feisal firdaus
JF-Expert Member
- Apr 6, 2022
- 424
- 675
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ni kama uliacha ndgo sana au macho yangu...niliaga huku nikiacha kumi moja maana sikuwa na namna.
unanitenga sanaAiseee 😊
Hamna Babu sikutengi si unajua tena mambo mengi nishachoka nipo mwishoni.unanitenga sana
Jitahidi ufanye mazoeziHamna Babu sikutengi si unajua tena mambo mengi nishachoka nipo mwishoni.
Kawa bannedChizi maarifa monitor wa hadithi ngoja akuamshe
Khaaaaa......!!!!Jack Daniel Kaka Muhandisi tuna arosto tupe kimoja
Kimoja? [emoji23][emoji23][emoji23]Jack Daniel Kaka Muhandisi tuna arosto tupe kimoja
Ila Jack Mungu anakuona[emoji26]Kimoja? [emoji23][emoji23][emoji23]
Basi kesho asubuhi na mapema.
Kimoja? [emoji23][emoji23][emoji23]
Basi kesho asubuhi na mapema.
Daniel Mungu akusaidieSEHEMU YA ISHIRINI
Kwa muda huo Kila mmoja alikuwa na hasira sana,licha ya kuwa bado moyo wangu uliniuma sana tu.
Jastini hana shukrani kabisa yaani kumpigania kote bado ananilaumu?
Nakosa usingizi, nashindwa kufanya na kukamilisha mambo yangu nikivunja ratiba kisa yeye, jinga sana hili jamaa. Pesa hana halafu analazimisha watu wamjali na kumpa heshima kama zamani, anasahau kuwa heshima hailazimishwi.
Maisha ni kama ligi ya mpira tu , timu inayofanya vizuri, ndiyo hukaa nafasi za juu huku ikijizolea wafuasi na wadau wengi, na ndiyo maisha yalivyo huwezi kuheshimika kama hujitumi, halafu Jastini hakubaliani na hali anataka watu wamjali hata kama yupo low level, Akhi haiwezekani. nilijiwazia.
Jioni ile nilirudi nyumbani kisha nikawakuta majamaa fulani pale home , wakionesha walikuwa wakinisubiri.
tukasalimiana.
Aisee Dani vipi , yaani umekuwa adimu mno, kwanini? Kwenye stadium huonekani, yaani umekuwa busy sana kaka vipi, njoo uokoe jahazi,wewe ndiye kila kitu kaka.aliongea kwa uchungu fulani yule jamaa wa kwanza.
Mnamaanisha nirudi kwenye mambo ya mpira wa miguu? niliuliza huku nikishangaa
Yes bro, watu wote tulikukubali na Kila mtu anaheshimu mchango wako hakuna tena kama wewe, ile ni timu uliianzisha wewe, licha ya kuwa ilianza kwa kusuasua lakini ilifanya vyema sana, ni mwaka sasa, hatukuoni bro hebu fanya jambo na hapa ilikuwa tuje wengi lakini tumeamua kuja watatu tukiwawakilisha wenzetu. tunaamini kwa uwepo wako Kila kitu kitakaa sawa. Aliongea jamaa wa pili huku wote wakitikisa vichwa kukubali.
Sawa nimewaelewa nitawajibu ndani ya wiki hii. niliwajibu wale jamaa Kisha wakaondoka wakiwa na matumaini nyuso zao zilionesha kitu .
Kisha kwa hasira nikaingia ndani huku mke wangu akionesha alikuwa ananingoja kwa hamu, hakutaka hata salamu.
Mume wanguuu hawa wageni wako Mimi nawatambua vizuri, naona hukomi wala huwazi mbali,
Mume wanguuu hizo harakati zako hizo!! hayo mambo yako hayo?
Hivi unafahamu ulitumia kiasi gani kipindi kile kwenye haya mambo ya kijinga ya mamipira? ukawa hutulii nyumbani, ukazidisha ulevi, yote hayo ni kwasababu timu lako halikuwa likifanya vizuri hivyo ukawa mwenye stress sana kweli vitu havina msingi wowote. aliongea kwa uchungu mke wangu.
