Robot la Matope
JF-Expert Member
- Apr 10, 2015
- 8,174
- 16,794
Tuendelee
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dan kwa misala, hujambo!SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
Moyo wangu ulisisimka sana kwa kile alichokisema Jastini huku nikimuona jamaa siyo wa kawaida hana uoga kwenye Mali ya mtu.
Jastini akaendelea........
Kwahiyo baada ya kukaa lockup kule mkoani kwa zaidi ya siku tatu Kisha nikarudi Dar es salaam kwa kuungaunga, ndipo nilipomtafuta afande Hussein nimpe habari kuwa mchongo umeharibika ,
Alipokea taarifa ile kishingo upande huku nikigundua amekasirika sana Lakini hakusema chochote, tukaachana kisha nikakupigia wewe simu ili tukutane unipe madini ili tukauze nikijua Kuna chochote kitu nitapata ili nisogeze maisha Lakini ukaniambia umeuza
Hakika nilichanganyikiwa sana , Lakini nashukuru ukaniambia kama ni asilimia zangu za udalali utanipa , tukapanga tukutane kwenye hotel ya (akitaja jina)ambapo kabla hujafika tayari nilishadakwa na maaskari nikapelekwa kituoni nikitambua afande Hussein ameshanichora. alifafanua Jastini.
Maelezo ya Jastini yalitugusa wote mle ndani si mkewe, si mke wangu, Wala Mimi mwenyewe, nyuso za wanawake wawili zilionesha huruma sana hata Mimi Kuna muda nilimuhurumia Jastini licha ya kuwa ni jana tu alitoka Kunitishia Mimi na familiar yangu ila harakati zake ambazo hazikuwa na matunda zilitia huruma.
Jastini akaendelea..........
Nilikaa kituo kidogo cha polisi kwa masaa zaidi ya nane kabla sijahamishwa na kupelekwa Kituo cha kati, hata hivyo niliwaza Ina maana Dani hana taarifa yeyote kuhusu kukamatwa kwangu? shukrani ziende kwa ndugu zangu ambao walikuja kunidhamini huku wakati natoka nikakutana na wewe Daniel pale nje kabla hatujatibuana kwa kukosana kiswahili.
Nilifika nyumbani kwangu nikaangalia huku na huko sikumuona mke wangu, nikaulizia kwa majirani wakasema hawajui huku wakikuhusisha wewe Dani kuhusu kupotea kwa mke wangu maana asubuhi ya siku hiyo kabla sijadhaminiwa ulionekana nyumbani kwangu huku ukimpa kiasi kikubwa cha pesa. aliweka kituo Jastini.
Ni kweli nilionekana nikitaka kumpa taarifa za wewe kuwa mahabusu Lakini kwa hali niliyomkuta nayo , nikaona nitamuongezea matatizo zaidi na sikumpa kiasi cha pesa wanachosema, Mimi nilitoa hela ya vocha tu kuwa anitafute baadaye ili tuwe tunawasiliana, nadhani ilikuwa ni noti moja ya elfu kumi. nilifafanua huku point ile nikimlenga mke wangu na nashukuru MUNGU kwanini siku ile nilijikuta nakuwa bahili? Ni kwamba my Lord alikuwa upande wangu.
Jastini akaendelea.......
kiukweli baada ya hapo sikuwa na imani na wewe tena na nilikuchukia huku nikiwa na asilimia miamoja kuwa wewe unahusika na upotevu wa mke wangu, lakini cha ajabu jana baada ya kutoka hapa mchana nilimkuta mke wangu nyumbani ambapo aliponieleza alipokuwa niliridhika ni kwamba alikuwa kwa ndugu zangu, na nilichelewa kujua haya kwakuwa simu yangu muda mwingine naizima kwasababu ya madeni niliyokuwa nayo, na Kwa taarifa za chini chini nasikia yule mke wa afande Hussein yupo mji huu toka huko porini anakofanyia kazi na atakuwa amekuja kwaajili yangu. aliweka kituo Jastini akionesha ni mwenye wasiwasi sana.
Kwahiyo hiyo million tatu shemeji huwezi kuilipa kwa namna yeyote ili uwe na amani? mke wangu aliuliza.
