpuuzi wa mwisho. Umeona majibu ya Jack Daniel ndo mwanaume wa kisawasawa anavyo jibu una type eti we mavi 😂🤣 eti legend,legend my foot.
ACha kusifia wanaume utafikwa na koni endelea kusugua vuzi la shemej hapo ushenzini ugeni wako wa jf usituletee umama na ushamba kaa kimya when men talks kifusi fool
 
Ni stor tu inawafanya mnaburuzana hv??? [emoji1787][emoji1787][emoji1787]nmecheka balaa
JF uwanja wa Fujo,halafu nakumbuka marehemu leadermoe aliniambia humu JF Kuna watu wa kila aina washenzi na waungwana muhimu wale washenzi kuwaepuka.halafu mtu utasikia sie ma legend JF wewe mgeni unaishia kucheka maana JF Niko miaka kwa ID nyingine ambayo nilisahau password ikabidi nifungue hii mpya.
 
SEHEMU YA SITINI NA NNE

Asubuhi na mapema niliamka huku kitu cha kwanza ikiwa ni kupiga simu ili nijue familia inaendeleaje,lakini kubwa zaidi ni kuhusu maendeleo ya Jane kuhusu afya yake.

Pole na safari mume wangu ,vipi ulifika muda gani? Maana mkoa ulioenda ni mbali sana.
mke wangu aliniuliza.

Mimi nilifika salama tu,
Ila naomba kujua vipi hali ya Jane anaendeleaje?na vipi kuhusu vitisho vya mume wake pamoja na ndugu zake wamefikia wapi?
Niliuliza.

Jamani mume wangu mbona unaulizia familia za watu badala ya familia yako,
Kwanza naomba ujue kuwa kijana wetu haonekani tangu jana Mida ya saa tano usiku jana.
Kabla hajamaliza maneno yake nikadakia.....

Alienda wapi na ilikuwaje akawa hayupo,na pia wewe ulijuaje kama hayupo? niliuliza maswali mfululizo.

Wote tukiwa na hofu haswa baada ya wewe kuondoka ghafla bila kujiandaa kama nilivyozoea na mbaya zaidi ukaniachia msala,wote tulipooza sana siyo mimi ,siyo dada wa kazi wala kijana wetu kila mtu alikuwa na mawazo.

Baada ya kupata chakula cha usiku ndipo nilipo mwambia kuhusu maagizo uliyotoa kuwa akiwa kama mtoto wa kiume anapaswa kuhakikisha ulinzi ndani ya nyumba kutokana na vitisho tulivyopata mchana kutoka kwa ndugu wa Jane.
Na kijana alinielewa vizuri sana huku akitoka ili akafunge geti vizuri lakini tulishangaa kuona harudi ndani licha ya dakika kadhaa kukatika.

Mimi na dada wa kazi tuliamua kutoka nje ili tujiridhishe nini kinakwamisha mwenzetu ashindwe kurudi,cha ajabu tulikuta geti lipo wazi na yeye hayupo huku tukigundua huenda katekwa na mtu kwani hata viatu vyake (sendoz)
Vilikuwa pale pale nje.
Ikabidi turudi ndani haraka baada ya kubaini uwepo wa watu wabaya.

Lakini hatukuwa na namna ikabidi turudi kufunga geti huku tukihakikisha sehemu zote haswa ndani kama huenda mtu yeyote mwenye nia ovu akajificha humu ndani lakini hatukuona mtu.

Nikaamua kupiga simu polisi kwenye kituo chetu cha karibu hapa lakini nikaambiwa niende leo asubuhi kwani kwa usiku ule hakuna askari atanisaidia . maana muda ulienda
Nikaamua kukupigia wewe niombe ushauri lakini hukupatikana nikajua labda uko njiani bado na network inasumbua.

Na kijana wako hata simu aliiacha sebuleni maana alikuwa anaenda tu akafunge geti vizuri kisha arudi lakini ndipo alipotoweka jumla ,sasa hapa nakuomba mume wangu fanya hima wasiliana na maaskari ili tujue mtoto wa watu anapatikana vipi na kumbuka namna wazazi wake walikuwa wanamkataza asiwe na mazoea na wewe wakikuona kama gangster la mjini

Daniel mume wangu fanya hima nisaidie mwenzio najua upo kwenye majukumu yako lakini ni vyema tukalitanguliza mbele hili kabla wenye mtoto wao hawajaingilia kati fanya chochote niokoe umeniachia mizigo mizito haya ya Jane hayajapoa,limejitokeza lingine.
aliweka kituo mke wangu baada ya kuongea muda mrefu sana.