Hebu kwanza kaa chini utulie huwezi kuongea na Mimi Ukiwa umesimama hivyo, hiyo ni tabia gani?
usiwe hivyo jua kuwa unaongea na nani, Mimi nakusikiliza na nakuelewa halafu hakuna haja ya kuongea kwa sauti kubwa my wife, Kaa tulia , eleza mtazamo wako, nitakuelewa. nilishauri
Daniel, Daniel sijakuita mume si kwamba sikuheshimu, bali nataka uelewe kuwa lazima nisimame kama mke kutetea maslahi na mustakabali wa maisha yako na ya watoto wetu, hao watu wanaokutaka urudi kwenye mambo ya mpira hawakutakii mema hata kidogo , Bali naiona harufu ya wewe kufilisika. mke wangu alikazia sana
Tulishindwa kuelewana ikabidi niingie chumbani kwanza maana unaweza kushitukia kofi limekutoka maana wake zetu wa kiswahili Hawa wakianza kuongea unaweza kujikuta unafanya jambo la aibu na jamii ikakucheka.
Baada ya kuingia chumbani niligundua watu kadhaa wamepiga huku Jastini akipiga mara nyingi sana, ikabidi nimtafute maana niliona huenda ana shida , huku nikijipanga kwa mashambulizi ikiwa tu atajitoa ufahamu nikasema lazima nitamsemea mbovu.
Wewe Dani sikia, wanaume wenzio tumeshakujua na nikwambie tu ukweli, Mimi siyo ndugu yako Wala jamaa yako unajua fika tumekutana tu mjini Sasa hiki ulichokifanya hakika utajutia na nina ushahidi wa watu kadhaa, hebu nirudishie mke wangu Daniel, namtaka mke wangu.
Vijisenti vyako haviwezi kuwa fimbo ya kuninyanyasa Mimi mpuuzi wewe.
aliongea Jastini kwa hasira akifoka
Kidogo nilitetemeka lakini nikajikaza na kuuliza, kwani mwanangu wewe una shida gani na Mimi?
Mbona hutulii Jastini?
Huongei jambo ukaeleweka?
Halafu wewe ni mwanaume kaka , punguza hasira zako mambo ya muda ule bado unayo tu? niliongea kwa upole maana jamaa yangu nasikia stori zake kuwa watu wa machimbo hawanaga huruma.
(Huku akicheka)
Mashuhuda wanasema wewe asubuhi ulipita hapa , tena alfajiri tu yaani baada ya kugundua nipo ndani mahabusu, ukatumia fursa hiyo kumtorosha mke wangu? Nimerudi hapa sijamkuta mke wangu, nimeuliza majirani wanasema walimuona akiondoka majira ya asubuhi ni muda mfupi baada ya wewe kuja kwangu na kuondoka, inaonesha hakuchukua muda na yeye akatoka kwa mlivyokubaliana
Dani nikueleweje.
Na tena ulimpa na pesa mke wangu Dani, watu walikuona mbona? yaani ulishindwa tu kumpandisha kwenye gari lako lakini mkapanga muonane mbele siyo, na nimejua ndiyo maana hukutaka kunidhamini, akili yako nifungwe ili umfaidi mke wangu si ndiyo? Sasa nikwambie tu kuwa kwa Sasa umeingia sehemu siyo wewe mjinga.
Na pamoja na kuwa Mimi na mke wangu tuna maisha magumu yanayosababishwa na hali ninayopitia, lakini hajawahi kuonesha anataka kuachana na mimi Sasa kwa hili Dani utanitambua Mimi siyo yule afande Hussein uliyelala na mkewe bila hata aibu,yaani wewe mtu unaonana naye siku hiyo hiyo mara tayari ukalala naye,na Kaa ukijua kuwa nafasi ya Hussein na kiapo chake vinamuweka njiapanda anashindwa kuamua akufanye nini.lakini siyo mimi nitakuonesha. aliongea kisha akakata simu.l
Licha ya kupiga mara kadhaa ili nimfafanulie ilivyokuwa lakini hakupokea nilianza kujuta, maana muda mwingine unaweza fanya jambo la huruma Kisha mambo yakakubadilikia, Sasa huyo mkewe atakuwa kaenda wapi? au ameamua kunitega tu huyu Jax? nilijiuliza
Kwa tahadhari nilitoka nje nikamuita mke wangu ambaye alifura kwa hasira akiwa hataki nijihusishe na mambo ya mpira, nikiwaza na kuona huyu ni mtetezi wangu hivyo napaswa nimtoe hofu kwanza lazima niongee naye, maana naweza kutekwa nikakosa msaada.
