SEHEMU YA SITINI NA TANO
Nikiwa njiani kurudi nyumbani huku dereva wa taxi akinitupia macho kila muda huku akionekana ni mwenye hofu kiasi,sijui nilikuwaje hadi akanitambua mapema.
Lakini nikaona labda muonekano wangu ulionesha kuna kitu kinanisumbua.
Nikiwa na mawazo nilishtuliwa na dereva kuwa simu yangu inaita.
Nikaitoa huku namba ikiwa ni ngeni hapa nilipata mashaka zaidi huku hasira zilizochanganyika na uoga zikipanda,nikapanga kama ni ndugu wa Jane nitajibizana nao tu sitaogopa chochote,lazima nipambane nao ili kuinusuru familia yangu maana ilionekana ile familia ni watata sana.
Hello Mr Dani mambo vipi!
Sauti ya kiume ilisikika.
Niko poa ningependa kujua naongea na nani! Niliuliza kibabe.
Aaaah Daniiii acha hizo mimi ni afande (jina kapuni) ina maana hata namba yangu huna?
Yaani mkipandishwa vyeo tu mnafuta namba zetu au siyo( huku akicheka)
Hapana afande namba yako wewe haipo kwenye simu hii,eeh niambie kuna mpya gani! niliuliza.
Mpya ni kuhusu mkeo kaja kituoni asubuhi kuripoti kuhusu upotevu wa kijana mnayekaa naye,ila wewe ukiwa kama mtu wangu wa karibu nilitaka kupata habari kiundani zaidi ili tu kama kuna namna iweze kufanyika.
Aliweka kituo.
Mimi sikuwepo kiufupi nimeambiwa tu kama ulivyoambiwa wewe na nipo njiani narudi nyumbani ila naomba kama kuna kitu unaweza basi fanya ndugu yangu.niliongea kinyonge.
Usijali damu yangu Daniel,tutashirikiana na maaskari wenzangu kuhakikisha kijana anapatikana na waliofanya hivyo sheria itafuata mkondo wake,japokuwa kwa taarifa za chinichini inaonesha hata wewe umeshitakiwa kwenye moja ya kituo cha kati tofauti na hiki cha kwetu.
Vipi Dani mbona mambo yako hayaishi au kuna mzimu unakutafuta?
Zamani nilijua labda bado kijana lakini kwasasa huna muda utaitwa babu lakini bado tu kwanini?
aliuliza.
Ndugu yangu fanya kitu kwenye hili linalonikabili mengine tutajengana taratibu.niliongea kisha nikakata simu huku nikishangaa gari limesimama na hatujafika.
Vipi suka kuna nini mbona hivyo twende nyumbani?
Tuwahi bwana unanichelewesha.
Niliamrisha kwa sauti kali.
Mmmmmh,hii kazi yangu ina changamoto sana,tena mno na najua ipo siku nitakufa kabisa maana kama kuumia nimeshaumia.
Any way tuachane na hayo,wewe unaenda nyumbani kweli au kuna sehemu unaenda kuanzisha shari?
aliuliza yule dereva.
(Huku nikishangaa)
Oyaaa wee vipi mbona sikusomi habari gani unaleta kama hutaki nashuka na sikulipi.nilimtishia.
Dah bro mimi nitakufikisha kwako ila pesa yangu nipe kabisa ,nasema hivi kwasababu ni juzi kati tu hapa nimetoka hospitali hata hili kovu halijapona vizuri (akinionesha kovu kwenye ubavu wake wa kulia)
Nilichomwa kisu na mtu baada ya kumpeleka mteja wangu ambaye alikuwa anaenda kufumania na hakuniambia ila baada ya kuingia lodge mule ilibidi mimi nimfuate anilipe changu ndipo yule jamaa ambaye alifumaniwa alimzidi nguvu mwenye mke na kumpora kisu na kumjeruhi huku akinijeruhi na mimi akidhani wote tulienda kwasababu ya kumfanyia noma.
aliweka kituo.
Nilimwangaliaaaa kisha nikamwambia asimamishe gari.