Sawa mke wangu nakupigia baada ya muda mfupi usijali kisha nikakata simu.

Niliamua kukata simu ili kuyatafakari yale maneno yake huku moyo ukiniuma sana,lakini pia hasira zilianza kuninyemelea niligundua familia ya Jane inahusika kwa asilimia nyingi juu ya upotevu wa kijana wangu, kijana ninayemkubali kinoma,akiwa hana jeuri wala kiburi.
Huku akiwa na adabu zote.
Huku nikiwa mbioni kumuandalia mazingira mengi ili awe kwenye ramani fulani ikiwa ni sehemu ya shukurani zangu kwake kutokana na mengi anayofanya nyumbani kwangu.

Sasa kwanini wapuuzi wachache wameamua kuhamishia matatizo kwa kijana wa watu masikini.
Ni mpole ,ni mtu asiyejua mambo mengi ,ni mchamungu haswa.
Sasa kwanini wamteke?
Kwani wasingenisaka mwenyewe?
nilijiuliza maswali mengi nikiwa nishakasirika kwa zaidi ya asilimia sabini.

Nilikumbuka kuwa jana Mida ya saa nne walinipigia simu wale ndugu wa Jane wakiendelea kunipa vitisho vyao ndipo nilipoizima simu na nadhani ndiyo maana mke wangu hakunipata kwenye simu.niliwaza sana.

Niliingia bafuni nikajiswafi kisha nikarudi huku nikiwaza kumwambia mke wangu ukweli kuwa nipo mjini sipo mkoa kama nilivyodanganya ili nirudi tumtafute kijana wetu lakini kuna akili iliniambia hakuna haja.

Kama kawaida niliripoti kazini nikiwa natokea lodge ambapo kwanza nilianza kujiona muoga sana why nijifiche lodge huku nikiiacha familia?
Je kama wangetekwa wote Ningejuaje?niliwaza kwa dakika kadhaa huku nikijiona mjinga na sikuwaza mbali kwasababu niliziba uso huku mwili mzima ukionekana.

Nikiwa nalazimisha tabasamu kwa wafanyakazi wenzangu,huku nikiwa nimepanga nisijulikane na yeyote kama nina matatizo na sikuwa tayari kumsimulia yeyote .
Niliendelea na kazi huku nikiwa na hasira nyingi sana nilitamani nione yeyote kutoka kwenye familia ya Jane wakinipigia ili nijibizane nao kiume lakini hakuna aliyepiga nikaishia kupokea simu zingine tu .

Baada ya muda fulani nilipokea simu kutoka kwa mke wangu.........

Mbona uliniambia utanipigia baada ya muda mfupi lakini hujapiga,ina maana haya mambo huoni kama ni mazito?

Huoni kama ni tuna janga kubwa sana mume wangu haswa kuhusu kijana wa watu?
Hata huyu dada leo sitaki hata atoke nje ya nyumba achilia mbali nje ya geti hili na pia kuna simu nimepokea kutoka kwa wale jamaa zake na Jane wanakuulizia na wametoa vitisho zaidi ya jana.sasa huoni kama nipo hatarini baba.
akilalamika mke wangu kwa sauti tulivu na ya chini kama vile alikuwa ananinong'oneza eti.

Nilikata simu kisha nikaenda kwa boss wangu yaani meneja mdogo,
Nilimwambia nina matatizo nikiwa naomba ruhusa huku nikiwa mnyenyekevu mno muda ule.

Danieli ndugu yangu unajua nafasi yako kwenye taasisi hii ni kubwa sana,yaani tunakuhitaji sana,
Hatuhitaji suti na huo muonekano wako,bali kile kilicho ndani yako.
Halafu sihitaji uniambie matatizo yako ila nakuruhusu uende nakupa siku tatu na pia kumbuka nikikuhitaji basi uje mara moja.
Pia nikutakie mema kwenye utatuzi wa changamoto zako.na utamuona
(Jina kapuni) ili umuage na yeye .
Ni maneno ya meneja akitaka nimpitie mtu mmoja ambaye huhusika na masuala ya nauli n.k.

Mpaka saa sita mchana nilikuwa natoka pale ofisini huku nikiliacha jengo na kuingia njia ielekeayo lodge.

Lazima niiokoe familia yangu,lazima nirudi nyumbani,wanaume tumeumbwa mateso,tumeumbiwa shida na matatizo si kuyakimbia bali ni kukabiliana nayo.
Nilijiwazia huku nikiwa nimeshafika lodge kuchukua vitu vyangu.