Lakini Jastini alicheka kidogo Kisha akaniangalia mimi na huku akikohoa kidogo.
Ndugu zanguni Mimi nadhalilika hapa mjini Nini million tatu? Kwa hela anazonidai yule mwanamke ni nyingi yaani million tatu ni kama elfu tatu tu kwa hela anazodai ni kwa kipindi kirefu, mbaya zaidi alishakataa ushirikiano na mimi, halafu Nina madeni kwa watu wengine pia hakika safari na nyumba ile naona inaenda kuuzwa. aliongea kwa hisia kali Jastini kiasi cha kudondosha chozi.
Jastini mtu mwenye kiburi na anayejiamini pande la mtu,jitu lenye kipara muda wote, aliwahi kusema huwa hapendi kufuga nywele kwani huwa zinachukua asilimia kadhaa za ubongo,na pia mwenyewe aliwahi kusema kamwe hawezi kudondosha machozi kizembe ,akidai machozi ni ya thamani kubwa kwa mwanaume lakini,hatimaye alilia mbele ya wanawake wawili,huku aibu nikiiona Mimi, hakika hakuna kitu kibaya sana kama shida.
Wakati huo mke wangu alikuwa na imani tena kwangu kwani maelezo ya Jastini yalijitosheleza mno. Kazi ilikuwa kwa mke wa Jastini ambaye alikuwa analia kama mfiwa haswa baada ya kusikia kuwa nyumba wanayoishi huenda ikauzwa muda si mrefu.
Tulifanikiwa kumbembeleza Kisha yale mambo yakawa yameisha na tukaendelea kupiga stori za kawaida tu, hakuna aliyewaza kwenda polisi eti Jastini aliyetutishia hatimaye yupo mikononi mwetu kama ambavyo mke wangu alishauri tupige simu polisi kimya kimya then waje wamkamate, lakini kwa harakati za maisha yake hakuna aliyewaza mambo mengine yasiyofaa.
Lakini hofu ya Jastini bado niliiona nilitambua licha ya kutueleza mambo mengi lakini bado Kuna vitu anaficha ikabidi nimuulize haswa baada ya kuwa wanawake wameondoka.
Jax haupo sawa hebu niambie Kuna nini kingie tofauti na maelezo yako kama ni m3 nipo tayari kulipa niliropoka.
Daniel mwanangu,
Fatma yupo mjini, na amekuja kwaajili yangu nilimdhulumu pesa nyingi sana,na kumbuka Hawa wote ni maaskari yeye na mumewe hivyo Wana msaada mkubwa sana, wanaweza kunipoteza mara moja.
aliongea kwa upole Jastini.
Niliinama chini nikawaza sana, nakumbuka ni Jana tu nilionana na Fatma, pisikali ya maana almanusura nijipendekeze kwa mara nyingine jana lakini mpango uliharibika baada ya mke wangu kuja kunipa taarifa za kusema kuna vitisho nyumbani , nilishawahi kutengeneza mazingira ili nilale naye lakini ilishindikana, Fatma mbona kama ni zaidi ya nimuonavyo kwanini Jastini anamuogopa hivi?
nilijiuliza sana.
Kumbe wakati tupo ndani Kuna mtego uliwekwa nje na hakuna aliyejua, geti liligongwa wakaingia watu watatu mbavu kwelikweli wakasalimia huku haraka wakitoa vitambulisho vyao na kunionesha.
Walikuwa ni askari polisi sura ngeni hakuna niliyemjua hata mmoja.
Bila shaka wewe ni Daniel (akitaja majina matatu)
Yeah ni Mimi karibuni.
Niliwakaribisha huku nikimuona Jastini akija tulipo
Kwahiyo kumbe plan na mipango yenu huwa mnafanyia hapa si ndiyo?
Yaani nyinyi mnajifunza utapeli,Wala si wazoefu Sasa jeshi la polisi linawasaka watu kama nyinyi , Tena mlivyo wajanja Kuna muda mnajifanya mmegombana ili kutuzuga lakini timu yetu imefanikiwa kujua mbinu zenu.jana tu umeenda kituo cha polisi eti unamshitaki huyu jambazi mwenzio kakutishia, kumbe lengo mnatuchezea ili tusijue mipango yenu. aliongea huku akikunja sura akionesha hatanii.
