Simulizi: Harakati za maisha

Simulizi: Harakati za maisha

SEHEMU YA HAMSINI NA NANE

Tafadhali baba, tunaomba utuoneshe mkeo yuko wapi, haiwezekani simu isipokelewe wakati anajua kabisa jana tuliongea nini.mimi ni mtu mzima hata umri nimempita mke wako parefu hivyo Kwa mtazamo wangu Kuna jambo naona haliko sawa.
alikuwa ni mmoja wa wale wanawake wageni akiwa anaongea taratibu lakini kwa kumaanisha.

Jamani karibuni sana ndugu zangu,
Karibuni ndani tuongee, naomba mnisamehe bure.
mke wangu aliwakaribisha wale watu kwa sauti ya unyonge sana.

Mmmh dada, why tukusamehe?
Kivipi yaani? eti jamani mnamuelewa huyu? (Huku akiwageukia wenzake)nilisemaa sikusemaaa?
eeeeh hiyo pesa haipo, mkishaona mtu anaanza na samahani hivi , jueni mambo hayapo sawa.
aliongea mwanamke fulani mwembamba huku akilazimisha kuingia ndani kwa nguvu.

My wife aliachia mlango mdogo Kisha wakaingia ndani watu wote, huku wakiongea maneno ya chinichini makali sana.
Nilibaki nimeduwaa getini nisijue la kufanya, nilitamani kwenda pale walipo nisikilize Nini kinaendelea lakini aibu nayo ilikuwa karibu,
Nikawa makini kutazama isije kutokea mtu akamuumiza mke wangu maana walikuja kishari mno.

Nilitoa simu mfukoni nikawa nascroll up and down lakini sikujua hata nachofanya nilikuwa naangalia pale walipo huku nikiwaza.
Dah hawa wanawake hawataki hata kukaa chini.nilizugazuga pale getini huku nikiona mke wangu anatoa maelezo kwa utulivu huku wao wakiwa makini kumuangalia, sijui aliwaambia Nini lakini mara kadhaa wale wanawake walikuwa wanageuka na kunitazama.

Mume wangu samahani nakuomba uje hapa. aliniita mke wangu.

Wale wanawake wakiwa wamesimama vile vile, safari hii walikuwa wakinitazama sana kupitia mwanga wa taa maana jua lilishakuchwa.

Jamani huyu ndiye shemeji yenu kwa wale wasiomfahamu, japo baadhi tunafahamiana.
mke wangu aliwaambia wale wageni wake huku nikigundua Kuna uchangamfu fulani kwake.

Samahani shemeji tena tusamehe sana Kwa kufika muda huu ambao pengine si rafiki maana huu ni muda wa kupumzika baada ya kazi za siku nzima, na pia naomba nijitambulishe kwako , naitwa Madam Jane ni mtumishi serikalini kama ulivyo wewe (huku akitaja nafasi yake)

Pia mimi ni mwenyekiti kwenye kikundi cha ujasiriamali , ambacho kinatambulika vyema sana,Kuna vikundi vingi sana hapa mtaani lakini kundi letu hili limekuwa mfano wa kuigwa sana na vikundi vingine.

Na nikupongeze kwa kuwa na mwanamke shupavu na imara sana,
Licha ya kuwa alichelewa kujiunga na sisi akiwa mtu wa mwisho kwenye timu yetu ya watu kumi na mbili, lakini watu wote tulimuamini mapema sana kiasi cha kumpa uhasibu na utunzaji wa Amana zetu.na hakuna mtu aliwahi kuwa na wasiwasi naye ila leo Kuna jambo tumeshindwa kulivumilia.

Kwenye mtiririko wetu Mimi ni
Mwenyekiti, na pia huyu ni katibu (akimuonesha msichana fulani ambaye umri ni kama miaka 30 hadi 35 nimemuita msichana kwasababu ya umbo lake dogo ila alikuwa kakomaa sana kiakili hata maongezi yake yalithibitisha.

Kisha madam Jane akaendelea.....
anaitwa Najma, tulimpa ukatibu kwasababu kuu mbili,
Kwanza ndiye msomi zaidi kwenye kundi letu, lakini pili ni mfano wa kuigwa sana mtaani. Ni mchamungu, ni mtulivu nadhani unajua fika namna wasichana wa kisasa walivyo,
Wengi wao wamejikita na mambo ya kidunia zaidi.lakini huyu anaswali na ni mwalimu kwenye moja ya chuo Cha kiisilamu (akitaja jina)

Kwa kumalizia tu ni kwamba kundi Lina watu kumi na mbili na hapa tupo tisa wengine tumewawakilisha.
Kundi Lina watu makini na wenye nidhamu.

