Jack Daniel
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 2,912
- 12,904
- Thread starter
- #181
Muda muda muda.We jamaa unafanya tunaisahau story yako
Mnisamehe kwa Hilo , pia uvumilivu unahitajika.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Muda muda muda.We jamaa unafanya tunaisahau story yako
pale kwa mganga hukuwaachia hata ela kidogo?SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA
Majibu mabovu ya mke wangu yalinitoa kwenye mudi sana yaani tayari alishanichefua,
Halafu huyu inawezekana huko kwenye biashara zake anakoshinda kunaanza kumpoteza, marafiki wasiokuwa kwenye ndoa wamembadilisha sana,siku hizi naye anajiamini tofauti na zamani , wanaitana malkia wa nguvu huko vijiweni kwao Sasa nitamkomesha nitahakikisha nafanya kitu hatonisahau, lakini piaaaaa nisiseme sana Mimi mwenyewe nimekuwa na mitihani isiyoisha nisije kufanya jambo Kisha nikaja kuharibu vitu vingi na kujutia.
Au nikajishushe nielewane naye tu maana hawa wanawake Kuna muda hupaswi kushindana nao utaumiza kichwa, lakini pia ndiye msaada mkubwa hapa mjini, licha ya kuwa nina ndugu kibao mjini , marafiki , mabinamu, watoto wa baba zangu wakubwa, lakini wote hao ukipata tatizo wanakutupa , sana sana wataishia kukupa pole tu licha ya kuwa wengi Wana maisha mazuri.
Lakini mke wangu nimetoka naye mbali mno, ndiye mtu ambaye Kuna muda huwa naona kama ananipenda kupitiliza, licha ya kuwa kwasasa anaanza kubadilika labda utu uzima hawezi kuwa vile milele. Ngoja nifike lazima nitumie uanaume wangu kuhakikisha ndoa yangu inakuwa imara. Nikaongeza spidi ya gari huku baadhi ya simu zilizokuwa zinaita nikizipuuza tu.
Niliingia mjini muda wa saa kumi huku siku nayo ikiwa inaisha, nilishuka ili ninunue maji kwenye grocery moja huku nikijizuia kunywa pombe kwani nilipanga kufanya mazungumzo na mke wangu hivyo nikaona lazima niwe timamu.
Lakini cha ajabu nyumbani kwangu sikumkuta mtu hata dada wa kazi hakuwepo nikaenda kwenye chumba cha dogo mmoja ambaye yeye hakupenda kukaa nyumba kubwa, akawa anakaa kwenye chumba fulani lilipo tank la maji lakini sikumuona yule dogo. Mara nyingi huwa anatoka hata wiki nzima anaweza asiwepo nyumbani huwa anakuwa kwao nje kidogo ya mji , nilimpendea kitu kimoja tu kujituma kwake pia adabu kwa mabinti zangu wa kazi.
Niliita mara kadhaa lakini sikusikia sauti ya mtu yeyote,
Hawa wapo wapi Sasa ngoja kwanza hata dada wa kazi naye hayupo na kwanini watoke waache nyumba ikiwa haina mtu na huwa nasema kama kuna yeyote anatoka wawe wanabadilishana .
Sasa leo Hawa watakuwa na kikao na Mimi ni lazima wajue kuwa wote wanalipwa na kama Kuna mtu anadai chochote wataeleza. wakati nikiwaza hayo simu yangu iliita mfululizo, nikaamua kuipokea huku nikiona ni kero kwani Mimi nawasaka ndugu zangu mtu mwingine anapiga na ingekuwa simu ya kazi ningejua kwani simu ya muhimu huwa haiiti Kila muda. Namba ya simu husika ilikuwa ni ngeni, nikaipokea.
Naongea na Daniel (akitaja full name)
Yeah ni Mimi , nani mwenzangu?
niliuliza.
Sawa, mimi naitwa Lydia nipo maeneo ya (akitaja jina).