Afande unaongea nini na Hawa?
Maelezo haya watapewa kituoni . aliamrisha askari aliyekuwa na silaha akisema muda unapotea.
Licha ya kujaribu kutaka kuuliza Kuna Nini lakini nilitishiwa na kubwa zaidi baada ya kujaribu kugoma kwenye gari lao lenye vioo vya tinted. Nilipigwa vizuri nikaona isiwe tabu na nitaumia nikaingia kwenye gari.
Itaendelea.................
Unywaji wa pombe kupitiliza ni hatari kwani husababishaDan kwa misala, hujambo!
huna baya samsonUnywaji wa pombe kupitiliza ni hatari kwani husababisha
1.kushuka kwa uchumi wa muhusika
2.kutoheshimika
3.kutofanya chaguzi sahihi
4.misala ya hapa na pale
5.Maamuzi yasiyo na tija
Yapo mengi ambayo simulizi itagusia huku nia na dhumuni ni burudani na kukumbushana pia.
tusameheane simulizi isipokuja kwa wakati lakini itaisha.
MBs zako ndiyo tiketi yako, enjoy.
Siku inapita bilabilaSEHEMU YA ISHIRINI NA SITA

Majukumu mkuu ngoja nikipata wasaa itakuwa freshiHivi JD unajua kuna watu tunafatilia hii simulizi seriously??
Majukumu mkuu ngoja nikipata wasaa itakuwa freshi
Uvumilivu utaitajika sanaUnywaji wa pombe kupitiliza ni hatari kwani husababisha
1.kushuka kwa uchumi wa muhusika
2.kutoheshimika
3.kutofanya chaguzi sahihi
4.misala ya hapa na pale
5.Maamuzi yasiyo na tija
Yapo mengi ambayo simulizi itagusia huku nia na dhumuni ni burudani na kukumbushana pia.
tusameheane simulizi isipokuja kwa wakati lakini itaisha.
MBs zako ndiyo tiketi yako, enjoy.
Pole mkuuSEHEMU YA ISHIRINI NA SABA
Tukiwa njiani kuelekea sehemu ambayo sikujua kwani hawakusema,
Simu yangu ndogo iliita, ni simu ambayo inahusika zaidi na ndugu tu.
Kuangalia anayepiga ni mke wangu. Lakini kabla sijapokea niliporwa ile simu na afande huku akiangalia jina la mtu anayepiga Kisha akanirudishia ikiwa imekata. Baada ya kuita kwa mara ya pili, Nilipokea.
Vipi mume wangu kwani imekuwaje tena mbona sielewi, nimesikia unaitwa jambazi? Halafu mnaelekea wapi saizi? Tafadhali naomba nijue ili nije nijue naanzia wapi. aliongea mke wangu huku nikiwa sijamjibu chochote,kisha afande yule akapokonya simu yangu na kukaa nayo.
Hakuna tena kuongea na simu humu acha ujinga usijione kama nani, halafu na wewe Black (akimaanisha Jastini)
hebu lete simu yako na wewe, nyie mpo chini ya ulinzi, acheni u****
aliongea kwa jazba yule afande huku akitukana.
Lakini Jastini hakuwa na simu jambo ambalo hata Mimi nilishangaa, kwanini asiwe na simu?
muda ule mbona niliwasiliana naye?
Oyaa afande Fox eeh, huyu boya hana simu eti, inawezekanaje?
Hebu simamisha gari. afande ambaye hakuwa na silaha aliamrisha yule dereva niliyesikia akiitwa Fox akimtaka asimame.
Hilo ndiyo tatizo lako afande punguza presha, kama hana simu atatuonesha ilipo ngoja tufike Central kwanza, hiyo ni michezo ya kitoto anafanya na kama Kuna mahali kaificha sisi tutajua tu . Yaani nilivyo na hamu naye huyu boya.
aliongea yule dereva anayeendesha gari akiwa anamjibu afande mwenzie.