Kwahiyo kisu kimoja kilichomchoma yule jamaa huku kikiwa na damu kikakuchoma na wewe pia siyo?
Niliuliza.
Yes,hata mimi nilishtukizwa tu jamaa akanichoma na kukimbia.
alijibu.
Dah pole sana,kwahiyo mjuba alifeli vipi hadi kuzidiwa na mgoni wake yaani mwizi wa mkewe.ilikuwaje mbona kama ni mzembe.
Niliuliza
Hapana ,siyo mzembe ila jamaa ambaye ndiye mwizi wa mke wa mtu alikuwa ni pande la mtu huku akiwa kashajiandaa kwani tulikutana nao wanatoka ndipo jamaa akachomoa kisu kiunoni na kikaporwa na jamaa na kumuumiza mwenyewe.
alijibu kwa hisia kali sana
Dah aisee pole sana,watu tujifunze kisu siyo silaha ya kupambana bali ni silaha ya kuchinja kilichosarenda kama nyanya na vitunguu basi.
Ila pole sana shika pesa yako niache hapa hapa nitapanda bodaboda, wakati huo mke wangu kila akipiga simu sikupokea niliiacha makusudi.
Nilishuka huku nikigeuka na kuona yule dereva kashuka kwenye gari ananiangalia nikachukua pikipiki hadi home huku nikiwa makini sana niliingia ndani nikamsalimia dada wa kazi kisha huyooo hadi ndani chumbani ambapo kwanza wife alishangaa kuniona wakati huo.
Imekuwaje,Dah afadhali umerudi japo nashindwa kuelewa umerudi kivipi na uliniambia upo mkoa wa mbali.aliuliza mke wangu bila hata salamu.
Hayo achana nayo hayo kwanza nataka kujua Jane anaishi wapi na nipe namba ya huyo malaya.
niliongea kwa pupa.
Hapo utaharibu mume wangu tafadhali achana na ubabe usio na maana wewe ni vyema ukachukua taratibu za kisheria ili tujue kijana tunampataje kisha tutadili na habari zako wewe na Jane na yule mume wa Jane nimeongea naye anaonekana ni mstaarabu tu japo ndugu kwa upande wa ndugu wa Jane ndiyo wakorofi lakini cha
Muhimu sisi tuwe wapole na nakuomba mume wangu Dani kuwa mpole kubali kosa ili tu tumalize huu msala.aliongea kwa upole mke wangu.
Baada ya muda kidogo nilitulia nikiwa napiga simu huku na huko haswa kwa maaskofu wakubwa ili kutafuta tag ubavu,wapo ambao ni wakubwa zangu kazini ningewaambia nilijua wangenisaidia tu ila niliona msala wenyewe umekaa kipuuzi mno ningejidhalilisha tu na kujishushia heshima yangu.
Nilitoka nje kisha nikagundua sina gari la maana kwaajili ya mizunguko yangu maana baadhi ya maaskari walijifanya kujua alipo kijana wangu
Najua lengo wanipige hela maana kuna mmoja aliniita akidai amepata taarifa kutoka kwenye vyanzo vyake.
Gari langu lilikuwa kazini kwangu na gari la mke wangu lilikuwa gereji hivyo nikaamua kuchukua pickup yangu nakuingia mtaani lengo nione upepo unavumaje haswa kwa upande wa polisi ambao ndiyo tulikuwa tukiwasikilizia watupe majibu ,kabla hata sijafika mtaa wa pili mke wangu alipiga simu na kunitaka nirudi haraka kuna wageni.
Niligeuza gari haraka na huku jasho likinivuja sikujua hata linasababishwa na nini niligundua nalazimisha kujiamini lakini kimsingi nilikuwa na uoga kwa kiwango kikubwa,
Hatimaye nilipakaribia kwangu huku jua likionesha linapungua nguvu kuonesha kunakuchwa.
Nilishuka huku nikiziona gari mbili nje moja ina usajili wa namba za serikali moja na moja ni namba za kawaida moyo ulishtuka lakini nikajikaza kiume kwani nilikuwa kwangu na ilikuwa vigumu mtu kukimbia kwake.