Mimi ni dada wa Jastini, tupo wawili tu, na Mimi ndiye niliyemtoa kijijini kwetu miaka hiyo aje mjini kwaajili ya kunisaidia kusimamia ujenzi wa nyumba yangu hata baada ya kuwa nyumba iliisha tukawa wote tupo mjini na biashara zake.
Kwa ninavyomfahamu mdogo wangu hajawahi kuwa tapeli, utapeli kauanza si miaka mingi baada ya kujuana na wewe na mpaka Sasa yupo mahabusu mpaka muda huu akikabiliwa na mashtaka kuwa alimdhulumu Ruby askari mmoja huku deni lake likiwa kubwa na hatujua tunawezaje kulipa , familia yote hata tuungane vipi hatuwezi kulipa Hilo deni , pesa zaidi ya million hamsini tunapata wapi usawa huu. Mimi mwenyewe Sina kitu hata vijisenti vyangu vya kustaafu nilishavitawanya sina kitu.hivyo unatakiwa kuchanga hii hela ya watu ipatikane
aliongea Yule mama mwenye lafudhi fulani hivi hata sehemu ya kuweka L yeye anaweka R.
Sasa dada Mimi hata sikuelewi una maana gani kwahiyo huyo mtu kadhaminiwa?
Na kama katoka kawaambia na Mimi nahusika kwenye misala yake?
Niliuliza.
Weeee tena ukome na tumefanya upelelezi wewe ndiyo chanzo cha mwenzio kuingia kwenye matatizo,
Miaka mitatu nyuma kauza nyumba yake nzuri sana.
Haya Sasa hivi nyumba yake itauzwa wakati kumbe wewe ndiyo chanzo.
Na hapa nimeweka speaker kubwa watu na ndugu wote wanakusikia, kwanza Kuna kipindi wewe ulikuwa unaonekana nyumbani kwa mdogo wangu , ni zaidi ya siku mbili unamuulizia kumbe unamtuma huko halafu mambo yakigeuka msalaba anabeba peke yake. unabadilisha magari ya serikali tu . unavimba tu mjini kumbe unamtumia mdogo wangu kama chambo Sasa nikwambie tu ukweli mbinu zako zote zimejulikana.
aliongea kwa kufoka yule dada aliyejitambulisha kwa jina la Lydia.
Kisha akakata simu.
Ina maana Jastini kawaambia kuwa Mimi nipo pamoja naye mbona maelezo aliyotoa kituoni yanaonesha alieleza vizuri ndiyo maana Mimi nikaachiliwa. Niliwaza sana Kisha nikaipiga Tena ile namba akapokea.
Eeeh niambie unasemaje, halafu usiniwekee kibesi Mimi ni sawa na mama yako, aliongea kwa ukali.
Sasa dada, Mimi hata nashindwa kujua nahusikaje hapo, je kwani Jastini wamemwachia?
Niliuliza.
Acha ujinga , hivi habari zake zilivyokaa vibaya unadhani atatoka yule, Kuna mwanamke anaitwa Fatma, yeye tumekutana naye Leo kituoni anadai hataki kumpeleka mahakamani hadi pale atakapolipwa pesa zake na wewe umeshajulikana, hakuna siku mume wa Fatma ambaye ni askari polisi mlifanya biashara ya madini? Huku wewe Ukiwa ndiye mnunuzi?
Yaani unamtanguliza ndugu yangu awe chambo halafu wewe unadunda mtaani Sasa nakwambia hii kesi nanunua, Mimi nitasimama na wewe mahakamani wewe si unajifanya mjanja hunijui Mimi na nawapenda sana nyie mnaojifanya vidume .jambazi mkubwa wewe nitakuonesha.aliongea huku akizidi kuniongezea hofu.
Geti liligongwa huku mke wangu akiingia akiwa na dada wa kazi wakiwa kama wenye simanzi fulani wote.