Baada ya muda fulani tulifika kituo cha kati huku pilika zikiwa nyingi muda ule, askari wote tuliokuja nao walishuka huku tukipokelewa na askari wengine kabisa wenye maneno ya kejeli.
Hebu muone huyu brazamen eti anaangalia saa, au akili yako unajua unarudi eeh,hapa ninyi ni wateja wetu,ukiwa na hotel lazima utake watu waje walale, wale,si ndiyo eeh?
Huko kwenye ma bar wamiliki wanataka wapate faida mara mia zaidi ya walivyowekeza.yaani wateja wajae,so na hizi Selo lazima wateja wajae,eeeh .aliongea kwa kejeli afande fulani mwenye umri uliosogea huku akiwa kavaa miwani yenye kamba ili isianguke.
Dakika zaidi ya kumi tulikuwa pale Kaunda lengo wachukue maelezo na taarifa fulani toka kwetu,yaani mimi na Jax lakini ikawa ni foleni hawa wamekuja kudhamini ndugu zao hawa ni wahalifu wapya wanaletwa yaani fujo zilikuwa nyingi.hatimaye tukapewa nafasi huku moyo ukiniuma sana kwani nilikuwa nafanyiwa uonevu mkubwa sana kiasi cha kuanza kumchukia Jastini lakini pia niliwaza simu yangu maana yule afande alishuka na sikumuona tena.
Baada ya afande kuchukua taarifa akataka kutuweka mahabusu lakini akaambiwa na mwenzake kwamba twende kwenye chumba cha mahojiano moja kwa moja .halafu baada ya hapo tutarudi mahabusu.
Tuliingia kule tukakuta kuna chumba kidogo chenye vifaa vikuukuu , virungu, pasi na vitu vingine ambavyo wanavijua wao.
Karibuni sana jamani,karibu sana bwana Daniel,alinitaja jina yule afande huku nikishtuka lakini nikaona labda ananifahamu,alikuwa ni kijana fulani mdogo tu mwenye mwili mwembamba ambaye mabegani alikuwa si haba,huku nikimpongeza kwa umri wake na vile vyeo hakika alishajipata
Hey bro unaitwa Jastiniiiiii ...... akimalizia kwa kutaja full name,
Mbona unalidhalilisha kabila letu bro eeeh,sisi sifa yetu kwenye hii nchi ni kujazana kwenye majeshi tu na siyo kuwa na sifa kama zako vipi kaka?
Hebu huyu mpelekeni Selo halafu huyu niongee naye kwanza.
Mimi nilitoka nikiwa na askari mmoja ambaye alikuwa mkalimkali sana,lakini badala ya kupelekwa Selo nikaambiwa nirudi mahali ilipo Kaunda,hapa nilikuta watu wameongezeka,huku wakiwemo wanaonijua huku wakishangaa why niwekwe chini ya ulinzi.
Hata baadhi ya askari ninaowajua wale ambao wanawatoa mahabusu kutoka vituo vidogo na kuwaleta pale nao walishangaa kuniona pale huku nikiona aibu na uoga kwani taarifa zangu zikifika ofisini ni neno lingine,watu wenyewe wanasubiri ujikanyage tu halafu uone nafasi yako itakavyojazwa mapema,wapo waliosoma taaluma yangu vyuo vya nchi za nje na hawana kazi au nafasi kama yangu wengi wanasukumiwa site huko,niliwaza huku mapigo ya moyo yakiongezeka.
Dani ndugu yangu vipi tena,ni leo tu nilikuona kwenye gazeti,nikasema alhamdullilah nitampigia simu rafiki yangu ili tutete jambo cha ajabu napiga simu hupokei na mimi hapa kuna jamaa yangu ni dereva nimekuja kumuwekea dhamana siunajua tena ile gari yangu kirikuu yangu huwa napatia hela ya mboga sasa nasikia jamaa aligonga mtu mbaya zaidi ni kwenye zebra sasa ndiyo nafanya marekebisho.japo wamenikamua vibaya ila nashukuru nimefanikiwa , kwani una kosa gani Daniel?
aliniuliza yule jamaa ,lakini kabla sijamjibu yule jamaa.