Siyo wewe tu wapo na wanaume wengine ambao hawatuamini wanawake tukiwa kwenye haya makundi mkidai ni chanzo cha baadhi ya migogoro, lakini nikuhakikishie tunapeana semina mbali kwa walio kwenye ndoa na ambao hawapo kwenye ndoa, na lingine ni kwamba Moja ya sifa kwenye kundi letu ili upate nafasi ya uenyekiti , ukatibu ama uhasibu kama ilivyo kwa mkeo ni lazima uwe kwenye ndoa. Alifafanua aliyejiita madam Jane.

Samahani shemu umeongea sana,
Swali langu liko hivi,

Imekuwaje kuja usiku huu watu wote ninyi , Kuna Nini mke wangu kafanya, maana naona unaongea mambo mengi ambayo mnayajua nyinyi mimi
siyajui. niliuliza.

Kiufupi ni kwamba Kuna pesa tuliitoa benki jana, kwaajili ya kuanza utekelezaji wa mambo yetu Sasa tatizo likawa kwa mkeo ambaye ndiye mwenye mzigo
Tangu asubuhi hapokei simu,
Kiasi cha wanakikundi wenzetu kunifuata Mimi kama mwenyekiti ili tujue tunafanyaje. Kabla hatujaamua kufika hapa. ila tunashukuru katutoa wasiwasi na tumeridhika na majibu yake hivyo tukuage tu shemu. aliongea yule Madam Jane kwa sauti ya kujipendekeza.

Sawa ila hamuwezi kumbadilishia majukumu mke wangu mkapata muhasibu mwingine kwenye kundi lenu. niliuliza swali la mtego.

Mmmh shemu kwani Kuna nini mbona unasema hivi?
aliuliza yule niliyesikia anaitwa Najma aliyevalia majuba.

Kwani nyie hamuoni ni usumbufu , oneni mmeacha kupumzika, mmekuwa na mashaka na wasiwasi kutwa nzima mtu hapokei simu, Sasa ushauri wangu Mimi ni Bora mumpunguzie majukumu abaki mwanachama wa kawaida tu.niliongea huku nikiwaangalia kwa zamu.

Hapana shemu sisi tunamuamini sana tu, na sababu aliyoitoa wote tumeridhika hivyo mambo yetu tutapanga wakati ujao. Walijibu wale wanawake huku tukiagana mke wangu akawa anawasindikiza.

Nilirudi ndani nikiwa na amani kiasi Kiukweli madam Jane alinifafanulia vizuri, tofauti na mke wangu ambaye alitanguliza kuingiza jazba pengine tusingeelewana.

Nikifikiria kidogo huku nikipanga namna ya kumaliza lile suala maana mke wangu namjua si mwepesi wa kichukia, ila akichukia mnaweza msiongee muda mrefu, na siku hiyo alichukia sana.

alisukuma mlango kuashiria anaingia
Huku nikiwa bize kuangalia TV kama kwamba naelewa chochote, lakini ukweli nilikuwa nazuga tu. Hata ile taarifa ya habari sikuwa muda nayo.

Jifunze,
Elimika,
Burudika.

Loading...................
 
SEHEMU YA HAMSINI NA TISA

Yaani hii aibu uliyonipa leo sitaisahau sijui unataka niishi maisha gani. maana hata sikuelewi mwenzangu,
alilalamika mke wangu.

Kwanza Sina Cha kujitetea zaidi ya kusema ni wivu tu ulinisumbua,
Tangu Jana niliona pesa zile nikajua labda utaniambia na kunifafanulia ni za nini lakini ikawa kimya na sikupanga kukuuliza. ila nisamehe mke wangu hata Mimi najisikia vibaya kwa yaliyotokea , aibu naona Mimi. nilianza kumpanga.

Daniel wewe ni mtu wa ajabu sana tena hata sijui nikuweke kundi gani,
Unaishi maisha ya kiswahili sana,
Hivi ile ni shilingi ngapi kiasi Cha kutaka kuharibu amani humu ndani,
Hizo hela wewe umeshika mara ngapi, ningekuwa sikufahamu ningesema labda ni mgeni wa pesa lakini unanishangaza sana.