Nikamuita mke wangu tukizunguka nyuma ya nyumba huku nikiwa napiga simu ya Jax Kila muda lakini haikupokelewa.
Mimi Nina kazi mume wangu naona umeniita lakini simu ipo sikioni , kama vipi maliza kuongea na hao Kisha utaniita, halafu hii kuongelea huku nyuma wakati tupo nyumbani Mimi sipendi, mke wangu alikosa amani.
Mke wangu, kwanza naomba nisamehe mimi kwa yale yaliyotokea kipindi kile, nilishajifunza mama, hela niliyopoteza ni nyingi mno , nikipiga hesabu nadhani ni mtaji mkubwa sana kama ningeanzisha biashara yeyote huenda ningekuwa mbali sana. lakini nilifilisika, nikajifunza. Ni kweli tangu zamani nilikuwa napenda mchezo wa mpira wa miguu, niliucheza na pia ni shabiki wa vilabu mbalimbali wewe ni shahidi , mara kadhaa nikikesha hapa home nikiangalia mpira kiasi cha kugombana mara kadhaa
Lakini pia kwa akili zangu timamu nikishirikiana na wadau na washauri kadhaa tulianzisha timu yetu ya vijana ambayo , ni kweli ilikuwa inaniburudisha , lakini baadaye tukaanzisha ligi yetu huku Mimi nikiwa kama mfadhili na muwezeshaji wa ile timu, na hapo ndipo kufilisika kulipoanzia kwani Hakuna aliyekuwa anatoa hata senti tano yake ni Mimi mwenyewe nilihusika kwa Kila kitu. nilifafanua
Lakini ukweli ni kwamba nilijuta na najuta hata leo hii na sipo tayari kurudia kosa hili mke wangu mwenyewe unajua Sasa nakushangaa kwanini umechukia kiasi hicho. niliuliza
Mume wangu,matajiri ndiyo husaidia timu za mpira kwa uwekezaji wenye mahesabu,huku hata wasipopata faida,wakiwa hawaathiriki na chochote kwani wengi wao ni sehemu ya kuridhisha nafsi zao. Sasa wewe na umasikini wako ukakurupuka, hebu heshimu pesa baba,.
Lakini pia wewe umewaambiaje wale watu waliotoka
Si umesema utawajibu ndani ya wiki hii, kumbuka nimesikia Kila kitu Sasa hii ina maana gani,
si wanakaa wakikutegemea?una maana gani kuwapa matumaini,si ungewakatalia tu. aliongea huku nikigundua hasira zimepungua.
Ile ni namna ya kuwatoa tu hapa, kumbe utafanyaje , utawafukuza? Haiwezekani. Lakini ukweli ni kwamba siwezi endelea na habari za mpira tena. niliweka kituo huku nikigundua mke wangu kaelewa.
Kwani mke wa Jax atakuwa kaenda wapi, halafu masikini Mimi nilitoa elfu kumi tu, ningempa hamsini au laki nzima ingekuwaje, mmmmh huu msala sasa, hizi habari zikimfikia wife ni shida, lakini pia Jax ana roho mbaya sana, MUNGU nisaidie mke wake apatikane, yule Jax ni mtu asiyeogopa chochote namjua, haogopi kudhulumu, haogopi jela, yaani ubinadamu umemtoka siku nyingi sana, Sasa nitafanyaje, halafuuuu Hawa majirani waliniona vipi mbona mtaa ule ulikuwa kimya sana? nilijiuliza huku uoga ukichukua nafasi kubwa.
Itaendelea...... ...................