Nilimuona Jastini akija akiwa na pingu kabisa mikono nyuma,nikaona mambo yameshakuwa mabaya , nikamsaidia kumvua viatu na mkanda kisha wakaondoka naye kwenda zilipo Selo,kisha na mimi nikarudi kwenye kile chumba cha mahojiano huku askari wakiwa wameongezeka nikaanza kupigwa spana.
Tuache siku zote tuongee ya leo,
Daniel, unaweza kutueleza ratiba zako za leo tangu ulivyoamka zilikuwaje, aliniuliza yule afande mdogo mwenye tabasamu muda wote
Nikajieleza ilivyokuwa na namna nilivyorudi kwa kuomba ruhusa ili nije nikutane na Jastini.
Wewe jana ukienda kituo X kwaajili ya kutoa taarifa za kutishiwa na Jastini,iweje utake kumalizana naye wakati taarifa ipo kituoni na ni mtu alitishia maisha yako,kirahisi tu ukataka kupatana naye kwanini?
Ni kwasababu alinitishia akinituhumu kuwa nimemtorosha mkewe,ila leo hii baada ya kusikia yupo nyumbani akiwa na mkewe,nikaona ngoja nikamsikilize.
Nilimjibu
Hivi unawezaje kuwa mwenye imani kiasi hicho huoni kama unajiweka kwenye hatari,kwanini usingetoa taarifa polisi ili yeye aeleze kampataje mkewe mbele ya polisi ambako wewe ulishitaki?
aliuliza
Nadhani hapa afande nilikosea ,ni mazoea yangu mimi na Jastini nilijua hasira zake zitakuwa zimepungua haswa baada ya kumpata mkewe.kiufupi hangenifanya kitu.
Nilijibu.
Aisseee sawa,wewe ni mfanyabiashara wa madini?
aliuliza.
Hapana afande mimi ni mfanyakazi tu,na nina biashara ya (nikitaja jina)
Halafu wewe upo humble sana na mimi nataka niwe humble kama wewe halafu wewe ni Braza wangu kwa muonekano tu,sitaki nikukosee heshima,mbona mwenzio hapa kasema wewe unafanya biashara ya madini tena yote,si lazima uwe na mabilioni hizo hizo hela za mafuta unazopata si faida ya unachofanya?
Sasa kwa kunidanganya unanikosea.
aliongea yule afande kwa sauti ya juu kidogo akinitisha
Ningependa yeye huyo aliyekwambia kuwa nafanya biashara hiyo athibitishe kwasababu hawezi kunisingizia,ataje wapi nanunua na wapi nauzia,si unasema kakuambia huyu Jastini?hayupo mbali aje aseme nimsikie.
niliongea kwa kujikaza kidogo.
Yule afande aliniangalia kwa muda huku akitabasamu, yule askari mwenye silaha yupo pembeni akiwa anaperuzi tu kwenye simu yake huku akicheka kwa vile alivyokuwa anaviona
Hebu washa hiyo taa wewe mwenzangu ni mrefu braza.aliniambia huku nikishangaa taa ipo karibu yake niiwashe mimi halafu hakuna urefu wowote hata yeye angewasha tu.
Ila Daniel wewe sijui upoje kwani kufanya biashara ya madini ni kosa?
Kwani ni madawa ya kulevya hayo hadi ukatae kiasi hicho,tena usichojua ni kwamba kuna matajiri wa Ruby wamekuja hapahapa nchini wanatoka Sri lanka,unajua wananunua bei gani gram moja?haya wewe jicheleweshe tu utashindwa kupata connection.aliongea kwa upole safari hii huku akitengeneza tabasamu rafiki.
Ukweli afande unaongelea jambo nisilojua na sijui linafananaje ungesema mbao sawa ni biashara naifanya na nina leseni na vibali vyote lakini sijui kitu kuhusu madini.niliongea bila wasiwasi.
Sawa ,afande nenda naye huyu kwa afande Fox kwanza alisema nikimalizana naye na yeye ana maswali anataka kumuuliza.Aliongea huku nikizodolewa na baadhi ya maaskari tuliopishana nao kwenye zile korido hata sikujua kwanini wanafanya vile.
