SEHEMU YA HAMSINI NA TISA
Yaani hii aibu uliyonipa leo sitaisahau sijui unataka niishi maisha gani. maana hata sikuelewi mwenzangu,
alilalamika mke wangu.
Kwanza Sina Cha kujitetea zaidi ya kusema ni wivu tu ulinisumbua,
Tangu Jana niliona pesa zile nikajua labda utaniambia na kunifafanulia ni za nini lakini ikawa kimya na sikupanga kukuuliza. ila nisamehe mke wangu hata Mimi najisikia vibaya kwa yaliyotokea , aibu naona Mimi. nilianza kumpanga.
Daniel wewe ni mtu wa ajabu sana tena hata sijui nikuweke kundi gani,
Unaishi maisha ya kiswahili sana,
Hivi ile ni shilingi ngapi kiasi Cha kutaka kuharibu amani humu ndani,
Hizo hela wewe umeshika mara ngapi, ningekuwa sikufahamu ningesema labda ni mgeni wa pesa lakini unanishangaza sana.
Na akili nyingine inaniambia wewe hunitaki , haunihitaji maana Kuna vitu vingine hata siyo vya kuweza kufikia hatua mbaya kiasi hiki,
Haya biashara leo kule wateja wametupita tu, eeenh tumepata faida gani?
Hata wewe naamini ulikosa amani maana simu ulizipiga kutwa ya leo naona kabisa nusu ya muda wako kazini umetumia kunipigia mimi, hata ni faida gani umepata?
Oooh mara utakuwa umehongwa hizo pesa, mara utakuwa na nani,
Hivi unadhani mwanamke akiamua lake wewe utajua? unadhani naweza kukaa na cash ndani kubwa ndani kama ni za kuhongwa?
Sikia mume wangu na kipenzi changu Daniel, pamoja na mapungufu yako mengi ila nakupenda sana siwazi na sifukirii kukusaliti, ila ni wazi unanituma nifanye mambo ya kipuuzi na Mimi siwezi.
Na haya yote yanatokea kwasababu wewe husali, kwenda kanisani hutaki, hata kushiriki jumuiya hutaki ,hata ikija hapa huwa unakimbia na kutafuta visingizio kibao.
Ni mbatizwa wewe, ndoa yetu imebarikiwa pia ,lakini upo mbali na Mungu sana mume wangu.
Haya yote yanatokea kwasababu umemkaribisha shetani kwenye hii nyumba, uchamungu ni unyenyekevu, busara na hekima eeeh.
Kumcha Mungu ni chanzo cha maarifa lakini Dani wewe upo tu hueleweki, bado unajiona kijana, si ndiyo eeh, najua ni kama juzi tu tangu tuoane lakini hebu fikiria namna first born wetu alivyo, ni Binti mkubwa angekosa kuwa shule au angekuwa kijijini pengine ungeitwa babu Sasa hivi, lakini mambo yote haya yanasababishwa na kuwa mbali na Mungu. aliweka kituo mke wangu huku akiinuka na kuingia chumbani.
Tuliendelea kukwepana hivyo hivyo nikiingia ndani mke wangu anatoka anakuja sebuleni, nikija sebuleni yeye anaingia ndani , niligundua ni kama alikuwa anaepusha Shari lakini nilipanga kuirudisha furaha yake hata robo tu. Nikiwa chumbani nawaza na kuwazua nilishangaa kuona haji chumbani, ikabidi nije sebuleni. Nikamkuta kama kawaida yake anasuka vile vipochi huku akifuatilia tamthilia fulani.
Dah mke wangu kwanza nikupongeze sana kwa kuweza kuaminika na wenzio uwe muweka hazina wao, hakika najivunia kuwa na mke anayeaminika kwenye jamii. Na hii bahati si Kila mwanaume amepata
Halafu kingine nimependa aina ya wale washirika wako haswa yule madam Jane na kale kadada sijui mnamuita katibu.
Nimependa aina ya maongezi yao , yaani ni tofauti na nilivyowaona , ama kweli umdhaniaye siye kumbe ndiye.
nilianza kwa kujibaraguza hivi.
Halafu mke wangu mbona waliokuja leo siyo wale walikuja Jana, wale wako wapi? niliuliza kusudi anijibu ili nipime hasira zake bado ziko upper ama low.
Wale siyo sehemu ya kikundi hiki, wale wanakikundi chao kingine tu ambacho ni wafanyabiashara wadogo wadogo na Mimi ni sehemu ya walimu wao,
Tumekuwa tukizunguka kutoa Elimu kwenye vikundi mbalimbali kwasababu.
Wengi wao wanakopa bila kuwa na Elimu ya kutosha mwishowe ile pesa inaishia kumfilisi badala ya kumuinua. Kwahiyo tumekuwa tukitoa Elimu ya namna hiyo. alijibu mke wangu huku nikigundua hasira zimepungua kama siyo kuisha kabisa.