Mume wangu tuachane na habari za asubuhi ulivyonipiga na kuniumiza , mwenyezi MUNGU atanilipia ila nakutaarifu kuwa maaskari wamekuja hapa zaidi ya mara mbili wanakutafuta na nasikia wameenda hata ofisini kwako. Huoni kama watakuharibia mume wangu, kwanini usijifiche. Kwanza ulikuwa wapi? aliuliza mke wangu.
Mimi nilienda huko pembeni ya mji mashambani ndani huko, na kwenye pickup Kuna vitu kibao mwambie huyo dada ashushe.niliongea huku nikitoa simu yangu nyingine nione kama imeita.lakini haikuwa hivyo.
Baba Jack, mume wangu, umeniumiza na kunionea hata muda ule mjumbe alisema ukirudi twende akatusikilize lakini siendi tena najiaibisha tu , bado Nina Imani na wewe kwani unatengeneza future ya watoto wangu. aliongea kwa hisia kali mke wangu.
Ila nilishavurugwa kusikia maaskari wananitafuta, na yake aliyoongea yule Lydia kwanini anishirikishe kwenye mambo yao, Sasa Mimi nalipaje pesa ambayo sijui alikulaje, hapa sikubali lazima twende mahakamani na hapa ndipo nilipouona umuhimu wa kuwa na mwanasheria.
Nilitafuta sehemu iliyotulia huku nikishukuru mke wangu kama ameahirisha mambo yake, nikatulia sehemu huku nikimpigia jamaa mmoja ambaye huwa anaiweza kazi ya uwakili na pia siyo mkubwa kivile hivyo ningemudu gharama maana Hawa wengine nisingewaweza.
Hello naitwa Daniel Nikitaja full name? Nafanya kazi katika taasisi ya...akanikatisha.
Daniel, Daniel yupi huyo, wewe ni yule uliyedhulumiwa mazao yako na dalali? aliuliza.
Siyo bwana, Mimi ni yule ambaye nilikuwa kwenye kampuni ya ujenzi wa barabara kwa mwarabu Kipindi
Kile (Nikitaja location kampuni ilipo)
Ahaaaa nimekupata kwanza hongera Kuna kipindi nikikuona kwenye gazeti fulani, kumbe ni wewe haya sema una shida gani maana niko bize kidogo, ongea haraka haraka.
aliongea akionesha yupo kwenye watu wengi.
Hili suala siyo la kuongea haraka kihivyo ni kwamba kama uko bize nikutafute hata kesho asubuhi na mapema nitakuja ofisini kwako.
nilimwambia.
Dah Niko na majukumu mengi lakini pia nitajitahidi kukusikiliza, halafu pia ofisi yangu haipo pale, kwasasa tupo wengi hivyo njoo maeneo fulani.
Nilimwelewa huku nikimtumia kiasi fulani ili aweke hata diesel kwenye gari kisha nikarudi ndani nikiwa mwenye mawazo.
Kweli madini ni kama majini kwanza hayapatikani kirahisi halafu yameniletea matatizo makubwa . Loh ngoja kwanza nimpigie mama yangu mzazi kule kijijini nitamwambia yote sitamficha.
Nilijikuta naropoka.
Itaendelea...............
Huwezi kuandika Kila kitu, kwa mfano tulibadilishana hata namba za simu, lakini sijaandika kwenye hiyo sehemu . Pia story inaendelea utajua umuhimu wa watu wale kwangu. endelea kufuatilia.nilifikiri pale kwa mganga ungewaachia pesa flani hivi au hujaamua tu kuweka hiko kipengele lakini uliwaachia?
pale kwa mganga hukuwaachia hata ela kidogo?
sawa mkuu japo ungeweza tu kunijibu ndio au hapana ili muhemko urudi pahala pakeHuwezi kuandika Kila kitu, kwa mfano tulibadilishana hata namba za simu, lakini sijaandika kwenye hiyo sehemu . Pia story inaendelea utajua umuhimu wa watu wale kwangu. endelea kufuatilia.