Enheee Daniel nilikuwa nakusubiri maana leo shift yangu nimeanzia kwako nafika tu hapa kazini napewa gari niwafuate wewe na jambazi mwenzio,halafu simu nimezima maana mkeo anakera sana yaani.
aliongea afande aitwaye Fox ambaye alikuwa anaendesha gari wakati wametuchukua pale home.
Itaendelea........................
Kama movieSEHEMU YA ISHIRINI NA SABA

NiceSEHEMU YA ISHIRINI NA NANE
Huku ilikuwa ni sehemu kubwa na meza kadhaa huku baadhi ya maaskari wakiwa bize na mambo yao.
Naitwa afande Fikiri, almaarufu Fox,
Naitwa hivyo kwasababu huwa sipendi uongo,nang'ata, Kila nachokuuliza sema ukweli, hii itarahisisha pande zote mbili kwako na kwangu ukweli utakaosema Leo, na utakaosema kesho kutwa au wiki ijayo ni sawa tu, ila tambua ukisubiri ubanwe mbavu ndipo uongee jua kuwa utajiweka kwenye mazingira hatarishi zaidi.
Kisha akaendelea
Naomba kujua urafiki wako wewe na Jastini ni wa muda gani?
aliuliza Fox.
Sina uhakika kwasababu watu mnafahamiana kwa njia nyingi ila ni zaidi ya miaka kumi na kitu hivi,toka nimfahamu.nilimjibu.
Sawa , tofauti na yeye familia yake unaijua? yaani mke na watoto.
aliuliza.
Namfahamu mke wake, na huwa anasema ana watoto ila sijawahi kuwaona. Nilimjibu ukweli kwasababu hata hivyo Jastini hakuwa rafiki yangu kihivyo, ni rafiki ambaye mnaweza Kaa miezi hamuwasiliani, hadi kuwe na shida maalumu ndiyo mnatafutana.
Daniel unakunywa pombe, ni jana tu kuwa watu wetu walikuona. Halafu nasikia unatumia pesa vibaya sana yaani kipato chako na matumizi yako havifanani, kazi yako ni nzuri ndiyo lakini si kwa fujo zako unazofanya. Taarifa zako tunazo, kwanini ni mlevi kiasi hicho? aliuliza
Kwanza Mimi si mlevi ni mnywaji na pia sinywi spirit nakunywa beer na baadhi ya grants.ila local beer ndiyo sana wewe mwenyewe unajua zinauzwaje mtaani. Kwahiyo nashindwa kuelewa nakuwaje nafuja pesa ,halafu pesa zangu napangiwaje cha kutumia ikiwa sivunji sheria yeyote. Nilimjibu
Kwenye maisha na Harakati zako uliwahi kudhulumiwa? Iwe nyumba , kiwanja, pesa, na vingine vingi
aliuliza.
( Nilijua ni mtego)
Sina kumbukumbu ila Kuna ambao niliwahi kuwadai zamani sana na nilishawasamehe kwani haikuwa pesa nyingi kwangu. nilijibu
Ulishawahi kukopa sehemu yeyote? aliuliza.
Mimi nakopa sana tu kwenye Dunia ya leo huwezi ishi bila kudaiwa, nadaiwa na Benki X na X , nitalipa na nitakopa tena, maisha lazima yaendelee. nilimjibu huku nikigundua huyu Fox yeye ana mbinu zake za kuuliza kwani alikuwa anauliza maswali huku anapekua vitu fulani kabatini ni kama hayupo na wewe.
Wewe Daniel ni tapeli mkubwa na mbinu zako ni za kimataifa na una nyota mbili kwenye eneo la utapeli yaani umefuzu, kwa muda mrefu mmekuwa mkifuatiliwa tukishirikiana na wasiri wetu ambao wanaiombea
Mema nchi hii , tumejiridhisha na tuna ushahidi wa kutosha kuhusu wewe, halafu baada ya kugundua tumewashtukia mkajifanya mmegombana, hiyo mbinu ni ya kizamani sana Dani, hata hivyo unafanya biashara ya madini kwa njia ya magendo na inawezekana una biashara kibao ambazo ni haramu.