Niliingia ndani nikakutana na watu watano yaani wanne ni wageni na watano ni mke wangu, niliwasalimia wakajibu huku wakinikaribisha.
Jamani huyu ni mume wangu ndiye mliyekuwa na hamu ya kutaka kumuona. Mke wangu aliwatambulisha huku nikiwa makini kuwaangalia kwa zamu kama Kuna yeyote angetaka kuzingua basi leo nisingeandika hapa huenda ningekuwa jela.
Ndugu Daniel , Mimi naitwa (jina kapuni) ni mume wa yule uliyempiga na kumsababishia maumivu makali,
Ila kuna muda sikulaumu kwasababu
Kwanza nawaza mambo mengi sana ingawaje Hawa ndugu wa mke wangu wanakuchukia lakini Mimi kama mume Kuna mazingira naona hayapo sawa kwasababu kama ungempigia sehemu tofauti na hapa ningekuona mshari lakini ulimpiga akiwa ndani kwako.
La pili ni muda yaani mke wangu aliniambia alikuja kwako saa nne za usiku Kuna taarifa alikuletea Sasa nashindwa kuelewa muda wote huo mke wangu alikuwa anafanya nini muda huo wa saa nne za usiku?
Muda ambao alitakiwa awe nyumbani na nilimpigia simu mida ya saa tatu tukaagana kuwa anaingia chumbani kupumzika lakini chaajabu napigiwa simu na watu kuwa kaumizwa na nyumbani Kafika mida ya saa sita usiku nikiwa kama mwanaume na muhusika ni mke wangu nashindwa kuelewa kumbukeni Nina zaidi ya miezi kadhaa nipo Mkoa lakini huku nyuma nasikia stori zenye mkanganyiko namna ile . Mume wa Jane aliweka
Huku akiwaangalia ndugu zake ambao walikuwa wakimshangaa.
Ina maana wewe shemeji unaungana na hawa mbona sikuelewi yaani hujali afya na uzima wa dada yangu?
Hujali heshima ya dada yangu kushuka kutokana na kupigwa na mtu tu?
Huoni kama huyu mpuuzi Daniel anakudharau, kampiga mkeo halafu bado huoneshi msimamo wa kiume? alilalamika Binti fulani ambaye anaonesha ni mdogo wake Jane.
Weeee usiniite mpuuzi kumbuka upo kwangu acha ujinga.
Niliongea baada ya kuona mume wa Jane kumbe wa kawaiiiiida tofauti na nilivyowaza. Halafu namfahamu ila yeye hanifahamu ni jamaa mmoja yupo kwenye chama kikongwe akiwa kwenye ujumbe anatumwatumwa tu huko kwenye matawi ya chama mikoani yaani kiufupi nilikuwa nammudu vizuri sana .
Tuliwahi onana mwa 2015 Dodoma kwenye kampeni halafu yeye alikuwa front sana akiwa kwenye sare za chama huku Mimi nikifukuzwa kutokana na ulevi wangu,
Nikakumbuka ndiyo maana hata mke wangu na Jane wamefanikiwa kulamba ule mkopo kutokana kuwa mume wa Jane .............
Maisha haya acha tu.
Baada ya kukorofishana na yule Binti mweusi ambaye ndiye mdogo wake Jane akinitukana huku nikiwa kimya wale wanaume wengine wawili walianza kumshambulia yule mume wa Jane kwamba hana msimamo walipanga Nini na kafanya nini?
Baada ya hapo wao ndiyo wakawa wanagombana ndani mwangu.
Mmmmh waganga wa kweli bado wapi amini usiamini.
Niliinuka na kufunga geti vizuri huku nikijipanga kuwasomea risala kwani Daniel huwa Nina tabia ya uharaka yaani kutukana siwezi ila vibao huwa vinanitoka mapema mno,ila mtego walionitegea sikuugundua mapema japo walikosea mpango ule kufanyia ndani mwangu.
Nini kilijiri sehemu inayofuata ina majibu
Jifunze
Elimika
Burudika.
Itaendelea............