Niliangalia kwenye mkoba wa kazini nikakuta manati yangu iko full ,na haikuwahi kutumika kizembe nikaisunda Chemba kisha nikatoka huku nikichukua usafiri binafsi na kuikamata njia ya nyumbani kwangu nikiwa siogopi chochote wala lolote.

Jifunze,
Elimika,
Burudika.

Itaendelea.......................
 
Ndugu wapenzi na wafuatiliaji wa simulizi hii kwanza niwaombe radhi kwa kuchelewesha ni majukumu yanabana.

Pili mimi naandika simulizi inayonihusu (code nazingatia)
si kwa kuuza bali ni kushare ili watu wajifunze na pia waburudike.

Tatu ningeomba tuishi kama marafiki na ndugu kwenye hii simulizi,kuna comments nimesoma kiukweli zimenisikitisha sana.
Ni vyema kubadilika.

Kwani ukitukana unapata faida gani?
Acheni utoto basi.badilikeni
 
Ndugu wapenzi na wafuatiliaji wa simulizi hii kwanza niwaombe radhi kwa kuchelewesha ni majukumu yanabana.

Pili mimi naandika simulizi inayonihusu (code nazingatia)
si kwa kuuza bali ni kushare ili watu wajifunze na pia waburudike.

Tatu ningeomba tuishi kama marafiki na ndugu kwenye hii simulizi,kuna comments nimesoma kiukweli zimenisikitisha sana.
Ni vyema kubadilika.

Kwani ukitukana unapata faida gani?
Acheni utoto basi.badilikeni
Sawa mkuu tuko pamoja .....Wanaojibu vibaya ww achana nao"Asiyejua maana haambiwi maana"
Usivunjike moyo tuko pamoja mkuu tukielimika na kujifunza mengi
 
JF uwanja wa Fujo,halafu nakumbuka marehemu leadermoe aliniambia humu JF Kuna watu wa kila aina washenzi na waungwana muhimu wale washenzi kuwaepuka.halafu mtu utasikia sie ma legend JF wewe mgeni unaishia kucheka maana JF Niko miaka kwa ID nyingine ambayo nilisahau password ikabidi nifungue hii mpya.
Sasa kama ulishauriwa uwapuuze mbona unashindwa kitu kidogo kama hiko we mrembo,.tatizo ushamba ungekua na id ya zamani ni rahis kujua kuwa hii ni mpya ila kwa vile wewe ni zero huwez jua aya fuata ushauri wa marehemu kuku mgeni wewe
 
Ndugu wapenzi na wafuatiliaji wa simulizi hii kwanza niwaombe radhi kwa kuchelewesha ni majukumu yanabana.

Pili mimi naandika simulizi inayonihusu (code nazingatia)
si kwa kuuza bali ni kushare ili watu wajifunze na pia waburudike.

Tatu ningeomba tuishi kama marafiki na ndugu kwenye hii simulizi,kuna comments nimesoma kiukweli zimenisikitisha sana.
Ni vyema kubadilika.

Kwani ukitukana unapata faida gani?
Acheni utoto basi.badilikeni
Tuko pamoja Samson Mzee wa misala 😄
 
SEHEMU YA THELATHINI NA SABA

Siku inayofuata baada ya kupunguza baadhi ya kazi zangu ofisini , niliamua kupiga simu kwa ndugu yeyote wa Jastini ili tupange namna ya kumsaidia,akili ikaniambia kumpigia simu mkewe ni kujitengenezea mazingira mabaya hasa ukizingatia jamaa yupo jela.

Nikakumbuka nina namba ya mtu ambaye nilikuwa nakwaruzana naye muda mwingi ambaye alidai ni dada yake ambaye hatujawahi kuonana ,kiufupi simfahamu na huenda hata yeye ananifahamu.
Nikampigia huku moyo ukinienda mbio maana nilijua natonesha vidonda vya watu na pia yule mdada sijui mmama hakuwa na lugha nzuri sana anaonekana ni mkali mkali,lakini nikalivaa tu lile jambo nikaweka simu sikioni.

Hello nani mwenzangu!
aliuliza upande wa pili mara baada ya kusalimiana.

Naitwa Daniel,mwezi uliopita ulinipigia kwaajili ya masuala ya ndugu yako Jastini.nilijitambulisha.

Oooh sawa nimekukumbuka,
Unasemaje? au unataka nini ?
aliuliza.

Nimepata taarifa za rafiki yangu Jastini kuwa yule gerezani,kifupi nimesikitika sana ila nina wazo fulani dada yangu.niliongea kwa tahadhari huku nikimsikilizia kwa umakini.