Mmmh kwanza nikupongeze kwa mara nyingine, kwa kuwa sehemu ya kuelimisha wengine, lakini mbona hujawahi kuniambia haya. niliuliza kwa kujipendekeza.
Ningekwambia saa ngapi , muda mwingi unarudi umelewa, na hata usipolewa huwa naona kama upo mbali na Mimi naamua kukuacha tu.kwanza niache naona kama unanichanganya tu kwanza si ukalale baba.alijibu huku akilaumu nikaona nitaharibu
Nikaamua kubadilisha mada,....
Hivi mke wangu vitu vingine vinachekesha sana tena mno , hivi Nini kinapelekea watu kujikuta wanafikisika. Maana haiwezekani mtu uanzishe biashara Kisha ukute unadidimia badala ya kuendelea.
niliuliza kama vile sjui kitu.
Mara nyingi watu wenye biashara kubwa ni nadra kufilisika kwani wengi wao Wana Elimu ya wanachokifanya.
Tatizo lipo kwa Hawa (sisi) wajasiriamali wadogo wadogo, kama wale wa milioni ishirini kushuka chini mara nyingi Hawa ni waathirika wakubwa , yaani mtu anajikuta anapoteza Kila kitu. Sababu ni kutokuwa na Elimu ya mikopo na biashara yenyewe.
Unakuta mtu anakopa pesa labda afungue duka fulani la mahitaji ya nyumbani, lakini badala ya kutafuta Fremu alipie Kisha aweke bidhaa , yeye ananunua tofali ili ajenge Fremu lake hapa ni rahisi mtu afeli kwani anakuwa nje ya malengo,hapo hapo pengine hajaangalia hata mzunguko wa biashara kutokana na mahali alipo yeye anaangalia mbona fulani anauza mwisho wa siku marejesho na riba vinarundikana kwake , biashara haiendi na mengine mengi.
Wapo wamachinga pia wasio na Fremu Hawa kutwa wanahenyeshwa ni wanamgambo, pia kipindi cha masika biashara huwa ni changamoto sana hivyo kujikuta wanahamahama kwenda huku na kule.
Kwa mfano Kuna wale rafiki zangu ambao uliwakuta Jana pindi unatoka kwenye safari zako ,Sasa yule mnene ana wakati mgumu na alikuja kuomba ushauri.
anadaiwa zaidi ya milioni mia Moja yule. aliongea mke wangu huku nikigundua ameshakuwa sawa
One hundred million, serious? mbona hafanani na hiyo hela yupo local sana ujue.ilikuwaje kukopa kiasi chote hicho.halafu why adaiwe peke yake na siyo kundi.niliuliza.
Ni Harakati za maisha tu Yule alikuwa vizuri sana na biashara yake ya kwanza ya kununua vinyago na kuvipeleka nchi jirani, biashara ilimuendea vizuri sana akaamua kufungua biashara nyingine ambayo hii ilikuwa ya kutulia ofisini na si kuzunguka, hii imemfelisha sana kiasi Cha kupukutisha mtaji wote,na hatujui ni wapi alikosea kwani haweki wazi , ila huenda ni baada ya kuajiri vijana wa kusaidiana nao. Unajua mpaka kufikia kuwa na wasaidizi kuanzia kumi na wanakutegemea siyo jambo rahisi . alifafanua mke wangu.
Sasa si huwa nasikia ana nyumba , si auze alipe deni? niliuliza kinafiki nikijifanya sijui kuhusu mikopo.
Nyumba imethaminishwa na benki inayomdai , na hata sehemu ya ofisi yake nayo imepigiwa hesabu, kwahiyo pamoja na vitu vyote kuchukuliwa na benki bado ana deni hilo kubwa, na sijui hata nimshauri nini maana ishu yake imekaa vibaya sana kutoka kumiliki kibanda Kisha kurudi kupanga chumba kimoja kisicho na umeme ni hatari sana. aliweka kituo mke wangu.
Dah mke wangu naomba kuwa na tahadhari na hizo mambo zako za vikundi mnaanzaga hivihivi mwisho wa siku yanakuwa kama ya rafiki yako ohooooo.nilitahadharisha.
Hapana bwana , miradi yetu haitahusisha wala kuingiliana na biashara zingine binafsi, na sioni kama kutakuwa na kitu kama hicho.japo ni vizuri kumtanguliza Mungu maana haya siyo rahisi kumudu malengo Moja kwa moja ,unaweza kujikuta unaishia pabaya .alifafanua
Nikopeshe kama mia mbili elfu hivi mke wangu nitakurudishia kesho kutwa. nilitania.
Nitakukopesha wala usijali, ukilewa zikiisha nakupa zingine,Kila ukilewa nitakuwa nakupa tu , si utanilipa eeeh.alitania huku nikifurahi kuona tumevuka kwenye ule upepo mbaya.
Utajiri huwa si kwa Kila mtu Bali maisha mazuri ni hitaji la Kila mmoja hivyo lazima Harakati ziendelee.
Tukutane sehemu ijayo.
Jifunze
Elimika
Burudika.
Itaendelea.................