Na akili nyingine inaniambia wewe hunitaki , haunihitaji maana Kuna vitu vingine hata siyo vya kuweza kufikia hatua mbaya kiasi hiki,
Haya biashara leo kule wateja wametupita tu, eeenh tumepata faida gani?

Hata wewe naamini ulikosa amani maana simu ulizipiga kutwa ya leo naona kabisa nusu ya muda wako kazini umetumia kunipigia mimi, hata ni faida gani umepata?
Oooh mara utakuwa umehongwa hizo pesa, mara utakuwa na nani,

Hivi unadhani mwanamke akiamua lake wewe utajua? unadhani naweza kukaa na cash ndani kubwa ndani kama ni za kuhongwa?
Sikia mume wangu na kipenzi changu Daniel, pamoja na mapungufu yako mengi ila nakupenda sana siwazi na sifukirii kukusaliti, ila ni wazi unanituma nifanye mambo ya kipuuzi na Mimi siwezi.

Na haya yote yanatokea kwasababu wewe husali, kwenda kanisani hutaki, hata kushiriki jumuiya hutaki ,hata ikija hapa huwa unakimbia na kutafuta visingizio kibao.
Ni mbatizwa wewe, ndoa yetu imebarikiwa pia ,lakini upo mbali na Mungu sana mume wangu.

Haya yote yanatokea kwasababu umemkaribisha shetani kwenye hii nyumba, uchamungu ni unyenyekevu, busara na hekima eeeh.

Kumcha Mungu ni chanzo cha maarifa lakini Dani wewe upo tu hueleweki, bado unajiona kijana, si ndiyo eeh, najua ni kama juzi tu tangu tuoane lakini hebu fikiria namna first born wetu alivyo, ni Binti mkubwa angekosa kuwa shule au angekuwa kijijini pengine ungeitwa babu Sasa hivi, lakini mambo yote haya yanasababishwa na kuwa mbali na Mungu. aliweka kituo mke wangu huku akiinuka na kuingia chumbani.

Tuliendelea kukwepana hivyo hivyo nikiingia ndani mke wangu anatoka anakuja sebuleni, nikija sebuleni yeye anaingia ndani , niligundua ni kama alikuwa anaepusha Shari lakini nilipanga kuirudisha furaha yake hata robo tu. Nikiwa chumbani nawaza na kuwazua nilishangaa kuona haji chumbani, ikabidi nije sebuleni. Nikamkuta kama kawaida yake anasuka vile vipochi huku akifuatilia tamthilia fulani.

Dah mke wangu kwanza nikupongeze sana kwa kuweza kuaminika na wenzio uwe muweka hazina wao, hakika najivunia kuwa na mke anayeaminika kwenye jamii. Na hii bahati si Kila mwanaume amepata

Halafu kingine nimependa aina ya wale washirika wako haswa yule madam Jane na kale kadada sijui mnamuita katibu.
Nimependa aina ya maongezi yao , yaani ni tofauti na nilivyowaona , ama kweli umdhaniaye siye kumbe ndiye.
nilianza kwa kujibaraguza hivi.

Halafu mke wangu mbona waliokuja leo siyo wale walikuja Jana, wale wako wapi? niliuliza kusudi anijibu ili nipime hasira zake bado ziko upper ama low.

Wale siyo sehemu ya kikundi hiki, wale wanakikundi chao kingine tu ambacho ni wafanyabiashara wadogo wadogo na Mimi ni sehemu ya walimu wao,
Tumekuwa tukizunguka kutoa Elimu kwenye vikundi mbalimbali kwasababu.

Wengi wao wanakopa bila kuwa na Elimu ya kutosha mwishowe ile pesa inaishia kumfilisi badala ya kumuinua. Kwahiyo tumekuwa tukitoa Elimu ya namna hiyo. alijibu mke wangu huku nikigundua hasira zimepungua kama siyo kuisha kabisa.

Mmmh kwanza nikupongeze kwa mara nyingine, kwa kuwa sehemu ya kuelimisha wengine, lakini mbona hujawahi kuniambia haya. niliuliza kwa kujipendekeza.

Ningekwambia saa ngapi , muda mwingi unarudi umelewa, na hata usipolewa huwa naona kama upo mbali na Mimi naamua kukuacha tu.kwanza niache naona kama unanichanganya tu kwanza si ukalale baba.alijibu huku akilaumu nikaona nitaharibu

Nikaamua kubadilisha mada,....