(Huku akitoa kicheko hafifu)
Mdogo wangu yupo jela ndiyo,lakini nikushangae wewe,kwani unataka nini kwetu?
Kwanza ulisema huhusiki na masuala ya Jastini ukidai tukuache na tulikuacha kweli licha ya Jastini kushindwa kukuhusisha moja kwa moja lakini ndugu tunatambua kuwa huenda mna kiapo mlichojipangia kuwa kama mmoja akikamatwa basi msitajane,ni kweli hakukutaja licha ya kupewa kibano kikali ataje wahusika na hakutaka kutaja yeyote.sasa ni biashara gani isiyo na washirika?
Ni kwamba ndugu yangu ni mjinga sana.aliweka kituo.

Samahani mama tunaweza kuonana tuongee kirefu ? niliuliza .

Inawezekana!
Lakini kwani unataka nini kwetu wewe,maana nahofia usalama wangu.aliongea akionesha ni mwenye wasiwasi kidogo.

Kuwa na amani dada ,mimi sina nia mbaya ni kwamba nahitaji tujadili hatima ya rafiki yangu Jastini kuwa usiogope.

Sawa mimi nipo maeneo ya mahakama ya (akiitaja mahakama ilipo)
Najaribu kuonana na watu fulani tujue namna ya kushughulikia haya masuala.alijibu.

Sasa dada kama upo hapo nadhani ni jambo jema kwanini tusionane tupange kabisa,eeeh ndani ya dakika chache nitakuwa hapo . niliongea kwa pupa .

Basi subiri nimalize mambo yangu kisha nitakupigia simu maana kuna mtu namsubiri hapa niongee naye . aliweka kituo.

Mida ya saa saba mchana tulionana yule mama ambaye kiukweli alikuwa ni mtu mzima tofauti na nilivyodhani huku akiwa na wenzake watatu , wanawake watatu akiwemo na yeye na mwanaume mmoja.walikuwa makini sana huku wakinitazama kwa hofu huenda walijua mimi si mtu mwema.

Nilijitambulisha kwa mara nyingine huku tukiingia kwenye mgahawa mmoja hivi,lakini hata mimi nilikuwa makini nao maana ni kama tunawindana.

Naitwa Lydia kama nilivyokuelekeza kwa siku ya kwanza,huyu ni mtoto wangu ,akimuonesha yule mwanaume ambaye ni kama umri tulilingana tu.na hawa ni ndugu wa mke wa jastini.alinitambulisha kwa wale watu huku akiniangalia pasi na kupepesa macho,sijui alijua labda nina manati nitamdhuru!!

Mimi kama nilivyowaeleza mwanzo ni kwamba sihusiki na habari za Jastini na mnavyosema hakunitaka huko kituoni licha ya kupewa mateso ,ni kweli kwakuwa asingeongea uongo kwakuwa sihusiki ila ni kwamba ni rafiki wa karibu,siyo kikazi ama kibiashara bali maisha ndivyo yalivyo.niliongea huku wakionesha wanakubali.

Kwanza bro mimi nikushukuru sana,kwa kuweza kutaka kushirikiana na sisi kumnusuru Jastini ambaye mimi ni mjomba wangu,na tangu mwanzo ,mama yangu na ndugu wote niliwaeleza kuwa wasihangaike kutafuta nani ama nani ,kifupi uncle wangu alishakuwa kwenye matatizo hivyo hakukuwa na haja ya kutaka kuwaumiza na watu wengine tusiokuwa na ushahidi nao.

Lakini kwa kufupisha maelezo ni kwamba Jastini anakabiliwa na kesi kubwa ya kufanya biashara ya nyara za serikali (madini)bila. Vibali huku akitambua kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.hivyo yupo jela kwa shitaka hilo na si vinginevyo.maana wale wadai wake walishamsamehe.alifafanua yule niliyetambulishwa kuwa ni mtoto wa dada yake Jastini.

Kwanza nilipenda maelezo yake lakini pia huenda tabia ya Jastini alikuwa anaijua siku nyingi hivyo hakushtuka hata kusikia mjomba wake yupo lockup . Baada ya hapo nilimuita tuongelee kwenye gari nikiwaacha wale wanawake wanakula.

Kwanza nikushukuru kwa kunifahamisha vizuri maana mama yako alikuwa anaongea kwa vitisho sana kiasi cha kumuogopa .niliongea huku nikijichangamsha.