Rudisha muhemko huo[emoji23][emoji23]sawa mkuu japo ungeweza tu kunijibu ndio au hapana ili muhemko urudi pahala pake
Yes tuko tangu story zako za nyumaSEHEMU YA THELATHINI NA TATU
Nikiwa nawaza na kuwazua huku nikishangaa ni nuksi gani hii ni wazi kila nitakayemuelezea jambo langu atajua Mimi ni jambazi tu kama ilivyo kwa Jastini.
Sasa ni lazima nifanye kitu nadhani naweza kupoteza Kila kitu kwanza Kuna namna fulani mke wangu anapoteza Imani na mimi, hata baadhi ya majirani wanajua Mimi ni jambazi jambo ambalo ni hatari kwangu .
Jamii inapokuwa na mashaka na wewe ni dhahiri unaweza kuja kuhisiwa hata jambo ambalo hujawahi lifanya.
Lakini pia hata kazini naanza kuona namna watu wanavyonichukulia hata Veronica mtu ninayemkubali , mshauri wangu wa mambo mengi ni kama amekata tamaa hivi Tena siku Hadi siku namuona akipunguza mazoea na Mimi nadhani ni muda wa kupambana, Mimi ni mwanaume lazima nipambane kurudisha heshima yangu na Imani kwenye jamii. Kuhusu wife huyo Hana shida ni mke wangu ipo siku nitamuweka chini nitamuelekeza Kila kitu. naamini atanielewa.
Simu iliita huku nikipunguza speed ili nipate kuisikiliza si mwingine alikuwa ni boss mdogo , kwa tahadhari na uoga nikaipokea huku nikipaki gari pembeni.
Uko wapi Daniel,
aliuliza mara tu baada ya kusalimiana.
Nilibabaika kidogo maana sikujiandaa na swali lile.
Nipo nje kidogo ya mji kuna mahali naelekea mkuu, nilimjibu huku mapigo ya moyo yakinidundadunda.
Boss anasafiri kesho nadhani muda wa mwezi mzima atakuwa nje ya nchi ,hivyo Kuna maagizo nimeachiwa utayakuta hata hivyo nilisahau kukutaarifu tangu mchana kuwa hata mwenzako aliyekuwa Mwanza amerudi jana mtaungana naye kwaajili ya kuelekea mkoa XX.
aliongea huku akiweka kituo.
Sawa ila hujasema ni lini tunatakiwa tuwepo?niliuliza
Kwani wewe si ulipewa ruhusa ya siku tatu na leo si umemaliza?kesho nitawaeleza kila kitu ukija.alijibu.
Sawa ,ila samahani sana kesho sitafika kwakuwa matatizo yangu hayajaisha mkuu ,nakuomba niongezee hata siku moja tu.nilijitetea.
Cha ajabu alikata simu,kisha baada ya muda akapiga tena,
Daniel acha ujinga ina maana kwa mfano nisingekupigia simu , taarifa yako ungempa nani,nyie ndio huwa mnakuja kulaumu watu baadaye kisa ujinga wenu.mimi sina jibu la kukupa uonavyo wewe fanya.
aliongea kisha akakata simu.
Tumbo lilinivuruga huku hofu ikiingia,
Mmmh lazima nifike kwa mganga hakuna namna tena,nilikoleza chombo huku siku nayo ikiisha.
Niliipita Morogoro mjini nikaendelea kisha nikaikamata barabara ya vumbi kuelekea nilipokusudia kwani nilikuwa napafahamu siku nyingi.
Niliendesha gari kwa fujo na kwa spidi huku gari ikiwa na spot light upande mmoja tu ,lakini nilienda speed hivyo hivyo,nikiwa katikati ya pori sikutani na mtu zaidi ya wanyama wadogo wadogo waliokuwa wakikatiza kwenye barabara Almanusra niwagonge ,mlio wa Pickup tu ndio niliousikia huku hata mtandao wa simu nikiuacha kwani simu yangu ilionesha ,nikaweka simu kwa dashboard huku nikiongeza mwendo zaidi .