Hivi mke wangu vitu vingine vinachekesha sana tena mno , hivi Nini kinapelekea watu kujikuta wanafikisika. Maana haiwezekani mtu uanzishe biashara Kisha ukute unadidimia badala ya kuendelea.
niliuliza kama vile sjui kitu.

Mara nyingi watu wenye biashara kubwa ni nadra kufilisika kwani wengi wao Wana Elimu ya wanachokifanya.

Tatizo lipo kwa Hawa (sisi) wajasiriamali wadogo wadogo, kama wale wa milioni ishirini kushuka chini mara nyingi Hawa ni waathirika wakubwa , yaani mtu anajikuta anapoteza Kila kitu. Sababu ni kutokuwa na Elimu ya mikopo na biashara yenyewe.

Unakuta mtu anakopa pesa labda afungue duka fulani la mahitaji ya nyumbani, lakini badala ya kutafuta Fremu alipie Kisha aweke bidhaa , yeye ananunua tofali ili ajenge Fremu lake hapa ni rahisi mtu afeli kwani anakuwa nje ya malengo,hapo hapo pengine hajaangalia hata mzunguko wa biashara kutokana na mahali alipo yeye anaangalia mbona fulani anauza mwisho wa siku marejesho na riba vinarundikana kwake , biashara haiendi na mengine mengi.

Wapo wamachinga pia wasio na Fremu Hawa kutwa wanahenyeshwa ni wanamgambo, pia kipindi cha masika biashara huwa ni changamoto sana hivyo kujikuta wanahamahama kwenda huku na kule.

Kwa mfano Kuna wale rafiki zangu ambao uliwakuta Jana pindi unatoka kwenye safari zako ,Sasa yule mnene ana wakati mgumu na alikuja kuomba ushauri.
anadaiwa zaidi ya milioni mia Moja yule. aliongea mke wangu huku nikigundua ameshakuwa sawa

One hundred million, serious? mbona hafanani na hiyo hela yupo local sana ujue.ilikuwaje kukopa kiasi chote hicho.halafu why adaiwe peke yake na siyo kundi.niliuliza.

Ni Harakati za maisha tu Yule alikuwa vizuri sana na biashara yake ya kwanza ya kununua vinyago na kuvipeleka nchi jirani, biashara ilimuendea vizuri sana akaamua kufungua biashara nyingine ambayo hii ilikuwa ya kutulia ofisini na si kuzunguka, hii imemfelisha sana kiasi Cha kupukutisha mtaji wote,na hatujui ni wapi alikosea kwani haweki wazi , ila huenda ni baada ya kuajiri vijana wa kusaidiana nao. Unajua mpaka kufikia kuwa na wasaidizi kuanzia kumi na wanakutegemea siyo jambo rahisi . alifafanua mke wangu.

Sasa si huwa nasikia ana nyumba , si auze alipe deni? niliuliza kinafiki nikijifanya sijui kuhusu mikopo.

Nyumba imethaminishwa na benki inayomdai , na hata sehemu ya ofisi yake nayo imepigiwa hesabu, kwahiyo pamoja na vitu vyote kuchukuliwa na benki bado ana deni hilo kubwa, na sijui hata nimshauri nini maana ishu yake imekaa vibaya sana kutoka kumiliki kibanda Kisha kurudi kupanga chumba kimoja kisicho na umeme ni hatari sana. aliweka kituo mke wangu.

Dah mke wangu naomba kuwa na tahadhari na hizo mambo zako za vikundi mnaanzaga hivihivi mwisho wa siku yanakuwa kama ya rafiki yako ohooooo.nilitahadharisha.

Hapana bwana , miradi yetu haitahusisha wala kuingiliana na biashara zingine binafsi, na sioni kama kutakuwa na kitu kama hicho.japo ni vizuri kumtanguliza Mungu maana haya siyo rahisi kumudu malengo Moja kwa moja ,unaweza kujikuta unaishia pabaya .alifafanua

Nikopeshe kama mia mbili elfu hivi mke wangu nitakurudishia kesho kutwa. nilitania.

Nitakukopesha wala usijali, ukilewa zikiisha nakupa zingine,Kila ukilewa nitakuwa nakupa tu , si utanilipa eeeh.alitania huku nikifurahi kuona tumevuka kwenye ule upepo mbaya.

Utajiri huwa si kwa Kila mtu Bali maisha mazuri ni hitaji la Kila mmoja hivyo lazima Harakati ziendelee.
Tukutane sehemu ijayo.

Jifunze
Elimika
Burudika.

Itaendelea.................
 
Back
Top Bottom