Sikia bro,mimi Jastini namjua vizuri sana,mimi mwenyewe kashachukua hela zangu nyingi sana huku akijaribu kunishirikisha kwenye biashara zake lakini nikawa nagoma,pia si mimi tu wapo wengi ambao kawatapeli ,huku wengine wakisamehe na wenye madeni makubwa makubwa ndiyo hao wanakuja.hivyo bro usiwe na shaka na mimi ndiye niliyemtuliza mama kuwa asikusumbue kwani nilijua moja kwa moja utakuwa huhusiki maana kwanza mjomba wangu kwenye biashara hiyo yupo kitambo sana,na kilichomfanya arudi nyuma kimaisha ni baada ya kutamani kununua kuliko kuwa mchimbaji.aliongea yule jamaa huku nikifurahi angalau nitapumua maana Dah mwezi mzima hata bia sinywi,zitashukaje na nina mawazo.

Tulibadilishana contacts zetu huku nikiona sasa yule ndiye mtu sahihi ambaye nitaongea naye jambo likaeleweka kuliko wanawake.

Naitwa Pastor Lewis unaweza kusave hivyo ndiyo utanikumbuka vizuri,pia karibu sana kanisani kwetu.aliongea huku akitabasamu.

Kwanza nilimuangaliaaa kisha nikamuuliza.

Kwani wewe ni mchungaji,maana nilikuwa nawaza tukitoka hapa upige hata mbili tatu japo mimi bado niko kazini nisingekunywa.niliongea nikiwa namshangaa maana hakufanania na uchungaji,

Ndugu yangu hakuna jipya chini ya jua ,sisi binadamu ni wakosefu na ipo njia impendezayo mwenyezi Mungu ambayo ukiifuata hutatetereka.hata mjomba wangu nilikuwa namwambia mara kwa mara lakini labda aliniona mpuuzi.kumbuka yanayofanyika yote leo yalishafanyika,na kwanza nikushukuru kwa hicho ulichotaka kunipa ,na nikushauri tu kuwa kwani ukinywa hizo bia bro unapata faida gani? sisemi unakosea ila waweza kunipa faida hata mbili tatu ili nijue.aliweka kituo.

Hapana ni mazoea tu hivi vitu vina faida basi,ni kwamba tulijikuta tunashawishika tu kuvitumia.niliongea kwa aibu fulani hivi maana kutangaza ulevi mbele ya hawa wachungaji huwa sipendi.

Daniel,una jina zuri la nabii mkubwa sana kwa mujibu wa biblia ,okoka sasa hujachelewa ,ukisoma kitabu cha Muinjili Marko,anatuonesha ni jinsi gani tunapaswa tutubu na kuiamini Injili, wakati ni sasa Danieli.
aliweka kituo.kisha nikaenda kuwaaga wale akina mama ambao imani ilirudi tuliagana kwa furaha kisha nikarudi ofisini huku nikiwaza vitu vingi ila tayari nikushukuru kuona wameamini kuwa sihusiki na msala wa ndugu yao.

Nilirudi nyumbani mapema ,kumbuka mwezi mzima na tangu nitoke kule kwa mganga sikuwahi kugusa pombe,kwanza bado sikuwa na imani ya moja kwa moja kuwa matatizo yangu yameisha nilijua naweza kukamatwa muda wowote na maaskari hivyo nikajiweka mbali na vyombo kwa muda ili nijue mbivu na mbichi kwanza.

Nikiwa barabarani katikati ya foleni kuna jamaa alikuwa anauza vitabu vingi sana,na mimi ni mpenzi wa vitabu nikaamua kumuita huku nikichukua kitabu fulani kinachohusu masuala ya uchumi kikiandikwa na mhadhiri fulani wa moja ya chuo kikuu bora Duniani Havard ,nikasema hiki kitanisaidia kuzugazuga ili nisiwe natoka ndani,kwanza mchungaji Lewis kaniongezea kitu pombe siyo ya kuendekeza.

Jifunze,
Elimika
Burudika.

Inaendelea......................
Leo nimieshia hapa
 
Ndugu wapenzi na wafuatiliaji wa simulizi hii kwanza niwaombe radhi kwa kuchelewesha ni majukumu yanabana.

Pili mimi naandika simulizi inayonihusu (code nazingatia)
si kwa kuuza bali ni kushare ili watu wajifunze na pia waburudike.

Tatu ningeomba tuishi kama marafiki na ndugu kwenye hii simulizi,kuna comments nimesoma kiukweli zimenisikitisha sana.
Ni vyema kubadilika.

Kwani ukitukana unapata faida gani?
Acheni utoto basi.badilikeni

Niombe radhi kwa niaba ya wanaokutusi,binafisi nimejifunza kuhusu Pombe kupitiliza na hasira vina madhara sana kwa familia.Mungu anisaidie
 
Back
Top Bottom