Baada ya muda niligundua uwepo wa mwanga nyuma,nikapunguza mwendo huku mwanga ukiongezeka,naam ilikuwa ni gari linakuja spidi huku kawasha hazard,mara awashe taa full na kuzima mara akinitaka nisimame. Nikabana pembeni na kushuka.
Nyoosha mikono juu , usifanye chochote ,piga magoti.
Sauti ya kiume huku nikimulikwa tochi ya mkono usoni huku watu watatu wakiruka na kuja kwangu ,mwanga wa tochi ulinisumbua lakini sikuwa na namna nilijua labda ni majambazi ,nikapanga kuwaambia pesa zilipo ili waniachie roho yangu hata kama ni gari wangechukua nilikuwa radhi,mtu mmoja mwenye bunduki SMG alikuwa pembeni akiwa kavaa shuka la kimasai huku akiwa na ile tochi ya kuvaa usoni aliniuliza.
Wewe ni nani?
Naitwa Daniel (nikitaja full name)
Unaenda wapi saizi halafu kwanini unakimbia hivyo na gari,umetushtua sana,na tuna taarifa za uwepo wa majangili ambao wametimuliwa na wenzetu huko mikumi mbugani ambao wanatafutwa ,afande hebu msachi kisha sachi na gari ,be careful pot wanakuwaga na vilipuzi hawa.
waliambizana wao kwa wao.
Walikagua siti zote,huku wakichanguachangua vitu lakini sikuwa na namna wakachukua simu wakaangalia mara ya mwisho niliongea na nani huku kila naloulizwa nilijibu vyema.
Wakaniambia niinuke huku wakipoa kidogo,halafu afande ana kisu kiunoni,.na pesa nyingi sana huyu ni wale wale mkuu,
Aliongea yule afande huku wakiangalia na kuniuliza ni cha nini nikawaambia mimi kama mwanaume ni lazima kuwa nacho.na mimi naenda kijiji cha (nikitaja jina) hivyo nawahi tu wala sina shida.
Waliangaliana huku wakinitaka niinuke,huku wakiwasha sigara zao na kuendelea kuvuta.
Sema jamaa unaendesha gari loh,yaani nusura nikate tamaa maana kila nikifukuza sikuoni na kona zilivyo nyingi loh. Ila pole sana,tulikuwa sehemu fulani kwenye gari tunashangaa huyu ni nani usiku huu anaendesha gari kwa speed licha ya barabara kuwa mbovu tukajua ni lazima kuna kitu anakimbia ila kwa maelezo yako tumeridhika.sema nini tuna njaa sana hapa vipi unatuachaje?
Waliongea huku wakinirudishia pesa zangu, sikuwa na namna niliwapa chochote kitu huku siamini kama nimepona maana Dah haikuwa poa ,tukachana huku wakiwa wapo pale pale wale maaskari wenye sare za Tanapa.
Nilitembea mwendo wa kawaida sana,saa saba usiku nikafika kwenye kile kijiji kidogo ,huku nikienda hadi kwa mganga husika,huku nikishangaa kukuta watu wengi huku wengine wakiwa hawajalala,nikaambiwa mganga yupo ila kuna watu kaondoka nao tangu saa mbili za usiku kaenda maporini na wateja wake kadhaa.
Nikiwa na kausingizi fulani nilimngoja huku nikishangaa magari kadhaa ya kifahari kuwepo pale,hii ikaniongezea imani kuwa huenda jamaa ni fundi siyo kwa wateja wale.