Japokuwa kwa uchunguzi wa maaskari wenzangu wanadai wewe huhusiki ila Mimi Sina Imani na wewe hata kidogo,nakuona mjanja mjanja mno , lakini pia na simu yako hii chukua halafu rudi kwa yule afande aliyekuhoji utamkuta nje kabisa Kuna maelekezo atakupa. Una bahati sana ingekuwa amri yangu ungelala ndani.
Nilirudi mpaka pale kaunda sikumuona yule afande Bali ni jamaa zangu kibao , mke wangu, mke wa Jax na wengineo.tukaruhusiwa baada ya afande fulani kusema wamegundua sina kosa.
Tukiwa njiani Mimi na mke wangu maana mke wa Jax aliongozana na ndugu zake akaniambia......
Mume wangu tulitaka tufanya taratibu ya dhamana kwa upande wa mwenzako Jastini lakini tumeambiwa tusijisumbue, kwani ni jambo lisilowezekana nasikia anakabiliwa na mashtaka zaidi ya sita sijui kafanya makosa gani masikini.
Achana na Jastini kwanza hebu tujadili hii nuksi yangu kwanza Kuna vitu naviona si vya kawaida.
Maana kwanza siamini kama nipo huru. niliongea.
Nilikupigia simu mara nyingi akawa anapokea afande Kisha mara ya mwisho akadai nisiwe na wasiwasi utarudi kwakuwa wewe huna kosa ila Kuna mambo wanayaweka sawa kwanza lakini nikaona ngoja nifike tu.
Halafu ni muda wa wewe mume wangu kuwa na mwanasheria, Kuna vitu una dharau lakini ipo siku mambo yatakuwa magumu.
Mwanasheria yupi?
Hapana mke wangu wanasheria wa kweli Wana gharama sana, labda kama Hawa akina mwafulani, halafu si kwamba Sina kwani yule (Nikitaja jina ) si yupo. Ila siyo kwenye vitu vya kipuuzi kama hivi , siwezi hata kumsimulia atanidharau tu.nilijibu.
Yule si mligombana iweje umtegemee?
Mke wangu aliuliza.
Hatukugombana Bali tulipishana baada ya Mimi kuhisi ananizunguka kumbe siyo, Bali ni mtu ambaye alikuwa anasimamia taaluma yake, kifupi yupo vizuri tu.nilijibu huku tukisimama kwenye mgahawa mmoja Nile Chakula maana nilikuwa na njaa sana lakini pia nilitaka nipunguze na mawazo kidogo kwa kupata mvinyo.
Nilipiga msosi huku wife akikataa na si mtu ambaye huwa anapenda kula migahawani hata kama ana njaa yeye ni nyumbani tu, labda kwa lazima akiwa mbali na nyumbani.
Baada ya kula nilipiga tarumbeta kadhaa , then nikarudi kwenye gari na kukuta mke wangu kakasirika kidogo baada ya kumchelewesha lakini pia Kuna simu kadhaa zilipigwa hususani dada Vero.
Huyo ni Vero kapiga si ndiyo?
aliuliza mke wangu.
Ndiyo hawa watakuwa wamesikia kuhusu matatizo yangu labda wanataka wajue Nini kimejiri, si unajua tena mambo ya magroup huko kunako Whatsapp nitakuwa najadiliwa Mimi tu.
Akujadili nani bwana, saa nne za usiku mtu anapiga simu ili iweje hata kama ni Mfanyakazi mwenzako, kwanza namba yangu si anayo kwanini asipige kwangu?
Maana wewe watu wote tukajua utalala mahabusu , Sasa mtu yupo huko unampigia vipi?
Halafu mume wangu najaribu kukutetea lakini naishiwa nguvu, neno ujambazi linatamkwa sana kuhusu wewe na watu wengi wanazungumza vibaya , kwanza ngoja tufike nyumbani ukanipe majibu ya maswali yangu . aliweka kituo mke wangu.
Itaendelea...............
Aiseee 😁😁😁mambo Msegemnege 😁 JBourne59 ulisema maana yake nini vile.SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE

Haya mkuuHaya sasa
Maliza kabisa ili unapoanza kusoma tusome kitu ambacho kilichokamilika, Wa sio nusu nusu