Asubuhi na mapema nilifuatwa na baadhi ya wanaoonekana wenye good life tukawa tunapiga stori huku nikiwa sijajua mganga alirudi au la
Eee bwana vipi tumeshangaa uwepo wa gari lingine ,hapa maana wenyewe tunatambuana tukasema huyu ni nani ndipo tulipoambiwa ni wewe.waliongea jamaa wawili ambao ndiyo wamiliki wa zile ndinga huku wivu ukiniingia,mimi kile Kigari kuwa dini nacho porini nikidai ni ya ofisini lakini wajuba wanakuja nazo hizi gari huku.loh ama kweli .
Oyaa una shida gani mzee, niliuliza nikijichangamsha.
Ah ni mambo ya biashara tu haziendi nikaona ngoja nije nimefika jana mchana na nishapewa dawa zangu sema niliambiwa ningoje kuna dawa ya mwisho ipo mbali,si unajua tena .aliongea kwa kujichekesha.
Na wewe bro vipi ,nilimuuliza yule anayeonekana kiumri katuacha parefu.
Dah kaka acha tu mimi nipo hapa mwezi wa pili sasa nina kijana wangu yupo huko ndani kaugua ukichaa, ndiyo tupo tunahangaika .alinijibu.
Vipi lakini maendeleo yake, niliuliza.
Mungu ni mwema,aliletwa hapa akiwa mwendawazimu kabisaa lakini kwa sasa naona kuna mabadiliko, kidogo,ananikumbuka mimi,anamkumbuka mama yake ,kiasi fulani analeta matumaini japo kuna siku anaweza kubadilika kiasi cha kukatisha tamaa.alijibu huku nikimpa pole na kumfariji.
Ila yule mganga mzee alishapungua nguvu aliyepo hapa ni mwanaye huyu ana uwezo mkubwa kuliko baba yake na ndiyo maana hao woooote wapo kwaajili ya kupata huduma.aliniambia yule jamaa.
Halafu vipi mwenzetu una shida gani? Aliuliza jamaa aliyedai yeye anasubiri tu dawa then aondoke.
Ni harakati za maisha tu,kuna msala nahitaji kuuzima.maana nikiyumba tu naweza poteza kila kitu.niliongea ukweli.
Dah pole mkuu tunaomba Mungu kila aliyekuwa hapa mambo yake yaende kama ilivyokuwa.alijibu yule jamaa.
Kuna watu hapa wamekuja kuroga ili kutesa wenzao hao unawaweka kundi gani ? niliuliza kiutani.
Dah kiongozi umewaza mbali sana,(huku akinipa tano) Mungu awalaani na wasitimize azma yao.
Tulipiga stori kibao huku tuliambiwa kuwa mganga anawataka wageni ambao hawajaonana naye wamfuate kwenye kilinge,nilikuwa ni mimi tu mgeni ambaye nipo siku ile hivyo nikamfuata huku nikishangaa kijana mdogo umri kati ya miaka 25 na 30 akiwa mganga.loh kweli kua uyaone.
Vua viatu vyako na hiyo kapelo pia kisogelee hicho kioo jitazame kisha ingia ndani .
mganga mwenye kiswahili lafudhi ya kiluguru aliongea huku nikifanya nayoambiwa kisha nikaingia ndani kwenye chumba kidogo ila kisafi sana.
Ni harakati za maisha tu endelea kufuatilia simulizi yangu hadi mwisho
Jifunze,
Elimika,
Burudika.
Itaendelea..............
Dah! Utamu umekataSEHEMU YA THELATHINI NA TATU

kijiji icho wachawi wengi km nini aseeeeJack Daniel
bila shaka ilikuwa kiberege
unakipata nini ni hatari kuanzia kisaki mpaka kiberege acha kabisa nlipata kutembea huko kipindikijiji icho wachawi wengi km nini aseeee
mimi sikukaa sana ila nilikuwa napewa story zao tuunakipata nini ni hatari kuanzia kisaki mpaka kiberege acha kabisa nlipata kutembea huko kipindi
mimi nlikwenda kabisa nikakaa kama week nikafika ifakara pia watu walozi mpaka imepitilizamimi sikukaa sana ila nilikuwa napewa story zao tu